Roisa group
Member
- Aug 20, 2023
- 8
- 11
Mwandishi: ROISA.
Namba ya simu: 0694840213.
Riwaya: JE UNANIKUMBUKA MARIAMU? ( USIPOHUKUMIWA NITAKUHUKUMU MIMI).
sehemu ya 1.
Nilikuwa nimebana macho yangu, nikihisi ubaridi wa ajabu lakini uliambatana na mguso wa joto la blanketi zito la sufu. Harufu ya kwanza kuingia puani mwangu haikuwa ya maji machafu ya mto, bali ilikuwa harufu ya kipekee ya mitishamba iliyochemshwa, moshi wa kuni, na mafuta ya mawese.
Nilitaka kunyanyua mkono wangu wa kulia, lakini maumivu makali yalinichoma kuanzia begani hadi kwenye vidole, yakanifanya nitoe mguno mzito wa maumivu.
“Tulia... tulia mwanangu usijitikise,” sauti moja nzito, ya kizee, iliyosheheni utulivu wa aina yake ilisikika pembeni yangu. Ilikuwa sauti iliyobeba mamlaka ya asili na upole uliotuliza hofu yangu. “Umekuwa ukipambana na dhoruba kwa siku nyingi sana mwili wako bado haujajishikiza vizuri kwenye ulimwengu wa walio hai.”
Nilikaza misuli ya uso wangu na kujilazimisha kufumbua macho mwanga hafifu wa taa ya chemli uliingia machoni mwangu, ukifungua picha ya paa la nyumba iliyoezekwa kwa makuti ya minazi na kuta za udongo zilizokandikwa kwa ustadi.
Niligeuza kichwa changu taratibu kuelekea upande ulikotoka ule sauti alikuwa amekaa mzee mmoja, mwenye mvi nyingi zilizotawala kichwa na ndevu zake ndefu.
Macho yake yalikuwa madogo lakini yenye busara ya kipekee, na alikuwa amevalia kanzu rahisi iliyochakaa. Pembeni alikuwa akisaga majani fulani kijani kibichi kwenye kinu kidogo cha mbao.
“Mimi... mimi niko wapi?” Nilijaribu kuongea, lakini sauti yangu ilikuwa kavu na iliyokwama kooni kama mtu aliyekuwa anameza mchanga“Mimi ni nani?”
“ Nimefikaje hapa?” nilijaribu kuuliza kwa pupa sana, maana ni maeneo ambayo yalikuwa mapya kwangu na maumivu yale sikujua yalipotoka. Kichwa changu kilikuwa kama kompyuta iliyofutwa kila kitu isiwe na kumbukumbu au uwezo wa kutenda kitu chochote kile.
Yule mzee alishusha kinu chake chini, akatabasamu kwa upole uliodhihirisha meno yake machache yaliyobaki. Alichukua kikombe cha udongo kilichokuwa na dawa ya vuguvugu, akasogea karibu na kuninyanyua kichwa changu kwa umakini mkubwa, kisha akaninywesha kijiko baada ya kijiko.
Ilikuwa chungu sana nikatamani niiteme lakini ilikuwa na ladha iliyorejesha uhai kwenye mishipa yangu.
“Jina langu naitwa Mzee Juma,” alianza kusimulia kwa sauti ya utulivu huku akifuta matone ya dawa yaliyomwagika kidevuni kwangu “ hapa ni kijiji cha kilimo kilichopo pembezoni mwa Mto Ruvu, mkoani Pwani wiki mbili zilizopita, baada ya yale mafuriko makubwa yaliyoharibu madaraja na kusomba nyumba za mabondeni, nilikuwa natembea ukingoni mwa mto kuangalia mitego yangu ya samaki.
Hapo ndipo nilipouona mwili wako ulikuwa umenaswa kwenye mizizi ya mkoko mkubwa, ukiwa umelowa matope, nguo zako zikiwa zimeranduka, na ukiwa na jeraha kubwa la damu iliyoganda kichwani kwako.”
Mzee Juma alishusha pumzi ndefu, akitazama nje kupitia mlango mdogo wa nyumba hiyo ambapo milio ya wadudu wa usiku ilikuwa ikisikika.
“Kila mtu aliyekuona alisema wewe ni maiti na tulipaswa kukuzika pembezoni mwa mto. Lakini mimi, nikiwa kama mtu niliyeishi miaka mingi na kufanya kazi ya uganga wa asili na tiba kwa muda mrefu, nilihisi moyo wako ukiwa bado unadunda kwa mbali sana nilikataa kukubali kifo chako.
Nilikubeba kwa msaada wa vijana wangu hadi hapa nyumbani kwangu umekuwa kwenye koma, ukizungumza maneno yasiyoeleweka”
Nilimsikiliza Mzee Juma kwa makini, machozi ya namna fulani yalianza kunitoka bila mimi kujua sababu yake. “Mzee Juma... mimi sikumbuki chochote. Sikumbuki jina langu, wala nilitoka wapi, wala kwa nini nilikuwa kwenye ule mto.”
Mzee Juma aliweka mkono wake wenye mikunjo juu ya kifua changu. “Usiwaze kuhusu jana, mwanangu ,Jana imeshazama kwenye mto ule na maji yameenda nayo. Kama Mungu amekupa pumzi ya pili, ina maana kuna sababu ya wewe kuwa hai jeraha lako la kichwa ni kubwa, na ndilo lililofunga milango ya kumbukumbu zako. “
Kwa miezi kadhaa iliyofuata, maisha yangu yakawa chini ya uangalizi wa Mzee Juma nilikuwa nakunywa dawa za asili asubuhi na jioni, huku akisafisha kovu kubwa lililokuwa nyuma ya kichwa changu.
Mwili wangu ulianza kupata nguvu; nilianza kumsaidia mzee yule kazi ndogo ndogo za shamba la mpunga na kulisha mifugo yake michache.
Kijiji kile kilikuwa na utulivu usio na mfano, mbali na kelele na hila za miji mikubwa ingawa akili yangu ilikuwa tupu, nilikuwa na amani ya kipekee. Mzee Juma hakuwa tu mganga wangu, alikuwa kama baba niliyemkuta kwenye ulimwengu mpya.
Hata hivyo, kila nilipokaa chini ya mti wa mwembe jioni nikitazama maji ya mto yakitiririka, nilihisi kuna dhoruba kubwa iliyojificha ndani ya kifua changu inayosubiri kufunguliwa.
Nilisahau kila kitu katika maisha yangu ya nyuma na kuanza upya ila kuna kitu kilichokuwa kinanisumbua ndoto za kujirudia rudia ambazo kuna muda nilikuwa nikipiga kelele usiku ule. Hali ile iliendelea mpaka nilipokuja kutambua nini kilinifanya nifike hapa na kitu gani.
Mwaka mmoja ulipita tukiwa kwenye ule utulivu wa kijiji cha pembezoni mwa Mto Ruvu katika kipindi hicho chote, nilikuwa “Kijana”mtu asiye na jina, wala asiye na asili.
Nilizoea maisha ya jembe la mkono, harufu ya udongo ulioloa, na amani ya kukaa mbali na dhoruba yoyote ya kijamii.
Mzee Juma alikuwa amekuwa nguzo yangu ya maisha; alinifunza jinsi ya kusoma alama za asili, tabia za mito, na namna ya kuishi kwa kutegemea ardhi.
Lakini, akili ya mwanadamu ina tabia moja ya ajabu hata iandikwe karatasi nyeupe kiasi gani, wino wa zamani ukikolea, lazima utajitokeza tu juu ya uso.
Ilikuwa ni jioni moja ya Jumanne, baada ya mvua kubwa ya msimu wa masika kukata, Mimi na Mzee Juma tulikuwa tumekaa mbele ya moto wa kuni nje ya nyumba yake ya udongo, tukichoma mihogo mibichi na kunywa chai ya mchaichai.
Hewa ilikuwa safi, na sauti ya mto ikitiririka ilikuwa inasikika kwa mbali Mzee Juma alikuwa ameweka redio yake ndogo ya mbao, ile ya mbao iliyokuwa inatumia betri kubwa za kienyeji, juu ya kigogo cha mti. Ilikuwa imetegwa kwenye stesheni ya taifa, wakisoma habari za jioni.
Mimi sikuwa makini na yaliyokuwa yakitangazwa; akili yangu ilikuwa inatazama cheche za moto zilizokuwa zinaruka angani. Ghafla, sauti ya mtangazaji wa redio ilibadilika na kuwa nzito, akasoma taarifa ya uchunguzi maalum wa kiuchumi:
”Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imemkamata na kumsimamisha kazi aliyekuwa meneja wa TRA mkoa wa Mwanza, Mzee Thomas Mvungi, kwa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha, ukaguzi ghushi wa kodi, na kujilimbikizia mali kwa kutumia majina ya ndugu na mke wake”.
“Thomas mvungi?” ni kama vile nilishitushwa ghafula jina lile liliingia masikioni mwangu kama dhoruba ya radi iliyopiga ndani ya fuvu la kichwa changu.
Ndani ya sekunde hiyo moja, ukuta mweupe uliokuwa umeziba akili yangu kwa mwaka mzima ulibomoka na kupasuka vipande vipande.
Ni kama mtu aliyewasha taa ya ghafla kwenye chumba chenye giza nene Kumbukumbu zote zilifurika kwa kasi ya ajabu, zikigongana zenyewe kwa zenyewe.
“Mimi ni John!” Nilipiga kelele ya ghafla huku nikisimama na kuruka kutoka kwenye kiti changu cha mbao. Kikombe cha chai kilianguka chini na kupasuka. Mikono yangu ilikuwa inatetemeka, na jasho la baridi lilikuwa linanitoka kwa kasi ya ajabu.
“Mzee Juma! Mimi ni John! Mimi si Kijana wa hapa... Mimi nilikuwa Afisa wa TRA! Nilimsomesha! Nilimtoa kwenye umaskini, lakini akanigeuka na bosi wangu!”.
Mzee Juma hakushtuka alishusha redio yake taratibu,
akatazama macho yangu yaliyokuwa yamejaa mchanganyiko wa hasira, maumivu, na fahamu zilizorejea. Alisimama, akaja na kushika mabega yangu kwa mikono yake yenye mikunjo na hekima.
“Kaa chini, John,” aliongea kwa sauti ya chini lakini thabiti “Kaa chini mwanangu mwaka mzima nimekusubiri useme jina nilijua ipo siku kila kitu kitarudi na kumbukumbu zako zitarejea “
Niliketi chini huku nikizika uso wangu mikononi mwangu, nikilia kwa sauti ya juu machozi ambayo sasa hayakuwa ya wendawazimu, bali yalikuwa ya mtu aliyerejesha utu wake lakini akakutana na majeraha yake yakiwa bado mabichi.
Baada ya kuketi karibu yangu, Mzee juma alivuta kiti huku akinishika bega langu la kushoto “ unaweza sasa nieleza kwanini ulifika hapa?”
Itaendelea.....