Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 30: Ugeni uliotarajiwa (expected visit)

Jimmy hisia zake zilikuwa ni sahihi kwani ndani ya sekunde kadhaa ulisikika mlio wa kengele ya mlango wa kuingia sebuleni kuashiria kwamba kuna ugeni muda huo

Aisha alinyanyuka na kwenda kufungua mlango na kuwaona watu wawili wamesimama mlangoni mmoja akwa ni mwanaume mwigine akiwa ni mwanamke. Mwanaume alionekana ni mkubwa kiumri huku mwanamke akiwa ni kijana zaidi

Wageni hao walikuwa wamevaa mavazi ya kawaida, mwanaume ambaye alikuwa ni kamanda Ramadhan alivalia t-shirt rangi ya zambsrau ambayo ilionekana kumbana kwa kiasi chake huku kifua chake na misuli ya mazoezi ikijichora, chini alivalia suruali nyeusi iliyombana na buti za kijeshi nyeusi zilizong'aa kana kwamba zimepakwa mafuta

Upande wa mwanamke alikuwa na asili ya kihabeshi na hakuwa mwingine bali ni Caren, naye alipendeza licha ya kuvalia kawaida kutokana na umbo lake matata. Chuchu saa sita za mrembo huyo zilionkana kusimama haswaa licha ya kuvalia shati kubwa la draft, rangi ya bluu lenye mikono mirefu, pia chini alivaa jinsi nyeusi iliyombana vyema na kuchora hipsi zake pamoja na mzigo wa wastani ulioko nyuma, bila kusahau buti nyeusi pia za doc matterns

"Karibuni ndani" Aisha aliwakaribisha na waliweza kuingia ndani.

"Msiishie kusimama tu hapo karibuni mpate kifungua kinywa haipendezi kwa wageni kula harufu ya misosi" aliongea Jimmy baada ya kuona wanaelekea kukaa sofani

Kama Rama na, Caren mara baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Jimmy walitabasamu na kuelekea mezani walikokaribishwa

"Ni wageni wako hawa?" Bianca aliumuuliza na Jimmy alitingisha jichwa kukubali

"Mbona hukutuambia kama una wageni asubuhi hii tuandae chakula cha kutosha" Bianca aliongea

"Usiwaze sana mummy watakunywa chai tu mimi mwenyewe sikutegemea ujio wao" Jimmy aliongea na alipomaliza kauli hiyo wageni waliweza kufika mezani na Bianca alinyanyuka kuwasalimia kwa heshima huku akiwapa tabasamu la kirafiki

"Miss lina sisi ndio tunapaswa kutoa heshima na kuomba radhi kwa ujio wa ghafla" aliongea Caren akimpa tabasamu

"Je haimpasi mke wangu kukaribisha wageni kwa heshima mahali pangu?" Jimmy aliongea

"Unanifahamu!" Bianca aliuliza kirafiki

"Kwa umaarufu ulio nao nani asikujue, mimi ni mmoja kati ya shabiki zako" alijibu Caren

"Haha! am humbled! Karibuni ten " Bianca aliwakaribisha kwa mara nyingine na walipokea ukaribisho

Aliwawekea juisi ya matunda kwenye glasi na vitafunwa baadhi kisha kwa kujiongeza yeye pamoja na vijakazi wa nyumba yake waliondoka kwa kisingizio cha kushiba kuwaachia 'privacy'

"Sikudhania kama utakuwa na mke mwenye kujiongeza haha" aliongea kamanda Rama huku akijichekesha

"Anyway sisi ni watu wazima haina haja ya kuzunguka nianze kujitambulisha mimi ni Ramadhan Suleiman Sudi na huyu hapa ni Caren nadhani mlishakutana"

"Ndio miaka mitanobiliyopita.. Hey long time no see!" aliongea Jimmy na kumpa ishara ya kirafiki Caren, naye Caren alirudisha kwa tabasamu la kirafiki

"Mimi ndiye mkuu wa kitengo cha Hidden Supremacy na lengo la kuja hapa ni kutaka....."

"Usiniambie unataka nijiunge kwenye hilo kundi lenu"

"Hilo lilikuwa ni kusudi langu la kwanza lakini nimebadili maamuzi"

"Ooh ni vizuri umebadili maamuzi maana hata kama usingebadili nisingekubali, unaonaje ukaniambia kilichokufanya ubadili maamuzi?"

"Mwanzoni nilidhani utakuwa ni mtaalamu uliyebobea kwenye mapigano kutokana na taarifa niliyopata kwa Caren na mimi huwa napenda kuendeleza vipaji kanma hivyo, na tulipofanya uchaguzi kuhusu wewe nikaja kugundua kwamba unafahamika sana katika ulimwengu wa kihalifu, of course ilikuwa ni taarifa nzuri sana kwa upande wetu na kupata sababu nzuri ya kukufanya uingie kundini hata kama hutaki" aliongea kamanda Rama na kunyanyua glasi yake ya juisi na kuigida yote kama maji

Jimmy alikuwa akimtazama tu huyo kamanda mweusi tii akisubiri muendelezo wa simulizi yake fupi, alijiambia hajawahi kukutana na binadsamu mweusi kama hiyo tangu azaliwe, aliwaza mbali na kudhani pengine wanawake aliokuwa nao wameondoka kwa sababu ya sura yake ngumu na weusi tii

"Lakini ulipotea kwa miaka mitano bila ya kujulikana ulikopotelea" alimalizia

"Kwahiyo kupotea kwangu ndio sababu ya wewe kubadili uamuzi?"

"Hapana"

"Sababu ni ipi?" Jimmy aliuliza akimkazia macho kusubiri jibu

"Tuachane na sababu lengo langu sio kuelezea sababu nimekuja hapa kuomba ushirikiano" aliongea kisha kunyamanza

"Ushirikiano wa nini kamanda mbona unaongea kwa mkato kwanini usitamke hotuba yote kuliko kuniambia kidogo kidogo"

"Nadhani utakuwa unajua kuhusu hivi viumbe vya ajabu ajabu vinavyotesa raia"

"Ndio ni vichaa tu waliopoteza ubinadamu" aliongea Jimmy

"Vyovyote vile tunataka kuwaondoa iliraia waishi kwa amani"

"Sasa mimi nahusikaje kwenye mpango wenu wa kutaka kuwaondoa?"

"Tunataka ushirikiane nasi kwenye huu mpango"

""Nini kinawafanya mdhani labda nitakubali na ninaweza kusaidia? "

" Ukweli uwezo wa kusaidia unao kuhusu wewe kukubali ni ombi letu, chukulia unaweka akiba ya msaada kwetu ukikubali na kutusaidia kwenye huu mpango kama una lolote utakalo ambalo tunaweza kukusaidia tutafanya hivyo"

"Mkuu mbona unanifanya mbuzi wa kafara? mimi ni binadamu tu wa kawaida sasa kutaka mimi kwenda kupambana na hao mashetani ni sawa na kunitoa kafara maana hatujui nini kitajiri, vipi mpango ukishindikana?"

"Ukijiunga nasi hauwezi kusgindwa!"

"Hahaha! Inashangaza sana hatujuani lakini unaniamini kupitiliza, au kwasababu ya kunifuatilia?"

"Kwahiyo ulikuwa unajua nakufatilia lakini ukaamua kujifanya, kwanini?" aliongea kamanda Rama, sio kama hakujua ameshtukiwa bali alitaka sababu

Ukweli Jimmy tangu ile siku alipodili na wale wahuni waliotumwa kumvunja miguu aliweza kugundua anafuariliwa lakini aliamua kujifanya kutoshtukia

" Kwasababu haukuwa na nia mbaya juu yangu" alijibu

"Unajuaje kama hakuwa na nia mbaya, inawezekanaje mtu kujua nia ya mwenzake?" Caren aliuliza

"Aura!" Jimmy alimjibu na kumfanya Kamanda Rama kutabasamu

"Aura anayosambaza muhusika hiubadilika kutokana na hisia na matendo, ni kama harufu ya mvua kabla haijanyesha. Mfano, mtu anayetaka kukuua, husambaza hisia flani zisizo za kawaida. Mapigo ya moyo wako hubadilika, na hata hewa inayokuzunguka huhisi kuwa nzito… kama kiza kinachofunika mwanga taratibu" aliongea na kunyamanza kidogo

"It’s like a feeling of something brushing against your soul" aliendelea akimaanisha "ni kama hisia flani ya kitu kinachogusa nafsi yako"

"Sawa tuseme Aura lakini uliwezaje kujua ni Kamanda Rama na si mwingine?" Caren aliuliza swali jingine

"Unauliza swali ambalo jibu unalo, jibu ni msisimko wa nguvu za kiroho anaotoa, ukweli sikujua kama ni kamanda wako zaidi ya kujua tu kuna mtu ananifatilia nimejua ni kamanda wako sababu msisimko wake naouhisi hauna tofauti na yule aliyekuwa akinifuatiliwa" Jimmy aliongea na kumgeukia kamanda Rama

"Ulifanya makusudi nikugundue si ndio? Ili ukija nitembelea nikutambue?" alimuuliza

"Haha! Kijana inaonekana una akili sana na mtu makini" aliongea kamanda Rama na ghafla tu alizima ule msisimko wa nguvu zake za kichaw

"Kwahiyo unataka kusemaje kamanda?"

"Nachotaka ni kujua chaguo lako, Ndio au hapana"

Jimmy alipiga kimya cha dakika kadhaa akiwaza na kuwazua kisha kumtazama kamanda Rama na tabasamu flani hivi na kunyanyuka pale mezani

"Hata hivyo bila ya msaada wa watu wako kipindi kile pengine nisingekuwa hapa leo hii" kisha alianza kutembea kuelekea juu na alipofika katikati ya ngazi kamanda Rama aliongea

"Nitakutaarifu mambo yakiwa tayari"

Hakuitaji maelezo zaidi kuelewa kwamba Jimmy amekubali kushirikiana nao kwenye mpango ambao Hidden Supremacy walikuwa wakuandaa na taratibu alinyanyuka pamoja na Caren kuondoka mahali hapo

Walipoufikia mlango Caren alisimama ghafla na kugeuza shingo nyuma akiangalia upande wa ngazi juu ambako Jimmy alipotelea na kuangalia kwa, sekunde kadhaa kisha kugeuza shinho na kuzipiga hatua kuondoka.

Jimmy aliweza kumuona Biancalina akiwa amesimama mlangoni mwa chumba chake akimsubiri na mkono wa kulia alikuwa ameshikilia nguo mpya kabisa, haikueleweka alinunua lini

"Mummy usiniambie ulikuwa unanisubiria muda wote huo" aliongea kiutani

"Shika hizi nguo ukabadili sasahivi" aliongea Bianca akimpatia nguo hizo

"Mummy kuna ulazima wakuvaa hizi nguo? mbona hata hapa nimependeza tu" aliongea Jimmy

"Darling bhana nishakwambia sipendi tabia yako ya kunikatalia vitu vidogo vidogo" aliongea huku akinuna na kumnyooshea nguo

Jimmy hakuwa jinsi aliona ni bora tu akubali kuliko kumkasirisha bila sababu za msingi maana ni jana tu hapo alitoka ku'confess alijiambia sasa kama alisema anampenda zaidi ya chocolate halafu amkasirishe si ataonekana muongo?

Baada ya Jimmy kuzipokea nguo hizo Bianca alifurahi moyoni na kumpiga busu la hatraka shavuni na kukimbilia chumbani kwake ambapo hakukuwa mbali na chumba cha Jimmy

Jimmy aliganda kwa sekunde kadhaa akiwa na tabasamu pana usoni huku akihisi mtekenyo kwenye moyo wake, hapana sio moyo tubali mwili mzima

"Sometimes, love surprises you when you least expect it… like now." alijiongelesha akimaanisha "muda mwingine upendo hukushangaza bila kutarajia.. Kama sasa hivi" na kuingia zake ndani

Dakika chache tu alitoka chumbani akiwa amebadili nguo na kuvaa zile alizopewa na mpenzi wake mpya

Alikuwa amevalia shati kubwa 'oversize' la mikono mifupi rangi ya urujuani(violet), design yake ilikuwa ni ya kipekee sana kama vile gwanda la juu la kijeshi maalum kwa jenerali, lakini halikuwa gwanda

Pia alivaa suruali nyeusi iliyokuwa stable, haikumbana sana wala haikuwa pana sana kifupi ilikuwa stable. Na miguuni alipigilia rubber safi nyeupe kama theluji kampuni ya Nike

Kwa staili hiyo ya mavazi Jimmy alitokelezea haswaa yaani alipendeza kinoma ukijumlisha na utanashati wake na mwili wake ndio kabisa hakuelezeka kwa maneno

Mdogo mdogo alishuka chini na kwenda zake sebuleni na kukaa kwenye sofa akimsubiri Bianca na kama mjuavyo tabia za wanawake kuchukua muda mrefu kujiandaa ilimbidi tu kuangalia Tv kusogeza muda

Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa hatimae aliweza kusikia hatua za miguu zikishuka na anageuza shingo yake kuangalia anakutana na bibie amepiga sare sawa na yake na alionekana kama tomboy fulani hivi

Itoshe kusema alipendeza kwelikweli, uzuri wake wa uso wake haukuhitaji make up kuupamba bali ulijidhihirisha wenyewe yaani ule uzuri wa asili

Kwenye macho ya Jimmy Biancalina alionekana kama vile mgeni kwake na muda wote alikuwa akimkodolea macho kama vile hakuwahi kumuona hapo kabla na mpaka Bianca anamkaribia ndio anashtuka kutoka kwenye kuzubaa. Kwa kizungu tunasema "he was in a daze"

"Mummy ni wewe kweli?" aliuliza kama vile haamini macho yake

"Nimependeza eeh!"

"Loh! For sure umependeza ni kama ndoto iliyosukwa kwa mkusanyiko wa nyota na mwezi ikawa halisi, yaani uzuri wako hauonekani tu, unahisiwa! Like a silent melody that plays in the soul." Jimmy alimwaga sifa kitaalamu sana akichanga kingereza na kiswahili

Bianca alisikia raha kusifiwa sio airi, japo hakuonyesha lakini alifurahi mno!

"Ni kama malkia asiyehitaji taji kujulikana. Na macho yako… ni kama galaksi mbili" aliendelea

"Inatosha" Bianca alianza kupatwa na aibu huku akiangalia chini

"Hehe mbona unanionea aibu? Lakini ndio unavyozidi kuvutia"

"Aah..." Bianca alitaka kuongea Jimmy akamuwahi

"Basi nitaacha..... My queen" aliongea akimpa ishara atangulie kama mfalme amfanyiavyo malkia

Bianca alitoa tabasamu kama la malaika na kutangulia kisha Jimmy akafuata na kumkaribia sawa na walipofika mlangoni Jimmy kama gentleman vile alimfungulia mlango na mrembo Bianca kupita

Walienda mpaka garage ya magari ambapo walimkuta Zuhura na walinzi wenzake wakimsubiri

"Zuhura leo hatutaongozana" Bianca alimtaarify mlinzi wake

"Lakini madam usalama wako ni muhimu isitoshe wewe ni celebrity utahitaji msaada paparazzi wanapojitokeza"

"Usiwe na wasiwasi nipo na Jimmy"

"Lakini madam huu ni wajibu wangu sio kwamba simuamini..."

"Nipo salama Zuhura leo sihitaji kuongozana na walinzi nahitaji uhuru na mume wangu"

Paah! Moyo wa Jimmy ulidunda na kuendelea kudunda mpaka ukadundika neno "mume wangu" hakulitegemea kulisikia mapema hivyo tena wakati kama huo mbele ya walinzi, ila hakujali sana kuhusu walinzi alipatwa na ile hisia ya kuitwa mume wangu kwa mara ya kwanza yaani jana love confession kesho yake ambayo ndio hiyo anaitwa mume wangu!

Hata hivyo alifurahi mnooo tena mno! Sura yake ilikuwa inang'aa kwa tabasamu kwa kuitwa mume, hata kama hawakufunga ndoa ila alifurahi sana kusikia hivyo

"Darling unajua kuendesha gari?" Bianca alimuuliza Jimmy ambaye alikuwa hajasikia, alikuwa mbali sana kimawazo akitabasamu bila ya kueleweka anawaza nini

"Hey.. Wewe.. Darling!" aliita na Jimmy alishtuka na kutoka kwenye mawazo na kumuangalia Bianca

"Naam mke wangu"

"Nimekuuliza unajua kuendesha gari"

"Ndio ndio mimi ni mtaalamu sana usiwaze" aliongea na Bianca aliingiza mkono kwenye suruali na kutoa funguo ya gari kisha kumpatia

Jimmy baada ya kupokea funguo alienda mfungulia mlango wa gari husika siti ya mbele ya abiria na baada ya Bianca kuingia alifumga na kumtolea tabasanu Zuhura

"Ondoa wasiwasi yuko salama" kisha alienda mlanfo wa dereva na kuingia. Dakika moja ilitosha kuliondoa gari hilo ndani ya nyumba na sasa lilikuwa barabarani likichanja mbuga kwa mwendo mtulivu

END OF SEASON ONE!.... THE RHYTHM CONTINUES.... 🔥
 
Kikwazo kikubwa ni mtaji. Watunzi wetu wanatunga kwa kwa kuweka vitu ghali sana kwa maandishi, sasa kwenye filamu unatakiwa uhalisia kwa kiasi fulani uonekane. Mfano, eti Cid akaja na gari Escalade ya milioni mia sita. Mara ya milioni mia tano. Kwenye filamu atazitoa wapi?
Nimecheka kinoma🤣🤣🤣
 
Hakika. Ila Ni ya kufanyia editing tu! Huwa wanazingua hata kuwapa majina wahusika. Wanapeana majina ambayo hata midomo yao inaonesha uzito kuyaita, "Wee Scanscastus unaitwa na Kendrick...." Wakati mtaani kwetu kuna Juma, John, Dimoso, Chacha, Chuma, Kidawa, nk...

Upuuzi kabisa.
🤣🤣🤣🤣Scanscastus
 
SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 26: Someone worth admiring for

Don mswahili pia alikuwa akipambana ili kupata pesa ya kuweza kula na kuishi vizuri isitoshe yeye pia alikuwa ni yatima na vilevile alikuwa akimuingizia kipato boss wake aliyemtoa mtaani

Yeye alikuwa akipigana hadi kuua kabisa wavulana wenzake ambao wengi wao alikuwa amewazidi umri na kama zifa kuwaua aliwajeruhi vibaya mno yote hayo ni ili kumtia hasara boss wa hao watoto na kupata bonus kutoka kwa boss wake, ilikuwa ni kwa pambano moja mkwanja ni millioni mia nne ambapo asilimia ishirini ni kwa mpiganaji na nyingine inayobaki ni kwenda kwa boss wake

Sasa fikiria asilimia ishirini ya millioni mia nne ni sawa na millioni themanini na ni pesa nyingi sana kwa mvulana wa miaka kumi na saba na hapo bado kupewa bonus kutoka kwa boss kubwa hivyo aliendeshwa na tamaa zaidi kiasi cha kutokuwa na huruma

Lakini siku ambaya aliingia ulingoni kupambana na Jimmy ndiyo siku ambayo alielewa maana halisi ya ghadhabu kuu, alichezea mkung'uto mtakatifu kutoka kwa mvulana mdogo kiumri kwake

Bahati nzuri Jimmy hakuwa ni muuaji na hakuwa hapo kwaajili ya kuua bali kujiimarisha kimapigano lakini jambo la uhakika alitaka amuonjeshe ladha halisi ya maumivu, ni kama alikuwa akiwalipizia wale wavulana waliouawa na mikono ya mswahili huyo, alimpiga na kumjeruhi vibaya sana na kumtegua tegua mifupa ya mwili wake

Na tangu mpambano ule mswahili huyo aliweka tamaa pembeni na kuwa na huruma kidogo na katika miaka saba ya kudumu kwenye mapambano hayo hatimae Jimmy alistaafu na kutoonekana tena mpaka siku hiyo wanakutana kwa mara nyingine tena

Ukweli sababu ya tabia ya Jimmy kulala nyakati za mchana ni kwasababu usiku alikuwa katika ulimwengu huo, alikuwa akiwavizia wanafamilia wake walale ndipo atoroke na kurudi mapema kabla hawajaamka na kutomkuta, na ni sababu nyingine ya kutotaka kwenda kanisani, ni kwasababu ya kuhisi hatia, ile hatia ya kujeruhi binadamu wenzake, ile hatia ya kushuhudia binadamu mwenzake akidhulumiwa uhai mbele ya macho yake bila kufanya chochote na ndio maana anathamini sana uhai na maisha ya mtu.

"Sikufikiria kama wewe ndio Jimmy isitoshe hatujuani majina yetu halisi, ukweli ni kwamba nilipokea kiasi kikubwa cha pesa kutoka kwa mteja wangu na kuniambia atamleta mahali hapa kutaka nimshushie kipigo na kumvunja miguu, nilishangaa kwa kiasi chote kile alitaka tu nimvunje muhusika mguu ndio maana nikataka kuona ni mtu gani huyo ambaye miguu yake ina thamani ya millioni sabini" aliongea Don mswahili

"Kumbe miguu yangu ina thamani kubwa hivyo" Jimmy aliongea

"Sikutegemea kama utakuwa ni wewe"

"Unaonaje ukanitumia nusu ya hiyo hela"

"Acha masikhara Triple"

"Masikhara ya nini? Miguu ni yako? Isitoshe watu wako wamenitoa kwenye starehe yangu ya kula na kunikalisha njaa"

"Aidha nikudunde na wewe au unitumie hiyo nusu uchaguzi ni wako" Jimmy aliongea kauli ya kibabe

Don mswahili alihisi ubaridi ukisambaa kwenye uti wake wa mgongo na kutoa tabasamu la uchungu ilionekana yule triple wa miaka ile bado hajabadilika tabia ni yule yule tu aliyemjua yeye

Alikuwa ni mbabe haijalishi alikuwa na roho nzuri au lah, hata kams angekuwa na roho nzuri, haitaondoa ule ubabe

"Ni zile zile au?" aliuliza Don mswahili akimaanisha za account ya blockchain na Jimmy alitingisha kichwa kukubaliana nae

Ili ieleweke kirahisi vhukulia blockchain akaunti kama sanduku la siri la kidijitali, hakuna majina ya mtumiaji, sura wala taarifa yoyote kumuhusu ni code tu, Na ngumu ku-hack na hakuna benki wala serikali inayoweza kuingilia. ni baina ya mtu na mtu, na ndio hutumiwa kwenye ulimwengu huo wa siri, kwa lugha nyingine unaweza kuita "ghost bank"

Na ndio sababu hutumiwa sana kwenye ulimwengu wa kihalifu, zipo sababu nyingi tu ila sina haja ya kuziongelea

Kuhusu Jimmy kuwa na blockchain akaunti ni kupitia mzee Momochi aliweza kuwa nayo, yule mzee myahudi alichofanya ni kumrithisha mpaka na blockchain akaunti ambayo ilikuwa imejaa pesa na pia katika mapambano alikuwa anapiga pesa sana bila Mzee momochi kumchuna hata mia, kifupi ni kwamba Jimmy alikuwa ni tajiri ambaye anafosi kuonekana maskini na licha ya utajiri wake bado anamchuna Don mswahili nusu ya pesa na wala mswahili hakuwa na pingamizi, hio ndio maana halisi ya ubabe wa Jimmy

Baada ya Don mswahili kukubali Jimmy hakutaka kuendelea kubaki hapo na alianza kuondoka

"Hey Triple subiri" Don aliita na Jimmy kumgeukia

"Unaonaje nikikupa lift mpaka unapotaka kufika?" aliongea

"Haina haja nitatembea" aliongea Jimmy na kuendelea kutembea zake akimuacha Don mswahili na dereva wake wakimuangalia tu mpaka anapotelea mbele ya macho yao

"Boss yule ni nani mbona unamuogopa?" dereva na kumfanye Don mswahili amkate jicho kali mpaka dereva alihisi kutetemeka

"Boss nisamehe kwa kurupuka kwangu" aliongea haraka haraka huku akiinama chini

"Huna haja ya kuwa hivyo na nitakujibu swali lako" aliongea Don mswahili na kupiga kimya cha muda kana kwamba akiusubiri ulimwengu wote ukae kimya ili aongee

"He is someone worth admiring for his strength and kindness" aliongea akimaanisha "ni mtu anayestahili kusifiwa kwa uwezo wake na fadhili" na kutulia akiangalia angani kama anakumbuka matukio kadhaa ya nyuma na baada ya kutulia kwa dakika kadhaa alishusha kichwa chake kutoka juu na kuangalia jumba ambalo bila shaka ndipo watu wake walipo

Alitembea kuelekea huko huku nyuma akifuatwa na dereva wake na alipoinhia tu aliweza kuwaona watu wake wakijinyanyua kwa tabu sana na aliishia kusikitika tu

°°°°°°°°°°

Jimmy alitembea zaidi ya kilomita 20 aliweza kuona taksi na aliona sio mbaya akipanda, ukweli sio kwamba alikuwa amevhoka, hapana ni kwasababu njaa ilikuwa inamsumbua na mtu kama yeye kusafiri umbali wote huo kwa miguu ni kawaida sana isitoshe mwanajeshi aliyepitia mafunzo ana uwezo wa kutembea zaidi ya kilomita sitini ndipo ahisi uchovu

Kingine pingu iliyoko mkononi ilikuwa haipo tena na haikueleweka imeenda wapi, hata mimi mtunzi sijui.

Alidandia taksi na kumuelekeza pa kufikia na dereva alimpeleka mahali husika na ndani ya dakika kadhaa walifika

Taksi hilo liliishia nje ya uzio mkubwa na Jimmy aliekuwa ndani ya gari alianza kuingiza mkono mfukoni lakini alikuja kugundua hana hela na kuishia kutoa tabasamu

Uzuri alikuwa amefika nyumbani hivyo alimwambia dereva amsubiri nje anakwennda kufata nauli yake

"How much driver?" Jimmy alimuuliza akimaanisha ni kiasi gani isitoshe dereva alikuwa ni mzungu na tangu muda apande taksi ilikuwa ni mwendo wa ngoma za kizungu tu hivyo aliona sio mbaya akiongea nae kizungu

"25,000 shilling my boss" alijibu na Jimmy aliisha kumuangalia tu na kujiambia yaani hazijapita hata dakika kumi mpaka wafike hapo lakini bei yake aaaa inaonekana kuwa kubwa au ni kwasababu ya hilo jumba lililombele ya macho yake na kudhani labda atakuwa ni "new boss man in town?"

"Sawa subiri kidogo hapa nilipo ni myupu mfukoni ngoja niingie ndani nikachukue pesa sikawii sana" alikubaliana na bei kishingo upande

"Eh-eh! Ebu ngoja kwanza hizo ndiyo lugha zenu zenu halafu mnapotea kama maninja, unaingia ndani, unafunga mlsngo poof! Hakuna mtu wala pesa itakayolipwa tunabaki na majuto na billi za petroli" aliongea dereva akionekana hamuamini

Come on unadhani mimi ni performer wa miujiza jukwaani? Ningekuwa hivyo ningekuwa na gari langu binafsi na sio kukushawishi uniamini mbele ya hili jumba kwanza jumba lenyewe sio langu" Jimmy aliongea akijaribu kumshawishi

"Nimekuwa nikiendesha gari tangu Nokia Zinatamba mjini. Nimesikia sana hizi kauli zenu za ‘niamini’ mara nyingi zaidi ya vile nilivyobadilisha matairi zikienda kinyume chake.”

" Kuwa na imani na mimi mzee hizo sio pigo zangu, ningekuwa sitaki kulipia ningekuwa nimeshakuvunjaxshingo kuepuka usumbufu, au huniamini nikuoneshe" Jimmy aliona atumie lugha ngumu sasa maana lugha za kichungaji zilikuwa zinaelekea kumshinda

Yule dereva mzee baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa abiria wake alimtazama kea umakini Jimmy na alipokutana na macho yasiyo na utani kiroho kilianza kumdunda ni ilibidi tu akubaliane naye maana sio kwa hali ile ni kama vile macho ya Jimmy yalikuwa yakisambaza aura flani hivi ya kuogopesha

"Ukweli sina hela mfukoni mzee lakini kimsingi mimi ni mwaminifu sana mzee, kuwa na imani na mimi" Aliongea na kushuka kwenye taksi hilo na kuingia ndani baada ya kufunguliwa geti na mlinzi

Baada ya kuingia ndani ya nyumba sebuleni aliweza kumuona mama yake pamoja na Bianca wakiwa na wasiwasi lakini walipomuona Jimmy wasiwasi wao ulipungua

Bianca alikuwa wa kwanza na kumkimbilia na alipomkaribia alisimama na kumtazama jimmy na walipokutanisha macho ghafla aliangalia pembeni na Jimmy aliishangaa aibu zimetokra wapi

"Si alikuwa ni kauzu huyu na wa kunikasirikia imekuwaje sasahivi amebadilika?" Jimmy alijiwazia kichwani mwake na aliona haina maana kujiuli maswali ya kijinga muda huo na aliona anapaswa kuikamatia fursa kama haijamponyoka

Palepale alichanua mikono yake kwa ishara ya kumkaribisha kwenye kumbatio na Bianca alikuwa akisita sita na Jimmy baada ya kuona hivyo alitamani kucheka kutokana na aibu za mrembo huyo lakini vilevile alimvutia na alimsogelea na kumkumbatia na Bianca hakuleta pingamizi, alitulia tulii

Jimmy alijihisi raha sana mwili wake ulipogusana na wa mrembo huyo, alikuwa akihisi joto mwilini pamoja na hisia za furaha na hisia nyingine zisizoelezeka kwa maneno

Lilikuwa ni kumbatio la nusu dakika na baada ya kutoka kwenye kumbatio hilo alimshika mabegani na kumuangalia usoni, uso wa malaika na kumpa tabasamu

"Baby nimerudi usiwe na wasiwasi sawa?" aliongea Jimmy

Upande wa mama yake licha ya kushuhudia hilo hakufanya chochote zaidi ya kutabasamu ilionekana alikuwa analijua hilo tokea mwanzo na hata Bianca kuishi naye sababu ilikuwa ni hiyo hiyo tu hivyo walikuwa na baraka zake kabisa

"Ulienda wapi?" Bianca alimuuliza

"Babe si nilichukuliwa na polisi kwenda kituoni au umesahau mapema hivyo?" aliongea

"Nilimpigia mama kumuambia alitatue hili lakini tulipata taarifa umewatoroka polisi njiani na hawajui ulipoenda unaona sasa unavyotutia wasiwas?" aliongea Bianca huku sura yake ikianza kubadilika taratibu kutoka kuwa mwenye aibu na kuanza kukasirika

"Na wewe umewaamini nawezaje kuwatoroka ni wamewapa taarifa feki, ukweli wale polisi walipewa hongo kunikamata na kwenda kunipiga ila uzuri kipenzi nina nguvu na mtaalamu nimewashinda" Jimmy aliongea huku akitoa ishara za kurusha ngumu huku uso wake umepambwa na tabasamu. Na jinsi alivyoongea hakuwa serious wala kujali

"Lakini yote hayo si yamesababishwa na wewe usingempiga yule beka na walinzi wake yote haya yasingetokea" aliongea Bianca na sura yenye kuvutia macho licha ya hasira iliyoknekana ni kama vile akikasirika ndivyo anazidi kuwa mrembo

"Usiwe na hasira yule mpuuzi alikuwa anakusumbua na kujifanya mjuaji kwenye nyumba za watu ndio maana nimemshikisha adabu"

"Ndio kumvinja miguu ili uje ukamatwe? , kazi kitutia wasiwasi tu halafu haujalia jinnsi tunavyokuwa na wasiwasi juu yako" aliongea kwa hasira na mutoa mikono ya Jimmy iliyokuwa begani mwake na kuondoka zake kuelekea juu na Jimmy alitaka kumfata lakini alipewa jicho moja kali sana na kubaki tu akimsindikiza na macho

Alijiambia inakuwaje amemkasirisha tena na kuishia kukuna kisogo chake

"Aah mama!" alipiga yowe mara baada ya mama yake kumfinya sikio lake la kushoto na kwenda nae mpaka jikoni

"We mtukutu nasikia hujala chakula subiri hapo nikupashie ule" aliongea mwanamama huyo mara baada ya kuingia nae jikoni na kumuachia sikio lake

"Yaani wewe ni kama baba yako tu kutwa nzima kukasirisha watu yaani umerudi tu siku ya kwanza tu unaleta matatizo hivi unataka kutuua kwa presha za ajabu ajabu?"

"Hapana mama ni vile yule bwana mdogo aliniita mpumbavu mbele ya mke wangu mtarajiwa na kutaka kuleta fujo" aliongea Jimmy

"Ndio mpaka umvunje miguu sasa? Hivi unajua yule ni mtoto wa waziri wa sanaa na michezo?"

"Hata kama angekuwa raisi wa nchi nisingejali" Jimmy aliongea na alishtukia mwiko wa kichwa na kukaa kimya

Alikuwa akimwangalia mama yake na macho ya "mama mbona hunipendi mwanao?" lakini unadhani mama yake angejali, wala!

"Umefikiria kuhusu nini kitampata mke wako mtarajiwa kwenye kazi yake ya usanii? "

"Usiwe na wasiwasi huyo mzee akileta hayo matatizo nitajua namna ya kudili nae kuwa na imani na mwanao" aliomgea huku akijipiga kifua

Mwanamama Mary aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko tu na kuendelea kumuandalia chakula

"Kwanza napanga kumshawishi aachane na hiyo kazi sitaki awe anaongelewa vibaya mtandaoni" aliendelea

"Yaani bado hata humjatuliza na bado ushaanza kuwaza huo upiuuzi kweli wewe ni hasara"

"Aah ndo nini sasa hivyo, kama mama unatakiwa kunisapoti mwanao bhana" aliongea Jimmy huku akijitiisha huruma

"Kama unataka nikusapoti kula kwanza umalize halafu uangalie namna ya kumtuliza mwenzako" alionngea mwanamama huyo na baada ya kumaliza kauli hiyo chakula kilikuwa kimepata moto na kumpakulia na alikula kulekule jikoni

"Mama?" Jimmy aliita na mama yake aliitikia

"Umeishi na Biancalina kwa muda gani mpaka sasa?" alimuuliza

"Tangu aliporudi masomoni na kukuta haupo" alimjibu

"Miaka miwili?" Jimmy aliongea na mama yake alitingisha kichwa

Jimmy alitaka kuongea tena lakini mama yake alimpa ishara anyamanze mpaka amalize ndipo waongee, kifupi Jimmy na mama yake walikuwa ni marafiki wakubwa sana ukiachana na marehemu baba yake

TO BE CONTINUED
Huwa nainjoi sana kazi yako ya uandishi big up 👊👊👊
 
SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 27: Love confession

Ni lisaa limoja limepita tangu jimmy arudi nyumbani na alikuwa ameshamaliza kula na kuzungumza mawili matatu na mamaye na muda huo alikuwa amekaa sebuleni ametulia tuli peke yake

Muda ulikuwa ukisoma saa kumi na moja na nusu, wakati akiwa ametulia ghafla zuhura aliingia ndani na kwenda moja kwa moja mpaka kwa Jimmy na kusimama mbele yake

Upande wa Jimmy alikuwa amekaa kwenye sofa akiegemea na kukunja nne utadhani labda ndiye baba mwenye nyumba, uso wake alikuwa ameuelekeza juu ukiangalia celling board lakini macho yake alikuwa ameyafumba akisikilizia upepo wenye ubaridi utokao kwenye "air conditioner"

Zuhura mara baada ya kusimama mbele ya Jimmy alikuwa akimtazama na sura iliyojaa ukauzu

Jimmy bila kufumbua macho alitabasamu na aliweza kujua nani aliyekuwa mbele yake

"Umeshalipa?" Jimmy aliuliza

"Kwahiyo umefanya makusudi si ndio?" Zuhura aliongea huku amekunja sura yake

"Sio makusudi niliweka matumaini kwako pengine utanisaidia na imekuwa kweli" alijibu na palepale alifumbua macho yake na kumtazama mlinzi huyo alivyomkazia macho

"Kukusaidia? Nani anataka kukusaidia?"

"Lakini si umenisaidia"

"Unawaza mbali sana bwana mdogo, nilichofanya sio kukusaidia bali kutosababisha matatizo zaidi kama unadhani nimekusaidia basi unakosea"

"Vyovyote unavyoona wewe sawa tu ila kwangu mimi naona umenisaidia" aliongea huku akimtolea tabasamu la kirafiki

Zuhura baada ya kusikia hivyo aliishia kukunja ndita na kumtazama kwa sekunde kadhaa kisha kugeuza zake akiondoka mahali hapo

Ukweli ni kwamba Jimmy baada ya kushuka kwenye taxi hakuwa na mpango wa kulipia nauli kabisa, kuhusu kutokuwa na hela mfukoni ni kweli hakudanganya lakini alioni ni bei kichaa kwa safari ya dakika kumi, alichofanya ni kutengeneza mazingira ya Zuhura kulipia, alijua kabisa Zuhura na wenzake walikuwa na nyumba yao ndani ya huo uzio na kamera zote ziliko nje walikuwa wana-access nazo na kwa maana hiyo alichofanya ni kumsubirisha dereva nje ya fensi hiyo na kupitia kamera iliyoko getini wangeweza kuona gari likisubiri nje bila kuondoka

Na kwa masuala za kiusalama basi Zuhura kama kiongozi angetoka na kutaka kujua nini kinaendelea na kwanini taxi hilo limesimama hapo muda mrefu na kweli mahesabu yake yalitiki.

Zuhura baada ya kutoka hapo sebuleni Jimmy naye alinyanyuka ilionekana kukaa hapo sebuleni ni kwasababu alikuwa akisubiri mrejesho. Huyo alipanda ngazi kwenda juu chumbani kwake

Baada ya kuingia alikwenda chumbani kitu cha kwanza kufanya ni kujitupa kitandani kama furushi la mzigo na kutulia tuli na haikuchukua muda alipitiwa na usingizi.

Alikuja kushtuka mara baada ya kusikia mlango wake ukigongwa hodi na kupitia giza lililosambaa chumbani humo alijiongeza na kujua usiku ulishaingia muda tangu akiwa usingizini

"Hodi sir!, Chakula tayari" ilikuwa ni sauti ya kike na bila shaka ilikuwa ni sauti ya Sandra

"Sawa nakuja baadae kidogo" aliongea Jimmy huku akipiga miayo na Sandra baada ya kusikia jibu hilo aliitikia na kuondoka

Jimmy alijinyanyua kivivu na kwenda kuwasha taa kwenye swichi ya ukutani na kisha kuelekea bafuni. Baada ya kama dakika kumi na tano Jimmy aliweza kutoka bafuni akiwa kifua wazi na kufunga taulo jeupe ambalo lilikuwepo huko bafuni

Bila shaka alitoka kuoga na alienda kuketi kitandani na kutulia kidogo, wakati ametulia zake kitandani ghafla mlango wa chumba chake ulifunguliwa na mrembo Bianca aliingia.

Jimmy alijiambis kulikoni jamani hata hodi? Bianca aliishia kumtazama Jimmy ambaye alikuwa ameshasimama tayari

"Chaku....." aliishia njiani

Bianca aliziba mdomo wake mara baada ya kuona mitu kilichomtia hofu na taratibu alianza kumsogelea huku mwili wake ukimtetema japo sio sana.
Jimmy alikuwa ametulia tu asijue nini cha kufanya na kubaki kumuangalia tu mwanamke huyo akimsogelea.

Bianca mara baada ya kumsogelea Jimmy karibu aliunyanyua mkono wake taratibu akitaka kugusa mwili wa Jimmy

"Naweza kugusa?" aliomba ruhusa mwanamke huyo huku macho yake yakiwa yamejaa maji na kuwa na wekundu

Sasa Jimmy aliweza kuelewa kwanini mwanamke huyo yupo hivyo mara baada ya kumuona.
Karika mwili wake kuanzia juu kifuani mpaka kiunoni kulikuwa na alama na makovu kadhaa, zilikuwa ni zile alama za kuchanwa na kutobolewa japo hazikuwa nyingi lakini ilitosha kwa mwanamke yeyote mwenye roho laini kumuonea huruma

Jimmy alitingisha kichwa kumruhusu mwanamke huyo kumgusa na Bianca alianza kugusu zile alama na yale makavu taratibu

"Inauma?" alimuuliza huku akibubujikwa na machozi, Jimmy alitingisha kichwa kukataa kwamba haiumi na kupeleka mmono wake kumfuta machozi

"Hey usilie sasa mummy roho inauma kukuona unalia, yalishapita"

"Imekuwaje ukaumia hivi? " alimuuliza akimwangalia Jimmy usoni

"Ni story ndefu sana siku nitakuelezea kila kitu sawa?"

"Inahusiana na wewe kuondoka kusikojulikanahmm?" alimuuliza Jimmy alikubali

"Jimmy am Sorry" Bianca aliomba msamaha na Jimmy alishangaa na kujiambia kwani amemkosea nini mpaka amuombe msamaha? Lakini hakuwa na jibu

"Hey kwanini unaniomba msamaha ilihali hujanikosea"

"Nisamehe kwa kukufikiria vibaya, nilijua uko na mwanamke wako lakini sikujua... kwamba unapitia magumu" aliongea na kulia kama mtoto, Jimmy mara baada ya kusikia hivyo alitamani kucheka lakini wakati haukuwa sahihi na alimkumbatia mwanamke huyo na kuzipapasa nywele zake akimtuliza

"Hey shhh it's okay.. Wa kulaumiwa ni mimi sikupaswa kukata mawasiliano na ni kawaida kunifikiria hivyo" aliongea

Jimmy alimtuliza alitafuta maneno mazuri-mazuri ya kumtuliza na baada ya dakika kadhaa alifanikiwa lakini hawakutoka kwenye kumbatio

"Unakumbuka nilikwambia nina siri nayotaka kukwambia"

"Ndio nakumbuka" aliitikia

"Unajua, nimekuwa nikishikilia kwa muda mrefu, nikijaribu kutafuta maneno sahihi na wakati unaofaa. Lakini ukweli ni kwamba, hakunaga wakati mzuri hasa wa kumwambia mtu kitu ambacho kinaweza kubadilisha kila kitu" Bianca aliongea akilegeza sauti

"Every time I looked at you And I tried to ignore it, to call it just friendship, to pretend my heart didn’t race when your smile lit up the room...... I LOVE YOU, I REALLY DO" Bianca alifunguka siri yake huku kamoyo kakimdunda lakini aliishia kukunja sura baada ya kumsikia Jimmy akicheka kwa sauti hafifu na kutoka kwenye kumbatio

"Unanicheka?"

"Hapana mummy nimefurah sana kujua unanipenda"

"Muongo unacheka hunipendi" alinuna na kutaka kuondoka lakini Jimmy angemruhusuje kwa mfano?

Aliudaka mkono wake na kumvuta kwake kiasi cha pua zao kukaribiana kugusana huku kila mmoja akihisi pumzi ya mwenzake

"Hapana unakosea mimi nakupenda tena sansaa...I love you, I love love love love you a lot" Jimmy aliongea na sauti yake ya kiume yenye kuushtua moyo wa mwanamke yeyote na Bianca mashavu yake yalianza kuvimba na kutabasamu huku akiangalia chini

"I love you more then chocolate, I love you more than memes, I love you more than rainy days and cozy blankets tight,
More than my favorite hoodie I wear almost every night" mwamba aliendelea kukazia maneno yake na kumfanya Bianca acheke

"Eh kumbe wewe ni sweet talker pia" aliongea huku akitabasamu

"Darling angalie kule" Bianca aliongea akinyoosha kidole sehemu ambayo anamtaka Jimmy aangalie

Jimmy si akageuza shingo bila kujua huo ni mtego Bianca haraka sana aliponyoka kwenye mikono ya Jimmy na kukimbilia mlangoni

"Huh? Babe ndio nini sasa kunikimbia" Jimmy alilalama

"Vaa nguo tukale chakula kinapoa" aliongea huku akimtolea tabasamu la uchokozi

"Unaonaje ukinipa busu kwanza kabla hatujashuka chini"

"No" aliongea huku akimpa akiachia busu la hewan, ni ile ishara ya kuubusu mono kisha kama unaruhusu upendo/busu kuelekea kwa mtu husika hewani

Jimmy kuona vile naye alitoa ushirikiano kama vile audaka upendo huo wa kuuingiza moyoni huku akifanya ishara ya moyo kudunda kwa kasi kwa kutingisha kifua

Jimmy aliishia kushusha pumzi nyingi, alikuwa akifikiria namna ya kuyajenga na mrembo huyo lakini nani angejua majeraha yake yangerahisisha mambo kiasi cha kukiri hisia zao?

Alifurahi sana moyoni na kushukuru mambo yamekuwa mepesi bila kueleweka anamshukuru nani, alianza kuvaa nguo nyepesi tu, T-shirt nyeupe na kaptula nyeusi na alishuka chini sebuleni mpaka kwenye meza ya kula

Alikuta chakula tayari kimewekwa mezani na wote wamekaa, ilionekana walikuwa wakimsubiri ndio waanze kula.
Jimmy alienda kuketi katikati ya mama yake na Bianca

"Leo tunakula nini? " aliuliza huku akimeza mate

Sandra na Aisha walinyanyuka na kuanza kufungua hotpot moja moja na harufu nzuri ya chakula ilisambaa na kufikia kwenye pua ya kila mtu. Kulikuwa na tambi, rosti, nyama ya kuku, mayai, matunda na maziwa ya kutosha, hakika ulikuwa ni msosi wa kueleweka wenye lishe

Ile Sandra anataka kupakua tu Bianca alimzuia

"Nitapakua mimi" aliongea na Sandra bila ubishi alikubaliana na mwajiri wake, upande wa mwanamama Mary alitabasamu na kumgeukia mwanaye akiwa na sura flani hivi ya udadisi, sura yake ilikuwa ikieleza kwamba anataka kutonywa kilichotokea huko juu mpaka baina ya hao wawili mpaka Bianca kuanza kupakulia kila mtu chakula tena akiwa na furaha kabisa

Jimmy alitingisha mabega kwamba hajui na kumuangalia Bianca anayepakua chakula akiwa na tabasamu tele usoni

Bianca aliwapakulia wote chakula na mwisho akajipakulia na yeye kisha kuwanawisha mikono na kukaa. Jimmy kama kawaida yake ya kutokulemba mbele ya chakula alipeleka mkono wake kwenye sahani ya tambi kuchota lakini alishtukia mkono wake ukipigwa na uma wa kulia

"Wewe acha uroho tuombe kwanza" alikuwa ni mwanamama Mary na Jimmy aliishia kujiambia tu mambo ya protokali bhana kuna muda yanaboa lakini hakuwa namna ilibidi akubali tu ila alijiambia kama watamtaka yeye ndiyo afanye sala hatofungua mdomo

"Jimmy ombea chakula" aliongea mwanamama Mary

"Aah mama! mi sijui kuomba bhana" aliongea kwa sauti ya kulalamika

"Nitaombea mimi" aliongea Bianca na wote walimgeukia

"Fumbeni mavho" aliwaambia na wote walifumba macho yao na Bianca alianza kusali na alipomaliza kila mmoja alifumbua macho na kuitikia "Eimen"

Basi shughuli ya kulihudumia tumbo la kila mmoja ilianza, walikuwa mpaka wakashibalakini jambo la kuvutia ni kwamba tangu waanze kula Bianca alikuwa akila kwa furaha sana, matabasamu kila muda mpaka vijakazi na mwanamama Mary wakajiuliza kulikoni?

Baada ya kumaliza kula Sandra na Aisha waliondoa vykombo na kwenda navyo jikoni, kwa upande wa mama yake Jimmy baada ya kumaliza kula aliaga na kwenda kulala isitoshe muda ulikuwa umeenda, ilikuwa ni saa tatu na dakika arobaini

Sebuleni alibaki Jimmy na Bianca wakiwa wamekaa kwenye sofa, kila moja alikaa kwenye sofa tofauti wakitazamana

Mara Bianca alinyanyuka na mumsogelea Jimmy na kumshika akimtaka asimame na mara baada ya Jimmy kusimama alitembea taratibu huku akimshika mkono akielekea upande wa piano iliyokuwa hapo sebuleni na kumkalisha kwenye stuli ndogo mfano wa benchi naye pia alikaa pembeni yake

"Darling" Bianca aliita na sauti yake tamu ya kumtoa nyoka pangoni, na Jimmy kama mwanaume aliitikia

"Unakumbuka ulisema utanifundisha kucheza piano"

"Nakumbuka kila neno uliloniambia tangu nikujue hivyo kuhusu hilo nalikumbuka pia, unataka nikufundishe sasa hivi?" Jimmy aliongea

"Nataka nikuone ukicheza" aliongea Bianca na kumfanya Jimmy atabasamu

"Ilimradi unataka nitacheza kwaajili yako"

"Lakini nataka mtindo special na wa tofauti na ile Moonlight sonata"

"Anything for you my love" aliongea Jimmy na kujiweka tayari kubonyeza lkeys za piano ile lakini kabla ya kuanza, Bianca aliongea

"Subiri" alinyanyuka na kwenda ukutani kwenye swichi kisha kama anapunguza sauti redioni mwanga wa taa hiyo ya sebuleni ulipungua na kuwa mwanga hafifu sana. Baada ya kufanya hivyo alirudi kukaa pembeni ya Jimmy na kuwa tayari kusikiliza

Taratibu mwamba alianza kumuonyesha utaalamu wake kwenye kucheza piano, mdogo mdogo alianza kubonyeza keys za piano hiyo na sauti zenye kuamsha hisia zilianza kusikika

Ulikuwa ni mtindo uitwao "Salut d'Amor" neno la kifaransa lenye maana ya "Salamu ya upendo"
Ni mtindo wa uchezaji piano wa kimapenzi, laini na wenye mvuto wa kihemko, melodi yake ni nyororo kama shairi la muziki ni kama kutuma barua ya mapenzi kupitia sauti.

Muundo wake ni mfupi lakini wenye hisia nyingi. Huanzia taratibu, hupanda kwa nguvu ya mapenzi katikati, kisha hushuka tena kwa upole.

Jimmy ahakuhitaji hata kuimba, Salut d'Amor pekee ilitosha kuelezea ni kwa namna gani anampenda Biancalina, na mpaka anakuja kumaliza Bianca alikuwa amesinzia kichwa chake kikiegemea kwenye bega lake

Jimmy baada ya kugundua mrembo huyo amelala alishusha pumzi nyingi na kumwangalia mwanamke huyo kwa tabasamu kisha taratibu akijitahidi asimuamshe alimtoa kwenye bega lake na kumbeba na alitembea na kupandisha ngazi juu akimpeleka Bianca chumbani kwake

Upande wa Sandra na Aisha walikuwa wakimuangalia Jimmy anapotelea Juu akimbeba Bianca, ilionekana hata wao waliuelewa mziki na kusitisha kazi zao za kuosha vyombo na kusikiliza, ni hakika kwamba Salut d'Amor uliamsha hisia zao

Jimmy aliingia mpaka kwenye chumba cha Biancalina na kwenda kumlaza kitandani taratibu asije kumuasha kisha kumfunika na shuka na kumpiga busu la paji la uso na kumuangalia

Lumbe akilala anazidi kuwa mziri hivi, alijiambia huku akiendelea kumtazama Bianca aliyekuwa amelala na baada ya kwa sekunde kadhaa aliondoka chumbani humo

Baadae Jimmy alionekana akiwa amekaa juu ya 'roof' (paa) ya jumba hilo akiangalia anga lilipendezeshwa na nyota nyingi angani pamoja na mbalamwezi

"Wewe ni nani? Na kwanini upo hapa?" aliongea Jimmy bila kugeuka

TO BE CONTINUED.......
Fire 🔥🔥🔥
 
SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 28: A man of many identities

Nyuma yake kulikuwa na mtu amesimama kwenye paa hiyo, alikuwa ni mzungu mwenye mwili kama wa Roman reigns mcheza mieleka wa Marekani, alikuwa amevaa nguo nzito na kujifunika mitambaa mzito kama vile mmaasai

Mtu huyo alikuwa na nywele ndefu za rasta na mkono wake wa kulia alishika fimbo ndefu sawa na kimo chake na katika fimbo hiyo juu kabisa kulikuwa na jiwe la madini rangi ya kijani limewekwa kiustadi na kuwa ngumu kutoka
Jiwe hilo lilikuwa ni Emerald , jiwe adimu ulimwenguni.

"I am Chitas Chitos D'sullivan and I have come from far away just to meet you and I wish to fight you, you see my purpose is to grow stronger and the only way is to fight opponents who are equal to me or even stronger, only by defeating them I can be stronger.... Though I don't know how strong you are but from what I heard you're equal to me" alijitambulisha akimaanisha yeye ni Chitas Chitos D'sullivan na ametoka mbali sana kuja kumuona na anataka kupigana naye, dhumuni lake ni kuzidi kuwa na nguvu na njia pekee ni kupambana na aliye nguvu sawa au zaidi na kwa kuwashinda ndio atazidi kuwa na nguvu... japokuwa hakujua Jimmy ana ngivu kiasi gani ila kwa alivyosikia atakuwa ni sawa na yeye

Upande wa Jimmy baada ya kusikia utambulisho aliishia kukunja sura yake na kujiambia ni jina gani hilo mbona limekaa kiajabu ajabu? Na alikunja zaidi baada ya kusikia mtu huyo wa kuitwa D'sullivan anataka kupigana na yeye, alijiambia kama sio ugomvi ni nini sasa?

"Sawa bwana Chotisi lakini sijakwambia unitajie jina lako nimekuuliza wewe ni nani?" aliongea Jimmy akiwa bado amekaa akitazama angani

"Sio chotisi ni Chitas Chitos D'sullivan " alimrekebisha huku akitaja majina yake yote

"Whatever your name is Mr Chotisi just tell me who are you? " Jimmy aliongea akimaanisha vyovyote vile jina lako lilivyo bwana Chotisi niambie wewe ni nani

"Kama nilivyokwisha jitambulisha mimi ni....."

"Sijataka kujua jina lako, unaonekana una IQ ndogo sana bwana Chotisi, ninachotaka kusikia ni kusema wewe ni mlozi" Jimmy alimkatisha

Tangu jimmy akiwa sebuleni anacheza piano akiwa na Biancalina aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ya kichawi ikisogelea eneo hilo na ndio maana hakwenda kulala na alipanda juu ya roof kumsubiria mgeni wake

"Unapata wapi udhubutu wa kuniita mlozi ilihali nawe ni mmojawao?" aliongea kwa hasira bwana D'sullivan kiasi cha jiwe la Emerald kutoa mwanga hafifu

Jimmy wala hakushtushwa na hasira ya bwana huyo zaidi ya kushusha kichwa chake kilichokuwa kikiangalia anga na kusimama kisha kumgeukia mtu huyo na kumuangalia kwa macho ya kumchunguza

"Unakosea mimi sio mlozi bali wewe ndiye, inasikitisha sana unashindwa kutofautisha kati ya mlozi na mtu mwenye nguvu zisizo za kawaida bwana chotisi" aliongea Jimmy

"Kwangu mimi wewe ni mchawi tu na huna tofauti na mlozi, kama hukuwa unajua nakwambia tena uchawi ni ulozi na kwa maana hiyo unahesabika kama mlozi"

"Kwahiuo umekubali kwamba wewe ni mlozi si ndio na haupo hapa kutaka kupigana tu si ndio, the fighting speech it was all bullshit right?" Jimmy aliongea huku akimpa tabasamu flani hivi lisiloelezeka

"Mimi sio mlozi na vilevile sio mchawi, mtu mwenye IQ ndogo kama wewe huwezi kunielewa, siku zote watu waliobarikiwa kuwa na nguvu ambazo ni nje ya uwezo wa kibinadamu huishia kuitwa wachawi, mnashindwa kujua kuwa hizo ni baraka. Sio kila mwenye nguvu ni mchawi na sio kila mchawi mwenye nguvu, sio kila mchawi ni mlozi na sio kila mlozi ni uchawi"Jimmy alinyamanza kidogo kisha kuendelea

"Nyinyi ndio mnaochafua neno" uchawi", neno uchawi halina tafsiri halisi na kwa wengi uchawi ni nguvu ila ni kwa sababu ya kunguni kama nyie mnafanya neno uchawi kila lisikiwapo inaonenakana ni laana

Sababu yenyewe ni ulozi, ulozi husababishwa na tamaa, wivu na chuki za kijinga ni Pale mtu anapotumia nguvu za kichawi kwa makusudi yoyote yale mabaya. na hapo ulipo umekuja sio kwasababu ya kupambana bali kuna kitu unakitaka kutoka kwangu si ndio?" Jimmy aliuliza

"Kama nilivyosikia una mdomo sana kijana, ni vile una kitu cha thamani sana ambacho nimetokea kukihitaji sana, ni kitabu ulichonacho chenye siri nyingi na kupitia hiko kitabu pengine naweza kuwa na nguvu zaidi" aliongea D'sullivan

"Mbona hamtaki kuniacha nikatulia kwa, amani, nilishasema na ninasema tena sina kitabu" aliongea Jimmy

"Mimi sio mjinga na wala si mtoto na usidhani kama sijui kuhusu wewe, moja ya sifa nilizozisikia ni kwamba wewe ni muongo kumzidi hata shetani" aliongea D'sullivan

"Umesema umesikia na hujanishuhudia hujui kama unajitafutia kesi ya kunisingizia mashtaka yasiyo ya kweli? Aya tuseme ninacho na sitaki kukupatia kwahiyo unanilazimisha?"

"Kama ni hivyo basi sina budi kutumia nguvu. kwenye huu ulimwengu mwenye kisu kila ndio hula nyama" aliongea bwana chitas na kugonga fimbo yake chini akisambaza nguvu za kichawi

Jimmy baada ya kuhisi msisimko huo aliishia kumeza mate yake tu na kujiambia mbona nguvu imeongezeka tofauti na mwanzo

"Hey bwana chotisi watu wamelala unaonaje tukienda mahali penye uwazi tukaone nani mwenye kisu kikali, ukinishinda nitakupa kitabu unachokitaka` aliongea Jimmy huku akimwangalia D'sullivan

" Usiwe na shaka mimi ni mkweli sana" aliongea na palepale midomo yake ilicheza kama ananena kilugha na ghafla kitabu kikatokezea kwenye mikono yake kichawi

"Si ndo hichi unachokitaka?" aliuliza Jimmy huku akikirusha juu kitabu kile na kukidaka kama vile kitenesi. Na mara ya tatu tu kurusha kikapotea hewani

Bwana D'sullivan mara baada ya kuona kile kitabu tamaa ilimzidia na alitoa tabasamu la uovu

Dakika moja mbele Jimmy na D'sullivan walikuws wamesimama ufukweni mwa bahari wakitazamana wakiachana umbali wa mita ishirini

Kulikuwa na giza kubwa usiku huo pengine kama sio mwanga wa mwezi umulikao angani ingekuwa shida kuona kwa macho ya kawaida. Kulikuwa na upepo mkali ukivuma ulioambatana na baridi kali usiku huo wa saa tano na dakika kadhaa

Jimmy alikuwa vile vile hakubadili mavazi niT-sheti na kaptula na alikuwa peku lakini hakuonekana kuadhirika na baridi, zaidi alisimama wima mikono yake akiichomeka mifuko akipigwa na upepo

Upande wa D'sullivan alikuwa amesimama na ule mtandio mzito ambao alikuwa amejitandika aliuvua na sasa kubaki kifua wazi, mwili wake wenye misuli na mishipa iliyotuna ulionekana. Kyanzia kifuani mpaka kiunoni mwili ulikuwa umechafukwa na michoro ya ajabu ajabu isiyoeleweka

Aliipiga fimbo yake chini na kuusimamisha kwenye mchanga na kukunja mikono yake akimwangalia Jimmy ambaye muda huo alikuwa anauchangamsha mwili akiriukaruka kidogo na kunyoosjha miguu na mikno na baada ya kumaliza alitulia na kumnyooshea mkono D'sullivan akimpa ishara ya kumkaribisha kwenye pambano yaani awe wa kwanza kufanya shambulizi

D'sullivan baada ya kuona hivyo alitabasamu na kuona kama Jimmy anamdharau, kufumba na kufumbua huyu hapa mbele Jimmy huku ngumi yake nzito yenye ujazo wa kutosha ikitangulia mbele kiasi cha kutoa sauti kama vile anga limechanika

Ilikuwa ni spidi ya ajabu sana ambayo hata Jimmy mwenyewe alishangaa lakini kwa spidi yake aliweza kupangusa ngumi hiyo iliyokuwa ikimlenga usoni kwa kukinga mikono yake mtindo wa X na sauti ya mgongano kati ya ngumi na mikono ya Jimmy ilisikika

Kutokana na ngumi hiyo kuwa na kasi na nguvu Jimmy aliishia kurushwa nyuma kwa mita tano lakini aliweza kutua kwa miguu na kutafuta balansi, hajakaa sawa shambulio jingine lilikuwa mbele yake, Dsullivan aliruka akitanguliza goti kumlenga kidevu, ilikuwa ni staili ya muay thay ijulikanayo kama "Flying knee"

Ni shambulio lenye madhara kama litampata kisawasawa mlengwa ukizingatia D'sullivan alikuwa na mwili mgumu wa mazoezi

Jimmy hakutoa mikono yake aliyokuwa amekinga shambulizi la mwanzo na badala yake alikaza na goto lile la, D'sullivan liligongana tena na mikono ya Jimmy ikitoa na mlio wa mifupa kugongana na Jimmy kuriudi tena nyuma hatua sita

Jimmy ni binadamu na si roboti hivyo maumivu yalimhusu hata kama alikuwa na nguvu zisizo za kawaida bado mwili wake ni wa nyama lakini huo haukuwa muda wa kusikilizia maumivu aliishia kung'ata meno yake kujikaza akivumilia

"Bado unataka nishambulie tena?" D'sullivan aliongea kwa dharau

"Damn! Licha ya uzito wa mwili anaonekana kuwa mwepesi" alijiwazia na kuweka sura ya tabasamu

"Hapana safari hii ni zamu yangu" aliongea Jimmy huku akimkazia macho na palepale kwa spidi ya ajabu alikuwa tayari ameshamsogelea D'sullivan akisindikiza ngumi ya kifua

Upande wa D'sullivan alikuwa ametegemea hilo hivyo alijipanga kupangua shambulizi hilo lakini hata ya ngumi kumfikia alishtukia ngumi ya tumbo na mkono mwingine wa Jimmy

Lilikuwa ni shambulizi la kushtukiza, ulikuwa ni mtego wa kumfanya aweke umakini kwenye shambulizi linalokuja huku kwa wakati mmoja akiwa amepanga shambulizi jingine eneo tofauti la mwili

Ilikuwa ni ngumi takatifu sana kiasi cha kumtoa, D'sullivan macho yanayoashiria maumivu makali, ni kama vile ngumi ya Jimmy ilibeba nguvu flani, maana kwa mwili wa Jimmy shambulizi lile ilikuwa ni ngumu kumsababishia maumivu kiasi kile lakini ukweli ilikuwa ni ngumi kama ngumi isiyobeba nguvu yoyote ya ajabu

Ni hakika pigo lile liliweza kumrusha nyuma D'sullivan mita kadhaa, hakutaka kumuachia nafasi ya kupumua kufumba na kufumbua Jimmy huyu hapa mbele ya macho yake na kuanza kutandikwa ngumi zisizo na mpangilio maalumu wala idadi, kila ngumi iliyogusa mwili wake ilikuwa ni kama chuma kugongana na misuli na mifupa yake na pigo la mwisho lililomrusha na kumdondosha chini lilikuwa ni teke takatifu la roundhouse kiasi cha D'sullivan kutema damu na kurushwa kwenda kuangukia fimbo yake aliyokuwa ameichomeka ardhini

"Nilidhani utakuwa mtaalamu kwenye masuala ya mapigano pia ila unaonekana una mbinu za kuungaunga, nyie walozi mnaendeshwa sana na tamaa mpaka inakera mkishapata mambinu kadhaa ndio mnajiona wafalme wa dunia na kutaka kutawala walio chini yenu" aliongea huku akisikitika

Baada ya Chitas Chitos D'sullivan kupokea mapigo yale aliishia kuugulia maumivu kwa nusu dakika na kibishi sana alijinyanyua na kuanza kucheka kama kichaa, meno yake yaliyochafukwa na damu yote yakiwa nje na kuendelea kucheka tu kiasi cha kupaaliwa na mate yake na ndipo kicheko chake kilikoma kisha alimtazama Jimmy kwa sura yake yenye tabasamu ovu

"Ni wakati sasa" D'sullivan aliongea akimwacha Jimmy akijiuliza ni wakati wa nini?
D'sullivan aliinua fimbo yake na kuichomeka tena ardhini na kuanza kuneno kwa lugha na mwanga wa kijani wa jiwe la Emerald uling'aa na mawingu ya usiku angani yalitanda na kuufunika mwezi na giza kuongezeka

"Velari omnisi! Bend and kneel, oh crumbling soul!" aliongea D'sullivan kwa kuamrisha akimaanisha "Inama na piga magoti oh nafsi anguka!"

Lakini alishangaa kuona maneno yake hayafanyi kazi mbele ya Jimmy, ni kama vile alikuwa akimpigia mbuzi gitaa akitegemea mbuzi kucheza lakini matokeo yakawa ndivyo sivyo

"What the... How come?" alishangaa sana akimaanisha inakuwaje

"Haiwezekani kabisa wewe kulingana na msisimko wa kiroho unaotoa utakuwa kwenye levo ya pili ya uchawi wa mabadiliko lakini kwanini manuio yangu hayafanyi kazi?" aliongea huku taratibu hofu ikimvaa

"Because am not a fragile mind like you" Jimmy aliongea akimaanisha kwasababu mimi sio fragile mind(akili dhaifu) kama wewe"
Fragile mind yaani akili dhaifu ni ngazi ya kwanza ya nguvu ya willpower naye hakuwa ngazi hiyo alikuwa ni zaidi na ndio maana shambulizi la kiroho la kunena halikuwa na athari kwake

Licha ya D'sullivan kuweza kujua ngazi ya uchawi aliyokuwa nayo Jimmy haikumaanisha naye ni mchawi mkuu pia, hapana yeye alikuwa ni mlozi(Enchanter), ameweza kujua ngazi kutokana na uzoefu wake wa kutofautisha msisimko wa nguvu za kiroho kwa sorcerers isitoshe Jimmy hakuwa mchawi pekee. kuna tofauti kati ya mchawi mkuu na mlozi, kwa Enchanter nguvu zake ni Anatumia nguvu za akili, maneno ya kichawi, na udanganyifu wa nafsi, anafunga akili ya watu, kuharibu fikra, au kulazimisha matendo ya viumbe wengine kupitia maneno au ishara.

Na maneno yake ya kichawi aliyoyaneno ni katika kuitawala akili ya Jimmy na kumlazimisha nafsi yake impigie magoti lakini ikashindikana yote hayo ni kwasababu ya willpower aliyokuwa nayo Jimmy

Hata kama angekuwa na nguvu nyingi za kichawi na kiroho asingefua dafu kumtawala, mchawi anaweza kuwa na nguvu kjmzidi mwenzie lakini kama willpower yake ni dhaifu na kwa mwenye kuzidiwa nguvu kuwa na willpower dhabiti basi ni sawa kusema huyo mwenye nguvu za kiroho nguvu zake hazitakuwa na athari kwa mlengwa labda kama watapigana ana kwa ana mwenye nguvu kuwa ni mtaalamu anaweza kushinda lakina kiroho hawezi kumdhuru

"I have completed the willpower circle you fool" aliongea Jimmy akimaanisha "Nimekamilisha mzunguko wa mapenzi ya dhamira(willpower) we mjinga"

"Wewe ni.... nani?"

"Si umesema umesikia habari zangu nikajua labda utanijua jina langu pia ila inaonekana hata taarifa ni za kuunga" aliongea

"Who the hell are you?" alirudia swali lake tena

"Me? I am a man of many identities, To some, I am the devil. To others, an angel. To many, a fool. In truth, I have no name beyond the one fate assigned me at birth. I am neither salvation nor damnation, only the mirror of what others dare to believe. Inshort I don't care who Iam or might be" (Kwa baadhi, mimi ni shetani. Kwa wengine, malaika. Kwa wengi, mpumbavu. Ukweli ni kwamba sina jina zaidi ya lile ambalo majaliwa yalinitunuku nilipozaliwa. Mimi si wokovu wala laana bali ni kioo cha kile ambacho wengine wanathubutu kuamini, kifupi sijali mimi ni nani au nitakuwa nani)

But to you... I am your.... worst nightmare.... Gravitus inversus!" aliongea na kunena na ghafla nguvu mkandsmizo ilianza kumkandamiza D'sullivan kwenda chini na kupiga magoti na bado alikuwa akishindana na nguvu hiyo akijitahidi kunyanyuka kupitia msaada wa fimbo yake

" Increase" Jimmy alinena na ile nguvu ya mkandamizo ilio ngezeka mara tatu na D'sullivan alishindwa kuhimili

TO BE CONTINUED......
Kama naangalia movie flan hv ya fantasy
 
SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 29: Shadowbound

Nguvu ilikuwa ni kubwa sana kwa D'sullivan kuhimili kiasi kwamba alianza kupiga mayowe maana mkandamizo huo ulikuwa ukimuathiri mifupa na misuli yake iliyokaza kushindana na nguvu hiyo.

Licha ya kuugulia maumivu hakuonekana kukata tamaa na alianza kunena kilugha tena kwa tabu sana na kadri muda ulivyozidi kusonga lile jiwe la kijani ghafla likaanza kubadilika rangi kutoka kijani kwenda nyeusi na ghafla moshi mweusi ulitoka kwenye jiwe hilo na kumzingira D'sullivan na ile nguvu ya mkandamizo ikawa haina athari kwake.

Ile michoro iliyokuwa mwilini mwake ilizidi kuongeza mithili ya nyoka atembeae na kusambaa mwili mzima kuanzia kichwani mpaka chini miguuni

"The JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala" Jimmy alishangaa na kujiambia ni nini hiko

"Hahaha ulidhani nitakubali kuwa mnyonge? Hahaha.. Haha.. Koh koh!" aliongea na kucheka kama chizi kiasi vha kupaaliwa

Jimmy kuona mkandamizo huo haumuathiri aliamuru na nguvu hiyo ikakoma hapo hapo. Hio ni moja kati ya sifa za Sorcerers yaani amri, kwao ni kuamuru na sio kuomba, na nguvu zao zinadhihirika kupitia neno la mdomo, linalobeba dhamira ya moyo(willpower) na nguvu ya kiroho. Hutamka, na ulimwengu hutii. Hutamkia hewa, na upepo hubadilika. Kwao, ulimwengu si kitu zaidi ya maandiko yanayosubiri kusomwa.

Katika sanaa ya uchawi wa Sorcerers na Enchanters, hakuna haja ya silaha, wala mihangaiko ya kusujudu kwa miungu. Mdomo wao ndio upanga, lugha yao ndio giza na nuru, na dhamira yao ni kama fataki inayochoma ukweli wa ulimwengu huu. Wanapoongea, hawasemi kwa maneno tu wanashusha matamko yaliyojaa nguvu za kiroho yenye mamlaka.

Na nguvu zao kuu ziko katika mambo manne, ni dhamira(willpower), bila dhamira dhabiti neno linakuwa hewa tupu na ndio maana D'sullivan licha ya kuwa na nguvu lakini matamshi yake hayakufanya kazi, yote ni kwasababu ya kukosa dhamira dhabiti. Pili ni "Conviction" kwa kiswahili tunasema imani ya ndani, Bila imani, neno halina mizizi. Mamlaka ya mchawi mkuu hutegemea zaidi imani yake kuliko nguvu ya mwili na kiroho, tatu ni ulinganifu wa nafsi na ulimwengu Sorcerer hawezi kuamuru kile ambacho hana ulinganifu nacho. Ni lazima moyo wake uwe sambamba na kile anachotaka kubadilisha.

Na mwisho kabisa ni lugha yaani wanatumia lugha ambazo hazijulikani kwa binadamu wa kawaida zenye nguvu za kiroho, hata wakitumia lugha inayotambulika mradi kuna dhamira na imani ya ndani hakuna shida

Hivyo Jimmy alitamka neno la kuamuru hali ile ikome nayo ikakoma na kuanza kujiuliza ni nini hiki kinatokea

Wakati Jimmy anaendelea kushangaa na kujiuliza upande wa D'sullivan hali yake ilianza kubadilika taratibu ule moshi mweusi ulianza kumuingia kupitia puani, mdomoni na masikioni kilikuwa kiitendo cha ajabu kweli

Mara sauti ya ngurumo kama simba aliaye nyikani ilisikika na macho ya D'sullivan yalibadilika na kuwa mekundukama damu na moshi mweusi ulikuwa ukimtoka kupitia michoro ile ya ajabu ni kama vile mwili wake ulikuwa ukitoa mvuke mweusi

Jimmy akili yake ilicheza baada ya kukumbuka kitu na kuishia kulaani ndani kwa ndani

"Pumbavu! huyu mshenzi tamaa ndio imempeka huku aisee huyu zaidi ya pimbi" Jimmy alilaani moyoni mwake

Neno "Shadowbound" ndio lilikuwa likizunguka kichwani mwake baada ya kushuhudia mabadiliko ya D'sullivan yaani alikuwa ni mfungwa wa vivuli

Mara nyingi mtu wa aina hiyo anakuwa ni sawa tu na mtu aliyefanya mkataba na mashetani kumpa nguvu na yeye kumpa nafasi kuishi ndani ya mwili wake kwa gharama ya sehemu ya nafsi yake shetani huyo. anakuwa ni kama kivuli cheusi na ndio mtu huyo huitwa Shadowbound(mfungwa wa kivuli)

"Sikutegemea kama utakuwa na tamaa sana kiasi cha kuuza nafsi yako kwa hilo lishetani, is it worth it?" Jimmy aliongea na kumuulizsa je inastahili?

"Enough of your blah blah blah you damn moron hand over the book!" aliongea kwa kufoka akimaanisha inatosha na blsh blah na amkabidhi kitabu

Jimmy alijiambia hilo halikuwa suala la dhamira tena huyo aliyekuwa mbele yake hakurwa binadamu wa kawaida kabisa, alikuwa akitawaliwa na nguvu za giza za shetani aishiye ndani ya nafsi yake

Msisimko wa nguvu hizo za giza ulikuwa ni mkubwa sana mara tatu, gna giza lilizidi kuongezeka kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele na kuwa shida kwa macho ya Jimmy kuona gizani

"Eyes of the darkness!" (macho ya gizani!) Jimmy aliongea kwa sauti yenye mamlaka na ghafla mboni za macho yake zilibadilika rangi na kuwa bluu hafifu na bila shaka aliweza kuona vizuri kwenye giza

"Simama kivuli cha milele!!" D'sullivan alitamka na ghafla kivuli kikubwa(roho) kikatokezea nyuma yake chenye umbo la miguu ya simba na mikono kama ya mwanadamu

"Funga mwili wake kwa minyororo ya giza!" aliamuru na ghafla kiumbe kile kikapanua mdomo na minyororo mingi ikatokezea ikimsogelea Jimmy kwa kwasi kama mishale yenye kamba na kutaka kumfunga

Unadhani Jimmy angekubali kufungwa kizembe tu bila kufanya chochote? Hapana asingekubali na kwa spidi na utaalamu wa hali ya juu sana aliikwepa minyororo ile kwa kuruka sarakasi nyingi hewani mfululizo kwa ustadi sana na mpaka anaruka ya mwisho hakuna mnyororo ulioweza kumgusa zaidi ya minyororo kujifunga yenyewe

"Fractura Dominus!" Jimmy alitamka neno la kichawi kwa lugha takatifu lenye maana ya kuvunjika na minyororo ile ya giza ikakatikakatika na kupotelea hewani

D'sullivan alikasirika mara baada ya shambulizi lake kushindikana na kudhibitiwa kirahisi alikasirika sana na kutoa shambulizi jingine

"Laana ya waliopotea!.. Shambulieniii!!" aliamuru na ghafla kivuli kile kiliongezeka ukubwa na mdomo kupanuka na fvivuli vingi kama roho za waliokufa vilitokezea kwenye mdomo wa kivuli hiko

Vilikuwa ni vivuli vingi sana na kwa mahesabu ya haraka haraka aliyopiga Jimmy jeshi hilo la vovuli lilikuwa si chini ya roho hamsini za vivuli na aliishia kumaka

"Pumbavu! Nikiendelea kumchekea nitakuja kuishia pabaya sana" aliongea Jimmy na ule muonekano wake wa kuchukulia poa ulibadilika na kuwa makini mno!

Vivuli vilisanza kumvamia kwa kasi na alikuwa akivikwepa na kushambulia lakini alishangaa mashambulizi yake ni kama anapiga hewa na alianza kujicheka alisahau kwamba vivuli hivyo vilikuwa katika mfumo wa roho hivyo havigusiki

Wakati anacheka na kujiongelesha alishtukia ngumi ya kifua iliyomrusha mita kadhaa na shambulizi hilo lilitoka kwenye moja ya roho ya kivuli

"Damn! Dude this ain't fair you know" Jimmy alimlalamikia D'sullivan moyoni akimaanisha hatendi haki

Hajakaa sawa majeshi ya vivuli vilimzingira umbo wa mduara na kumshambulia kwa pamoja kama mazombi wanaogombania nyama kiasi kwamba Jimmy hakuonekana

"Hahaha! What a loser!" D'sullivan alicheka na kufurahia lakini alisita mara baada ya kuhisi kuna kitu hakipo sawa, kulikuwa na ukimya wa ajabu mpaka alihisi moyo wake unavyodunda na aliangalia mahali ambapo Jimmy amefunikwa na roho zile

"Awaken!" ilisikika sauti yenye ghadhabu na mwangaukungu wa bluu ulionekana mahali alipovamiwa Jimmy na ghafla roho zote zilirushwa hewani na kutawanyika nyingine zikitumbukia baharini

Alionekana Jimmy amepiga goti na mguu mmoja huku uso wake ukiangalia chini ametulia tuli kama uso wa bahari. Mwili wake mzima ulikuwa umezingirwa na nishati kama ukungu wa bluu na taratibu aliinua uso wake

Alikuwa akisambaza aura iliyobeba nguvu ya uharibifu kiasi kwamba hakuna roho yoyote ya kivuli iliyothubutu kumsogelea, kwa nguvu aliyokuwa akihisi D'sullivan alikuwa akitetemeka kwa woga kama vile mbwa aliyemuona chatu na kushindwa kufanya chochote zaidi ya kutawaliwa na hofu kuu

"Ni... ni nguvu..gani hii?" aliongea kwa kusita sita

Taratibu Jimmy aliinuka na kusimama wima na kukazia macho umbo la kivuli kikubwa kilicho nyuma ya D'sullivan.

Kivuli kile baada ya kukutanisha macho yake na ya Jimmy kilianza kupiga kelele na kunguruma kana kwamba ameona mlango wa kifo mbele yake

"Burn beyond time, erase the whole dark spirits, Let the end be done!" aliamuru akimaanisha "Teketea, futa kila roho ya giza, mwisho na utimie!"

Ghafla wimbi kubwa la upepo kama kimbunga liliibuka na kusomba roho zote ikiwemo na kile kivuli kikubwa na ndani ya kimbunga hiko ulionekana moto mkali kama wa volcano ukiwaka na makelele ya vilio vya roho hizo vilitawala eneo hilo na ndani ya dakika moja kimbunga hiko kikapotea kwenda chini ardhini isibaki hata roho moja ya kivuli

D'sullivan mzobe mzobe alianguka kwa kuishiwa nguvu mwili, ni dhahiri roho ile ya kivuli ilikuwa ikinyonya nguvu zake za kimwili na roho

Upande wa Jimmy taratibu alirudi katika hali yake ya kawaida na mboni za macho yake pia zilirudi katika rangi yake halisi.
Jimmy alimsogelea D'sullivan aliyelala chini akipumua kwa shida sana na kuchuchumaa

"Nani mwenye kisu kikali?" Jimmy alimuuliza huku akitabasamu

Upande wa D'sullivan alimtazama tu Jimmy huku akipumua kwa taratibu asiweze kumfanya lolote, hakuwa na nguvu hata ya kunyanyua kidole

"How could you?" D'sullivan aliuliza kwa nia njema tu akitaka kujua akimaanisha amewezaje

"You're curious huh?" aliongea Jimmy akimaanisha "una shauku huh?"

"Ukweli ni kwamba sio nguvu inayonibeba bali ni weqe ni kwasababu ulikuwa unapambana ushindwe na sio kushinda" aliongea Jimmy

D'sullivan aliishia kukunja uso wake asielewe Jimmy anamaanisha nini

"Elewa nachomaanisha sio maana ya maneno, ona… uligubikwa na tamaa. Unapigana kwa sababu ya kutaka kupata kitu. ulitaka kuchukua, kumiliki, kupanda juu ya kila mtu hata kama ilibidi uteketeze kila kitu njiani. Lakini nguvu inayotokana na tamaa haidumu

Umepofushwa na tamaa yako kiasi cha kutokujua madhara yake, ulikuwa unapambana ukiendekeza tamaa na sio kutumia akili" aliongea na kusimama

"Anyway muda umeenda sina muda wa kupoteza kuongea na mlozi, usiku mwema kamanda" aliongea Jimmy na kuondoka zake mahali hapo akimuacha D'sullivan taratibu akipoteza uhai

Mpaka kuitwa shadowbound maana yake nafsi yake ilifungamana na roho ya lile shetani hivyo kifo kwa kiumbe kile maana yake ni kifo pia kwa muhusika aliyefungamana nae

Upande huo huo kwa mbali sana alioneka mtu amesimama akitazama na bila shaka alishuhudia kila kitu na mara baada ya Jimmy kuondoka naye aliondoka pia

°°°°°°°°°°

Kama kawaida kukachuka na muda ulikuwa ukisoma saa mbili na dakika kadhaa na katika chumba cha kulala chenye harufu ya kiume Jimmy alionekana bado amelala fofofo

Mwanga wa jua ulipenya ndani ya chumba hiko. Pazia lilikuwa limeachwa wazi kiasi kwamba miale ilimwangukia usoni. Lakini hakuamka… mpaka sauti ya mwanamke iliingilia utulivu huo.

"Darling amka kumekucha, mbona unalala kama umepigwa na radi?" sauti tamu ya Bianca ilisikika

Jimmy alifumbua jicho moja polepole akimwangalia mrembo huyo aliyekuja kumuaribia usingizi wake na sauti yake tamu mpaka kuhisi mtekenyo

"Ugh... kwani saa ngapi sahivi.." Jimmy aliuliza kivivu

"Saa mbili na nusu sahivi amka bhana"

"Mbona mapema hivyo jamani"

"Mapema? Umelala vya kutosha amka" aliongea huku akivuta mkono wa Jimmy lakini alishangaa yeye ndio anavutwa na kuangukia kitandani na kukumbatiwa, alifurukuta lakini wapi, ilishindikana.

"Siwezi kuamka bila kunibusu, babe hivi hujui morning kiss humuondolea mpenzi wako uchovu" Jimmy aliongea huku akimuwekea shavu na kusubiria busu

Biancalina alikuwa akisita sita kutokana na aibu za kike lakini mwisho wa siku ili kujinasua kwenye kumbatio hilo aliishia kutekeleza kile alichoambiwa na ndipo kuachiwa

Jimmy baada ya kupokea busu la asubuhi ni kama vile amezaliwa upya, uchovu wote kwisha pamoja na usingizi na kunyanyuka

"Babe kumbe busu lako lina nguvu hivi, itabidi kila napohisi uchovu uwe unanibless mpenziwo" alitania

"Nakupa dakika kumi uwe chini tayari" aliongea Bianca na kukimbia zake baada ya Jimmy kumpa ishara ya kutaka kumkabata tena na Jimmy aliishia kucheka na kujiambia asubuhi hio imekuwa nzuri sana kwake

Baada ya dakika kumi Jimmy alishuka chini akiwa msafi ameshajiandaa na kwenda kukaa kwenye sofa na kuwasha runinga kisha kutuljia akiburudisha macho yake na nyimbo za bongo fleva mpaka pale ilipokuja video ya Biancalina akiimba nyimbo ya SIO MBAYA

Japokuwa aliisikiliza hakuona video yake na hapo sasa ndipo anaiona na aliishia kujiambia kweli mke wake mtarajiwa ana kipaji sana lakini alikuwa akijiuliza pia, kwanini anahisi hio nyimbo ni kama yeye ndiye anayesemwa lakini aliamua kupotezea

"Darling kifungua kinywa tayari njoo ule" aliongea Bianca ambaye alikuwa anamalizia kuandaa kifungua kinywa mezani akisaidiana na Sandra na Aisha

Alinyanyuka na kwenda zake mezani na kukaa pamoja nao na kupata kifungua kinywa

"Mama tuko wapi?" Jimmy aliuliza

"Ameondoka asubuhi na mapema kwa mjukuu wake" Bianca alijibu na Jimmy alitingisha kichwa chake kumuelewa na kuendelea kunywa chai

"Darling ukimaliza tunaenda shopping sawa?" aliongea Bianca macho yake yakimwangalia Jimmy kwa upole

"Asubuhi yote hii mummy kwanini tusisubiri mchana au jioni, mida hio kunakuwa kumechangamka sana" aliongea Jimmy huku akimtazama kwa tabasamu

Bianca alikunja midomo yake kwa hila, akijifanya kukasirika. "Unajua siipendi hiyo tabia yako ya kunikatalia mambo madogo madogo"

Sura yake tu ilivyo ilimfanya Jimmy atake kucheka lakini alijizuia na kuishia kutoa tabasamu pekee

"Unacheka?"

"Hapana mummy tunaenda sawa? Usikasirike basi" alibembeleza na Bianca alifurahia Jimmy kukubali kwenda naye

Wakati wanaendelea kupata kifungua kinywa Jimmy aliweza kuhisi ujio wa watu wawili lakini alipotezea na kuendelea kula

TO BE CONTINUED........
🔥🔥🔥
 
SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 30: Ugeni uliotarajiwa (expected visit)

Jimmy hisia zake zilikuwa ni sahihi kwani ndani ya sekunde kadhaa ulisikika mlio wa kengele ya mlango wa kuingia sebuleni kuashiria kwamba kuna ugeni muda huo

Aisha alinyanyuka na kwenda kufungua mlango na kuwaona watu wawili wamesimama mlangoni mmoja akwa ni mwanaume mwigine akiwa ni mwanamke. Mwanaume alionekana ni mkubwa kiumri huku mwanamke akiwa ni kijana zaidi

Wageni hao walikuwa wamevaa mavazi ya kawaida, mwanaume ambaye alikuwa ni kamanda Ramadhan alivalia t-shirt rangi ya zambsrau ambayo ilionekana kumbana kwa kiasi chake huku kifua chake na misuli ya mazoezi ikijichora, chini alivalia suruali nyeusi iliyombana na buti za kijeshi nyeusi zilizong'aa kana kwamba zimepakwa mafuta

Upande wa mwanamke alikuwa na asili ya kihabeshi na hakuwa mwingine bali ni Caren, naye alipendeza licha ya kuvalia kawaida kutokana na umbo lake matata. Chuchu saa sita za mrembo huyo zilionkana kusimama haswaa licha ya kuvalia shati kubwa la draft, rangi ya bluu lenye mikono mirefu, pia chini alivaa jinsi nyeusi iliyombana vyema na kuchora hipsi zake pamoja na mzigo wa wastani ulioko nyuma, bila kusahau buti nyeusi pia za doc matterns

"Karibuni ndani" Aisha aliwakaribisha na waliweza kuingia ndani.

"Msiishie kusimama tu hapo karibuni mpate kifungua kinywa haipendezi kwa wageni kula harufu ya misosi" aliongea Jimmy baada ya kuona wanaelekea kukaa sofani

Kama Rama na, Caren mara baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Jimmy walitabasamu na kuelekea mezani walikokaribishwa

"Ni wageni wako hawa?" Bianca aliumuuliza na Jimmy alitingisha jichwa kukubali

"Mbona hukutuambia kama una wageni asubuhi hii tuandae chakula cha kutosha" Bianca aliongea

"Usiwaze sana mummy watakunywa chai tu mimi mwenyewe sikutegemea ujio wao" Jimmy aliongea na alipomaliza kauli hiyo wageni waliweza kufika mezani na Bianca alinyanyuka kuwasalimia kwa heshima huku akiwapa tabasamu la kirafiki

"Miss lina sisi ndio tunapaswa kutoa heshima na kuomba radhi kwa ujio wa ghafla" aliongea Caren akimpa tabasamu

"Je haimpasi mke wangu kukaribisha wageni kwa heshima mahali pangu?" Jimmy aliongea

"Unanifahamu!" Bianca aliuliza kirafiki

"Kwa umaarufu ulio nao nani asikujue, mimi ni mmoja kati ya shabiki zako" alijibu Caren

"Haha! am humbled! Karibuni ten " Bianca aliwakaribisha kwa mara nyingine na walipokea ukaribisho

Aliwawekea juisi ya matunda kwenye glasi na vitafunwa baadhi kisha kwa kujiongeza yeye pamoja na vijakazi wa nyumba yake waliondoka kwa kisingizio cha kushiba kuwaachia 'privacy'

"Sikudhania kama utakuwa na mke mwenye kujiongeza haha" aliongea kamanda Rama huku akijichekesha

"Anyway sisi ni watu wazima haina haja ya kuzunguka nianze kujitambulisha mimi ni Ramadhan Suleiman Sudi na huyu hapa ni Caren nadhani mlishakutana"

"Ndio miaka mitanobiliyopita.. Hey long time no see!" aliongea Jimmy na kumpa ishara ya kirafiki Caren, naye Caren alirudisha kwa tabasamu la kirafiki

"Mimi ndiye mkuu wa kitengo cha Hidden Supremacy na lengo la kuja hapa ni kutaka....."

"Usiniambie unataka nijiunge kwenye hilo kundi lenu"

"Hilo lilikuwa ni kusudi langu la kwanza lakini nimebadili maamuzi"

"Ooh ni vizuri umebadili maamuzi maana hata kama usingebadili nisingekubali, unaonaje ukaniambia kilichokufanya ubadili maamuzi?"

"Mwanzoni nilidhani utakuwa ni mtaalamu uliyebobea kwenye mapigano kutokana na taarifa niliyopata kwa Caren na mimi huwa napenda kuendeleza vipaji kanma hivyo, na tulipofanya uchaguzi kuhusu wewe nikaja kugundua kwamba unafahamika sana katika ulimwengu wa kihalifu, of course ilikuwa ni taarifa nzuri sana kwa upande wetu na kupata sababu nzuri ya kukufanya uingie kundini hata kama hutaki" aliongea kamanda Rama na kunyanyua glasi yake ya juisi na kuigida yote kama maji

Jimmy alikuwa akimtazama tu huyo kamanda mweusi tii akisubiri muendelezo wa simulizi yake fupi, alijiambia hajawahi kukutana na binadsamu mweusi kama hiyo tangu azaliwe, aliwaza mbali na kudhani pengine wanawake aliokuwa nao wameondoka kwa sababu ya sura yake ngumu na weusi tii

"Lakini ulipotea kwa miaka mitano bila ya kujulikana ulikopotelea" alimalizia

"Kwahiyo kupotea kwangu ndio sababu ya wewe kubadili uamuzi?"

"Hapana"

"Sababu ni ipi?" Jimmy aliuliza akimkazia macho kusubiri jibu

"Tuachane na sababu lengo langu sio kuelezea sababu nimekuja hapa kuomba ushirikiano" aliongea kisha kunyamanza

"Ushirikiano wa nini kamanda mbona unaongea kwa mkato kwanini usitamke hotuba yote kuliko kuniambia kidogo kidogo"

"Nadhani utakuwa unajua kuhusu hivi viumbe vya ajabu ajabu vinavyotesa raia"

"Ndio ni vichaa tu waliopoteza ubinadamu" aliongea Jimmy

"Vyovyote vile tunataka kuwaondoa iliraia waishi kwa amani"

"Sasa mimi nahusikaje kwenye mpango wenu wa kutaka kuwaondoa?"

"Tunataka ushirikiane nasi kwenye huu mpango"

""Nini kinawafanya mdhani labda nitakubali na ninaweza kusaidia? "

" Ukweli uwezo wa kusaidia unao kuhusu wewe kukubali ni ombi letu, chukulia unaweka akiba ya msaada kwetu ukikubali na kutusaidia kwenye huu mpango kama una lolote utakalo ambalo tunaweza kukusaidia tutafanya hivyo"

"Mkuu mbona unanifanya mbuzi wa kafara? mimi ni binadamu tu wa kawaida sasa kutaka mimi kwenda kupambana na hao mashetani ni sawa na kunitoa kafara maana hatujui nini kitajiri, vipi mpango ukishindikana?"

"Ukijiunga nasi hauwezi kusgindwa!"

"Hahaha! Inashangaza sana hatujuani lakini unaniamini kupitiliza, au kwasababu ya kunifuatilia?"

"Kwahiyo ulikuwa unajua nakufatilia lakini ukaamua kujifanya, kwanini?" aliongea kamanda Rama, sio kama hakujua ameshtukiwa bali alitaka sababu

Ukweli Jimmy tangu ile siku alipodili na wale wahuni waliotumwa kumvunja miguu aliweza kugundua anafuariliwa lakini aliamua kujifanya kutoshtukia

" Kwasababu haukuwa na nia mbaya juu yangu" alijibu

"Unajuaje kama hakuwa na nia mbaya, inawezekanaje mtu kujua nia ya mwenzake?" Caren aliuliza

"Aura!" Jimmy alimjibu na kumfanya Kamanda Rama kutabasamu

"Aura anayosambaza muhusika hiubadilika kutokana na hisia na matendo, ni kama harufu ya mvua kabla haijanyesha. Mfano, mtu anayetaka kukuua, husambaza hisia flani zisizo za kawaida. Mapigo ya moyo wako hubadilika, na hata hewa inayokuzunguka huhisi kuwa nzito… kama kiza kinachofunika mwanga taratibu" aliongea na kunyamanza kidogo

"It’s like a feeling of something brushing against your soul" aliendelea akimaanisha "ni kama hisia flani ya kitu kinachogusa nafsi yako"

"Sawa tuseme Aura lakini uliwezaje kujua ni Kamanda Rama na si mwingine?" Caren aliuliza swali jingine

"Unauliza swali ambalo jibu unalo, jibu ni msisimko wa nguvu za kiroho anaotoa, ukweli sikujua kama ni kamanda wako zaidi ya kujua tu kuna mtu ananifatilia nimejua ni kamanda wako sababu msisimko wake naouhisi hauna tofauti na yule aliyekuwa akinifuatiliwa" Jimmy aliongea na kumgeukia kamanda Rama

"Ulifanya makusudi nikugundue si ndio? Ili ukija nitembelea nikutambue?" alimuuliza

"Haha! Kijana inaonekana una akili sana na mtu makini" aliongea kamanda Rama na ghafla tu alizima ule msisimko wa nguvu zake za kichaw

"Kwahiyo unataka kusemaje kamanda?"

"Nachotaka ni kujua chaguo lako, Ndio au hapana"

Jimmy alipiga kimya cha dakika kadhaa akiwaza na kuwazua kisha kumtazama kamanda Rama na tabasamu flani hivi na kunyanyuka pale mezani

"Hata hivyo bila ya msaada wa watu wako kipindi kile pengine nisingekuwa hapa leo hii" kisha alianza kutembea kuelekea juu na alipofika katikati ya ngazi kamanda Rama aliongea

"Nitakutaarifu mambo yakiwa tayari"

Hakuitaji maelezo zaidi kuelewa kwamba Jimmy amekubali kushirikiana nao kwenye mpango ambao Hidden Supremacy walikuwa wakuandaa na taratibu alinyanyuka pamoja na Caren kuondoka mahali hapo

Walipoufikia mlango Caren alisimama ghafla na kugeuza shingo nyuma akiangalia upande wa ngazi juu ambako Jimmy alipotelea na kuangalia kwa, sekunde kadhaa kisha kugeuza shinho na kuzipiga hatua kuondoka.

Jimmy aliweza kumuona Biancalina akiwa amesimama mlangoni mwa chumba chake akimsubiri na mkono wa kulia alikuwa ameshikilia nguo mpya kabisa, haikueleweka alinunua lini

"Mummy usiniambie ulikuwa unanisubiria muda wote huo" aliongea kiutani

"Shika hizi nguo ukabadili sasahivi" aliongea Bianca akimpatia nguo hizo

"Mummy kuna ulazima wakuvaa hizi nguo? mbona hata hapa nimependeza tu" aliongea Jimmy

"Darling bhana nishakwambia sipendi tabia yako ya kunikatalia vitu vidogo vidogo" aliongea huku akinuna na kumnyooshea nguo

Jimmy hakuwa jinsi aliona ni bora tu akubali kuliko kumkasirisha bila sababu za msingi maana ni jana tu hapo alitoka ku'confess alijiambia sasa kama alisema anampenda zaidi ya chocolate halafu amkasirishe si ataonekana muongo?

Baada ya Jimmy kuzipokea nguo hizo Bianca alifurahi moyoni na kumpiga busu la hatraka shavuni na kukimbilia chumbani kwake ambapo hakukuwa mbali na chumba cha Jimmy

Jimmy aliganda kwa sekunde kadhaa akiwa na tabasamu pana usoni huku akihisi mtekenyo kwenye moyo wake, hapana sio moyo tubali mwili mzima

"Sometimes, love surprises you when you least expect it… like now." alijiongelesha akimaanisha "muda mwingine upendo hukushangaza bila kutarajia.. Kama sasa hivi" na kuingia zake ndani

Dakika chache tu alitoka chumbani akiwa amebadili nguo na kuvaa zile alizopewa na mpenzi wake mpya

Alikuwa amevalia shati kubwa 'oversize' la mikono mifupi rangi ya urujuani(violet), design yake ilikuwa ni ya kipekee sana kama vile gwanda la juu la kijeshi maalum kwa jenerali, lakini halikuwa gwanda

Pia alivaa suruali nyeusi iliyokuwa stable, haikumbana sana wala haikuwa pana sana kifupi ilikuwa stable. Na miguuni alipigilia rubber safi nyeupe kama theluji kampuni ya Nike

Kwa staili hiyo ya mavazi Jimmy alitokelezea haswaa yaani alipendeza kinoma ukijumlisha na utanashati wake na mwili wake ndio kabisa hakuelezeka kwa maneno

Mdogo mdogo alishuka chini na kwenda zake sebuleni na kukaa kwenye sofa akimsubiri Bianca na kama mjuavyo tabia za wanawake kuchukua muda mrefu kujiandaa ilimbidi tu kuangalia Tv kusogeza muda

Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa hatimae aliweza kusikia hatua za miguu zikishuka na anageuza shingo yake kuangalia anakutana na bibie amepiga sare sawa na yake na alionekana kama tomboy fulani hivi

Itoshe kusema alipendeza kwelikweli, uzuri wake wa uso wake haukuhitaji make up kuupamba bali ulijidhihirisha wenyewe yaani ule uzuri wa asili

Kwenye macho ya Jimmy Biancalina alionekana kama vile mgeni kwake na muda wote alikuwa akimkodolea macho kama vile hakuwahi kumuona hapo kabla na mpaka Bianca anamkaribia ndio anashtuka kutoka kwenye kuzubaa. Kwa kizungu tunasema "he was in a daze"

"Mummy ni wewe kweli?" aliuliza kama vile haamini macho yake

"Nimependeza eeh!"

"Loh! For sure umependeza ni kama ndoto iliyosukwa kwa mkusanyiko wa nyota na mwezi ikawa halisi, yaani uzuri wako hauonekani tu, unahisiwa! Like a silent melody that plays in the soul." Jimmy alimwaga sifa kitaalamu sana akichanga kingereza na kiswahili

Bianca alisikia raha kusifiwa sio airi, japo hakuonyesha lakini alifurahi mno!

"Ni kama malkia asiyehitaji taji kujulikana. Na macho yako… ni kama galaksi mbili" aliendelea

"Inatosha" Bianca alianza kupatwa na aibu huku akiangalia chini

"Hehe mbona unanionea aibu? Lakini ndio unavyozidi kuvutia"

"Aah..." Bianca alitaka kuongea Jimmy akamuwahi

"Basi nitaacha..... My queen" aliongea akimpa ishara atangulie kama mfalme amfanyiavyo malkia

Bianca alitoa tabasamu kama la malaika na kutangulia kisha Jimmy akafuata na kumkaribia sawa na walipofika mlangoni Jimmy kama gentleman vile alimfungulia mlango na mrembo Bianca kupita

Walienda mpaka garage ya magari ambapo walimkuta Zuhura na walinzi wenzake wakimsubiri

"Zuhura leo hatutaongozana" Bianca alimtaarify mlinzi wake

"Lakini madam usalama wako ni muhimu isitoshe wewe ni celebrity utahitaji msaada paparazzi wanapojitokeza"

"Usiwe na wasiwasi nipo na Jimmy"

"Lakini madam huu ni wajibu wangu sio kwamba simuamini..."

"Nipo salama Zuhura leo sihitaji kuongozana na walinzi nahitaji uhuru na mume wangu"

Paah! Moyo wa Jimmy ulidunda na kuendelea kudunda mpaka ukadundika neno "mume wangu" hakulitegemea kulisikia mapema hivyo tena wakati kama huo mbele ya walinzi, ila hakujali sana kuhusu walinzi alipatwa na ile hisia ya kuitwa mume wangu kwa mara ya kwanza yaani jana love confession kesho yake ambayo ndio hiyo anaitwa mume wangu!

Hata hivyo alifurahi mnooo tena mno! Sura yake ilikuwa inang'aa kwa tabasamu kwa kuitwa mume, hata kama hawakufunga ndoa ila alifurahi sana kusikia hivyo

"Darling unajua kuendesha gari?" Bianca alimuuliza Jimmy ambaye alikuwa hajasikia, alikuwa mbali sana kimawazo akitabasamu bila ya kueleweka anawaza nini

"Hey.. Wewe.. Darling!" aliita na Jimmy alishtuka na kutoka kwenye mawazo na kumuangalia Bianca

"Naam mke wangu"

"Nimekuuliza unajua kuendesha gari"

"Ndio ndio mimi ni mtaalamu sana usiwaze" aliongea na Bianca aliingiza mkono kwenye suruali na kutoa funguo ya gari kisha kumpatia

Jimmy baada ya kupokea funguo alienda mfungulia mlango wa gari husika siti ya mbele ya abiria na baada ya Bianca kuingia alifumga na kumtolea tabasanu Zuhura

"Ondoa wasiwasi yuko salama" kisha alienda mlanfo wa dereva na kuingia. Dakika moja ilitosha kuliondoa gari hilo ndani ya nyumba na sasa lilikuwa barabarani likichanja mbuga kwa mwendo mtulivu

END OF SEASON ONE!.... THE RHYTHM CONTINUES.... 🔥
🍸🍸🍸
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom