Simulizi ya kijasusi: Nyayo za Shetani

Simulizi ya kijasusi: Nyayo za Shetani

singanojr

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2020
Posts
2,153
Reaction score
10,849
Damiani ni kijana wa miaka ishirini na mbili, mhitimu wa chuo kikuu cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) akiwa amechukua kozi ya Finance and Accounting in Public Sector (kozi inayohusu maswala ya uhasibu). Mara baada ya Damiani kumaliza masomo yake hakutaka kubaki ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwani hakuwa na kazi maalumu ambayo ingemuwezesha kujiingizia kipato ndani ya jiji hilo. Pia maisha ndani ya jiji hilo yalikuwa ghali sana na yalihitaji pesa ili kuweza kuishi.

Hivyo mara baada tu ya kumaliza masomo yake aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini mkoani Tanga kwa ajili ya kusikilizia upepo wa ajira. Kwani mwaka ambao alikuwa amemaliza haukuwa kama miaka ya nyuma kwamba ukimaliza tu unasubiri matokeo na kupata ajira. Kinyume chake ni kwamba utasubiri matokeo yatoke na kuomba ajira kwa makampuni ambayo yatakuwa na uhitaji au serikali pale itakapotangaza nafasi za ajira na kuomba. Na kwa kuwa kipindi hicho kulikuwa na wimbi kubwa la vijana ambao walikuwa wahitimu na hawakuwa na ajira mtaani, hivyo ilikuwa ngumu sana kupata ajira. Ilikuwa ni kama kubahatisha tu pale nafasi zinapotoka kwani wengi wa waombaji wana sifa zinazofanana.


Mkuzi ndio kijiji cha kijana Damiani. Kijiji hiki kilikuwa ndani ya wilaya ya Lushoto, kilomita kadhaa kutoka Lushoto mjini. Yaani kama utasafiri kwa gari ni muda wa dakika thelathini mpaka arobaini kufika ndani ya kijiji hicho. Ni moja ya vijiji ambavyo vilikuwa vimezungukwa na misitu na kuwa na mazingira ya kuvutia sana. Yalikuwa ni moja ya mazingira ambayo watalii wengi wa mataifa ya nje na hata watalii wa ndani walikuwa wakipenda kutembelea. Na hiyo yote ni kutokana na hali yake ya hewa ilivyokuwa safi na ya kuvutia.


Basi kijana Damiani ndani ya kijiji cha Mkuzi ndipo alikulia na kujipatia elimu yake ya msingi na sekondari.


Damiani alikuwa kijana mpole, mcheshi, mrefu maji ya kunde, mwenye sura yake ya kuchongoka lakini iliyoumbwa vizuri. Alikuwa ni moja ya vijana walio kuwa na miili mikubwa ya wastani. Damiani alikuwa akiishi na mama yake tu kwani baba yake alikuwa amekwisha kufariki miaka mingi nyuma kipindi akiwa tu na umri wa miaka kumi.


Kurudi kwa Damiani kijijini baada ya kumaliza masomo ilikuwa ni moja ya furaha kubwa sana kwa mama yake kumuona mwanae kurudi ndani ya kijiji hicho, kwani mama huyo alikuwa akimpenda sana mwanae.


“Karibu sana mwanangu,” mama alifurahia sana kwa mwanae kumaliza masomo yake ya ngazi ya juu, na kujihisi kuwa mwanamke aliyefanikiwa kulea kwani watoto wengi ndani ya kijiji hicho hawakufanikiwa kufika ngazi ya juu ya kielimu kama ilivyokuwa kwa Damiani.


“Asante mama, hatimae nimemaliza chuo na nimerudi rasmi,” aliongea Damiani huku akiachia tabasamu. Huku nje watoto wengi walikuwa wakimwangalia na kumshangaa. Hiyo ilikuwa ni kawaida sana kwa vijiji kushangaa watu walio tokea mjini na hata kwa wageni pia.


Basi Damiani alikaribishwa vizuri na mama yake katika nyumba yao hiyo ya vyumba vitatu iliyoezekwa kwa mabati, na kwa kuwa Damiani alikuwa na chumba chake tokea akiwa shuleni ndiko mama yake alipeleka begi lake na kukifanyia usafi.


Maisha ya kijana Damiani yanaanza rasmi ndani ya kijiji cha Mkuzi. Licha ya Damiani kuwepo ndani ya kijiji hicho lakini alikuwa na mipango mikubwa sana ya maisha yake hapo mbeleni, kwani alihitaji kuja kuwa mfanya biashara mkubwa sana katika maisha yake na hiyo ilikuwa ndiyo moja ya ndoto yake kubwa. Japo alikuwa amesoma na alikuwa akitarajia kuwajiriwa lakini ajira kwake haikuwa kipaumbele. Ila kipaumbele kwake ilikuwa ni kupata mtaji utakaomwezesha kuanzisha biashara. Hakika alikuwa na safari ndefu sana na hata kwa yeye pia alilijua hilo na hivyo kwa umri aliokuwa nao hakuwa na sababu ya kukatishwa tamaa na mazingira aliokuwemo na aliokulia. Kwani alichokuwa akikiamini katika maisha yake ni juu ya uchapaji kazi kwa bidii na kutokukata tamaa na kuwa na malengo ndiyo nguzo kubwa sana ya kuja kufanikiwa. Hakutaka kabisa kukatishwa tamaa na hali ya maisha yao ya umasikini yaliyopo hapo nyumbani, ila aliamini katika mawazo chanya tu.


Basi hatimae wiki, mwezi na hata miezi ilikatika na matokeo yake yalikuwa yamekwisha kutoka na akiwa amefaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza. Kwake na kwa mama yake ilikuwa ni furaha na faraja kubwa sana, kwani aliamini kupitia ufaulu mkubwa basi angeweza kumrahisishia kupata kazi kwa wepesi zaidi.


Hakutaka kusafiri mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya kuomba kazi ilihali kulikuwa na njia rahisi. Alichokifanya yeye ni kutuma maombi kwa kila kampuni ambayo ilikuwa ikitangaza nafasi za ajira kwa njia ya mtandao.


Mwezi wa kwanza uliisha kijana Damiani akiwa amekosa kabisa uelekeo wa ajira kwani ni makampuni zaidi ya matatu ambayo alikuwa ameomba kwa ajili ya kupata ajira lakini amekosa hata wito wa interview (mahojiano ya kiufanisi). Zikiwa zimepita siku kadhaa za kijana Damiani kukata tamaa, hatimae kwenye moja ya kampuni ambayo haikuwa imetoa majibu ilirudisha jibu kwa kijana Damiani kwa ajili ya kuhudhuria interview.


Ilikuwa ni moja ya kampuni iliyokuwa ikipatikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, kampuni moja ya usafirishaji iliokuwa na makao yake makuu ndani ya Posta. Kwake Damiani alifurahia kwani aliona tumaini la kupata ajira linaridhisha zaidi. Alimwambia mama yake juu ya taarifa hiyo na mama yake pia alifurahia na kumpa baraka zote mwanae kwa ajili ya kuhudhuria interview hiyo.


Ilikuwa ni siku ya Jumatatu ndiyo siku ambayo kijana Damiani alikuwa ndani ya basi akielekea jijini Dar kwa ajili ya kuhudhuria interview. Alifanya maombi juu ya safari yake hiyo na kusudio lake analoliendea kulifanyia kazi.


Kutoka Lushoto mpaka ndani ya jiji la Dar ni umbali wa masaa sita mpaka saba. Hivyo Damiani alikuja kufika ndani ya jiji hilo kwenye muda wa saa nane kamili mchana. Siku hiyo alipanga akifika ndani ya jiji hilo kwa kuwa hakuwa na ndugu wa kufikia, alipanga kwenda kwa rafiki yake mmoja aliyekuwa amemuacha ndani ya chuo akiendelea na masomo kwa ajili ya kumuhifadhi mpaka siku inayofuata afanye interview na kisha ageuke kurudi nyumbani.


Basi baada tu ya kushuka ndani ya basi akijisogeza mpaka kwenye daladala zinazoelekea Mbagala na kisha alipanda huku malengo yake aje ashukie Mtongani kwa Azizi Ally kwani hapo ndipo rafiki yake huyo alipokuwa akipatikana kwa kuishi. Barabara haikuwa na foleni sana hivyo hawakuchukua masaa mengi kufika sehemu aliokuwa amekusudia.


Mara baada tu ya kushushwa hatimae alinyoosha moja kwa moja upande wa kushoto wa barabara, huku akipita vichochoro viwili vitatu na kuja kutokelezea mbele ya nyumba moja kubwa iliokuwa na ukuta. Hatimae alisimama nje ya geti la nyumba hiyo huku kama ni mtu aliyekuwa akijishauri agonge ama asigonge. Ila kwa kuwa kilichomleta hapo ni kuonana na rafiki yake na rafiki yake alikuwa akiishi ndani ya nyumba hiyo basi hakuwa na budi ya kugonga geti hilo.


Haikuchukua muda mrefu hatimae alikuwa amefunguliwa na msichana mmoja aliyekuwa amejifunga khanga moja, na alionekana alikuwa akifua kwani alikuwa na mapovu mikononi.


“Karibu,” sauti hiyo nyororo ilimkaribisha ndani huku dada huyo akitangulia mbele na kumuacha kijana Damiani kumsanifu mdada huyo kwa nyuma. Alikuwa ni mlimbwende kweli aliyekuwa amejaliwa umbo zuri haswa la kumvutia kila mwanaume atakayemtia machoni. Alikuwa mrefu wa wastani mwenye rangi yake ya chocolate, alibarikiwa uso wa duara na kwa tathmini za haraka haraka mdada huyo alionekana umri wake haukuwa chini ya miaka ishirini kwenda juu.


“Nimemkuta Elvis??”


“Katoka sema anakuja muda si mrefu. Wewe ndio Damiani??”


“Ndio ni mimi.”


“Okey! Alinipa maelekezo yako kwamba ukifika nikukaribishe ndani,” aliongea msichana huyo huku akimkaribisha Damiani ndani kwani muda wote huo alikuwa amesimama. Damiani alijua lazima huyo mdada atakuwa hawara (mwanamke anayeishi na mwanaume pasipo kuolewa au mpenzi) wake Elvis maana alimjua mngoni huyo songea kwa kupenda warembo hakuwa nyuma na ndiyo maana kabla ya kutoka nyumbani alimtaarifu kuwa atakuja kulala kwake.


Basi mdada huyo alimuongoza Damiani ndani ya nyumba hiyo iliokuwa imepakwa rangi nyeupe mpaka kwenye chumba cha katikati upande kushoto na kisha alimkaribisha ndani. Kilikuwa ni chumba kimoja kikubwa saizi ya kati kilichokuwa kimejaa makorokocho mengi. Damiani alikuwa akikijua chumba hicho sana kwani hata kwa baadhi ya vitu hivyo vilikuwa vyake na ni baada ya yeye kumaliza masomo alimuuzia rafiki yake huyo.


Basi baada ya kukaribishwa dada yule alitoka nje na kuendelea na shughuli yake ya ufuaji huku akimwacha Damiani akimsubiri rafiki yake. Na haikuchukua hata dakika ishirini rafiki yake Elvis aliingia ndani ya nyumba hiyo. Elvis alifurahia sana kumuona Damiani na hata kwa Damiani ilikuwa ni hivyo hivyo. Wote walifurahia kuonana kwa mara nyingine.


“Karibu sana HB asiyetaka warembo,” aliongea Elvis akionesha kumtania mwenzie na kwa Damiani kwa kuwa alikuwa ashamzoea rafiki yake huyo kwa matani basi na yeye alicheka.


“Mzee wa totozi, naona shemeji yangu wa awamu hii ni shida.”


“Yaani acha tu mzee toto la toto na isitoshe limedata na ndiyo limenifanya nihangaike siku ya leo.”


“Unahangaishwa na nini sasa??”


“Hahaha lazima kuhangaika. Unajua jana ulivyonicheki unakuja ilikuwa ghafla sana na sikutaka kukwambia naishi na mtoto wa kike. Kwa hiyo unavyoniona hapa kuna msela nimetoka kumpanga ili ukale mbonji kwake ukamilishe mambo yako maana hapa sikuwa na jinsi.”


“Daah! Hapo ndiyo maana nakukubali mshikaji wangu.”


“Hahaha… usijali mzee si unajua hata wewe umenisaidia mara kibao. Hata mavitu haya ni kama ulinipa tu kutokana na bei ile.”


Basi Damiani walichukana na rafiki yake na kutoka eneo hilo kuelekea barabarani na kupanda magari ya kuelekea Rangi Tatu. Walivyofika Mbagala Zakhemu walishuka na kuchukua upande wa kushoto barabara. Umbali wa mita kadhaa hatimae waliingia chochoro ambayo walikuja kuibukia mbele mtaa mwingine, na wakaja kutokea mbele ya kanisa la KKKT na hapo walipinda kushoto tena na kukuta nyumba moja kubwa iliokuwa na geti na kwa nje ilisomeka kwa maandishi ya lodge. Elvis alisukuma mlango na kisha aliingia ndani. Kwa Damiani yeye alikuwa akifatisha tu kuona mwisho wake kwani kuna hisia zilizokuwa zikimwambia kaletwa lodge.


“Oya mshikaji anakaa hapa, si lodge hapa tena japo ilikuwa lodge. Mwenye nyumba kaamua kuifanya nyumba ya kupangisha,” aliongea Elvis na kumfanya Damiani aelewe. Walipita kwenye vyumba kadhaa na hatimae walisimama nje ya mlango na Elvis aligonga na nusu dakika mlango ilifunguliwa na jamaa mmoja wa makamo mfupi mwenye mwili mkubwa wa kibonge.


“Karibuni.”


Waliingia ndani ya chumba hicho. Kilikuwa ni chumba kikubwa na kizuri sana, na pia hata kitanda na samani (furniture) zilizokuwemo humo ndani zilionesha jamaa anayeishi humo ndani hakuwa mnyonge kipesa.


“Oya huyu ni Joshua rafiki yangu sana mwaka wa kwanza hivyo ndiyo utachilia hapa kwake mpaka utakapokamilisha mambo yako,” aliongea Elvis na Joshua alimkaribisha Damiani na Elvis aliaga akaondoka.


Basi siku nyingine iliingia ambayo ni siku Damiani alikuwa akielekea mtaa wa Posta kwa ajili ya kufanya interview. Alikuwa amevaa akapendeza maana kwenye nguo alikuwa nazo na mkopo ulimsaidia sana kipindi akiwa chuo.


Alijisogeza mpaka barabarani ili kusubiri gari ya kwenda stesheni Posta apande. Ila mara baada ya kufika tu kwenye barabara nje kabisa ya supermarket iliyosomeka kwa jina la Kivoni, ilisimama gari moja aina ya Vanguard nyeusi na kioo kilishushwa na akaonekana bwana mmoja wa makamo, makadirio ya miaka 30 kuendelea mweusi alivalia shati jeupe na koti akiwa na miwani. Damiani wakati huo gari hiyo ikisimama alikuwa akiiangalia na hata jamaa huyo alivyoshusha kioo alikuwa pia akimwangalia. Damiani alijikuta akijishtukia na hiyo ni mara baada ya jamaa huyo kumuonesha ishara ya kumuita. Alijithibitishia kama ndio yeye aliyekuwa akiitwa na hapo ndipo alipopiga hatua kulisogelea gari hilo.
 
02
"Vipi, wapi unaelekea?" aliuliza mwanaume yule.


"Naelekea Posta."


"Sawa, ingia twende — naelekea upande huo. Nina baadhi ya maswali nataka nikuulize," aliongea jamaa yule, na kumfanya hata Damiani ashangae: inakuwaje mtu asiyemjua awe na maswali ya kumuuliza? Jambo hilo lilimpa mashaka mengi juu ya mtu huyo.


"Fanya haraka, ingia, acha uoga — asubuhi yote hii unawaza mambo mabaya," aliongea yule jamaa. Ni kama alijua ni kitu gani alikuwa akikimaanisha. Damiani, kwa mashaka mengi, alijiingiza kwenye gari hilo, kisha likawashwa na kuondoshwa eneo hilo.


"Unaenda kufanya mahojiano?" aliuliza yule bwana, na kumfanya Damiani ashangae zaidi — ni vipi alijua kuwa anaenda kufanya mahojiano?


"Usiwe na wasiwasi. Mimi nimeishi miaka mingi na najua hulka ya vijana wengi, hasa wanapoenda kuomba kazi. Wewe kwa uvaaji wako unaonekana wazi kwamba unaenda kufanya mahojiano, kama sio kuomba kazi."


"Ndiyo, naenda kufanya mahojiano," alijibu.


"Umesomea kozi gani na elimu yako ni kiwango gani?"


"Degree ya Finance and Accounting in Public Sector."


"Sawa, safi, na hongera. Unapaswa kujiamini tu. Maswali wanayouliza ni ya kawaida sana — unaweza kuulizwa 'elfu kumi ina mnyama gani' na ukakuta swali hilo lina maksi nyingi zaidi," aliongea yule bwana, huku akiongeza umakini katika barabara iliyokuwa na magari mengi asubuhi hiyo.


Hawakuchukua muda mrefu — walikuwa Posta. Gari ilisimamishwa kwenye jengo la Waterfront na Damiani akashuka. Bado alikuwa na dukuduku la maswali mengi kichwani mwake kuhusu jamaa yule — alivyomwambia wakati wa kumpandisha gari kwamba alikuwa na maswali ya kumuuliza, lakini cha kushangaza, hayo maswali hayakuulizwa. Hata hivyo, hakutaka kufikiria sana, na aliona labda jamaa huyo hakuwa na nia ya kweli ya kumuuliza maswali, bali alitaka tu kumsaidia kwa kumpa lifti — na kama alivyosema, alijua kwamba alikuwa akielekea mahojianoni.


Wakati akitembea kuelekea upande wa Samora, alijikuta akikumbuka yale maneno: "unaweza kuulizwa 'elfu kumi ina mnyama gani'." Hapo ni kama amekumbuka kitu. Alianza kujiuliza — elfu kumi ina mnyama gani? Lakini hakuweza kabisa kupata jibu. Alijaribu kuchochea akili yake ili kupata jibu, lakini alijikuta akikosa kabisa. Aliinua mkono wake wenye saa — bado alikuwa na muda wa kutosha kabla ya mahojiano kuanza.


Basi kijana Damiani aliamua kusogelea duka moja lililokuwa na Tigo Pesa, kwa ajili ya kutoa kiasi kidogo cha pesa ambacho kitamsaidia katika mahitaji yake ya siku hiyo, na kilichobaki angefidia nauli ya kurudi nyumbani Lushoto.


"Kumbe tembo! Daah, upuuzi kabisa — yaani siku zote naishika hii hela, nimeshindwa kujua kwamba mnyama ni tembo! Haha..." aliongea huku akivuka barabara. Hatua chache tu mbele aliona jengo alilokuwa akilitafuta — mita kadhaa tu mbele — ndipo kampuni ya usafirishaji ilipokuwa, na ndipo alipokwenda kufanya mahojiano.


Alijikuta akipigwa na mshangao mara baada ya kufika ndani ya eneo hilo, maana kulikuwa na watu wengi sana waliokuwepo, na wote hao walionekana walikuwa wameitwa kwa ajili ya mahojiano.


"Hapa kweli kweli kuna kupata ajira?" alijiongelesha huku akiingia ndani kabisa ya jengo hilo, kwenda mpaka eneo la mapokezi. Aliarifiwa kwamba utaratibu ni kusubiri, kwani mahojiano yataanza muda si mrefu.


Basi alijiunga na wenzake kusubiri. Hakutaka kukata tamaa kirahisi, kwani alikuwa amejiandaa vya kutosha. Siku zote aliamini kwamba katika nafasi ya watu kuchaguliwa, kama wote wana nafasi sawa, basi hakuna sababu ya kukata tamaa — hata yeye anayo nafasi ya kushinda na kupata ajira. Hivyo alizidi kujipa moyo na kujiandaa. Baada ya dakika arobaini hivi, watu wote waliitwa kuanza mahojiano — yalikuwa ni mahojiano ya maandishi kwa nafasi ya Msimamizi wa Fedha (Finance Manager).


Wasimamizi wa rasilimali watu waliokuwa wakisimamia mahojiano hayo walitoa maelekezo ya kila namna, hatimaye mahojiano yalianza. Ajabu kwa Damiani ni kwamba jambo lile aliloambiwa na yule mtu aliyempa lifti lilikuwa kweli kabisa — hata yeye mwenyewe alijikuta akishangaa sana. Ilikuwaje jamaa yule akajua kwamba ataulizwa swali la "elfu kumi ina mnyama gani"? Ilikuwa ni ajabu iliyojaa bahati.


Mahojiano yale yalienda vizuri upande wake, huku akiamini kabisa alifanya vizuri. Kilichofuata ni matokeo tu ya mahojiano hayo. Japo mtu yule wa asubuhi alikuwa amempa mashaka, sasa alijikuta akimwona kama malaika aliyetumwa na Mungu.


*****


Upande mwingine, ndani ya jengo la LPPF Tower lililokuwa likipatikana ndani ya Mikocheni Sayansi, gari moja nyeusi aina ya Range Rover Sport ilisimama asubuhi hiyo ndani ya eneo la maegesho. Alishuka mwanaume mmoja mwenye umri kati ya miaka hamsini hivi, aliyevalia suti nadhifu iliyomkaa vizuri. Alikuwa na mwili mkubwa kidogo na alionekana ana afya nzuri. Alitanguliwa na bwana mmoja aliyevalia miwani — bila shaka alikuwa mlinzi wake au msaidizi wake.


Basi alitembea kuingia ndani ya jengo hilo, mkononi akiwa ameshikilia miwani yake ya jua, huku msaidizi wake akiwa ameshikilia mkoba mweusi (briefcase). Walifuatana mpaka kwenye lifti na kisha walibonyeza kitufe cha nambari kumi na sita, kuashiria ghorofa waliokuwa wakielekea. Haikuwachukua muda mrefu — walikuwa ndani ya ukanda mrefu kidogo uliokuwa na mandhari ya kuvutia. Mbele kabisa kulikuwa na maandishi: KIMBONA INTERNATIONAL LINK AND COMPANY (KILAC).


Mzee huyo alitembea kwa mwendo wa taratibu lakini wenye nguvu, na kufika eneo la mapokezi. Alikutana na dada mmoja aliyevalia nadhifu, aliyekuwa akisimamia mapokezi. Mara alipomuona mzee huyo, alisimama haraka na kumsalimu — alikuwa ni katibu (secretary).


"Shikamoo, boss. Karibu kazini," aliongea dada huyo kwa heshima kubwa, na mzee huyo aliitika bila kujali sana, akapita kuelekea ofisi moja iliyosomeka jina la Mkurugenzi. Aliingia ofisini humo, kisha yule mlinzi aliweka ile mkoba juu ya meza.


Ilikuwa ni ofisi ya kuvutia sana, iliyonakishwa vyema. Samani zilizokuwepo humo ndani zilikuwa za bei ya juu sana, lakini bei hiyo iliendana na ofisi kwani ziliipendezesha kwa ujumla wake.


"Sawa, Derick, tutaonana baadaye. Hakikisha unafuatilia lile swala kwa umakini mkubwa, kwani baadaye nina kikao na nataka kuwa katika nafasi nzuri kwenye kikao hicho."


"Sawa, boss," aliongea kijana huyo kwa sauti ya uthabiti, kisha aligeuka na kutoka ndani ya ofisi hiyo.


Hazikupita dakika kumi, simu ilipigwa — ilitoka kwa katibu, akimjulisha bosi wake kwamba kuna mgeni wake. Bwana huyo aliruhusu mgeni huyo kuingia.


"Mister Kimbona!"


"Samueli! Hahaha... Umefika lini Tanzania?" aliongea Mister Kimbona kwa bashasha sana, huku akimkaribisha mwanaume huyo aliyesimama mbele yake. Alikuwa ni mwanaume wa umbo lake — si mrefu sana — umri wa miaka arobaini hivi kwa makadirio, akiwa amevalia suti yake ya gharama ya rangi ya buluu.


"Nimefika juzi, mara baada tu ya kupata taarifa za kunifurahisha moyo."


"Hahaha, karibu sana. Nipe hizo taarifa — huenda hata kwangu pia zikawa za kufurahisha."


"Wewe ushazisikia sana, na kama ni za kufurahisha basi zishakufurahisha mpaka zimechuja."


"Hahahaha... ni kweli kabisa usemayo. Najua ni kipi unamaanisha. Karibu sana Tanzania kwa mara nyingine, kwenye nchi yako."


Walionekana kuwa marafiki wakubwa sana hawa watu, kwani walionesha furaha kubwa nyusoni mwao na walifurahia mazungumzo hayo.


"Nimekuja Tanzania kwa kazi maalumu. Naamini unaelewa jinsi biashara zetu zilivyoyumba ndani ya utawala wa mwendazake. Sasa baada ya kusikia taarifa kwamba keshatutangulia mbele za haki, kwangu ilikuwa habari njema sana, na niliona ni wakati mzuri tena wa kufufua biashara zetu."


"Ni kweli usemayo, lakini sidhani kama itakuwa rahisi wala jambo la kufanyika haraka haraka, maana linahitaji unganiko sahihi (connection). Unajua nchi yetu imeimarika kiusalama kwa sasa."


"Ndiyo, hilo nalifahamu fika. Na ndio maana nikasema nimekuja kwa kazi hiyo. Mtu ambaye naamini atanisaidia kwenye mpango huo ni wewe. We have to establish our destroyed system once again."


"Nimekusikia na ninaelewa shauku na mipango yako, lakini mimi nakusaidiaje katika hilo?"


"Nafikiri unaelewa — Mister Bruno ndio alikuwa chanzo cha mfumo wetu (system) kufa hapa nchini, mara baada ya mwendazake kuchukua madaraka."


"Ndiyo, nalielewa fika swala hilo."


"Sasa hapo ndio pa kuanzia."


"Vipi, Sam?"


"Come on, Kimbona! Usiniambie siku hizi umekuwa mcha Mungu kiasi cha kupelekea akili yako kushindwa kung'amua swala dogo kama hilo."


"Haha... You mean to kill him?"


"Correct. Na naamini hilo ni swala unaloweza sana na lipo ndani ya uwezo wako. Naujua upande wako mwingine. Ukiutumia vyema tutafanikiwa katika hili. Na nakwambia, mtu wa kwanza kupata faida si mimi tu — ni wewe pia, maana utakuwa kwenye mfumo," aliongea mwanaume huyu anayejulikana kwa jina la Samueli, kwa lugha yake iliyojaa ufasaha.


Bwana Kimbona alijikuta akiwaza na kukuna kichwa. Aliinua uso wake, akamwangalia Sam usoni, kisha aliachia tabasamu.


"Assume it's done from now on. We are back, my friend," aliongea, huku akimfanya Sam afurahi sana. Walipeana mikono na kutakiana siku njema, kisha wakaagana, huku Sam akisisitiza kwamba swala hilo lifanyike mapema iwezekanavyo.


*******


Miongoni mwa watu waliotoka na nyuso zilizojaa tabasamu alikuwa ni kijana Damiani, huku wenzake wengi wakitoka na nyuso zinazoonesha kukata tamaa kwa kile walichokutana nacho.


"Daah! Nimetumia pesa zangu zote kuja hapa, eti leo nimeshindwa kung'amua 'elfu kumi ina mnyama gani'? Hata hawa HR wenyewe wanazingua!" aliongea kijana mmoja aliyekuwa na marafiki zake hapo, akionesha kulalamika. Lilikuwa ni swali ambalo halikuwa la kawaida wala la kutegemewa, hasa kwa nafasi kama hiyo ya Msimamizi wa Fedha. Hakuwa kijana mmoja tu aliyelalamika — wengi walionesha kuchukizwa na aina hiyo ya swali. Kilichowakasirisha zaidi ni kwamba maswali yale magumu yaliwekewa maksi chache.


"Mambo!" Ilisikika sauti moja nyororo sana iliyoamsha hisia kwenye ngoma za masikio ya Damiani, na kumfanya ainuke. Wakati huo alikuwa ameegama ukuta, akitazama upande wa barabara, magari yakipita na watu wakiwa katika hekaheka za siku hiyo.


Alikuwa ni msichana mrembo kweli kweli. Alikuwa mrefu wa wastani, mwenye rangi ambayo kwa haraka haraka ungeona wazi kwamba mlimbwende huyu alikuwa ni mchanganyiko wa mataifa mawili — kama si wa Kihindi basi ni mzungu na Mwafrika, huku baba yake akionekana kuwa mzungu kamili au Mhindi. Alikuwa mvutia kweli, na hasa tabasamu alilokuwa amelitoa usoni mwake lilifanya mashimo yake kwenye mashavu yampambe zaidi uso wake, na kumfanya kijana Damiani abung'ae kidogo.


"Poa, mambo," alijikuta akiitikia kwa aibu kidogo.


"Naitwa Merina. Wewe je?"


"Damiani."


"Ohoo! Na wewe ulikuwepo kwenye mahojiano?"


"Ndiyo."


"Hata mimi pia. Nafurahi kukufahamu, Damiani," aliongea msichana huyo, akionekana mchangamfu — ndiye aliyekuwa akitawala mazungumzo hayo.


"By the way, how was the written?" alimuuliza mwanadada huyo, na kumfanya Damiani atabasamu kidogo kabla ya kujibu.


"Nashukuru Mungu — ilikuwa safi. Na wewe?"


"Mimi pia." Jibu hilo lilimfanya Damiani awaze kidogo — kati ya watu waliofanikiwa kung'amua "elfu kumi ina mnyama gani," basi hata mlimbwende huyu atakuwa amepatia. Swala hilo kidogo lilimnyima raha, kwani aliona nafasi yake inakuwa ndogo. Hata hivyo hakutaka kuonesha hilo wala kukata tamaa.


"Umetoka chuo gani?"


"Harvard."


Jibu hilo lilimfanya Damiani ashangae, kwani alijua duniani chuo kinachotamkika kwa jina hilo kilikuwa ni chuo kikubwa kabisa, na kilikuwepo si Tanzania bali Marekani.


"You mean USA?"


"Yeah!"


Hapo Damiani ndipo alipochoka kidogo moyoni — kwani alijua kama mwanadada huyo alipita maswali yote ya maandishi, basi hata kama yeye pia atapita kwenda mahojiano ya mdomo, asingefua dafu mbele ya bidii huyo. Kwanza chuo peke yake kingemwandalia.


"Congratulations!"


"Thanks! And you?"


"TIA."


"Ooh! Kipo wapi?"


"Tanzania Institute of Accountancy — kipo njia ya Mbagala," aliongea Damiani, huku hata hamu ya kuendelea na mazungumzo ikipotea ghafla, kwani aliamini kwa nafasi hiyo moja iliyokuwa ikipiganiwa na mamia ya wahitimu, hangeipata.


Basi Damiani aliachana na mlimbwende yule, na hilo lilifanyika mara baada ya kutangaziwa kwamba majibu yatatoka kesho. Wale waliofaulu kwenda hatua inayofuata watajulishwa, na kama mpaka saa nne asubuhi hujapata ujumbe wowote au simu kutoka kwao, basi ujue hujapita, nao wanakushukuru kwa kushiriki.


Kwa Damiani, alipoteza tumaini kabisa na aliona ni kama alipoteza pesa zake tu za kuja jijini Dar. Alitamani kuondoka siku hiyo hiyo kurudi Lushoto kwao, lakini alibadili nia. Alisema moyoni mwake — ngoja nishindane na mwanadada yule. Kwani aliamini pia kwamba kumaliza chuo kikubwa peke yake si ushindi — ushindi ni kuwa na uwezo (competence) wa kweli kwa kile unachokijua.


Alirudi Mbagala huku akiwasiliana na mama yake kuhusu siku yake ilivyokwenda. Mama yake aliendelea kumpa nguvu na kumwambia asikate tamaa bali azidi kujipanga. Alirudi Mbagala Zakhemu — bahati nzuri au mbaya, hakumkuta Joshua ndani. Kwa kuwa alikuwa amepewa ufunguo, aliingia na kujipumzisha. Alianza kufikiria matukio yote ya siku hiyo, kuanzia asubuhi mpaka wakati huo. Alijikuta akitabasamu. Kulikuwa na jambo moja lililompa nguvu zaidi — alikuwa ameona wazi kwamba kama Mungu alikuwa na makusudio ya kumpatia ajira wiki hiyo, atapata. Kwani alivyokumbuka yule mtu wa asubuhi aliyemwambia kuhusu "elfu kumi ina mnyama gani," na swali hilo kweli likawepo kwenye mahojiano, aliona ni Mungu mwenyewe aliyejidhihirisha kwake kupitia mtu yule. Kwa hiyo hakuona sababu ya kukata tamaa.


Siku nyingine iliwadia. Kwa Damiani alikuwa na furaha kubwa sana, kwani alikuwa tayari amekwisha kupokea ujumbe kwamba amepita kwenda mahojiano ya mdomo (oral interview). Kwake ilikuwa jambo la baraka kubwa, alimshukuru Mungu, na alijipanga vizuri kwa ajili ya kilichokuwa mbele yake.


Aliaga Joshua, huku akimtakia mafanikio mema. Pia alimpigia simu mama yake mpendwa, kumwambia hatua aliyoifikia, na mama yake akamwambia anamuombea. Alifika barabarani na alibahatika kupata gari mara tu alipofika, lililokuwa likienda stesheni. Alipanda, na ndani ya dakika chache alikuwa chini ya jengo la kampuni hiyo.


Alitembea kando ya barabara kisha alipinda kushoto, akiingia eneo hilo. Wakati huo huo, gari aina ya Audi modeli mpya ya rangi nyeupe ilisimama, na alishuka yule dada mzuri Merina — akionesha alikuwa akiendesha yeye mwenyewe. Alimwona Damiani, na Merina ndiye aliyeita jina lake kwanza, kwani Damiani alikuwa hata hana habari naye.


"Mambo!"


"Poa. Za toka jana?"


"Safi. Hongera!" aliongea Merina na kutabasamu, akionekana hana wasiwasi wowote — hali iliyomfanya Damiani aamini kwamba mdada huyo alikuwa na uhakika wa kupata nafasi hiyo.


Waliongozana na kupewa maelekezo, kisha kidogo baadaye mahojiano yalianza. Siku hiyo walikuwa wanne tu ndani hapo. Aliingia Merina kwanza — ndani ya dakika kumi na tano alitoka. Aliingia mwingine. Kisha akaingia Damiani. Aliulizwa maswali kadhaa na akajibu kwa ufasaha kadri anavyoweza, kisha akamalizia mahojiano yake.
 
03
Baada ya Damiani kumaliza mahojiano, alitoka huku akiwa amepewa maelekezo kwamba majibu yatatoka siku kumi zijazo — awe amepata kazi au hakupata.


Alitoka moja kwa moja na kuondoka eneo hilo. Alipanga siku hiyo hiyo kuondoka kuelekea Tanga, maana muda uliruhusu.


Saa sita kamili alikuwa ndani ya basi la Morning Nice akielekea Lushoto. Alikuwa na nusu tumaini la kupata ajira. Kwani kila alipomkumbuka yule dada, aliona wazi kwamba kumshinda mtu aliyetoka katika moja ya vyuo vikubwa duniani ilikuwa vigumu. Ndio maana alikuwa na nusu tumaini tu — ingawa pia alijua alikuwa amejibu vizuri maswali yote aliyoulizwa. Hata hivyo, alijua mfumo wa Tanzania uliangalia sana aliyetoka chuo gani.


Saa moja kamili ndio muda alioingia Lushoto mjini. Alishuka kisha alijisogeza mpaka kwenye moja ya magari ya Noah yaliyokuwa yakielekea kijijini kwao. Bahati nzuri, yalikuwepo. Alipanda na kusubiri abiria wachache wajae, hatimaye walifanikiwa kuondoka kuelekea kijiji chao cha Mkuzi.


Japo alikuwa na mawazo mengi, picha ya yule mwanadada ilikuwa mara kwa mara ikimjia akilini. Kuna wakati alijisemea moyoni: "Kama ingekuwa ni rafiki yangu Elvis mpenda warembo, hata mahojiano asingetaka kuyafanya — angejali zaidi kumtongoza yule mwanamke." Maana kila alipomkumbuka, alimaliza kutabasamu na kukiri kwamba alikuwa mrembo wa kipekee — mrembo ambaye hakuwa katika kiwango chake.


Alikuja kushituka kutoka kwa mawazo yake mara baada ya gari kufika Mkuzi na kondakta kumshitua. Aliangalia nje — ndiyo, hii ilikuwa sehemu yake. Alimtaarifu kondakta na mara baada ya kufika eneo husika alishuka, akaanza kuporomoka kwenye kijipande cha mlima kuelekea kijijini kwao. Kijiji cha Mkuzi kilikuwa na umeme kila kona, na kilikuwa kimechangamka. Hata baada tu ya kushuka, alionekana na baadhi ya watu waliomfahamu, waliomsalimu. Watoto pia walimkimbia na kumchukua mizigo hadi nyumbani.


********


Ilikuwa ni siku kadhaa tangu Rais wa Tanzania apoteze maisha. Raia wengi wa Tanzania walikuwa katika maombolezo ya siku ishirini na moja. Japo kiongozi huyo alikuwa amezikwa, Watanzania wengi waliomupenda walikuwa wakimlia, na hilo lilikuwa ni kutokana na upendo mkubwa waliokuwa nao kwa Rais huyo.


Naam! Bendera Onyango ndiye Rais wa awamu ya nane ndani ya taifa la Tanzania. Alikuwa ni mmoja wa marais waliokuwa na msimamo imara sana katika uongozi wake, na kupitia hilo alipendwa sana na kundi kubwa la Watanzania, huku kundi lingine likiwa halimpendi — na hilo ni kawaida sana katika siasa. Licha ya kutopendwa na kundi dogo la watu, alikuwa Rais aliyejitahidi sana kutekeleza majukumu yake, hususani yale aliyoyaahidi katika kampeni zake. Makamu wake alikuwa bwana Henri Mushi.


Hakika bwana Onyango alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha atimiza kila aliyoahidi — hususani katika maswala ya miundombinu. Msimamo wake katika kusimamia ukusanyaji kodi wa raia ulimpa wafuasi wengi. Lakini hata hivyo, walikuwepo waliomchukia kwa sababu zao — ziwe za msingi au la. Kwa kuwa binadamu hakuwa mkamilifu na alikuwa na udhaifu wake, hata bwana Bendera alikuwa miongoni mwa binadamu hao wasiokuwa wakamilifu.


Miongoni mwa mambo ambayo bwana Onyango alifanikiwa kuyakomesha ndani ya utawala wake, moja ilikuwa ni swala la madawa ya kulevya nchini. Alijitahidi kwa kushirikiana na wasaidizi wake na polisi kuhakikisha anaziba njia zote za uingizaji wa madawa ya kulevya hapa nchini, na vile vile madawa kupitishwa nchini. Kwa asilimia kubwa, hilo lilifanikiwa. Lakini mwanzo wa kufanikiwa kwa jambo hilo ulikuwa pia mwanzo wa kujitengenezea maadui — hao wafanya biashara wa madawa.


Moja ya wafanya biashara hao alikuwa ni bwana Bruno Lamberk. Huyu alikuwa ni mzungu aliyekuwa ndani ya nchi ya Tanzania kwa muda wa miaka ishirini, na alikuwa mmoja wa wawekezaji wakongwe ndani ya taifa hilo. Licha ya biashara zake za halali, alikuwa pia muuzaji wa madawa ya kulevya ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki — kwa kifupi, yeye ndiye alikuwa bosi mkubwa katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.


Bwana huyu haikujulikana kama alikuwa na familia — kwani katika maisha yake hakuwahi kuishi na mwanamke zaidi ya wale waliokuja kwa starehe tu na kuondoka. Mara baada ya Rais Bendera kuingia madarakani, hakikujulikana mbinu gani aliyotumia kumnasa bwana Bruno, hadi kupelekea Bruno kutoa ushirikiano na kuwasaliti wauza madawa wenzake. Biashara hiyo Tanzania ilifungwa kabisa, na wauza madawa maarufu wakakimbia nje ya nchi. Mmoja wa waliokimbia alikuwa ni bwana Samuel Saitoto, pia anayejulikana kama "Rich Sam." Huyu alikuwa muuzaji wa madawa mkubwa sana ndani ya mtandao wa bwana Bruno, na baada ya kusalitiwa na rafiki yake, aliamua kukimbia Mexico pamoja na familia yake.


Basi habari ya kifo cha Rais Bendera ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa bwana Bruno, kwani Rais huyo ndiye aliyekuwa akimpa ulinzi mkubwa dhidi ya maadui zake. Ilikuwa siku ya ishirini sasa tangu kuzikwa kwa Rais Bendera. Bwana Bruno alikuwa amejificha ndani ya jiji la Tanga, wilayani Lushoto.


"Mkuu, nimefanikiwa kuongea naye. Anaonekana ni kijana shupavu — kama atapewa mafunzo maalumu, atafaa kabisa," aliongea bwana mmoja — yule tuliyemwona ndani ya jiji la Dar es Salaam, aliyempa lifti kijana Damiani. Siku hiyo bwana huyo alikuwa ndani ya wilaya hiyo, na walioonekana walikuwa wakizungumza mambo kadhaa.


"Good. Nimempenda yule kijana. Piga juu, piga chini — lazima tumuingize kwenye mfumo. Kwa hiyo endelea kumwangalia. Muda si mrefu tutatekeleza mpango. Maadui wangu wananifuatilia. Bendera amekufa. Hakuna anayeweza kunilinda sasa," aliongea huku akimaanisha kwamba muda mfupi ujao watatekeleza mpango wao, kwani Bendera amekufa na hakuna wa kumkinga.


"Inabidi uondoke ndani ya nchi hii."


"Siwezi, Danny. Nitafia hapa hapa Tanzania."


"Lakini ni hatari sana."


"Najua. Na ndio maana nakwambia endelea kumfuatilia Damiani — tunahitaji kumwandaa mapema."


*******


Kimbona, kama alivyoahidiana na Sam kuhusu kumtafuta Bruno na kumpotezea mbali mzungu huyo, hakutaka kabisa swala hilo lifeli. Alikuwa na nia ya kweli ya kulitekeleza — hasa kila alipokumbuka kiasi gani alikipoteza mara baada ya Bruno Lamberk kuwasaliti kwenye mtandao wao. Ilikumuuma sana. Hasara yake ya pesa ilimpa nguvu ya kukamilisha jambo hilo.


Haikuwa vigumu kwake, kwani ni kama alikuwa amepumzika tu katika biashara hiyo. Watu wake (genge lake) walikuwepo ndani ya nchi hiyo, naye alikuwa akiwalipa kwa siri — kwani aliamini siku moja atarudi kwenye uwanja na kuendelea na biashara hiyo. Kwake, baada ya kifo cha ghafla cha Rais Bendera, aliona hiyo kama fursa nyingine ya kurudi kwa kishindo katika biashara ya uuzaji wa madawa ya kulevya.


"Derick, hakikisha unawapanga vijana mkutano wa kazi. Taarifa zilizopo kwa sasa kutoka kwa chanzo chetu ndani ya TISS ni kwamba bwana Bruno amejificha ndani ya wilaya ya Lushoto — Mambo View Hotel."


"Sawa, mkuu. Vijana kwa sasa wako tayari na wanasubiri maelekezo yako tu."


"Basi safi. Pumzika kwa leo, na kesho nitakuambia nini cha kufanya. Hakikisha swala hili linafanyika kwa weledi mkubwa — hakuna kufeli."


"Sawa, boss," alisema huku akitoka.


"Hahahaha... hii ni fursa nyingine kabisa kwangu. Naenda kurudi kwenye uwanja muda si mrefu. Bruno... Brunooooo... ama zako ama zangu," aliongea tajiri Kimbona kwa kicheko cha dharau, huku akisip wine yake ya Black and White.


Siku iliyofuata, Derick alipokea simu kutoka kwa bosi wake, akimtaarifu kufika kwenye kampuni ndani ya jengo la LAPF Tower — kampuni iliyojulikana kwa jina la KILAC (Kimbona International Link and Companies).


Derick hakuchukua muda mrefu kufika ndani ya jengo hilo la LAPF. Alifika moja kwa moja, aliripoti kwa katibu na aliruhusiwa kuingia. Alisalimiana na bosi wake kisha alipewa ramani nzima ya jinsi ya kutekeleza tukio hilo.


"Kuweni makini. Danny huyu ni jasusi wa kimataifa na ana mbinu nyingi za kuwazidi. Lakini nanyi pia mna mbinu nyingi za kumzidi akili. Narudia tena — swala hili halina kufeli. Hakikisheni mnalimaliza baada ya siku kumi zijazo."


"Sawa, boss."


Derick alitoka ofisini hapo na bila kupoteza muda, aliwashitua genge lake la kimafianá kuwapa ramani ya mahali pa kukutana ili waweze kuelekea Lushoto.


********


Baada ya siku kumi kupita, kijana Damiani alikuwa bado hajapokelea ujumbe wowote kutoka kwa kampuni aliyofanya nayo mahojiano. Japo mama yake alimtia moyo asikate tamaa, kwa upande wake — akiunganisha na yale aliyoyajua mwenyewe — hakuona nafasi kabisa ya kushinda kazi ile. Alimwangalia mama yake aliyevaa nguo zilizochakaa na zisizovutia, akamhurumia sana. Alitamani amtoe mama yake katika dimbwi hilo la umasikini kadri ya uwezo wake. Kwa kifupi, alimpenda mama yake sana. Kila alipokumbuka misongo mama yake aliyopitia kwa ajili ya kuhakikisha anasoma, ilimwuma zaidi. Aliilaumu serikali sana kwa kutokuwa na mfumo mzuri wa kuwapatia ajira wahitimu. Kwani wahitimu walijitolea kusoma kwa bidii, na wazazi walisomesha watoto wao kwa juhudi zote — lakini mwisho wa siku, wakimaliza, hakuna ajira. Ilikuwa ni swala la kukatisha tamaa sana, kwa wazazi na kwa wahitimu wenyewe.


Siku hiyo Damiani aliamua kukaa nyumbani na mama yake tu. Mama yake naye siku hiyo alikuwa na maumivu ya kichwa, hivyo hakuweza kwenda kwenye vibarua vyake ambavyo vilimwezesha kupata kitu cha kuleta nyumbani.


Basi siku hiyo Damiani alikuwa akitengeneza banda lao la mbuzi uwanjani, huku mara kwa mara akiangalia barua pepe yake au kusubiri simu. Alikuwa na shauku kubwa ya kujua kama amepita au la. Saa la kwanza likapita. La pili nalo likapita. La tatu. Hatimaye la nne. Mpaka saa kumi na moja hakukuwa na ujumbe wala simu yoyote.


Aliweka simu chini huku akiona wazi kwamba hakukuwa na tumaini lolote lililobaki. Hakuona sababu ya kukaa nyumbani — alimuaga mama yake kwa kumwambia anarudi muda si mrefu, anaenda kwenye shamba lao la miti kuchukua miti kidogo ili amalizie banda lao la mbuzi. Maana hakupenda kabisa kulala mbuzi hao nyumba moja — mikojo yao ilikuwa na harufu kali sana.


Alitembea kwa muda wa nusu saa hivi, akapita kijijini kwao. Siku hiyo watu wengi walionekana barabarani, kwani kulikuwa na sherehe kwenye kanisa moja la Kirumi. Watoto walikuwepo, na hata baadhi ya mama pia. Ni mama yake peke yake na baadhi ya wanakijiji — hasa wazee waliokuwa hawawezi kutembea — waliokuwa majumbani. Alitembea huku akila tofaa (apple), kwani kijiji chao kilikuwa na kilimo cha matunda — tofaa, matunda ya damu, peasi, na hata mananasi.


Baada ya dakika arobaini na tano hivi, aliingia kwenye shamba lao kubwa la miti ya biashara. Hakutaka kuchelewa — mara alipofika alianza kutafuta mikalitusi iliyonyooka na kuikata. Wakati akiendelea na kazi hiyo, simu yake ilitoa mlio — ujumbe umeingia. Aliendelea kukata miti kwanza — kama ishirini — na aliridhika kwamba inatosha. Ndipo alipotoa simu yake kuangalia ni ujumbe gani.


"HONGERA BWANA DAMIANI RABANI! UMEFANIKIWA KUPITA KWENYE MAHOJIANO ULIYOFANYA. UNAPASWA KURIPOTI KAZINI MAPEMA KABLA YA TAREHE ILIYOTAJWA."


Ulikuwa ni ujumbe uliomtoa machozi bwana Damiani. Ndiyo — yalikuwa ni machozi ya furaha. Alijikuta akirukaruka kwa furaha. Hata ile kazi ya kukata miti iliishia hapo. Jambo moja tu alilolifikiri wakati huo ni kurudi nyumbani haraka na kumuonesha mama yake ili wafurahie pamoja. Muda ulikuwa umeendelea na giza limeanza kuingia. Alipanga miti yake haraka haraka, huku akipiga mluzi wa furaha — hata yeye mwenyewe hakujua ni wimbo gani ulikuwa ukiimbwa.


Lakini wakati hayo yakiendelea, ghafla alisikia kishindo kikubwa upande wa kushoto — kitu kilichoanguka. Lahaula! Alikuwa mtu — mwenye ngozi nyeupe — aliyedondoka, akionekana anavuja damu nyingi usoni na ubavuni. Damiani alipigwa na woga, na akili yake yote ilimwambia akimbie wakati huo huo. Lakini alishuhudia mtu yule akimpungia mkono kwa shida — kama anaomba msaada.


Damiani aliangalia kulia na kushoto kuona kama kuna mtu anakuja. Akili yake ilicheza na kufanya kazi kama mashine wakati huo, na alihisi wazi kwamba mtu yule alikuwa anawindwa au anakimbizwa. Alimsogelea kwa tahadhari.


"Help me to get out of here — they will kill me. Please, help me," aliongea, na kweli alikuwa mzungu — kama Damiani hisia zake zilivyomwambia. Damiani hakutaka kujishauri sana, kwani aliona wazi mtu huyo alihitaji msaada. Lakini alifikiri ni msaada gani angeweza kumpa. Alichofanya ni kurudi pale alipoacha miti yake, akaisukumia kichakani ili isinonekane, kisha alirudi kwa yule mtu na kumubeba begani mwake.


Mzungu yule aliinua uso wake polepole.


"Shika hii — just in case tusipofanikiwa. Kimbia uniache." Ilikuwa ni bahasha iliyofunikwa kwa mfuko wa plastiki.


Damiani alipokea bahasha hiyo huku akiwa hajui mzee yule alikuwa akimaanisha nini. Lakini kwa kuwa wakati huo alichokuwa akifikiri ni kumuokoa tu, alijitahidi kadri ya uwezo wake kumtoa msituni na kumfikisha nyumbani kwao — kwani aliamini hapo ndio ingekuwa sehemu salama. Angehisi anafanya nini baadaye.


Uzuri ni kwamba giza lilikuwa limetamalaki, hivyo kwa kupita njia za vichaka aliweza kupita bila kuonekana kwa urahisi. Pia kwa kuwa watu wengi walikuwa kwenye sherehe, alitembea na kufanikiwa kutoka msituni. Hatimaye aliingia ndani ya kijiji chao. Alionekana na bibi mmoja tu aliyekuwa hawezi kutembea vizuri — bibi huyo pia alikuwa na mdomo uliopotoka kwa upande mmoja. Kwa habari za kijijini, ilikuwa adhabu aliyoipata kwa sababu ya ushirikina wake.


Alimpitisha mzungu yule hadi nyumbani kwao. Mama yake alipigwa na mshangao karibu apige kelele — lakini Damiani alimzuia na kumwambia kwamba mtu huyo anahitaji msaada, alimkuta msituni. Mama yake alifungua mlango na walimuingiza ndani, wakamlaza kwenye kipande cha mkeka. Wakati huo mzungu huyo alikuwa hana fahamu — labda kutokana na kupoteza damu nyingi.


"Mama, inabidi tumuite mzee Kivinje — anaweza kumsaidia, huku mimi nikifanya taratibu za kupata usafiri wa kumpeleka hospitalini." (Mzee Kivinje alikuwa mganga wa mitishamba na dawa za asili.)


"Kwa nini usimpeleke moja kwa moja? Akitufia hapa si itakuwa kesi?"


"Hapana, mama. Hali yake inaonesha anawindwa, na inatupasa kumsaidia kwanza na kufanya mambo kwa umakini," aliongea Damiani kwa ujasiri, kisha alitoka na kwenda kwa Kivinje — daktari wa mitishamba na mganga wa kienyeji.


Haikuwa mbali sana. Kutokana na mwendo wake wa haraka, alifanikiwa kumkuta bwana Kivinje akiwa nje, akishikilia kikombe — alionekana akinywa maziwa ya mbuzi. Damiani alieleza shida yake, na Kivinje alishitushwa sana. Hakutaka kupoteza muda — aliingia ndani, akatoa zana zake za kazi, na wakaongozana na Damiani.


Haikuwachukua muda mrefu. Walifika, na Kivinje alihitaji Damiani amwonyeshe mgonjwa alipo. Lakini hapo ndipo Damiani alipokutana na jambo ambalo hakukutarajia kabisa.


Alimwona mama yake akilala kwenye dimbwi la damu. Huku mwili wa yule mzungu nao ukiwa kwenye dimbwi la damu. Alitaka kutamka neno moja tu — "Mama" — lakini sauti haikutoka.
 
04
Damiani alijikuta akijikaza na kumkimbilia mama yake pale alipo, wala hakujali zile damu.


"Mamaaa! Mama, amka — nini kimetokea mama yangu? Mamaaaa! Mama amka!" Mama yake Damiani alikuwa akitapatapa, na hatimaye aliinyosha mkono kuelekea mlangoni — hapo hapo akakata roho. Ilikuwa ni huzuni kubwa kwake. Alilia na kuutingisha mwili wa mama yake ili aamke, lakini haikuwezekana kabisa. Kivinje ndiye aliyemsogeleea na kumshikilia aendelee.


"Mama, mama wee! Mama amka — mimi mwanao, unaniacha na nani? Mama yangu, bado sijapata nafasi ya kukutoa kwenye umasikini. Mama yangu wee! Amka, mama — nimefanikiwa kupata ajira, sijakuambia bado! Mama amka, mama weeee..."


Ilikuwa ni huzuni iliyosimamisha moyo. Mama yake alikuwa ameuawa kikatili sana. Watu tayari walikuwa wamejaa eneo hilo kwani walisikia vilio hivyo. Kila mtu aliyemjua mama huyo, mara alipojulishwa na Kivinje kwamba mama wa Damiani amefariki, aliungana na kilio hicho.


Watu waliendelea kulia. Damiani mwenyewe alikuwa amezimia wakati huo.


Chapaa ilisikika ikitua eneo la karibu ndani ya kijiji hicho, na mwili wa yule Bruno ukichukuliwa kupelekwa upande chapaa ilipokuwepo. Polisi nao walikuwa eneo la tukio. Ilikuwa ni tukio la kusikitisha, na kila mtu alikuwa akiongea lake. Wakati hayo yote yanaendelea, vijana wa Kimbona walionekana hapo — Derick mwenyewe akiwa amesimama upande wa juu kidogo kuepuka watu wawaone. Mara baada ya kuona mwili wa Bruno ukitolewa, waliondoka eneo hilo.


*******


"Hahaha! Hahahah! Safi sana Derick — kazi nzuri, vijana wangu," aliongea Kimbona, uso wake ukijaa furaha ya ushindi, baada ya kusikia kwamba Bruno amepigwa risasi na amekwisha kufa.


Hakutaka kuchelewa. Alinyanyua simu yake na kumpigia Sam, akimpa taarifa hizo. Sam alizipokea kwa furaha kubwa sana, akamshukuru sana Kimbona, na kumualika kwamba siku hiyo hiyo aende Serena Hotel — kulikuwa na watu anaotaka wakutane nao.


Bila kusita, mzee huyo aliitikia wito huo — alikuwa atakuwepo eneo hilo bila kukosa. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Kimbona. Katika hatua hiyo ya kwanza ya kurudi kwenye biashara yake, aliona wazi kwamba safari yake inaelekea mafanikio makubwa.


Ilivyofika saa nne usiku, Kimbona alimuaga mkewe na familia yake kwa ujumla, kisha alitoka na mlinzi wake kuelekea kwenye miadi yake kama alivyoelekezwa na Samuel. Kwa kuwa ni usiku, gari halikukawia kufika ndani ya hoteli hiyo ya hadhi ya juu ndani ya jiji la Dar es Salaam.


Alifika mpaka mapokezi na kujitambulisha. Ni kama ujio wake ulikuwa umetegemewa — aliongozwa mara moja mpaka kwenye lifti na dada mmoja mrembo sana aliyekuja eneo hilo kumchukua. Lifti ilipanda hadi kwenye ghorofa iliyokuwa na vyumba vya VVIP — yaani sehemu ambayo ilikuwa ikiingiwa na watu wa hadhi ya juu sana ndani ya jiji hilo. Alitabasamu — muda kidogo kuingia sehemu zilizokuwa na ulinzi mkali kama aliouona hapo ndani.


Yule dada mrefu mrembo, aliyevalia suti ya rangi ya zambarau na viatu vya visigino virefu (high heels), alitembea hadi kufika kwenye moja ya vyumba, kisha akafungua mlango na kumkaribisha bwana Kimbona. Kimbona alijikuta akishangaa — watu waliokuwepo hapo ndani, hakuwatarajia kabisa.


"Mheshimiwa..." alijikuta akisema kwa mshtuko, kwani aliyekuwa mbele yake alikuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya saba, bwana Athumani Ndalu. Upande wa kulia alikuwepo Waziri wa Mambo ya Ndani, bwana Musiba. Mbele yake alikuwepo Samueli. Walikuwa jumla ya wanne — yeye akijumuishwa — lakini kiti kimoja kilionekana hakikuwa na mtu.


"Hongera sana, bwana Kimbona, kwa ushindi wa leo," aliongea Rais Mstaafu.


"Asante sana, mheshimiwa. Unajua hii ni mara yangu ya kwanza kukuona uso kwa uso — ni heshima kubwa sana."


"Hahahaha! Kimbona, huu ni mwanzo tu. Na sasa unakwenda kukutana na mtu mkubwa zaidi — na pengine wakubwa zaidi. Karibu kwenye U-97!" aliongea Sam kwa sauti ya majivuno.


"U-97?" aliongea Kimbona, akimwangalia Sam. Lakini hapo hapo mlango ulifunguliwa, na hapo ndipo Kimbona aliposhangaa zaidi — kwani mtu aliyeingia mahali hapo hakumtarajia kabisa.


"Mheshimiwa Rais!!!" alijisemea moyoni kwa mshangao.


*******


Watu walikuwa wakizungumza hili na lile ndani ya kijiji hicho, na habari zilitapakaa kila kona. Kila mtu alikuwa akizungumza swala la mama Damiani kupigwa risasi na watu wasiojulikana, na pia mzungu kupigwa risasi ndani ya nyumba hiyo hiyo. Hata chapaa kuja kumchukua mzungu — kila kitu kilizungumzwa. Watu hawakulala. Lakini pia kulikuwa na wale waliokuwa katika majonzi ya kweli ya kupoteza maisha ya mama Damiani, kwa kifo kilichokuwa cha kikatili sana. Watu walilaani vikali kilichotokea.


Damiani alikuja kupata fahamu saa moja baadaye, akijikuta amelazwa ndani ya zahanati. Ni kama akili zake hazikuwa sawa wakati wa kuzinduka. Daktari na wauguzi walimuona akizinduka, nyuso zao zikiwa za majonzi na huruma kwa kijana huyo — kwani waliona ni mambo magumu na mazito ambayo alikuwa anakwenda kupambana nayo katika maisha yake.


Ni kama mkanda wa filamu ulikuwa ukipita ndani ya kichwa chake — picha ya kumuona mama yake akilala kwenye dimbwi la damu zilianza kupita mara moja baada ya nyingine.


Alijikuta akitoa ukelele uliowafanya madaktari wamsogeleee haraka na kumtuliza. Hawakuwa na njia nyingine — ilibidi wamchome tena sindano ya usingizi, ambayo ilifanya kazi yake hadi siku nyingine.


Ilikuwa asubuhi iliyofuata ambapo habari za mauaji hayo — majambazi kumuua mama Damiani na mzungu — zilisambaa Lushoto nzima na kwenye vyombo vya habari. Jeshi la polisi lilithibitisha kwamba wahusika wa mauaji hayo walikuwa ni majambazi yaliyokuwa na makazi yake katika msitu wa Mlola, huku wakihusisha tukio hilo na uvamizi wa zamani kwenye chuo kikuu cha Sebastiani Koroa Memorial University (SEKOMU). Waliahidi uchunguzi utaendelea hadi kuwatia hatiani wahusika wote.


Upande wa Damiani, alifumbua macho asubuhi akiwa na akili zake zote. Roho yake ilimuuma mno pale alipokumbuka kwamba sasa duniani amebaki peke yake — yatima. Alijilaumu sana kwa kumsaidia mzungu yule, kwani aliona kama angemuacha pale pale msituni, huenda yote hayo yasingemkuta mama yake. Alijilaumu na kuhuzunishwa na moyo wake. Lakini hakuwa na la kufanya wakati huo — ilibidi aruhusiwe ili akashuhudie mazishi ya mama yake. Watu walimhurumia sana na kumpa pole. Alizipokea huku akijitahidi kujikaza kiume.


Taratibu zote za mazishi zilikuwa zimekwisha kufanywa na serikali, akiwemo Mkuu wa Wilaya aliyehudhuria mazishi hayo.


Padri alifanya sala fupi na kuruhusu watu waage mwili — akiwemo Damiani, aliyelia sana baada ya kumuona mama yake akilala kwenye jeneza. Alitolewa na wengine, watu wakipewa nafasi zao, na hatimaye mwili ulipelekwa makaburini.


"SARAH RABANI — ALIZALIWA MWAKA 1979, ALIFARIKI MWAKA 2019, AKIWA NA MIAKA 40. AMEACHA MTOTO MMOJA."


Wosia mfupi ulisomwa, na hapo mwili ukapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.


*******


Maisha mapya ya kijana Damiani yalianza — maisha ya huzuni, kwani alikuwa amemzoea mama yake sana, na sasa hakuwepo tena duniani. Kwake aliona kama ndoto — asubuhi ataamka na kumkuta mama yake. Lakini haikuwa ndoto tena. Ulikuwa uhalisia, na mama yake hakuwepo tena. Kila alipokumbuka ahadi alizojiwekea za kumtoa mama yake katika umasikini, alijikuta akizidi kuhuzunika.


Wiki moja ilipita. Siku hiyo aliamka asubuhi na mawazo mapya — aliona wazi kwamba yaliyotokea yamekwisha kutokea, na sasa alitakiwa kujikaza kama mwanaume na kuruhusu maisha yaendelee. Lakini siku hiyo pia alikumbuka tukio la yule mzungu kumpa bahasha iliyofungwa kwa plastiki. Alifikicha kichwa, na hapo hapo alikumbuka sehemu aliyoiweka — ilikuwa nje kwenye banda la mbuzi, kwenye dari la nyasi. Anakumbuka ndipo alipoweka siku ile kabla ya kwenda kumuita mzee Kivinje.


Alitoka nje na kusogelea banda hilo. Aliingiza mkono sehemu aliyoamini aliweka — lakini hakuipata. Alijaribu tena, bado hakuona. Alijikuta akitafuta hadi kukata tamaa. Akailalia dari hiyo kwa macho, akiangalia chini — na hapo aliona kitu kimoja kwenye kinyesi cha mbuzi: plastiki kama ile ile. Alikurupuka na kukimbia upande wa nyuma wa banda hilo, akishika ile plastiki na kuivuta — na kweli, ilikuwa yenyewe. Alitabasamu kidogo na kuifuta uchafu, na bahati nzuri ilikuwa imehifadhiwa vizuri ndani ya mfuko wa plastiki — hivyo ilichafuka nje tu.


Alisogea ndani ya nyumba na kisha akaitoa kwa makini bahasha ile. Alitoa karatasi nne kwa haraka na kuanza kuzipitia, moja baada ya nyingine.


Ya kwanza ilisomeka: "BRUNO LAMBERK — BORN 1947." Hapo alitambua — mzungu yule alikuwa akiitwa Bruno Lamberk.


Chini ilikuwa orodha ya mali anazomiliki bwana Bruno — ilikuwa ni mali nyingi. Mashamba, nyumba, na nambari za akaunti za benki ya Uswisi ambayo Damiani hakuitambua.


Alipitia karatasi ya pili — ilikuwa ni ramani ya Tanzania, ndani yake kulikuwa na sehemu zilizochorwa kwa alama nyekundu, kama zikionesha maeneo husika. Hakutaka kuiangalia sana kwa wakati huo, akaitupa pembeni.


Karatasi ya tatu ilikuwa na akaunti za benki ya CRDB — lakini jina halikuwa la Bruno. Iliandikwa: "Seline Amber." Akaitupa pembeni.


Ya mwisho ilikuwa na majina mengi — karibu tisini. Hakutaka kujisumbua nayo kwa wakati huo.


Alifungua kimkebe kilichokuwa ndani ya bahasha hiyo. Ndani kulikuwa na vitu viwili — flash disk, na mkufu wenye kidani kilichoumbwa kwa muundo wa msalaba, lakini wenye tofauti kidogo na msalaba wa kawaida. Aliachana na mkufu huo kwa sasa, na kuhamia kwenye flash disk. Alijua kulikuwa na kitu muhimu ndani yake.


Alikumbuka alikuwa na laptop — aliifuata kwenye begi lake, akaitoa na kuiwasha. Alisubiri Windows iload, ikakubali. Bila kupoteza muda, aliingiza nenosiri lake na kisha akachomeka ile flash disk.
 
05
Bwana Kimbona hakuamini kwamba mtu aliyekuwa mbele yake alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, aliyeapishwa juzi kuwa Rais.


"Karibu sana, Mheshimiwa," aliongea Sam na kumkaribisha Bwana Henry Mushi ndani ya eneo hilo. Bwana huyo mwenye mwili wa wastani kidogo, kitambi kikionekana kwa mbali, alisogea mpaka kwenye nafasi yake na kukaa.


"Asanteni, mnaweza kukaa," aliongea. Kila mtu alikaa, na hapo hapo Rais huyo hakutaka kupoteza muda.


"Jamani, kwanza niwashukuru wote kwa kuitika wito wa kufika kwenye kikao chetu. Wapo wengi ambao walipaswa kuwepo katika kikao hiki, lakini ninyi mliopo hapa mkijua kwamba nyie ndio mpo ngazi za juu," aliongea Samueli.


"Dhumuni la kikao hiki: kwanza ni kufurahia suala la Bendera kupoteza maisha. Huu ni zaidi ya ushindi, kwani katika mfumo wetu hakuna aliyewahi kumpenda huyu bwana, na sasa ameondoka — ni suala la kujipongeza na kushukuru waliotujalia. Suala la pili ni juu ya kifo cha Bwana Bruno, ambaye naamini wote tuliokuwepo hapa tunajua ameshapoteza maisha — jambo ambalo ni haki yake kwa dhambi yake ya kutusaliti. Hili ni mpongezi kwa Kimbona, na kupitia hili amepanda nafasi nne katika umoja wetu. Hayo ni maagizo ya Mkuu wetu, Ukanda wa Afrika," aliongea Kimbona. Hapo kila mmoja aliinua glasi yake ya divai na kugonga cheers kufurahia jambo lao.


"Jambo kubwa zaidi ya yote ni juu ya biashara yetu. Nadhani kila mmoja anaelewa ni kwa jinsi gani tumekwama katika biashara hii katika miaka mitano iliyopita ya Mwenda Zake. Hivyo, kwa kuwa neema ipo mikononi mwetu, basi ni muda wa kufufua mtandao wetu ndani ya nchi hii."


"Ni kweli kabisa, Bwana Sam, suala hilo — lakini si kirahisi kama unavyoona," aliongea Mheshimiwa Rais.


"Naelewa, Bwana Henry, na ndio maana leo hii wewe ni Rais. Kupitia wewe, kila kitu hakitakuwa na ugumu wa aina yoyote — ni suala la kimkakati tu. Isitoshe, si wewe tu utakayenufaika, bali pia wananchi watanufaika, kwani miradi yote iliyoanzishwa na Mwenda Zake tutaikamilisha. Biashara yetu itaendelea, nawe utaimarika kisiasa."


"Ni sawa unachosema, Bwana Sam Balozi, lakini suala hili ili kufanikiwa na biashara yetu kuneemeka na hatimaye kutuingizia faida, lazima tuwe na mpango imara na wa kuaminika," aliongea Mstaafu Rais Bwana Ndalu.


"Suala hili lipo kwenye mpango, na kila jambo linaloendea ndani ya nchi hii limeratibiwa na wakubwa. Kwa hiyo, hata kifo cha Mwenda Zake, huwezi kujua — labda lilikuwa ni mpango pia wa U-97." Wote walishituka, lakini Sam alitabasamu.


"Mpango uliopo kwa sasa ni kutakiwa kufumua mfumo wa kiuongozi. Hii inamaanisha kuanzia Mkuu wa TSS, Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Mambo ya Nje, na Waziri wa Katiba na Sheria. Watu wote watakaokaim hizo nafasi — faili lao litakuja ofisini kwako, Mheshimiwa Rais. Suala la pili ni kuhakikisha vibaraka wote wa Mwenda Zake wanakuwa neutralized kwenye mfumo wa kiserikali. Tatu ni kuhakikisha biashara za Bwana Bruno zote zinaingia kwenye mikono ya U-97."


"Biashara hizi za Bwana Bruno — suala hili tutafanikiwa vipi? Tunaweza kupata baadhi ya mali zake, lakini si pesa zake, kwani mpaka sasa haijaeleweka Bwana huyu ni wapi anahifadhi pesa zake. Hata nyaraka zake hazijulikani mpaka leo."


"Kimbona, hili lipo juu yako. Utafuatilia watu wote wa karibu wa Bwana Bruno, na kuhakikisha unapata nyaraka hizo."


"Sawa, Sam, nitalifanyia kazi."


"Vizuri. Mwisho kabisa, natangaza nafasi kama nilivyopewa maagizo na Level 01."


"Bwana Kimbona amepanda kutoka Level 73 hadi Level Unity 45. Bwana Henry, Mheshimiwa, amepanda hadi Level Unity 33. Mheshimiwa Mstaafu amepanda hadi Level 32. Mheshimiwa wa Mambo ya Ndani amepanda hadi Level 34. Ni hayo tu," aliongea Sam. Kisha kikao kilifungwa.


* * * * *


Upande wa mashariki, alionekana mwanamke Merina akiwa juu kabisa ya balcony akifurahia upepo wa bahari. Alikuwa amevalia shati refu la mikono mirefu la rangi nyeupe, na alionekana wazi hakuwa amevaa kitu kingine ndani. Mkononi alikuwa ameshikilia cocktail, na alionekana kuzama katika mawazo.


"Damiani, where are you? I am going crazy thinking of you," alisema kimya kimya — akimaanisha: Damiani, uko wapi? Nakuwa mwendawazimu kukuwaza.


Mrembo huyu hakuwa muombaji wa kazi katika kampuni ya Damiani aliyofanya mahojiano. Alikuwa ndiye Chief Executive Officer (CEO) wa kampuni hiyo. Siku ya kwanza aliyomwona kijana Damiani ilikuwa ni siku ya mtihani wa maandishi. Hapo ndipo mrembo huyu alivutiwa sana na kijana Damiani, na hata wakati walipomaliza mahojiano, alitamani sana kuongea japo kidogo na kijana huyo.


Kwa hiyo, yote aliyomwambia kwamba alikuwa naye mahali hapo kwa sababu ya kutafuta kazi ilikuwa ni uongo tu wa kumpumbaza Damiani, aamini kwamba mrembo huyo naye alikuwa akiomba kazi kama yeye.


Lakini ajabu aliyoiona Merina kwa Damiani ni kwamba hakuwa na hata dalili za kumchangamkia, tofauti na wanaume wote waliowahi kumkabili. Alitarajia kama ni mwanaume anayependa warembo, basi siku hiyo hiyo angeombwa namba ya simu. Lakini ilikuwa tofauti kabisa kwa Damiani — hakujali kabisa mrembo huyo. Jambo hilo lilimfanya apende zaidi.


Kilichomshangaza zaidi ni kutoonekana kwa kijana Damiani hata pale walipompa taarifa ya kupata ajira ndani ya kampuni hiyo kama Msimamizi wa Fedha (Finance Manager). Jambo hilo lilimfanya mlimbwende huyu akae na kusubiria Damiani, lakini hakuweza kumtia machoni hadi siku ya mwisho. Aliongeza wiki moja zaidi kusubiria Damiani, lakini bado kijana huyo hakuonekana. Mwishowe alijikatia tamaa kabisa na kuona kwamba hakukuwa na uwezekano wa kijana huyo kuja kufanya kazi katika kampuni hiyo. Walifanya uamuzi wa kuajiri mtu mwingine. Lakini hilo halikuwa mwisho kwa Merina kumuwaza Damiani — usiku na mchana, kazini na nyumbani, alimuwaza kijana huyo. Alitamani muujiza utokee, amwone kijana huyo tena.


Mpenzi wake alishangaa hali aliyokuwa nayo Merina, kwani alikuwa amebadilika sana. Hakuwa tena yule aliyemjua hapo awali — alikuwa na uhakika Merina alimpenda yeye. Sasa kubadilika kwa Merina kulimchanganya, na aliamini kabisa kuna jambo halikuwa sawa.


"Merina, kuna tatizo gani, mpenzi wangu? Mbona siku hizi umebadilika sana? What is going on, my love?"


"Nothing, Pat. I am okay. Everything is alright with me. It is just... I need time."


"Lakini Merina, mpenzi, napaswa kujua kinachoendelea kwenye maisha yako. Kumbuka, wewe ni mpenzi wangu."


"Naelewa, Patrick. Lakini kwa sasa unapaswa kunielewa — siko sawa kihisia. Nahitaji muda. And soon, I will be fine."


* * * * *


Patrick Henry Mushi alikuwa ni mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Henry Mushi. Alikuwa na miaka ishirini na saba.


Alikuwa ni kijana mtanashati sana — mrefu, mzuri wa uso, mmoja wa wale wanaume wanaopendwa sana na wanawake kutokana na muonekano wao.


Licha ya yote hayo, Patrick pia alikuwa msomi aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown, kilichoko jijini Washington D.C., Marekani. Alikuwa miongoni mwa vijana wenye mafanikio makubwa ndani ya Tanzania, kwani alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa mali zote za baba yake.


Mwaka 2019 ndio mwaka aliokutana na mrembo Merina, ndani ya Hoteli ya The Hay-Adams iliyoko jijini Washington D.C., downtown. Siku hiyo, ingawa Bwana Patrick alikuwa na mwanamke mwingine, macho yake hayakuweza kuacha mrembo aliyekuwa mapokezi, ambaye alionekana alikuwa akingoja mtu.


"Mary, go ahead — am coming in minutes," aliongea akimwambia mchumba wake aende mbele, atakuwa nyuma yake.


Baada ya mrembo aliyekuwa na Patrick kutangulia, Patrick alisogea kwenye soffa karibu na Merina eneo la mapokezi. Alipomkaribia, Merina alitoa simu yake na kuongea kwa Kiswahili. Hapo ndipo Patrick alipomjua mrembo huyo kuwa ni Mtanzania au Mkenya. Lakini lafudhi yake ilimjulisha kuwa ni Mtanzania, ingawa hakuwa na uhakika.


"Mambo!" Patrick alimwambia kwa Kiswahili. Jambo hilo lilimfanya Merina atabasamu, na hapo ndipo Patrick alizidi kuvutiwa. Dimples zake zilizidi kuurembesha uso wake.


"Safi," alijibu Merina huku akiwa bado na tabasamu — kutokana na kusalimiwa kwa Kiswahili. Alijua kabisa mwanaume huyo alikuwa Mtanzania.


"Wewe ni Mtanzania?" aliuliza Patrick.


"Yeah, and you?"


"Mimi pia ni Mtanzania. Nafurahi kukutana na mtanzania mwenzangu ndani ya jiji hili."


"Mimi pia."


"Naitwa Patrick."


"Naitwa Merina."


"Nashukuru kukufahamu, Merina."


Kuanzia siku hiyo ndipo Patrick alijuana na mrembo huyo na kuvutiwa naye sana. Alifanikiwa kupata namba ya simu yake ya Tanzania.


Baada ya Patrick kurudi Tanzania, ndipo alianza mchakato wa kumpata mrembo huyo, kwani alimota kila siku na hakutaka kuendelea kuumia ilhali dawa ilikuwepo. Alijaribu kuomba kukutana naye; mwanzo ilikuwa ngumu, lakini siku moja alifanikiwa. Urafiki ulianza na kudumu kwa wiki mbili, hatimaye Patrick alirusha ndoano — lakini mrembo huyo alimkataa kwa mara ya kwanza. Patrick hakutaka kukata tamaa, aliendelea kubembeleza, na mwishowe alikubaliwa rasmi — lakini kwa masharti ya kutoshiriki mapenzi hadi watakapooanana. Kwa kuwa Patrick alimpenda kweli, na umri wake ulikuwa ukiomba ndoa, alikubaliana naye.


Mapenzi yalinoga pande zote mbili. Merina alimzoea sana Patrick, na Patrick naye alimpenda sana Merina. Tabia ya Patrick ya kuwa na wanawake wengi, aliiacha rasmi — jambo lililowashangaza marafiki zake. Lakini alipowaambia msimamo wake kuhusu Merina, kila mmoja alimuelewa.


Mwezi wa kumi na moja, mwishoni — baada ya miezi mitano ya mapenzi — ndipo likawa chungu kwa upande wa Patrick. Merina alibadilika sana; mawasiliano yalipungua ghafla.


Kubadilika kwa Merina kulimtesa sana na kumkosesha furaha. Alijaribu kulipigania penzi lake, lakini hakuna kilichosaidia. Aliapa kutomkatia tamaa mrembo huyo, akiamini lazima atakubali na kurudi kwenye njia siku moja — bila kujua kwamba mrembo huyo alikuwa akimuwazia mwanaume mwingine kabisa.


"Come on, Patrick! Unajitesa kwa sababu ya mtu hivyo, rafiki yangu. Mbona umebadilika sana? Yule msichana hakupendi — achana naye. Rudi kwenye maisha yako ya zamani. Tuamke, unaboa!" alisema Ahmed.


"Ahmed, niache. Nampenda Merina — nampenda kuliko kitu chochote. Yeye ndiye mwanamke niliomwota usiku na mchana, na kumwacha si kirahisi kama unavyosema."


"Najua unampenda, lakini yeye hakupendi. Unajihangaisha bure tu, rafiki yangu, na kujitafutia matatizo."


"Bwana, niache na maisha yangu. Anipende au anipende, mimi atakuwa wangu milele. Na yeyote atakayeingilia penzi letu — nikimgundua, ama yangu ama yake — nitamtoa ubongo."


Hayo yalikuwa ni ulevi wa Patrick siku hiyo — alikuwa amelewa, lakini alichokuwa akisema alimaanisha kweli. Hakutaka kabisa kukubali kwamba Merina hakumpenda.


* * * * *


Laptop ile ilizimika ghafla, kuashiria haikuwa na chaji. Hapo ndipo alipokumbuka kwamba siku zilizopita aliizima ikiwa imeisha chaji na hakuipeleka kwa jirani yake kuchaji. Alitoka na kuelekea nyumba ya jirani yao hapa kijijini, iliyokuwa na umeme. Aliomba kubustishwa kwa dakika tano hivi, akikaa kwenye soffa sehemu hiyo la sebuleni, akisubiria. Zilivyopita dakika tano, aliichukua na kurudi nayo nyumbani, akiahidi kuileta baadaye kuijaza chaji kamili.


Alirudi nyumbani, akawasha kompyuta, kisha akachukua ile flash drive na kuiingiza. Ilifunguka bila tatizo, na haikuwa na mafaili mengi — ilikuwa na faili moja la video. Aliplay na kuisikiliza.


"NADHANI UNAANGALIA VIDEO HII HUKU MIMI SIPO TENA DUNIANI. INAWEZEKANA HATUKUJUANA VIZURI, NA TUMEKUTANA KWA MUDA MFUPI, LAKINI HILO HALIJALISHI. ILIMRADI ULICHONACHO MIKONONI MWAKO KIPO SALAMA."


"DHUMUNI YA KUREKODI VIDEO HII NI KUKUAMBIA KWAMBA WEWE NDIO MRITHI HALALI WA MALI ZANGU ZOTE NINAZOMILIKI. LAKINI ILI KUMILIKI MALI HIZO, KUNA HATUA ZA KUPITIA — NA ILI KUJUA HATUA HIZO, NI LAZIMA UWE JASIRI."


"TAFUTA MTU MWENYE NAMBA 0713**** — ATAKUPA MAELEKEZO YA KILE UNACHOPASWA KUFANYA. MWISHO, TAFUTA MTU MWENYE KIDANI HIKI" — (ALIKIONYESHA) — "KISHA MUONYESHE KIDANI KILICHOKUWA KWENYE MKEBE. HUYO ATAKUWA NI MWANANGU. NAOMBA UKIFANIKISHA HILO, CHUKUA KIDANI HICHO — KITAKUWA NI UFUNGUO UNAOELEKEZA ENEO NILILOACHA HAZINA YANGU NA HATI INAYOKURUHUSIWA KUMILIKI MALI ZANGU ZOTE."


Video iliishia hapo.


Damiani alielewa, lakini ni kama mtu ambaye hakutaka kuelewa Bruno alichokuwa akimaanisha. Hakujua la kufanya wakati huo. Alikumbuka siku Bwana huyo alipomkabidhi bahasha ile — ni kweli kama alivyosema, hawafahamiani vizuri. Lakini pia, Damiani alikuwa na hasira kuu kwa mzungu huyo, kwani alimwona ndiye chanzo kikubwa cha kifo cha mama yake kwa njia ya kikatili.


Aliwaza na kuwazua maisha yake kuanzia siku hiyo mbele — akijiuliza atakwenda vipi. Hakuona njia wazi. Lakini wakati akizama katika mawazo, kitu kilimjia akilini — kama picha, kama kitu alichokuwa amesahau. Alikumbuka mama yake akiwa anataka kutamka kitu, na alionekana kuna kitu alichomnyooshea kidole. Hakuelewa ni nini alikuwa akionyesha, lakini aliamini kulikuwa na sababu. Alijikuta akikurupuka na kukaa juu ya kitanda, mapigo ya moyo yakienda mbio, jasho likianza kumtoka. Alifumba macho, akavuta kumbukumbu kwa nguvu, na alifanikiwa kukumbuka kwamba siku ile alikuwepo Kivinje. Aliendelea kujiuliza: ilikuwaje mama yake akawa akinyoosha mkono?


Alijikuta akiamka na kwenda mahali pale mama yake alipomkuta. Alijaribu kumuigiza jinsi mama yake alivyokuwa amenyoosha mkono — na hapo ndipo aliona mwelekeo. Ilikuwa ni nyuma ya mlango, sehemu iliyokuwa na majembe na kuni zilizosimamishwa. Hisia zake zilicheza, na akaanza kuvuta picha, akagundua kwamba kulikuwa na mtu aliyejificha nyuma ya mlango ule.


"Inamaanisha siku ile muuaji alikuwa amejificha nyuma ya mlango?" alijikuta akijiuliza. Hisia zake zilimwambia ana uhakika.


"Ngoja niende kwa Mzee Kivinje," aliamua. Alitembea haraka na kufika nyumbani kwake, akaomba kumwona. Aliamiwa yupo, lakini ana mtu anayemtembelea. Aliamuua kusubiri. Baada ya kama saa moja, Kivinje alitoka.


"Karibu, Bwana Damiani," alisema Kivinje. Damiani hakutaka kupoteza muda — alimueleza kwa ufupi na Kivinje alielewa. Sasa alikuwa na jibu.


"Uko sahihi, Bwana Damiani. Nilitaka kulizungumza hili siku nyingi, lakini kwa kuwa umekuja, acha nikuambie nilichoshuhudia."


"Siku ile, pale nyumbani kwenu, kulikuwa na watu wawili. Mmoja alikuwa amejeruhiwa kwa risasi. Wakati tulipofika, hukuwa makini, lakini nilimwona akikimbia — alikuwa ameshika silaha, na mimi pale nilishikwa na hofu kubwa."


"Wa pili alikuwa ndani, nyuma ya mlango — lakini alikuwa amejiziba uso. Sikuweza kuona sura yake. Na yule wa nje pia sikuweza kuona sura yake. Lakini naweza kuwaelezea maumbo yao," aliongea Kivinje. Hapo Damiani alijikuta chozi likimtoka. Alikumbuka jinsi mama yake alivyonyoosha mkono nyuma ya mlango — kumbe alikuwa akimwonyesha muuaji.


"Je, polisi umewaambia kuhusu hili?"


"Ndio, nilitoa ushahidi wangu. Walisema wataniwasiliana, lakini hawakufanya hivyo hadi leo."


Hapo Damiani alichoka. Hakujua la kufanya wakati huo — roho ilimuuma sana. Aliagana na Mzee Kivinje na kuelekea nyumbani. Ilikuwa asubuhi, na wanakijiji wengi walikuwa hawapo bado.


Alirudi nyumbani na kujilaza kitandani, akiwaza. Wazo lilimjia na mara aliona alifanyie kazi mara moja. Alichukua vitu vilivyokuwa kwenye bahasha, akaviweka kama vilivyokuwa, kisha alitoka nyuma ya choo na kuchimba shimo, akafukia vitu vyote, akarudisha mazingira yalivyokuwa, kisha akarudi.


Lakini alipofika mlangoni, kitu kilimshika — mlango ulikuwa wazi, wakati alikuwa ameuacha umefungwa. Alishindwa na wasiwasi wa ghafla. Alisimama dakika chache, akiangalia. Mwishowe alijaribu kupuuza na kuingia — lakini hiyo ndiyo ilikuwa kosa lake.


Aliingia tu, akakamatwa mara moja. Kitambaa kikawekwa puani. Akaona nyota. Akazimia.


Alibebwa bila fahamu, mchana kweupe, kupitishwa kwenye vichaka. Mtu aliyembeba alikuwa amefunika uso wake kwa kitambaa. Alipofika mbele, akakivua — na hapo sura yake ilionekana wazi.


Alikuwa ni DERICK — kijana wa Kimbona.
 
06
Derick alikuwa kama mwenyeji wa eneo hilo. Alimbeba Damiani na kumpitisha kwenye njia ambazo hazikuwa na watu walioweza kuwaona. Walitoka kwenye barabara ndogo iliyoingia msituni — ilikuwa ni njia iliyotumika na magari ya kusafirisha mbao na miti. Hapo mbele kidogo kulikuwa na gari linalosubiri.


"Fungua mlango," aliamrisha. Jamaa mmoja mfupi mwenye mwili wa mazoezi alitokea na kufungua mlango. Damiani aliingizwa ndani, na mara moja gari iliondoka eneo hilo kwa kasi. Damiani alitoa simu yake na kumpigia simu bosi wake.


"Boss, yupo mikononi mwetu."


"Safi. Mpelekeni kule chimboni. Hakikisheni mnafanya aongee — lazima Bruno alimpa kitu, kama mlivyosema kwamba alikuwa na bahasha."


"Sawa, Boss."


Gari iliendesha kuelekea barabara ya mlalo kwa kasi kubwa. Ndani ya nusu saa, waliondoka kwenye maeneo ya watu na kuendelea mbele. Walipinda kushoto na kuingia barabara ndogo. Mbele kidogo kulikuwa na eneo lenye maua yaliopandwa vizuri, pamoja na nyumba iliyozungukwa na uzio wa wire ya michongoma.


Gari iliingizwa ndani kupitia geti lililofanywa kwa mabati na mabanzi. Damiani alishushwa bila fahamu na kuingizwa ndani ya jengo hilo, ambalo halikuwa baya — nyumba nzuri, bustani zilizotunzwa vizuri, kama kuna mtu aliyekuwa akiishi hapo.


Aliingizwa mpaka kwenye chumba kimoja ambacho haikuwa na samani — mazaga mazaga tu kama stoo. Aliwekwa humo ndani, mlango ukafungwa, wakaondoka.


* * * * *


Nusu saa baadaye, Damiani alijikuta akizinduka kwa kupiga chafuo. Alishangaa sehemu aliyokuwepo, kisha akaacha akili yake ifanye kazi. Alikumbuka kukamatwa na mtu aliyekuwa ndani ya nyumba yao, na hapo akajua kwamba alitekwa. Ilikuwa wazi kabisa — eneo hilo halikuwa salama kwake.


Alijua pia kwamba kwa vyovyote vile, waliomteka ndio waliouawa mama yake na Bruno. Hasira zilimkamata. Alijaribu kujinasua, na hapo akagundua alikuwa amefungwa kwa kamba ngumu. Aliangaza huku na huko — kulikuwa na mwanga hafifu, na makorokocho mengi yaliyojaza chumba hicho.


Muda si mrefu, chumba kilifunguliwa na Derick aliingia, akiwa na kijana mwingine — tofauti na yule aliyekuwa naye walipomtoa Damiani.


"Naona umeamka, kijana. Kwanza, pole sana kwa kufiwa na mzazi wako," aliongea Derick kwa dharau. Maneno hayo yalimgusa Damiani hasa, hasira zikazidi. Alijaribu kuvuta kamba kwa nguvu — bila mafanikio. Alikuwa amefungwa vizuri.


"Nakuambia — nitakuua," aliongea Damiani kwa hasira kali. Derick alimtazama kisha akacheka kwa nguvu. Hata yule mwenzake alitoa tabasamu.


"Sikiliza, kijana. Kwanza, hatutaki hata kujua jina lako. Tunachokihitaji kutoka kwako ni kitu kidogo tu. Ukitupa hicho, tunakuachia huru. Nadhani unajua ni kitu gani tunachohitaji — hivyo usipoteze muda."


"Mnachokitaka kutoka kwangu — sina. Na hata kama ningekuwa nacho, nisingewapa. Na lazima niwalipe kisasi," aliongea Damiani kwa ujasiri kamili, na kumfanya Derick aone kwamba bila nguvu hawatapata chochote.


"Kazi kwako — muonyeshe. Tuone kama msimamo wake utadumu muda gani. Mimi nina shauku ya kuona hilo," aliongea Derick. Hapo yule bwana pembeni alinyanyuka, akakunjua ngumi, akamtandika Damiani kofi la shavuni — pigo zito kama jiwe. Alipigwa ngumi mfululizo hadi akalegea.


"Nadhani sasa utaongea."


Damiani alihisi uchungu mkubwa moyoni mwake — kiasi kwamba hata maumivu ya mwili hayakuwa na nguvu zaidi ya chuki aliyokuwa nayo kwa Derick. Kwa sababu moja kwa moja alijua — huyu aliyekuwa mbele yake ndiye aliyehusika katika mauaji ya mama yake.


Derick alimsogelea Damiani na kumshika kidevu.


"Tupe tunachokitaka uwe huru, bwana mdogo," aliongea Derick. Lakini bila kutarajiwa, Damiani alimtemea mate yaliyochanganyikana na damu. Hapo ndipo Derick alipompigia kipande — mpaka Damiani akazimia. Lakini hawakutaka kumwacha. Walimwagia maji, kisha wakaleta chombo kingine cha kutesa.


Chombo hicho kilijulikana kwa Kiingereza kama cattle prod — aina ya fimbo iliyogunduliwa huko Texas, Marekani, iliyotumika awali kwenye malisho ya ng'ombe. Inatoa mkondo mkali wa umeme wa voltage ya juu — shoti moja ya kutisha. Sasa hivi ilikuwa mkononi mwa Derick.


"Bwana mdogo, sitaki kukufikia na hiki chombo. Lakini kama utaamuua kusema uliweka wapi mzigo uliopewa, basi utaondoka huru mahali hapa na kuendelea na maisha yako."


Damiani alimwangalia Derick kwa chuki ya hali ya juu. Ingawa alikuwa amelegezwa sana na mapigo, hakuwa tayari kusema lolote. Hasa akikumbuka jinsi mama yake alivyofariki kikatili — moyo ulizidi kujaa hasira.


"Maaaaaaaaaa...!" Ulikuwa ni ukelele wa aina yake baada ya kuwekewa shoti ya umeme.


"Hahahaha... Wapi mzigo wetu ulipo?" Damiani aligugumia kwa maumivu. Aliona muda si mrefu angeweza kushindwa kustahimili. Shoti nyingine ilimkumba — maumivu yake yalikuwa makali zaidi.


Yule bouncer aliyempa Damiani mateso alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya sana — haikuwa kazi yake ya kwanza. Kimbona alimtumia sana kuwafanya watu waongee. Lakini siku hiyo alitoka jasho — kwani Damiani alikuwa kama maiti aliye hai. Hakufurukuta, hakuomba, hakusema neno. Kijana huyu alikuwa na moyo mgumu kuliko wote aliyowahi kukutana nao kazini. Na kilichomshangaza zaidi ni kwamba kijana huyo hakuwa na mafunzo yoyote ya kustahimili maumivu.


"Nadhani hajui kitu," aliongea yule bouncer akimwangalia Derick.


"Hata mimi nadhani hajui kitu — na inawezekana hakupewa mzigo," alijibu Derick. Alitoa simu yake na kupiga namba ya Kimbona. Simu ilipokelewa baada ya sekunde kadhaa.


"Vipi, Derick — ameshaongea?"


"Hapana, Boss. Inaonekana hajui kitu na mzigo hana — tumempa mateso ya daraja la kwanza."


"Kama hana, tutachunguza washirika wake mmoja baada ya mwingine. Tutaanza na Danny — naamini ndiye aliyeaminiwa sana na Bruno."


"Sawa, Boss. Nitamfuatilia alipo."


"Kazi hiyo huwezi kuifanya, Derick. Danny si wa mchezo — ni Kommando yule. Nitampa mtu mwingine kazi hiyo. Endelea kumwangalia huyo mdogo — asiachiwe."


"Sawa, Boss."


* * * * *


MIAKA MITANO NYUMA



Ni mwezi wa kumi na moja — mwezi ambao Rais Bendera aliingia Ikulu mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nane wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kushinda uchaguzi kwa asilimia 58 ya kura dhidi ya mpinzani wake.


"Karibu sana Ikulu, Mheshimiwa," aliongea Rais aliyestaafu muda mfupi uliopita, Bwana Athumani Ndalu.


"Nashukuru sana, Mtangulizi wangu."


Bwana Athumani hakutaka kuchukua muda mrefu. Alianza kumkabidhi ofisi Mheshimiwa kwa muda wa siku mbili — siri za nchi, nyaraka mbalimbali, na mikataba iliyokwisha kusainiwa pamoja na ile ambayo bado ilikuwa ikingoja saini.


Siku iliyofuata baada ya Rais Bendera kukabidhiwa madaraka, alifanya kikao chake cha kwanza na wakuu wa usalama wa nchi — akiwemo Mkuu wa TISS na wadau mbalimbali wa kitengo cha usalama wa taifa na maswala ya ujasusi kwa ujumla.


"Ndugu zangu, nadhani mnajua hiki ni kikao changu cha kwanza tangu niingie Ikulu. Dhumuni la kikao hiki ni kujua mwenendo wa usalama wa nchi yetu kwa ujumla, na pili, kuweka msimamo wangu wazi juu ya mambo ambayo nataka yafanyike chini ya uongozi wangu — kabla hata sijaunda Baraza la Mawaziri," aliongea Mheshimiwa Rais.


"Ndio, Mheshimiwa. Kuhusu usalama wa nchi kwa sasa, ni imara kabisa. Idara zetu za usalama wa taifa zinafanya kazi kwa weledi mkubwa. Tunazo operesheni kadhaa ambazo tunaendelea nazo na tupo mbioni kuzifanikisha. Hapa ni jalada la Idara ya Usalama wa Taifa na mawakala wake wote," aliongea Mkuu wa TISS, Bwana Hassan Matumwa, na kumkabidhi Mheshimiwa lile jalada.


"Suala la pili ni juu ya msimamo wangu. Kwa taarifa nilizonazo kwa sasa, biashara ya madawa ya kulevya hapa nchini imetamalaki. Kutokana na takwimu za kitabibu, inaonyesha vijana wengi wanaharibika na madawa haya, na kupelekea taifa kukosa nguvu kazi — kwani vijana ndio urithi wa taifa. Hivyo basi, msimamo wangu chini ya uongozi wangu ni kukomesha biashara hii kufanyika ndani ya nchi hii. Kazi hiyo siwezi kuifanya peke yangu — watu ambao nataka kufanya nao kazi ni nyie hapa," aliongea Mheshimiwa Rais kwa nguvu. Wakuu wa usalama walitoa leso zao na kufuta jasho — walijua ni vigumu kiasi gani kuufuta mtandao huo.


Kikao kilifungwa. Mheshimiwa alitoa msimamo wake kwa msisitizo mkubwa, na kila mtu alielewa alichokuwa akizungumzia.


Mara baada ya kutoka kwenye kikao, alienda moja kwa moja mpaka ofisini kwake akiwa ameshikilia jalada la usalama wa taifa. Alikaa kwenye kiti chake, akafunua jalada na kuanza kupitia majina yaliyopo — vitengo vyao na operesheni walizokuwa wakifanya — kwa umakini mkubwa.


Baada ya kupitia, aliweka jalada chini huku akionyesha kutoridhika. Alichukua simu yake, akabonyeza namba fulani, akaweka sikioni.


"Nakuhitaji ofisini kwangu," aliongea Rais Bendera kwa sauti kavu. Alikuwa Rais mwenye umbo zito, bila kitambi, rangi nyeusi, kichwa kilichopambwa na mvi nyeupe.


Dakika chache baadaye, bwana mmoja mwenye mwili mkakamavu uliojaa misuli, aliyevalia suti nyeusi na earpieces masikioni, aliingia.


"Nimefika, Mheshimiwa."


"Nassani, fanya maandalizi — nataka nifanye ziara yangu ya kwanza Hospitali ya Muhimbili na Mwananyamala," aliongea Mheshimiwa.


"Sawa, Mkuu."


Ilikuwa saa saba mchana Mheshimiwa Bendera alipotoka ofisini kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Vinga'ora vya pikipiki ndio vilivyosikika Barabara ya Luthuli. Msafara ulipita Sokoine, Kisutu, ukaingia Barabara ya Obama, UN, Maliki — hadi hatimaye ukaingia ndani ya hospitali hiyo.


Wafanyakazi walikuwa na hekaheka kubwa baada ya kusikia ujio wa Mkuu wa Nchi. Kila mtu alikuwa akijipanga. Miongoni mwa waliokuwa na wasiwasi alikuwa mganga msaidizi mfawidhi, kwani mkuu wake wa kazi hakuwepo ofisini na hakutoa taarifa yoyote ya kutokuwepo.


"Karibu, Mheshimiwa," alisema mwanamama mmoja wa makamo aliyejitambulisha. Kwa makadirio, alikuwa na umri wa miaka 40 hadi 45, na alifahamika kwa jina la Sofia Mohamed Babu.


"Mkuu wako wa kazi yuko wapi?" aliuliza Katibu Muhtasi.


"Hajafika kazini leo. Nadhani kuna tatizo limetokea, kwani hajatoa taarifa mpaka sasa."


"Kama hajatoa taarifa, basi kuanzia leo wewe ndio Mkuu wa Hospitali hii," aliongea Rais kwa ujasiri kamili, na kumfanya Sofia atoe jicho la mshangao.


"Au huwezi?"


"Si hivyo, Mheshimiwa."


"Nahitaji kuonana na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Akili, na pia nahitaji takwimu zote za wagonjwa wa akili wanaotokana na madawa ya kulevya."


Haikuchukua muda — Daktari Fileuka Ndimbo alifika ofisini kwa Mganga Mkuu akiitikia wito. Alijitambulisha, kisha akaanza kutoa takwimu.


"Kwa sasa, ndani ya hospitali yetu tunapokea wagonjwa kumi na tano kwa siku, huku zaidi ya mia moja wakiwa wagonjwa wa nje. Katika wagonjwa 15 tunaopokea kwa siku, wanne wanatokana na madawa ya kulevya — wanaletwa hapa na ndugu au wazazi wao. Tunazo kata nne zinazopokea wagonjwa hawa: Mwananyamala, Magomeni-Ilala, Kinondoni, na Temeke," aliongea Daktari Ndimbo. Rais alijisikia huzuni kubwa — idadi ilikuwa ikiongezeka, si kupungua.


Alipitia wodi zilizokuwa na wagonjwa hao — hali ilikuwa ya kusikitisha sana. Vijana wengi walionekana katika hali mbaya, na wazazi wakiwa katika majonzi makubwa. Kama baba wa watoto watatu, alihisi kitu moyoni mwake — alifikiria ingekuwaje kama wangekuwa watoto wake. Roho ilimuuma. Aliazimia kupambana na magenge yote ya kuuza madawa ya kulevya na kuyatokomeza.


"Nassani, tunaelekea Mzena Hospital — Mikocheni," aliongea Rais. Wasaidizi wake walishangaa, lakini hawakuhoji.


Dakika kumi pekee zilitosha kufika ndani ya hospitali hiyo iliyotumika kwa ajili ya matibabu ya viongozi wa taifa na wakuu wa usalama. Alipokelewa na Mganga Mkuu, akaangalia hali za wagonjwa waliokuwepo, akatoa pole, na mwishowe alizungumza na Mganga Mkuu — akitaka kuonana na Marco Ngalu. Huyu alikuwa Mkuu Mstaafu wa Kitengo cha Usalama wa Taifa, na alikuwa hospitalini hapo kwa ugonjwa wa moyo.


"Karibu sana, Mheshimiwa," aliongea Bwana Marco Ngalu huku akionekana ana shida ya kuongea.


"Asante sana."


"Nassani, nahitaji kuongea na Mzee huku nikiwa peke yangu." Nassani alitoka na kuungana na wanausalama wengine kulinda nje ya mlango.


"Mzee wangu, nimeitika wito wako. Kama ulivyonipa maagizo kabla sijakabidhiwa majukumu — nipo hapa sasa nikiwa na majukumu na madaraka kamili ya nchi hii."


"Kwanza, nikupe hongera kwa kuchaguliwa. Lakini pia niseme pole sana — unakwenda kuanza majukumu mazito sana ndani ya serikali hii."


"Nalifahamu hilo, Mzee wangu. Ndiyo maana nipo hapa kuchukua mwongozo wako. Hali ya vijana wetu inanisumbua sana — naona taifa lipo hatarini kupoteza nguvu kazi."


"Ni kweli kabisa unachosema. Na kila kitu nimekiandaa kwa muda mrefu sana, kwa kushirikiana na Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tatu," aliongea Mzee huyo. Ingawa alikuwa mgonjwa, afya yake haikuwa mbaya sana — alikuwa hospitalini kwa uangalizi maalumu wa kitabibu.


Alitoa flash disk kutoka mfukoni mwa shati lake — ilionekana wazi alikuwa akitembea nayo muda wote.


"Kila kitu kipo hapa, Mheshimiwa Rais. Unachopaswa kujua ni kwamba kulikuwa na sababu kubwa ya kukuteua kuwa Rais ndani ya chama chetu — hali ya nchi hii ni mbaya sana. Hivyo nikutakie utekelezaji mwema, na nikuambie tu: usikate tamaa. Safari unayokwenda kuianza ni ngumu na ya hatari sana."


Bwana Bendera, baada ya kumaliza mazungumzo na Mzee Marco, hakutaka kubaki eneo hilo. Alichokuwa akifikiri wakati huo lilikuwa ni kurudi Ikulu na kuangalia kilichokuwa ndani ya flash disk aliyopewa.


Dakika ishirini baadaye, alikuwa ndani ya ofisi yake, tarakilishi mbele yake, flash disk ikichomekwa. Ilianza kusomwa kwenye skrini. Bila kusita, alikutana na faili la PDF yenye ukubwa wa megabyte moja — aliona mara moja kwamba faili hilo lilikuwa na maudhui mazito sana.


* * * * *


Siku chache baada ya Rais kukutana na Marco na kupewa flash disk ile, alitangaza uteuzi mpya kuanzia ngazi ya usalama wa taifa — wakuu wa majeshi na wakuu wa polisi. Kila mtu alishangaa, kwani hakuna aliyetegemea kwamba Rais angeweza kuteua watu hao. Walikuwa watu wa ngazi ya chini kabisa.


Mkuu wa TISS alikuwa Bwana Elly Matinde. Mkuu wa Majeshi (CDF) alikuwa Bwana Abdallah Khalifa. Mkuu wa Polisi (IGP) alikuwa Bwana Kizito Kabwela.


Hakuna aliyepinga maamuzi ya Mkuu wa Nchi. Siku tatu baadaye waliapishwa rasmi. Mara baada ya kuapishwa, kilifanyika kikao cha dharura kilichokuwa na watu watano — wateule wanne pamoja na Makamu wa Rais, Bwana Henry Mushi.


"Mnaweza mkashangaa kwa nini nimewateua kuwa wakuu wa idara za usalama. Kuna sababu kubwa — kitu tunachokwenda kukifanya ni cha hatari sana na kinahitaji wazalendo wa nchi hii. Na wazalendo niliowaona mnafaa ni nyie hapa," alisema Rais, akitulia na kuwaangalia mmoja mmoja.


"Sitaki kupoteza muda — nina majukumu mengi. Lakini jambo kubwa ninalonisema ni juu ya biashara ya madawa ya kulevya ambayo imetamalaki hapa nchini. Nahitaji kupitia msaada wenu kuiondoa kabisa katika uso wa Tanzania — kwani vijana wetu wanazidi kuharibika siku hadi siku, na taifa linaingia kwenye hatari ya kukosa nguvu kazi."


"Ni kweli, Mheshimiwa. Suala unalolizungumza lilikuwa linanisumbua sana — hata mmoja wa ndugu zangu ni mhanga wa suala hilo," aliongea Bwana Kizito.


"Pole sana, Bwana Kizito. Na nadhani sikukosea kukupa nafasi hiyo, kwani unaujua uchungu wa suala hili. Kwa sasa, mpango uliopo ni kuundwa kwa Tume ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya — ile iliyokuwepo nimeibatilisha rasmi, na Mkuu wa Polisi, hili litakuwa kazi yako ya kwanza: nenda utolee taarifa vyombo vya habari baada ya kutoka hapa. Nahitaji kuunda Tume mpya kwa msaada wenu. Na kwa kuwa suala hili ni nyeti sana, tunapaswa kupata njia ya kuingia kwenye mfumo wa madawa ya kulevya wenyewe," aliongea Rais, na kuwafanya wote watoe macho.


"Mheshimiwa, suala hilo litakuwa gumu sana kufanyika," aliongea Abdallah.


"Si gumu — mpango tayari ninao. Mnachopaswa kufanya kwa sasa ni kunitafutia vijana wenye mafunzo ya hali ya juu ya kijasusi, ambao wataifanya kazi hii. Mkuu wa TISS, Mkuu wa Polisi, na Mkuu wa Majeshi — mkitoka hapa mkae kikao pamoja na mbaini ni vijana gani wanafaa. Kesho nahitaji ripoti kamili na utambulisho wa vijana hao. Kazi ianze rasmi," aliongea Mheshimiwa, na kikao kikafungwa.


* * * * *


Upande mwingine — mwaka huo huo, mwezi huo huo — hali ya msukosuko ikiendelea Ikulu, ndani ya Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa VIP, kulikuwa na kikao kizito.


Kikao hicho kilijumuisha watu hawa: Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Mkuu wa TISS Mstaafu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Tajiri mkubwa Tanzania Bwana Samuel (akijulikana kama Rich Sam), Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Bwana Athumani Ndalu, na Bruno Lamberk.


"Jamani, kama nilivyotabiria, hali si shwari kabisa," alianza kuongea Rais Mstaafu.


"Ni kweli, Mheshimiwa. Ilikuwa kosa kubwa sana kwa Bendera kupita katika Halmashauri ya Chama na hatimaye kuwa Rais wa nchi hii. Haya yote tuliyatarajia," aliongea Rich Sam.


"Ni kweli unachosema. Lakini sikuwa na jinsi wakati ule — wakongwe wa chama walinilemea, na mpango wetu wa kumweka Rais tunayemtaka haukufanikiwa. Lakini suala hilo si la kujilaumu kwa sasa — swali lililopo mbele yetu ni: tunafanyaje?"


"Kwa sasa ni vigumu kujua la kufanya, kwani hatujui Bendera ana mpango gani. Na kama amekutana na Marco, jua kuna jambo kubwa sana linalotungojea mbeleni," aliongea Mkuu wa TISS Mstaafu.


"Mimi nafikiri kwa sasa hakuna sababu ya kuogopa. Mtandao wetu una mizizi mirefu sana, na washirika wetu ni waaminifu. Kinachohitajika kwa sasa ni kuangalia upepo kwanza — na kuzuia mzigo wowote kuingia nchini kwa muda huku tukitafuta ni mbinu gani Rais anaipanga," aliongea Bruno — kwani ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa Umoja wa Wauza Madawa Nchini.


"Mkuu, ulichosema ni sahihi kabisa. Lakini suala hili ili lifanikiwe, lazima tuwe na mtandao wetu pale Ikulu — ambao utakuwa ukitupatia taarifa." Waliendelea na kikao, mpaka mlango ulifunguliwa.


Aliingia mwanamke aliyevalia suti ya zambarau, mwenye rangi nyeupe, mrefu na mrembo. Alimsogelea Bwana Bruno na kumiinamia, akionekana kumwambia kitu puani. Hapo Bruno alijikuta akitoa macho ya mshangao.
 
07
"Kuna nini, Mkuu?" aliuliza Mkuu wa Majeshi.


"Washa televisheni hiyo," aliongea Bruno.


Ilikuwa ni taarifa ya Mkuu wa Polisi akitangaza rasmi kuvunjwa kwa Kamati ya Ulinzi ya Maswala ya Upambanaji na Madawa ya Kulevya (DCEA).


"Hili ni suala ambalo tulilitegemea Rais kulifanya," aliongea Athumani.


"Si hilo tu — kuna kubwa zaidi."


"Lipi hilo, Bruno?"


"Mheshimiwa Rais amevunja kamati zote za ulinzi, chakula, hadi usafi Ikulu," aliongea Bruno. Hapo kila mmoja alitoa leso yake na kufuta jasho.


"Naona mambo yanazidi kuwa magumu, na tunahitaji kulifanyia kazi hili haraka iwezekanavyo. Mpaka sasa hatuna mtandao wa kutupatia taarifa kwa kile kinachoendelea Ikulu," aliongea Sam.


"Mkuu, tunafanyaje?"


"Hapa hakuna la kufanya — inabidi tuisimamishe biashara kwa sasa. Nitaandaa ripoti na kuisambaza Makao Makuu ya U-97. Nyie wengine mwaambie washirika wenu kusimamisha biashara na kufuta ushahidi."


Kikao kilifungwa, kila mmoja akatoka. Hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa katika hali nzuri kimuonekano — wote walionekana walikuwa kwenye wasiwasi mkubwa.


* * * * *


Siku mbili baadaye, Rais Bendera alisaini sheria mpya ya ubadilishaji fedha, iliyowasilishwa na Gavana wa Benki Kuu. Sheria hiyo ilizuia taasisi zote na maduka yaliyokuwa yakibadilisha fedha kukubali au kufanya ubadilishano wa pesa za kigeni zaidi ya kiwango cha dola elfu kumi — sawa na shilingi milioni ishirini au zaidi. Pili, sheria ilizuia wasafiri kuingia nchini wakiwa na kiasi zaidi ya dola elfu kumi bila kutoa maelezo kwa TRA.


Sheria hiyo mpya ilikuwa ni mwiba kwa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya nchini, na waliipokea kama pigo jingine zito.


Baada ya mswada huo wa sheria, Rais aliendelea na mabadiliko yake makubwa — kuanzia ngazi za juu bandarini hadi ngazi za chini. Aliteua Wakuu wa Mikoa mipya wa Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Tanga, Katavi, na Kigoma. Lakini hakuishia hapo — aliunda Baraza jipya la Mawaziri, na pia akateua Waziri Mkuu mpya, jambo lililoacha wananchi mdomo wazi pamoja na washirika wake, kwani mtu aliyeteuliwa hakutarajiwa kabisa na mtu yeyote.


Bwana Hamduni Saidi Rajabu ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu mpya — aliyekuwa awali ni Katibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.


Baada ya uteuzi huo, Rais aliitisha kikao kingine — kikubwa zaidi. Walihudhuria Waziri Mkuu, wakuu wote wa idara ya usalama, Mkuu mpya wa DCEA aliyeteuliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Rajabu Ngasu, Waziri wa Katiba na Sheria Alfred Peter, na Waziri wa Fedha Bwana Innocent Mushi.


"Hongereni, Waheshimiwa, kwa kuteuliwa katika nafasi zenu. Lakini niseme pia kwamba nawapongeza kwa uzalendo wenu kwa nchi hii — kwani kupitia hilo ndio leo hii tunakutana katika kikao hiki. Simaanishi kwamba sisi peke yetu ndio wazalendo wa nchi hii — wapo wazalendo wengine — lakini sisi ndio wawakilishi wao. Na naamini huko nje, wananchi kwa sasa wana matumaini makubwa juu yetu katika ufanyaji maamuzi yenye maslahi mapana ya nchi hii." Alitulia kidogo, kisha akaendelea.


"Nafasi mlizopo zina sababu kubwa, na niseme wazi — ni nafasi ngumu sana, zenye majukumu makubwa mnayokwenda kuyatekeleza kwa maslahi ya nchi hii, nyie kama wazalendo. Kama mnavyojua, taifa hili lipo katika wakati mgumu sana. Kipindi tunachopitia sasa ni kibaya sana — vijana wanaendelea kuangamia kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Hivyo basi, nimewaalika hapa kwa nia kuu mbili: moja, kuwapa mwelekeo wa serikali yangu; mbili, kuwapa mpango wa hatua za mapambano dhidi ya madawa ya kulevya."


"Bwana Lazaro Kitwana —" (huyu alikuwa ndiye Mkuu mpya wa DCEA) "— kazi yako kuanzia sasa ni kuunda timu ambayo itakuwa na polisi wenye kazi moja maalumu: kukamata kila mshukiwa yeyote wa biashara ya madawa ya kulevya hapa nchini." Aliendelea.


"Mkuu wa TISS, Mkuu wa Majeshi, na IGP — nadhani faili langu lipo tayari?"


"Ndio, Mkuu."


"Vizuri. Nikitoka hapa nitalihitaji."


"Hivyo basi, kwa umoja wetu hapa ndani, nataka nitangaze: kuanzia sasa, nyie ni wajumbe wa Mamlaka ya Kupambana na Madawa ya Kulevya Nchini. Mamlaka hii itaongozwa na Makamu wa Rais, na mwenendo mzima wa maswala haya mtahusika. Niwaambieni tu — vita imeanza. Na ndani ya mwezi ujao, sitaki kunusa harufu ya aina yoyote ya madawa ya kulevya hapa nchini." Aliongea Mheshimiwa, kisha kikao kiliisha. Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, na IGP walibaki.


"Waheshimiwa, nadhani kazi mmeimaliza. Hivyo nahitaji orodha ya vijana wa kazi."


Mkuu wa TISS alianza kusoma:


"Danieli Mtalemwa, namba ya utambulisho N00D — huyu ni Kommando wa daraja la kwanza. Amepata mafunzo yake nchini Cuba, China, na Thailand, huku elimu yake ya kipelelezi na ujasusi akiichukua nchini Israeli. Mafanikio yake ni makubwa katika operesheni alizofanya hapa nchini, ikiwemo Operesheni Ambone Tanga, Kibiti, na Rusumo. Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha UDSM ngazi ya Shahada, na pia ni mhitimu wa Chuo cha Monash nchini Australia katika maswala ya Uhandisi.


"Suzzane Rashidi, aka Miss K, namba ya utambulisho N02S — huyu ni Kommando wa daraja la kwanza, lakini pia ana mafunzo ya ukaguzi na upelelezi. Kwa sasa yuko nchini Urusi kama undercover agent katika misheni ya Umoja wa Mataifa. Mafunzo yake aliyachukua Cuba na Thailand. Huyu ni hatari zaidi katika udunguaji, lakini pia ni mbobezi katika maswala ya teknolojia ya habari (IT).


"Zakayo Yakobo, aka Agent Z, namba ya utambulisho N01Z — huyu pia ni Kommando, lakini pia ni mhitimu wa maswala ya upelelezi na ni mhitimu wa chuo cha uigizaji nchini Marekani. Elimu yake ya kimapigano aliimasilisha nchini China. Kwa sasa yupo Indonesia kwenye mashindano ya mitindo.


"Wengine ni Irene Joseph, Martine Sheiza, na Abasi Ndumbalo — hawa wote ni wanausalama chini ya kitengo cha TISS."


Alimaliza Mkuu wa TISS, kisha akamkabidhi Mheshimiwa faili hilo.


"Kazi nzuri. Naamini upembuzi wenu ni yakinifu. Mkuu wa Idara, kazi ya kwanza anayotakiwa kufanya Agent Z ni ya utekaji."


"Unamaanisha nini, Mheshimiwa — utekaji? Ni nani anapaswa kutekwa?"


"Hiyo ndiyo kazi ya kwanza itakayotuingiza katika mtandao wa madawa ya kulevya. Mtu anayetakiwa kutekwa ni sehemu dhaifu ya mtandao huo, na tunatakiwa kuitumia kikamilifu. Lengo letu kwa sasa ni Bwana Bruno Lamberk." Akanyamaza kidogo, kisha akaendelea.


"Kwa taarifa nilizonazo, huyu ndiye mkuu wa usambazaji wa madawa ya kulevya hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla. Chini yake ana washirika wengi ambao hawajulikani, na wapo hapa nchini. Tukifanikiwa kumpata Bruno, basi washirika wake tutaweza kuwapata pia. Lakini kazi hiyo si rahisi, kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja. Ili kufanikiwa, inatupasa kumgeuza mshirika wetu."


Wazee walichoka — kwani wote walimjua mzungu huyo. Alikuwa ni mwekezaji mkubwa hapa nchini, na ukiachana na uwekezaji wake, alikuwa pia mmoja wa watu waliokuwa wakisaidia jamii sana. Sasa kutajwa kwake kama muuzaji wa dawa mkubwa nchini lilikuwa jambo kubwa, la kuogopesha, na la kushangaza kwa wakati mmoja. Lakini ndivyo alivyokuwa — bwana huyu alijificha biashara zake haramu kwa kujivika ngozi ya kondoo.


"Mheshimiwa, kama unachosema ni kweli, suala hilo linahusiana vipi na misheni unayotaka aifanye Agent Z?"


"Safi. Iko hivi — Bruno ana mtoto wake wa siri. Kwa taarifa nilizonazo, bwana huyu anampenda sana mtoto huyo, na anaweza kufanya chochote ili mtoto huyo asidhurike, kwani ndiye anayetarajiwa kuwa mrithi wake. Nadhani mpaka hapo mnaelewa kwamba udhaifu mkubwa wa Bruno ni huyo mtoto. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba Bruno hamfahamu mtoto wake kabisa — mwanamke aliyemzaa aliamuua kumficha. Anachojua Bruno ni kitu kimoja tu: ana mtoto wa kike."


"Sasa, kama hamjui mtoto wake, sisi tutafanikiwa vipi kumshawishi kwamba huyo ni mtoto wake?"


"Hiyo kazi iaachieni mimi. Mpango huu haujaanza leo tu — umeanza muda mrefu. Mimi ni mtekelezaji tu, na nyie pia mnatakiwa kutekeleza suala hilo."


Baada ya Mheshimiwa kutoa maagizo hayo, Zakayo alitumiwa ujumbe wa misheni aliyotakiwa kuifanya nchini Marekani, huku akipokea maagizo ya moja kwa moja kutoka Ofisi ya Rais.


"Unapaswa kupiga picha baada ya kumteka. Mkufu aliomvaa hakikisha sura haionekani. Mtoto huyo yuko Chuo X — na picha yake ni hiyo."


* * * * *


Tajiri Lamberk alikuwa katika wakati mgumu sana wa kiuongozi ndani ya umoja wao waliouita UNITY 97 (U-97). Aliandaa ripoti, akaimasilisha, kisha akaituma Makao Makuu ya umoja huo yaliyokuwa nchini Mexico. Ripoti hiyo ilijumuisha mwenendo wa maswala ya kibiashara kwa ujumla nchini Tanzania.


Masaa machache baada ya kutuma ripoti hiyo, alipokea ujumbe kutoka Makao Makuu:


"We received your report and Level 01 Unity Leader has conceded with your recommendations until further notice." — akimaanisha kwamba Kiongozi wa Juu Kabisa wa U-97 amepokea na kukubaliana na mapendekezo yake, mpaka pale taarifa nyingine itakapotolewa.


Baada ya kupokea majibu hayo, alisambaza habari kwa wakubwa waliokuwa chini yake, huku akitoa onyo la kuchukua tahadhari mapema — kwani muda wowote hali ingeweza kubadilika.


Siku mbili baadaye, ilikuwa saa mbili usiku. Akiwa kwenye jumba lake la kifahari eneo la Mbezi Beach, alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu. Simu hiyo ilimwelekeza kwenye WhatsApp, kwamba kuna zawadi yake huko.


Bruno hakuamini macho yake. Mapigo ya moyo yalipiga mbio — kitu alichokiona na taarifa aliyoona vilimshika kwa nguvu.


Kilikuwa ni Mkufu fulani uliotengenezwa kwa madini ya almasi. Na Mkufu huo ulimrudisha miaka ishirini nyuma — mwaka ambao alikuwa na miaka miwili tu tangu aanzishe makazi yake nchini Tanzania.


Mwaka huo, mara baada ya kuanzisha makazi yake nchini Tanzania, alikuwa kwenye mawazo mazito ya familia yake — ile aliyokuwa akiishi nayo jijini New York — iliyouawa kikatili sana. Tukio hilo lilitokana na ugomvi mkubwa aliokuwa nao na wauza madawa ya kulevya wenzake, huku akituhumiwa kuwasaliti. Mkuu wa kikundi hicho alituma watu wake na kuiteketeza familia yake yote. Baada ya tukio hilo la kusikitisha, alikimbilia nchini Tanzania. Kuanzia siku hiyo aliishi akiwa na kisasi moyoni, na kupitia tukio hilo alijiapia kutokutengeneza familia katika maisha yake yote.


Lakini baada ya miaka miwili, alikutana na mwanamke wa Kitanzania — Mkinyaturu. Mwanamke huyu alikuwa mfanyakazi wa Hoteli ya Singita Grumeti iliyokuwa ndani ya Mbuga ya Wanyama ya Serengeti. Urafiki ulianza ndani ya hoteli hiyo, na mwishowe ukazaa mapenzi. Kutokana na hali ya ulevi siku moja, Bwana Bruno alijikuta akifanya mapenzi na mwanamke huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Wema Sufiani. Alipolipambazuka, akashituka — alikuwa amelaliwa na mrembo huyo. Kuanzia siku hiyo, kila alipofika hoteli hiyo, Bruno hakuacha kukutana na Wema.


Baada ya mwaka mmoja wa mahusiano yao, siku moja alipofika hotelini, alipokea habari kwamba Wema alikuwa mjamzito.


Ilikuwa habari mbaya kwake — alikuwa ashaweka nadhiri ya kutokutengeneza familia katika maisha yake yote. Lakini pia aliogopa lililomtokea miaka iliyopita lijirudie kwa Wema na mtoto atakayezaliwa. Hakutaka kumwonyesha Wema jinsi habari hiyo ilivyomfanya ahisi — badala yake alionyesha furaha ya bandia, huku kichwani akipanga yake.


Baada ya miezi tisa, Wema alijifungua. Wakati huo alikuwa ameshaacha kazi yake ya uhudumu wa hoteli na alikuwa nyumbani kwao Singida. Bruno alipata taarifa ya kujifungua kwake — mtoto wa kike. Ilikuwa habari ya kufurahisha, lakini ya kuogopesha pia. Siku mbili baadaye ndio siku aliyofika Singida kwa siri, akakutana na Wema. Hapo ndipo alipofanya jambo ambalo kwa Wema lilimhuzunisha sana — alimpa kadi ya benki, akimwambia pesa zilizomo zilikuwa kwa ajili ya matunzo ya mtoto na yeye mwenyewe. Pia alimpa Mkufu wa almasi wenye mfumo wa kipekee.


"Wema, consider me dead from now on. I have a family and I don't need trouble with your baby. My family will not accept her, and I can't do anything about it. For the child's safety and yours — don't ever, ever look for me."


Kwa Wema ilikuwa ni kilio. Lakini baada ya muda alikubaliana na hali hiyo. Aliuangalia Mkufu ule kisha akamvalisha mwanae. Alikwenda benki na kuangalia kiasi cha pesa alichoachiwa na mzungu huyo — zilikuwa nyingi sana kwa wakati huo. Kwa kuwa Wema alikuwa mwanamke mwenye akili ya biashara, akafanya biashara, na biashara hiyo ikamtambulisha na kumfanya mwanamke mashuhuri ndani ya nchi — na hilo lilikuwa baada ya miaka kumi.


Katika wakati wote huo, Wema alikuwa akisikia habari za Bruno, na Bruno naye alikuwa akisikia habari za Wema. Baadaye, Wema alioolewa na Henry Mushi — kipindi hicho bwana huyo akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Lakini jambo lililomshangaza Bruno ni kwamba hakuwahi kumwona mtoto wake kabisa. Hata ndani ya familia ya Henry na Wema, jina la mtoto hakikuwahi kutajwa. Suala hilo lilimla kichwa sana — alitaka kujua mtoto wake alipo, lakini liligonga mwamba. Alipojaribu kuongea na Wema, hakupata ushirikiano wowote — jibu lake lilikuwa moja tu: asahau kwamba ana mtoto katika maisha yake, na kama angedelemuka kumfuatilia, angempoteza. Kwa kuwa Bruno hakutaka ugomvi na mwanamke huyo — ukizingatia kwamba wakati huo Wema alikuwa na nguvu kubwa nchini, na mume wake walikuwa watu wenye msimamo ndani ya serikali — hakutaka kabisa purukushani.


Upande wa Henry, hakuwahi kujua kwamba mke wake Wema alikuwa na mtoto kabla ya ndoa yao — kwani Wema hakuwahi kumtambulisha mtoto wake kwake. Miaka kadha baadaye walifanikiwa kupata watoto wao wenyewe.


Hiyo ilikuwa kumbukumbu ya miaka ishirini iliyopita.


* * * * *


Basi turudi kwenye miaka mitano nyuma. Siku hiyo ndiyo siku ambayo Bwana Bruno alitumiwa picha na mtu asiyemfahamu — ikionyesha Mkufu ule. Chini ya picha kulikuwa na maelezo:


"Ukitaka ukweli juu ya mahali alipo mtoto wako, fika New Africa Hotel, chumba namba 108, siku ya Ijumaa, saa nne kamili usiku. Hakikisha jambo hili linakuwa siri yako — kosa moja tu, utampoteza mtoto wako."


Pamoja na ujumbe huo kulikuwa na video ya mtoto wake — akionekana amekuwa mfungwa.


Itaendelea panapomajaliwa.. unaweza pia kuisoma zaidi kupitia link hapo chini au nicheki watsapp namba 0687151346

endelea hapo
 
Damiani ni kijana wa miaka ishirini na mbili, mhitimu wa chuo kikuu cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) akiwa amechukua kozi ya Finance and Accounting in Public Sector (kozi inayohusu maswala ya uhasibu). Mara baada ya Damiani kumaliza masomo yake hakutaka kubaki ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwani hakuwa na kazi maalumu ambayo ingemuwezesha kujiingizia kipato ndani ya jiji hilo. Pia maisha ndani ya jiji hilo yalikuwa ghali sana na yalihitaji pesa ili kuweza kuishi.

Hivyo mara baada tu ya kumaliza masomo yake aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini mkoani Tanga kwa ajili ya kusikilizia upepo wa ajira. Kwani mwaka ambao alikuwa amemaliza haukuwa kama miaka ya nyuma kwamba ukimaliza tu unasubiri matokeo na kupata ajira. Kinyume chake ni kwamba utasubiri matokeo yatoke na kuomba ajira kwa makampuni ambayo yatakuwa na uhitaji au serikali pale itakapotangaza nafasi za ajira na kuomba. Na kwa kuwa kipindi hicho kulikuwa na wimbi kubwa la vijana ambao walikuwa wahitimu na hawakuwa na ajira mtaani, hivyo ilikuwa ngumu sana kupata ajira. Ilikuwa ni kama kubahatisha tu pale nafasi zinapotoka kwani wengi wa waombaji wana sifa zinazofanana.


Mkuzi ndio kijiji cha kijana Damiani. Kijiji hiki kilikuwa ndani ya wilaya ya Lushoto, kilomita kadhaa kutoka Lushoto mjini. Yaani kama utasafiri kwa gari ni muda wa dakika thelathini mpaka arobaini kufika ndani ya kijiji hicho. Ni moja ya vijiji ambavyo vilikuwa vimezungukwa na misitu na kuwa na mazingira ya kuvutia sana. Yalikuwa ni moja ya mazingira ambayo watalii wengi wa mataifa ya nje na hata watalii wa ndani walikuwa wakipenda kutembelea. Na hiyo yote ni kutokana na hali yake ya hewa ilivyokuwa safi na ya kuvutia.


Basi kijana Damiani ndani ya kijiji cha Mkuzi ndipo alikulia na kujipatia elimu yake ya msingi na sekondari.


Damiani alikuwa kijana mpole, mcheshi, mrefu maji ya kunde, mwenye sura yake ya kuchongoka lakini iliyoumbwa vizuri. Alikuwa ni moja ya vijana walio kuwa na miili mikubwa ya wastani. Damiani alikuwa akiishi na mama yake tu kwani baba yake alikuwa amekwisha kufariki miaka mingi nyuma kipindi akiwa tu na umri wa miaka kumi.


Kurudi kwa Damiani kijijini baada ya kumaliza masomo ilikuwa ni moja ya furaha kubwa sana kwa mama yake kumuona mwanae kurudi ndani ya kijiji hicho, kwani mama huyo alikuwa akimpenda sana mwanae.


“Karibu sana mwanangu,” mama alifurahia sana kwa mwanae kumaliza masomo yake ya ngazi ya juu, na kujihisi kuwa mwanamke aliyefanikiwa kulea kwani watoto wengi ndani ya kijiji hicho hawakufanikiwa kufika ngazi ya juu ya kielimu kama ilivyokuwa kwa Damiani.


“Asante mama, hatimae nimemaliza chuo na nimerudi rasmi,” aliongea Damiani huku akiachia tabasamu. Huku nje watoto wengi walikuwa wakimwangalia na kumshangaa. Hiyo ilikuwa ni kawaida sana kwa vijiji kushangaa watu walio tokea mjini na hata kwa wageni pia.


Basi Damiani alikaribishwa vizuri na mama yake katika nyumba yao hiyo ya vyumba vitatu iliyoezekwa kwa mabati, na kwa kuwa Damiani alikuwa na chumba chake tokea akiwa shuleni ndiko mama yake alipeleka begi lake na kukifanyia usafi.


Maisha ya kijana Damiani yanaanza rasmi ndani ya kijiji cha Mkuzi. Licha ya Damiani kuwepo ndani ya kijiji hicho lakini alikuwa na mipango mikubwa sana ya maisha yake hapo mbeleni, kwani alihitaji kuja kuwa mfanya biashara mkubwa sana katika maisha yake na hiyo ilikuwa ndiyo moja ya ndoto yake kubwa. Japo alikuwa amesoma na alikuwa akitarajia kuwajiriwa lakini ajira kwake haikuwa kipaumbele. Ila kipaumbele kwake ilikuwa ni kupata mtaji utakaomwezesha kuanzisha biashara. Hakika alikuwa na safari ndefu sana na hata kwa yeye pia alilijua hilo na hivyo kwa umri aliokuwa nao hakuwa na sababu ya kukatishwa tamaa na mazingira aliokuwemo na aliokulia. Kwani alichokuwa akikiamini katika maisha yake ni juu ya uchapaji kazi kwa bidii na kutokukata tamaa na kuwa na malengo ndiyo nguzo kubwa sana ya kuja kufanikiwa. Hakutaka kabisa kukatishwa tamaa na hali ya maisha yao ya umasikini yaliyopo hapo nyumbani, ila aliamini katika mawazo chanya tu.


Basi hatimae wiki, mwezi na hata miezi ilikatika na matokeo yake yalikuwa yamekwisha kutoka na akiwa amefaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza. Kwake na kwa mama yake ilikuwa ni furaha na faraja kubwa sana, kwani aliamini kupitia ufaulu mkubwa basi angeweza kumrahisishia kupata kazi kwa wepesi zaidi.


Hakutaka kusafiri mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya kuomba kazi ilihali kulikuwa na njia rahisi. Alichokifanya yeye ni kutuma maombi kwa kila kampuni ambayo ilikuwa ikitangaza nafasi za ajira kwa njia ya mtandao.


Mwezi wa kwanza uliisha kijana Damiani akiwa amekosa kabisa uelekeo wa ajira kwani ni makampuni zaidi ya matatu ambayo alikuwa ameomba kwa ajili ya kupata ajira lakini amekosa hata wito wa interview (mahojiano ya kiufanisi). Zikiwa zimepita siku kadhaa za kijana Damiani kukata tamaa, hatimae kwenye moja ya kampuni ambayo haikuwa imetoa majibu ilirudisha jibu kwa kijana Damiani kwa ajili ya kuhudhuria interview.


Ilikuwa ni moja ya kampuni iliyokuwa ikipatikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, kampuni moja ya usafirishaji iliokuwa na makao yake makuu ndani ya Posta. Kwake Damiani alifurahia kwani aliona tumaini la kupata ajira linaridhisha zaidi. Alimwambia mama yake juu ya taarifa hiyo na mama yake pia alifurahia na kumpa baraka zote mwanae kwa ajili ya kuhudhuria interview hiyo.


Ilikuwa ni siku ya Jumatatu ndiyo siku ambayo kijana Damiani alikuwa ndani ya basi akielekea jijini Dar kwa ajili ya kuhudhuria interview. Alifanya maombi juu ya safari yake hiyo na kusudio lake analoliendea kulifanyia kazi.


Kutoka Lushoto mpaka ndani ya jiji la Dar ni umbali wa masaa sita mpaka saba. Hivyo Damiani alikuja kufika ndani ya jiji hilo kwenye muda wa saa nane kamili mchana. Siku hiyo alipanga akifika ndani ya jiji hilo kwa kuwa hakuwa na ndugu wa kufikia, alipanga kwenda kwa rafiki yake mmoja aliyekuwa amemuacha ndani ya chuo akiendelea na masomo kwa ajili ya kumuhifadhi mpaka siku inayofuata afanye interview na kisha ageuke kurudi nyumbani.


Basi baada tu ya kushuka ndani ya basi akijisogeza mpaka kwenye daladala zinazoelekea Mbagala na kisha alipanda huku malengo yake aje ashukie Mtongani kwa Azizi Ally kwani hapo ndipo rafiki yake huyo alipokuwa akipatikana kwa kuishi. Barabara haikuwa na foleni sana hivyo hawakuchukua masaa mengi kufika sehemu aliokuwa amekusudia.


Mara baada tu ya kushushwa hatimae alinyoosha moja kwa moja upande wa kushoto wa barabara, huku akipita vichochoro viwili vitatu na kuja kutokelezea mbele ya nyumba moja kubwa iliokuwa na ukuta. Hatimae alisimama nje ya geti la nyumba hiyo huku kama ni mtu aliyekuwa akijishauri agonge ama asigonge. Ila kwa kuwa kilichomleta hapo ni kuonana na rafiki yake na rafiki yake alikuwa akiishi ndani ya nyumba hiyo basi hakuwa na budi ya kugonga geti hilo.


Haikuchukua muda mrefu hatimae alikuwa amefunguliwa na msichana mmoja aliyekuwa amejifunga khanga moja, na alionekana alikuwa akifua kwani alikuwa na mapovu mikononi.


“Karibu,” sauti hiyo nyororo ilimkaribisha ndani huku dada huyo akitangulia mbele na kumuacha kijana Damiani kumsanifu mdada huyo kwa nyuma. Alikuwa ni mlimbwende kweli aliyekuwa amejaliwa umbo zuri haswa la kumvutia kila mwanaume atakayemtia machoni. Alikuwa mrefu wa wastani mwenye rangi yake ya chocolate, alibarikiwa uso wa duara na kwa tathmini za haraka haraka mdada huyo alionekana umri wake haukuwa chini ya miaka ishirini kwenda juu.


“Nimemkuta Elvis??”


“Katoka sema anakuja muda si mrefu. Wewe ndio Damiani??”


“Ndio ni mimi.”


“Okey! Alinipa maelekezo yako kwamba ukifika nikukaribishe ndani,” aliongea msichana huyo huku akimkaribisha Damiani ndani kwani muda wote huo alikuwa amesimama. Damiani alijua lazima huyo mdada atakuwa hawara (mwanamke anayeishi na mwanaume pasipo kuolewa au mpenzi) wake Elvis maana alimjua mngoni huyo songea kwa kupenda warembo hakuwa nyuma na ndiyo maana kabla ya kutoka nyumbani alimtaarifu kuwa atakuja kulala kwake.


Basi mdada huyo alimuongoza Damiani ndani ya nyumba hiyo iliokuwa imepakwa rangi nyeupe mpaka kwenye chumba cha katikati upande kushoto na kisha alimkaribisha ndani. Kilikuwa ni chumba kimoja kikubwa saizi ya kati kilichokuwa kimejaa makorokocho mengi. Damiani alikuwa akikijua chumba hicho sana kwani hata kwa baadhi ya vitu hivyo vilikuwa vyake na ni baada ya yeye kumaliza masomo alimuuzia rafiki yake huyo.


Basi baada ya kukaribishwa dada yule alitoka nje na kuendelea na shughuli yake ya ufuaji huku akimwacha Damiani akimsubiri rafiki yake. Na haikuchukua hata dakika ishirini rafiki yake Elvis aliingia ndani ya nyumba hiyo. Elvis alifurahia sana kumuona Damiani na hata kwa Damiani ilikuwa ni hivyo hivyo. Wote walifurahia kuonana kwa mara nyingine.


“Karibu sana HB asiyetaka warembo,” aliongea Elvis akionesha kumtania mwenzie na kwa Damiani kwa kuwa alikuwa ashamzoea rafiki yake huyo kwa matani basi na yeye alicheka.


“Mzee wa totozi, naona shemeji yangu wa awamu hii ni shida.”


“Yaani acha tu mzee toto la toto na isitoshe limedata na ndiyo limenifanya nihangaike siku ya leo.”


“Unahangaishwa na nini sasa??”


“Hahaha lazima kuhangaika. Unajua jana ulivyonicheki unakuja ilikuwa ghafla sana na sikutaka kukwambia naishi na mtoto wa kike. Kwa hiyo unavyoniona hapa kuna msela nimetoka kumpanga ili ukale mbonji kwake ukamilishe mambo yako maana hapa sikuwa na jinsi.”


“Daah! Hapo ndiyo maana nakukubali mshikaji wangu.”


“Hahaha… usijali mzee si unajua hata wewe umenisaidia mara kibao. Hata mavitu haya ni kama ulinipa tu kutokana na bei ile.”


Basi Damiani walichukana na rafiki yake na kutoka eneo hilo kuelekea barabarani na kupanda magari ya kuelekea Rangi Tatu. Walivyofika Mbagala Zakhemu walishuka na kuchukua upande wa kushoto barabara. Umbali wa mita kadhaa hatimae waliingia chochoro ambayo walikuja kuibukia mbele mtaa mwingine, na wakaja kutokea mbele ya kanisa la KKKT na hapo walipinda kushoto tena na kukuta nyumba moja kubwa iliokuwa na geti na kwa nje ilisomeka kwa maandishi ya lodge. Elvis alisukuma mlango na kisha aliingia ndani. Kwa Damiani yeye alikuwa akifatisha tu kuona mwisho wake kwani kuna hisia zilizokuwa zikimwambia kaletwa lodge.


“Oya mshikaji anakaa hapa, si lodge hapa tena japo ilikuwa lodge. Mwenye nyumba kaamua kuifanya nyumba ya kupangisha,” aliongea Elvis na kumfanya Damiani aelewe. Walipita kwenye vyumba kadhaa na hatimae walisimama nje ya mlango na Elvis aligonga na nusu dakika mlango ilifunguliwa na jamaa mmoja wa makamo mfupi mwenye mwili mkubwa wa kibonge.


“Karibuni.”


Waliingia ndani ya chumba hicho. Kilikuwa ni chumba kikubwa na kizuri sana, na pia hata kitanda na samani (furniture) zilizokuwemo humo ndani zilionesha jamaa anayeishi humo ndani hakuwa mnyonge kipesa.


“Oya huyu ni Joshua rafiki yangu sana mwaka wa kwanza hivyo ndiyo utachilia hapa kwake mpaka utakapokamilisha mambo yako,” aliongea Elvis na Joshua alimkaribisha Damiani na Elvis aliaga akaondoka.


Basi siku nyingine iliingia ambayo ni siku Damiani alikuwa akielekea mtaa wa Posta kwa ajili ya kufanya interview. Alikuwa amevaa akapendeza maana kwenye nguo alikuwa nazo na mkopo ulimsaidia sana kipindi akiwa chuo.


Alijisogeza mpaka barabarani ili kusubiri gari ya kwenda stesheni Posta apande. Ila mara baada ya kufika tu kwenye barabara nje kabisa ya supermarket iliyosomeka kwa jina la Kivoni, ilisimama gari moja aina ya Vanguard nyeusi na kioo kilishushwa na akaonekana bwana mmoja wa makamo, makadirio ya miaka 30 kuendelea mweusi alivalia shati jeupe na koti akiwa na miwani. Damiani wakati huo gari hiyo ikisimama alikuwa akiiangalia na hata jamaa huyo alivyoshusha kioo alikuwa pia akimwangalia. Damiani alijikuta akijishtukia na hiyo ni mara baada ya jamaa huyo kumuonesha ishara ya kumuita. Alijithibitishia kama ndio yeye aliyekuwa akiitwa na hapo ndipo alipopiga hatua kulisogelea gari hilo.
Welcome back mzee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom