Sinagogi hili la Siloam Ministries

Sinagogi hili la Siloam Ministries

Dini ya leo ni biashara inayolipa sana na kila mwenye uelewa kidogo wa theolojia hutaka kuanzisha kanisa lake
Kuna baadhi licha ya pesa Kuna mambo ya siri wanafanya au wana taratibu zao zenye kuacha maswali mengi
Hivi karibuni nilikutana na mwamimi aliyekimbia kanisa la Sialom mkoani pwani akanihadithia mengi ya kushangaza
-kwao majina si kama haya yetu bali majina yao ni kama haya..Siku yake!Ahadi!Agano! Kimbilio! Jaribu nk nk
-Chakula kwao wanaita karamu
-Maji yanaitwa damu yake
-wakipigiwa simu hawataji eneo husika bali wanasema wako mlima wa moto ili adui asijue uko wapi
-Wanaamini makombo ni tiba (makombo ya Chakula wanakula makuhani wao )
-viongozi wao wanajulikana kwa jina la makuhani
-ibada zao huanza saa sita alfajiri kwa kughani maneno ya kujirudiarudia tena kwa sauti ya juu (kupayuka)
-nguo zao ni suruari fupi nyeupe na kanzu
Maisha yao kwa sehemu kubwa wanategemea malipo kwa wale wanaokuja kuponywa kanisani
Hii ni imani lakini ni vema ukaamini kitu kisicho na ukakasi...muumini huyu amefanikiwa kukimbia na sasa yuko huru

Wahi huko natafuta,,, utabadili jina liwe nimepata,,,hahaha
 
Kitanda wanaita madhabahu kuna jamaa tulikua tunakaa nae room moja anasali hilo kanisa,sasa one time akawa anaongea na demu wake kwenye simu akamwambia demu " mi niko madhabahuni" yaani kitandani.
Zanzibar wanaita kaanani, kuna siku jamaa akapata safari ya kwenda Zenji akawa anatuaga " jamani mi naenda kaanani" Dah! tulichoka.
Jina la jamaa sasa WISDOM GOD OF MERCY
 
Pale morogoro pia wapo,nilikuwaga nasikiza redio yao,nilikuwa sijawajua,ila walikuwa wanamtaja zaidi nabii eliya
 
Ha ha ha mkuu mshana jr, shika neno.....

Watu wanaojiita wakristo ni wapumbavu sijawahi ona
Usirudie tena kutumia hilo neno,,,,,Wakristo ni watu wa kuheshimiwa duniani kote,,,maana wanafanania Kristo mwenyewe,,, hao wengine wasiomfanania wanahubiriwa habari njema za kristo,,,,
 
Dah! Mdogo wangu yupo huko kweny Hilo dhehebu asee amesema mimi nina pepo kisa natwanga kilaji
 
Wanadai kwamba wao hawamuamini yesu kwakuwa alikufa. Wanamfuata Eliya kwani ye hakufa bali alipaa.
Sabato yao ni jumanne
 
Pool of Siloam!

Hili kanisa ni moja kati ya makanisa ya kiroho lililo tofauti na makanisa yote ya kikristo. Ngoja nikupe story kidogo juu ya hili kanisa,
Mosi.... Hakuna popote penye ishara/alama ya msalaba kama ilivyo makanisa mengine ya kikristo, ndani ya majengo ya makanisa yao.

Pili... Kila mkoa Tanzania una jina lake, Kwa mfano Moshi panaitwa Ararati, Singida panaitwa Sayuni, Mwanza - Yericko,

Hata hapa DSM kila kitongoji kina jina lake, Mfano TABATA inaitwa, .... wanajua wenyewe

Tatu: Kiongozi wao anaitwa MUNGU WA MAJESHI- MIAKA 1000 , wanamwabudu kama mungu, wanaamini hata huwezi kumuona

Nne: Mwanzilishi wa hilo kanisa , alikuwa anaitwa Munuo (Mmachame), alifariki mwaka juzi bila kukosea, akazikwa huko Bagamoyo, wanasema alipaa mbinguni kama Yesu, hata vyombo vya habari ya CNN , BBC vilionyesha. Ajab hakuna local media hata moja iliyoripoti tukio kubwa kama hilo.

wachungaji wengi wa hilo kanisa ni Wamachame

Tano: Biblia yao haina kava la juu, wameweka lakwao, kila siku wanabadili na kupunguza mistari kwenye biblia, MUNGU WA MAJESHI anasemu MUNGU wetu aliye hai ndie kamwaguza kufanya hivyo. Kwa kifupi biblia yao ina viaraka

Sita: wanaposali /wakiwa kwenye maombi wanatingisha vichwa , na kubana sauti inakuwa kavu hatari. Kama ni mara ya kwanza kwenda hapo, huwezi kusikia chochote.

Saba: waumini wao wana hali mbaya sana kiuchumi.

Nane:
Hawatumii miezi yetu, sijui February, Janurary au March , wao miezi yao ni Zifa, n.k

Ukienda hapo utastaajabu....
Pia ni marufuku muumini kukopa au kukopesha pesa.

Hawaruhusiwi kushiriki misibani
 
5c59d71f254c8430e4e2a0a0fd2026fe.jpg

Mama yangu Amefika hatua hii
Kisahawaruhusiwi kwenda hospitali
Hatari sana.
Hizi dini zinapaswa kufutwa.
 
Ningekuwa Rais wa Tanzania, ningeyafunga na viongozi wangepelekwa nanii ili wa pone.

Wanachumia tumbo kwa kutumia ujanja wa viini macho.
Angalia mabango yao. Haya mtukuzi MUNGU, bali mapicha yao na majivuno eti Dr. Mtume. Asikofu rev. transfoma. Bulidoza....mzee wa upako...hii ni sawa na sifa na utukufu ni kwao????????wana boa
Kibaya zaidi mahubiri yao yamejaa maneno ya miujiza sijui kufufu misukule yaani utapeli kabisa wa wazi wazi mtu ameathirika na h.I.v na keshaanza kutumia dose ukifika kule wanaacha mwishowe mauti, halafu kinachoniuma zaidi kuna watu wanakuta ni waathirika wa huo ugonjwa wanasema walikuwa wanatumia dawa na baada ya kufanyiwa maombi wamepona na vyeti vya hosp wanavionyesha ilihali wataalamu wanakuambia ule ugonjwa ukiwa unatumia dawa vizuri kuna mida ikifika unaweza kupima na virusi visionekane sio kwamba havipo ila ni kutokana na mambo ya kisayansi ya vile virusi vinabadilika kusema kweli ukaguzi wa haya makanisa ya kileo inabidi ufanyike kujua yanayoabudu kweli na roho ni yepi na ya utapeli ni yepi
 
Ukienda pale ukiwa uneoa hiyo ndoa ni halam kwahiyo inafutwa mnafunga nyingine
Hahaa kuna kanisa lingine nasikia ukiwa na watoto wa kuwazaa inabidi uwakane unapewa watoto wa kiroho ambao unawakuta mle kanisani hao ndio wanakuwa wa kwako unawalea unawasomesha yaani huku ndipo laana zinapoanzia ndio maana hatupati mvua
 
Siloam Church ni believers ambao wana ufahamu mkubwa sana, hoja za mtoa mada ni dhaifu. Pilipili ziko shambani, wewe zinakuwashia nini?
Yaani ningekuwa na uwezo nyie ni jipu na moja
 
Back
Top Bottom