know-ledge
Member
- Sep 4, 2024
- 70
- 94
Kiukweli
Mwandishi uko vyema sana japo mimi nipo mbele kidogo naisoma kule fasihinet ila kiukweli unajua kinoma kuandikaBy Samuel jk_Euphoria
SOLO KING: ANCIENT LEGACY
CHAPTER 22: Nakupa namba kumi
"Ningekuwa najua nisingeuliza mzee wangu" Jimmy alimjibu mlinzi huyo
"Huyo ni msanii maarufu wa hapa bongo, anaitwa Bakari Juma almaarufu kama Beka"
"Oh sasa msanii anakuja kufanya nini huku muda ambao anatakiwa studio?"
"Kijana inaonekana hujui mengi licha ya kumiliki simu janja, mimi na huu uzee wangu lazima nizame mtandaoni kujua nini kinaendelea nchini na suala la huyo dogo kuja hapa iko hivi, kuna tetesi kwamba jamaa anampenda madam mdogo na ndiio yupo kwenye mchakato wa kummiliki na hii ni mara ya tatu kuja hapa"aliongea mlinzi huyo na kumfanya Jimmy akunje sura bila kupenda
"Hahaha... Hahaha.. Haha" ghafla tu Jimmy alianza kucheka bila ya kueleweka anacheka nini
"Vipi kijana mbona unacheka?" aliuliza mlinzi
"Huyu Beka anafurahisha sana mzee wangu, kitendo cha kuja mpaka nyumbani kwa madam mdogo maana yake ni kwamba madam anakaza si ndio?" aliongea Jimmy
"Yrah inaonekana ila kijana bado hajakata tamaa na ni mwaka wa pili anamfukuzia madam pemgine juhudi zake zitazaa matunda" aliongea mlinzi
"Kuna muda ni bora kukubali matokeo yalivyo l kuliko kulazimisha yawe tofauti, kwa maelezo yako inaonekana hapendwi ila anafosi kupendwa" aliongea Jimmy huku akifurahi moyoni
"Ndio vijana wa siku hizi walivyo halafu utasikia ndiyo nguvukazi ya taifa letu"
"Unaonaje mzee wangu kwa busara ukimfundisha kwamba kama moyo wa mtu hauko kwako, hata ujitume vipi, ni kupoteza muda tu."
"Haha kijana unataka kunitafutia matatizo sio"
Jimmy na mlinzi wa geti walijikuta wakipiga story mbili tatu kwa zaidi ya masaa matatu na bado Beka hakuwa ametoka ilionekana alikuwa akimsubiri Bianca na kweli muda huo wa saa tisa Jimmy na mlinzi waliweza kusikia honi kutoka nje ya geti na bila shaka alikuwa ndiye madam mdogo aliyekuwa akisubiriwa
Mlinzi alikwenda kufungua geti na gari jeusi liliingia na kwenda kujiegesha mahali pake kisha mlango ukafungulia na Zuhura aliweza kutoka na walinzi wawili ndani ya gari na kisha Bianca
"Amekuja tena" aliongea Bianca mara baada ya kuliona gari analolitambua mmiliki wake
"Je nimwambie aondoke?" aliuliza Zuhura
"Haina haja twende ndani" Bianca aliongea kikauzu
Ile wanataka kupiga hatua kuelekea ndani walisikia sauti ya mtu ikiongea
"Hatimae malkia umwrudi" aliongea Jimmy akiwasogelea mikono akiweka mfukoni mwa suruali na uso uliopambwa na tabasamu
"Tafadhali Jimmy"
"Aw sio mbaya angalau umeniita jina langu kwa mara ya kwanza zio mbaya ila usikasirike nimekuja tu kukupa hi na pole ya kazi"
"Inaonekana una muda mwingi sana wa kupoteza si ndio?" aliongea Zuhura huku amekunja sura ni wazi hakumpenda
"Ndio ndio lakini pia kutazama watu muhimu wakifika kwa kuchelewa ni mojawapo ya mambo yangu mapya ya kujifurahisha. Hasa wakati kama huu ambao kuna drama nakwenda kushuhudia" alijibu huku akitabasamu
"Drama?"
"oh tena ni pale mtu mashuhuri anapomtembelea mtu mashuhuri mwenzake bila taarifa" aliongea Jimmy
"Isn’t it though? He’s been showing up here thrird time now in two years, and you keep playing ice queen. You dont love him do you?" aliendelea akimaanisha kwamba Beka amekuwa akija hapo ni mara ya tatu sasa kwa miaka miwili na humpendi si ndio?
"Zuhura twende ndani" aliongea Bianca kisha kutangulia akifuatwa na Zuhura na walinzi wawili
"Haha very cute!" aliongea jimmy huku akicheka na kuunga trela kuingia ndani akiwaacha wale mabaunsa wa Beka wakimuangalia na macho yao yasiyo na utani lakini hakujali
Picha linaanza baada ya wote kuingia ndani Beka alikuwa sebuleni amekaa akinywa juisi ya matunda na mara baada ya kumuona Bianca alisimama
"Hatimae subira yangu imezaa matunda" aliongea Beka
"Beka kwanini upo hapa?" Bianca aliuliza
"Nimekuja kuzungumza kuhusu sisi"
"Hilo tu?"
"Pia kuhusu ile hafla ya hisani itakayofanyika wiki ijayo, wanataka sisi wawili kuwa sura ya kampeni hiyo"
"Wanataka au unataka?"
"Vyote"
"Oh sawa si ungempigia tu simu meneja wangu kulikuwa na haja gani ya kuja huku bila taarifa?"
"Pia nilikuwa nataka nije kukuona tuzungumze"
"Kuzungumza kuhusu nini?" aliongea na Beka alisita akimwangalia Jimmy ambaye muda wote alikuwa akisikiliza maongezi
"Ni jambo la faragha hivyo sio jambo la busara kuongea mbele za watu"
"Mbele za watu? Kijana yaani uvamie nyumba ya mpenzi wangu na bado tu haitoshi na unataka kwenda naye faragha? Hata kama wewe ni maarufu angalau kuwa na heshima kijana" Hatimae Jimmy aliongea
Kauli hiyo kutoka kwa Jimmy ilimfanya gBeka kukunja sura bila kupenda ilionekana hakutegemea hilo licha ya kujipanga vyema kabla ya kuja, upande wa Bianca hakubadilika muonekana wake alikuwa katika pozi lilelile la kikauzu Beka alimwangalia Jimmy kwa macho makali kisha kumpotezea na kumgeukia Bianca
"Bianca kwanini unashindwa kuuelewa moyo wangu, ninakupenda sana tena zaidi ya sana lakini kwanini hutaki kunielewa? Juhudi zangu zote kwako unazichukulia poa, unataka nifanye nini ili uniamini nakupenda kwa dhati? Niambie nina mapungufu gani ili nijirekebishe" Beka aliongea bila kujali uwepo wa Zuhura na Jimmy sebuleni humo
"Nishakwambia mara nyingi kwamba sipo interesyed kuanzisha mahusiano na mwanaume yoyote hivyo ulitakiwa unielewe wewe na sio mimi nikuelewe wewe" aliongea Bianca
"Lakini mbona huyu dogo anadai wewe.ni mpenzi wake"
"Hey usiniite dogo mbele ya mpenzi wangu, in case hujui jina langu, naitwa Jimmy halafu acha kufosi mambo pia kama mwanaume unatakiwa kujiongeza. Sababu ya kukwambia hataki kuanzisha mahusiano ni kwasababu tayari alikuwa na mtu anayempenda moyoni na huyo mtu ni mimi" aliongea Jimmy kibabe
Japo Bianca alitaka kuongea neno lakini alichagua kukaa kimya na kuona mwisho wake kati ya hao wanaume
"Tafadhali dogo naomba ukae kimya kwenye mambo yasiyokuhusu" aliongea Beka kwa hasira
Jimmy alitabasamu na kutoa mikono yake mfukoni kisha kuongea
"Hujakaribishwa, hupendwi lakini bado unajikuta mwamba sana, sikia we pimbi nani sijui ili kufanya mambo yasiwe magumu kwako nadhani unajua mlango ulipo" aliongea Jimmy
"Jimmy!" Bianca aliita ilionekana hakupenda kauli aliyoitumia hususani "pimbi"
"Hahaha unpaswa kufikiria mara mbili kati yangu mimi na wewe nani atakuwa wa kwanza kuusogelea mlango" aliongea Beka na alipiga kelele kuwaita mabaunsa wake na punde mabaunsa hawa hapa ndani!
"Tafadharini ndani kwangu sio uwanja wa fujo" Bianca aliongea na Zuhura alitaka kuchukua hatua lakini alipewa ishara ya macho na Jimmy akimtaka atulie na alijikuta tu anatii tu bila kupenda ni kama macho yake yalikuwa yakiogopesha kwa wakati huo hadi alijishangaa kulikoni anatii?
"Nilidhani utakuwa na akili ila inaonekana wewe ni mpumbavu na siku zote wapumbavu hujidhihirisha kupitia upumbavu wao yaani pamoja na kushobokea nyumba za watu lakini unataka kuanzisha na vurugu pia...Asee katika wapumbavu niliokutana nao nakupa namba kumi" Jimmy aliongea
"Wewe mshenzi nyamanza, Abuu mshikisheni adabu huyu punguani hakikisheni mnamvunja na mguu tuone kama ataendelea kuongea pumba" alimaka Beka na palepale baunsa aitwaye Abuu akiongozana wenzake walimsogelea Jimmy wakidhamiria kutekeleza kile walichoambiwa
Jimmy hakusogea alisimama palepale na Abuu baada ya kumsogelea alinyanyua mikono yake akitaka kumkunja vest yake na kumtandika utosi na kichwa chake kigumu kama jiwe
Lakini kabla hata mikono yake haijatua alishtukia kofi la uso kama wahindi wanavyowatandikaga maadui kwenye muvi na hata hakuelewa limemfikiaje
Halikuwa kofi la kitoto hata kidogo, lilisikika nyumba nzima, kofi lile lilimyumbisha Abuu na kurudi nyuma hatua nne na kutema mate yalichanganyika na damu pamoja na meno mawili
Mabaunsa wenzake wawili baada ya kushuhudia kitendo kile walipigwa na butwaa na kusita kidogo, walijiambia inawezekanaje mtu mwenye mwili wa kawaida tu wa mazoezi na kuonekana mwepesi kuweza kumpiga baunsa kofi lenye madhara kama yale, tena jitu lizito lililotuna na kukomaa mwili na mifupa. Hakika ilishangaza hata Beka macho yalimtoka pia bila kumsahau Zuhura na wenzake
"Pumbavu unathubutu vipi kunipiga kofi!" Abuu alimaka kwa hasira
"Nikufahamishe mapema nikishamaliza kudili na nyinyi pamoja na boss wenu unasafisha huo uchafu wako hapo chini" aliongea Jimmy bila ya kujali hasira ya baunsa huyo
"Mnazubaa nini mshambuliani kwa pamoja huyo" Beka alifoka
Mabaunsa mara baada ya kumsikia boss wao akifoka wote kwa pamoja walichomoa fimbo flani hivi ndogo za chuma zijulikanazo kwa kingereza kama batons ambazo hutumiwa na walinzi(security guards/bodyguards). Walibonyeza kitufe kilicho karibu na sehemu ya kushikia na urefu kuongezeka mpaka inchi ishirini na nne(24 inches)
Palepale kwa kasi kulingana na uzito wa miili yao walimsogelea Jimmy wakimshambulia kwa pamoja kutumia fimbo zile
Jimmy alizikwepa kwa ustadi wa hali ya juu bila kusogea sana pale aliposimama, alikuwa akikwepa na kupiga kupiga hatua mbili kusini, hatua mbili mashariki, harua mbili magharibi, hatua mbili kazini. Alikuwa akikwepa kwa mtindo huo huku akiuchezesha na kuuzungusha mwili wake kwa ustadi wa hali ya juu sana na kama vile alikuwa akicheza mchanganyiko wa Tango na rhumba
Walishambulia mpaka walichoka lakini hakuna hata fimbo moja iliyomgusa na sasa Jimmy alichukulia fursa ya wao kuchoka kufanya mashumbulizi yake
"Crack! Crack! Crack!" ilikuwa ni sauti ya kuvunjika kwa mifupa
Wale mabaunsa walipige makelele ya maumivu wakiwa chini na kila mmoja alikuwa ameshika mguu wake na bila shaka Jimmy aliwavunja, ile kauli ya "hakikisheni mnamvunja mguu" kutoka kwa boss wao imegeuka kuwa jukumu la Jimmy.
Upande wa Zuhuru alikuwa ni "wow! What a style!" hakutegemea mwanaume huyo kuwa mtaalamu kwenye suala hilo pia hata hivyo hakuonyesha waziwazi
"Wanaume kupiga kelele mbele ya wanawake haipendezi" aliongea Jimmy na kisha kumgeukia Beka
"Bado unataka kubaki au nikusindikize mlangoni? " aliuliza huku akitabasamu
Tabasamu lile lilitosha kumtoa Beka kijasho cha woga na mdomo wake ulianza kutetema
"Nitaondoka" alijibu na haraka haraka alipiga hatua kutaka kuondoka lakini Jimmy alimzuia kwa mbele wakiangaliana uso kwa uso
"Hey sijasema uondoke nimeuliza kama unataka kubaki au nikusindikize mlangoni ila unaonekana unataka nikusindikize basi sawa nitakusindikiza" aliongea, Jimmy
"Hapana... Unajua... aarggh" kabla hata hajamaliza kuongea alichotwa mtama matata sana na kuanguka chini akijipigiza upande wa kushoto wa komwe lake chini na kuishia kutoa ukelele wa maumivu. Hazikupita hata sekunde tano nundu lilitokelezea tayari
"Tafadhari Jimmy acha unachokifanya inatosha" aliongea Bianca akiwa na wasiwasi
"Unajua mimi ni nani eeh... Aargggh mamaaa!" aliongea Beka na sauti yake ya kuugulia maumivu na Jimmy alimuongezea teke lililomvunja goti lake na kutoa ukelele wa maumivu
"Mama? Hakuna mama hapa we pimbi"
"Jimmy acha!" Bianca aliongea kwa sauti ya juu
"Oh sawa nitaacha" aliongea
"Yaani tangu urudi umekuwa ni wa kunitia hasira tu na ona sasa haijapita hata siku tumeanza kuishi lakini ushanisababishia matatizo unajua Beka ni mtoto wa nani?" aliongea Bianca akilipukwa na hasira
"Si huyu hapa alikuwa anataka kuleta vurugu ndio nimechukua jukumu la kuzuia"
"kuzuia? Kuwavunja miguu ndio kuzuia? Hivi unajua hata baba yake ni nani?"
"Baba yake mimi simjui na sitataka kumjua" aliongea Jimmy
"Baba yake ni waziri wa sanaa na michezo we mkorofi" aliongea huku mishipa ikionekana kwenye paji lake
"Oh lumbe!" Jimmy hakushtuka
"Unapata wapi ujasiri wa kusema "oh kumbe" yaani unataka niletewe vikwazo kwenye kazi yangu kwa makosa yako?"
"Madam tafadhali usikasirike" aliongea Zuhura huku akimwangalia Jimmy kwa macho ya ajabu kweli, alitamani kumshushia kichapo kwa kumkasirisha boss wake lakini alichoshuhudia hakuthubutu hata kumsogelea kwa kuhofia kutolewa meno, Ingekuwa ni jana yake angekuwa na ujasiri huo kwasababu ya kutokujua lakini hapo tayari ashajua sasa kwamba ana mafunzo na kama aliweza kudili na mabaunsa kirahisi tu yeye ni nani?
"Usiwaze sana babe nitajua jinsi ya kufanya ikitokea au ushasahau mimi ni mwanasheria?" aliongea Jimmy na Bianca aliposikia kauli hiyo kutoka kwa Jimmy hakujua hata afanye nini alijiambia yaani bado tu huyu mkorofi anapata muda wa kumuita babe?
Aliona kuendelea kubaki hapo ataishia kukasirishwa zaidi na zaidi hivyo aliondoka akipandisha zake juu
"Haya ninyi pimbi safisheni huo uchafu wenu na muondoke hapa haraka iwezekanavyo vinginevyo msinilaumu kwa luwavunja mguu mwingine
Abuu harakaharaka alienda kufuta mate yake kwa shati lake jeusi na kuokota meno yake kisha yeye, wenzake na boss wake Beka kwa kuburuza miguu yao iliyovunjwa walitoka humo ndani lakini Beka kabla hajapotelea mlangoni aligeuka na kuongea
"Utajutia sana kwa hiki kitendo ulichokifanya" aliongea na Jimmy aliishia tu kumpa tabasamu na kumtishia kwa ishara kuwa anakuja kumvunja mguu mwingine akiendelea kusimama hapo mlangoni
Beka alishtuka na haraka japo kwa tabu alijivuta na kuondoka na sekundechache zilisikika ngurumo za gari kuondoka na Jimmy alijinyoosha mikono yake na kutulia lidogo akisimama pale sebuleni
Wakati amesimama alihissi kuangaliwa sana na ni kweli Zuhura alikuwa akimuangalia kana kwamba anataka kummeza
TO BE CONTINUED........