Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

BY Samuel jk_Euphoria

SEASON 2

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 31: Revenge

MIAKA MITATU NYUMA, JAPAN

Kuna mkusaanyiko wa visiwa 14,125 ambavyo huunda nchi ya japan, lakini vilevile kuna visiwa vitano vikuu ambavyo ambavyo huitambulisha nchi hiyo kimataifa, Tukiachana na hivyo visiwa vitano katika maelfu ya visiwa kulikuwa na kisiwa kimojawapo kilichojitenga mbali na visiwa vingine

Kilikuwa na ukijani uliopitiliza na mazingira yake yalivutia na kupendeza macho, katika kisiwa hiko kulikuwa na miti mingi kiasi kwamba ilikuwa ngumu kujua kama kuna watu walikuwa wakiishi kisiwani humo lakini katikati ya kisiwa hiko kulikuwa na uwazi mkubwa sana kama mita 80,000 za mraba na eneo hilo la uwazi kulikuwa na uzio mkubwa uliozunguka na katika geti kubwa la kuingilia kulikuwa na bendera nyeusi yenye chata isiyoeleweka na maandishi mekundu ya kijapani

Naam maandishi hayo yalikuwa na maana ya warriors of darkness kwa lugha ya kingereza na hapo ndipo yalipo makao makuu ya kundi daraja B la kininja la Yami no aenshi na ndani ya uzio huo kulikuwa na majengo mengi ya kitamaduni, bustani nzuriza kuvutia na miti mingi ya "cherry blossom" au "sakura" kwa kijapani

Ni ile miti yenye majani flani ya kipekee rangi ya pink, naam ndiyo miti hiyo.

Na muda huo ulikuwa ni saa kumi na moja asubuhi, Eneo hilo kama ingekuwa jana yake basi tungesema ni paradiso lakini siku hiyo haikuwa ni paradiso tena, ilikuwa ni kinyume chake

Maninja wote wa eneo hilo waliokuwa wakilinda nje walikuwa wametapakaa chini kula mahali wakiwa hawana uhai, walikufa vifo vibaya sana na vya kikatili, pia harufu ya damu ilikuwa ni kali sana ikisambaa eneo lote

Wengi wao baadhi ya viungo vyao vilikuwa vimetenganishwa na miili yao, huyu mikono, huyu miguu yule moyo umenyofolewa, mwingine utombo wake ulikuwa nje kabisa ukionekana hakika vilikuwa ni vifo vya kutisha sana

Yale majengo ya kitamaduni yakuvutia hayakuwa hayatamaniki tena, kifupi eneo hilo liligeuka kuwa kama jalala la wafu. Idadi ya maninja waliokufa eneo zima tena lenye mita elfu themanini ilikuwa haiesabiki kirahisi na nyumba nyingi zilikuwa zikiwaka moto

Sasa kwenye jengo ambalo kwa kulitazama tu lilionekana ndio lilikuwa jengo kuu kuu kuliko majengo yote kabla halijaaribiwa na kuchafuliwa na michirizi ya damu ilisikika milio ya panga kugongana na kukwaruzana bila kukoma

Na ndani ya eneo hilo alionekana wanaume wawili wakipambana mmoja akionekana ni kijana aliye kwenye miaka ya 20s na mwingine akiwa ni mzee wa kwenye late 50s

Kwa mwanaume kijana alionekana kuwa kifua wazi ambapo yaliyonekana majeraha ya kuchanwa na mapanga huku michirizi ya damu ikimtoka lakini hakuonekana kupoa
Na kwa mwanaume mzee alikuwa amevaa nguo za kitamadunki ambazo muda huo hazikuwa hazitamaniki hata kwa kuziangalia

Nguo zake zilichanwa kila mahali na kuonekana kama vile chokoraa, naye pia alikuwa na majeraha ya kuchanwa na panga lakini hayakuwa memgi kuzidi ya yule kijana

Mpambano ulikuwa ukipamba moto yaani ulikuwa ni mshike mshike patashika nguo kuchanika! Bila kusahau moto ulikuwa ukiwaka jengo zima lakini wataalamu hawakujali moto wala nini kifupi ilikuwa ni show ya kufa mtu

Pembeni mita kadhaa alionekana mwanamke amejikunyata huku akitetemeka kwa hofu isiyo na maelezo na alikuwa akitiririkwa na Jasho jingi sana ambalo joto la moto uwakao ulichangia pia

Alikuwa akitetemeka na kutapika kila baada ya dakika kadhaa hasa aliposhuhudia miili ya maninja waliokufa ikiungua na moto. Alikuwa akitia huruma sana mwanamke huyo, sauti yake ilikuwa imekauka kwa kulia muda mrefu na macho yake yake yalionekana kuvimba sana na machozi bado yalikuwa yakimtiririka bila kutoa sauti

Upande wa wale wanaume ni kama vile hawakujali uwepo wake, waliweka umakini wao kwenye pambano. Wakati wanapambana kwa kupamgua mapanga mara yule mzee alipata upenyo wa kufikisha shambulizi kwenye mwili wa mpinzani wake na hakutaka kuipoteza hio fursa, palepale kwa spidi ya hali ya juu alimchoma yule kijana upande wa karibu na figo kisha kuchomoa na kumtandika teke lililomrusha mita ksdhaa kijana yule

Licha ya kuchomwa.na panga na kurushwa na teke la mzee huyo lakini aliweza lujidhibiti na asiamguke na aliishia kupiga magoti kwa msaada wa upanga wake huku mkono mmoja akiwa ameziba eneo alilochomwa kuzuia damu isivunje zaidi

Alionekana kuwa myu aliyechoka sana kwa shughuli kubwa usiku kucha mpaka kunaanza kupambazuka na alikuwa akihema kwa nguvu

"Wewe m*ng nitahakikisha unakufa kifo kibaya sana kwa hasara uliyonisababishia hata ukienda huko kuzimu unikumbuke daima" aliongea yule mzee kwa lijapani

Yule kijana baada ya kusikia kauli hiyo alianza kucheka japo kwa sauti hafifu akivumilia maumivu ya majeraha yake

"Nyie washenzi mmeniulia mzee wangu na kuanza kuniandama kwa miaka miwili je hamjanisababishia hasara? Alimuuliza yule mzee kwa lugha ya kijapani pia

"yule punguani ana thamani gani mpaka kuanya huu u*eng" wako ulionitia hasara? Yule ni punda tu asiye na shukrani"

"Kwako wewe ni punda sawa sikatai ila kwangu yule alikuwa ana thamani sana pengine hata hizi roho nilizozipeleka kuzimu hazitoshi kulipia kifo chake" aliongea kijapani kisha kunyamanza kidogo na kumkazia macho yule mzee

"He wasn't just an old timer who I used to knew, he was also like a father to me somehow but you damn motherf***ers killed him, all for just a damn book! A book that you don't even know what it contains and then you're calling it a precious thing huh? What is the difference between you motherf***ers and some fools I happened to meet along the way?. For sure you're the dumbest fool I have ever met" aliendelea kwa kingereza akimaanisha " Hakuwa tu mzee niliyemfahamu zamani, alikuwa pia kama baba kwangu kwa namna fulani lakini nyie washenzi mkaamua kumuua, kwa sababu ya kitabu tu! Kitabu ambacho hata hamjui kina nini ndani, halafu mnakisema kuwa ni kitu cha thamani? Kuna tofauti gani kati yenu na wale wapumbavu niliokutana nao njiani? Hakika wewe ndiye mpumbavu mkubwa zaidi niliyewahi kukutana naye.

"You call me a dumbest a fool but what about you son? But what about you huh? F
Killing hundreds of human for just an old man who you hardly knew? You're difference to a devil" mzee alijibu kwa kingereza pia akimaanisha "

"It was you motherf****ers who made me do this don't forget not to forget... "(Ni nyinyi ndiyo mmenifanya nitende haya, bila kusahau...) aliongea na kugeuza shingo yake akiangalia upande alioukusudia na mzee huyo pia aliangalia sehemu hiyo

Ulikuwa ni mwili wa mtu mwanaume umeninginia juu ukutani kwa kuchomwa na mkuki uliotoboa moyo na kutokelezea upande wa pili na kunasa ukutani, damu zikiwa zikimvuja masikioni, puani, mdomoni na eneo la moyo alilochomwa na bila shaka alikuwa ni marehemu tayari

"... that fucker of yours tried to mess with my family" alimalizia sentensi yake akimaanisha kwamba huyo mshenzi mwenzake alijaribu kuvuruga familia yake

Mzee huyo mara baada ya kumtazama mtu yule ukutani aliishia kushusha pumzi ya masikitiko

"I used to admirer him for his talent and loyalty too bad he's gone" aliongea kwa kingereza akimaanisha "Nilikuwa namkubali sana kwa kipaji chake na uaminifu lakini sasa amenitoka"

Baada ya kumaliza kauli hiyo alimsogelea kijana yule aliyepiga magoti akiugulia maumivu kwa kujikaza kiume

"Pengine nikikata kichwa chako na kuwatupia papa baharini nitafarijika piar sio mbaya nikiuza viungo vyako kupata hela ya soda" mzee huyo aliongea na kuupiga upanga ambao kijana yule ambaye ni Jimmy ameutumia kama kisaidizi cha kupiga goti asianguke chini

"Haha! We mzee unanitania si ndio" Jimmy aliongea kimasihara akimwangalia huyo mzee ambaye muda huo alinyanyua upanga wake tayari kukata kichwa chake

"utulivu wa nafsi! Tulia eeh roho ovu" alinena kwa kilatini japo kwa tabu na ghafla tu yule mzee kabla hata hajatimiza kusudi lake alijikuta ameganda kama sanamu bila ya chanzo, ni kama vile nafsi yake imeparalyze na alishindwa kufanya chochote

Hata kuongea alishindwa na sura yake pekee ilionesha kwamba alikuwa na hofu isiyo na kifani

Jimmy alijinyanyua kibishi na kumpokonya upanga ambao mzee huyo alikuwa ameunyanyua akitaka kumkata kichwa

"Scary right?" aliongea akimaanisha inatisha eeh

"You know it was just yesterday that I completed the willpower circle It took me two year trying to practice while struggling fighting with you fools, I just wanted to have a fair fight but the world has always been unfair" aliongea akimaanisha "Unajua, ilikuwa ni tu jana nilipokamilisha mduara wa nguvu ya nia/dhamira. Ilinichukua miaka miwili nikijaribu kujifunza huku nikipambana na nyinyi wapumbavu. Nilichotaka tu ni pambano la kiungwana, lakini dunia imekuwa ikinidhulumu kila mara." bila kujali kama mzee huyo alikuwa anaelewa anachomaanisha au lah

"Sayonara Senshi" alimuaga kwa kijapani akimaanisha kwaheri kamanda na bila kupoteza muda alikifyeka kichwa cha mzee huyo bila huruma na damu kuanza kurukaeuka kwenye shingo yake kwa fujo sana zikimvhafua uso na mwili wake lakini hakujali

Alichana kitambaa kutoka kwenye nguo ya mzee yule ambaye alikuwa ni marehemu tayari na kujifuta usoni kisha alifumba macho na kuanza kuneno kilugha kwa kurudiarudia kama vile chanting na zile sehemu ambazo zilikuwa zinavuja damu ziliacha japo hakuweza kujiponya lakini kupitia uchawi wake aliweza kuzuia damu zake zisivuje kwa mda maalumu

Upande wa yule mwanamke alikuwa ameshazimia sekunde aliyoshuhudia kichwa cha cha binadamu kikitenganishwa kwenye mwili wake

Muda mchache mbele Jimmy alionekana akitoka kwenye geti kubwa la uzio wa eneo hilo huku mikononi amembeba mwanamke aliyekuwa hana fahamu, alikuwa akitembea kwa kujivuta huku mwanga wa jua ambalo lilikuwa likichomoza muda huo ukimmulika

Upepo mwanana wa asubuhi jlikuwa ukivumia taratibu ikiambatana na baridi iliyokuwa ikimtonesha majeraha yake lakini alivumilia kama mwamba na kuonekana kama mfalme aliyetoka vitani kumuokoa malkia wake kwa ushindi mkubwa

Mbele yake kulikuwa na helikopta kubwa nyeusi na miili ya maninja wachache isiyo na uhai, rubani wa helikopta hiyo naye alionekana hana uhai pia kwani kisu kidogo cha nyota kilionekana kuzama kwenye koo yake

Alienda mpaka kwenye helikopta hiyo na kumketisha mwanamke yule kwenye siti ya nyuma akimfunga mikanda ya siti na kuhakikisha amemfunga kisawasawa na bado ya kuhakikisha alienda kwenye siti ya rubani na kumhamisha rubani siti nyingine na kumfunga pia mikanda licha ya kwamba alikuwa amekufa

Alikaa siti ya rubani na kuvaa headset za helikopta hiyo na kuanza kushangaa akitafuta pa kuwashia na aliishi kujikuna kichwa tu asielewe hata maneno ya vitufe vilivyojazana mbele ya macho yake

"Damn! Why me! Why always me!!!!" alilalama kwa mayowe akijiambia kwanini ni yeye kwanini kila mda ni yeye tu

Mayowe yake yaliweza kumshtua mwanamke yule aliyekuwa kwenye usingizi wa kukosa fahamu.
Baada ya kushtuka na kujiona yupo kwenye helikopta alianza kujigeuza kuangalia kulia na kushoto asione mtu na alipoangalia siti ya rubani alikutana na Jimmy ambaye alikuwa anamtazama kwa tabasamu la uchungu

"Aaaaaah mamaaa Mungu wangu nisaidieeeeeee!! Shetaniiii anataka kunouaaa" alipiga mayowe ya msaada kwa lugha ya kingereza huku akihangaika kunyanyuka kwenye siti lakini alishangaa anashindwa kunyanyuka kutokana na mikanda ya usalama aliyofungwa na mwanamke huyo alikuwa mwenye asili ya Asia

Haraka haraka alijifungua mikanda ile na kutoka nje ya helikopta hiyo na kuanza kukimbia kusiko julikana, Jimmy mwanzo mwisho alikuwa akimshangaa tu bila ya kujifanya chochote na mpaka mwanamke huyo anakimbia aliishia tu kumsindikiza kwa macho na kupotezea

Kama yeye anasumbuliwa na stress za kuhangaika kuwasha helikopta ya nini kujisumbua na mwanamke asiye na msaada kwake alijiambia kama mwanamke huyo anataka kubaki msituni humo ni yeye na anamuombea uzima, alijiambia ngoja ahangaike na vitufe vya helikopta hiyo akitafuta bahati

Dakika tano zilipita bila mafanikio na aliishia kukunja ndita na kuishia kuitukana helikopta hiyo pamoja na engineer aliyeiunda matusi yaliyomjia akilini mwake muda huo

Aliona sio mbaya akipumzika kidogo kutuliza uchovu ndiyo mengine yafuate na ainyoosha miguu yake juu ya vitufe vingi vya helikopta hiyo na kufumba macho na kutulia tuli kwa nusu saa

Jimmy alikuwa na masikio kama sumanku yenye kuweza kuvuta chuma yoyote iliyo umbali mrefu, aliweza kusikia hatua za miguu ya mtu ikija eneo hilo na baada ya kusikiliza kwa makini aliishia kutoa tabasamu pana usoni na kufumbua macjo yake na aliweza kumuona mwanamke yule akirudi kinyonge sana

Alikuwa akimshikilia mti akimnyooshea Jimmy kama silaha yake ya kujihami huku akimsogelea taratibu

Wewe shetani ndio, wewe unayeniangalia. Mimi ni Mstahiki Malkia wa Kifalme, Princess Amirah wa Brunei, Mrithi Halali wa Enzi Tukufu ya Dhahabu. Kwa heshima ya kifalme na neema ya mababu zangu, nakuamuru kwa unyenyekevu mkubwa kabisa, usinidhuru. Tafadhali" aliongea huku akitetemeka kwa hofu

"Ebu jiongeze basi mrembo Amirah fanya unisaidie na hii helikopta kama unaweza, achana na suala la kukuua mbona mpaka sasahivi uko hai? kama ni kukuua ningekuwa nishakuua kitambo sana hayo maneno yako ya kifalme hayana msaada zaidi ya kuonekana unapiga kelele" aliongea kibabe na kumfanya mwanamke huyo princess Amirah kuzidi kutetemeka

"Bt the way naitwa Jimmy sip shetani"

TO BE CONTINUED......

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 32: Friendship out of the blue

Crown princess Amirah wa Brunei kilichomfanya amuite Jimmy shetani ni kutokana na kushuhudia mwanaume huyo alivyokuwa akiua maninja wa yami no senshi kikatili sana na kama binti mfalme ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia mauaji ya kikatili ambayo hakuwai kuwazia yatakuja kutokea mbele ya macbo yake

Hatahivyo alistahili kuitwa binti mfalme kwa uzuri alionao na kama mjuavyo mabinti wenye damu ya kifalme siku zote huwa ni warembo sana na Crown princess Amirah alikuwa ni mzuri kwa kila kitu alikuwa amekamilika kila kona ya mwili, sio vifuu, sio shepu, sio msambwanda yaani kila kitu, alikuwa ni mrembo haswa!

Lakini kwa wakati huo ule urembo wake ulipotea wote, alikuwa amechafuka sana ngozi kiasi cha kudhani labda alikuwa akicheza kwenye vumbi la mkaa, gauni lake nalo lilikuwa halitamaniki tena, lilikuwa limechafuka na kuchanika baadhi ya sehemu na kibaya zaidi alikuwa miguu peku

Taratibu alishusha mti ule aliokuwa amemnyooshea Jimmy na kuutupa pembeni na kuanza kusogelea helikopta

"Ninajua jinsi ya kuwasha engine mjomba wangu alinifundisha" aliongea kwa sauti ya upole akiwa bado na hofu

Jimmy baada ya kusikia mwanamke huyo anajua kuwasha engine ya helikopta alipatwa na ahueni na alitoka kwenye siti ya rubani na kumpa ishara binti mfalme huyo aingie na bila ubishi princess Amirah aliingia na kuketi kisha kuvaa headset na kuanza kubonyeza vitufe vilivyoko mbele yake na juu yake huku Jimmy akiwa pembeni akitazama jinsi mrembo huyo akiwasha engine kitaalamu

Sekunde kadhaa mbele engine za helikopta zilianza kunguruma pamoja na feni kubwa za juu kuanza kuzunguka taratibu huku zikiongezeka kasi ya kuzunguka kadri sekunde zinavyosogea

Jimmy alitoa tabasamu la furaha baada ya kuona sasa amepata rubani na wanaondoka kwenye kisiwa hicho lakini tabasamu lake lilipotea taratibu baada ya engine kuzima ghafla

Princess Amirah pia alishangaa kuzimika kwa ghafla engine za helikopta hiyo na baada ya kukagua kujua shida aligundua kwamba mafuta(gas) ya helikopta hiyo yameisha

"Nadhani gas ime...." kabla hata mwanamke huyo hajamaliza alishtuka tu mkono wa mtu umepita pembeni yake kama vile unakamata kitu, ilikuwa ni spidi ya ajabu na alishtuka tu mkono umeshapita pembeni yake karibu na shingo

Machozi yalianza kumbubujika bila taarifa huku akilia akijitahidi kutotoa sauti, macho yake yalikuwa yamejaa hofu hasa baada ya kufikiria angekuwa katika hali gani kama mkono ule ungeidaka shingo yake

Jimmy aliurudisha mkono wake la haula! Alikuwa amekamata kichwa cha nyoka aina ya black mamba akiwa hana uhai, ilionekana kasi aliyotumia kumdaka nyoka huyo ilibeba na uhai wa kiumbe huyo

Mara baada ya, princess Amirah kumuona nyoka huyo mwenye sumu kali mkononi mwa Jimmy palepale akili yake ilimwambia kwamba nyoka huyo alikuwa pembeni ya shingo yake na kama sio Jimmy pengine angekuwa ameshang'atwa na pengine ndani ya dakika mbili angekuwa marehemu isitoshe nyoka huyo alikuwa anasifika kwa kuwa na sumu kali inayosambaa kwa spidi mwilini na kukuua ndani ya muda mfupi

Kufikiria vile tu palepale alizimia na haraka jimmy alikidaka kichwa chake kwa mkono mwingine ambacho ilikuwa kidogo tu kijipigize kwenye chuma ya helikopta hiyo na aliishia kushusha pumzi nyingi

Baadae kidogo kama dakika arobaini kupita princess huyo aliweza kufumbua macho yake taratibu na kitu cha kwanza kukiona baada ya kutoka kwenye usingizi wa kupoteza fahamu ni anga la bluu safi lililoipendezesha dunia

Aligeuza shingo yake na aliweza kumuona Jimmy akiwa amekaa chini kwa kukunja miguu akipaka majeraha yake dawa ambsyo ilionekana kutengenezwa kwa majani ya mimea mbalimbali na alikuwa akimalizia kupaka kwenye jeraha lililo karibu na figo yake ambalo alichomwa na upanga akiwa kwenye pambano na kiongozi wa kundi la yami no senshi

Alinyanyuka taratibu na kukaa kitako na aliweza kugundua walikuwa kwenye mazingira tofauti na yale kabla hawajazimia, mbele yake kulikuwa na bahari kubwa ambayo haikuonekana kutulia kutokana mawimbi madogo madogo yasababishwayo na upepo mkali wa muda huo

Alitembea kumsogelea Jimmy ambaye alikuwa ameshamaliza kupaka dawa ya mimei iliyiochanganywa na kusagwa na alikuwa ameishikilia isitoke kwenye jeraha lake la karibu na figo

"Umezinduka?" aliuliza huku akimwangalia

"Bila shaka utakuwa unahisi njaa kula matunda hayo nimekuandalia" aliongea huku akimuonyesha basdhi ya matunda yaliyokusanywa sehemu moja

Princess Amirah alimeza mate yake mara baada ya kuona matunda ambayo Jimmy aliandaa ni ilionyesha dhahiri kwamba alikuwa na njaa.

"A... are you going to kill me?" aliuliza kama Jimmy anataka kumuua huku akionekana kuwa na mashaka

"You think there is poison? Why don't you just have a little faith in me? I told I ain't gonna kill you young lady, if you think I am that evil that I'll kill you why are you still here anyway? You should run to save your life" Jimmy aliongea akimaanisha "Unadhani kuna sumu? Kwanini usiniamini hata kwa kiasi kidogo? Nishakwambia sitokuua binti kama unadhani ni mbaya kiasi cha kuweza kukuua kwanini bado uko hapa? Unatakiwa ukimbie kuokoa maisha yako"

"It's just that you're scary, I feel like you can kill me any time especially after witnessing you killing people mercilessly"(ni kwasababu unatisha na ninahisi unaweza niua muda wowote hasa baada ya kukushudia ukiwaua wale watu bila huruma) aliongea princess Amirah

"Unamaanisha wale wajinga? Lakini kwa kuwaua umeokoka kwa namna fulani na unalijua hilo" Jimmy aliongea akiwa ametulia kabisa na kunyamanza akimwangalia binti mfalme huyo mwenye mashaka

"...Unajua watu wengine katika dunia hii hawastahili kuishi, unajua? Hasa hao wajinga. Hawaheshimu maisha ya watu, wanaua tu yeyote wanayemtaka kwa sababu ya tamaa zao. Na nina uhakika watanikumbuka huko kuzimu jinsi nilivyowapeleka huko. Labda kwa njia hiyo watajifunza kuheshimu maisha ya wenzao huko waliko"

"Asante" aliongea princess Amirah huku macho yake yakionyesha nia ya dhati

"kwa lipi?"

"Kwa kuniokoa. Ingawa sikujui, sijui umetokea wapi, wala kwa nini ulikuwa pale… lakini uwepo wako pale uliokoa maisha yangu. Sijui hata nini kingenipata kama usingetokea"

""Sasa unaniamini? Kwamba sitakuua?"" Jimmy alimuuliza huku akitabasamu, lilikuwa ni tabasamu flani la amani

"Ni vile..."

"Vile nini?"

"Maisha yangu yote yamekuwa ya huzuni. Yaliyojaa hila chafu na michezo ya kishetani hasa kutoka kwa watu wa karibu. Ndiyo maana siamini watu kirahisi."

"Na mbona unaniamini sasahivi?

"ni kwa sababu nimechagua kukuamini." aliongea na kumfanya Jimmy atabasamu

"Iam starting to like you princess Amirah" aliongea, Jimmy kirafiki akimaanisha ameanza kumkubali

Ule woga na mashaka aliyokuwa nayo princess huyo vuote vilimtoka baada ya kuzungumza na Jimmy.
Alikuwa akimwangalia Jimmy anavyovumilia maumivu ya majeraha yake ambayo amepaka, japokuwa Jimmy hakuonyesha waziwazi lakini aliweza kugundua

Na aliinama na kuchana gauni lake kwa chini mtindo wa duara na kitambaa hiko kilichotoka kwenye gauni lake alikishika na kumsogelea Jimmy na kupiga magoti nyuma yake

Jimmy alikuwa akiangalia tu mwanzo mwisho sio kwamba hakuelewa anachofanya mwanamke huyo bali aliamua kutulia tu na kumpa nafasi mwanamke huyo afanye anachokusudia kufanya

Princess Amirah taratibu alimfunga Jimmy jerehe lile kubwa la karibu na figo kutumia kitambaa ichochana kwenye gauni lake na mpaka anamaliza Jimmy alikuwa ametulia vilevile

Baada ya kumaliza kimfunga alitoka nyuma ya Jimmy na kukaa pembeni yake,

"Vipi mbona hauli hayo matunda unapanga kuwa na njaa" Jimmy aliongea na sasa princess huyo ndio anakumbuka ana njaa na bila kuremba alichukua tunda moja na kuanza kula

"Mbona wewe hauli?" alimuuliza Jimmy

"Nimeshakula usiwaze we kula umalize na kama hujashiba unaniambia nakwenda kukuletea mengine"

Kimya kikafuata Jimmy akiwa kimya akitazama bahari iliyokuwa mbele ya macho yake huku princess Amirah pia akiitazama huku akila matunda yake

"So beautiful!" aliongea princess Amirah

"Yeah" Jimmy alimjibu na kuendelea kupiga kimya

"Hey....." princess Amirah aliita mara baada ya kuona kimya kimetawala na Jimmy alimgeukia kumtazama ishara kwamba ameitikia

"Mbona huniulizi kwanini nimekuwa mateka wa wale maninja?"

"Sijataka kuuliza"

"Kwanini? hutaki kujua?

"That’s just my altitude, I mind other people's business but if you feel like you wanna tell me just spit it, I may learn a thing or two through your story" Jimmy aliongea akimaanisha "Ndio tabia yangu, najua mipaka lakini kama unahisi kuniambia we niambie tu huenda nikajifunza mawili matatu kupitia story yako"

"Naam ni tamaa za watu ndizo zilizoni fikisha huku, Unajua tamaa ni kama ugonjwa fulani unaokua polepole, ni kama kivuli kilichojificha nyuma ya tabasamu

Huanzia kwa watu wako wa karibu, familia yako, wale wanaokuambia wanakupenda. Ni wale wale unaocheka nao, unaokula nao, unaoshirikiana nao siri. Hao ndio wanaoanza kukuona kama chombo cha kutumia, jiwe la kukanyaga au ufunguo wa hazina wanayodhani umeficha. Yote hayo mzizi wake huanzia kwenye tamaa

Kaka yangu mwenyewe wa tumbo moja, damu yangu amenisaliyi kwasababu ya tamaa ya madaraka. Inauma sana pale ndugu yako anapokwambia anakupenda alafu kumbe ameandaa njama ya kukuondoa kwenye uso wa dunia ili tu arithi nafasi yako
Tamaa ni kama ugonjwa fulani ambao huondoa ule ubinadamu na kupandikiza ushetani, mtu mwenye mwenye tamaz hatoona hasara kukuua kama kufanya hivyo kutatimiza mahitaji yake" princess Amirah aliongea kwa huzuni huku chozi likimdondoka bila kutoa sauti

"Na kitu cha kuogopesha zaidi? Tamaa haina mwisho. Ukimpa mtu mwenye tamaa dunia, kesho ataomba nyota. Ni njaa inayokua kila inapolishwa. Itaharibu chochote na yeyote ili ipate zaidi. Hata kama 'zaidi' hiyo inamaanisha kuondoa maisha ya watu waliowahi kuahidi kumlinda" aliendelea

"So yeah that young blood of mine did plan to end my life in here, making deal with those devils... I knew he was greedy but never thought hell go this far" alimalizia huku akifuta machozi yake akimaanisha alikuwa akijua ndugu yake alikuwa na tamaa lakini hakufimiria kama angefikia hatua hiyo ya kutaka kumdhulumu maisha yake

"Unaongea kama mtu anayevuja damu licha ya kutokuwa na jeraha, I feel you" aliongea Jimmy akimaanisha anamwelewa

"Uko sahihi Amirah, Tamaa ni sumu. Ni kama kutu kwa roho. Inapoingia, huharibu kila kitu, wajibu, upendo, heshima yani kila kitu mpaka kinachobaki ni njaa tu. Nimeiona pia... si kwa familia kama wewe, bali kwenye uwanja wa mapambano wa dunia. Wafalme, wakuu wa vita, hata maskini... wote hutamani kile wasicho nacho, na wakikipata, hutaka zaidi. Hawatosheki. Hawajawahi kutosheka kamwe...

Na watu kama ndugu yako hujificha nyuma ya ustaarabu, huvaa kinyago. Huita usaliti wao 'mkakati' Tamaa zao zitakuja kuwagharimu pakubwa sana na hakuna kiasi cha pesa kitakachowaokoa wakati wao ukifika
Usinishukuru kwa kukuokoa. Kumbuka tu kuwa maisha yako hayakuwa yao kuchukua. Na sasa kwamba uko huru… usiwahi kuruhusu tamaa yao itengeneze thamani yako tena sawa mrembo" Jimmy aliongea maneno ya kumfariji na kauli ya mrembo ilimfanya princess Amirah kutabasamu huku chozi likidondoka na haraka haraka alilifuta na kutingisha kichwa kukubali kama mtoto anayemtii mzazi wake

"Unajua ni ngumu sana kuamini mtu kama wewe kuwa na upande mwingine wa utulivu"

"Kwanini? "

"Ni ngumu tu kuamini mtu anayeua kikatili anaweza pia kuongea kistaarabu na kwa ukarimu kiasi hiki"

"Mimi sio muuaji ni hao wapuuzi ndio walioanzisha na kutaka kuniua na kwa ajili ya amani sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kuwaondoa katika uso wa dunia"

"Unapaswa kujua si kila anayeua ni shetani na si kila anayetabassmu ni malaika" Jimmy aliongea

"Kama hutojali tunaweza kuwa marafiki? Nataka kujua mengi kuhusu wewe" Princess Amirah aliomba urafiki na kumfanya Jimmy acheke kidogo

"Hakuna shida chukulia tayari sisi ni marafiki" Jimmy alimjibu huku akitabasamu

"Lakini kumbuka mimi na wewe tuna maadui kuwa marafiki ni sawa tu na kuongezeana maadui, huogopi?"

"Kuogopa? Maisha yangu yote ysmekuwa ni kupambana na kujinasua kwenye mitego ya maadui zangu japokuwa ni kweli naogopa lakini angalau nina wewe"

"Mara hii ushaanza kuniamini kupita kiasi cha kunifanya bodyguard wako?" Jimmy alitania

"Sio hivyo, ni kwasababu nataka kujua mengi kuhusu wewe na pia kujifunza vitu kutoka kwako unaonekana kuwa na hekima"

"Kwakuwa unataka kunijua sio mbaya nikakueleza kidogo kuhusu mimi" aliongea na kumfanya princess Amirah atege masikio yake vizuri tayari kwa kusikilizainion

"In my not so humbe opMaisha ni kama mchezo wa bodi bila kanuni zilizoandikwa.
Wakati mwingine unadhani unashinda, kumbe unarudi nyuma kwa kete tano.
Na wakati mwingine unadhani unapotea lakini kumbe ndio unakaribia ushindi.
Mimi ni yule aina ya mtu anayesema ukweli kwa tabasamu na utani ndani yake.
Sio kwa sababu sijali, bali kwa sababu nimejifunza maisha yakikupiga ngumi, ni bora ucheke kuliko kulia, maana machozi hukauka lakini kicheko hubaki kumbukumbu.

Ushawahi kuona jinsi watu wanavyopoteza utu kwa vitu vidogo?
Watu wanagombana kisa WiFi, wanachukiana kwa maoni ya mtandaoni, na wanavunjika moyo kwa likes chache. Lakini mimi ni naheshimu mtu ambaye anakaa kimya lakini anajua anachofikiria kuliko yule anayesema mengi lakini hajui aendako

Watu wanasema nina mtazamo wa kipekee, Sijui kama ni kweli, au ni tu sababu sina mbele wala nyuma. Lakini ninachoamini ni hiki: dunia hii inahitaji watu wanaojua kucheka, hata kama wamepotea; watu wanaojua kusamehe, hata kama waliumizwa; watu wanaojua kupenda, hata kama waliwahi kukataliwa.

Kwa hiyo, ukiniuliza mimi ni nani...
Mimi ni kijana anayekumbatia dhoruba huku akitafuta upinde wa mvua.
Anayependa usiku kwa sababu nyota huonekana gizani. Na anayepigwa chini mara kumi lakini atasimama mara kumi na moja na mara ya kumi na mbili, atakaa chini aseme, “Acha nipumzike kidogo, lakini sijasalimu amri.” Jimmy alijielezea kwa namna fulani hivi ya kipekee sana hali iliyomfanya princess Amirah kuvutiwa naye zaidi

TO BE CONTINUED

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 33: Huyu ni siri yangu

"Unajua kujielezea kwa njia ya kipekee sana, nani alikufundisha hivyo? princess Amirah aliuliza

"Hakuna, ni maisha ndiyo yaliyonifunza.... mambo mengi sana" Jimmy alimjibu

"Unajua unanikumbusha maneno flani niliyowahi kusikia hapo kabla, yanasema "Si kila azururae amepotea" aliongea princess Amirah

.... na msemo huo unakufaa sana, unaonekana kuishi maisha ya kawaida ya kuzurura na kuonekana wa kawaida lakini ukweli unaonekana ni wa ajabu sana aliendelea

Unaweza sema hivyo, iwe kweli au si kweli mimi sijali, lakini kuhusu maisha kama ningeyafupisha maneno machache ningesema "YANASONGA TU" Jimmy aliongea

"Haijalishi nini kitatokea maishani, maishayanasonga tu. Yawe mazuri au mabaya yanasonga tu. Umesalitiwa na mtu wa karibu na muhimu kwako na unahisi labda dunia inapaswa kusimama lakini jua litachomoza tena na siku nyingine inaaanza, watu wanaendelea kuishi maisha yao ya kila siku, ndege wataendelea kuimba kila asubuhi uamkapo na polepole unaanza kupona, maumivu si ya kudumu na nyakati nzuri hazidumu pia" aliendelea kuongea kisha taratibu alisimama

""Wandering is not the same as being lost, it's just another way of learning about the so called life, anyway we have to find a way to get out of this Island" akimaanisha "kuzurura si sawa na kupotea ni njia nyingine tu ya kujifunza kuhusu maisha anewei tunapaswa kutafuta namna ya kutoka kwenye kisiwa hiki"

°°°°°°°°°°

PRESENT DAY

Vuta picha wenzi wawili waliovaa sare wakapendeza wakitembea pamoja uone jinsi inavyovutia ndugu msomaji

Jimmy pamoja na Biancalina walikuwa tayari wamefika sehemu husika na walikuwa wakitembea pamoja kama wenza wa siku nyingi sana, kuelekea ndani ya shopping mall iliyokuwa mbele yao

Ilikuwa ni shopping mall kubwa sana yenye kila sifa ya kuitwa shopping ya kifahari, ilikuwa imesheheni vitu vya bei ghali. Wawili hao waliweza kuingia ndani humo na kuingia kwenye lift na kwenda floor ya tatu ambapo bila shaka nguo zilipatikana

"Mummy usiniambie unataka kuninunulia nguo za bei mbaya hivyo halafu sio kama sina nguo" aliongea Jimmy

"Kuna ybaya kwani mimi kukunulia nguo?"

"Hapana sio hivyo lakini nina nguo za kutosha"

"Unamaanisha hiyo jeans yako iliyopauka?"

"Hey hii haijapauka bhana ndivyo ilivyo kiufupi hii ndio staili ya mjini*

" Nadhani itapendeza kama utabadili fashion zako kuanzia sasa, unatembea na celebrity halafu unavaa nguo za hovyo unaiaibisha bhana! "aliongea Bianca japo kwa utani

"Bianca kiutani alimuonyesha jimmy sanamu zilizovikwa suti za kila rangi kwa ishara ya kichwa huku akitabasamu na ghafla tu alijifanya kusikia sauti na kutega sikio huku taratibu akisogea kwenye sanamu la plastiki la mwisho kabisa

"Unasikia hiyo? "Bianca alimuuliza, Jimmy

"Mbona sisikii kitu?"

"Suti hiyo! it's calling your name, it's saying" come wear me, come wear me!!" aliongea Bianca akiigiza sauti ya suti kuongea na kumfanya Jimmy acheke

Wakati Bianca akiendelea kumshawishi Jimmy mara wahudumu wawili wa eneo waliwakaribia

"Karibuni maboss, oh my!" aliongea muhudumu na mara alipatwa na mshangao baada ya kugundua kitu kiasi cha kufunika midomo yake kana kwamba ameona kitu cha ajabu

"Ni wewe kweli au macho yangu yananidanganya? Hapana macho yangu hayadanganyi ni wewe bhana ni malkia wa muziki Lina!" aliongea kwa furaha sana muhudumu huyo

"Ni yeye kweli" alijibu muhudumu mwenzake

Biancalina alikuwa ni maarufu sana nchini kwenye tasnia ya muziki wa bongo na pia umaarufu wa mama yake ulichangia kwa yeye kujulikana nchini kwa muda mfupi tu tangu aingie kwenye tasnia hiyo na alifahamika sana kwa jina la Lina, kifupi vha jina lake

Licha ya kuja shopping mall kwa kujisitiri sura kwa kuvaa kofia aina ya pama na miwani ya jua lakini aliweza kugundulika kirahisi na mashabiki zake kindakindaki ndani ya mall hiyo

"Mimi naitwa Halima ni shabiki yako mkuuubwa, nakupenda sana Lina, nyimbo zako huwa zinautuliza moyo, yani ni kitu roho inapenda, nilikuwa naomba sana ata siku moja nikuone live" aliongea kwa bashasha sana

"Shhh taratibu Halima, nimefurahi kusikia wewe ni shabiki yangu na unapenda nyimbo zangu, nafurahi sanaa tena sanaa lakini si unajua paparaz na mashabiki wengine hawakawii kuanzisha vurugu lisitoshe nipo public na nimekuja kwa amani" aliongea kirafiki kana kwamba alikuwa akimjua Halima kwa muda mrefu hali iliyomfanya muhudumu mwingine kupatwa na wivu

"Mimi ni Die hard fan zaidi ya huyo, tena nina nyimbo zako zooote, pia kama hutojali naomba kupiga picha nawe" aliongea

"Hilo msiwaze" Bianca aliongea huku akitabasamu kisha kupiga nao picha kadhaa na wahudumu wale pasipo kushtukiwa na watu wachache walioko kwenye floor hiyo

Upande wa Jimmy alikuwa ndiye camera man kwani nduye aliyekuwa na jukumu la kuwapiga picha wanawake hao

"Kaka samahani, naomba utupige picha" aliongea muhudumu Halima huku akimpatia simu yake Jimmy, na mwamba hakuwa mchoyo hususani kwa wanawake warembo

"Bila samahani mrembo, hilo usiwaze" aliongea Jimmy kirafiki huku akipokea simu hiyo

Aliwapiga picha kadhaa na kurudisha simu kwa mwenyewe na kudhani kazi imeisha lakini haikuwa hivyo, muhudumu yule mwingine naye alimpatia simu yake akiomba picha zipigwe humo(kwenye simu yake)

"Na mimi" aliongea huku akimpatia Jimmy simu yake aina ya Iphone. Jimmy aliishia kutoa tabasamu tu na kupokea huku kichwani akijiwazia na kujiambia bora hata Zuhura angeambatana nao na jukumu la kupiga picha lingekuwa kwake, "yaani nimegeuka kuwa mpicha ghafla?" alijiambia

"Ila sio mbaya mradi na kula kwa macho hehe! Sio mbayaaaaaa" alijifariji huku akiimba kiitikio cha nyimbo ya sio mbaya kichwani mwake

"Miss lina naweza kuuliza huyu ni nani, nimeona anaambatana nawe muda wote" aliuliza Halima

"Ooh huyu?" aliongea Bianca huku akimshika Jimmy bega lake ishara ya kuuliza kama ndiye yeye anayeuliziwa na Halima alitingisha kichwa

"Huyu ni siri yangu" aliongea huku akitabasamu

"Ohoo" waliitikia hivyo tu

"Je mnajua kutunza siri?" aliwauliza

"Ndio" walijibu

Ukweli hawakuhitaji kuelezwa sana ili kumuelewa anachomaanisha Biancalina hivyo walijiongeza tu, hata hivyo walifurahi kukutana na role model wao

"So do I, hata mimi pia najua kutunza siri" aliongea Bianca huku akiwatolea tabasamu, upande wa Jimmy pia aliishia kutoa tabasamu fulani hivi lisiloelezeka lakini lenye kumuangazia nuru yeyote amuangaliae

"Nimefurahi sana, pia karibuni maboss, bidhaa zote hizo zimetengenezwa kwaajili yenu pia huwa tuna utaratibu wa kutoa discount kwa mteja yeyote ambaye ni mara ya kwanza kununua bidhaa katika mall yetu" aliongea Halima kwa kuchangamka

Basi ilifanyika shopping ya kibabe sana huku mifuko yote ya nguo akibebeshwa Jimmy na mpaka wanamaliza walinunua nguo nyingi sana

"Mummy kulikuwa na haja gani ya kununua nguo zote hizi" aliongea Jimmy ambaye alikuwa amebeba mifuko mingi ya nguo

"Zingine ni kwaajili ya kuvaa kwenye sehemu maalumu, halafu unawaza nini ilihali hujatoa hata senti moja? relax"

"Shida sio kutoa senti shida ni gharama iliyotumika kwenye manunuzi"

"Mbona gharama inakutia presha hivyo? Chukulia nimefanya uwekezaji kwenye mwili wako"

"Unataka kusema mwili wangu unagharima shillingi millioni hamsini sio?"

"Hey darling mbona unawaza mbali hivyo, nilichokuwa ni kutaka kukunulia nguo kama hujapenda basi nitazitupa" aliongea, Bianca huku taratibu uso wake ulianza kubadilika na macho yake kuanza kujawa na majimaji na alitembea haraka haraka kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye gari lake huku akibamiza na mlango kabisa

"Bam!" ilikuwa ni sauti ya mlango wa gari kubamizwa

Jimmy asingebaki kuzubaa tu naye haraka haraka alimfata na kuingia ndani ya gari akiitupa mifuko ya nguo kwenye siti za nyuma

Bianca aligeuza kichwa chake na kumwangalia Jimmy kwa sekunda kadhaa na mara ghafla tu alianza kuangua kilio kana kwamba amekosewa pakubwa sana

"Jimmy kwanini unaomgea maneno makali ya kuumiza moyo" aliongea Bianca huku akilia kwa kwikwi

"Nia yangu ilikuwa uvae upendeze lakini unaidharau na kusema kwamba naununua mwili wako"

"Sijamaanisha hivyo mummy, nisamehe nilikuwa natania" aliongea Jimmy, alijisikia vibaya kumuona Bianca akilia na kisababishi ni yeye

"Kutania au lah, maneno huwa yanabeba uzito, hujui kama umeniumiza na maneno yako"

"Am sorry mummy sitarudia tena"

"Nimefanya haya kwasababu nakujali, kwasababu nakupenda, ziko sababu nyingi" aliongea na kunyamanza kidogo

"I just wanted to spend time with you, for five damn years I have been lonely I..." alikuwa anaongea kwa kigugumizi na kabla hata hajamaliza kuongea Alikumbatiwa kwa nguvu na Jimmy

"Am sorry" Jimmy aliongea kwa sauti ya upole yenye kumaanisha

Taratibu Bianca alianza kutuliwa na pumzi zao pekee zilikuwa zikisikika na baada ya kama sekunde kadhaa Jimmy alitoka kwenye kumbatio na kumfuta mwanamke huyo machozi kwa mikono yake

Wakati anamfuta machozi macho ya wawili hao yalikuwa yakitazama kwa namna isiyoelezeka, ilikuwa ni kama roho mbili zilizopotea kwa muda mrefu na hatimae kukutana tena.

Alipomaliza kuvuta chozi la mwisho kwenye shavu la Bianca alisogeza kidole gumba mpaka karibu na lips na kukitembeza taratibu kwenye lips za mrembo huyo

Bianca hakumzuia bali alitulia na kumruhusu mwanaume huyo afanye kile anachofanya huku macho yao yakiendelea kutazamana kwa hisia kali sana

Taratibu Jimmy aliusogeza uso wake na kukaribiana na sura ya Biamca kiasi cha kila mmoja kuhisi joto la pumzi ya mwenzake, Bianca alifumba macho yake yaliyokuwa yamelegea sana kama mlenda ikionekana kumkaribisha Jimmy kwenye dunia ya denda

Kilichofuata hapo ni denda moja la taratiiiiibu lenye hisia kali kupita maelezo, lilikuwa ni denda zaidi ya neno lenyewe! Lilipigwa denda la viwango vya juu kana kwamba walikuwa ni wataalamu. Wawili hao walidendeka kiroho safi mpaka pale Bianca alipohisi pumzi kutaka kumuishia na ndipo Jimmy alipomuachia

"Usiniacha tena, nakuomba usiniache" aliongea Bianca huku akivuta pumzi nyingi, paji lake la uso likigusana na Jimmy

"Haitakuja kutokea nikakuacha, sio leo, sio kesho wala kamwe, nitakuwa nawe siku zote mpaka pale kifo kitakapotutenganisha" aliongea Jimmy na maneno yake yalimfurahisha moyo Bianca

"Kweli hutoniacha?" aliulia kama vile haamini

"Kipi kinakufanya unitilie shaka?"

"Ni kwasababu hutimizagi ahadi zako" aliongea Bianca na kumfanya Jimmy aanze kukuna kisogo chake

"Safari hii nitaitimiza mummy usiwaze sawa?"

"Na kama usipoitimiza?"

"Usiombee mabaya sasa, sitokuacha kwasababu nakupenda" aliongea Jimmy kwa kutabasamu

"Rudia tena" aliongea Bianca, ilionekana alipenda kumsikia Jimmy akiongea hivyo

"Sitokuacha kwasababu nakupenda!" alirudia

"Tena!"

"Sitokuachaa kwasababu nakupendaaaaa!!" Jimmy aliongea kwa nguvu kana kwamba amepatwa na uchizi na kitendo kile kilimfanya Biancalina acheke

Jimmy nafsi yake iliweza kutulia baada ya kumuona Bianca akiwa na furaha hata hivyo hakujilaumu kutamka maneno yale maana kupitia maneno yale ameweza kupata fursa ya kudendeka na mrembo huyo kama masikhara tu yaani

"Mbona ghafla unakuwa chizi? Unataka watu wakusikie?"

"Wewe ndiye umenifanya niwe hivi, na itapendezacwakisikia ili wajue nakupenda, halafu mummy niwe mkweli wewe ni mtamu sana, ni kama vile ulimi wako unachemchem ya asali" Aliongea Jimmy na kumfanya Bianca aanze kupatwa na aibu sasa
Aligeukia pembeni huku akitabasamu kisirisiri

Jimmy alisogeza kichwa chake mpaka karibu na sikio la Bianca na kunong'ona

"Bianca... nataka kila mtu ajue kwamba wewe ni wangu. Sio kwa sababu ni lazima, bali kwa sababu moyo wangu umechagua hivyo."

Bianca alimgeukia Jimmy baada ya kusikia maneno hayo, ilionekana yalimwingia kisawasawa mpaka kwenye roho yake maana sio kwa hisia zile zilizokuwa zikimtekenya mwili mzima

°°°°°°°°°°

Muda ulikuwa ukisonga kwa kasi sana na muda huo ulikuwa i mchana wa saa nane ndani ya hotel ya nyota tatu, ndani ya hoteli hiyo ya kifahari kulikuwa na mgahawa pia wa hadhi na watu walionekana wakipata huduma ya kula.

Katika meza moja iliyoko kwenye ya kulia ya hotel hiyo walionekana wenza wawili wakila na kuongea kwa curaha na hawakuwa wengine bali ni Jimmy na Bianca

Upande mwingine wa mgahawa huo kwenye kona ya kushoto kulikuwa na wanaume wanne wamekaa meza moja wote wakiangalia upande walio Jimmy na Bianca

Wanaume hao walionekana kama vile mapacha ukiwaangalia kwa mbali, lakini ukisogea karibu na kuwaangalia kwa umakini utagundua hawakuw mapacha bali walifanana kwenye vitu vingi, vimo vyao vilikuwa ni sawa, miili yao iliendana sawasawa na hata mtindo wa nywele pia isipokuwa nguo tu ndio hazikufanana

Kila mmoja alivaa mtindo tofauti lakini kwa hakika walipendeza sana na kuonekana kama vile fashion influencers

"Dude! Am I dreaming?" aliongea wa kwanza akimaanisha kama anaota ama

"No man you ain't dreaming it's definitely him am sure of it" aliongea wa pili akimaanisha "Hapana huoti ni yeye kweli nina hakika nalo"

"“Bruh, that’s him!. Ain’t no way he’s just chillin' here like it’s some normal Tuesday.” aliongea wa tatu akimaanisha" Kaka ni yeye, halafu hana hata habari"

“Man, he don’t look like much. Kinda scrawny. Quiet." aliongea wa nne akimaanisha “Mwana, haonekani mtu wa maana. Anaonekana mkimya.”

“That’s how he is. You think he’s harmless, then boom! next thing you know, weird stuff starts happening.” aliongea wa pili akimaanisha “Ndio jinsi alivyo. Unadhani hana madhara, halafu boom! Mambo ya ajabu yanaanza kutokea.”

" Thought he was on a vacation" Aliongea wa kwanza akimaanisha "Nilidhani yuko likizo"

"Then who is the beautiful woman sitting with him? " aliongea wa tatu akimaanisha "Yule mwanamke mrembo aliyekaa naye ni nani"

"Use your brain bruh she's might be our in-law. I ain't gonna sit here watching lez go say Hi" aliongea wa nne akimaanisha "Tumia akili kaka anaweza kuwa shemeji yetu, siwezi kukaa hapa nikiwaangalia tu, twendeni tukasalimie"

TO BE CONTINUE.....

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 34: Brotherhood

Walinyanyuka wote kwa pamoja na kutembea mpaka mahali alipokaa Jimmy na Bianca

"Brotherhood is proud of you fam" aliongea wa kwanza huku akitabasamu akimaanisha "Undugu unajivunia kuwa nawe"

Jimmy kidogo apaaliwe na chakula mara baada ya kuwaona wanne hao kwenye meza yao

"Nyie mnafanya nini hapa?" Jimmy aliwauliza

"Hilo swali ndio tukuulize wewe si ulisema uko likizo" aliongea wa kwanza

"By the way huyu mrembo ni nani?" aliendelea

"Kuwavna heshima kidogo huyu ni shemeji yenu, mummy hawa ni rafiki zangu huyu wa kwanza anaitwa Felix, wa pili huyu ni Celeb, wa tatu ni Dylan na huyu wa mwisho ni Harry kifupi hawa ni kama ndugu zangu"

"Oh kumbe una marafiki, nimefurahi kuwajua, pia inaonekana mapacha" aliongea Bianca

Wanne hao kwa pamoja waliinama kana kwamba wanamsalimia malkia kisha wote kwa pamoja wakamgeukia Jimmy kwa macho fulani hivi ni kama vile walikuwa wakisema "Bro mbona hutupi Jina la shem wetu" na Jimmy naye aliwapiga jicho ambalo bila shaka lilisema "Shemeji inatosha"

`Unakosea hawa sio mapacha, japo wanaonekana mapicha kwasababu ya kufanana kila kitu ila sura ni tofauti" aliongea Jimmy na Bianca aliweka umakini kwenye sura zao na kugundua ni kweli hawakufanana

"Ni kweli lakini, hata hivyo mapacha sio lazima wafanane sura ushawahi kusikia fratemal quadruplets?" Bianca aliongea akimuuliza

"Mummy mi sio mwanasayansi ningejuaje sasa"

"Shemeji inaonekana unajua sana sayansi na upo sahihi sema huyu Jimmy ni mbishi sana kuelewa" aliongea Felix kwa kingereza

"Fratemal quadruplets ndio nini?" Jimmy aliuliza

Kwa maelezo ya Bianca fratemal quadruplets ni aina ya mapacha wanne ambao wamezaliwa pamoja lakini hawafanani sura, wanaweza kufana kwa vitu kama vimo, miili yao na kadhalika ila sio sura, tabia, sauti na vimgine vingi

Fratemal quadruplets au kwa kiswahili tuseme mapacha wasiofanana ni ndugu wanne waliozaliwa pamoja lakini hawafanani sura, hiyo ni kwasababu kila mmoja alitokana na yai tofauti na mbegu tofauti ya baba, kwahiyo hata kama wanaitwa "Mapacha wanne" hawafanani kwa sura wala DNA ni kama ndugu wanne waliokuja duniani kwa pamoja tu

Tukija kwenye ufafanuzi wa kisayansi ki kawaida mwanamke huyoa yai moja kila mwezi ambalo likikutana na mbegu ya mwanaume huunda mtoto. Lakini kwa wakati mwingine anaqwaze kutoa mayai manne kwa wakati mmoja, japo hii kutokea ni nadra sana

Na kila yai linakutana na mbegu yake tofauti na kutunga mimba kwa wakati moja ndipo watoto wanne tofauti huzaliwa siku moja, pia tukija kwenye mfano wa maisha halisi wanaweza na macho tofauti, rangi ya ngozi iliyotofautiana, mtazamo tofauti wa kimaisha n.k

"Asee kwa maelezo yako shemeji utakuwa ni professa mmubwa sana" aliongea, Celeb

"Asante sana nashukuru kwa kudhani hivyo" Bianca alipokea sifa licha ya kwamba hakuwa profesa

"Vyovyote vile nishasema nyinyi sio mapacha" Jimmy aliendelea kukaza licha ya kupewa maelez5na hawakutaka kubishana nae maana walijua jamaa huwaga ana maneno sana ambayo yanaleta ushawishi na ukaamini bila kujali ni ukweli au uongo

"Kwahiyo Bro huyu ndo shemeji yetu uliyekuwa ukimzungumzia? Asee una macho yenye kuona sana hakika huyu ni mrembo kuliko hata....." aliongea Harry lakini aliishia njiani baada ya kukatwa Jicho na Jimmy

"Kuliko nani?" Bianca aliuliza

"Shemeji mpotezee tu huyo huwa anaropoka sana na kupenda kufananisha wanawake" aliongea Dylan huku akijichekesha na wenzake kumuunga pia

"Msiishie kusimama tu hivyo mnaweza kuketi" aliongea Biancalina na kwakuwa meza ilikuwa na viti vinne na viwili vilikuwa wazi walilazimika kuongezea viwili na kukamilisha idadi ya watu sita kwenye meza moja. Uzuri wanne hao walikuwa wameshamaliza kula na walikuea wakipumzika tu mpaka palecwalipomuona Jimmy na kuja hapo

Jimmy na Bianca pia walikuwa wakimalizia misosi yao na baada ya hapo wahudumu walitoa vyombo vyao na kuweka vinywaji na maongezi yakafuatia

"Imekuwaje mmekutana na Jimmy?" Bianca aliuliza

"Ukweli ni kwamba kukutana kwetu na Jimmy ilikuwa ni kama bahati, Tulikutana kwenye harakati zetu za hapa na pale nchini Russia" aliongea Harry

"Russia? Honey kumbe ulikuwa urusi? Ulikuwa unafanya nini?"

Jimmy aliishia kutoa tabasamu fulani hivi lisiloelezeka huku akimwangalia Harry

"Mummy si nilikwambia nilikwenda kusomea uanasheria ndio ilikuwa Russia na baada ya kumaliza niliweza kufanya kazi kama mwanasheria wa kujitegemea na ndio kwenye hio kazi nikakutana na hawa"

"Ohoo kumbe kwahiyo kumbe shemeji zangu ni warusi ila mbona hamfanani na warusi?" aliuliza Bianca

"Kweli sisi sio warusi ni raia wa Maldives" aliongea Felix

"Maldives! unamaanisha visiwa vya maldives kusini mwa Asia?" aliongea Bianca kwa mshangao

"Yeah, mpaka kujua ipo kusini mwa Asia bila shaka uliwahi kufika" aliongea Celeb

"Hapana sijawahi kufika bali nilisikia ni pazuri na katika kufuatilia ndio nikajua ipo kusini mwa Asia na pazuri kweli"

"Oh siku ukitaka kwenda usisite kututaarifa tutakutembeza visiwa vyote mpaka useme basi pia gharama zitakuwa juu yetu" aliongea Dylan huku akitasamu

"Mshaanza kutaka kunitenga na shemeji yenu hilocsahauni" aliongea Jimmy kibabe na alipomaliza tu kauli yake simu yake ilianza kuita

Aliitoa simu yake mfukoni na kuangalia namba ya mpigaji alikuta imefichwa, zilikuwa ni zile private number na bila hiyana alipokea na kuweka simu sikioni

"Hallo" aliongea Jimmy

"Ni muda muafaka wa muanza mpango sema upo wapi tuje kukuchukua" sauti upande wa pili ilisikika na kumfanya Jimmy akunje sura

"We mjeda unanitania au? Si asubuhi tu hapo tumetoka kuongea mbona mapema hivyo"

"Ukweli hatukutarajia kama hili lingetokea tunapaswa kuharakisha"

"Kuna nini kimetokea? Nyie wajeda mnazingua sana badala ya kwenda kwenye point mnazunguka"

"Upo wapi?"

"Hotelini"

"Hotel gani?" aliuliza tena na kumfanyia Jimmy kukuna kichwa. Na kumuangalia Felix

"Sunleaf haven" alimtajia, ukweli walikuwa wanasikia upande wa pili wa simu isipokuwa kwa Bianca tu
Jimmy alimtajia hotel aliyopo pamoja na location na alipomaliza tu akakatiwa simu

"Damn!" alilaani kimoyomoyo

"Darling kuna nini?" Bianca aliuliza

"Ni yale ya asubuhi tu" alijibu kwa ufupi na, Bianca alijiongeza, uzuri hakuwa mbea kama dada zetu waswahili ambao kila jambo wanataka kulijua

Waliendelea kuongea na kunywa na baada ya dakika kumi kupita tu ulisikika ngurumo ya helikopta na uzuri hoteli hiyo ya nyota tatu ilikuwa na roof top na helikopta hiyo ya kijeshi aina ya Mil Mi-17 Russian made ilikwenda kutua

Ndani ya dakika kadhaa walionekana Freya na Caren wakiingia kwenye mgahawa huo wa hotelini wakiwa wamevalia nguo ambazo kwa macho ya kijasusi utagundua kwamba kuna misheni maalumu wanakwenda kufanya maana sio kwa nguo zile.

Ujio wao ulikuwa ni wa ghafla sana pia jinsi walivyokuja kuliibua maswali kwa raia waliokuwepo ndani humo, bila kusahau mafisi waliokuwa wakiwaangalia kwa macho yenye uchu.

Walikwenda mpaka kwenye meza ya Jimmy na kusimama na ni kama vile simu ya Jimmy ilikuwa ikiwasubiri wafike kwani baada ya wanawake hao kufika hapo simu ilianza kuita na alipoangalia mpigaji alikuta ni yuleyule ti na alipokea

"Safari inaanza sasa, maelezo yote atakupatia Caren" aliongea Kamanda Rama na kukata simu

Jimmy alicheka kidogo kwa sauti hafifu na kuitoa simu sikioni kisha kuwaangalia wanawake wale waliokuja kutibua amani hotelini

"Mkuu wenu amejua kuniharibia siku, ni bahati tu kwamba mimi ni mtu wa maneno yangu" aliongea Jimmy

"Mummy utanisamehe kidogo ninatoka na hawa wajeda sawa? Sitokawia sana narudi" aliongea Jimmy na Bianca alitingisha kichwa kumuelewa

"Na nyie hakikisheni shemeji yenu hawi mpweke"

"Usiwaze sana Bro yuko mikononi salama na wala hatohisi upweke" Celeb alimjibu

"Dasvidaniya" aliwaaga kirusi akimaanisha kwaheri

"Beregite sebya" wanne wote walijibu kwa pamoja wakimaanisha "take care"

Basi Jimmy aliongozana na wanawake hao wawili mpaka juu ya rooftop ya Hotel hio na kuingia ndani ya Helikopta hiyo ya kijeshi

Ndani ya helikopta kulikuwa na watu wawili ukiachana na Rubani, nao walikuwa wanaume, mmoja akiwa ni Ben na mwingine akiwa ni Joshua na Jimmy aliwatambua vyema

"Caren usiniambie huyu ndiye tunayeshirikiana naye kwenye mission" aliongea Joshua huku akimwangalia Jimmy kwa kumchunguza

"Bro si ndio wewe wa kipindi kile uliyekuwa ukitudhania sisi ni wachawi" Joshua aliendelea

"Ndio ni mimi na sikukosea kuwadhania" Jimmy alimjibu kwa tabasamu

"Lakini mwisho wa siku nawe umekuja kuwa mchawi" aliongea Freya

"Bro achana nao hawa kuongea nao ni sawa na kupoteza muda, ila bro tofauti na kipindi kile leo nahisi utofauti mkubwa, mara ya mwisho ulionekana ni wa kawaida sana tofauti na sasa ambapo una nguvu nyingi za kiroho mpaka nazihisi hadi kwenye mifupa yangu" aliongea Ben kirafiki

"Nguvu za kiroho ama za kichawi?" Joshua aliuliza

"Vyovyote unavyoona wewe mimi sijali" Ben alimjibu kisha kumgeukia Jimmy na mpaka muda huo helikopta ilikuwa tayari angani ikisafiri

"Nipe siri bro msisimko wa nguvu unazotoa ni wa kipekee sana pia licha ya kwamba uko sawa na sisi katika levo ya damu inayobadilika lakini kuna utofauti wa msisimko wa nguvu kati yetu na wewe" Ben aliendelea

"Ni nyinyi ndiyo mpo hiyo levo sio mimi" alijibu Caren

"Tukiachana na haya mambo ya nguvu nguvu niambie ni nini kimejiri mpaka mkuu wenu kuniharibia siku yangu"

"Iko hivi kundi la wanywa damu limevamia mijiji cha jirani na kuanza kuua raia mchana kweupe" aliongea Caren

"Ooh kwahiyo mpango ukoje?" Jimmy aliuliza akitaka kujua A, B, C ya operesheni hiyo itakavyoenda

"Ni rahisi tu, tunafika mahali husika na mengine ni juu yetu" alijibu Freya na kumfanya Jimmy ashangae na kujiambia kwahiyo wanaenda kichwa kichwa siyo?

"Inaonekana mnajiamini sana asee" aliongea Jimmy na kimya kikafata

"Hey mrembo?" Jimmy alimuita Caren baada ya kuona anaboreka ndani ya helikopta hiyo

"Mbona sihisi nguvu yoyote kutoka kwako tofauti na wenzio?" alimuuliza na Caren wala hakumjibu, alimwangalia kwa sekunde kadhaa kisha kumpotezea

Jimmy kuona hivyo alijua kwamba mwanamke huyo hataki kuliongelea hilo suala na alimgeukiaBen akitarajia labda atamuelezea maana nj yeye pekee ndiye aliyekuwa mropokaji lakini haikuwa hivyo, Ben ni kama vile hakumuona Jimmy na kujifanya yuko bize kuangalia mandhari kupitia dirisha la helikopta

Baada ya kukaa angani kwa zaidi ya dakika arobaini hatimae waliweza kufika mkoa wa, Tanga wilaya ya Handeni katika kijiji husikana kupitia angani waliweza kushuhudia uharibifu uliotokea kwenye kijiji hiko na baadhi ya watu wakiwa wamelala chini ardhini, miili yao isiyo na uhai ikiwa imekauka

"This is Talon 1, we're reached the landing zone, coordinates confirmed, but the area appears insecure, over!" aliongea Rubani wa helikopta hiyo akimaanisha wamefika mahali penyewe lakini sehemu ya kutua si salama

"Then we jump" aliongea Freya akimaanisha wanaruka kutoka juu angani futi 15,000 juu mpaka kwenye ardhi

Hakuna aliyekuwa na pingamizi na wa kwanza kusimama alikuwa ni Joshua

"Tukutane chini" aliongea na kujirusha chini na akafatia Ben kisha Freya halafu Caren na kubaki Jimmy pekee akitabasamu na kujiambia au ndio show-off?
Hata hivyo na yeye hakutaka kuzubaa na huyo alijirusha kizembe kutoka kwenye helikopta hiyo bila woga

"Boom, boom, boom, boom!" vishindo kama vile vimondo kugongana na ardhi vilisikika mfululizo na hawakuwa wengine bali bali ni HIdden Supremacy wenyewe. Walitua vizuri bila madhara yoyote na wote kwa pamoja waliangalia juu angani.

Jimmy alikuwa anganj akianguka tu kibaya zaidi alikuwa amefumba macho kichwa kikiwa chini miguu juu akisikilizia kasi ya upepo na alipokaribia kutua ardhini alijiviringisha sarakasi moja matata

"Exsomnia Gravitus!" alitamka kilatini na ghafla tu kabla hata hajatua ardhini aliiganda hewani ni kama vile hakukuwa na gravity kwa wakati huo. Aliganda kwa sekunde tano kisha kutua chini taratibu kana kwamba hakuwa ameruka urefu mkubwa

Kitendo hicho kiliwashangaza kina Ben, Joshua, Freya na Caren na walianza kumuangalia kwa utofauti

"Nadhani sasa mnaelewa kwanini kamanda amemuingiza kwenye misheni" aliongea Caren akiwaambia wenzake

"Asee kuna harufu kali ya damu na uvundo hili eneo" aliongea Jimmy kana kwamba hakuna kilichotokea

"Hawa Wapuuzi wanapata mpaka uthubutu wa kufanya watakavyo ana kwamba ni chi ya baba yao, Nchi ya amani my foot" aliongea Ben

"Kazi ianze hatupo hapa kuimba ngonjera" aliongea Freya kisha kuchuchuma na kuangalia sehemu ya ardhi na kulikuwa na ute yte flani na katika kufatilia kwa macho ute ule ulipotelea msituni

Kijiji hicho kilikuwa ni katikati ya msitu au kwa lugha nyepesi unaweza sema kimezungukwa na msitu mkubwa na karibia raia wa kijiji hiko wamekimbia makazi yao wengine waliuawa kwa kunyonywa damu na kutokua na binadamu yeyote eneo hilo zaidi ya Jimmy na hidden supremacy

Joshua aliwaangalia wenzake kisha akageuza macho yake msituni ambako ute ute mwingii ulikopotelea na kufumba na kufumbua alichomoka kwa spidi akikimbia kuelekea uelekeo ule

"Damn huyu mpuuzi siku zote huwa anakuwaga wa kwanza kukurupuka" aliongea Ben, naye pia alimfuata Joshua alikoelekea kwa spidi kubwa

Freya na, Caren nao hawakuwa na sababu ya kubaki hapo hivyo nao walielekea upande huo wakimuacha Jimmy peke yake ambaye kwa kumuangalia tu hakuonyesha dalili ya kuwafata bali alitulia tu akiangalia uelekeo ambao wametokomea na kuishia kutingisha kichwa kwa masikitiko

TO BE CONTINUED....
 
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 35: One versus thousands

Jimmy alianza kutembea kuzunguka kijiji hiko maeneo mbalimbali pengine kutakuwa na raia waliojificha wakisubiri msaada.

Baada ya kuzunguka huku na huko katika kijiji hicho aliweza kufika sehemu yenye uwanja mkubwa wa nyasi zenye urefu wa inchi kumi na upande wa mbele ambapo uwanja huo unaishia umbali wa kama mita mia moja kulikuwa na miti mingi mirefu na bila shaka ukitokomea kwenye miti hiyo ni sawa na kuingia msituni

Alisimama kwenye uwanja huo akiangalia kulia na kushoto akijaribu kutafuta chochote kile cha kutilia shaka lakini hakukuwa na jipya zaidi ya hewa na harufu kali isiyoeleweka ni harufu ya nini, ilikuwa ni harufu mbaya zaidi ya uvundo ni kwavile tu mwamba alikuwa anaivumilia

Jimmy alikuwa na masikio yenye kusikia mbali kuliko kawaida na vilevile alikuwa na mafunzo ya hisia.
Aliweza kusikia hatua za miguu na alipoweka umakini zaidi aligundua ni hatua za mtu anaekimbia na kadri alivyozidi kuweka umakini aligundua sio mtu mmoja bali ni hatua za mamia ya watu

Kwakuwa sauti ilikuwa ikisikika kwa mbali hakuweza kugundua inatokea upi hivyo alichuchuma na kugusanisha kiganja chake na ardhi yenye nyasi kisha kufumba macho yake na kuruhusu hisia zake zitawale kujua uelekeo wa sauti hizo na kadri sekunde zinavyoenda ndivyo sauti za hatua zilizidi kuongezeka

"Msaada, jamani msaada!" ilisikika sauti ya mwanamke ikiomba msaada na ndipo Jimmy alipofumbua macho yake na kutazama mbele yake ambapo kulikuwa na msitu mnene lakini kwa bahati mbaya hakuweza kuona chochote kutokana na giza liliopo ndani ya msitu huo

Taratibu mawingu nayo yalianza kutanda angani na kuziba mwanga wa jua na kuonekana kama vile mvua ikitaka kunyesha, kifupi hali ya hewa ilibadilika ghafla

"Eyes of the darkness!" aliongea kwa sauti hafifu na palepale macho yake yalibadilika, rangi ya mboni za macho yake ilibadilika kutoka nyeusi kwenda bluu kisha kusimama

Mbinu hiyo ya jicho la gizani licha ya kwamba inasaidia kuona vizuri kwenye giza lakini vilevile iliwezesha muhusika kuweza kuona umbali mrefu kwa urahisi sana

Alielekeza macho yake mbele ya msitu uliokuwa mbele yake nakwa umbali wa mita chini ya mia na sabini na aliposimama, yaani ukijumlisha mita mia moja za urefu wa uwanja na mita chini ya sabini ya urefu kuanzia kwenye miti kuingia msituni aliweza kumuona mwanamke akikimbia nduki kama kichaa, ilikuwa akianguka anainuka tena na kuendelea kukimbia na hakujali majeraha atakayoyapata kifupi alijali uhai wake zaidi kuliko majeraha ambayo anaweza kupona iwapo atanusurika.

Pia nyuma ya mwanamke huyo umbali wa kama mita mia kulikuwa na kundi kubwa la binadamu wakikimbia kama vichaa waliorukwa na akili. Kibaya zaidi walikuwa ni wachafu kupita maelezo, walichafukwa na damu, wengine walikuwa uchi na hawakuonekana kujali, ni kama vile hawakuwa na akili. Ndugu msomaji iwapo ungepata fursa ya kuwashuhudia mamia ya viumbe hao wenye miili ya kibinadamu ungedhani ni wendawazimu waliotoroka mirenmbe dakika chache zilizopita.

Hivyo Jimmy aliweza kuona kwa urahisi umbali wa zaidi ya mita mia mbili bila shida yoyote

Jimmy hakutaka kuzama msituni bali alisimama palepaleakisikilizia makelele ya hatua mpaka pale yule mwanamke aliyekuwa akiomba msaada kutokelezea kwenye miti iliyokuwa mbele ya macho yake na alionekana amechoka vibaya sana na hata mwendo ulipungua lakini bado tu aliendelea kujivuta kibishi

Alikuwa ni msichana mzungu ambaye kwa kumuangalia tu ungejua ana umri wa miaka kati ya 18 hadi 20, alikuwa amevaa gauni zito lililochakaa na kuchafuka, pia alikuwa akiloa jasho kana kwamba ameibukia baharini, Jimmy alijiuliza huyo mzungu anafanya nini kijijini hapo? Lakini hakupata jibu

"Msaada!... Kaka nisaidie.." aliongea kwa sauti hafifu sana iliyokauka huku akipumua kwa tabu na hapohapo alipoteza fahamu na kutaka kuanguka lakini unadhani Jimmy angeruhusu litokee?

"Exsomnia Gravitus!" Jimmy alinena akimlenga msichana yule na kabla hata kichwa hakijagusa ardhi yenye nyasi aliganda hewani dizaini kama anaelea kwenye maji kisha alimfata na kumbeba msichana huyo na kwenda kumuweka mahali salama alipoona yeye kisha alirudi kwenye uwanja ule akijinyoosha viungo vyake, akiruka na kufanya squarts kadhaa

Dakika si nyingi jeshi la mazombi hatimae liliweza kutoka msituni na kuingia uwanjani ambao uwanja huo uligeuka kuwa uwanja wa vita. Jimmy ni kama vile alikuwa anajua watafika muda gani kwa kupiga mahesabu kulingana na mbio zao alizozipima kwa hisia.

Ni nusu tu ndio waliweza kukanyaga uwanjani na wengine wakiwa bado msituni na wote walikuwa wamesimama wakimuangalia Jimmy. Hiyo ni kutokana na msisimko wa ajabu waliokuwa wakiuhisi. Waliachana umbali wa mita hamsini

"Mnazubaa nini si mlikuwa mkifukuzia mwili mkitaka kuufanya kitoweo? Haya sasa ndio mimi nimegeuka kuwa mwanaume" aliongea Jimmy licha ya kujua kwamba hawatamuelewa

Mmoja wa mazombi walio mstari wa mbele ni kama vile ameelewa alichomaanisha Jimmy kwani alinguruma kama simba na huyooo! na wenzake wakamfuata nyjma. Ni kama vile askari wakisubiri Jenerali achukue hatua ndio wao wafuate

Zilikuwa ni mbio za mamia ya mazombi kuwahia kitowea ambapo kitoweo hiko nacho kilikuwa kikiwasogelea

Wa kwanza kukaribiana Jimmy alitandikwa ngumi moja takatifu yenye ujazo wa kutosha kichwani ambayo ilimpeleka moja kwa kuzimu kwani kichwa kilipasuka poof! Kama puto lichomwavyo na sindano

°°°°°°°°°°

NATIONAL SECURITY COUNCIL BRIEFING ROOM

Ndani ya chumba maalum cha usalama wa taifa kwenye meza kubwa ya mbao alionekana Jenerali John Merizesta akiwa katika gwanda zake safi amesimama, mbele ya macho yake walionekana viongozi wakubwa wa serikali wanne wameketi macho yao yakitazamana na ya Jenerali huyo

"Jenerali tumekuwa tukipokea taarifa—tata. Vifo vingi. Miili haina damu. Raia wananong’ona kuhusu… viumbe vya ajabu" aliongea kiongozi wa kwanza

"Je uvumi huu kuhusu wanywa damu ni kweli?" aliuliza kiongozi wa pili

"Mpaka mnapata taarifa kilichotokea Tanga na kinachotokea Tanga si uvumi tena huo ni ukweli? Kwa miaka mingi mmekuwa mkipuuza kuhusu hili ila nadhani madhara yake yamewafanya muamini sasa" aliongea Jenerali huyo

"Imewezekanaje kutokea chini ya uangalizi wetu? Na kwa kasi hii?" aliongea kiongozi wa tatu

"Tatizo linaanzia kwenu, zile kauli zenu za kukanusha licha ya dalili kuonekana. Jeshi lilitoa ishara na ushahidimkapuuza na kutokuamini" alimjibu

"Jenerali kwahiyo unatushumu sisi kupuza tishio la kitaifa?" aliongea wa nne

"Sio shutuma ni ukweli mlioukataa kwa muda mrefu, ni matumaini yangu mheshimiwa raisi ameliona hili na kulifanyia kazi" aliongea Jenerali huyo

"Kwahiyo tunalitatuaje hili?" aliuliza kiongozi wa kwanza

"Ukweli hakuna haja ya nyinyi kusumbua kichwa kuhusu hili tatizo" Jenerali aliwatuliza

"Elezea vizuri"

"Nimeshapeleka kikosi maalumu kazini, wamefundishwa kudili na hali kama hizi kwa utaalamu wa hali ya juu hivyo msiwaze sana. Sasa wako kimya ishara ya kuwa wako kazini"

"Bila kibali?"

"Mimi ni Mkuu wa majeshi, kibali kutoka kwa nani ilihali jeshi naliongoza mimi? Au mnataka kusema kwa muheshimiwa raisi ilihali ndiye mstafi wa kwanza kulipuuza?" aliongea Jenerali John na kuwafanya viongozi wale kuangaliana wenyewe kwa wenyewe

"Ni kikosi gani? Jeshi? Upelelezi?" aliuliza kiongozi wa kwanza

"They operate under a silent protocol independent, autonomous, and invisible by design. We call them Unit 9-H. But internally… they’re known as Hidden Supremacy." aliongea Jenerali akimaanisha "Wanafanya kazi chini ya itifaki ya kimya inayojitegemea, na isiyoonekana kwa muundo. Tunawaita Unit 9-H. ndani ya mfumo ... Lakini wanatambulika kama Hidden Supremacy."

"Kwahiyo hawa wanywa damu ni viumbe gani hasa?" aliuliza kiongozi wa nne

"wachukulie kama vichaa flani hivi wanaopandwa na mashetani kiasi cha kupoteza ubinadamu wao au kwa lugha nyepesi tuwaite mazombi" aliongea Jenerali huku akitabasamu tabasamu la ajabu kana kwamba anawatisha

°°°°°°°°°°

Ukisikia kukuru kakara basi ndio huku sasa kwani mamia ya miili ya viumbe hao isiyo na uhai ilizagaa kila kona ya uwanja na nyasi za uwanja huo kuchafukwa na damu, na waliobaki walikuwa si chini ya mia mbili. ukijumlisha na waliokufa kwa hesabu ya haraka haraka unapata idadi ya mazombi mia tatu na ushee na hapo ni mia tu ndio aliopoteza uhai kwa kutobolewa mioyo na kupasuliwa vichwa

Jimmy alionekana kuchafuka mnoo zile nguo alizovaa sare na mpenzi wake zilikuwa hazitamaniki tena

Viumbe wale licha ya kubakia mia mbili lakini walionekana kutotosha hivyo walianza kunguruma tena ishara ya kuwaita wenzao walioko msituni

"Pumbavu!" Jimmy alilaani baada ya kugundua wanawaita wenzao zaidi alijiambia hayo ndo madhara ya kuja kichwa kichwa pasipokuwa na mpango madgubuti na aliwaza wenzake aliokuja nao huko waliko wanafanya nini

Hazikupita dakika nyingi tu Jimmy allizingirwa na mamia ya wanywa damu na kukamilisha idadi ya zaidi ya wanywa damu elfu moja, vutavpicha mtucaliesimama katikati ya uwanja wa mpira halafu viti vya mashabiki vilivyomzunguka ndio walikuwa hao mazombi, kifupi kijiji kizima kilifunikwa na maelfu wanywa damu kana kwamba kuna mkutano wa kukisengenya chama cha siasa

"Ni muda sasa!" aliongea na kuangalia juu angani kwa sekunde kadhaa na kushusha kichwa chake chini akitoa na tabasamu la kikatilivkana kwamba amemnasa adui mtegoni

"Awaken!" alinena na ghafla upepo mkali ulianza kuvuma huku ukungu wa buluu usioeleweka umetokea wapi ulimfunika mwili mzima kuanzia kichwani mpaka miguuni na kutengeneza jmbo kama lake ni kama vile alikuwa na miili miwili mmoja wa nyama mwingine wa ukunhu

Macho yake ya bluh nayo yaliongezeka rangi na kukolea kiasi kwamba ungedhani ni tochi mbili zimulikazo. Ni dhahiri kwamba alikuwa katika uwezo wake wote katika levo aliyofikia

"Infinite gravity! Over a thousands let weight become wrath" alinena akimaanisha "Mvutano usio na kikomo! Juu ya maelfu na uzito uwe ghadhabu" na ghafla mkandamizo wa hewa wa hali ya juu ulitokea katika kijiji hicho kiasi kwamba nyumba kadhaa za makuti na tofali zilianza kubomoka. Pia maelfu wote ya wanywa damu walikandamizwa kisawasawa mpaka ardhini wakiugulia maumivu, ilionekana hata sauti walishindwa kutoa na kuonekana kama mabubu wanaotapatapa wakijaibu kunyanyuka, wengine kujiburuza lakini ilishindikana

"Oh shit!" Jimmy alimaks baada ya kugundua kitu na kufumba na kufumbua alipotea pale alipo na kutokelezea sehemu ambayo alimficha msichana yule wa kizungu ns kumkua ameshazinduka na alikuwa akiteseka na mkandamizo wa ghafla uliotokea na ni bahati tu nyumba hiyo aliyofichwa haikubomoka

"Ngao takatifu ya hewa na ikufunike!" Jimmy alinena kama vile anamuombea msichana huyo huku akimnuooshea koganja cha mkono wake wakulia na ghafla ngao ya hewa ilijitengeneza kimaajabu na kumfunika msichana yule na kisha kutoka ndani humo

Alifika nje na kuwashuhudia maviumbe hayo yanavyoteseka na kujiambia ngoja awawaishe kuzimu angalau kutawapunguzia kuteseka sana. Ni huruma ilioje!

"Shwii! Shaa! Fwuuuu! Shaa!" ilikuwa ni milio ya hewa kusuguana kutokana na spidi aliokuwa akitumia Jimmy na vichwa vya maelfu ya hao wanywa damu vilitenganishwa na miili yao na ndani ya nusu saa aliweza kuwashughulikia wote na kubaki peke yake na ile anamaliza tu ghafla alianza kuhisi maumivu ya viungo vya ndani na akili kutaka kumtawala

"pfft … pfft … pfft” Jimmy alitema damu mara tatu mfululizobkiasi cha kudondoka chini na kupiga magoti na ule ukungu uliomfunika ulipotea na macho yake yalirudi kawaida pamoja na mkandamizo wa hewa kuacha pia na hata ile ngao ya hewa iliyotumika kumkinga msichana yule wa kizungu ilipotea. Yaani vilipotea vyote kwa pamoja na sababu ya kupotea ni kukosa mawasiliano na chanzo kikuu ambacho ni nguvu za Jimmy zilizojizima

Jimmy alionekana kulegea sana, ilionekana nguvu alizotumia ni kubwa sana kiasi cha yeye kutohimili kwa muda mrefu na huyo mdogo mdogo alipoteza fahamu na kuanguka chini

°°°°°°°°°°

Anakuja kushtuka muda ukiwa umeenda sana, giza tayari lilikuwa limeshaingia na alikuwa amelala kwenda mkeka kifua wazi pamoja na boksa ndani ya nyumba mojawapo ya kijiji hiko iliyonusurika kubomoka. Pia alikuwa amesafishwa mwili wake

Pembeni yake mita tano na alipolala kulikuwa na moto ukiwa unawaka na bila shaka ulikuwa ukizuia baridi pamoja na kutoa mwanga ndani ya nyumba hiyo ndogo

Aliinuka taratibu na kukaa kitako na kujikagua na alishangaa kukuta yale makovu aliyokuwa nayo mwilini yamepotea na kuonekana imara kabisa isionekane kovu hata moja na kitendo hiko kilimuacha na maswali mengi yasiyo na majibu na aliona bora apotezee kwa muda kuliko kuumiza kichwa muda huo

Alipogeuka upande wake wa kushoto aliweza kuona nguo nyingine zimekunjwa pembeni yake na hakujiuliza mara mbili mbili alizivaa na zilionekana kumtosha

"Hawa wajeda wamepotelea wapi?" aliwaza Jimmy akimaanisha unit 9 H aliokuja nao

Wakati anazunguka zunguka ndani ya kijumba hiko yule msichana mzungu aliingia ndani humo akiwa amebeba ungo uliosheheni viazi na mihogo mibichi na ilionekana imetoka kuchimbwa muda si mrefu

"Umeamka!" aliongra msichana yule waa kizungu huku akitabasamu

Mara ghafla Jimmy alihisi msisimko wa nguvu unakaribia eneo hilo na haraka alimpa ishara msichana huyo anyamanze kisha kutega masikioyake kwa umakini akisikilizia.

Je wenzake Jimmy wako wapi?

Na ni nani anayesogelea mahali walipo Jimmy na msichana huyyo?

TO BE CONTINUED.....

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 36: Binadamu watatu

"Kuna nini kw.." kabla hata hajamaliza sentensi yake Jimmy alimsogelea haraka na kumuwekea mkono mdomoni huku kwa haraka akimvuta na kujificha nyuma ya mlango

"Sshhh" alinong'ona huku akimkazia macho msichana yule wa kizungu

Msichana yule pia alikuwa akimuangalia Jimmy usoni na alimtii huku akitulia tuli, ukweli mwanamke huyo alibarikiwa kuwa na sura nzuri sana na mashavu mamono pamoja na macho makubwa yenye kuvutia, kifupi alikuwa na sura kama ya kitoto fulani hivi. Umbile lake nalo lilikuwa si haba

Dakika moja si nyingi aliingia mwanaume ndani humo ambaye alionekana kujeruhiwa vibaya sana na alikuwa amejikaza na hakuwa mwingine bali ni Ben

Haikuwa na maana kwa Jimmy kujificha ilihali alikuwa akisambaza msisimko ambao unaweza kuhisiwa na mtu kama Ben hivyo alitoka mafichoni

"wenzako wako wapi?" Jimmy alimuuliza

"Hali si shwari wako hatarini" alijibu Ben huku akigugumia maumivu

"Kwahiyo umewaacha wateseke"

"Hakukuwa na namna zaidi ya mmoja wetu kutoka kuomba msaada, vifaa vya mawasiliano vimeharibiwa"

"kwahiyo unataka kuniambia wale vichaa wanauelewa na vifaa vya mawasiliano?"

"ukweli hatukutegemea kitu kama hicho kutokea" aliongea Ben kisha kumuangalia mwanamke aliyekuwa nyuma ya Jimmy

"Huyo ni nani?" aliuliza na Jimmy kugeuka na kumuangalia yule msichana ambaye muda huo alikuwa akiwatazama tu

"Naitwa Mia" alijitambulisha kwa ufupi kwa lugha ya kiswahili yenye lafudhi kama ya mzawa

Baada ya kujitambulisha aliweka ungo wake chini kisha kuwasogelea wanaume hao

"Vua vazi lako la juu" alimwambia Ben, Ben kusikia vile alimwangalia Jimmy kutaka kujua msichana huyo anataka kufanya nini mpaka kumwambia avue shati lakini Jimmy alikuwa akimwangalia tu asimwambie lolote

"Usiwaze sana unaonekana kuwa na majeraha ninachotaka ni kusaidia kuponya majeraha yako" aliongea Mia na kumfanya sasa, Jimmy aelewe, inaonekana aliyehusika na makovu yake mwilini alikuwa ni huyo msichana aitwaye Mia

"Unataka kusema unaweza kuniponya majeraha? Wewe ni nani?" Ben aliuliza

"Acha maswali mengi bro fanya kama unavyoambiwa" aliongea, Jimmy na Ben bila ubishi alivua vazi lake la juu na baada ya kuvua Mia alimpa ishara ya kukaa chini na alikaa

Mia alimsogelea Ben na kupiga magoti karibu yake na kugusa majeraha kwa viganja vya mikono yake miwili kisha kufumba macho na midomo yake kucheza kama vile anasali

Ghafla mwanga hafifu wa rangi ya kijani kibichi ulionekana kutoka kwenye mikono ya msichana huyo iliyogusanisha na majera na kadri sekunde zilivyozidi kusonga majeraha yalianza kupona taratibu bila kuacha hata kovu. Aliendelea hivyo hivyo kwenye majeraha mengine mpaka alipomaliza kumponya majeraha yote

"Ni miujiza ya uponyaji iliyoje" alijiambia Jimmy kichwani mwake baada ya kushudia maajabu hayo

Mia baada ya kumaliza alinyanyuka taratibu lakini ghafla alianza kuhisi kizunguzungu na kupoteza balansi ya kusimama lakini Jimmy alimuwahi asihanguke

"Nipo sawa" aliongea Mia akitaka kutoka mikononi mwa Jimmy lakini alishindwa kutokana na Jimmy kukaza

"Hauko sawa, umefanya kazi kubwa ya kutusaidia kuponya majeraha licha ya kwanza unaonekana na nguvu za upanyi lakini unapotumia nguvu za mwilini hupungua" aliongea Jimmy huku akimkazia macho

"Asante" Jimmy alimshukuru na kumfanya Mia akwepeshe macho yake

"Mimi pia" Ben naye alidakia

"Ni jambo dogo tu nilichotaka ni kulipa fadhila maana bila wewe wangeninyonya na mimi" aliongea, Mia baada ya kufanikiwa kujitoa mikononi mwa Jimmy huku akuibeba ungo wake wenye viazi na mihogo

"Hey bro ni wewe ndiye umedili na hiyo miili iliyozagaa uko nje?" aliongea Ben huku akionekana kutoamini lakini Jimmy alimpa ishara ya kwamba "uamini usiamini hilo ni juu yako"

"Pia Mia wewe ni nani? Inakuwaje unakuea na nguvu za ajabu namna hiyo? Kwanini uko hapa?" aliuliza Ben lakini Mia alionekana kutotaka kujibu

"Tuachane na maswali yako wenzako wako wapi?" Jimmy aliamua kuingilia baada ya kuona jamaa ana maswali mengi

FLASHBACK

Baada ya wanne hao kuzama msituni na kumuacha Jimmy akiwaangalia walianza kufuatili ute ute mwingi uliokuwa umepotelezea msituni huko

Baada ya mbio za dakika kadhaa hatimae waliweza kufika sehemu yenye uwazi na miti michache na mbele ya macbo yao kulikuwa kuna pango dogo la mawe yasiyojulikana nivya aina gani likiwa katika muundo wa pembe tatu kama vile Bermuda triangle
Ilishangaza kuona kuna pango katikati ya msitu huo, lilikuwa kama vile ni lango la kuingia ulimwengu mwingine na kwa wakati huo huo kuonekana kama pango dogo la kujikinga wakati wa baridi na mvua

"Ni maajabu yalioje" aliongea Joshua akivutiwa na mawe yaliyotumika kuunda pango hilo

"Kuna mengi sana ya kuvutia kwenye dunia hii ndugu yangu usishangazwe na hako kapango au sio bro.. " aliongea Ben huku akitabasamu huku neno bro akimlenga Jimmy lakini hakuweza kumuona

"Hey yule braza yuko wapi?" Ben alimuuliza Caren

"Jimmy?"

"Kumbe anaitwa Jimmy, ndio yuko wapi? Mbona sihisi uwepo wake eneo hili"

"Unamtaka? Unaweza kurudi tu kama unashida nae tumemuacha kijijini" aliongea Freya

"We manzi mzungu huu sio uungwana unajua? Unamchukulia poa sana au ni kwasababu ulimsaidia miaka ile mikononi mwa wale wanywa damu?" alimuuliza Ben

"Hata kama namchukulia poa unasemaje? Hakupaswa kushirikishwa kwenye hii misheni kisa tu amebahatika kuwa vijinguvu sawa na sisi... Inaonekana hata mkuu hatuamini vya kutosha." Freya alimjibu

"Hehe nishaelewa sasa, inaonekana kinachokuuma ni kwasababua l ya yeye kuweza kuwa na nguvu na hata kutufikia.. ooh sio kutufikia ni kukufikia ndani ya muda mfupi.. Imekuchukua miaka kumi na mbili mpaka kufika hapo ulipo lakini kwake ooh itapendeza nikisema "mtu uliyemuokoa" ame.. ..."

"Shut up you stupid imbasile!" Freya alimfokea kabla hata Ben hajamaliza sentensi yake

"Tafadhalini huu sio muda wenu wa kugombana, tumalizane kwanza na kile kilichotuleta ndio muendelee na ugomvi wenu na sitoingilia hata mkipigana" Caren aliingilia

Shida huyu mzungu wivu unamsumbua haiwezekani kila mtu ni wakumuonea wivu" aliongea Ben na kumfanya Cafen kukasirika kiasi kwamba alitaka kumshikisha adabu lakini Caren alimuwahi na kumpa ishara atulie

Freya aliishia kumkazia macho makali Ben huku Ben akimpa tabasamu flani hivi ni kama anamwambia "nimefurahi kukuona unakasirika"

Caren aliwapotezea na kisha kuangalia ardhini ambako kulikuwa ute mwingi umesambaa na moja kwa moja ulielekea kwenye lile pango dogo na bila shaka ilionekana ndiko walikotokea viumbe hao

"Tunaingia" aliongea Caren na kuwapa ishara wenzake kuwa tayari na kisha kuwa wa kwanza kuzama ndani akifuatiwa na Joshua kisha Freyya na mwisho Ben

°°°°°°°°°°

`Yule manzi licha ya kutokujali uwepo wako lakini ndiye aliyenitaka nije kukutafuta kuomba msaada na kufanikisha mpaka nikatoka mikononi mwa wale watu" aliongea Ben akimwelezea Jimmy

"Umesema baada ya kuingia ndani ya lile pango mlijikuta mko katika jangwa?" Jimmy alimuuliza

"Ndio, na pia kulikuwa na binadamu watatu wenye asili ya Asia" Ben alimjibu kwa urefu

"Nini kikafuata?" Jimmy alimuuliza

"we unadhani ni kitu gani kama sio kupigana? Inaonekana wao ndio walioko nyuma ya pazia kuhusiana na hawa wanywa damu" aliongea Ben na kumfanya Jimmy ashushe pumzi ndefu

"Kipi kinakufanya uamini kwamba wanahusika na hawa mazombi"

"Ni chungu, japokuwa sijui ni chungu cha nini lakini nilikuwa napata hisia ya ajabu ni kana kwamba kuna maelfu ya nafsi zimefungwa ndani ya chungu hiko"

"pango lenye muundo wa pembe tatu, binadamu wa tatu na chungu" Jimmy alikuwa akiwaza

"Pumbavu! Wale walozi wako mpaka huku!" alipayuka baada ya kukumbuka kitu

"Unawajua?" Ben alimuuliza Jimmy

"Nadhani hao binadamu watatu unaowazungumzia nimewaona pia" aliongea Mia

"Na ndio sababu ya wewe kukimbizwa na kundi la hao mashetani?" Jimmy aliuliza na Mia alitingisha kichwa kukubaliana nae

"Wakati wanavamia Kijiji mimi sikuwepo nilitoka kwenda msituni, huwa ni ratiba yangu kila saa sita natoka kijijini na kwenda mto saunyi na wakati wa kurudi nilipita njia nyingine na kukutana nao wamewateka baadhi ya watu kutoka vijiji vingine" Mia alieleza kwa ufupi sababu ya yeye kukimbia na kukimbizwa na wale mashetani

Ukweli sababu ya yeye kukimbia ni baada ya kushuhudia wakifanya utekaji na kukimbia baada ya kushtukiwa, hakujua kama atakimbizwa na yale mazombi na kwa bahati nzuri amenusurika baada ya kukutana na Jimmy

"Twende!" Jimmy alimwambia Ben na kabla ya kuondoka alikumbuka kitu

"Simu, simu yangu iko wapi?" Jimmy alimuuliza Mia

Uzuri Mia aliihifadhi mahali wakati anavivua nguo za Jimmy kumponya makovu hivyo alikwenda kuichukua na kimpatia

Simu yake ilikuwa imepasuka kioo kana kwamba ilipigwa ngumi na kusababisha nyufa nyingi. Licha ya hivyo bado ilikuwa ikifanya kazi na baada ya kuiwasha aliweza kuona saa ikisoma saa moja na dakika kumi pamoja na missed calls kumi na nne na jumba nyingi

Kati ya missed calls kumi na nne, nane zilikuwa kutoka kwa Biancalina, mbili kutoka kwa mama yake mzazi, mbili kutoka kwa Cid na mbili kutoka kwa dada yake Monica

Jimmy aliishia kumeza mate mengi tu na kujiambia inamaana alikuwa akitafutwa hivyo?

Kati ya missed calls ni namba ya Cid pekee ndiyo aliona inafaa kupiga kwa wakati huo

"Vipi shemeji" aliongea Jimmy baada ya simu kupokelewa

"Bro tuachane na ushemeji, hivi mbona hunitakii amani?" aliongea Ciid upande wa pili

"Kuna nini?

"Kwanza uko wapi?"

"Niko Tanga"

"Nini! Bro mbona hutulii? Kuangaika kwako kunanikosesha amani ujue. Uliondoka wapi sijui na baada ya miaka mitano unarudi lawama naangushiwa mimi, sasa hivi umerudi haijapita hata wiki ushaanza kuruka, napigiwa simu na Bianca kuulizia ulipo na nimewaambia sijui lakini haniamini ameenda mbali mpaka kunichongea kwa mke wangu kwamba nakataa kusema ulipo na hata mke wangu haniamini eti kisa nilihusika na wewe kuondoka kipindi kile, nina stress za kulea mtoto na bado unaletea stress zako huu sio uungwana kabisa" Cid alianza kutoa lawama

"vumilia bro fanya unikingie kifua we waambie tu soon narudi"

"Unatakiwa ufike kabla ya saa tatu"

"Saa tatu kuna nini?"

"Inaonekana Bianca hajakwambia"

"Sasa si unieleze"

"Iko hivi saa tatu Biancalina anatakiwa kuhudhuria mualiko wa Marriage anniversary ya thelathini ya msanii mkongwe nchini na siku hiyo pia kuwa siku ya kuzaliwa ya mtoto wao mpendwa"

"kumbe ndio sababu alikuwa anakomalia kwenda, shopping asubuhi asubuhi" Jimmy alijiwazia

"Asante kwa taarifa bro nitawasili kama muda unavyosema by the way unahudhuria?"

"Ningependa kuhudhuria maana nimesikia mzee ametumia ushawishi wake kwenye sanaa, pesa nyingi na koneksheni kuweza kuwaleta wasanii maarufu barani Asia na duniani kote kwa ujumla wajulikanao kwa jina la Four souls nchini ili kuja kutumbuiza kwenye siku hiyo, nimepata mualiko pia"

"Kwanini usiende sasa"

"Kaka najuta sana kuoa mapema yaani sina uhuru kabisa, unadhani dada yako angeniruhusu nikazurure usiku nimuache na mtoto peke yake?"

"Hehe! Pambania kujenga familia bro ujana ushakuishia sahivi we ni mzee, pambana kulea mtoto" aliongea Jimmy huku akicheka na kusababisha kukatiwa simu

Walitumia dakika saba tu kuweza kuzungumza kwenye simu na kumaliza

"Mia sisi tunatoka" aliongea Jimmy huku akivaa viatu vyake

"Subirini kwanza.." aliongea na kisha kuchukua viazi vitamu vibichi.na kuwarushia na walidaka

"Mtie chochote tumboni angalau mpate nguvu kidogo, isitoshe mmepoteza ngucu kudili na hawa viumbe" aliongea Mia kuwafanya wanaume hao kutabasamu tabasamu la shukrani

°°°°°°°°°°

Dakika kadhaa mbele Jimmy na Ben walikuwa wamesimama eneo la wazi msituni wakitazama pango la pembe tafu lililokuwa mbele yao

"Ndio hapa" aliongea Ben na kumfanya Jimmy alichunguze kwa dakika mbili bila kusema chochote

"Hili sio pango licha ya kuonekana kama pango" aliongea Jimmy

"Unataka kusema..."

"Ndio inaonekana hili ni lango la kuingia ulimwengu mwingine , ushawahi kusikia Bermuda Triangle? "

"Ndio inapatikana kusini mwa bahari ya antlantic na inasemekana meli zipitazo sehemu hiyo hupotea pasipo kuacha ushahidi wa aina yoyote pia inasemekana japo hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba ni lango la kuingilia ulimwengu mwingine ulioko chini ya maji, lakini mimi siamini"

"Bado mpaka sasa huamini tu licha ya kushuhudia kwa macho yako"

"Unamaanisha nini"

"We si umesema baada ya kuingia humo mlitokezea jangwani?"

"Unataka kusema kwamba ni ulimwengu mwingine tumeingia?"

"Bro inaonekana akili yako inafanya kazi polepole... Mpo msituni mnaingia kwenye pango mnajikuta jangwani bado hujaelewa tu" aliongea Jimmy huku akitingisha kichwa kwa masikitiko

"Japokuwa sijawahi kushuhudia ila nimesoma kuhusu mambo ya aina hii. Kuna hadithi za kale zinazosema kuna maeneo duniani ambayo ni ‘miingilio’ ya dunia nyingine ambapo sheria za asili hazifanyi kazi kama tunavyozijua" aliendelea

Jimmy alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kisha kupiga hatua na kuingia ndani ya pango hilo akifuatiwa na Ben

Baada ya kuingia tu walijikuta wametokezea upande mwingine, kukiwa jangwa tupu na majira kuonekana kama asubuhi ya saa kumi na mbili bila ya kujua chanzo cha mwanga hafifu ni nini maana angani hakukuwa hata na jua wala mwezi wala nyota. Pia baridi lilikuwa si la kitoto ni bahati tu walikuwa na mafunzo na nguvu zisizo za kawaida kuweza kuhimili

Jimmy alikuwa akishangaa eneo hilo na bila shaka ilikuwa nj mara yake ya kwanza kuingia kwenye ulimwengu usio na kitu chochote zaidi ya jangwa tu na mbele yake umbali wa kama mita thelathini na aliposimama aliweza kuwaona wenzake wakiwa katika kuelekea kukata tamaa kwenye pambano dhidi ya binadamu watatu, kwani walionekana kuchoka sana na kujeruhiwa na hata kusimama kwao kulikuwa ni kwa tabu sana

TO BE CONTINUED.....

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 37: It's Fury!

Pia ukiachana na hao kulikuwa na miili ikiwa imezagaa chini mchangani, ilikuwa ni miili ya wanywa damu si chini ya mia na ilionekana walitumia nguvu sana kuwashughulikia

Wale binadamu watatu na wakina, Caren waliweza kuhisi ongezeko la watu wawili na walipoangalia kupitia lango la kuingilia waliweza kumuona Jimmy na Ben

Kati ya wale watatu mmoja alibeba chungu cheusi cha wastani chenye michoro ya ajabu rangi ya dhahabu, wa pili alibeba kitu kama box la wastani ambalo limefunikwa na kitambaa kulisitiri, na wa tatu alikuwa mikono tupu

"J? Unafanya nini hapa? Na umefikaje huku?" aliongea mmoja wa wale binadamu watatu aliyekuwa mikono tupu akimtazama Jimmy

"Hilo swali nilipaswa kuwauliza nyinyi, mnafanya nini huku?" aliongea Jimmy

"Sisi kufanya nini huku kunakuhusu nini?" aliongea mwingine kwa kiburi aliyebeba chungu

"Nilidhani kuwasamehe kutawafanya muungame dhambi zenu ila inaoneka nilikosea kuwaonea huruma, na huruma yangu imewafanya muwe na kiburi na tamaa zaidi" aliongea Jimmy hukucakiwakazia macho

"Nasikia unaheshima sana freewill bwana J" aliongea aliyebeba boksi

"Mpo kwenye nchi yangu, mnaua mamia ya wanakijiji halafu mnaongelea kuhusu uhuru wa kuchagua? Mnaona mimi fala mwenzenu si ndio" aliongea Jimmy kikauzu

"Unakosea kusema nchi yako, hatupo tena kwenye nchi yako tupo ulimwengu mwingine" aliongea aliyebeba chungu

"Vyovyote vile nimesema mpo kwenye nchi yangu, lango mlilotumia kufika hapa ni la nchi yangu hivyo ni mali yangu pia, tukiachana na hilo mmesababisha machafuko na kuuwa raia wa nchi yangu"

"Tangu lini umekuwa raisi wa nchi mpaka kuimiliki?" aliongea aliyekuwa mikono tupu

"Inaonekana wewe ni empty set kabisa, hivi hujui kwamba nchi ni mali ya wananchi? Hata huyo raisi anateuliwa na wananchi wewe kunguni usiye na akili" aliongea Ben

"Bro kuongea nao ni sawa na kupoteza muda" Ben aliendelea kuongea huku akiwakazia macho watu wale

Ghafla Caren, Freya na, Joshua waliishiwa nguvu na kukosa udhibiti na kuanguka chini mchangani kwa magoti huku Caren ndiye aliyeonekana kutia huruma zaidi

" Hawa rafiki zako niseme tu ni wako imara sana lakini inasikitisha kwamba si ligi moja nasi"aliongea aliyekuwa mikono tupu

" Hio ni kwasababu nyinyi ni walozi hivyo ni sawa kusema si ligi yenu" aliongea, Jimmy

"Bro inaonekana unaonekana unawajua hawa watu, ni wakina nani?" aliuliza Joshua kwa sauti hafifu

"Soul shifters! Kuhusu majina yao hata sikumbuki ila huyo aliyebeba chungu tunaweza kumuita punguani, halafu huyo aliyebeba boksi ni pimbi na huyo mikono mitupu ni kunguni tu" Jimmy alijibu

"pumbavu! Unathubutu vipi kututukana?" aliyebeba boksi alifoka lakini Jimmy alimpotezea

"Nini? wabadili nafsi?" Ben aliuliza kwa mshangao

"Ndio hawa washenzi ni walozi wanaobadili nafsi za wengine. Mwanzoni nilijua hawa viumbe ni wachawi waliopoteza ubinadamu wao kutokana na kutumia sana mbinu ya damu inayobadilika lakini inaonekana nilikosea" aliongea, Jimmy

"Inamaana hao wanywa damu ni binadamu ambao nafsi zao zimebadilishwa?" alouliza Ben

"Ndio mi nilidhani hawa washenzi wanahusika kwenye kubadili nafsi za binadamu kwenda kwa binadamu wengine ila safari hii wameenda mbali sana mpaka kuingiza nafsi za mashetani kwenye miili ya binadamu huku nafsi za hao binadamu wakiziteka na kuzifungia ndani ya chungu" Jimmy alieleza

"Shabash! Hawastahili kuishi hawa washenzi" alimaka Freya kwa tabu kutokana na maumivu

"Hujakosea hawa walozi wanastahili kwenda kuzimu" alidakia Joshua

"Nyinyi vikaragosi bado mnathubutu kuongea tu, inaonekana kipigo bado hakijawaingia" aliongea aliyebeba chungu lakini walimpotezea na mkwara wake

"Hisia zangu zilikuwa na sahihi kuna nafsi zimefungwa kichawi ndani ya chungu" aliongea Ben

"Licha ya chungu hicho kutumika kuteka nafsi lakini vilevile kina nafsi za mashetani zikiishi ndani ya hiko chungu, ushawahi kusikia Tartarus?"

"Hapana" Alijibu Ben

"Itakuwa ngumu sana kukueleza ila kwa lugha nyepesi Tartarus ni neno la kigiriki lenye maana ya Gereza la nafsi ambako nafsi ovu za mashetani hufungiwa" alieleza kwa ufupi

"Kwahiyo hiko chungu ni gereza la nafsi!" Ben aliongea na Jimmy alitingisha kichwa kukubaliana nae

"Niwe mkweli huwa nakukubali sana upande wa maarifa, inaonekana unajua mengi sana" aliongea ambaye jimmy alimtambulisha kama punguani

"Aya sasa muda wa ngojera umekwisha ni wakati wenu wa kwenda kukutana na ndugu zenu walozi huko kuzimu" aliongea Jimmy kikauzu na ghafla aliziamsha nguvu zake za kichawi

"Awaken!" alitamka na upepo ukaanza kuvuma lakini ulikoma muda huo huo na Jimmy kuanza kutema damu

"pfft... Pfft.." alitema damu na mwili wake kuanza kulegea hata yeye mwenyewe alijishangaa

kitendo hiko kiliwafanya maadui kutabasamu na kumuangalia Jimmy kwa macho ya dharau na furaha ya kwenda kumshinda

"Nilikuwa na hofu ya bure tu, lakini nani angejua hofu yangu ingebadilika na kuwa ujasiri" aliongea mtu yule aliyebeba boksi

"Inaonekana bahati imetuangukia haha! Golden chance never comes twice lazima nihakikishe nawapeleka kuzimu" aliongea aliyekuwa mikono tupu

"Uzito wa tani millioni moja wa hewa!" aliongea yule bwana mwenye mikono mitupu na ghafla hali ya hewa ilibadilika na kuwa nzito kiasi kwamba ikawa tabu kupumua

Upande wa Caren na wenzake walionekana wanaelekea kukata tamaa kwani waliemtegemea kuwaokoa naye anapitia tabu kama wao

" Bro fanya kit..u" aliongea Ben kwa kujalizimisha kana kwamba amekabwa

"Caren! Caren!.. Car..en!" aliita Freya baada ya kumukna mwenzake akipitia mateso kuzidi wao na macho yake yalikuwa yakianza kupoteza uono, na bila shaka muda wowote angepoteza uhai kutokana na tabu ya kupumua

"Jimmy tafadhali fanya kitu tunakwenda kufa, Tunakwenda kumpoteza Caren" hakuwa Freya yule mwenye kiburi tena bali mwenye kuomba kusaidiwa ilionekana alikuwa na ukaribu sana na Caren

"Hahaha.. Hahahaha! Ni drama ilioje" aliongea bwana huyo kunguni

"Awaken... A. awak.en.. awaken! Aaa..." Jimmy alikuwa akijaribu kuziamsha nguvu zake lakini haikusaidia kitu na badala yake alipoteza nguvu na kutema damu mdomoni

Jimmy alimwangalia Ben anayehangaika kupumua kisha kuwaangalia na wengine na kupatwa hisia za ajabu zisizoeleweka

" Hakuna kukata tamaa...msiruhusu mioyo yenu ikubali..kushindwa, nimepigana vita vingi sana na unajua kwanini bado niko hai? ni kwasababu sikati tamaa...nyanyukeni mmpambane haijalishi ni nguvu kiasi gani mlizobaki nazi au mateso gani mnapitia mnatakiwa kupambana bila kukata tamaa" aliongea Jimmy kwa sauti hafifu lakini yenye kusikika vyema akijaribu kuwashawishi kuwa-motivate wasikate tamas huku akijinyanyua na kujikaza

"Sababu ya mimi kuwa hai sio kwasababu ya nguvu nilizonazo bali ni Hasira ya kutokata tamaa hasira kuu.. Its fury!

Ni hasira si chuki, si ghadhabu isiyo na mwelekeo, ni moto unaokataa kuzimika, hata pale kila kitu ndani yako unapohisi kama tayari kimekufa. Ni hasira ya kusimama tena wakati dunia inakukandamiza" aliendelea kuongea huku akisimama wima

"Ni kilio ndani ya kifua chako wakati hakuna anayesikiliza. ni nguvu inayochipuka kutoka kwa maumivu, hasara, kushindwa, yote hayo na kusema, ‘Sikubali kushindwa.’
Ni kukataa kuruhusu wewe mwenyewe kuharibiwa, ni kushikilia wakati miguu yako inatetemeka, wakati moyo wako unavunjika, wakati kila kitu kinacheka dhidi yako

Ni kuchagua kusonga mbele hata pale kila sehemu yako inaomba usimame. Mnadhani nguvu ni kushinda mapambano kirahisi? Kama ndivyo mnavyodhani basi mnakosea
Nguvu ni kupigwa, kuvunjwa, kuaibishwa na bado ukachagua kuinuka

Hasira ya kutokata tamaa ni sauti ndani yenu inayosema "najua maumivu, najua hofu, najua kukata tamaa lakini sitaruhusu kupiga magoti na kujikatia tamaa"

Ninawaka sio kwa sababu naichukia dunia, bali kwa sababu nakataa kuiruhusu dunia kunivunja. Na nyinyi... ndio nyinyi mnaofikiria kukata tamaa mna moto huo huo ndani yenu mnahitaji tu kuuruhusu upumue tena

Huitaji kuwa mkamilifu Unachohitaji ni kuwa na hasira kuu ya kutosha ili usiruhusu kukata tamaa" aliendea kwa sauti ya kawaidi lakini yenye kusambaza nguvu ya ajabu sana na taratibu Caren alijiinua kibishi na kusimama ni kama vile kuna nguvu ghafla imemuingia na uchovu kumpotea vivyo hivyo kwa wenzake

Watatu wale walishangaa kitendo hiko ni kama vile maneno ya Jimmy yamewapa nguvu tena na ghafla kwa pamoja waliweza kusimama wima na imara licha ya uzito wa hewa lakini hawakupata tabu kubwa kwenye kupumua ni kama vile uzito wa hewa ulipungua

"Inawezekanaje hii..? Aliongea aliyebeba boksi

"Sasa ni muda, shift phase one!" aliongea Freya na kutamka neno la kuiamsha damu yake na ghafla mabuja buja yalionekana kwenye ngozi yake kana kwamba damu iliyoko ndani yake ilikuwa ikichemka na kufumba na kufumbua aligeuka kuwa mbeha wa rangi ya chungwa

Shift!" Joshua naye alimtaka na kufumba na kufumbua naye pia alibadilika na kuwa simba dume mwenye manyoya meusi

" Blazing fist! blazing feet! "Joshua naye hakuwa mbali kwenye mabadiliko kwani baada ya kutamka tu hayo maneno moto wa njano uliwaka kwenye ngumi za mikono yake miwili na miguuni pia mpaka viatu kuungua na kubaki miguu peku iwakayo moto

Caren aliokota upanga wake uliokuwa chini ya mchanga na kukaa tayari kwa mpambano unaofuata na Jimmy naye alisimama imara bila kuweka staili yoyote ya kupigana zaidi ya kuwakazia macho, macho yao hayakuwa na utani hata kidogo.

"Kuweni makini" aliongea Jimmy akiwatahadharisha na kuchomoka ama mshale akisindikiza na shambulizi la teke la sarakasi moja matata sana akimlenga shingo bwana aliyeshika boksi

Ilikuwa ni spidi ndogo kutokana nguvu zake kichawi kutofanya kazi wakati huo bila ya kujua chanzo ni nini hivyo ilikuwa Rahisi kwa bwana yule kulikwepa na Jimmy alitegemea hilo kwani sekunde anayokwepa tu alimshtukiza na teke jingine la kifua lililo mrudisha nyuma

Jimmy hakutaka kumpa nafasi ya kupumua na kurusha mashambulizi yake ya kichawi kwani alirusha mashambulizi mengi ya haraka haraka kwa staili mbali mbali na utaalamu wa hali ya juu

Bwana yule alijikuta akiweka umakini wake kwenye kukwepa mashambulizi huku kwa wakati mmoja akijaribu kuhakikisha boksi alilolibeba haliguswi kwa namna yoyote ile.

Upande wa Freya na Caren walimshambulia adui as liyekuwa mikono tupu wakiwa na lengo sawa na Jimmy, kuhakikisha hawamruhusu kupata nafasi ya kushambulia vivyo hivyo kwa Ben na Joshua walikuwa wakipambana na Bwana aliyebeba chungu

Yalikuwa ni mapambano ya ana kwa ana bila kutumia uchawi wowote zaidi ya mbinu za mapigano na baada ya dakika kumi wote walisitisha pambano kuvuta hewa kidogo huku Frwya na Joshua wakirudi katika maumbo yao ya kibinadamu wakifuata kanuni ya uchawi wa damu inayobadilika ya kutotumia maumbo mengine zaidi ya dakika kumi

"Ben ondokeni!" Jimmy aliwaamuru na kuwafanya wote wamuangalie kwa macho ya kiulizo

"Haiwezekani tukuache peke yako ukihangaika kupambana na hawa mashetani, tumekuja wote tunaondoka wote" aliongea, Caren na wote walikubaliana nae

"Tukiendelea hivi mwisho tunachoka na kupoteza nguvu na kuwapa fursa ya kutumaliza, hivyo ondokeni" aliongea akiwa siriaz

"Nimesema ondokeni" alifoka baada ya kuona hawataki kumtii

"Never thought someone like you would want your fellas to choose a coward side" aliongea aliyeshikilia boksi akimaanisha "Sikudhani mtu kama wewe ungewataka wenzako wachague upande wa unyonge"

"Sometimes it's better being a coward you know? .. Better to live and fight another day than die chasing pride." aliongea Jimmy kwa utulivu akimaanisha "Wakati mwingine ni bora kuwa mwoga unajua? … Ni heri kuishi na kupigana siku nyingine kuliko kufa ukifukuza kiburi."

"Hivyo ndivyo unavyoita Tahadhari? Mbinu? Au ni woga tu" alicheka kwa dharau bwana yule

"Pengine huo woga utawafanya waendelee kuishi" aliongea Jimmy na kuwakazia macho senzako

"Ninachojaribu ni kuwaokoa kutoka kwenye kifo mbona hamuelewi? Msiwaze kuhusu mimi nishajua namna ya kudili nao na kutoka salama hivyo naomba msiniangushe kwa hili.."aliongea na kuwafanya wenzake waangaliane wao kwa wao kama vile wanashauriana wamsikilize ama wampuuze na mwisho wa siku walikubali kumsikiliza

Jimmy kwa kasi ya juu ya uwezo wake aliwashambulia mabwana wote watatu akiwapa nafasi ya kuondoka na kuhakikisha wanatoka na waliweza kutoka tu Jimmy alipoteza umakini na kupigwa teke moja takatifu lililomrusha umbali mrefu na kuanguka chini huku akitema damu nyingi mdomoni

Asingekubali kuonekana mnyonge kwani alijinyanyua kibishi na kusimama tena japo kwa tabu na ile anasimama tu alipokea shambulizi jingine lililomrusha na kuanguka chini lakini kiburi cha kusimama kilikuwa juu sana kwani alijivuta tena na kusimama huku akiyumbayumba kutokana na kukosa balansi na nguvu kumpungua

"Wewe ni mpumbavu sana, wenzako walikuwa tayari kupigana kufa kupona pamoja nawe lakini unawafukuza ona sasa unavyotia huruma" aliongea bwana aliyebeba Chungu na kumpiga ngumi nzito ya tumbo hali iliyomfanya Jimmy kujikunja mgongo huku akilegea na kuangukia chini kwa magoti huku damu zikimtoka mdomoni kama udenda

"Haha.. Hahaha.. Koh.. Kkk" Jimmy alianza kucheka kwa sauti hafifu huku akikohoa na kutema damu pasipo kueleweka nini kimemchekesha ni kama vile amekuwa chizi ghafla

Kitendo hiko kilimfanya bwana aliyebeba boksi kupandwa na hasira aliona ni dharau sana kuchekwa na mtu dhaifu ambaye muda wowote anakwenda kufa na palepale alifungua kitambaa na kuonekana boksi la kioo na kufumba macho yeye pamoja na wenzake, Jimmy baada ya kuona kilichopi ndani ya boksi alipiga makelele ya maumivu

"Aaarfhhh... Aaarghhh!" ulikuwa ni ukelele hafifu lakini wenye kuashiria maumivu. Jimmy aliposhuhudia na kupiga makelele hayo ya maumivu alifunika boksi lile

TO BE CONTINUED.....

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 38: I fight not to win, I fight not to lose

Katika hadithi za kale Baba yaga alisemekana kuwa mchawi wa kutisha, mzee mwanamke mwenye macho ya kutisha ambaye anaishi ndani ya msitu mnene

Nyumba yake aishiyo ilikuwa ni ya ajabu na inasemekana ilikuwa na miguu ya kuku na ina uwezo wa kutembea na kujificha popote msituni
anatajwa kuwa na macho ya laana yenye uwezo wa kupofusha unapomuangalia

Sasa katika boksi lile la kioo kilipatikana kichwa chake na haikueleweka bwana huyo alikipata wapi kichwa cha mchawi afahamikaye kwa jina la Baba yaga lakini jambo la uhakika kichwa hicho kilikuwa kinatoa msisimko wa ajabu ambao haukuelezeka na kitendo cha Jimmy kukutanisha macho yake na macho ya kichwa hicho chenye laana ya upofu ghafla alipiga kelele na kupatwa na upofu hapo hapo na hakutegemea hilo lakini ndio hivyo lishatokea

"Hahaha! unastahili kabisa kuwa kipofu mwanaharamu wewe!" aliongea bwana yule mwenye boksi na hakuishia kuongea tu, alimpiga teke lenye nguvu lililomrusha Jimmy na kubiringita mchangani kama tairi la gari umbali wa mita saba na kutulia tuli uso wake ukiwa umelalia mchanga

Alikuwa akipumua kwa tabu sana, alikuwa amelala chini kama mtu asiyekuwa na tumaini, alijigeuza na kulala chali akiangalia angani huku uso wake ukichafukwa na damu na michanga ya jangwa hilo

Hakuona akiona chochote, mbele yakealiona giza neno na taratibu alifumba macho, hata kama angeacha macho wazi isingekuwa na maana, kwa kipofu kufumba au kufumbua macho giza litabaki palepale

Alikuwa akivuta kumbukumbu mpaka alipokuwa mdogo akiongea na marehemu Baba yake

"kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa ata kama unapitia changamoto pambana mpaka mwisho usikate tamaa sawa? " aliyakumbuka hayo maneno kwa ufasaha na kuanza kuwakumbuka ndugu zake, mama yake, rafiki zake na Biancalina pia na alijiambia vipi akifa nani atawalinda?

Alisema hapana hatakiwi kuruhusu hilo litokee

"Inasikitisha unakwenda kufa katika umri mdogo sana kijana" aliongea bwana aliyebeba chungu

"Wema ni akiba sana J kwakuwa ulituacha tukaishi kipindi kile nasi tunaeeza kusamehe uhai wako iwapo utatupa hazina unayobeba" aliongea yule bwana asiyebeba chochote

"Natumai utafanya maamuzi ya busara na kutupatia hiyo hazina" aliongea aliyebeba boksi

"Nilijua tu lazima mtaleta upumbavu wenu, nimekuja mikono tupu hazina naitolea wapi? Hata kama ningekuwa na hiyo hazina nisingekubali itue mikononi mwa mashetani kama nyinyi" aliongea Jimmy akiwa bado amelala ardhini

"Hiyo hazina ina thamani gani kiasi cha kujitoa na kuwa tayari kufa? Ina maana uhai wako hauna thamani?"

"Swali zurii...." alijibu Jimmy huku akijikakamua kuinuka na kusimama japo si wima ila alisimama kwa kulegea sana

"Kwangu mimi uhai una thamani sana kuliko kitu chochote katika dunia hii, si uhai wangu tu bali na raia wema wasio na hatia nyinyi was*ng* kazi yenu ni kuwateka binadamu na kuzifunga nafsi zao kisha kuingiza nafsi za mashetani kwenye miili yao ambapo matokea yake wanakwenda kuua binadamu wengine wasio na hatia, kuwapa ninyi hiyo hazina ni sawa na kuchoma kisu kidonda kibichi na kusababisha madhara makubwa" aliendelea

"Oh ni shujaa ulioje! Lakini kwa bahati mbaya shujaa unakwenda kufa"

"Kufa? Unakosea kusema hivyo, kwenye maisha yangu nina sheria nyingi nilizojiwekea na moja katika hizo ni" I fight not to win, I fight not to lose"* aliongea Jimmy na kufanya watu wale kutoelewa anamaanisha nini

"Najua hamjaelewa na haishangazi maana watu waliobahatika kusikia hii kauli walikuwa na nyuso kama zenu tu hiyo ni kwasababu hawataki kuelewa nachomaanisha bali wanaelewa maneno...."

".... The reason why I survive in battles is because I try my best not to lose my life, not to chase victory. You see, when you fight to win, you become less careful you get blinded by desire, by ambition, by the thirst to be on top. And when that happens, your guard lowers... your weakness gets exposed." aliongea akimaanisha" Sababu ya mimi kuendelea kuishi kwenye mapambano ni kwa sababu hujitahidi kadri ya uwezo wangu nisipoteze maisha yangu, na siyo kwa ajili ya kutafuta ushindi. Ona, unapopigana ili kushinda, unakuwa mzembe unatawaliwa na tamaa, na kiu ya kuwa juu. Na hali hiyo ikitokea, umakini unapungua… na udhaifu wako unaonekana wazi."

"You understimated me just cause I was powerless and now you think you could kill me just because you made me blind, you're wrong!" aliongea uso wake ukiangalia chini huku akinyanyua mkono kizembe na kufuta damu mdomoni akimaanisha "mmenichukulia poa kwa sababu sina nguvu, na sasa mnafikiri mnaweza kuniua kwa sababu umenifanya kipofu, mnakosea!"

"Asee J katika sifa zako moja ya sifa kuu ni unabwabwaja sana yaani unahubiri kinoma na kuwageuza mashetani kuwa malaika ila usidhani maneno yako yatatuyumbisha" aliongea bwana asiyebeba kitu

"Ndio unavyodhani?" aliongea Jimmy huku taratibu akitoa tabasamu la ajabu usoni, alikuwa ni kama shetani katika sura ya malaika

"Pumbavu! Kufa mwanaharamu wewe!" alimaka na palepale kufumbua na kufumbua aliibukia mbele ya Jimmy kama jini akitanguliza mkono kwenye shingo yake akidhamiria kumvunja na kuyakatisha maisha yake papohapo

Jimmy mwanzo mwisho amesimama vilevile kama sanamu lakini sasa ile mkono unakaribia kukamata shingo yake bwana yule asiyebeba kitu alishtukia tu anakamata hewa, Jimmy hakuwa mbele yake na alishangaa tu yuko pembeni upande wa kushoto wa mkono wake

Ilikuwa ni spidi kubwa ya kukwepa, ilikuwa ni kana kwamba anaona licha ya upofu alioupata

"Inawezekanaje hii?" alijiuliza bwana yule akiwa haamini macho yake, spidi aliyotumia Jimmy kusogea ilikuwa ni kubwa mara tano na ya kwake kibaya zaidi hakuwa anatoa msisimko wowote kuashiriia kama nguvu zake za kichawi zimerudi bali ni Jimmy kama Jimmy bila nguvunguvu zozote za ziada na hakika iliwashangaza na hata Jimmy uwezo huo ulimshangaza pia na kujiambia aliuchukulia poa sana

"Suprised?" Jimmy alimuuliza na bwana yule alishtukia ngumi ya uso iliyomrusha kama mpira na kwenda kumuangukia bwana mwenzake aliyebeba chungu na wote kuanguka kiasi cha chungu kupasuka kwani msukumo ulikuwa ni mkubwa sana

Chungu kupasuka ni kama amefungulia gereza la nafsi kwani maelfu ya nafsi zilianza kuzagaa angani huku na huko zikipiga makelele ya ajabu

Jalokuwa Jimmy hakuweza kuwaona lakini aliweza kuwahisi na kuwasikia wakipiga kelele za ajabu

"What the ***?" Bwana aliyebeba boksi alimaka kwa mshangao

"Ni nguvu ya aina gani hii?" aliuliza na swali hilo lilimuacha Jimmy na tabasamu

Ukweli kitabu alichorithi kwa mtawala wa uchawi mzee Salazar Soledad si tu kilikuwa na mbinu za kujifunza uchawi, kilikuwa pia na mbinu nyingine nyingi tu za kuweza kujifunza na kuwa na nguvu za ajabu na nyingi katizo hizo ni Instinict(mzio wa asili) na power of intuition(hisia za ndani)

Jimmy kabla ya kuanza kujifunza kuvuna nguo za kichawi alikuwa akijifunza mbinu mbalimbali kutoka kitabu na ndio hizo mbili na aliweza kuzimaster kikamilifu, nguvu hizo hazikuhitaji maswali ya kupanda levo bali ni kuziamsha mwilini kwakuwa ni nguvu za asili ambazo kila binadamu kuzaliwa nazo. Licha ya kufanikiwa kuziamsha hakumalizia hatua ya mwisho ya kuzipa utawala mwilini zaidi ya kuziweka kiporo

Hiyo ni kutokana na tamaa kubwa ya kutaka kujifunza uchawi lakini kwa wakati huo uchawi wake ulikuwa haufanyi kazi bila ya kueleweka sababu ni nini, na wakati kama huo aliona zina umuhimu mkubwa

Japo ni mbinu mbili ila ni uwili katika umoja yaani hufanya kazi pamoja, ni sawa na kusema sisi binadamu ili tuitwe binadamu ni ni lazima tuwe na mwili wa nyama, nafsi na roho. Licha ya hivyo vitatu ila tunakua binadamu mmoja aliye hai na pasipo kimoja wapo kati ya hivyo tunakuwa hatujakamilika, maana pasipo roho mwili unakuwa mfu sawa na maiti na pasipo nafsi hatuna utambuzi wa kiakili na kihisia na pasipo mwili wa nyama tunakuwa si binadamu kamili

Vivyo hivyo zichukulie hizo mbinu mbili yaani pasipo zote mbili nguvu inakuwa haina maana

Sasa wakati huo Jimmy aliweza kukamilisha hatua ya mwisho ya kuzipa hizo nguvu utawala kwenye mwili wake na automatically kuwa on muda wote

Chukulia kuzipa utawala ni sawa na kuzipa uhai na zinakuwa nguvu ambazo muda wote zinafanya kazi pasipo kukoma kama vile moyo wa mtu udundavyo bila kuacha mpaka pale atakapokufa

Kitabu kinaeleza kwamba Instinict ni nguvu ya ajabu ambayo mwili hufanya kitu au kujibu pasipo hiari yako ni kama programmu ya asili a.mbayo binadamu huzaliwa nayo.

Ni ule msukumo wa ndani wa kiasili ambao unakuongoza kulinda maisha yako au kushughulikia hatari bila kutumia akili ya kawaida yaani ukiwa kwenye hatari huna haja ya kufikiria bali mwili hujibu papo hapo automatically

Nikupe mfano rahisi, ushawahi kuona mtu ambaye hawezi kuruka ukuta hata ajaribu vipi anashindwa lakini baada ya kumuona simba ghafla tu anajikuta ameweza kuruka ukuta mpaka mwenye anajishangaa na baadae akijaribu tena anashindwa, unajua ni kwanini?

Hiyo ni kwasababu ile hatari na hofu imeweza kuishtua instinict ambayo imemuwezesha kufanikisha hilo jambo. ni mfumo wa "fight or flight" (pigana au kimbia) ambao uko ndani ya mwili tangu kuzaliwa Hio ndiyo nguvu ya instinict au kwa kiswahili tunasema "mzio wa asili"

Sasa kuipa kukamilisha hatua ya kuipa utawala ni kuipa uhai na mwili kuwa kama na ufahamu wake binafsi na macho yake ya kuona

Na pia tukija na nguvu ya hisia za ndani(power of intuition) ni ile nguvu ya hisia ya kuweza kuhisi nguvu hasi na chanyi na kuhisi vituvyote vilivyopo ndani ya dunia hii, ni kama kila kitu kinatambulika kwa hisia yake binafsi

Ni kama mwanga usioonekana unaowashwa ndani ya ubongo wako, ukikupa taarifa kabla macho, masikio au akili ya kawaida haijachakata. Wataalamu wa saikolojia huuita subconscious pattern recognition lakini kitabu cha Salazar kinaenda mbali zaidi: kinaeleza kwamba kila kitu kilicho hai au kisicho hai kinatoa “muungurumo” fulani wa nishati. Intuition ni kipokezi chako cha kuzisoma sauti hizo zisizo sikika. Mara tu nguvu hii inapopewa utawala, mwili wako unaongeza “kiungo cha sita” (sixth sense) kinachoendelea kufanya kazi 24/7 kana kwamba umepachikwa rada ndogo kifuani

Kama ulivyosema, hizi nguvu mbili ni kama “nafsi na roho” ndani ya binadamu mmoja. Instinict hukusukuma kutenda (fight or flight) bila kupoteza muda; Intuition hukupa taarifa ili ujue ni nini hasa kinakuja. Bila Intuition, Instinict inaweza kukukimbiza ovyo; bila Instinict, Intuition inaweza kukujaza hofu bila mwitikio. Pamoja, zinaunda mtandao kamili wa kujilinda na kufanya maamuzi katika sekunde sifuri.

Kwa lugha nyepesi ni kama vile Jimmy alikuwa akiisikiliza dunia, alikuwa akipata hisia ya kila kitu kilichopo ndani ya ulimwengu huo

"Mnakumbuka mara ya mwisho niliwaambia nini? Jimmy aliwauliza na alijua hawatojibu hivyo aliwasaidia kujibu

"Niliwaambia ninyi ni kunguni tu haijalishi mna nguvu kiasi gani lakini kunguni siku zote ni kunguni tu na stabaki kuwa kunguni" aliongea na kuwafanya kukunja nyiso zao kana kwamba wamenusu harufu ya yai lililooza

Walilipukwa na hasira kiasi kwamba hawakuwa hata na neno la kusema zaidi ya nyuso zao kuonyesha ni kwa namna gani wamechukia na kukasirika

"Bwana mdogo naona unavuka mipaka sasa hata kama una nguvu hivyo hupaswi kuvuka mstari wa maneno"

"Mipaka?" aliongea huku akianza kucheka kana kwamba amesikia kituko na kisha kutulia na kusimama kikakamavu huku sura yake ikibadilika nakuwa ya kuogopesha kwa jinsi alivyo kauzu

"Ngoja niwaambie kuhusu sheria yangu na nataka msikilize kwa makini sababu nataka pambano la haki, nataka mpambane mkiwa mnajitambua ili muone ukweli ya kwamba ninyi ni kunguni" aliongea na kunyamanza kidogo kisha akaanza kueleza

"Adui mkubwa tunayekabiliana naye si yule aliye mbele yetu, bali ni uwanja wa vita ulioko ndani ya mioyo yetu wenyewe. Hisia zetu wenyewe hutusaliti: tamaa, hasira, furaha kupita kiasi, hofu, kiburi, majivuno, huzuni, hata matumaini... Ndiyo, wakati mwingine.

Kila mojawapo ya hisia hizi zinaweza kutuangamiza ikiwa tutaziruhusu zitutawale.

Unapokasirika kupita kiasi, unashambulia bila kufikiri. Unapojivuna sana, unamdharau adui yako. Unapofurahi kupita kiasi, unasahau kujilinda. Unapohofia sana, unagandia mahali, na kifo kinakupata., Hata matumaini... hata matumaini, yakishikiliwa kwa nguvu kupita kiasi, yanaweza kukufanya kuwa mzembe.

Unaona... kuishi ni suala la usawa.

Ni kuhusu kupumua wakati mapafu yako yanapolia kwa hewa, kusimama imara wakati miguu yako inatetemeka, na kufikiri kwa uwazi wakati moyo wako unataka kuzama katika machafuko.

Kupigana ili usipoteze maana yake ni kupigana kwa akili, kwa unyenyekevu, kwa ufahamu daima ukijua kuwa kosa moja tu linaweza kugharimu kila kitu.

Sipigani kwa ajili ya utukufu. Sipigani kuthibitisha chochote. Napigana kwa sababu maisha yangu ni muhimu, kwa sababu wale wanaoningojea ni muhimu.

Napigana kwa tahadhari. Napigana kwa subira. Napigana kwa heshima ya maisha yangu na hata ya adui yangu."

Wakati Jimmy anaongea anga lote lilikuwa kimya kana kwamba lilikuwa likimsikiliza pia na sauti yake kusikika hata kwa umbali wa kilomita tatu

Alikuwa ni kama mfalme anayeng'aa ambaye anaingia vitani kuokoa raia wa himaya yake, kutokana na mwanga hafifa wa rangi ya dhahabu iliyofifia kummulika alionekana aking'aa kama ana utukufu fulani hivi hasa ukizingatia ni mweupe wa ngozi, ule weupe wa njano wa kibongobongo

Alipomaliza tu kuongea ghafla hali ya hewa ilianza kubadilika na wale watu watatu walianza mtafaruku wa kihisia na msisimko wa nguvu za ajabu na Taratibu walimshuhudia Jimmy akipitia mabadiliko

TO BE CONTINUED..........

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 39: Breakthrough(Kiini cha mabadiliko)

Upande mwingine ndani ya ofisi kubwa yenye mwanga hafifu alionekana mwanaume mweusi aliyevalia gwanda nyeusi na mwanaume huyo hakuwa mwingine bali kamanda Rama, mkuu wa Unit 9-H au Hidden Supremacy

Alikuwa amesimama huku mkono mmoja ukiwa sikioni kuashiria kwamba alikuwa katika maongezi kwenye simu

"Mkuu hali ni mbaya zaidi kuliko tulivyofikiria. Tunahitaji msaada wa haraka sasa hivi" ilisikika sauti upande wapili

""Nipe ripoti Freya kuna nini kinaendelea?" aliongea Kamanda huyo

"Tumeweza kudili na kundi la wanywa damu lakini tumekutana na adui wengine wenye nguvu, tumefanikiwa kutoka kwenye hatari ya kifo lakini Jimmy yuko kwenye hatari ya kupoteza uhai tukiendelea kuzubaa" Freya alijibu

"Sawa nitakuja mimi na wengine, niambie kuhusu raia, wangapi wamesalimika?"

"Kuhusu raia mara baada ya sisi kufika hatukuweza kuwaona lakini baadae tukaaja kugundua kwamba miili ya wanywa damu tuliyoikuwa ni ya wanakijiji"

"Nini! Ebu eleza ukaeleweka"

"Kamanda hatuna muda wa kupoteza, si kitu ambacho naweza kueleza kwenye simu kikaeleweka ni muhimu ukatuma kikosi mengine yafuate"

"Sasahivi nafika na kikosi" aliongea kamanda huyo kisha kukata simu

°°°°°°°°°°

Upande mwingine ndani ndani wenye nyumba nyingi za kifahari na mazingira safi, taa za rangi nyeupe zikimulika kila kona ya mtaa huo na kufanya kuonekana kama vile mchana

Katika moja nyumba nzuri ndani yake alionekana mwanamke ameketi sebuleni na bila shaka alionekana kukaa hapo muda mrefu akisubiri, pembeni ya sofa alilokuwa ameketi kulikuwa na simu janja na kila muda alikuwa akiiangalia

Mwanamke huyo hakuwa mwingine bali ni Biancalina, mpaka muda huo wa saa tatu kasoro alikuwa bado hajaondoka nyumbani kwake kuhudhuria mualiko wa sherehe ya msanii mkongwe nchini katika siku ya miaka thelathini ya ndoa yake na vilevile siku ya kuzaliwa ya mwanawe

Alikuwa akimsubiri Jimmy mpaka muda huo, mwanzoni alijiaminisha lazima atarudi kabla ya saa tatu, na pia kupokea simu kutoka kwa Cid kwamba Jimmy atarudi ndani ya muda lakini alionekana alikuwa akijifariji bure tu na pia kutumainia ahadi hewa

Muda ulikuwa ni saa mbili na dakika hamsini na kitu kupitia saa ya ukutani. Mwanamke huyo alionekana kuwa mnyonge sana kiasi cha kutia huruma.

Mwanamama Mary alikuwa amesimama mahali akimtazama mkwe wake mtarajiwa alivyokuwa akitia huruma na hakuwa na mpango wa kumuingilia na badala yake alimtazama huku moyoni akimtupia lawama za kila aina mwanae na alikusa akijiuliza huyo mtoto yuko wapi muda huo? Na anafanya nini? Hajui kama anasubiriwa na mke wake mtarajiwa?

Simu ya Bianca ilianza kuunguruma mlio wa alarm kuashiria ni saa tatu kamili na baada ya kuona alinyanyuka zake sofani na kupandisha juu na alikuwa ameghairi kabisa kuhudhuria sherehe hiyo. Alienda moja kwa moja mpaka chumbani kwake na kujifungia

°°°°°°°°°°

Kwanini wasipatwe na hofu kwa mfano? Kwa mabadiliko hayo ya kushtukiza na kutotegemea lazima hofu iliwavaa.

Upepo mkali ulikuwa ukivuma kutoka pande zote kuu nne za dunia na kana kwamba upepo huo mkali ulikuwa ukishangilia kwa shangwe baada ya kuhisi uwepo wa mfalme wao na kwenda kumlaki

Msisimko wa nguvu zake za kichawi uliongezeka mara ttatu zaidi ya mwanzo, nafsi zilizokuwa zikitangatanga angani zilikuwa zikipiga kelele za ajabu kana kwamba msisimko huo ulikuwa ukiwaathiri kwa kiasi fulani

Upande wa wale mabwana watatu walihisi ni kama nafsi zao zilikuwa zikivutwa na nguvu ya ajabu kama sumaku na walishindwa kuelewa ni nguvu ya aina gani hiyo lakini jambo la hakika walifahamu kwamba Jimmy amepiga hatua yani ni sawa na kusema amepanda levo

Mara taratibu Jimmy alianza kuelea hewani kana kwamba anavutwa na kamba kwenda juu mpaki kufikia urefu wa mita kumi kutoka hewani mpaka ardhini

Aliweza kuhisi hisia mchanganyiko za ajabu zikisambaa mwili mzima, kulikuwa na hisia za ubaridi, joto, shoti kusambaa mwilini na hisia nyingine nyingi, vuguvugu hilo la hisia lilimfanya ajishangae na kuishangaa nguvu hiyo. Alihisi pia ufahamu wake ukipanuka na kuongezeka kupita kawaida ni kama alikuwa akipokea funuo/ufunuo mbalimbali akilini mwake

Alikuwa akielea juu kama unyoya ueleavyo kwenye hewa, akiwa katikati ya nguvu isiyoelezeka alikuwa akisikilizia hisia alizokuwa akizipata na taratibu ukungu ulianza kujitokeza ukianzia chini ya miguu na kupanda juu taratibu na hatimae kumfunika mwili wake mzima

Mwili wake uliofunikwa, na ukungu ule haukuwa wa kawaida. Ulikuwa ni kama mvuke wa moto na baridi kwa wakati mmoja

Nywele zake ni kama vile zilikuwa zikichemka kana kwamba zilikuwa zinaishi; zikitetemeka kana kwamba zilikuwa zikipigwa na shoti

Haukuwa ule ukungu wa bluu tena bali mwekundu, ieleweke ukungu umtokao Jimmy ni ile nguvu ya kiroho aliyonayo ambayo msingi wake ni kutokana na nguvu za kichawi alizonazo. Kwa jinsi ukungu ule uliokithiri kumzingira alikuwa ni kama kivuli ndani ya moto wa ajabu, kila pumzi aliyovuta ilionekana kuongeza kasi ya mtiririko wa nguvu ile

Ilikuwa ni nguvu ya kipekee na scenerio ya ajabu iliyowaacha kwenye mshangao mabwana wale na hawakuwa na la kufanya zaidi kuendelea kustaajabu, sio kama walikuwa na hofu kubwa kiasi cha kutofanya chochote, walichohofia ni nini kitawakuta iwapo watakurupuka kushambulia

Naam mwamba alikuwa katika levo ya tatu ya uchawi, hatua ya kiini cha mabadiliko!(Breakthrough)

Licha ya hivyo Jimmy alishindwa kuelewa imekuwaje akapanda levo? au ni kwasababu ya mateso aliyokuwa akipitia? na kwanini ghafla tu nguvu zake za kichawi zinatenda kazi ilihali mwanzoni ziligoma?
Maswali yote hayo hkuweza kupata jibu hivyo kupotezea na kutua chini taratibu na ukungu kumpotea

Baada ya kutua tu alielekeza uso wake waliposimama mabwana wale usoni akiwa na tabasamu lenye nia ovu kisha kunyanyua mkono wake akiwanyooshea na kuwapa ishara ya wao kuanza kuchukua hatua

Maneno hayakuwa na maana wakati kama huo, haukuwa wakati wa ngojera bali vitendo kwani mabwana wale mara baada ya kupokea ishara walitazamana wao kwao kwa sekunde kadhaa
Kufumba na kufumbua hawa hapa mbele ya Jimmy kila mmoja akitanguliza shambulizi lenye nguvu

Spidi yao iliongezeka tofauti na mwanzo lakini licha ya hivyo kwa Jimmy ilionekana ni spidi ya kitoto sana mbele ya nguvu ya instinict aliyokuwa nayo, walishambulia mfululizo wa mashambulizi mengi tofauti lakini hakuna hata moja lililomgusa bwana mdogo Jimmy

Alikuwa akikwepa kitaalamu sana yaani kulia, kushoto, mbele, nyuma, juu, chini kwa utulivu wa hali ya juu kana kwamba alikuwa ni master aliyebobea kwenye kukwepa mashambulizi ya aina yoyote, licha ya upofu lakini kwa jinsi alivyokuwa akikwepa usingeamini kama ni kipofu

Ni kama vile alikuwa akifanya mazungumzo na hisia zake, alikuwa akijua kila ngumi, kila teke, kila shambulizi linatokea wapi na linakusudiwa kutua wapi na akwepe vipi, ukisikia mtaalamu basi alikuwa ni mtaalamu haswa!

Ni sauti za misuguano ya hewa pekee ilisikika na zilipita takribani dakika ishirini za kukuru kakara kati ya Jimmmy na mabwana wale.

"Pumbavu! Tukiendelea hivi tutaishia pabaya ni muda sasa wa kumuonyesha nguvu yetu halisi" alifoka mmojawao baada ya kuona wanavyosota kushambulia bila kufanikiwa kugusa hata unywele, na hakika jambo hilo lilimkasirisha sana yaani licha ya kumsababishia upofu hawakuweza kumgusa, na ilikuwa ni zaidi ya fedheha kiasi kwamba alipandwa na jazba na kutamani amkamate na kumkatakata viungo vyote vya mwili lakini sasa kumkamata ilikuwa ni ndoto ya mchana!

Baada ya mwenzao kutoa kauli hiyo walikubaliana nae bila ubishi waliona kuliko kujichosha na kupoteza muda ambapo mwisho wa siku wataishia kufa ni bora wkutumia nguvu zao zote kumaliza pambano kisha kuendelea na kile kilichowaleta ndani ya ulimwengu huo wa ajabu, kuendelea kujidhalilisha kwa mtu kipofu ni ushenzi uliopitiliza

Kwa pamoja walianza kutamka maneno ya ajabu kama vile wanasali na kadri muda unavyosonga hali ilianza kubadilika, Jimmy alipata hisia kwamba kuna kitu kibaya kinakwenda kutokea na hisia zake zilikuwa sahihi

Miili yao ilianza kutuna kana kwamba inataka kupasuka, urefu wao uliongezeka na makucha makali kujitokeza, nyuso zao zilibadilika na kuwa za kutisha, harufu nayo ilibadilika na kuwa mbaya zaidi kiasi kwamba Jimmy alijihisi kichefuchefu

Pamoja na kubadilika wote walikuwa vimo sawa, baada ya hatua hiyo walinyanyua mikono yao kuelekea angani kama vile wanaabudu na kuanza kutamka kwa pamoja

"Nafsi elfu, nguvu elfu eeh nafsi kwa damu na wimbo ingieni ndani yetu!"

Waliongea kwa kurudiarudia kana kwamba wanaimba na maelfu ya nafsi zilizokuwa zikitangatanga angani zilikuwa zikipiga kelele na ghafla zilijikusanya makundi matatu si kwa hiari bali kuna nguvu ya ajabu ilikuwa ikiwaendesha na kisha kama vile sumaku yenye nguvu kubwa walivutwa na kuingia ndani ya wale mabwana kupitia midomo yao mikubwa na kadri zilivyowaingia ndivyo walivyozidi kurefuka na kutuna

Ndani ya dakika mbili tu mabwana wale hawakuwa binadamu tena bali ni majitu makubwa yenye urefu wa futi nane na upana wa mita 2.3, walikuwa kama ma, hulk fulani hivi wenye sura kama fisi na pembe kama ng'ombe

Walikuwa wakitisha kwelikweli na nguvu zao ziliongezeka lakini hazikumuogopesha Jimmy, kwake neno woga halikuwepo kwenye dictionary yake. Zaidi tu aliweka uso wake siriaz

Bila hata kupoteza muda jitu la kwanza lenye sura kama fisi lilirusha ngumi yenye uzito wa kutosha akidhamiria kumkandamiza Jimmy kama chapati

"BOOM!" sauti ya ngumo kugongana ardhi ilisikika kiasi kwamba ni kama ardhi ilikuwa ikitetemeka na kusababisha shimo na vumbi kubwa

Jimmy aliweza kukwepa shambulizo hilo huku moyoni akitamka neno "Asee!"
Pengine ngumi ile ingempata angegeuka chapati kweli, aliweza kuhisi kabisa nguvu iliyotumika kurusha shambulizi ilikuwa ni kubwa sana

"Damu inayobadilika awamu ya pili, ngozi ya chuma!" alinena Jimmy akitumia mbinu ya damu inayobadilika

Baada ya kutamka taratibu cell za damu yake zilianza kuchemka na misshipa ya damu kuanza kutuna huku ngozi yake ikianza kubadilika kuanzia shingoni mpaka miguuni na kuwa ngumu kama chuma

Ni kama vile ngozi yake imebadilika na kuwa kama gamba la mgongo wa mamba, Kama jinsi ngozi ya mamba ilivyo ngumu na yake ilikuwa vivyo hivyo lakini ugumu ulikuwa mara tatu yake, hakuongezeka mwili wala kutuna ni ngozi yake pekee ndiyo iliyobadilika

Ngozi yake ilibadilika na kuwa kama mwangaza wa mwezi umulikao baharini na kung'aa. Yalikuwa mabadiliko ya kasi yaliyochukua nusu dakika pekee kukamilika

Ieleweke kwamba katika levo za uchawi wa mabadiliko mbinu zinazotumika ni zilezile tu hata ukipanda levo, kinachoongezeka ni makali na kina cha nguvu, mfano mtu aliyekatika levo ya kwanza na aliye katika levo ya pili wanatumia mbinu moja lakini aliye katika levo ya pili mbinu yake inakuwa na nguvu kubwa kuliko wa yule aliye katika levo ya kwanza

Hii ni kwa sababu kila unapopanda levo, damu na nafsi yako inakua ikitengeneza uhusiano wa ndani na chanzo cha uchawi. Hali hii inafanya mwili wako kuhimili mzigo mkubwa zaidi wa mabadiliko, bila kuvunjika au kuungua kwa ndani

Fikiria kama varnish(ni rangi ya kung’arisha mbao au kipako cha kung’arisha) inayowekwa kwenye mbao. Awali, mbao haina kinga kubwa inaweza kulowa na kuoza. Lakini unapoongeza varnish moja juu ya nyingine, mbao hiyo inakuwa ngumu, inang’aa na inastahimili mvua, jua na miale ya moto. Vivyo hivyo, kila levo mpya unayopanda kwenye uchawi wa mabadiliko ni kama kuweka varnish nyingine juu ya nafsi yako: unakuwa mgumu zaidi, wenye uthabiti na una uwezo wa kuhimili shinikizo kubwa la uchawi.

Kwa mfano, katika levo ya kwanza mtu anaweza kutumia mbinu za damu inayobadilika lakini anatumia kwa dakika chache mpaka kukosa udhibiti lakini kwa aliyekatika levo ya pili anatumia mbinu hiyohiyo kwa muda mrefu kuliko wa yule aliye katika levo ya kwanza

Ndiyo maana wachawi wengi wanaogopa wale walio katika levo za juu kwa sababu mbinu yao hiyo hiyo ya awali inakuwa ni kama dhoruba inayoangusha majumba

Mara baada ya mijitu ile kushuhudia mabadiliko hayo ilianza kunguruma na kupandwa na morali na wote kwa pamoja walianza kushambulia kama vichaa, pamoja na uzito wao lakini walikuwa wepesi kwenye kurusha mashambulizi

"BOOM! BAM! BAM! BOOM! BAM!"

Hatimae pambano lilichukua hatua nyingine, binadamu mmoja dhidi ya majitu matatu ni sauti za mipanguano ya ngumi kati ya majitu watatu na binadamu mmoja

Ulikuwa ni mpambano wa kibabe kwelikweli, kila ngumi, kila teke yaani kila shambulizi lilikuwa limebeba ujumbe maalumu, ni kama walikuwa wakizungumza kupitia mashambulizi, walikuwa wakidhihirisha ule msemo wa "Fighting is conversation" kwamba kupambana ni kuzungumza

Je wanazungumzaje? Kila shambulizi lilikuwa kama hoja yenye uzito wake. Kila teke lilikuwa kama nukta ya maelezo, na kila ngumi ilikuwa kama alama ya mshangao. Jimmy hakupigana tu kwa mikono na miguu, bali kwa moyo na roho, akitoa ujumbe kwa kila pigo alilolitoa

TO BE CONTINUED..........

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 40: The dance of survival

Majitu matatu pia hayakubaki nyuma, kila mmoja alionekana kutoa hoja zake kwa nguvu za ajabu. Vilio vyao vilikuwa kama sauti za giza, na kila pigo lililoachwa angani lilionekana kama dokezo la kifo.

Yote kwa yote Jimmy bado alibaki imara akisoma kila harakati zao, akijibu hoja kwa hoja, akigeuza kila shambulizi kuwa jibu. Halikuwa tu pambano la ana kwa ana ulikuwa pia kama mjadala wa maisha na kifo, na kila mmoja alikuwa na kitu cha kusema.

Kupitia kila ngumi na teke, Jimmy alionyesha kwamba nguvu pekee haishindi, bali akili na ujasiri vina nafasi yake. Majitu yalikuwa na nguvu, lakini Jimmy alikuwa na sababu na sababu hiyo ilimfanya awe imara kama mwamba.

Lilikuwa ni pambano la ujasiri dhidi ya nguvu, akili dhidi ya ukatili, mwanadamu dhidi ya majitu. Hakika walikuwa wanazichapa kwelikweli si lelemama, kasi yao haikuwa ya kawaida. Ukisikia pambano la haki ndiyo hilo sasa

Zilipita takribani dakika ishirini na tano kwenye uwanja vita bila mapumziko na hakuna aliyeonekana kuchoka na kama kawaida waliendelea kuzichapa, Jimmy alishangaa licha ya dakika zaidi ya ishirini kupita mbinu hiyo ya damu inayobadilika haikumletea madhara yoyote ni kama vile haina kikomo cha kutumia na jambo hilo lilimfurahisha

Upande wa lango la pembe tatu la kuingilia ulimwengu huo walionekana watu wakiingia ndani humo na aliye mbele kabisa alikuwa ni kamanda Rama, nyuma akifuatiwa na Freya, Caren, Ben Joshua na wengine waliokuwa katika kitengo cha unit-9 H, na Mia pia alionekana kuwepo kwenye kundi hilo, haikueleweka imekuwaje akawa pamoja nao lakini ilionekana amesaidia kuwaponya majeraha wakina Freya

Walikuwa wameingia jumla yao wakiwa kumi na wote mikono yao miwili walikuwa wamebeba masanduku makubwa meusi isipokuwa Mia pekee, Bila shaka yalikuwa ni yale masanduku ya kuhifadhia siraha za moto za kijeshi

Ile wanaingia tu kitu cha kwanza ni kuduwaa kwa mshangao mkubwa, hawakuamini macho yao kwa kile walichokuwa wakishuhudia mbele yao

"Damn! Oh dear mother Theresa!" aliongea Ben huku akimeza mate yake kwa shida sana

Wakina Freya pia hawakutegemea kukutana hali hiyo, Mkuu wao kamanda Rama naye kwa maelezo aliyopewa na anachoshuhudia ni sawa na mbingu na ardhi, aliambiwa watu lakini anakutana na majitu

Jimmy aliweza kuhisi ongezeko la watu ndani ya ulimwengu huo umbali wa mita sabini na alipo lakini alipotezea na kuweka umakini kwenye pambano na alionekana akilifurahia kwelikweli alijiambia ngoja kwanza apate uzoefu

Spidi na nguvu tu inayotumika kwenye pambano walijiambia hilo si levo zao kabisa ni bora kubaki shabiki kuliko kuingilia na kuishia kugeuzwa mlenda kwa shambulizi moja

"Nani ambaye hajipendi?" Ben alouliza na kufanya wote wamuangalie kwa macho ya ajabu, si kwamba hawakumuelewa anamaanisha nini bali walimuona anataka kuwageuza mbuzi wa kafara

"Kwanini usiende wewe Bwana Bernard kidoto?" Freya alimjibu akitaja majini yake mawili na bila shaka wote walikuwa wakisubiri kuona atasema nini, Ben ni kama vile hakusikia na kujifanya akiangalia pambano kwa umakini wa hali ya juu akitafuta upenyo wa kuingilia kutoa msaada

Kamanda Rama licha ya kuwa kiongozi wao lakini alikuwa levo sawa na wengine wote walikuwa katika levo ya pili ya damu inayobadilika, alichowazidi ni cheo tu lakini likija suala la nguvu ni walewale tu

"Anaonekana kama vile haoni bali anatumia hisia" aliongea Mia na kuwafanya wote wamuangalie ni kama vile hawakumuamini

"Unataka kusema ni kipofu? Mia acha utani basi, mimi na wewe wote tunajua Jimmy si kipofu" aliongea Ben

"Huwezi jua nini kilitokea baada ya kumuacha hapa!" Kamanda, Rama alidakia

"Japokuwa miondoko yake anaonekana kama anaona lakini ukweli ni kwamba haoni" Mia aliongea huku akitazama pambano kwa makini

"Wewe ni nani?" alouliza kamanda Rama alijiambia kama msichana huyo aliweza kugundua hilo bila wao kugundua ilitia mashaka

"Naitwa Mia" alijibu msichana huyo huku akitabasamu

"Hilo tayari ushaniambia nachotaka kujua ni asili yako na ni mtu wa aina gani?"

Mia alitabasamu kidogo, macho yake yakielekea kwenye pambano, kama vile hakutaka kutoa jibu kisha kusema "Some things are better unsaid" kwamba Baadhi ya mambo mengine ni bora kutosemwa na jibu hilo lilimfanya Kamanda huyo kukunja sura kwa kutoridhika

“Msichana, usinizungushe. Nimekuuliza swali wazi. Unatoka wapi na wewe ni nani haswa?”

"Wakati mwingine, majibu yapo kwenye vitendo, siyo maneno.” Mia liongea maneno yenye busara kama mzee licha ya kuonekana bado kijana

“Kama kweli unataka kujua mimi ni nani, labda ni muhimu kwanza uelewe kwa nini niko hapa. Hata bila kujua jina langu au historia yangu, unaweza kuelewa dhamira yangu kupitia kile ninachofanya.” Mia aliendelea kuongea

"Unazungumza kama mtu mwenye siri kubwa" aliongea kamanda huyo na Mia kutikisa kichwa taratibu na kufungua kinywa chake akinena

"Kila mtu ana siri zake, Kamanda. Lakini wakati mwingine, cha muhimu zaidi siyo siri yenyewe, bali ni jukumu unalochukua mbele ya wengine....."

"Tuangalieni namna ya kumsaidia mwenzetu kumalizana na hawa mashetani" Caren aliingilia kabla hata Mia hajamaliza sentensi yake, alifanya hivyo kwasababu aliona msichana huyo hakuwa akitaka kuelezea kuhusu yeye na kamanda anaonekana kufosi

"Heshimu siri za watu kamanda" aliongea Ben huku akimshika bega kamanda Rama na kuishia kupigwa jicho na kujikuta akitoa mkono bila kupenda

Walianza kuweka masanduku makubwa waliyokuja nayo chini ardhini moja baada ya jingine kisha kufungua na zilionekana siraha za moto aina tofauti

Kulikuwa na mabomu ya pini(granade) hamsini kwenye sanduku la kwanza na pili na kukamilisha idadi ya mabomu mia, magazine kubwa na ndogo si chini ya arobaini zilizojaa risasi kwenye sanduku la tatu na nne na kukamilisha idadi ya magazini zaidi ya Themanini, bastola ndogl kumi kwenye sanduku la tano na sita, Jegeja kumi kwenye sanduku la saba na nane, sanduku sita kila moja limebeba bazoka mbili na jumla ya bazoka kwenye sanduku zote sita zilikuwa kumi na mbili na sanduku nne zilizobaki zilikuwa zimebeba rocket za mabomu zitumiwazo na bazoka jumla zikiwa ishirini(tano kwenye kila sanduku)

"Asee nilidhani mtakuja kichwa kichwa tu kuja kujidhalilisha kwa kuchezea kichapo cha mbwa koko ila naona mmekuja na back up za kutosha sio mbaya, nfiyo maana unaitwa Kamanda" aliongea Ben huku akijivhekesha mwenyewe na kamanda Rama alimpuuzia alijiambia katika wagmtu anaowaongoza ni Ben pekee aliyekosa adabu

Ukweli kamanda huyo baada ya kupokea maelezo mafupi tu alijua lazima kutakuwa na jambo kubwa linakwenda kutokea hivyo kuandaa back-up plan mapema

Wanajeshi hao walianza maandalizi ya kuandaa siraha za kuingia nazo vitani, Mia aliishia kumeza mate mengi huku karoho kakitaka kumtoka kwa hofu ya kile kinachokwenda kutokea muda si mrefu

Upande wa pambano majitu yale yalifanikiwa kumzingira na kwa pamoja waliruka juu angani wakidhamiria kummaliza kwa kumkanyaga kwa kishindo

"BOOM!" mshindo kama kimondo kugongana na ardhi ulisikika na kusababisha wimbi kubwa la presha na vumbi, katika alipokuwa amesimama Jimmy kulikuwa na shimo kubwa lililosababishwa na majitu yale lakini Jimmy hakuonekana na hakukuwa na ishara yoyote kwamba shambulizi lile limempata

Alikuwa amepotea kimazingira, wakati wanajiuliza na kugeuka huku na huko kujua alipo Jimmy mara mmoja wa majitu yale alishtukia teke moja moja takatifu sana la mgongo lililomrusha kama furushi umbali mrefu sana huku akidunda dunda ardhini kama mpira

Mwingine ile anageuka upande ambao ambao shambulizi hilo linatoka naye alishtua ngumi nzito ya taya iliyomrusha hewani na kabla hajatua ardhini Jimmy aliweka miguu sawa kutafuta balansi kisha misuli ya miguu kutuna na kufyatuka kwenda kwenda hewa akisindikiza na shambulizi la "flying knee" ambapo goti lake humu kama vhuma lilimpiga tena kwenye taya kiasi kwamba ilisikika sauti ya migupa kuvunjika na baada ya shambulizi hilo alitua chini kwa ustadi wa hali ya juu kwa kuruka sarakasi

"BAM!" ilikuwa ni sauti ya jitu lile kutua ardhini vibaya sana, mashambulizi yote hayo yalifanyika ndani ya sekunde tatu pekee na kuwaacha kwenye bumbuwazi wenzake ambao walikuwa wakishuhudia

Jitu la mwisho mara baada ya kuona wenzake wamejeruhiwa vibaya sana alikasirika na kunguruma kilio cha maumivu na kwa hasira kama zote kufumba na kufumba alikuwa nyuma ya Jimmy, lakini unadhani Jimmy angeruhusu hilo?

"Exsomnia Gravitus!" hatimae alitumia uchawi wa maneno

Ile anadhamiria kumvunja Jimmy shingo anajishtukia ameganda hewani na kuwa katika slow motion! Kisha Jimmy alimgeukia akitanguliza na tabasamu la kishetani na alimtandika ngumi nyingi mfululizo

Ngumi zake zilikuwa na kasi kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuhesabu na kujua idadi ya ngumi alizompiga, jitu lile mimacho ilitaka kumtoka kwa mauteso aliyokuwa akipata na hawakuwa na uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kusikilizia maumivu

Ni kama vile alikuwa amefungwa na kamba zisizoonekana. Jimmy baada ya kumshushia ngumi mfululizo aliruka hewani huku akijizungusha kama feni na kumsindilia teke la kifua ambalo lilimtoa kwenye kifungo cha hewa na kumrusha kama furushi na kwenda kumuangukia mwenzake aliyekuwa anasimama "BAM!"

Jimmy alikuwa na uwezo wa kukwepa shambulizi lile ni vile tu aliona anapoteza muda baada ya kukumbuka anahitajika nyumbani

Tokea mwanzo alikuwa na uwezo wa kuwamaliza ndani ya dakika moja tu kwa uchawi wake wa maneno lakini hakufanya hivyo ni kwasababu alikuwa akipata uzoefu wa pambano la ana kwa ana na majitu hayo

Kingine majitu yale uchawi wao mkubwa ulikuwa ni kwenye kubadili nafsi na kusababisha uzito wa hewa, hawakuwa na jipya jingine hivyo aliona ni kama atakuwa anafanya uonevu ndiyo maana alichagua pambano la ana kwa ana angalau kuchangamsha mwili kidogo, isitoshe haikuwa mara ya kwanza kupambana nao, mara ya mwisho aliwashinda je awamu hiyo ambapo amepanda levo atashindwaje kwa mfano? Hata kama asingepanda levo bado angewashinda tu ni vile tu nguvu ziligoma kutenda kazi pasipo kujua sababu

Lakini kulikuwa na tofauti kwenye pambano hilo na mara ya mwisho anapambana na hao walozi, kipindi kile alikuwa akipambana yeye kama yeye akitumia mbinu hiyo hiyo ya ngozi ya chuma na hawakuwa na chungu cha nafsi wala boksi lenye kichwa cha Baba yaga

Kipindi hiko sasa kulikuwa na ugumu kidogo, ukiangalia amepatwa na upofu wa ghafla ambapo chanzo chake ni laana iliyokuwa kwenye kutazama macho ya mchawi wa kale aitwaye Baba yaga, kingine nguvu zake ziligoma kwa muda na pia mabwana hao kunyonya maelfu ya nafsi za mashetani na binadamu kwa ujumla na kubadilika kuwa viumbe vya kutisha.

Yule jitu aliyeharibiwa taya alisimama tena japo kwa shida na kukusanya pumzi nyingi na kupumua kama nyati aliye tayari kumtimua yeyote akatizaye mbele yake na taya kurudi sawa

Lakini sasa la haula! Rocket lililokatika kasi lilikwenda kumbamiza jitu hilo kwa nguvu na kusababisha mlipuko na kumtupilia mbali

"BOOM!!"

Na kwa mbali alionekana kamanda Rama amebeba bazoka begani akilenga upande huo na bila shaka ni yeye aliyefanya shambulizi hilo la kushtukiza

Jimmy aliyesimama umbali kidogo aliweza kulishtukia hilo mapema na ndiyo maana hakuwa na mpango wa kufanya chochote zaidi ya kutulia tuli

Jitu lile baada ya kushambuliwa na rovket alipatwa na majeraha madogo tu ilionekana alikuwa na ngozi ngumu pia lakini haikumaanisha hakupata maumivu!

"We strike!" aliongea kamanda Rama kwa amri akimaanisha sasa wanashambulia na baada ya kauli hiyo wote walijipanga kisawasawa wakiwa wamepakia siraha na magazine huku mikononi wakishikilia majegeja wengine bazoka isipokuwa Mia aliyekuwa amekwenda kukaa mbali nao kujilinda

"as usually we go the dance of survival!" aliongea Freya akimaanisha "kama kawaida tunakwenda mtindo wa ngoma ya kusalia hai"

Mara baada ya kumaliza kauli hiyo walianza kukimbia kwa pamoja wakijipanga kwa safu maalumu huku kila baada ya sekunde tatu wakibadilisha safu zao kwa ustadi sana ni kama vile walikuwa wakicheza mchezo wa kubadilisha nafasi zao

"Namba nne shambulia!" aliongea Kamanda Rama na wote kwa pamoja walisimama huku wakipiga goti la mguu mmoja na namba 4 ambaye alikuwa ni Joshua alikimbia na kuukanya goti la mmoja wapo na kuruka angani huku akielekeza shabaha yake kwa moja ya yale majitu mawili yaliyoanguka pamoja

Wakati akiwa hewani alifyatua rocketi na kutua ardhini kwa kujiviringisha sarakasi murua na kutua vizuri

"FwOOOOOSH.... BOOM!" roketi ilifyatuka na kwenda kumlenga kisawasawa lile jitu na kurushwa hukooo

"Namba sita" Ile Joshua anatua tu Rama alitamka tena na namba sita naye aliyepiga goti na kulenga shabaha yake alifyatua roketi

"FWOOOOSH...... BOOM!" shabaha ililenga palepale ilipokusudiwa na kwenda kumshambulia jitu la mwisho na kwenda mumbamiza na kumlipukia

"Safu ya mshale!" aliongea kamanda Rama na ghafla walibadili safu na kusimama kama ungekuwa angank ungeona wamesimama kama vile wamechora umbo la mshale

"Songa mbele!" na kama kawaida walianza kusonga mbele wakikimbia kuelekea kwa wale majitu. Na kama ilivyotegemewa hawakuweza kufa kirahisi kwani walisimama tena

"Namba, moja, tano na tisa" baada ya hiyo kauli wote walipiga magoti chini isipokuwa namba moja ambaye ni kamanda Rama aliyesimama kushoto kabisa, namba tano ambaye ni Ben aliyesimama kulia kabisa na namba tisa mwanamke aliyesimama mwisho kabisa na wote kwa pamoja walifyatua rocketi wakiwalenga majitu yale mawili

"FWOOOOSH...... BOOOOM... BOOOM. BOOOOM!!!"

TO BE CONTINUED........

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 41: Mtu anayepita tu

Makombora yote matatu kila moja lilikwenda kuwalipukia wale majitu watatu na kuishia kutoa ngurumo za maumivu iliyochanganyika na hasira lakini wangefanyaje? Wanajeshi wale hawakuwaachia hata nafasi ya kupumua walishambuliwa mfululizo na rocketi za mabomu, mabomu ya pini na kufyatuliwa bastola kana kwamba wapo vitani

"Tu tu tu tu tu tu!... Boom!.... Tu, tu, tu, tu... Boom! Boom!" zilikuwa ni sauti za risasi kufyatuliwa na mabomu kulipuka mfululizo

Miondoko yao ilikuwa ni ya kipekee sana, kama ni wataalamu basi walistahili kuitwa wataalamu haswa! Pngine kupewa hata tuzo za utaalamu wa matumizi ya siraha kijeshi. Kwa jinsi miondoko yao ilivyo na jinsi walivyokuwa wakishambulia kwa mpangilio maalumu hawakukosea kuiita mbinu hiyo "dance of survival"

Walikuwa wakishambulia na wakati huohuo kujilinda iwapo kutatokea la kutokea. Laiti Jimmy asingepatwa na upofu angevutiwa na jinsi walivyokuwa wakishambulia na mpaka wanakuja kumaliza risasi na mabomu ni vumbi pekee ndio lilikuwa likitamalaki eneo walilokuwepo kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuona kwa macho kilicho mbele zaidi ya vumbi tu

Ni kana kwamba kulitokea dhoruba kubwa ya vumbi isababishwayo na upepo mkali na vumbi kufunika eneo lote walilokuwepo.
Kadri muda ulivyosonga vumbi lilianza kupotea na hatimae waliweza kuona vizuri, yale majitu yalikuwa chini hoi bin taaban. Ilionekana kabisa mapigo waliyopokea yalikuwa ni zaidi ya maumivu. Japokuwa hayakuweza kuwaua lakini yaliwajeruhi pakubwa sana na taratibu walianza kupungua vimo na kubadilika kutoka majitu kurudi kuwa binadamu wa kawaida huku wakitema damu nyingi mdomoni

Jimmy naye alionekana kurudi katika hali yake ya kawaida huku macho yake akiwa ameyafumba na sasa waliweza kugundua kwamba ilikuwa ni kweli jamaa hakuwa anaona, kwa maana hiyo Mia alikuwa sahihi

"Mnaonekana kukurupuka sana lakini sio mbaya kikubwa mmeweza kuwadhibiti hawa kunguni" aliongea Jimmy huku akitabasamu, ni kama vile kupatwa kwake kwa upofu lilikuwa jambo la kawaida

"Bro ni kweli huoni?" aliuliza Ben lakini Jimmy hakujibu zaidi ya kutoa tabasamu

"Acha kuuliza maswali ambayo majibu unayo" Freya alimwambia Ben

"Kwanza tumalizane na hawa kunguni mengine ndio yafuate" aliongea Jimmy na kuwasogelea wale watu kisha kuchuchumaa, yaani hata tembea yake haikuwa imebadilika ni kama vile hakuwa kipofu

"Hivi kweli haoni huyu?" aliuliza mzube mara baada ya kuona Jimmy ameweza kujua mahali walipo mabwana wale lakini hakuna aliyejibu zaidi ya kukaa kimya.

"Mna bahati sana nilitaka niwatoe utumbo lakini bahati mbaya wasamaria wema wameingilia hivyo chukulieni kama ukombozi kutoka mikononi mwa shetani" Jimmy aliongea na hakuwa anajali watamwamini au lah

"We.. wee mshe..n...zi usijion..e wa maana sana kisa tu umeweza kutud..hibit..i.. ni kwasababu u.." alikuwa akiongea kwa tabu sana, ilikuwa ni sauti ya yule bwana aliyebeba chungu hapo mwanzo lakini kabla hata hajamaliza kuongea aliishia kutoa mimacho na kupana mdomo lakini sauti haikuwa inamtoka

Jimmy alikuwa amemtoboa tumbo kwa mkono wake na kuuchomoa utumbo wake na kumuonyesha kabisa. Kilikuwa ni kitendo cha kikatili na kishetani kwelikweli.

"Sijakupa ruhusa ya kuongea wewe kunguni, siku zote kunguni ni kunguni tu, ni wadogo hawana cheo wala hadhi zaidi ya kuitwa kunguni tu. Nyinyi kunguni daima mnanyonya damu za wengine ili kuishi hamna thamani yoyote" aliongea na kuutupa ule utumbo pembeni

Bwana yule hakupata hata nafasi ya kumsikiliza mpaka mwisho kwani alikata roho palepale, damu nyingi zilikuwa zikimtoka kama bomba la maji, zilikuwa damu nyeusi zenye harufu mbaya kishenzi lakini Jimmy hakuonekana kujali sana harufu hiyo

Kamanda Rama na wengine pamoja na wale mabwana wawili waliobaki walihisi ubaridi ukisambaa kwenye uti wao wa mgongo na hogu kuwatawala bila kupenda. Hawakuelewa kwanini lakini walijikuta tu wakitawaliwa na hofu kiasi kwamba nywele ziliwasisimka na hakuna aliyedhubutu kufungua mdomo. Hakuwa yule Jimmy wa masaa kadhaa yaliyopita alikuwa mtu mwingine kabisa

"Mna kingine cha kuongea?" Jimmy aligeuza uso wake kwa wale wawili waliobaki na kuwauliza lakini hakuna hata aliyedhubutu kufungua kinywa chake, zaidi ya kutetemeka huku vijasho kuwatoka

"Hamna? sasa nisikie kunguni yeyote anaongea pumba na nataka mnijibu maswali yangu kwa ufasaha mmenisikia?" aliwauliza

Licha ya kwamba Jimmy alitoa kauli hiyo kwa mabwana wale lakini wenzake walihisi ni kama vile na wao kauli hiyo iliwahusu hasa ile sentensi ya" sasa nisikie kunguni yeyote anaongea pumba"

"Tutakwambia kila kitu lakini kwa mabadilishano ya kutuacha hai" aliongea mmoja kwa kutetemeka alikuwa ni yule ambaye hakubeba kitu hapo mwanzo

"Hahaha..hahahaha!!"Jimmy baada ya kusikia kauli hiyo alianza kucheka kwa sauti hafifu huku taratibu ikipanda na kuwa kubwa, alionekana ni kama kichaa fulani hivi

Sekunde ambayo anamaliza kuangua kicheko aliikamata shingo ya bwana yule kwa mkono uleule aliotumia kumchomoa utumbo mwenzao na kuibana koo kwa nguvu
Kutokana na maumivu makali yaliyosababishwa na mashambulizi ya siraha ya kijeshi hakuwa hata na nguvu ya kunyanyua mkono hivyo alibaki kuteseka ndani kwa ndani akikosa pumzi bila kufanya chochote zaidi ya macho kuwa mekundu na machozi kumtoka

"Nimekupa ruhusa ya kuongea? Nani kakwambia kwamba mimi ni mfanya biashara? Sikia we kunguni mimi sio mfanya biashara na sipo hapa kufanya barter trade, kwangu mimi sijali kama utakuwa hai au lah, uniambie au usiniambie mimi sitopungukiwa na kitu nadhani hujui mimi ni nani. Ngoja nikwambie" aliongea huku akiendelea kuibana shingo ya bwana yule

"I am a man of many indentities but my most honest indentity is 'a man passing by' I ain't a hero nor a devil, I am the wind that cuts through the night, the shadow that comes and goes I don't care whether you die or live because your fate is yours alone. I carry no burden of mercy, no chains of pity
You are nothing but a stepping stone on my path a speck of dust, just like every other man who crossed my way. Whether you beg or scream or curse me, I don’t care. I just pass by, I move on, and life goes on.” aliongea kwa sauti ya kawaida lakini iliyosikika vyema kwenye kila sikio lililoko eneo hilo akimaanisha

"Mimi ni mtu mwenye nyuso nyingi, lakini utambulisho wangu wa kweli ni mtu anayepita tu. Mimi sio shujaa, wala sio shetani, mimi ni upepo unaopita usiku, kivuli kinachokuja na kuondoka. Sijali kama utakufa au kuishi, kwa sababu hatima yako ni yako mwenyewe, sibebi mzigo wa huruma wala sina huruma.
Wewe si kitu zaidi ya jiwe nalokanyaga kwenye njia zangu, chembe za vumbi kama wengineo tu waliokatiza mbele yangu, omba sana, piga kelele, nilaani mimi sijali, mi napita tu, nasahau na maisha yanaendelea"

Itoshe kusema yalikuwa ni maneno yenye kuvuruga hisia za kila mmojawapo aliyeko mahali hapo na mpaka anamaliza kuongea bwana yule alikuwa ameshakata roho tayari na kumuacha shingo

""Nadhani wewe ndiye uliyenisababishia upofu huu si ndio?" aliongea lakini bwana yule aliyesalia hai hakuthubutu kufungua kinywa zaidi ya kutingisha kichwa, nguvu ya kuongea anaipata wapi kwa mfano? Licha ya Jimmy kuwa na sura ya kimalaika lakini vitendo alivyokuwa akifanya ni shetani mtupu

"Safi" jimmy alijibu baada ya bwana yule kutingisha kichwa ni kana kwamba amemuona akitingisha kichwa

"Sasa nataka kusikia ndio na hapana, tofauti na kauli hizo napasua pumbu" aliongea akiwa siriaz kiwango cha kimataifa

"Je miaka zaidi ya tano iliyopita ni nyinyi mliohusika na wanywa damu waliokuwa wakiua raia nchini?"

"Hapana"

"Unanidanganya?"

"Hapana?"

"Unataka kuniambia kwamba hamkuhusika?"

Ndio"

"Na kwamba wahusika ni wengine?"

"Ndio"

"Kwa maana hiyo mpo wengi si ndio?"

"Ndio"

"Je wenzako bado wako nchini?"

"Hapana"

Ulikuwa ni mwendo wa maswali na majibu ya ndio na hapana mpaka Jimmy ananyamanza kwa sekunde kadhaa

"Safi una adabu sana, nimependa! Aya nataka maelezo yaliyonyooka kuhusu wanywa damu"

"Kuhusu wanywa damu ni binadamu ambao tunawateka na kuzitoa nafsi zao kisha kuingiza nafsi za viumbe ambao hutegemea damu kuishi, ndio maana licha ya kuwa na maumbo ya binadamu lakini tabia ni tofauti na uhalisia wa binadamu ni rahisi kusema si binadamu tena bali ni mashetani waliovaa sura za binadamu." bwana yule alieleza kwa ufupi lakini yaliyonyooka

"Kuna namna yoyote ya kurudisha nafsi za binadamu kwenye miili yao?" aliuliza kamanda Rama

"Hapana kwasababu nafsi zao si hai tena" alijibu na Jimmy alishaelewa kwani nafsi zilizotekwa za binadamu zikinyonywa, umejuaje? Ni ile hisia ya ndani 'power of intuition'

'Hata kama zingekuwa hai bado isingewezekana chukulia mfano wa bastola na ili bastola ifanye kazi inahitajika magazini na risasi, chukulia magazini ni roho ya mwanadamu na risasi ni nafsi halafu bastola ni mwili. Risasi ikishafyatuliwa hakuna uwezekano wa kuirudisha tena labda uchukue risasi mpya ambayo haijatumika. Vivyo hivyo kwa nafsi, nafsi ikishatolewa kwenye mwili husika hakuna namna ya kuirudisha unajua kwanini?"aliongea Jimmy na kila mtu alitingisha kichwa kutokujua isipokuwa Mia ambaye alijibu

"Ni kwasababu nafsi si kitu kinachoweza kuhifadhiwa kwenye kopo au mfuko, haiwezi kushikika wala kuonekana kwa macho. Nafsi ni kiini cha maisha, ni mwanga wa uhai. Ikitoka mwilini, haikimbii tu kama ndege inafungamanishwa na kanuni za ulimwengu ambazo haziruhusu kurudi tena "

"Exactly Mia unaonekana kujua mengi ni kama kujaribu kuunganisha kioo kilichovunjika vipande elfu moja. Hata ukiviunganisha, hakitarudi kuwa kile kioo cha mwanzo kitakuwa kimepoteza thamani na kiini chake cha kwanza chukulia mfano wa moto, unapowasha moto na ukazima, moshi wake unapaa na kupeperushwa na upepo si ndio? . Unaweza kuupata tena? Hapana. moto unaweza kuwashwa tena, lakini moshi ule ule huwezi kuurudisha. Vivyo hivyo kwa nafsi, ikitolewa au kunyonywa, imepotea milele, no turning back!" aliendelea kuongea ni kama vile mwalimu anayewafundisha wanafunzi darasani

"Kwahiyo zile nafsi zilizotekwa zimenyonywa? Na ndio sababu ya hawa washenzi kubadilika na kuwa majitu?" aliuliza Caren

"Yeab, nafsi ya binadamu inaponyonywa na waseng* kama hawa hubadilishwa kuwa sehemu yao, wanaitumia kama nguvu yao ya kuishi na kuimarika. Kwa hivyo, nafsi hiyo huangukia chini ya nguvu za giza, kama kinyesi kilichogeuzwa mbolea. Nafsi hiyo haingekuwa tena safi au huru inakuwa imepoteza utu wake na heshima yake. hata kama tukijaribu kuirudisha, tungekuwa tunarudisha kitu ambacho hakina thamani tena. Nafsi hiyo inakuwa na sumu ya uovu, na mwili usingeweza kuipokea. Ingekuwa ni kama kutia sumu kwenye maji safi, kingine mikli yao imeshakufa na roho kuwatoka” Jimmy alimjibu kwa kirefu

"Kitu pekee ni kuziombea tu nafsi zilizopotea, be it buddha, Jesus or Allah whoever you believe in just pray for them folks" jimmy aliongea kisha kusimama

"Kamanda una swali lolote la kutaka kumuuliza huyu kunguni?"

"Nataka kujua hapa wapi?"

"Umesikia wewe kunguni toa maelezo!" Ben aliropoka

"Huu ni ulimwengu wa utupu, ulimwengu ambao ni jangwa tupu, hakuna mwezi, hakuna jua wala nyota kifupi hakuna chochote zaidi ya anga na mchanga" aliongea Bwana yule

"Kumbe ulimwengu wa utupu ndio uko hivi?" alijiwazia Jimmy, ni kama vile amewahi kuusikia au kuusoma mahali

"Agenda yenu ni ipi kuingia ndani ya huu ulimwengu?" Joshua aliuliza

"Ushasikia ni ulimwengu wa utupu sasa kuna agenda gani itakayofanyika sehemu ya utupu? Ukizunguka huku na kule hakuna utakachokutana nacho zaidi ya upepo unaosafiri kama mpumbavu asiye na malengo" Jimmy alijibu kisha kuchuchumaa tena chini uso wake ukitazamana na uso wa bwana yule aliyetawaliwa na hofu isiyo na kifani

"Hey usiniambie mlikuwa hapa kutafuta hazina" aliongea Jimmy

"Hazina? Kuna hazina humu? Ni ipi hiyo?" aliuliza Freya fululizo

"Inasemekana kuna hazina ambayo ina nguvu kubwa sana iliyofichwa kwenye ulimwengu huu hapo kale na mmiliki wake akihofia kuanguka kwenye mikono ya watu wabaya, well who believe this bullshit?" aliongea Jimmy

"Ninaamini" alijibu Mzube

"Kwahiyo kama unaamini ndo tuseme unataka kuitafuta na wewe?" Jimmy aliongea kwa masikitiko

"Hii dunia haitoishiwa na wapumbavu" alimalizia na kauli yake ilimtia hasira Mzube

"We dogo! kwasababu tulikusaidia kipindi kile sasahivi ndio unajikuta mjuaji sana, unadhani kama tusingefika kukusaidia kipindi kile leo hii ungekuwa hapa ukinitukana?" Mzube aliongea kwa hasira

"No hard feelings!" aliongea Jimmy

"Halafu sio kama nimekutukana na pia sijakosea bali ni ukweli kwamba hii dunia kuna wapumbavu wanaibuka kila siku" aliendelea kukazia

"Nikuulize swali labda, unajua hiyo hazina ni hazina gani?" aliuliza na Mzube aliishia kujing'atang:ata mdomo

“Unaona sasa! Hujui ni hazina gani na inapatikana wapi zaidi ya kuamini upuuzi wa mpumbavu mwenzio. Sasa unajiona una utofauti gani naye? Sikulaumu kwa kuamini, isitoshe imani ni suala la kuchagua, lakini kuamini kitu bila kufikiria mara mbili-mbili, huo ni upumbavu wa hali ya juu.
Halafu neno mpumbavu sio tusi bali ni utambulisho wa mtu yoyote ambaye kichwani mwake kumejaa pumba tu, kilichoongezwa ni neno "vu" ambacho ni kivumishi. kinachoashiria hali ya mtu huyo asiye na uelewa wala fikra timamu.
Mpumbavu hakosi kuwa na macho lakini haoni, ana masikio lakini hasikii, hana akili lakini hajui kwamba hana. Anaamini kila kitu kama vile mzizi wa ndizi unavyonyonya maji, bila hata kujua yupo wapi au anatoka wapi.

Wewe ni binadamu mwenye uwezo wa kufikiri, usikubali kuamini kila kitu kama punda anayeamini nyasi ni chakula bila kuhoji ubora wake. Fikiria, tafakari, jadili, halafu uchague. Usikubali upuuzi wa mpumbavu kuwa mwanga wako; kwani mwanga wa mpumbavu ni sawa na giza nene lisilo na mwisho. Ndio maana nikasema, imani ni jambo la kuchagua lakini kufikiri kabla ya kuamini ndilo linatofautisha mpumbavu na mwenye hekima"

Bt Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 42: My lord

Jimmy kwa maneno alikuwa ni mtu mwingine kabisa, alikuwa anajua sana kuchambua maneno na wa wapi pa kupigilia msumari na hiyo ni moja kati ya Sifa alizonazo yaani 'talkative'

Japokuwa aliongea kama mzee mwenye busara na hekima nyingi lakini kwa Mzube ilionekana kama anatukanwa na hilo lilizidi kumkasirisha. Wenzake walijitahidi sana kujizuia wasicheke maana ilikuwa ni wazi maneno yale yalimwingia kisawasawa

Mzube alipandwa na hasira kiasi kwamba mishipo kwenye komwe lake ilijitokeza na kutuna, alikunja ngumi zake na kutaka kumshikisha adabu Jimmy lakini alizuiwa na Kamanda Rama kwa ishara ni kama vile kamanda anamwambia "Fikiria mara mbili mbili acha upumbavu huyo sio levo yako" ndipo alipotulia na kujiona kweli alikuwa ni mpumbavu lakini haikumuondolea hasira ya kudhalilishwa mbele ya wenzake

Jimmy alimpotezea Mzube na kumgeukia yule bwana kisha kumpa mkono asimame, japo alikuwa ana hofu lakini alihofia kitakachokwenda kutokea iwapo atakaidi hivyo alipokea na kusimama pamoja naye

"Wewe kunguni hivi unajua hata maandiko yanasema jino kwa jino, jicho kwa jicho na pia kuna msemo wa karma is a bitch! halafu kuna msemo mwingine usemao 'malopo ni hapahapa duniani' nadhani kupitia misemo hiyo sitakuwa na dhambi" aliongea Jimmy na kabla hata hajaelewa anamaanisha nini alishtukia vidole viwili vikizama machoni mwake

"Aaarghhhh!!" alipiga makelele ya maumivu bila kupenda. Alikuwa amegeuzwa kipofu

Jimmy mara baada ya kumtoboa macho bwana yule alisimama akimwacha akiugulia maumivu na kumsogelea Caren, alimsogelea mpaka karibu kabisa kiasi kwamba pumzi zao ziligongana. Caren moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi asielewe Jimmy anataka kufanya nini lakini alikuja kuelewa mara baada ya Jimmy kuchomoa kisu aina ya dagger kiunoni mwake

Kufumba na kufumbua Jimmy alikuwa amepotea mbele ya uso wake ni kama vile amemezwa na hewa na kutokezea nyuma ya bwana yule na baada ya sekunde tatu kupita tu damu zilianza kuruka kama chemchem ya maji kutoka shingoni mwa bwana yule na kuanza kuhangaika akiziba shingo yake iliyokuwa ikivuja damu na kuanguka chini akiangukia magoti

Spidi aliyotumia Jimmy ilikuwa ni kubwa sana kuliko neno lenyewe, kisu kile hakikuwa hata na tone la damu kuashiria kwamba spidi iliyotumika ilikuwa ni nje ya fikra za mwanadamu. Iliwashangaza mno, ilikuwa ni spidi kubwa kuliko hata ile aliyokuwa akitumia kupambana na ile mijitu hapo kabla. Ilikuwa ni spidi ambayo haikuendana hata na macho yao
Dakika moja si nyingi bwana yule alikata roho palepale.

"Kwanini umemuua kuna maswali nilitaka kumuuliza" aliongea Kamanda Rama huku akikunja sura akionekana kutopenda kabisa

"Kama ni kutaka kumuuliza mahali walipo wenzao wanaohusika na kubadili nafsi ashasema kwamba hawapo nchini"

"Na unaamini kirahisi hivi? Sasa una utofauti gani na....."

"Kamanda usiige mtindo wangu, kama ulikuwa ukitaka kuniita mpumbavu basi unakurupuka, alichoongea ni kweli hawako nchini" Jimmy alimuwahi kabla hajamaliza sentence yao

"Kipi kimekufanya umuamini?"

"Intuition sir, just a true feeling." alijibu moja kwa moja huku akinyoosha mikono yake akipiga miayo

"Intuition?"

"Hutonielewa kamanda usiumize sana kichwa, by the way nina njaa" aliongea huku akipiga hatua kuelekea lango la ulimwengu huo, licha ya kupatwa na upofu tembea yake haikubadilika, ni kama vile hakuwa kipofu

Hakukuwa na mtu mwenye sababu ya kuendelea kubaki ndani ya ulimwengu huo wa ajabu hivyo nao waliondoka na baada ya kufika nje ya lango hilo walimkuta jimmy amesimama tuli akitulia kama anga lituliavyo angani

"Ni saa ngapi?" Jimmy aliuliza

"Saa nane usiku bro, ni mida ya wanga" Ben alijibu baada ya kuangalia muda kwenye saa yake ya mkononi

"Nini!" Jimmy alishangaa, hakuamini dakika arobaini ndani ya ulimwengu ule na ghafla muda huo ni saa nane

"Ni kama ulivyosema bro, miingilio ya dunia nyingine sheria za asili hazifanyi kazi kama tunavyozijua" alijibu Ben kisha kupiga chafya

"Dakika kumi za mule ni sawa na lisaa na nusu, wakati mimi na wenzangu tunaingia na kupambana na adui tulichukua dakika kumi kupambana na adui mpaka kuzidiwa na nilipo fanikiwa kutoka kuomba msaada nilishangaa kuona giza na kucheki muda ilikuwa ni saa moja kasoro" aliendesha Ben

"Mummy natumaini utanisamehe tu" alijiwazia na alipomaliza tu palepale mwili ulimlegea na mzobe mzobe lakini hata hajaanguka Caren alimuwahi haraka, Jimmy alikuwa amepoteza fahamu.

°°°°°°°°°°

Ndani ya chumba binafsi cha mgonjwa alionekana mwanaume akiwa amelala kwenye kitanda maalum cha mgonjwa, pembeni yake kukiwa na msichana aliyeketi kwenye kiti, msichana huyo alionekana kuchoka sana na bila shaka alikuwa amesinzia

Yule mwanaume taratibu alifumbua macjo yake lakini licha ya kuyafumbua mbele yake kulikuwa kuna giza nene, alikuwa kipofu na mwanaume huyo hakuwa mwingine bali ni Jimmy Julian Jairo a.k.a Triple strikes

Alijinyanyua taratibu na kukaa kitako kitandani huku miguu yake akiwa ameikunja(mkao wa tahajudi) uso wake akiuelekeza chini kama mtu asiye na matumaini

"Bwana wangu, umeamka?" ilikuwa ni sauti ambayo Jimmy aliitambua vyema, lakini kilichomshangaza ni sauti hiyo kumuita 'Bwana wangu'

"Mia! Unafanya nini hapa?" Jimmy aliuliza. Ndio msichana yule alikuwa ni Mia, yule Mia aliyekutana naye kwenye misheni ya kuwaangamiza wanywa damu.

"Nipo hapa kukuangalia Bwana wangu"

"Hey Mia unanichanganya ujue, Tangu lini nikawa bwana wako?"

"Tangu uzaliwe umekua bwana wangu, samahani kwa kukushtukiza najua utakuwa na maswali mengi, na mimi niko tayari kukujibu yote lakini kabla ya hayo kuanza tafadhali kula kidogo bwana wangu" aliongea Mia kwa sauti ya unyenyekevu sana

Ni kweli Jimmy alionekana kuchanganyikiwa lakini aliposikia neno kula tu ni kama njaa ilimuingia hapohapo na kujiambia ngoja kwanza ale ndio mengine yafuate

Baada ya Jimmy kukubali kula Mia alitabasamu na kutoka ndani ya chumba hicho na hakuchukua mda sana alirudi na sinia kubwa lenye sahani zilizojazwa aina mbali mbali za vyakula.

Alikwenda kuviweka kwenye meza iliyoko ndani ya chumba hiko kisha kumfata Jimmy na kumsaidia kusimama na kumpeleka kwenye kiti na kuketi naye.

Ilikuwa ni harufu mchanganyiko nzuri sana ya vyakula iliyokuwa ikiisumbua pua ya Jimmy, shida inakuja sasa kujua sahani hii ina chakula gani na hii ina chakula gani, hiyo ni kwasababu hakuwa anaona

"Bwana wangu hapa kuna rosti ya viazi iliyochanganywa na nyama, kuna wali, samaki, maharage kwenye bakuli, uji kwenye kikombe na tambi pia" aliongea Mia huku akimshika Jimmy mkono wake na kumuelekeza

"Niite tu Jimmy, sijisikii vizuri kuitwa Bwana" aliongea kwa kifupi tu, pia Jimmy si kama alikuwa hajui sahani inachakula gani hapana alikuwa anajua, pua yake ilikuwa ni mara mbili ya pua ya mbwa, aliweza kutofautisha harugu ya vyakula licha ya harufu kuchanganyika ni vile tu hakutaka kujisumbua
Kingine bila hata ya kuelekezwa angejua tu alikuwa na 'intuition sharp' sana.

"Sawa Jimmy nitakulisha kwanza" aliongea Mia

Angekataaje kwa mfano? Kwa mwanaume rijali kulishwa na msichana mrembo kama Mia ilikuwa ni kama ndoto kutimia sasa kukataa kulishwa ungekuwa ni ushenzi wa hali ya juu hivyo Jimmy aliishia kutingisha kichwa tu kukubali asiongee neno

Mwanzo mwisho ulikuwa ni mwenda wa kulishwa vyakula mpaka pale vilipoisha kisha kuwekewa uji na kumaliza chupa nzima kabisa na kushiba
Baada ya kama kimya cha dakika kumi hatimae Jimmy alivunja ukimya.

"Mia" aliita kwa sauti tulivu

"Abee!" msichana huyo aliitikia

"Tuko wapi? Najua niko hospitali lakini ni hospitali gani?" alimuuliza

"Ukweli sijui hapa ni wapi lakini nadhani ni kwenye makao makuu ya wale wanajeshi" alijibu

"Ooh kwahiyo tuko dar si ndio? aliuliza tena na Mia alimjibu ndio, alipouliza ni saa ngapi alijibiwa saa tisa mchana, maana yake ni kwamba alikuwa amepoteza fahamu kwa takribani masaa kumi na nne

"sawa nipeleke nje sehemu iliyotulia nataka kupunga upepo" aliongea Jimmy

Dakika chache mbele alionekana Jimmy akiongozwa na Mia sehemu yenye uwazi mkubwa yenye miti na maua mengi, bila shaka ilikuwa ni bustani na hali ya hewa mahali hapo ilikuwa ni safi iliyotulia pamoja na ukimya wa hali ya juu

Wote wawili walikuwa wamevaa nguo zenye rangi moja nayo ni nyeusi, Mia alitafuta sehemu yenye kivuli kikubwa na kwenda kuketi pamoja na Jimmy

"Najua kichwani mwako utakuwa na maswali mengi ya kwanini mimi kukuita wewe Bwana wangu" Mia alianza kuongea

"Ndio nina maswali mengi, lakini la kwanza kabisa ni una umri wa miaka mingapi?"

"Mia mbili arobaini na nne" alijibu na kidogo tu Jimmy apaaliwe na mate, aliona ni kama msichana huyo anajaribu kucheza na akili yake

"Mia mbili arobaini na nne my foot!" Jimmy alijiambia kichwani mwake

"Mia ebu kuwa serious basi, kweli una miaka mia mbili wewe?"

"How could I dare make a joke in your presence, my lord?"

"You serious? kwa muonekano wako unaonekana ni binti wa miaka kumi na tisa"

"Kuna mengi ambayo hujui Bwana wangu, na nilikuwa nikisubiri muda muafaka wa kukuambia, Japokuwa sijui kama huu ndio muda sahihi wa kukuelezea ila nitakwambia machache" aliongea na kumfanya Jimmy atege masikio yake kwa umakini

"Mimi ni mtumishi wa ukoo wa Magnus, moja ya koo yenye nguvu kubwa kati ya koo kumi na mbili za wachawi, ambayo ilitawaliwa na marehemu mtukufu babu yako kabla ya anguko. Jina langu ni Damiana Daria Magnus." alianza kujitambulisha

"Unasema?" Jimmy ni kama vile hakusikia, ukweli alisikia vizuri lakini ilikuwa ngumu sana kumeza

"Unadhani kukutana kwangu mimi na wewe ni kwa bahati? Hapana nimekuwa nikikuangalia tangu ulipozaliwa" aliendelea kumchanganya

"Hry subiri, sidhani kama nina babu, mzee wangu hakuwahi kuniambia kama nina babu halafu baba yangu hakuwa mchawi kingine Jina langu la mwisho ni Jairo na si Magnus, unachojaribu kuniambia ni sawa na hadithi za kusadikika" aliongea Jimmy

"Jairo ni Jina ambalo umepewa na baba yako baada ya kujitenga na ukoo wake halisi kuficha ubini wako, baba yako aliitwa Julian Magnus" aliongea na kumfanya Jimmy atafakari kwa kina

"Umesema umekuwa ukinijua tangu utoto wangu si ndio?"

"Ndio bwana wangu"

"Na umesema pia wewe ni mtumishi, maana yake ulimtumikia marehemu baba yangu"

"Baba yako alikuwa ni mtu mzuri sana ni kwa bahati mbaya hatunae tena"

"Nataka kujua sababu iliyomfanya baba yangu kututoka, siamini kama ilikuwa ni ajali tu, isitoshe hawakusema ni ajali gani zaidi ya kusema ni ajali kazini" alimuuliza Mia lakini hakujibiwa zaidi ya kimya tu

"Nilijua tu" aliongea Jimmy huku akikunja sura

"Samahani Bwana wangu"

"Msamaha wa nini? Kuna lolote umenikosea?" alimuuliza lakini hakujibu zaidi ya kuangalia chinii

"Usiwaze sana halafu mimi sio bwana wako, sipendi kufuga watumwa" aliongea kisha kusimama

"Sawa nitakuamini lakini je lengo lako la kujitokeza sasahivi na kuniambia haya nini ilihali tangu mwanzo ulikuwa ukijificha?"

"Ni..."

"Litunze hilo jibu lako" Jimmy aliongea kabla Mia hajaanza wala kumaliza kauli yake

Jimmy mara baada ya kumwambia hivyo aliondoka eneo hilo isieleweke anakwenda wapi

°°°°°°°°°°

Saa kumi na mbili jioni giza likiwa limeanza kuufunika mji mzima Jimmy alioneka kusimama nje ya geti la jumba kubwa, haikueleweka amefikajefikaje hapo ukizingatia ni kipofu lakini la muhimu ni kwamba amefika nyumbani salama

Alikuwa amevaa miwani nyeusi za jua, shati jeusi, suruali nyeusi na buti nteusi, kifupi alikuwa ni full black.
Alisogelea geti na kubonyeza kitufe kilichokuwa pembeni ukutani kisha kusubiri na haikuchukua hata dakika alifunguliwa mlango na mlinzi

Mdogomdogo aliingia ndani bila ya kuongea chochote ni kama vile yeye ndiye aliyekuwa mmiliki wa nyumba hiyo

Ila anafungua tu mlango wa sebuleni alihisi hatari mbele yake na alichofanya ni kusogea pembeni na kilipita kijiko karibu na uso wake kwa kasi sauti ya Ting! Ting! Ting! Ilisikika kuashiria kimegonga mahali

"Rudi ulikotoka!" ilikuwa ni sauti yenye hasira si kitoto kutoka kwa Bianca na ni yeye ndiye aliyerusha kijiko

Jimmy aliishia kutoa tu tabasamu la uchungu na kushusha nyingi kisha kunyanyua mikono akielekeza mbele na kupapasapasa hewani kama vipofu wafanyavyo, aliona hiyo ndio njia pekee ya yeye kusalimika

"Mummy, mummy? Uko wapi?" aliongea huku akitembea na kupapasa hewani pasipo kujua kitendo hiko kilimkasirisha zaidi mwanamke huyo

Safari hii hakurusha kijiko bali sahani nzima ya glass lakini Jimmy hakukwepa bali alijikaza na kuzuia instinict yake isitende kazi na sahani ilimpiga usoni kiasi kwamba ilipasuka na vichupa kadhaa kumjerujhi usoni

"Aaah..!" Bianca aliziba mdomo baada ya kitendo kile, yeye alitegemea Jimmy kukwepa lakini matokeo yakawa tofauti

Yalikuwa ni majeraha mawili madogo usoni ya vichupa kuchana ngozi ya usoni moja kwenye paji a uso, jingine kwenye shavu la kulia

"Mummy najua nina makosa ya kutorudi nyumbani jana nisamehe" aliongea Jimmy kama vile hakupigwa na sahani lakini upande wa Bianca alionekana kutokwa na maji machoni akionekana kujuta kwa kitendo chake cha kumrushia sahani huku kwa huohuo akiwa bado na hasira ya Jimmy kujifanya kipofu

TO BE CONTINUED

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 43: Saa nane usiku

Bianca alikuwa ni mwanamke mpole na mstaarabu sana lakini ukimkera ni rahisi sana kukasirika, alikuwa ni aina ya wale wanawake wenye hasira za karibu, kadri anavyoonekana kuwa mpole ndivyo anakuwa mwingi wa hasira. Ogopa sana mtu mpole ukadhani labda ni mnyonge, watu wa aina hiyo huwaga ni ndivyo sivyo, unamdhania hivi kumbe ni kinyume chake!

Pia sebuleni humo kulikuwa na ndugu zake wanne pamoja na mwanamama Mary ambaye ni mama yake Jimmy wameketi sofani
Mama yake Jimmy wala hakuonekana kushtuka ni kama vile alikuwa akiwaza kichwani mwake "Safi sana! muongezee sahani nyingine, mtoto anazurura sana huyu" pia upande wa rafiki zake kina Felix walijifanya hawakuona kitu yaani walikuwepo kama vile hawapo! Kifupi walijivunga

Bianca taratibu alimsogelea Jimmy ambaye hata hakujali kama amepigwa ba sahani zaidi aliendelea kupapasa hewa na mikono yake

"Kwanini umeruhusu sahani ikakupata?-aliongea kama vile anamfokea

"Mummy sio kama nimefanya makusudi, ukweli mpenzio sioni nimepatwa na ajali ya macho hata hivyo nimestahili" aliongea akiwa na tabasamu

"Nini! Huoni? Hivi Jimmy kwahiyo unaniona mimi ni mjinga si ndio?"

"Hapana sio hivyo"

"Sio hivyo? Aya kama sio hivyo ni nini sasa? Unakwepa kijiko mbele ya macho yetu hapa halafu unadai huoni, au ndio mbinu yako ya kutaka kunisahaulisha eeh" huyu hakuwa yule Bianca ambaye kazi yake ni kudeka, alikuwa ni mtu mwingine kabisa tena akiongea kwa jazba kiasi kwamba yeyote aliyekuwa ndani angemsikia, hata kama huyo 'yeyote' alikuwa juu ya rooftop angesikia tu

Upande wa Felix aliishia kumeza mate na kumuangalia mwenzake Harry na kumnong'oneza akimwambia "Dude! ndio maana mpaka sasa niko single, wadada wa siku hizi wana kelele sana"

"Kuwa na heshima kaka huyo ni shemeji yako ngoja Jkmmy akusikie" mwenzake alimnong'oneza pia

Upande wa Jimmy hakujua afanye nini maana hata kumueleza kilichotokea ataonekana ni kama alfu lela ulela mwingine tu hivyo alibaki kuwaza namna nzuri ya kutaliza hali

"Jimmy ebu acha utoto na umalizane nae" mama yake aliingilia

"Mama na wewe huniamini?" aliongea Jimmy huku akiivua miwani yake na kumuacha kila mtu kimya kwa dakika kadhaa wakimtazama

Macho yake yalikuwa ni tofauti kabisa, mbona za macho yake ambayo hapo kabla zilikuwa nyeusi tii sasa zilikuwa na rangi ya kijivu na huo ulikuwa ni ushahidi tosha ya kwamba alikuwa ni kipofu

Bianca aliishia kuganda tu kama sanamu akimwangalia tu bila kufanya chochote, mama yake Jimmy harakaharaka alinyanyuka sofani na kumsogelea mwanae huku akiwa na wasiwasi mikono yake ikimtetemeka na kumshika mashavu yake

"Niambie nini kimekupata mwanangu" aliongea kwa wasiwasi sana

"Hakuna kitu mama ni ajali ndogo ilitokea wakati nikiwe nashughulika na jambo?" aliongea na kuvaa miwani yake

"Jambo gani hilo la kukusababishia upofu"

""Nadhani wote mmeshasikia kuhusu watu kupotea usiku na wengine kukutwa wamekufa wakiwa wamekauka damu, jana wakati narudi njiani nikakutana nao kwa bahati mbaya hao wanaohusikana vifo vya vya raia na katika purukusheni za kujiokoa mikononi mwao ndio kunisababishia haya" aliongea akichanganya ukweli na uongo

"Tatizo lako ni kwamba hutulii, hujawahi kutulia, usiku unazurura kufanya nini? Unaona sasa kilichotokea, itakuwaje kuhusu future yako eeh?" aliongea kwa hasira na uchungu huku machozi yakimtoka taratibu, alitamani hata kumpigapiga

Kama mama aliumia sana kwa kilichompata mwanae na hakujua afanye nini zaidi ya kuumia ndani kwa ndani

"Bi mkubwa usiumie sana, tatizo lake sio suala la kuwazia sana ziko njia nyingi za kulitatua kwa ubora kabisa" aliongea Celeb akijaribu kumtuliza

"Kweli bi mkubws kwenye dunia ya sasa ya teknolojia haitokosekana njia sisi kama rafiki pia tuko tayari kusaidia" Dylan aliongezea

°°°°°°°°°°

Upande mwingine muda kama huo kwenye sehemu iliyojitenga alionekana mwanaume akitembea kutumia mkongpjo wa chuma, ilionekana mguu mmoja ulikuwa umevunjika

Alikuwa akitembea kwa tahadhari sana kana kwamba hakutaka kujulikana yeye ni nani, mwanaume huyo alikuwa ni Beka msanii maarufu nchini

Alitembea mpaka kwenye kijumba kidogo na kuingia moja kwa moja bila hata ya kugonga hodi
Ndani ya hiko kijumba kulikuwa kukifuka moshi pamoja na kutoa harufu tofauti tofauti za madawa ya kienyeji, kulikuwa na mashuka rangi nyeusi na nyekundu yakiwa yametandikwa ukutani na katikati aliketi mzee mwenye mvi nyingi, Bila shaka hapo kulikuwa kwa mganga.

"Karibu sana bwana mdogo... karibu sanaa" aliongea mzee huyu kwa sauti yenye mkwaruzo kana kwamba ndiyo ametoka kunywa konyagi kwa mara yake ya kwanza huku kama vile anafukuza nzi kwa kifaa chake cha uganga

Beka bila ubishi aliketi chini japo kwa tabu kidogo kutokana na mguu wake ambao haukupona bado na kila muda alikuwa anakunja ndita kuvumilia maumivu.

"Umekuja sehemu sahihi bwana mdogo.... Hahaha.. Mimi ndio kiboko yao, mkali wao, babalao.. Naam mimi ndio konki hahaha!" aliongea huku akicheka kama zombi na sauti yake yenye mkwaruzo

"Kama nilivyokuelwzea mara ya kwanza nataka uifanyie kazi mzee konki babalao!" Beka aliongea na ilionekana hiyo ilikuwa ni mara yake ya pili kufika mahali hapo

"Naam usiwaze kijana.. Umesema anaitwa Jimmy?"

"Ndio ndio"

"Safi sana hapo hesabu kazi imekwisha kufanyika... Gruuuuh! Graah!" aliongea huku akinguruma

"Nakuaminia sana konki" aliongea Beka

"Kabisa kabisa weka kwanza sadaka kamili hapo kabla ya kazi kuanza, si umekuja na nilivyokuagiza" mzee huyo aliuliza huku akimsogezea uongo ambao bila shaka Beka alitakiwa kuweka malipo

"Ndio ndio mzee, jogoo mweusi na mweupe, njiwa na kifaranga cha mwewe" Beka alijibu huku akitoa maburungutu ya fedha na kuweka kwenye ungo

"Saw.. Hahaha... Sawasawa.. Hahaha Gruaah! Gruuuh!"

Mganga huyo alikuwa ni kama chizi fulani hivi aliyekataa kutibiwa afya yake ya akili hospitali ya mirembe, Beka wala hakujali kikubwa aliamini kazi yake inakwenda kufanywa kwa ufanisi hivyo hayo makelele yalikuwa ni ya kuvumilia

" Sasa bwana mdogo mengine niachie mimi, kazi inaanza saa nane usiku"

°°°°°°°°°°

Muda ulizidi kutembea mpaka kufikia saa nne na dakika kumi usiku, walikuwa wamekwishakula na kila mtu alikwenda zake kulala isipokuwa Jimmy na ndugu zake wanne ambao walikuwa juu ya rooftop wakinywa kahawa muda huo

Haikueleweka Jimmy alilimalizaje suala ya yeye kuwa kipofu lakini kikubwa aliweza kutuliza hali ndani ya nyumba hiyo
Wote watano walikuwa wamekaa chini wakikunja miguu yao kama watoto huku wakinywa kahawa.

"kumbe huku nchini kwenu anga linapendeza hivi" aliongea Dylan huku akitazama nyota zilizoko juu angani

"Yeah anga limetulia sana hakuna na hali ya hewa si mbaya" aliongea Harry

"Hey J" Felix alimuita na Jimmy wala hakuitikia zaidi aliendelea kunywa kahawa yake

"Funguka bro, sio kama amekuwa kiziwi" Celeb alimwambia

"Sawa kaka mimi kama ndugu yako nina wasiwasi na hali yako ujue" Felix alianza kuongea kama vile anaongea na kaka yake mkubwa

"Kuna nini la kuhofia bro, tuliza kichwa acha kuwaza sana" aliongea Jimmy

"Unaona sasa ndio maana unakasirisha sana, ndugu zako tunakujali lakini unachukulia poa sana, unaona kawaida sana, Hio tabia yako ya kubadilisha mada tunapoongelea tatizo lako ndio unatia hasira zaidi" Felix aliongea hisia na hasira

"kwahiyo unataka nini? Nimesema tulia nitajua namna ya kulitatua mbona unapayuka usiku usiku bro"

Kitendo cha Jimmy kuongea kauli hiyo kulimfanya Felix anyanyuke kwa hasira na kutupa kikombe chini, uzuri kikombe kilikuwa ni cha plastiki hivyo hakikuharibika zaidi ya kahawa kumwagika

Upande wa Jimmy na wenzake wala hawakushtuka walikuwa wakimjua sana Felix, ni mtu ambaye yuko emotional sana.

"Damn! Ninachohofia ni maadui kujua kuhusu hili" alifoka na kumnyooshea kidole Jimmy huku akitamani kumtandika ngumi za kichwa lakini hilo lisingewezekana

"Taratibu kaka punguza jazba, halafu si wewe pekee ni mwenye kutaka kusaidia, hata sisi pia tunataka lakini ndio anatuzuia na unamjua vizuri huyu fala, akisema hivi ndio hivo sasa hivyo kuwa mpole tu" aliongea Dylan

Felix palepale alianza kulia huku hasira zikibaki palepale

"I... I just want to help" aliongea huku huku akivuta pumzi makamasi yasoimtoke alikuwa akimaanisha kwamba anataka kusaidia

Sifa mojawapo ya Felix ni kuwa 'mtoto wa mama' yaani yeye pekee ndiye legelege kati ya wenzake, alikuwa emotional kupita kiasi.

Harry aliinuka na kumshika bega huku mkono mwingine akimsugua mgongo kumtuliza na dakika mbele mbele Felix alitulia na kukaa chini akifuta machozi yake

Jimmy aliishia kutoa tabasamu tu na kujiambia "Huyu dogo anadeka sana" na kuendelea zake kunywa kahawa mpaka ilipoisha

Muda ulizidi kusonga mbele mpaka kufikia saa sita ambapo rafiki zake Jimmy walimuaga na kuondoka na kubaki peke yake juu ya roof akifanya tahajudi usiku huo wa utulivu

Alifanya tahajudi kwa zaidi ya lisaa na nusu na kuchanua tabasamu na kujiambia "kumbe ndio iko hivi"

Mara baada ya Jimmy kupanda levo hakujua amepandaje na imekuwaje hivyo aliamua kufanya tahajudi na kutafakari kwa kina na ndipo sasa alipopata ufunuo

Alielewa ili kuingia levo ya Breakthrough alihitajika ku-break ili kuingia, swali linakuja ana'break nini? Ndipo alipopata uelewa kwamba alitakiwa kuvunja msingi wowote mojawapo wa nguvu zake za kichawi na ndio maana ikaitwa "to break through"

Kikawaida misingi ya nguvu zake za kichawi ni minne nayo ni Imani ya ndani, dhamira, ulinganifu wa nafsi na lugha za kichawi. Basi swali linakuja ni msingi gani huo aliovunja jibu analipata kwamba ule msingi wa ulinganifu wa nafsi na ulimwengu

Kwamba hawezi kuamuru au kufanya kile ambacho hana ulinganifu nacho na hata kama akiweza basi atapata madhara, ni pale Jimmy alipoamsha nguvu kubwa ya mkandamizo wakati akipambana na maelfu ya wale wanywa damu ambayo hakuwa na ulinganifu nayo na matokeo yake ndiyo kuja kuidhuru nafsi yake na kuishia kutema damu na nguvu zake kushindwa kufanya kazi

Sasa mhusika anapovunja msingi anatakiwa kuvumulia kila changamoto atakayokutana nayo na kupitia hio changamoto akiweza kuamsha nguvu zake ndipo anakuwa ameingia katika levo nyingine

Haikukuwa na njia yoyote ya kuamsha tena nguvu bali ni wewe na ujuzi wako na hapo ndipo kuliko na ugumu wa kufika levo hiyo lakini kwa Jimmy ilikuwa ni kama bahati, ni pale aliporuhusu utawala wa nguvu mbili(intuition na instinict) ndizo ziliweza kuishtua nguvu yake na kuanza kutenda kazi

"Asee sijui ingekuwaje kama nisingejifunza zile mbinu" alijiwazia

Taratibu Jimmy alisimama na kusogea kabisa mpaka kwenye ukingo wa rloof hiyo na kusimama kisha kujiongelesha "ngoja nijaribu"

Palepale alijitupa kihasara kutoka juu ya rooftop hiyo na kabla hajajibamiza ardhini ghafla aliganda hewani kisha kujiviringissha sarakasi na kutua vyema

Awamu hio hakuhitajika kuongea bali ni kuamua tu ndani ya nafsi yake na kitu inatokea, jambo hilo lilimfurahisha maana alishachoka kutamka kilatini

Mpaka hapo ilikuwa ni saa nane usiku na Jimmy alijiandaa kuingia ndani kulala lakini ghafla alihisi uwepo wa mtu ndani ya uzio wa jumba hilo

Msisimko tu wa mtu huyo aliutambua vyema, i ule wasambazao washirikina hiyo ni kwasababu ulikuwa ni wa chini sanaa! Jimmy aliishia kujiambia kwahiyo huyu mshenzi amekuja kuroga usiku?

"Simama hapo" aliongea Jimmy akimuamuru mtu yule, ndio alikuwa ni yule mzee konki babalao

"Nini! Umewezaje kuniona?" aliongea mzee akiwa haamini kabisa huku wakati huohuo akipatwa na woga. Alikuwa amepaka madawa yake ambayo yalimuwezesha kutoonekana kwa macho ya kawaida vinginevyo angekuwa ameshakamatwa kupitia kamera zilizoko kila kona

Japokuwa Jimmy alikuwa kipofu lakini haikumaanisha hawezi kutambua uwepo wa mtu kiroho

"Swali ni unafanya nini kwenye nyumba yangu? Usiniambie umekuja kuroga"

Mganga yule kiroho alionekana kubeba ungo ambao kulikuwa na madawa aliyoyatengeneza huko na alikuwa hapo kumalizia ishu yake lakini ndii hivyo anakuja kukamatwa

Itoshe kusemza mganga alipanic kinoma na kuanza kuimba nyimbo zake za kishirikina huku akipuliza unga hewani na kutamka maneno ya ajabu ajabu, lengo lilikuwa ni kumzimisha Jimmy kishirikina lakini sasa uganga wake haukuwa na madhara yoyote

Njia pekee aliyoona inafaa kwa wakati huo ni kutoroka tu lakini ni kama vile Jimmy alikuwa ameyasoma mawazo yake hivyo kabla ya mzee kuchukua hatua alijikuta anaelea hewani bila taarifa

Aliiimbaa weee! Alihangaika wee! Lakini alionekana kujichosha bure tu na sauti kumkauka

"Wewe ni nani?" mganga aliuliza mara baada ya kuona amekamatika

"Mimi? Usiwaze sana unakwenda kunijua muda sio mrefu" aliongea na mganga kusikia hivyo kijasho kilimtoka na hofu kumzidia na kujikuta akijikojolea

"Tafadhari bwana naomba uniache niende sitakuja kurudia... Tafadhali... Nina familia" alianza kulia huku akiomba kuachiwa

Jimmy wala hakuwa na muda wa kumsikiliza na badala yake alinyoosha mkono wake kuelekea uelekeo alionasa mzee huyo hewani na kuruhusu nguvu zake za kichawi za kumfanya mganga huyo aonekane kwa macho ya nyama

"Tulia we mshenzi! Nachotaka ni kukufundisha adabu sio kukuua" aliongea Jimmy kisha kupiga filimbi ya mdomo iliyowashtua walinzi

JIMMY ANATAKA KUFANYA NINI?

TO BE CONTINUED

SOLO KING: DARK MAJESTY

CHAPTER 44: Mapigo na mwendo

Haikuwa hata na haja ya kupiga filimbi muda huo kwani walinzi walikuwa mbioni kuja eneo hilo.
Tangu Jimmy aruke juu ya ghorofa na kutua chini salama kutumia nguvu zake aliweza kugundulika kwenye CCTV kamera ziliyofungwa kila kona.na jambo hilo liliwashangaza sana wakina Zuhura, kwao kumuona binadamu wa kawaida kudondoka kutoka juu ya ghorofa moja kisha kabla ya kujibamiza ardhini anaganda hewani ilikuwa kama wako ndotoni, kibaya zaidi mtu mwenyewe ni kipofu.

Hawakutaka kuamini kabisa licha ya kwamba kile walichokiona ni uhalisia hivyo waliendelea kumfuatilia kupitia kamera.
Mwanzoni walidhani labda Jimmy ana utaahira fulani ndani yake kwa kuongea mwenyewe usiku usiku lakini dakika moja mbele mawazo yao yalibadilika na kupigwa na bumbuwazi mara baada ya kushuhudia uelekeo ambao Jimmy amenyoosha kiganja chake binadamu kuibuka kichawi akiwa amening'inia hewani kana kwamba amefungwa minyororo! Cha kushangaza minyororo yenyewe haikuonekana.

Ndipo walipoamua kuchukua hatua na kuja eneo hilo, ni pale jimmy alipopiga filimbi tu walikwisha fika. Walikuwa wakimtazama mzee aliyekuwa akining'inia hewanii huku mwili wake wote ukitetemeka kwa hofu kubwa sana, hakuwa yule kiboko yao tena wala sijui babalao, mzee konki hapo alikuwa ni kama panya anayeomba kuhurumiwa na paka

Ikumbukwe ndani ya Jumba hilo kulikuwa na walinzi wanne tu, mmoja akiwa ni mzee wa getini na watatu waliobaki ni Zuhuru na wenzake ambao huambatana na Bianca kwa sana pamoja na kuzingatia ulinzi wa nyumba

Waliofika eneo hilo ni Zuhura pamoja na wenzake wawili ambao kwa majina mmoja aliitwa pendo na mwingine Esta, wote watatu walionekana kuwa na hofu licha ya kuficha na kujivika ujasiri.

Mzee konki alikuwa amevaa vitambaa rangi nyeusi na nyekundu, alikuwa amevaa kiganga zaidi.

"Tafadhalini si........" Mzee alianza kuomba kuhurumiwa tena lakini kabla ya kumaliza alijikuta mdomo wake ukimsaliti na kujifunga wenyewe pasipo kueleweka imekuwaje, yaani ghaflatu alijikuta bubu na alijua itakuwa ni Jimmy ndiye aliyefanya hivyo, lakini hata kama ni yeye angefamfanyaje?

"Zuhura umefika? Safi nataka unitafutie
Bakora nzuri uniletee" aliongea Jimmy

"Nini! Kwahiyo nimekuwa mtumwa wako? Elezea kwanza nini kinaendelea" alijibu kwa hali ya dharau

"Sikia zuhura fanya kama nilivyosema, hutakiwi kuuliza maswali wewe fata amri" aliongea kwa sauti dhabiti na yenye amri

Sauti ya Jimmy ni kama ilikuwa ikisambaza Aura fulani hivi ya ajabu

"Sawa bwana mkubwa!" alitii bila shuruti, haikueleweka ni kwasababu ya woga ama ni nini lakini Zuhura alienda fata bakora bila ubishi akiwaacha wenzake wakizubaa tu, ni kama askari akipokea maagizo kutoka kwa mkubwa wake

Dakika tatu si.nyingi Zuhuru aliweza kuja na fimbo tatu zilinyooka, zenye urefu wa zaidi ya nchi ishirini na kumpatia mikononi mwake kisha kutulia tuli kuona nini kinafata, hakuthubutu kufungua kinywa hata!

Kati ya zile fimbo tatu alizopokea jimmy kwa mkono wa kulia alichomoa mbili na kuzishika mkono wa kushoto huku moja ikibaki mkono wa kulia, kulikuwa hakuna haja ya kuelezea ni nini kinakwenda kutokea mda si mrefu

"Bila shaka kwa sauti yako utakuwa ni mzee na mimi kusema ukweli huwa naheshimu sana wazee, ila je wazee nao hawapaswi kufundishwa adabu pale wanapokosea?" Jimmy aliongea akimuuliza mzee huyo bila kujibiwa

Sio kwamba mzee huyo hakuwa akitaka kujibu bali ni kwasababu kila akijaribu kufungua mdomo sauti ilikuwa haitoki na sababu yenyewe hakuijua, alitamani sana kuongea ni vile tu haikuwezekana kwa wakati huo. Ni sura yake pekee iliyoonyesha ni nini alichotaka kuongea.

"Kwamba kuwafundisha adabu itaonekana kwamba hatuna adabu?" aliuliza tena huku akinyanyua mkono wake wa kulia alioshika fimbo

"Chwaaa! Chwaaa! Chwaaa!" Ilikuwa ni milio ya sauti ya kuchalazwa kwa bakora

Sio siri mzee alikuwa akiumia na kulia bila sauti huku mimacho ikimtoka kuashiria kwamba zinamuingia kisawasawa, kama ni kuyakanyaga basi ameyakanyaga haswa!

"Nachowapendea wazee ni kwamba wanatumiaga sana busara kwenye mambo mengi lakini kwa bahati mbaya sina busara hasa kwa washirikina kama nyinyi" aliongea huku akiendelea kumchalaza bakora mzee wa watu

Maskini mzee wa watu alikuwa akijikunjakunja hewani kwa tabu sana, ilifikia hatua mpaka makamasi yalianza kumtoka. Macho yalikuwa mekundu kama mvuta bangi kwa kulia, ubaya ni kwamba huko kulia kote sauti haikuwa ikimtoka. Hakika alijuta sana kuingia kwenye anga ya mwenyewe

Zuhura na wenzie walikuwa wakimuonea sana huruma mzee wa watu lakini hakuna aliyedhubutu kumtetea. Zilichalazwa bakora zaidi ya ishirini hivi kisha kutulia kwa sekunde kadhaa

"Hizi zinatosha?..... nahisi bado..ngoja niongezee mbili tatu" Jimmy ni kama vile alikuwa akiongea na nafsi yako na kujijibu mwenyewe

Kwa mara nyingine tena alinyanyua mkono wake wa kulia alioshika fimbo kutaka kuendeleza kichapo kama kawaida na hakuwa na hatia kabisa, yani kifupi kwake alichokuwa akifanya aliona ni ushujaa wa hali ya juu na ile anataka kushusha mkono Zuhura alikusanya ujasiri na kumuwahi

"Jimmy inatosha! Huoni unachofanya ni ukatili?"

"Hujakosea mimi sioni isitoshe sasa nina upofu pia kama unataka kumtetea huyu fala na kutaka kutandikwa kwa niaba yake unakaribishwa, Je uko tayari?" aliongea kibabe

"Sijamaanisha hivyo nachomaanishi ni utaendelea kumpiga mpaka aaa ngapi?-

"Mpaka nitakaporidhika" alijibu

"Kwanini tusimalize hili swala na kumprleka polisi" aliongea zuhura na kumfanya mzee atingishe kichwa kukubaliana nae, aliona ni bora kwenda selo kuliko kuendelea kula kichapo na aje kushtuka kumekucha tayari

"Tangu lini mshirikina anapelekwa polisi? Siku zote mshirikina anapokamatwa kwenye harakati zake za kuroga anatakiwa kuuawa ashukuru tu mpaka sasahivi yuko hai.... kwanza watu kama hawa kazi yao ni kuharibu tu maisha ya watu ukiwauliza tumewakosea nini jibu ni hakuna tulilowakosea zaidi ya chuki tu na tamaa zao za kijinga" aliongea huku kama kawaida akiendelea kushusha kichapo

"Chwaa! Chwaa! Chwaa! Chwaa! Chwaaa!" Ulikuwa ni mwendo wa kushushiwa kichapo kwa zaidi ya nusu saa mpaka mzee alihisi kutaka kuzimia

Baada ya Jimmy kuridhika na bakora za haki aliruhusu uchawi wake wa kifungo cha hewani kumuachia mzee huyo na kuanguka makalio

"Yereuwiiiiiii!!" Kitendo cha kuachiwa hewani na kuangukia makslia ni kama vile amefunguliwa na sauti na kilichofuata ni yowe la maumivu makali hakudhubutu hata kugusa makalio yake maana kugusa ni sawa na kuweka chumvi kwenye kidonda kibichi

"Sasa mzee ni muda wa kutumia busara au turudi tulikotoka?" alimuuliza, Mzee asingeelewaje kwa mfano?alielewa kabisa hapo amepewa nafasi ya kujielezea vinginevyo ni mapigo na mwendo

Ukweli alichofanya Jimmy kilikuwa ni ukatili sana kwa mzee lakini hiyo yote ni kutaka kurahisisha mambo, kusudi lake lilikuwa ni kumuadhibu na kwa wakati huohuo kumuonjesha ladha halisi iwapo ataleta ujuaji pale anapotaka maelezo. Ni mbinu ya kikuda lakini ndiyo mbinu iliyomjia kichwani mwake, hakujali kama alikuwa ni mzee au nani.

"Nasema! Nasemaaa!"aliongea huku akibubujikwa na machozi. We vuta picha jinsi mzee mwenye mvi nyingi anavyolia kama mtoto hakika ilitia huruma sana!

"Ongea sasa'

"Ukweli mimi ni mganga na nipo hapa kutimiza mahitaji ya mteja wangu ambaye ana chuki nawe"

"Nani huyo?"

"Ni Bakari Juma maarufu kama Beka nadhani unamjua, japokuwa sijui imekuwaje mpaka kutengeneza chuki na wewe ila alichotaka ni kukufanya kilema wa miguu ushindwe kusimama wala kutembea" alieleza

"Kudadeki huyu mshenzi amevuka mipaka" alijiongelesha Jimmy akimaanisha Beka

"Na kama unavyojua sisi waganga kazi yetu ndio kama hizi pia kibunda kilinona hivyo sikukataa" aliongea na kumfanya Jimmy afikiche pua yake kwasababu ya harufu ya ajabu iliyokuwa ikisumbua pua yake

"Kwahiyo ulipanga kunifanyia nini usiku huu?"

"Hiyo hapo ni mchanganyiko wa damu ya kuku, mwewe, njiwa na baadhi ya dawa nilipanga kukupaka miguuni kishirikina lakini...."

".....mpango umefeli si ndio ulivyotaka kusema" Jimmy alimalizia sentensi yake na mzee huyo kutingisha kichwa huku akifuta machozi yake

"Sasa sikiliza mzee unaona huo ushenzi wako?" alimuuliza huku akinyooshea mkono alipohisi harufu ile inatokea kwenye ungo na mzee alitikia "ndio"

"Nataka ukamfanyie huyo fala mwenzako sasahivi nikiamka asubuhi nataka kusikia huyo fala ni kilema wa maisha unanisikia?"

"Ndio ndio!"

"UNANISIKIA?" alirudia tena kwa sauti na mzee pia kuitikia kwa sauti

"Aya potea!" aliongea kibabe na kwa amri, mzee kusikia hivyo alinyanyuka haraka japo kwa tabu na kubeba ungo wake na kupotea kishirikina eneo hilo hali iliyowashitua na kuwaacha midomo wazi wakina Zuhura. Kwa mara ya kwanza waliweza kushuhudia binadamu akipotea kishirikina mbele ya macho yao

"By the way usiku mwema mi nakwenda kulala" aliongea jimmy huku akizitupa zile fimbo na kuweka mikono yake mfukoni kisha kuanza kupiga hatua kutoka eneo hilo

"Unakoelekea siko" aliongea pendo na kumfanya jimmy ajikwae kidogo kisha kujiweka sawa na kugeuza kushoto

"Hapana sio huko unakosea" aliongea tena na Jimmy kusimama huku akijikuna kichwa

"Ooh wapi tena?" alijiuliza kujua uelekeo wa kuingia ndani

Zuhura kwa kujiongeza tu alimfata mpaka karibu yake na kumshika mkono wa kulia kisha kumuongoza mpaka mlango wa kuingia ndani kisha kumuacha, uzuri haukufungwa bado.hivyo Jimmy alifungua na kisha kuanza kutembea kuelekea chumbani kwake, uzuri ramani ya nyumba aliijua vizuri hivyo ndani dakika mbili alikuwa chumbani kwake

Upande wa Zuhura na wenzake waliishia kumuangalia akitokomea huko juu kisha kufunga mlango na kurudi kwenye nyumba yao

Jimmy mara baada ya kufika chumbani kwake alienda mpaka kitandani kwake na kulitoa godoto na kuliweka chini ya sakafu kama tamaduni za wajapani na kulala zake. Hakutaka tabu ya kupanda kitandani na kushuka mwisho wa siku aje kuanguka au kujigeuzageuza na mwisho wa siku kusnguka! Hakutaka kabisa, hata kama alikuwa na intuition kali kipofu ni kipofu tu.

°°°°°°°°°°

Kesho yake kukakucha kama kawaida ikiwa ni asubuhi ya saa tatu mwamba aliweza kuamka huku akipiga miayo na kujinyoosha.

Kiuchovu alitambaa mpaka mlango wa kuingia washroom na kusimama kisha kuingia na humo kwa kuhangaika kupapasapapasa alifanikiwa kupata mswaki wake na dawa na baada ya kuweka alipigs mswaki fresh na kumaliza

Baada ya kumaliza alitoka na kwenda mpaka kwenye kabati la nguo na kurudia mahsngaiko ya kupapasapapasa mpaka kulipata taulo na kufsnikiwa.

Alivua shati lake na kulitupia hukooo! ile anataka kuvua suruali ghafla anasikia sauti ya kike iliyomshitua mpaka kuruka juu kidogo

"My lord." aikuwa ni Damiana au kwa kifupi Mia, haikueleweka amefikaje hapo na ni saa ngapi amefika

"We Mia unafanya nini humu?"

"Nipo hapa kukuhudumia Bwana wangu katika hizi nyakati ngumu"

"Nyakati ngumu zipi? Halafu nishasema uniite Jimmy"

"Okay Jimmy ni kwasababu kwa sasa huoni hivyo nitakusaidia kwenye mambo kadha wa kadha"

"Kwanza umeingiaje humu?"

"Kupitia mlango "

"Unataka kusema umeingia humu ndani bila mtu yoyote kukuona?"

"Ndio, kwangu mimi hilo ni suala jepesi sana" alijibu na mara ghafla zilisikika hatua za miguu zikikaribia mlango wa chumba hiko

"Damn!" Jimmy alipaniki sio kitoto

"Oya Mia ingia uvunguni fasta" alinong'ona lakini ghafla anakumbuka uvungu wenyewe uko wazi kwakuwa alilitoa godoro

Mia haraka haraka aliingia kwenye kabati la nguo na kujificha humo na Jimmy kujituliza na baada ya sekunde tatu mlango ulifunguliwa na Bianca kuingia ndani humo

"Mummy ni wewe?" Jimmy aliuliza huku akisogea mlangoni taratibu

"Harufu yako ni nzuri sana kama kawaida hakika siwezi kuisahau tangu iliponisisimua mara ya kwanza kuisikia" aliongea huku akitabasamu

Bianca aliangalia chumba hiko kulia na kushoto na kukuta hakijatulia, kitandanj hakukuwa na godoro, kule chini kulikuwa na taulo, huku kulikuwa na t sheti, kule viatu, mlango wa kuingia washroom ulikuwa umefunguka na baadhi ya vitu kuanguka inshort chumba kilikaa kifujo zaidi

Bianca mara baada ya kukikagua chumba alimgeukia kumtazama Jimmy ambayo muda wote sura yake ilikuwa imepambwa na tabasamu na palepale alimsogelea na kumkumbatia

Jimmy alishtushwa tu na kumbatio hilo la ghafla na kuishia kumeza mate mengi huku naye akitoa ushirikiano kwa kupapasa nywele za mrembo huyo

"Mummy kuna tatizo?" aliuliza na Bianca alijikaza asilie yaani tabia ya Jimmy ilimkasirisha na kumhuzunisha pia, hiyo tabia ya kujifanya yuko sawa ilihali hayuko sawa na kuuliza kama anatatizo ilihali yeye ndo mwenye tatizo ilimuuma

"Kuanzia sasa nitakulinda sawa?I will take care of you" aliongea Bianca na kutoka kwenye kumbatio hilo na kumwangalia usoni

"Fumbua macho" Bianca alimwambia, huyo ni kwasababu Jimmy muda wote huwa anayafunga macho yake na Jimmy bila ubishi aliyafumbua

Bianca aliyatazama macho yake kwa dakika kadhaa na kubusu kabisa karibu na macho hayo kwa upendo wa hali ya juu na kumkumbatia tena huku akiegemesha kichwa kwenye kifua cha mwanaume huyo

TO BE CONTINUED.......
 
Hiyo Jimmy anatamka hayo maneno ya kilatini halafu anaganda hewani as if hakuna gravity dah riwaya kali kinoma big up mwandishi
 
Kali sana big up mwandishi,

"What the JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala" Bwana aliyebeba boksi alimaka kwa mshangao

Uandishi mkali sana huu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom