Pool of Siloam!
Hili kanisa ni moja kati ya makanisa ya kiroho lililo tofauti na makanisa yote ya kikristo. Ngoja nikupe story kidogo juu ya hili kanisa,
Mosi.... Hakuna popote penye ishara/alama ya msalaba kama ilivyo makanisa mengine ya kikristo, ndani ya majengo ya makanisa yao.
Pili... Kila mkoa Tanzania una jina lake, Kwa mfano Moshi panaitwa Ararati, Singida panaitwa Sayuni, Mwanza - Yericko,
Hata hapa DSM kila kitongoji kina jina lake, Mfano TABATA inaitwa, .... wanajua wenyewe
Tatu: Kiongozi wao anaitwa MUNGU WA MAJESHI- MIAKA 1000 , wanamwabudu kama mungu, wanaamini hata huwezi kumuona
Nne: Mwanzilishi wa hilo kanisa , alikuwa anaitwa Munuo (Mmachame), alifariki mwaka juzi bila kukosea, akazikwa huko Bagamoyo, wanasema alipaa mbinguni kama Yesu, hata vyombo vya habari ya CNN , BBC vilionyesha. Ajab hakuna local media hata moja iliyoripoti tukio kubwa kama hilo.
wachungaji wengi wa hilo kanisa ni Wamachame
Tano: Biblia yao haina kava la juu, wameweka lakwao, kila siku wanabadili na kupunguza mistari kwenye biblia, MUNGU WA MAJESHI anasemu MUNGU wetu aliye hai ndie kamwaguza kufanya hivyo. Kwa kifupi biblia yao ina viaraka
Sita: wanaposali /wakiwa kwenye maombi wanatingisha vichwa , na kubana sauti inakuwa kavu hatari. Kama ni mara ya kwanza kwenda hapo, huwezi kusikia chochote.
Saba: waumini wao wana hali mbaya sana kiuchumi.
Nane: Hawatumii miezi yetu, sijui February, Janurary au March , wao miezi yao ni Zifa, n.k
Ukienda hapo utastaajabu....