Sinagogi hili la Siloam Ministries

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,666
729,801
Dini ya leo ni biashara inayolipa sana na kila mwenye uelewa kidogo wa theolojia hutaka kuanzisha kanisa lake. Kuna baadhi licha ya pesa Kuna mambo ya siri wanafanya au wana taratibu zao zenye kuacha maswali mengi

Hivi karibuni nilikutana na mwamimi aliyekimbia kanisa la Sialom mkoani pwani akanihadithia mengi ya kushangaza

-kwao majina si kama haya yetu bali majina yao ni kama haya..Siku yake!Ahadi!Agano! Kimbilio! Jaribu nk nk

-Chakula kwao wanaita karamu
-Maji yanaitwa damu yake

-wakipigiwa simu hawataji eneo husika bali wanasema wako mlima wa moto ili adui asijue uko wapi

-Wanaamini makombo ni tiba (makombo ya Chakula wanakula makuhani wao )
-viongozi wao wanajulikana kwa jina la makuhani
-ibada zao huanza saa sita alfajiri kwa kughani maneno ya kujirudiarudia tena kwa sauti ya juu (kupayuka)

-nguo zao ni suruari fupi nyeupe na kanzu
Maisha yao kwa sehemu kubwa wanategemea malipo kwa wale wanaokuja kuponywa kanisani

Hii ni imani lakini ni vema ukaamini kitu kisicho na ukakasi...muumini huyu amefanikiwa kukimbia na sasa yuko huru
 
Dini ya leo ni biashara inayolipa sana na kila mwenye uelewa kidogo wa theolojia hutaka kuanzisha kanisa lake
Kuna baadhi licha ya pesa Kuna mambo ya siri wanafanya au wana taratibu zao zenye kuacha maswali mengi
Hivi karibuni nilikutana na mwamimi aliyekimbia kanisa la Sialom mkoani pwani akanihadithia mengi ya kushangaza
-kwao majina si kama haya yetu bali majina yao ni kama haya..Siku yake!Ahadi!Agano! Kimbilio! Jaribu nk nk
-Chakula kwao wanaita karamu
-Maji yanaitwa damu yake
-wakipigiwa simu hawataji eneo husika bali wanasema wako mlima wa moto ili adui asijue uko wapi
-Wanaamini makombo ni tiba (makombo ya Chakula wanakula makuhani wao )
-viongozi wao wanajulikana kwa jina la makuhani
-ibada zao huanza saa sita alfajiri kwa kughani maneno ya kujirudiarudia tena kwa sauti ya juu (kupayuka)
-nguo zao ni suruari fupi nyeupe na kanzu
Maisha yao kwa sehemu kubwa wanategemea malipo kwa wale wanaokuja kuponywa kanisani
Hii ni imani lakini ni vema ukaamini kitu kisicho na ukakasi...muumini huyu amefanikiwa kukimbia na sasa yuko huru
Umesahau huwa wananawishwa miguu na kufutwa miguu wallah hizi ni nyakati za mwisho kisa cha kuambikizana mifangasi nini Tenda Neno shika Neno
 
Umesahau huwa wananawishwa miguu na kufutwa miguu wallah hizi ni nyakati za mwisho kisa cha kuambikizana mifangasi nini Tenda Neno shika Neno
Shika neno tenda neno mtumishi, ukiwa wa imani tofauti hata salamu hupati na wanaoana wao kwa wao, ukimtaka mtumishi lazima ukasali kanisani kwake na uvae kanzu/gauni jeupe na ushinde kanisani siku nzima
 
Halafu wana shuhuda za kushangaza kweli eti kuna binti alifanikiwa kupata mchumba hapo kanisani kwa kula makombo ya kuhani na mwingine aliponywa meno
 
Ila jama katika majipu naona na Viongozi wetu wangeanzia humu kwenye haya makanisa yaliyochipukia sasa ule uhuru wa kuabudu naona umevuka mipaka kuna mambo ya ajabu sana humu mtu tooka asubuhi mpaka jioni sijui mikesha mwanzo mwisho hizo kazi huwa wanafanya saa ngapi alafu useme maisha magumu
 
Shika neno tenda neno mtumishi, ukiwa wa imani tofauti hata salamu hupati na wanaoana wao kwa wao, ukimtaka mtumishi lazima ukasali kanisani kwake na uvae kanzu/gauni jeupe na ushinde kanisani siku nzima
Hili nalo jipu linatakiwa kutumbuliwa wanalitumikia Taifa saa ngapi hata kwenye Biblia imeandikwa asiyefanya kazi na asile halafu zile Biblia magamba ya nje huwa wanayatoa duu haki ya nani tembea uone mambo
 
Pool of Siloam!

Hili kanisa ni moja kati ya makanisa ya kiroho lililo tofauti na makanisa yote ya kikristo. Ngoja nikupe story kidogo juu ya hili kanisa,
Mosi.... Hakuna popote penye ishara/alama ya msalaba kama ilivyo makanisa mengine ya kikristo, ndani ya majengo ya makanisa yao.

Pili... Kila mkoa Tanzania una jina lake, Kwa mfano Moshi panaitwa Ararati, Singida panaitwa Sayuni, Mwanza - Yericko,

Hata hapa DSM kila kitongoji kina jina lake, Mfano TABATA inaitwa, .... wanajua wenyewe

Tatu: Kiongozi wao anaitwa MUNGU WA MAJESHI- MIAKA 1000 , wanamwabudu kama mungu, wanaamini hata huwezi kumuona

Nne: Mwanzilishi wa hilo kanisa , alikuwa anaitwa Munuo (Mmachame), alifariki mwaka juzi bila kukosea, akazikwa huko Bagamoyo, wanasema alipaa mbinguni kama Yesu, hata vyombo vya habari ya CNN , BBC vilionyesha. Ajab hakuna local media hata moja iliyoripoti tukio kubwa kama hilo.

wachungaji wengi wa hilo kanisa ni Wamachame

Tano: Biblia yao haina kava la juu, wameweka lakwao, kila siku wanabadili na kupunguza mistari kwenye biblia, MUNGU WA MAJESHI anasemu MUNGU wetu aliye hai ndie kamwaguza kufanya hivyo. Kwa kifupi biblia yao ina viaraka

Sita: wanaposali /wakiwa kwenye maombi wanatingisha vichwa , na kubana sauti inakuwa kavu hatari. Kama ni mara ya kwanza kwenda hapo, huwezi kusikia chochote.

Saba: waumini wao wana hali mbaya sana kiuchumi.

Nane:
Hawatumii miezi yetu, sijui February, Janurary au March , wao miezi yao ni Zifa, n.k

Ukienda hapo utastaajabu....
 
Kuna kikanisa mtaani kwetu..kuanzia jtatu mpk jtatu kanisa liko on firee kuanzia asubuhi wanatumia vipaza sauti na spika kubwa...ukipita unakuta ni watu wawili au watatu tu..ss najiulizaga kazi ya kipaza sauti ni nini..km mko wawili si mnahubiriana na kuimba kwa sauti ya kawaida tu mnasikilizana..
 
Back
Top Bottom