By Samuel jk_Euphoria
SOLO KING: ANCIENT LEGACY
CHAPTER 23: Mimi sio mtu mbaya
Upande mwingine ndani ya chumba kwenye kitanda kikubwa chenye inchi themanini na nne urefu na upana Bianca alikuwa amekaa kitandani akiwa katika hali ya mawazo
Chumba chake kilikuwa ni kikubwa kilichosambaa harufu nzuri ya kike, kulikuwa na shelve la vitabu mbalimbali, kulikuwa pia na masofa ya bei ghali, upande wa dirishani kulikuwa na piano kubwa ya mbao, japokuwa hakukuwa na viyu vingi sana licha ya ukubwa wa chumba lakini kilipambwa kikike zaidi na kupambika.
Bianca alikuwa amekaa akitulia tuli akitazama dhini, kwa jinsi alivyoonekana alikuwa ni mpweke sana na alitia huruma haswaa
Alinyanyua kichwa chake na kutazama upande wa dirisha kubwa la kioo kama ukuta, macho yake yalikazia ile piano kubwa ya mbao. Taratibu alinyanyuka na kutembea kuisogelea piano ile na kisha kukaa kwenye kistuli mfano wa benchi dog
Aliipitisha mikono yake juu ya kinanda kile cha mbao kwa mtindo kama wa kuburuza ni kama vile ameimisi sana na alisitisha mara baada ya macho yake kutua kwenye sehemu ambayo "sheet music" iliyojaa alama za muziki hupatikana, ni ile sehemu ya juu katikati ya kinanda
Lakini sehemu hiyo hakukuwa "sheet music" bali kulikuwa na karatasi nyingine ngumu na katika karatasi hiyo kulikuwa na sanaa ya uchoraji ikidhihirika, ilichorwa mwanaume na mwanamke kwa ustadi wa hali ya juu sana, ulikuwa ni mchoro wa viwango vya kimataifa kiasi kwamba ilionekana ni kama vile picha imepigwa
Mwanaume aliyexhorwa alikuwa ni Jimmy na hakika mchoraji hakukosea alimpatia haswaa na hakukuwa na kasoro yoyote vivyo hivyo kwa mwanamke aliyechorwa ambaye ni Bianca
Walikuwa katika pozi la kirafiki sana pengine ungedhania labda ni wapenzi, walikuwa wamesimama Bianca akimgeukia Jimmy na kumkumbatia ubavu huku mguu moja akiunyanyua na kuukunja, mkono wake akiwa ameunyanyua na kuusogeza karibo na uso wake uliopendezeshwa na tabasamu akiweka ishara ya amani, yaani vidole viwili(shahada na cha kati) vikisimama na vingine vikiwa vimekunjwa na mkono mwingine alkiupitisha kwenye bega la jimmy ambaye naye alikuwa katika tabasamu na pozi linaloendana vizuri na pozi la Bianca, vichwa vyap vilikuwa karibu kiasi cha mashavu yao kugusana.
Huo ndio ulikuwa mwonekana wa mchoro uliokuwa kwenye karatasi ambalo Bianca alikuwa akilitazama.
Aliupeleka mkono wake na kuishika ile karatasi upande wa mwaume na kuachia tabasamu la upole sana.
Mchoro huo ulikuwa ni picha waliyoipiga miaka mitano nyuma kabla ya kuondoka kwenda masomoni nchini Uingereza. Na alipokuwa uingereza alikutana na rafiki ambaye kazi yake ilikuwa ni kuchora na kumuomba amvhoree picha hiyo na kumlipa kabisa.
"Unaona mmh" aliongea kwa sauti ya upole akiangalia mchoro huo
"Upendo wamgu kwako ulikuwa na wa kunishangaza sana, sikuelewa ulitokana na nini nilipenda ghafla tu kama cheche itokezayo kwenye giza totoro pasipo kujua chanzo, moyo wangu ulikupenda siku ya kwanza mukuona kwa macho, na nilikupenda zaidi nilipokuona ukicheza moonlight sonata na nilizidi kukupenda mara kumi yake uliponiokoa mimi na kaka yangu katika tukio. Ni kama vile nafsi yangu ilikutambua bila hata mimi kujua" aliongea kwa utulivu kisha kunyamanza akiendelea kukazia macho mchoro
"Like a song I’d never heard before, but somehow knew all the lyrics. Like waking up one morning and the sky just felt bluer, the air so sweeter, But why?" aliendesha akimaanisha "Ni kama wimbo ambao sikuwahi kuusikia hapo kabla lakini kwa namna fulani nilijua maneno yake. Kama vile kuamka asubuhi moja na kuhisi anga kuwa safi, hewa tamu, lakini kwanini?"
"Kwanini uliondoka? Kwanini? Kwanini hukuitimiza ahadi? Au kwasababu ulishaijua siri yangu kabla sijakwambia? Mmmh?" alikuwa akiuliza maswali mfululizo kana kwamba huo mchoro ndio Jimmy halisi
Baada ya kuongea hivyo aliutoa mkono wake kwenye karatasi na kunyanyua mkono mwingine kisha yote aliielekeza kwenye keys za piano hiyo
Taratibu alianza kuibonyeza bonyeza kwa utulivu na kwa ustadi sana, haikuwa haraka haraka bali ni polepole na mpangalio wa sauti nzuri sana ulisikika, japokuwa hakubobea sana kwenye kucheza piano lakini mziki huo ulikuwa na ubora
Uzuri chumba hiko kilikuwa ni sound proof hivyo sauti ziliishia humohumo. Baada ya kama dakika tano za sauti kusambaa chumba kizima hatimae alisitisha kucheza na chozi lilianza kumdondoka na haraka haraka alifuta
°°°°°°°°°°°
Jimmy alikuwa akijiambia "kuna nini kwani mbona ananiangalia sana huyu manzi" huku akipeleka mkono wake wa kulia nyuma ya kisogo na kukikuna
"Kuwa na amani bibie, pia manzi kama wewe kumkata jicho mtu bila sababu haipendezi unaonaje ukitabasamu
" Koma kuniita kuniita bibie na leo ni mwanzo na mwisho kuniita hivyo, tumeelewana?"
"Nimekuelewa bibie" aliongea Jimmy huku akimtolea tabasamu
"Yaani wewe.... Laiti ungejua nini kinakwenda kutokea kutokea baadae usingethubutu kufanya ukatili" aliongea huku amekunja sura yake kana kwamba amemeza dawa chungu
"Ukatili gani kwani mi nilichofanya ni kuwafunza jinsi ya kuwa na heshima kwenye nyumba za watu anyway nina njaa sana" aliongea na kumpotezea Zuhura na kwenda zake uelekeo wa jikonina kuwakuta Sandra na Aisha wakimalizia kuandaa cha kula
Zuhura aliishia kumsindikiza na macho mwanaume huyo mpaka anapotelea jikoni na kutingisha kichwa kwa masikitiko, kisha aliwapa ishara wenzake waondoke, wale walinzi wawili kufafa maagizo tu pengine utadhani ni mabubu maana muda wote ni kimya tu hata kupiga chafya hakuna! Ni kimyaaaa.
"Kuna kitu unataka Sir?" aliongea Sandra kwa wasiwasi alipomuona Jimmy ameingia Jikoni
Ukweli ni kwamba Sandra na Aisha walishuhudia kila kitu kilichotokea sebuleni na vile tu hawakuwa na ujasiri wa kujitokeza na kuangaliza ni vile vitabia vya wadada kupenda umbea ndio viliwafikisha huko, waliposikia sauti ya kofi tu iliwashtua na kutaka kujua kulikoni.
Kitendo cha kushuhudia, Jimmy akiwavunja wageni miguu bila wasiwasi wala hati ilihali na yeye ni mgeni kiliwafannya wamuogope. Ni jana tu hapo alikuja na ni mtoto wa boss wao mkubwa(mwanamama Mary) lakini waliweza kushudia upande wake mwingine. Walijiuliza itakuwaje huko mbeleni wakimkasirisha? Je atawavunja miguu? Kufikiria hivyo ilikuwa ni haki yao kuwa na hofu
Jimmy aliweza kujua wasiwasi wake unatokana nini na alitaka kumtoa wasiwasi maana uwepo wake utawafanya wasiwe na amani kila siku na hakutaka iwe hivyo
"Nina hamu tu ya kula matunda" aliongea Jimmy kirafiki
"Una njaa? Bado kidogo tu tunamalizia utuvumilie kidogo" aliongea Sandra kwawasiwasiwasi na kufanya vitu haraka haraka
"Aisha muandalie bwana mdogo matunda" Sandra alimwambia mwenzake huku akiendelea na shughuli ya kuandaa msosi haraka haraka
Naye Aisha haraka haraka alisogelea friji na kulifungua na kutoa matufaa manne na kisha kuyaosha na kuanza kuyakatata
Jimmy alikuwa hajui nini cha kufanya, alitamani kucheka lakini hakuthubutu kufanya hivyo na alisubiri mpaka Aisha alipomaliza kumuandalia na kumpatia sahani iliyojaa vipande vya matufaa na alipokea kisha taratibu alianza kuondoka
Alipoufikia mlango wa jikoni alisimama na kuwageukia vijakazi wale nao walimwangalia wakijua anataka kuwaambia kitu
Jimmy alitoa tabasamu la kirafiki na kuongea
"Kuweni na amani, mimi sio mtu mbaya" kisha alichukua kipande cha tufaa na kukipeleka mdomoni na kugauka kuondoka zake
Upande wa Sandra na Aisha waliishia kumuangalia akiondoka na angalau nafsi zao zilitulia ni kama sauti ya Jimmy yalikuwa na nguvu flani hivi ya amani ndani yake na ilipowafikia masikioni walitulia na ule uharakishaji wa mambo wakaacha na kuendelea na kumalizia kuandaa bila wasiwasi
Jimmy alikwenda kukaa zake sebuleni kwenye sofa na kula vipande vya tufaa huku akitazama runinga kubwa iliyoko mbele ya macho yake na muda huo ilikuwa ikionyeshwa taarifa ya habari.
Kichwa cha habari kwenye runinga kilikuwa kikisomeka VIFO VYA KUTATANISHA NA UPOTEVU WA RAIA MKOANI TANGA
Na katika skrini alionekana mwanamke mtu mzima mweusi wa ngozi akivalia miwani ya macho
"Habari za mchana. Tunakatiza matangazo ya kawaida kuwaletea taarifa ya dharura kutoka mkoa wa Tanga. Ripoti zinaeleza juu ya matukio ya kutoweka kwa watu na vifo vya ajabu katika kijiji kidogo kilichopo ndani kabisa ya msitu, katika Wilaya ya Tanga" aliongea na sauti yake yenye kusikika vyema
"Kulingana na vyanzo vya ndani, ndani ya saa arobaini na nane zilizopita, watu zaidi ya kumi na wawili wametoweka. Mamlaka zimethibitisha kuwa miili mitano imepatikana yote bila majeraha ya wazi, lakini ikiwa imetokwa damu yote." aliendelea na kisha kuonyeshwa raia mbalimbali wakitoa maoni
" Hawana majeraha… lakini wanakufa ghafla… kama wamekamatwa na pepo" aliongea mkazi mmoja kwa sauti ya kutetemeka
"Kila siku usiku watu wanapotea. Tunahisi kuna kitu kinaishi gizani.” aliongea mwingine na kisha mtangazaji alionyeshwa tena
" Jeshi la Polisi limeanzisha uchunguzi, lakini hadi sasa wameshindwa kuelewa kilichotokea. Wengine wanaamini huenda ni kazi ya kundi la ibada haramu au virusi visivyojulikana. Lakini wengine wana hofu… ya kitu kibaya zaidi.”
"Wakazi wanashauriwa kukaa ndani baada ya jua kutua, na kuripoti matukio yoyote ya ajabu. Kwa sasa, eneo hilo limewekwa chini ya uangalizi mkali. Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kuhusu tukio hili kadri linavyoendelea. Tanga pamekuwa mahali pa utulivu kwa muda mrefu… lakini hivi karibuni kumekuwa na hofu .”
Kisha taarifa ya habari ikatoweka na kurudishwa kipindi kilichokuwa kikionyeshwa hapo kabla.
Jimmy alikuwa akila vipande mpaka vikaisha na baada ya habari kutoweka alianza kutafakari juu ya suala na palepale alikumbuka kuhusu wale viumba wanywa damu aliowashuhudia miaka tano iliyopita na palepale alipata majibu juu ya utata wa vifo
"Ina maana wale mashetani bado wapo wanaranda ramda wapendavyo" alijiwazia Jimmy kisha kupotezea
Harufu ya chakula kitamu ambacho maandalizi yake yalikamilika na kuwekwa mezani tayari kwa kula ililisumbua tumbo lake ambalo halikuridhika na matunda
Hakutaka kuendelea kuteseka na njaa na aliachana na kutazama runimga na kusimama kuelekea kwenye "dining table" lakini kabla hajafika aliweza kumuona mrembo Bianca akishuka chini kwenye ngazi
Alikuwa amebadili nguo na kuvaa kinyumbani zaidi alikuwa amevaa t-sheti kubwa oversize rangi nyeupe na kikaptula kifupi kilichoacha mapaja yake meupe wazi, pia alikuwa akinukia harufu nzur sana, haikueleweka ni marashi ya aina gani lakini yaliifurahisha pua ya kila mwenye kuinusa
Kama mwanaume alianza kupatwa na hisia na mawazo ya ajabu ajabu kichwani mwake kiasi cha kusahau kama alikuwa ana njaa muda huo
"Unazubaa nini?" ilikuwa ni sauti kutoka kwa Bianca na kumtoa Jimmy kwenye mawazo ya kikuda
"Nashangaa uumbaji wa Mungu na ujuzi wake katika hakika hakukosea ni alitumia muda mwingi na kwa umakini mkubwa kukuumba" aliongea Jimmy bila aibu
"Unafiki tu unadhani sijui unachokiwaza kichwani mwako? Halafu sio kama hujawahi kuona mwanamke"
"Hata kama nimeona lakini kwako nikikutazama ni kama ndiyo mara yangu ya kwanza" aliongea huku akitabasamu
"Sitaki kusikia ujinga wako" aliongea Bianca na kumpita. Jimmy alifumba macho kuisikilizia harufu nzuri ya mwanamke huyo alipompita karibu yake na kujiambia "Asee kwa staili hii sidhani kama nitaweza kuvumilia kadri siku zitakavyosonga" na kuelekeza macho yake chini mpaka katika ya mapaja na mwanajeshi wake alikuwa tayari ameshajipanga kwa vita lakini kwa bahati mbaya hakukuwa na vita
Uzuri singlendi yake ilikuwa kubwa na kusitiri hali ile na kufanya iwe ngumu kugundilika na hilo alishukuru alijiambia ingekuwaje kama angevaa shati na kuchomekea? Si angeonekana ni kitombi?
Basi naye alikwenda mezani kwa ajili ya kula, alipoketi vijakazi Sandra na Aisha walichukua jukumu la kuwapakulia maboss wao
Sandra kwa Jimmy na Aisha kwa Bianca na walipomaliza walitaka kuondoka lakini Jimmy aliwazuia
"Mmekula?" aliwauliza
"Hapana ndio tunaenda kula" Aisha alijibu
"Wapi, jikoni? Kwanini msiungane na sisi, chakula huwa ni kitamu zaidi kinapoliwa na wsmgi" Jimmy aliwakaribisha mezani na bila ubishi walikubaliana nae na kupakua chakula chao kisha kuka
"Vipi kuhusu walinzi hawali?" Jimmy aliuliza
"Wameshakula" alijibu Bianca bila ya kumuangalia, umakini wake ulikuwa kwenye chakula
"Ooh bila shaka itakuwa wana na ratiba yao ya kula wanapokuwa kazini lakini vipi kuhusu yule mzee pale getini" aliongea Jimmy
"Yule hana ratiba maalumu ya kula, ni muda wowote tu anakula hivyo tunamwekea chakula jikoni akiwa na njaa anapitia mlangovwa pili na kuingia jikoni kupakua chakula" Sandra alieleza na Jimmy alitingisha kichwa kumuelewa na sasa alianza kula
Ulikuwa ni wali, samaki mboga za majani na matunda mchanganyiko
Alichota kijiko kimoja cha wali na kukipeleka mdomoni na alipomeza tu ghafla kundi la watu watatu waliovalia sare za polisi waliingia ndani na kumfanya Jimmy akunje ndita na kulaani ndani kwa ndani
"Samahani kwa ujio wetu wa ghafla lakini tupo hapa kwa mtu anayeitwa jimmy" aliongea Inspecta kolo
"Ni mimi afande kuna shida kwani?" aliongea Jimmy
"Tafadhali ongozana na sisi mpaka kituo cha polisi una kosa la kumshambulia raia pasipo sababu pili ni unyanyasaji" aliongea inspekta kolo na kumpa ishara wa pembeni yakre kwenda kumpiga pingu Jimmy
"Hey kwanini msisubiri nimalize kula kwanza nina njaa ujue" aliongea Jimmy huku akipeleka kijiko kuchota wali mwingine na kuupeleka mdomoni
TO BE CONTINUED........