Kwa fikra zangu naona hiyo ni dini ya kiyahudi. wayahudi walimuona Yesu lakini hawaamini katika yeye, ndio maana hakuna alama ya msalaba kwenye masinagogi yao.
Ndiyo maana wanatumia majina ya kiyahudi kwa viongozi wao kama kuhani n.k.
Kuhusu kalenda, kama hutambui ujio wa Yesu hata kalenda yetu ya kawaida hutaifuata. kalenda zetu za kawaida zinazingati mwaka wa kuzaliwa Yesu kuwa ni mwaka wa kwanza, hadi leo ni miaka 2017 toka kuzaliwa Yesu.
Wanatumia biblia sawa, lakini huenda wanazingatia agano la kale tu maana hilo hata Yesu alilikuta.
Dini ni njia ya iimani kwa Mungu wetu, Wakristu wanaamini ktk YESU na kwamba njia sahihi ya kwenda mbinguni ni kupitia kwake. waislam wanamini katika Mtume Mohamed (SAW). Hawa nao wako poa!