By Samuel jk_Euphoria
SOLO KING: ANCIENT LEGACY
CHAPTER 17: unatuepuka
"Vipi kuhusu miili ya walinzi waliokufa?"
"Tunatoa taarifa kwa polisi kwamba wamekufa kwenye majukumu yao ya kulinda usiku na ni ukweli, kuhusu vifo vyao hatutasumbuliwa isitoshe kesi kama hizi za watu kufa usiku vifo vya ajabu hazijaanza leo wala jana"
Kesho yake baada ya kutoa taarifa ya vifo vya walinzi walianza mchakato wa kuwazika kwa heshima walinzi hao na baada ya kumaliza maisha yakaendelea
Siku zikakata, wiki kadhaa zikapita na hatimae mwezi mwingine ukaingia, katika siku hizo zote tangu tukio lile la kutisha hakukutokea kingine zaidi ya kuishi kwa amani na kuongeza umakini kwenye usalama, kifupi ni kwamba waliamua kusahau na kuendelea na maisha mengine
Na katika siku zote mpaka kufikia siku hiyo Jimmy aliishi kwa kujitenga sana, alikuwa akiamka asubuhi na mapema na kurudi siku, kesha yake tena hivyo hivyo mpaka siku hiyo, Tangu ashuhudie maajabu na kutaka kupoteza uhai kwa mara ya pili na kusaidiwa na kundi la watu asiowajua aliamua kuwekeza muda wake mwingi kwenye kuielewa nguvu halisi aliyorithishwa na mzee asiyemjua kwa undani zaidi ya utambulisho wake tu
Alikuwa akijifunza namna ya kuiamsha na kuicontrol, alikuwa akijiimarisha kimwili, kiakili, kihisia na kiroho pia kufuatia muongozo kitabuni na alizingatia umakini sana kwenye kujifunza
Alikuwa akilalamikiwa sana na nduguze kwamba amekuwa mtu wa kujitenga sana kibaya zaidi hakuwa na simu, tangu simu yake iharibike hakujisumbua kununua mpya kiufupi ni kwamba alikuwa akiwekeza muda wake kwenye kitu kimoja nacho ni nguvu. Alitaka kuwa na nguvu maana dunia ina mengi na hawezi jua nini kitawatokea huko mbeleni hivyo alihitaji kujiandaa ipasavyo ili kuweza kukabiliana na Changamoto zijazo
Sasa mwezi huo ulikuwa ni mwezi wa kuanza elimu ya chuo kikuu kwa upande wa Jimmy,licha ya ku-apply chuo na kufanikiwa lakini hakujiandaa kabisa ni kama vile hakujali sana kuhusu hilo
Ilikuwa ni siku ya mchana wa saa sita na siku hiyo jimmy hakutoka zaidi ya kujifungia chumbani kwake asirleweke anafanya nini
"We J unafanya nini huko chumbani?"aliita mams yake kwa kifupi lakini hakukuwa na jibu lolote
"We Jimmy si nakuuliza?" aliita tena na alipoona kimya aliingia chumbani kwa wasiwasi lakini aliishia kumkuta Jimmy ameketi chini ya sakafu amekunja miguu mbele yake kukiwa na kitabu kilichofunguliwa kurasa kadhaa
Alikuwa amefumba macho na mdomo wake kucheza ksma vile anasali kwa kurudia rudia maneno, alikuwa ametulia kama uso wa bahari usio na upepo
Kwa picha alilolishuhudia mama yake alibaki kushangaa tu na kujiuliza huyu mtoto anafanya nini?
"Wewe mtoto yaani mimi nakuita wewe upo umekaa hapo chini ukipiga kimya tu, kwanza unafanya nini?" aliongea na sauri yenye lawama lakini bado mwanaye alikuwa kimya tu
Alisogea karibu yake na kuchukua kitabu kilicho cbini lakini aliishia kukunja sura tu baada ya kukutana na maandishi ya ajabu
"Umeanza lini uganga? "
"We Jimmy... Jimmy, we Jimmy" alikasirika baada ya kuona bado yupo kimya, uzuri kabla ya kuja hapo alikuwa jikoni akiandaa vitu kwa ajili ya kupika cha mchana na alikuwa amebeba mwiko, Alinyanyua mwiko na kutaka kumpiga nao begani kumshtua kwenye kile anachokifanya lakini kabla hata mwiko haujatua kwenye bega Jimmy aliudaka na kisha kuvumbua macho
"Naam mama unasema?" aliongea akiachia tabasamu usoni
"Kwanza kwanini nakuita hunisikii?" aliuliza
"Hapana nilikusikia cyema tatizo nilikuwa nasali" alijitetea
"Sala gani hii unakaa chini na mkitabu wa ajabu ajabu kwanza hiki ni nini? Usiniambie umeanza uganga"aliongea mama yake akitaka maelezo kuhussu hiko kitabu
" Usiwaze sana mwanao siwezi kuwa mganga kuhusu hiko kitabu, hiko ni kitabu cha hadithi ni vile tu wswe ni mshamba wa lugha" aliongea
"Kwanza sitaki kusikiliza hizo ngojera zako, nilikuwa na wasiwasi nilipoona upo chumbani muda wote ila kumbe wasiwasi wangu ni wa bure tu"
"Halafu kaka yako amenipigia simu anakuja"
"Nani, Cid?"
"Tena anakuja na Bianca uwape maelezo kwanini hupatikani, umekuwa ukiwaepuka na hata kuwatembelea"
"Cid si nilimwambia sina simu? Halafu sio kama nawaepuka" aliongea Jimmy, ukweli ni kwamba alikuwa akijua Cid na Bianca walikuwa wakitaka awafundishe kutumia ala za muziki na yeye alikuwa akijikita kwenye kitu kingine ambacho aliona nj muhimu zaidi kukizingatia na sio kwamba alikuwa akiwaepuka ni kutoka kwake asubuhi na kurudi usiku asieleweke ametoka wapi ndio kulimfanya aonekane kama anawaepuka.
Walikuwa wakifika mara kadhaa hapo kwao kwaajkli yake kila mmoja kwa wakati wake na wasimkute na hata waliposubiri mpaka giza linaingia hakuwa amerudi hivyo ilikuwa ni haki yao kusema wanatengwa. Ilifika wakati mama yake alikuwa akimpigia makelele kwa kuchelewa kwake usiku na kuwasubirisha mpaka alichoka hata hivyo Jimmy alikuwa mtu mzima aliishia kumuacha aendelee na mambo yake huku akiombea kimoyomoyo awe salama
"Utajijua mwenyewe yaani mtu mwenyewe hujali wala nini, kwani kununua simu ni ghali?"
"Sioni umuhimu wa kununua simu"
"Unasemajr? Yaani unatuacha na presha kuhusu usalama wako na hatujui umeennda wapi hata kupiga simu tu nafsi itulie ni ndoto, na unasema huoni umuhimu akili zako ni kama za baba yako tu ebu nikuache mie mambo yako utayajua mwenyewe" aliongea mama yake na kuondoka, aliona ataishia kupoteza muda na kijana wake ambaye hata hajali kuhusu simu, alikuwa na kazi ngumu sana ya kuwalea watoto wake.
Jimmy aliishia kumtazama mama yake akitoka chumbani na tabasamu usomi na mara alisikia chafya ikipigwa nje ya chumba chake na aliishia kusema "Bless you mama"
°°°°°°°°°°
Upande mwingine makao makuu ya jeshi la nchi ndani ya ofisi ya mkuu wa majeshi alionekana Jenerali John ameketi kwenye kiti katika hali ya mawazo uso wake ukielekea dirishani
Ghafla mlango ulifunguliwa na aliingia Luteni Jenerali Mwachitete ndani ya ofisi hiyo na ujio wake haukumshtua Jenerali katika hali ile ya mawazo ilionekana alitegemea ujio wake
"Una uhakika ni yeye?"
"Ndio ni yeye na kuna haja ya kutengua na kuteua upya kila ngazi kwenye usalama wa taifa?"
"Kuna ulazima?"
"Ww unadhani kwanini wale wapuuzi wameingiaje nchini bila kushtukiwa? Ni kwasababh kuna pandikizi"
"Wakina nani? Wale maninja au unazungumzia wale wapumbavu waliotaka kuwaua watoto wako?"
"Na kakikundi ka wahuni kutoka somalia kuja kutibua amani nchini, na kwa uimara wa jesho letu na ulinzi wangenaswa kitambo sana lakimi ikawa tofauti, mpaka wanakuja kusababisha maafa ndio tunaamka kutoka usingizini kwa hili tumefeli sana"
"Hilo niachie mimi nitadili nalo upesi pia shukrani ziende kwa kijana vinginevyo ingekuwa ni habari nyingine"
"Vijana siku hizi hawajui hata ni nini kizuri kwao amekataa kabisa kujiunga na jeshi na ninaheshimu uamuzi wake"
"kwahiyo baada ya kutoa maelezo yote....." aliongea Luteni Jenerali lakini kabla hajamaliza Sentensi yake Jenerali alitoa ishara ya mkono kuelekea shingoni kwake akimaanisha kwamba amewaua ni kama alikuwa anajua mzee mwenzake alikuwa anataka kusema nini
"Washenzi kama wale hawafai hawafai kuwepo kwenye uso wa dunia" aliongea Jenerali John kwa ukauzu akimaanisha wale wahuni waliotaka kutelekeza mauaji ya wanawe
"Pia wale maninja wa yami no senshi wamefanikiwa kutoroka nchini bila kukamatwa" aliongea Luteni Jenerali Mwachitete
"Ndio maana nikasema kuna haja ya kupanga safu upya, kuna vijana wapo kule kulamba maokoto na sio kulitumikia taifa"
°°°°°°°°°°
Jimmy mara baada ya kumaliza ile alixhokuwa akikifanya alitoka zake chumbani na kwenda sebuleni, kama bossi alikaa kwenye kochi miguu yake akiinyosha kwenye meza iliyokaribu, mkononj akishika rimoti ya king'amuzi cha azam na kila baada ya sekunde kadhaa alikuwa akibadili channel
Hakukuwa na channel yenye kuonyesha kipindi cha maana na aliona bora kwenda kumsaidia mama yake aliyekuwa jikoni akikatakata mboga akiandaa vya kupikia chakula cha mchana
"Mama, unahitaji nikusaidie!?"
"Ooh ni nadra sana kukuona unakujza jikoni kusaidia kulikoni?"
"Kwani lazima nimsaidie mama yangu nikiwa na sababu? Hata hivyo nimeboreka ni bora angalau kufanya kitu kuliko kuzubaa tu"
"Hmm! Sio mbaya kata vitunguu" alimpa vitunguu na kisu na mdogo mdogo alianza kukata
"Aisee macho yashaanza kuwasha tayari, hivi unavumiliaje haya mateso kila siku?" aliongea Jimmy
"Nishazoea, wewe ni mwanaume tayari jikaze utazoea" "
"Nikija kupofuka lawama zije kwako" alitania akiendelea kukata vitunguu
"Lione kwanza ebu endelea kukata!" alitabasamu
"Kwahiyo tunapika nini leo?" Jimmy aliuliza
"Chakula chako pendwa, mchuzi wa nyama wenye viungo na wali"
Wakati maongezi kati ya mama na mwana yakiendelea huko jikoni mlango wa sebuleni ulisikika ukigongwa na Jimmy alisitisha msaada wake Jikoni na kwenda kuuufungua mlango
Uso kwa uso na sura anayoifahamu huku nyuma ya hoyo sura kukiwa na sura nyingine anayoifahamu, zote zikiwa hazina hisia zozote baada ya kumuona Jimmy
Jimmy aliishia kutoa tabasamu flani hivi na kuwakaribisha ndani
"Karibuni ndani wapendwa msiishie kusimama nje" aliwakaribisha na Cif aliishia kutoa tabasamu la uchungu na kuingia huku Bianca akiwa na sura ya ukauzu
Wote kimya kimya waliingia ndani na kwenda kuketi kwenye makochi.
"Jisikieni huru kabisa hapa ni nyumbani kwenu pia" aliongea Jimmy
"Mnakunywa kinywaji gani ndugu zangu? Kuna juisi mbili za matunda kwenye friji, kuna embe na passion, mtapendelea kunywa nkni" aliendelea, yaani kwa jinsi alivyokuwa akiongea ji kwa unyenyekevu kana kwamba ni mara yake ya kwanza kukutana nao
Upande wa jikoni mama yake aliishia kumsikitikia tu
"Haina haja ya kutusahaulisha bro ila mimi niletee juisi ya embe" aliongea Cid akishaudtukia mchezo wa Jimmy
"Vipi Bianca na wewe..." alimuuliza lakini aliishia kukutana sura yenye kutia huruma kana kwamba amemkosea na hakujibiwa chochote zaidi ya kuangaliwa
Alijiongeza tu na kwenda kuleta glasi mbili za juisi na kuwapatia na alipatwa na ahueni baada ya Bianca kupokea pia
" Yo ebu utuambie umekuwa ukitukwepa kwa wiki kadhaa sasa",aliongea Cid baada ya kunywa pafu moja la juisi
"Tumekukosea nini bro mbona unatuepuka?"
"Sio kuwaepuka ni vile tu nimekuwa na mambo mengi"
"Mambo mengi karibia mwezi mzima? Hata kwenye simu hupatikani*
"Bro si nilikwambia sina simu au umesahau?"
"Unazingua sana bro yani simu tu unashindwa kununua? Anyway mimi sina neno unapaswa kuhakikisha huyu binti anakwenda masomoni" aliongea Jimmy akimnyooshea mkono Bianca ambayr muda wote alikuwa akimtazama Jimmy na hakujisumbua kunywa juisi zaidi ya kuishika tu
"Hnamaanisha nini?"
"Sikia huyu amegoma katakata kwenda chuo kuanza masomo rasmi kwa kisingizio cga kutaka kukuona" alieleza na Jimmy aliishia kushangaa tu na kumuangalia Bianca, na alipokutanishamacho mrembo huyo alikwepesha na kuangalia pembeni
"Ilitakiwa mwezi uliopita mwishonu aanze safari ya kwenda Uingereza kuwasili chuoni ila ona sasa uliyoyasababisha" Cid alimlaumu kana kwamba Jimmy ndiye aliyemzuia asiende masomoni
Bianca alinyanyuka na kutoka nje akiwaacha wenzake kwenye mshangao wakiangaliana wao kwa wao, upande wa mama yake alikuwa anasikia kila kitu na alikuwa akitabasamu tu huku akiendelea na shughuli yake ya kuandaa msosi
Lakini mara baada ya kusikia hatua za mtu akiondoka haraka haraks alihisi itakuwa Bianca na alikuwa sahihi, alitoka jikoni na kwenda sebuleni na kukuts Vijana wawili wakiangaliana tj
"Wewe mtukutu ebu nenda ukayamalize na binti yangu" aliongea huku akimfukuza na mwiko na Jimmy hakuwa ns jinsi zaidi ya kumfuata Bianca guko nje
"Shikamoo bi mkubwa nilihisi utakuwa jikoni unapika maana si kwa harufjmu hii kumbe nilikuwa sahihi"
"Haha marahaba mwanangu, vipi huko nyumbani mnaendeleajd?"
"Kama kawaida majukumu yamezidi leo nduo tumepata nafasi nhingind kuja kuwasalimia"
"Karibuni tena jamani*
" Tumeshakaribia, leo usiwaze tumekuja na matumbo empty kabisa"
"Haha kwakweli, lazima nihakikishe mnakula na kunisifia mapishi yangu" aliongea huku akicheka
"Sio mbaya nikija kukusaidia?" aliuliza Cid huku akijiambia anapaswa kujenga mahusiano mazuri na mama mkwe ajaye maana alimwelewa sana Monica
Upande wa mama mkwe ajaye hakuwa mtu wa kufikiria sana na alomkaribisha kwa tabasamu, Cid aliishia kufurahi moyoni na kuvua koti lake akibaki na T-sheti jeupe, alijiambia anapaswa kutupia maneno ya ucheshi huko jikoni kumfurahisha mama mkwe wake ajaye
Upande wa nje Jimmy mara baada ya kutoka alikimbilia upande wa ngazi na kushuka chini mpaka kwenye uwanja kabisa wa Apartment yao
Na Bianca alikuwa amesimama karibu na gari akimpa mgongo
"Bianca..." Jimmy aliita na mara baada ya mrembo huyo kusikia sauti ya mwanaume huyo ikimuita aligeuka na kutazamana macho kwa macho
Sekunde mbili si nyingi mrembo huyo machozi yalianza kumtoka na kuangua kilio cha kwikwi kama mtoto mdogo aliyeachwa na mama yake, Jimmy alikuwa akijiuliza amemkosea nini lakini hakuwa na jibu na badala yake alimsogelea karibu na kumkumbatia
TO BE CONTINUED..........