Sinagogi hili la Siloam Ministries

Sinagogi hili la Siloam Ministries

Mshana jr Hembu kama unaelewa utupe historia kidogo eti lile hekalu pale nyuma ya petrol station ya pale kinondoni Morocco huwa wanasali watu gani na siku gani na ibada zao zipoje unaruhusiwa kwenda mtu yeyote au kwa watu maalum na huwa linaitwaje
Na pale victoria sheli pia kuna kanisa, kama kuna aliyewahi sali pale atujuze pia
 
Mshana jr Hembu kama unaelewa utupe historia kidogo eti lile hekalu pale nyuma ya petrol station ya pale kinondoni Morocco huwa wanasali watu gani na siku gani na ibada zao zipoje unaruhusiwa kwenda mtu yeyote au kwa watu maalum na huwa linaitwaje
Ile ni sect ya freemason lilianza kujengwa miaka ya tisini mwishoni na kukamilika early 2000
 
Pool of Siloam!

Hili kanisa ni moja kati ya makanisa ya kiroho lililo tofauti na makanisa yote ya kikristo. Ngoja nikupe story kidogo juu ya hili kanisa,
Mosi.... Hakuna popote penye ishara/alama ya msalaba kama ilivyo makanisa mengine ya kikristo, ndani ya majengo ya makanisa yao.

Pili... Kila mkoa Tanzania una jina lake, Kwa mfano Moshi panaitwa Ararati, Singida panaitwa Sayuni, Mwanza - Yericko,

Hata hapa DSM kila kitongoji kina jina lake, Mfano TABATA inaitwa, .... wanajua wenyewe

Tatu: Kiongozi wao anaitwa MUNGU WA MAJESHI- MIAKA 1000 , wanamwabudu kama mungu, wanaamini hata huwezi kumuona

Nne: Mwanzilishi wa hilo kanisa , alikuwa anaitwa Munuo (Mmachame), alifariki mwaka juzi bila kukosea, akazikwa huko Bagamoyo, wanasema alipaa mbinguni kama Yesu, hata vyombo vya habari ya CNN , BBC vilionyesha. Ajab hakuna local media hata moja iliyoripoti tukio kubwa kama hilo.

wachungaji wengi wa hilo kanisa ni Wamachame

Tano: Biblia yao haina kava la juu, wameweka lakwao, kila siku wanabadili na kupunguza mistari kwenye biblia, MUNGU WA MAJESHI anasemu MUNGU wetu aliye hai ndie kamwaguza kufanya hivyo. Kwa kifupi biblia yao ina viaraka

Sita: wanaposali /wakiwa kwenye maombi wanatingisha vichwa , na kubana sauti inakuwa kavu hatari. Kama ni mara ya kwanza kwenda hapo, huwezi kusikia chochote.

Saba: waumini wao wana hali mbaya sana kiuchumi.

Nane:
Hawatumii miezi yetu, sijui February, Janurary au March , wao miezi yao ni Zifa, n.k

Ukienda hapo utastaajabu....
3580a8ecd71e0d75d0f9d36fa648ecae.jpg
 
Shika neno tenda neno mtumishi, ukiwa wa imani tofauti hata salamu hupati na wanaoana wao kwa wao, ukimtaka mtumishi lazima ukasali kanisani kwake na uvae kanzu/gauni jeupe na ushinde kanisani siku nzima
Ukienda pale ukiwa uneoa hiyo ndoa ni halam kwahiyo inafutwa mnafunga nyingine
 
Kuna jamaa yangu kakimbilia huko alikuwa mlutheli,sasa ukimpigia simu ukitaja jina lake anakata simu then anakutumia sms anakwambia mimi naitwa nuru huyo unayemtaja ni mdudu gani simfahamu!
 
Back
Top Bottom