Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 10: Salazar Solren Soledad


Upande wa Jenerali hakuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya kutoa tabasamu tu maana alishaizoea hali hiyo kutoka kwa mwanae.

"Wewe mtukutu ifike muda uonyeshe heshima kwa wakubwa zako" aliongea Jenerali huyo na kumpotezea

Aliwaangalia wengine walioko lakini zaidi macho yake yalitua kwa Jimmy ambaye pia alikuwa akimuangalia

"Samahanini kwa ujio wangu wa ghafla mahali hapa sijaja kwa kutibua amani bali nimekuja kwa nia njema kabisa mimi ni Jenerali Johnson Merizesta mkuu wa majeshi ya ulinzi wa nchi, nina muda mchache kuwepo hapa, lengo ni kuzungumza na Jimmy Julian Jairo" alijitambulisha na kusema dhumuni la kuja mahali hapo

"Kuweni na amani sitochukua muda mrefu sana kwa mgonjwa" aliendelea kuongea na kuwaomba wawapishe kidogo, maongezi mengine ni siri. Nani wa kumpinga Jenerali kwa mfano? Kila mmoja alitoka nje wakibaki watano tu, Jenerali, walinzi wake pamoja na jimmy

Jenerali alivuta kiti na kwenda kukaa pembeni kidogo akikunja nne

"Upo unajiuliza kwanini mkuu wa majeshi amekutembelea si ndio?" aliuliza

"Najiulizaje ilihali umeshasema unahitaji mazungumzo na mimi mzee Jenerali" aliongea Jimmy na kumfanya Jenerali aachie tabasamu

"Unajua maongezi gani ambayo yamenitoa makao makuu mpaka kuja hapa hospitalini kwa raia wa kawaida kama wewe?"

"Mkuu nitajuaje bila ya wewe mwenyewe kuniambia isitoshe mimi sio malaika mpaka kujua kila kitu"

"Hahaha! Napenda vijana jasiri kama wewe, mara nyingi nikiongea na watu huwaga waoga sana na kuchagua maneno ya kuongea lakini kwako wewe ni tofauti.... just like your father"

"Unamjua baba yangu?" Jimmy aliuliza akiwa amekunja sura yake

"Ndio alikuwa rafiki yangu jeshini, niseme tu baba yako alikuwa ni mtu muhimu sana ya jeshi lakini inasikitisha ha......." aliacha sentensi yake ieleee hewani

"Anyway hilo sio lengo langu la kuja hapa"

"Lengo lililokuleta ni lipi?" Jimmy aliuliza na Jenerali alitoa ishara na mmoja wa walinzi alitoa faili na kumpatia

"Unamfahamu huyo?" Jenerali alimuuliza baada ya kumpatia faili na Jimmy alikubaliana naye

"Ndio huyu ni mzee wangu nilikuja kujua Jina lake halisi ni Momochi Saizo juzi-juzi" alijibu na Jenerali alimpatia faili jingine tena

"Unamfahamu huyo?" aliuliza tena na Jimmy baada ya kulitazama faili alikataa

"Hapana simfahamu huyu"

"Angalia vizuri usiangalie sura angalia majina"

"Unataka kusema?" Jimmy alipatwa na mshangao kidogo baada yakugundua kitu

"Nadhani ushaelewa sasa hao wote ni mtu mmoja"

"Kama ni mtu mmoja ipi ni sura yake halisi?"

"Kuhusu sura yake halisi hilo nalo ni shaka jingine amekuwa akiishi nchi tofauti tofauti kwa sura tofauti, tumeweza kupata taarifa hiyo kwa msaada wa Uingereza kwamba yupo nchini" aliongea Jenerali

"Sawa, lakini nini maana ya kuniambia hizi siri za jeshi? Jimmy aliuliza

" Inashangaza eeh? Huyo ni "Former ninja assasin" yaani alikuwa na alitekeleza mauaji mengi sana kutoka mataifa tofauti na katika kustaafu kwake alipotea kusikojulikana na hivi karibuni aliweza kugundulika nchini humu baada ya msako wa muda mrefu. Umekuwa ukiishi na mtu hatari kwa muda mrefu"

"Mzee ana siri sana yule Mkuu sishangai"

"Kingine ameuawa na kundi lake la kininja alilokuwa akilihudumu kwa muda mrefu cha kushangaza uliweza kudili nao na kuwamaliza kwa maana hiyo umefanya kazi ambayo kitengo chetu kilipaswa kufanya"

"Kidogo nipoteze uhai wangu, niseme ni bahati tu"

"Ni kundi daraja B lijulikanalo kama Yami no Senshi lenye maana ya Warriors of Darkness ni kundi lenye maninja wasomi wanaojificha kwenye vivuli/giza" alieleza kwa kifupi

"Kwahiyo unataka kusemaje Mkuu?" Jimmy aliuliza na kumfanya anyanyuke na kusimama akiachia tabasamu

"Ninakukaribisha kujiunga na Jeshi letu ninaamini kwa uwezo wako ulionao tukikuongezea ujuzi utalisaidia taifa kwa namna nyingi sana"

"Asante lakini sivutiwi na kuwa mwanajeshi" alijibu Jimmy

"Usiwe na haraka ya kutoa jibu haraka je hutaki kuwa na heshima kama ya baba yako? hutaki kujua nini sababu ya baba yako kutangulia mbele za haki?"

"Kwasababu ya baba yangu kuwa mwanajeshi haimaanishi na mimi nitataka kuwa kama yeye kingine nachojua ni kwamba baba yangu alikufa kwa ajali, hata kama isingekuwa ajali bado kazi yake ni ngumu kutoka salama... Asante sana kwa ofa hiyo mkuu lakini jibu langu ni hapana"

"Kijana acha kukurupuka ni ngumu sana Mkuu wa majeshi kumualika raia ndani ya jeshi bila utaratibu" aliongea mmoja aa walinzi lakini jimmy alitingisha kichwa kukataa

"Sawa sitokulazimisha kijana kuheshimu uamuzi wa mtu ni jambo muhimu sana" aliongea Jenerali na kuzipiga hatua zake kuondoka alipoukaribia mlango alisita

"Ooh nimekumbuka" aliongea Jenerali na kumgeukia Jimmy "Una sbukrani zangu za dhati kijana umeiokoa familia yangu, hilo nashukuru" aliongea na kuondoka zake akimuacha Jimmy katika hali ya kutafakari

Ndugu zake waliingia mara baada ya Jenerali na jeshi lake kuondoka, wa kwanza kutangulia alikuwa ni Cid akifuatwa na Monica, Bianca na Mamaye

"Bro huyo mzee alikuwa anakwambia nini?" Cid aliuliza na kila mtu alitega masikio kusikiliza na Jimmy alitoa kicheko na kuwaangalia mmoja baada ya mwingine

"Amekuja kunipa pole tu na kutoa shukrani" alijibu

"Shukrani za nini?" Cid aliuliza na wengine kutingisha kichwa kukubaliana na swali lake

"Nenda kamuulize si mzee wako yule halafu kumbe ni mkuu wa majeshi asee"

"Kuhusu hilo hapana kwakweli bro fanya ututonye ndugu zako basi" aliendelea kumtaka amuelezee lakini Jimmy aliendelea kukomalia kwamba akamuulize mwenyewe na mpaka kufika jioni saa kumi na mbili walizungumza mengi na waliaga kwakuwa muda wa kutembelea wagonjwa umeisha

Kama kawaida baada ya wote kuondoka wakikwishakumuaga aliuchapa usingizi kama maiti vile.

°°°°°°°°°°

Jimmy alijikuta yuko mahali pasipojulikana ni wapi akiwa peke yake

Mahali hapo kulikuwa ni patupu kupita maelezo, ardhi yake ilikuwa ni tambarare yenye mchanga mweupe kama wa baharini, anga nalo lilikuwa ni la buluu safi lisionekane wingu hata moja

Wakati anajiuliza yuko wapi mara alisikia sauti kama mwangwi ikinena

"Welcome to my world young man" ilikuwa ni sauti yenye kusikika vyema masikioni mwa mtu yeyoteikimaanisha karibu katika ulimwengu wangu kijana

"Where am I and who are you?" aliuliza kwa lugha sawasawa na aliyoisikia akimaanisha Niko wapi na wewe ni nani

"I am Salazar Solren Soledad, Sovereign of the Arcane, The Forbidden Monarch of ancient knowledge, The Sorcerer, The Enchanter, Spellweaver, The Ancient legacy" sauti ilijitambulisha ikimaanisha "Mimi ni Salazar Solren Soledad, mtawala wa uchawi wote, Mfalme wa maarifa ya kale, Sorcer(mchawi), Enchanter(mchawi), spellweaver(mchawi wa spells), Uridhi wa kale"

Upande wa Jimmy licha ya utambulisho huo hakuelewa chochote licha ya kujua kingereza, aliishia tu kukaa chini akijikuna kichwa chake

"Unaonekana hujanielewa bado kijana" ilisikika tena sauti hiyo

"Unajua kuzumgumza kiswahili?" jimmy aliuliza

"Ninafahamu lugha nyingi sana kuliko unavyofikiria"

"Kumbe! Unaweza kuniambia kwanini niko hapa"

"upo hapa kwasababu unakwenda kuwa mrithi wangu"

"Mrithi? Usinitanie we mzee kwanza kwanini unajificha" aliongea jimmy na sekunde anamaliza kauli yake alihisi kuna mtu yuko nyuma yake na aligeuka haraka lakini hakumuona mtu na ile anarudisha kichwa chake tu anakutana na sura ambayo ilimshtua kiasi cha kuruka kama wadada wanavyorukia juu ya kochi baada ya kumuonda mende akiwakaribia

Alikuwa ni mzee mwenye sura iliyojikunja kiasi cha sura yake kumtisha yeyote atakaye muangalia kwa mara ya kwanza, meno yake nayo yalikuwa ni ya njano yenye mapengo yasiyo na idadi ya kueleweka, sasa vuta picha ndugu msomaji jinsi mzee huyo alivyo, kibaya zaidi alikuwa akitabasamu

"Sikujificha, sijajificha na sijawahi kujificha" aliongea mzee Salazar akivalia joho jeusi refu lililofunika mikono yake na miguu yake

Jimmy alivuta pumzi ndefu na kuzishusha akimtazama mzee huyo aliyekuwa akimtazama pia

" Unaweza kuniambia kwanini nipo hapa?" jimmy aliuliza

"Unataka kujua kwanini?"

"Ndio"

"Kaa chini kwanza" alimwambia aketi chini na Jimmy alikaa pamoja na huyo mzee

"Umekiona hiki kitabu" aliongea mzee Salazar baada ya kunyanyua mkono kumuonyesha na ghafla kitabu kilijitokeza kichawi hali iliyomfanya Jimmy kushangaa na kukunja ndita

"Kilitaka kunitoa uhai wangu na kusababishia familia yangu kutekwa bila kusahau mzee wangu Momochi ametangulia mbele za haki kwa sababu ya hako kakitabu ka kipuuzi"

"Hapana hiki kitabu sio upuuzi umepitia yote hayo ni kwasababu ya kile kilichomo humu"

"kilichomo my foot! Unataka kuniambia bizo kurasa tupu zilizomo humo ndio zilikuwa zikitafutwa" Jimmy aliongea kwa hasira alitamani jata kutukana lakini alikuwa akiogopa hata yeye mwenyewe alijishangaa kwanini anaogopa

"Fungua" aliongea mzee Salazar akimpatia kitabu na kutaka akifungue.
Jimmy alikipokea na kukifungua na alishangaa kukikuta kimeandikwa lugha zisizoeleweka tofauti na mwanzo ambapo hakukuta maandishi yoyote

Jimmy alimwangalia mzee huyo kwa sura yenye maswali na kutaka maelezo

"Hizo ni lugha za kale ambazo zimesahaulika katika dunia hii sababu ya wewe kutokuta maandishi ni kwasababu niliyaficha na kwasababu ya agano nililoliweka nilipokaribia kufa"

"kwamba damu ya awaye yote itakayomwagika katika kitabu hiki huyo ndiye atakayekuwa mrithi wangu atake asitake ndipo roho yangu ipumzike kwa amani..... "

"Umesema ulipokaribia kufa sasa mbona mpaka sasa hujafa" Jimmy alimkatisha

"Tulia kijana, subiri nimalize ndiyo uulize maswali yako ila ngoja nikujibu hilo kabla ya kuendelea. Mimi nilikwisha kufa kitambo mimi ni roho iliyokataa kwenda mahali pake kwasababu ya kudhulumiwa uhai wangu" aliongea mzee Salazar na Jimmy kufunga mdomo wake

"Hapo zamani nilikuwa ni mchawi mwenye nguvu sana na mwenye maarifa mengi ambayo ambayo mpaka kwenye dunia ya sasa hayapo"

"Unasema ni mchawi mwenye nguvu ilikuwaje sasa ukafa lakini sasa upo hai"

"Watu tunakufa kwa njia nyingi sana, inaweza kuwa ajali, magonjwa, kuuawa. na vifo vingine vinatokea bila sababu yoyote si ajali, si ugonjwa wala chochote kilichosababisha unajikuta tu unakufa, ila unajua ni kifo gani kinaumiza?" alimuuliza jimmy

"Sijui"

"Ni kile kifo cha kuuawa hasa kwa mtu ambaye hukutegemea atakuja kufanya hivyo, na mtu huyo ni mwenye kujua siri zako na udhaifu wako na kuzitumia kukuondosha kwenye uso wa dunia. Na mara nyingi mtu huyo ni mtu wa karibu sana kwako anaseza kuwa mpenzi wako unayemuamini, rafiki yako wa karibu na hata mwanafamilia wako." aliongea mzee Salazar na kunyamanza kidogo akimeza mate kisha kuendelea

"Yote hayo huanzia kwenye wivu, kijana unapaswa kujua wivu ni mbaya sana, Wivu husababisha tamaa na chuki na kwasababu ya chuki na tamaa za kijinga ndiyo husababisha kuuana"

Jimmy alikuwa kimya tu akimsikiliza mzee huyo kana kwamba yupo kanisani akipata mahubiri.

"Nimeuawa na mtu ambaye sikumtegemea, mtu ambaye nilikuwa nikimjali sana na kuhakikisha hapati tabu lakini ndiyo hivyo shukrani ya punda ni mateke, alinilipa wema kwa kuondoa uhai kwa tamaa ya kuwa na nguvu lakini hakufanikiwa kuzipata hizo nguvu, ni kwasababu nilizificha kanuni zake"

"Ooh ni hadithi ya kuhuzunisha iliyoje!" aliongea Jimmy huku akionyesha sura ya masikitiko

"Kijana unadhani nakwambia haya yote ili unisikitikie?"

"Hapana nakuhurumia tu mzee hakuna cha ziada, hata hivyo nimejifunza kitu kupitia maneno yako"

"kwamba?"

"No one can claim something truly precious without sacrifice. The greater the treasure, the higher the price" aliongea jimmy akimaanisha "Hakuna anayeweza kupata kitu cha thamani bila ya sadaka/kafara. Kadiri hazina inavyokuwa kuu, ndivyo gharama inavyokuwa kubwa"

"Safi sana kijana inaonekana una akili sana nadhani unafaa kuwa mrithi wangu"

" Sitaki kuwa mchawi mimi mzee" aliongea jimmy na kumfanya mzee acheke

"Watu mnatafsiri uchawi kwa namna tofauti sana ila kwa tasfiri yangi namaanisha nguvu zisizo za kawaida simaanishi kurogana na kuwangiana usiku uchi kijana"

"Mimi sioni tofauti yoyote uchawi ni uchawi tu kama uchawi mwingine" jimmy alikazia na mzee huyo alitabasamu na kusimama

"Unafanya nini?" Jimmy aliuliza naye akisimama

"Nakuonesha nguvu halisi niliyo nayo" aliongea yule mzee na kusogea umbali wa mita kumi na alipo jimmy

"Gravitas Inversus!" alinena kilugha na palepale gravity iliongezeka upande aliosimama jimmy ni kama kuna nguvu inamkandamiza kwenda chini na alianguka akipiga magoti, kila akijaribu kunyanyukka anashindwa, alifanya kila awezalo lakini wapii

"We mzee ndo nini sasa kunisababishia ha...." aliongea kwa tabu

"Gravitas Relinquere!" alinena tena yule mzee na kufanya ile hali kusitisha

"Vipi bado unakataa kurithi nguvu zangu?" alimuuliza Jimmy

Upande wa jimmy ambaye alikuwa amechoka na mwili kumlegea alikubali na kutamani sana kuijua nguvu hiyo na kumfanya mzee Salazar acheke

Alijiambia kuwa na nguvu ya ajabu kama hiyo kutamfanya aweze kuwalinda awapendao hakutaka lile kosa kujirudia kiasi cha kutaka kuondolewa uhai

"Unaweza kujifunza na kurithi nguvu zote lakini ni kwa sharti moja"

"Masharti tena mbona umegeuka kuwa mganga ghafla!"

"Nimesema sharti sio masharti"

"Lipi hilo"

"Unapaswa kunisujudia" aliongea mzee Salazar na kumfanya Jimmy acheke kama chizi mpaka kupaaliwa na mate







TO BE CONTINUED............

JIMMY YUPO KWENYE ULIMWENGU MWINGINE KUPITIA NDOTO BAADA YA KUSINZIA😁😁

ENDELEA KUFATILIA SIMULIZI HII TARATIBU NDUGU MSOMAJI, SIMULIZI BADO YA MOTO SANA🔥🔥
 
By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 10: Salazar Solren Soledad


Upande wa Jenerali hakuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya kutoa tabasamu tu maana alishaizoea hali hiyo kutoka kwa mwanae.

"Wewe mtukutu ifike muda uonyeshe heshima kwa wakubwa zako" aliongea Jenerali huyo na kumpotezea

Aliwaangalia wengine walioko lakini zaidi macho yake yalitua kwa Jimmy ambaye pia alikuwa akimuangalia

"Samahanini kwa ujio wangu wa ghafla mahali hapa sijaja kwa kutibua amani bali nimekuja kwa nia njema kabisa mimi ni Jenerali Johnson Merizesta mkuu wa majeshi ya ulinzi wa nchi, nina muda mchache kuwepo hapa, lengo ni kuzungumza na Jimmy Julian Jairo" alijitambulisha na kusema dhumuni la kuja mahali hapo

"Kuweni na amani sitochukua muda mrefu sana kwa mgonjwa" aliendelea kuongea na kuwaomba wawapishe kidogo, maongezi mengine ni siri. Nani wa kumpinga Jenerali kwa mwamba huyu hapa kama singano akimsimulia ROM aka HADES
 
SEASON ONE IMEKAMILIKA INA VIPANDE 30 KARIBU FASIHINET KUNISAPOTI

AU WAWEZA NICHEKI WHATSAPP 0748690130

Screenshot_20250511-161118.png
 
By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 11: "officially solo"


"Mimi Jimmy Julian Jairo tangu nizaliwe sijawahi kumsujudia mtu yoyote, hata atokee shetani mwenyewe sitomsujudia, wewe ni nani mpaka utake nikusujudie?"

"Mbona unafanya mambo kuwa magumu kijana kuna ugumu gani wa wewe kuinama?"

"Sikia we mzee Sa... nani sijui, nimesema hiviii sitoinama!"

"Unajua unayesimama mbele yake? Naweza kufuta uwepo wako kwa mkono mmoja tu, lakini kwa moyo mkunjufu ninataka kukurithisha nguvu zangu, nachohitaji ni uiname

"Hapana siinami"

"Unadhani nguvu zina thamani sana kuliko utu wangu? hata kama nimekubali kurithi haimaanishia nitakusujudia" Jimmy aliendelea na msimamo wake

"Utu ni ngao dhaifu ya wasio na nguvu kijana, unapaswa kujua wenye nguvu ndiyo wanaoweka sheria za ulimwengu huu, nami sheria yangu ni wewe uiname"

"Try me!" aliongea jimmy na ghafla anga lilibadilika na kuwa jeusi, upepo mkali ulianza kuvuma na ghafla ulitokea mkandamizo ambao Jimmy alikuwa akishindana nao, ni nguvu iliyokuwa ikimkandamiza kwenda chini lakini jimmy alijizuia asiiname kwa hali yoyote ile ilifika mpaka miguu yake kutetemeka kama jenereta lakini Jimmy alikomaa na kiburi cha kutoinama

"Interesting!" aliongea mzee Salazar na kunyanyua mikono yake yote miwili kuelekea juu angani na kuanza kunena kilugha na nguvu ya mkandamizo ilizidi kuongezeka

Jimmy nguvu ilimzidia kiasi cha kupiga goti na mguu mmoja na damu kumtoka mdomoni na puani lakini bado hakuruhusu mwili wake kusujudia pasipo hiari yake

Mzee Salazar alishangaa kuona bado aliweza kuhimili nguvu kubwa ya mkandamizo kiasi hicho

"Why don't you bow? It's easier that way"

"I already told you old man I ain't gonna bow you witch" aliongea Jimmy akikataa kusujudia

Alinena kilugha mzee Salazar na ghafla hali ile ilikoma na Jimmy mzobemzobe kama furushi alianguka chini kwa kuishiwa na nguvu

"Interesting… Perhaps you are worth of my legacy" (inavutia... Unastahili urithi wangu) aliongea mzee Salazar na kumkaribia jimmy kisha akamuwekea mikono yake kwenye kifua kisha kufumba macho na kutamka maneno ya ajabu yasiyoeleweka na kadri muda ulivyokuwa ukisogea Jimmy alirejewa na hali yake ya kawaida, uchovu pamoja na maumivu vilipotea mara moja!

"At last, you have inherited my legacy" (hatimae umekuwa mlinzi wangu) aliongea mzee Salazar kwa sauti ya upole

"Unamaanisha nini?" Jimmy akiwa bado chini aliuliza

"Tayari una nguvu zangu na jinsi ya kuzitumisa mwongozo wake na kanuni ni kupitia kitabu kuhusu lugha usiwaze sana utatamka tu neno "Verba mutatio" (word transformation) na utasoma kwa lugha yoyote unayoitaka" aliongea mzee Salazar kwa sauti hafifu na taratibu alianza kugeuka majivu kuanzia chini miguuni kwenda juu taratiibu sana

"Farewell young man you're officially Solo" hiyo ilikuwa ni kauli ya mwisho kutoka kwa mzee Salazar na mwili wake uligeuka majivu ambayo yalipotelea hewani

°°°°°°°°°°

Jimmy aliamka kutoka kwenye usingizi mzito sana na kukuta muda umeenda sana, Alipoangalia muda kupitia saa ya ukutani alikuta ni saa sita na nusu usiku.

Alijihisi njaa kali sana muda huo hata yeye mwenyewe alijishangaa kwanini njaa kali hivyo na kwanini muda huo, kibaya zaidi mwili ulikuwa umeloa jasho.
Alijiambia ina maana hakuna huduma ya chakula kwa mgonjwa hospitali hiyo? Kama ipo kwanini hawakumuamsha apate kula?

Mara alijihisi haja ndogo ikimbana hivyo alinyanyuka kutoka kitandani, wakati anasimama alisikia sauti ya kitu kudondoka chini na alipoangalia chini alikuta ni kitabu kile cha kale, alipoona alichoka sana aseeh

Alijiuliza hivi alikuwa akiota ama ni uhalisia? lakini hakupata jibu na aliamua kupotezea na alielekea kwanza chooni na baada ya dakika moja alitoka na kurudi kitandani.

Njaa aliyokuwa akihisi hakuweza kuivumilia tena aliona ni bora hata azimie kimaajabu kuliko kubaki kuhesabu namba usiku mzima mpaka kunakucha. Hakutaka kabisa!

Uzuri hospitali hio kuna manesi ambao wanahudumia usiku(part time job), kingine kulikuwa na kitufe cha kubonyeza kuitia nurse/daktari hivyo alibonyeza mara mbili lakini hakukuwa na jibu, alibonyeza tena lakini hakupata jibu wala yeyote kuingia.

"Aah kudadadeki!" haikueleweka alikuwa akilalamikia njaa au ni nurse kutokuja

Alishuka kitandani na kuuendea mlango na kuufungua kuchungulia kulia na kushoto kwenye korido asionekane mtu, alitoka kutembea kwenye korido kuelekea upande wa kulia

Mara alisikia sauti za watu wawili zikilia alipoukaribia mlango wa stoo, zilikuwa ni sauti za miguno baina ya watu wawili jinsia mbili tofauti na alijiongeza akilini kujua kinachoendelea humo ndani
Lakini hali ile ilimfanya kukunja ndita, haiwezekani ateseke na njaa halafu nurse na mwenzake wanapelekeana moto, kibaya zaidi kwenye floor hiyo mgonjwa ni yeye peke yake na manesi wawili wa kutoa huduma ya kiafya lakini ndio hivyo wanafurahia utamu wa penzi ndani ya stoo.

Ilimbidi avunge tu na njaa yake, kumuharibia burudani mwanaume mwenzake haikuwa staha. Alielewa maumivu ya kukatiwa burudani murua namna hiyo hivyo mdogo mdogo alirudi kwenye chumba chake kinyonge sana.

Kitu pekee alichoona ni kuvumilia tu kesho nayo ni siku, aliketi juu ya kitanda akiikunja miguu yake na kuanza kukifungua kitabu kile na kukuta lugha za ajabu ajabu a.k.a lugha za kale

Ili kudhibitisha kile alichokuwa akiota kama ni uhalisia ama ni ndoto kama ndoto zingine, alitamka yale maneno aliyoambiwa atamke na mzee Salazar Solren Soledad

Alinena sawasawa na alivyoambiwa na maajabu ya kumshangaza macho yalianza kutokea. Yale maneno yalibadilika na kuwa lugha ya kiswahili.

°°°°°°°°°°

Mpaka kunakucha alikuwa amesoma kitabu nusu ya kurasa zote akiwa katika mkao uleule na alikuwa bado akisoma, Mara mlango ukafunguliwa na aliingia nurse mwanamke

Alikuwa ni mwanamke mnene kiasi mwenye shepu ionekanayo kwa mbali, nyuma nako hakukuwa pakuchukulia poa, alijazia kwelikweli kwa lugha nyepesi alikuwa ni mshangazi tena mshangazi haswaaa!!

Jimmy aliondoa umakini wake kwenye kitabu na kumgeukia nurse aliyeingia

"Ulikuwa wapi?" Ndiyo kauli ya kwanza kutoka kwa nurse baada ya kuingia

"Nilikuwa hapahapa sikuenda mahali popore" aliongea Jimmy

"Mbona jana usiku wakati nakuja kukuletea chakula sikukuona? "

"Hukuniona?" Jimmy alipatwa na mshangao

"Ndio sikukuona nilikuta kitanda kitupu kabisa nikadhani labda umetoka na baadae saa nne niliporudi tena sikukukuta"

"Ilikuwa ni saa ngapi?"

"Ilikuwa ni saa mbili nikaja tena saa nne lakini sikukukuta nilipatwa na wasiwasi pengine umetoroka" kauli hiypo kutoka kwa nurse ilimfikirisha sana Jimmy na kujiuliza maswali ya hapa na pale uyasiyo na majibu

"Hapana sikutoroka nilikuwa hapahapa nimelala nawezaje kuondoka bila kupita reception ambapo wewe upo masaa yote, si ungeniona" aliongea Jimmy huku akijiuliza wasiwasi gani ndiyo kulana kwenye stoo badala ya kutoa taarifa manurse wengine miyeyusho sana

"Pengine ni stress za kazi tu usiwaze sana, muhimu sasahivi umenikuta" Jimmy aliamua kuwa mnafiki kwa muda huo, na nurse ilimbidi akubaliane naye kishingo upande

"Sawa unatakiwa umeze dawa asubuhi hii lakini unatakiwa kula kwanza" aliongea nurse mshangazi

Neno kula ni kama lilimvuruga nafsi yake iliyosahau njaa na palepale njaa ilianza kumjia kwa kasi ya ajabu sana, alitamani kulia jinsi alivyokuwa akipambana kuivumilia njaa usiku kucha, licha ya kujisahaulisha njaa kwa kusoma kitabu lakini hakuna hata neno moja alilolielewa, Chezea njaa wewe!

Muda ulikuwa ni saa moja na dakika tatu ya asubuhi tulivu, makelele ya ndege kuimba nyimbo nzisizoeleweka asubuhi-asubuhi yalifikia masikioni mwao na mwanga hafifu wa jua ukipenyeza madirisha ya upande wa mashariki uliwamulika.

Mlango ulifunguliwa na mrembo Bianca kuingia mikononi akishikilia mifuko miwili yenye rangi nyekundu

"Good morning!" ilikuwa ni sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni kutoka kwa mrembo Bianca

Upande wa Jimmy alishangaa kumuona mrembo huyo asubuhi na mapema hivyo hata hivyo aliitikia salamu na nurse aliwapisha kwa kisingizio cha kwenda kufata kifungua kinywa kwaajili ya mgonjwa kabla ya kutumia dawa lakini Bianca alimwambia asijisumbue kwani alikuwa amekuja na kifungua kinywa tayari

Jimmy aliposikia neno kifungua kinywa kimeletwa angalau nafsi yake ilifarijika lakini sio kufarijika kiasi cha kusahau njaa, na kitu cha kwanza alichojali ni kula kwanza hakujali kingine zaidi, maana aliteseka vya kutosha

"Umeamkaje Jim" Bianca alimjulia hali akiliita jina lake kwa kifupi

"Nimeamka na njaa kali hivyo sio salama kwangu"

"Inaonekana nimefanya jambo zuri sana kuamka mapema na kuandaa kifungua kinywa" aliongea Bianca na Jimmy kutabasamu

"Hukuwa na haja ya kujisumbua hivyo isitoshe hospitalini kuna huduma ya chakula pia"

"Kwani ni kosa kukujali?" Bianca aliuliza

"Hapana sio kosa" jimmy alijibu

"Wewe ni rafiki yangu hivyo kukujali ni jukuma langu" aliongea Bianca

"Sawa umepika nini mrembo?" Jimmy aliuliza na sura ya tabasamu

"Unatakiwa upige mswaki kwanza uoge ubadili nguo ndio ule" Bianca aliongea na kumfanya Jimmy kuona huku sasa ni mateso yaani atawezaji kufanya yote hayo ilihali mwili huna nguvu

"Si una nguvu za kufanya hivyo?" Bianca alouliza huku akitoa mswaki mpya na dawa ya mswaki, sabuni yenye harufu nzuri pamoja na nguo mpya kwenye mfuko mojawapo aliokuja nao

"Ndio ndio naweza kufanya yote japokuwa nina njaa ila mwili una nguvu kidogo ya kuweza kumudu mambo madogo madogo"

Uzuri chumba hiko kilikuwa ni VIP hivyo washroom na bathroom hazikukosekana na kwa kujivuta Jimmy alibeba mswaki na dawa kuelekea huko.

" Mimi nitakuwa nje ukimaliza kujiandaa utaniita" aliongea Bianca na haraka haraka aliondoka na kumuacha jimmy akijiwazia "Kumbe kuwa na rafiki jinsia tofauti raha sana"

Haikuchukua muda sana Jimmy aliweza kujisafisha na kujiandaa vizuri akivalia zile nguo alizoletewa na kuanzia kila kitu, boxer mpaka sendo zilikuwa ni size yake, vilimtosha vyema

Alikuwa amevalia suruali flani hivi stable rangi ya Navy blue, haikubana sana wala haikuwa bwanga inshort ilikuwa ni stable! , pia alivalia na vest nyeipe na kwenda kufungua mlango akimuita Bianca aliyekuwa nje

"Mbona hujavaa shati?" aliuliza Bianca akimkodolea macho mikono yake yenye misuli na mishipa iliyojipanga vyema na kifua chake kilichojichora kwenye singlendi(vest)

"Hilo sharti ni jeupe nina wasiwasi nitalichafua" aliongea Jimmy huku akiketi kwenye kiti au naweza sema sofa na Bianca alielewa kwamba mpaka amalize kula ndiyo alivae

Bianca aliufata mfuko uliokuwa na vyakula na kutoa vibakuli vidogo vidogo vyenye muundo wa boksi na kuviweka kwenye meza ndogo na kuvifungua pamoja na chupa ya chai

Harufu nzuri ya vyakula hivyo viliifurahisha pua ya Jimmy huku akimeza mate mengi

"Unaweza kula sasa!" Alipewa ruhusa na hakuwa na muda wa kuzubaaa, njaa haizoeleki kabisa. Alianza kuufakamia msosi kwa raha kama zote, alikuwa akichukua hii, mara ile, mara hii nichovye pale, ninywe hii, nichukue ile kifupi ulikuwa ni mlo wa draft(kula bila mpangilio maalumu wa cha kukipeleka mdomoni)

Upande wa Bianca alikuwa akimshangaa Jimmy ambaye alikuwa akila kwa fujo bila hata ya kuona aibu

Jimmy alisita baada ya kumuona Bianca akimtazama bila kula

"Vipi mbona wewe huli?" Jimmy alimuuliza

"Hapana sina njaa nimekuandalia kwaajili yako" alijibu na jimmy wala hakuwaza sana, aliendelea kushughulika na kuliridhisha tumbo lake lisilo na adabu.

Nusu saa jimmy aliweza kumaliza msosi wote huku akijilamba vidole akimalizia na chai ya maziwa yote iliyo kwenye chupa kitendo kilichomtoa macho Bianca na kujiuliza hivi huyu mwanaume ana tumbo la aina gani? Ina maana alikuwa na njaa kali kiasi hiki?

"Mmmmh tamu sana aseeh, bibie una sifa zangu zote kwenye suala la upishi, umepika chakula kitamu sana" Jimmy alimwaga sifa na kumfanya Bianca atabasamu na kuangalia pembeni, ni wazi alikuwa amefurahi kusifiwa ni vile tu aliona aibu

"Nimeona kula bila kutoa pongezi sio sawa kabisa, utakuwa ni ukatili wa hali ya juu sana" aliendelea kukazia msumali

"Haha! nii kawaida tu mbona"

"Kawaida? Unajichukulia poa sana mrembo chakula ni kitamu sana kama cha mgahawa wa nyota tano pengine hata kuzidi, una kipaji sana mrembo"

"Nilifata tu recipe, si ngumu kihivyo"

"Acha kujikataa mrembo si kila mtu mwenye recipe anaweza kupika chakula kitamu kiasi hiki"

"Ni chakula tu... Unazidisha sifa"

"Hahaha! Mimi nakuwa mkweli tu mrembo"

"Usiniite mrembo... bhana, mimi... sio mrembo mimi ni Bianca" aliongea Bianca kwa kujiumauma mdomo na aibu maana sifa zilimzidia mpaka akaona shida kuongea

"Sawa mrembo Bianca" aliongea Jimmy kwa tabasamu, alivutiwa sana na Jinsi sura ya mrembo huyo inavyokuwa akipatwa na aibu

Ile anataka kuendeleza kumwaga sifa kedekede mara paap mlango unafunguliwa na nurse nshangazi kuingia na gurudumu lenye madawa

Jimmy alilaani ndani kwa ndani kwa kukatizwa na nurse huyo aliyeingia humo bila hata ya kugonga mlango
"We mshangazi ndio nini sasa kukatiana stimu asubuhi-asubuhi mbona mimi jana usiku sikuwakatizia starehe yenu?" alijiwazia kichwani mwake

"Muda wa kumeza dawa umefika" aliongea Bianca na kunyanyuka akimsogelea nurse ambaye alikuwa akiandaa vidonge vya kumeza na maji kwenye glass.



TO BE CONTINUED.................
 
Kama mtunzi hii ni simulizi yangu ya kwanza kuandika na kuitsngaza nje ya jukwaa husika. Mimi ni mwandishi wa simulizi kutoka jukwaa la fasihinet.com ya boss singanojr 😁

Nisielezee ssna kuhusu mimi. Mimi ni Samuel jk(jins halisi) lskini nalipenda neno Euphoria kutokana na maana iliyopo na hii ni Imulizi yangu ihusuyu uchaei, mapenzi, mapigano, fantansia n.k inaitwa SOLO KING: ANCIENT LEGACY

Ninaposema uchawi simaanishi kuwangisna usiku😅😅 Ni new fashioned kinda type!

UTANGULIZI

Hapo zamani, kabla ya historia kuandikwa, aliishi mtu mmoja ambaye alivuka mipaka ya asili. Alikuwa mchawi mwenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani, aliyefikia upeo wa juu lakini jina lake lilisahaulika, na urithi wake ulipotea kwa muda mrefu.

Kitu kimoja kilichobaki ni kitabu cha kale, kilichoandikwa kwa lugha zilizozungumzwa zamani, lugha ambazo sasa ni za kihistoria. Kitabu hicho kilijulikana kama FORBIDDEN GRIMOIRE, na kilikuwa na masalia ya maarifa yake pamoja na nguvu zisizo za kawaida.

Karne zilipita, falme zilikuja na kupita, dunia ilibadilika, na uchawi ukawa ni hadithi tu za kusadikika.

Lakini hatima haikupotea. Kijana mmoja aitwaye Jimmy anakuja kubeba hatima yake bila kujua.

Usikose simulizi hii ya kusisimua, yenye matukio ya ajabu na mabadiliko ya nguvu. Inamhusu kijana machachari aitwaye Jimmy, anavyopitia changamoto na majira, na jinsi anavyotoka kuwa dhaifu hadi kuwa mwenye nguvu kubwa.

°°°°°°°°°°

CHAPTER 01: Normal life(maisha ya kawaida)


Yalikuwa ni majira ya asubuhi jijini dar es salaam chini Tanzania jua likichomoza kutoka mashariki na mwanga hafifu wenye kupendeza macho, upepo wa asubuhi ukivuma taratibu na kufanya hali ya hewa kuwa yenye utulivu. Watu walikwishaamka kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya kutafuta ridhiki za kila siku.

Apartment ya hali ya kati yenye ghorofa tatu kwenda juu ipatikanayo maeneo ya Mbezi majirani walikuwa wakiendelea na shughuli zao za hapa na pale. Ndani ya apartment hiyo ghorofa la kati kwenye chumba kidogo cha wastani alionekana mwanaume kijana akiwa amelala fofofo mpaka wakati huo na hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka muda huo, ni wazi kwamba usingizi ulikuwa ni mtamu mno.

Wakati bado amelala mlango wake wa chumba uligongwa kuashiria kuna mtu yupo nje ya mlango wa chumba hiko

"ngo! ngo! ngo!' uligongwa tena safari hii kwa sauti kuzidi mwanzo

"We monica acha kunikata stimu basi" aliongea mwanaume huyo kwa sauti ya lawama

"Amka kumekucha"

"Sawa naamka subiri kidogo" alijibu akiwa bado amelala

Mara mlango ukafunguliwa na kuingia mwanamke mrefu wa wastani, mweupe wa ngozi na kwenda kufungua dirisha lililokaribu na kitanda kisha kulivuta shuka alilojifunika mwanaume huyo kwa fujo

"Asee we monica kuna kitu unakitafuta sio?" Hatimae aliweza kuamka akiwa hana furaha kabisa

"amka wewe kumekucha unalala-lala hovyo acha uvivu dogo"

"Si uniache sasa kwani kulala kwangu hovyo unapungukiwa na nini?" Aliuliza na bila kusubiri jibu alirudi zake kulala lakini alikuja kushtuka kwa kifinyo mguuni na kwa hasira alinyanyuka akitaka kumkamata lakini ilionekana monica alikuwa ashajipanga kwani alikimbia nduki kutoka chumbani humo kabla hata hajadakwa

Hehehe na ubabe wote lakini mwisho wa siku unakimbia tu" alijiongelesha na kuamka maana usingizi ulikuwa umekata kabisa

Hao walikuwa ni dada na kaka wa damu walikuwa wakilumbana asubuhi hio monica akiwa ndie mkubwa na mwanaume huyo aitwae jimmy akiwa mdogo

Ndugu hao walikuwa ni kama paka na panya waishio pamoja kwani kila siku ni malumbano tu na ugomvi usioisha muda yaani kifupi ni kwamba upendo wao kama ndugu ulikuwa ukidhihirishwa kwa ugomvi tu, ni bahati sana kuwakuta wakiwa pamoja bila kuzozana.

Mwanaume huyo ambaye kwasasa anatambulika kama jimmy alikuwa kijana ambaye umri wake ulikuwa miaka ishirini ya mwanzoni(early 20s).

Alikuwa ni mwanaume mtanashati na mweupe wa ngozi kama dada yake, alikuwa mrefu wa wastani na asubuhi hio alikuwa amevalia suruali nyepesi ya kulalia rangi nyeusi juu akiwa kifua wazi kuonyesha mwili wake machachari uliojengeka vizuri kuanzia mabegani mpaka kiunoni kama mwanariadha na urefu wake wa wastani

Basi Jimmy kama ilivyo kawaida ya wanaume wengi baada ya kuamka aliupasha mwili joto kwa push-ups na sit-ups kadhaa kabla ya kwenda kuusafisha mwili na baada ya kumaliza shughuli ya usafi wa mwili alivaa nguo za kawaida na kuzichana nywele zake fupi zilizonyolewa mtindo wa low fade na kumfanya azidi kuwa mtanashati haswaa. baada ya kumaliza mdogomdogo alielekea sebuleni

Kufika sebuleni aliwakuta wanawake wawili ambao ni muhimu kwake na kukamilisha familia yenye idadi ya watu watatu ambao ni yeye, dada yake na mama yake mzazi. Baba yao yeye dada yake alikwishatangulia mbele za haki miaka mingi nyuma wakiwa na umri mdogo

"Shikamoo mama" jimmy alimsalimia mama yake kipenzi

"Marahaba, umeamkaje mwanangu"

"Sio salama mama kuna kunguni alikuwa akinipigia kelele"

"Kuwa na heshima dogo nani unamuita kunguni?"

"Wewe unaniheshimu?"

"Dogo......."

"Hey hey mtapasua ngoma za masikio ysngu jamani nimeshachoka makelele yenu ebo! "mama yao alilalama ilioonekana kweli alikuwa na kazi ngumu sana kuwalea hao watoto mpaka kufikia wakati huo

"Angalau kuwe na amani basi tukipata kifungua kinywa ndio muendelee na hizo ngojera zenu" aliendelea na ndugu hao waliamua kutii mara moja

"Enhee asubuhi hii tunakula nini mama nimemisi sana chapati zako tamu kama asili" jimmy aliuliza

"Tena zipo za kutosha tu ni wewe na tumbo lako" monica alidakia

"Haya ndio mambo sasa ndio maana mama yangu nakupenda huwaga huniangushi kwenye misosi hahaha" jimmy alianza kumsifia mama yake

Basi familia hiyo walikula na kifungua kinywa kwa amani mpaka kumaliza na kila mmoja aliendelea na mambo yake jimmy aliondoka kwenda kwenye kibarua chake, dada yake akielekea chuo akibaki jimmy ambaye muda huo alikuwa amemaliza elimu yake ya advance akisubiri kuanza chuo hivyo alibaki peke yake

Licha ya kusubiria "selection" za chuo haikumaanisha akae tu kizembe,hapana kijana huyu alikuwa akifanya kazi ndogo ndogo za u'dayworker angalau apate pesa za kujikimu hapo baadae isitoshe familia yake ilikuwa ni ya hali ya kawaida hivyo kuna mda pesa inakosekana


Hakukaa sana humo ndani aliondoka baada ya kufungo mlango wa apartment yao.

°°°°°°°°°°

Muda ulienda na hatimae kufika saa kumi jioni. upande wa mbezi beach beach ufukweni mwa bahari ya hindi kulikuwa kumechangamka sana mida hio kutokana na watu kuwa wengi wakipunga upepo wa jioni hio ulioambatana na baridi kwa mbali wengine wakiogelea majini wengine wakiwa na wenzi wao wakifurahia mandhari nzuri ya bahari na kadhalika

ilikuwa ni kawaida kwa jimmy baada ya kumaliza mishemishe zake kuja hapo kutulia kabla ya kurudi nyumbani na siku hiyo alionekana kumaliza mapema sana. alienda kwenye chimbo lake pendwa la kila siku na kujilaza kwenye mchanga bila kujali kama atachafua nguo au lah

kabla ya kulala alijifunga kitambaa kichwani ili nywele zake zisiingie mchanga na kuuchapa usingizi.

Moja ya sifa ya jimmy ni kupenda sana kulala na hachagui sehemu yeye popote kambi tu ilimradi ni salama na ana usingizi wa kutosha

ameshalalamikiwa sana kulala mchana lakini yeye wala hajali anadai kwamba usingizi wa mchana na jioni ni mzuri sana kwa afya ya akili huongeza nishati mwilini na kuondoa uchovu na kupunguza msongo wa mawazo n.k

Muda ulizidi kusonga taratibu, jua nalo lilianza kuzama hatimae giza kuingia Jimmy akiwa bado amelala mahali alipokuwa. Muda ulikuwa ukisoma saa moja na dakika arobaini na hakuonyesha dalili ya kuamka muda huo

°°°°°°°°°°

Katika sehemu tulivu yenye bustani nzuri iliyopendeza kulikuwa na watu wawili wamekaa kwenye benchi mmoja akiwa ni mwanaume wa makamo na mwingine akiwa ni mvulana mdogo ambaye kwa kumuangalia tu alikuwa kati ya miaka sita au saba. Muda huo ulikuwa ni jioni, mwangaza wa jua uking'aa kwa rangi yake ya dhahabu na kufanya mandhari waliyokuwa wakiangalia kuzidi kupendeza.

"Jimmy"

"Naam*

" kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa ata kama unapitia changamoto pambana mpaka mwisho usikate tamaa sawa? "

" sawa baba nimekuelewa lakini kwanini unaniambia saaahivi" aliuliza

"kwasababu nataka uwe mwenye nguvu, siku zote wenye nguvu huwa hawakati tamaa kirahisi"

"kwahiyo wale wanaokata tamaa ni dhaifu?"

"Ndio, vipi unataka kuwa dhaifu?"

"Hapana"

"vizuri kuanzia sasa nataka uwe 'strong' mwanangu ili ikifika wakati ambao mimi sioo uweze kuwalinda dada na mama yako na wale wote uwapendao*

"Nakuwaje sasa mwenye nguvu?"

"kuhusu hilo usijali mimi nipo nitakufundisha"

Hayo yalikuwa ni maongezi kati ya jimmy na Baba yake kipindi cha nyuma wakati marehemu baba yake alipokuwa hai

°°°°°°°°°°

Mara taratibu jimmy alifumbua macho yake ikionyesha ni wazi alikuwa kwenye kumbukumbu akiikumbuka siku aliyokuwa akiongea na marehemu baba yake na hakutegemea kama siku ile ingekuwa ndio siku yake ya mwisho kumuona baba yake kwenye uso wa dunia kwani siku iliyofuata baba yake alifariki kwa kupatwa na ajali mbaya.

Alinyanyuka mahali pale na kuikung'uta michanga iliyonasa kwenye nguo zake kisha alijinyoosha vizuri na kupiga miayo

"Nina njaa sasa ngoja ninunue chochote kitu angalau nipooze kidogo kabla ya kurudi nyumbani kula" alijiongelesha na kuingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa shillingi elfu tano kisha kuangaza huku na huko na kugundua kulikuwa hakuna wate wengi na mda ulikuwa umeenda

"ina maana nimelala mda mrefu kiasi hiki" aliongea baada ya kuangalia muda kwenye saa yake ya mkononi na kukuta ni saa mbili na nusu

"Nitasema kulikuwa na foleni kubwa" alijiambia na kuanza kuzipiga hatua kuondoka maeneo hayo.

°°°°°°°°°°

Upande wa mbezi kwenye apartment ya waishio jimmy na familia yake sebuleni alionekana mama yao akiwa peke ameketi kwenye meza ya chakula na chakula kilikuwa tayari kimeandaliwa mezani na alikuwa akiwasubiri wanae warudi waweze kula.

"Hivi hawa watoto mpaka muda huu bado hawajarudi tu" alilalama mwanamama huyo

Alichukua simu yake aina ya Samsung S22 na kufungua kisha kuingia kwenye apo ya 'contact' na kuanza kuisaka namba ya bintiye monica na alipoipata alipiga lakini aliishia kusikia sauti nyororo ikimwambia "namba unayopiga haipatikani kwa sasa* na kuishia kukunja sura

Alipoona hivyo alimpigia mwanae Jimmy na uzuri ni kwamba alikuwa hewani kwani simu ilikuwa ikiita

°°°°°°°°°°

" Twiiii twiiii twiii twi twiiii!!" simu ilikuwa ikiita kwa nguvu kama 'mic' mbovu, Ilikuwa ni kiswaswadu aina ya Tecno zile za zamani

Jimmy alipokea simu baada ya kuona ni mama yake ndiye anapiga

"Hallo ma...."

"Uko wapi?" alimkatisha na swali

"Ndo niko njiani naelekea huko nyumbani" alijibu huku mkononi alikuwa ameshika Ice cream aliyokuwa anailamba huku akiongea na simu

"Mpigie rafiki yake na dada yako umuulize monica alipo maana kwenye simu hapatikani"

"Usiniambie bado hajarudi mpaka muda huu"

"wewe umerudi?"

"lakini si ndo niko njiani"

"utajua mwenyewe fanya ujue dada yako yuko wapi mana kila siku kunitia presha tu"

"usijali nafika naye hapo nyumbani"

"eeh ndio mmefike mapema chakula kinapoa"

"sawa mama" kisha akakata simu na kumpigia simu mtu mwingine

°°°°°°°°°

Ndani ya Bar moja maarufu ya kisasa iliyoko maeneo hayohayo ya mbezi beach watu walionekana wakipata huduma yao ya ulevi, kila mmoja akiwa bize na chupa yake.

Sasa kulikuwa na mwanamke aliyeketi sehemu yake akinywa bia kwa fujo sana huku machozi yakimtoka na pembeni yake kukiwa na mwenzake ambaye alikuwa akimuangalia kwa kumuonea huruma

Wakati akiendelea kunywa kulikuwa na mziki ukilia taratibu kusindikiza huzuni yake

🎶Ila siri ya penzi, siri ya moyoS Siriya nani?🎶

🎶Siri ya chozi ni maumivu ndani kwa ndani🎶

Alinyanyuka mwanamke huyo na chupa yake ya bia lakini kwa bahati mbaya alikosa balance kutokana na kulewa hivyo kudondoka lakini hakuweza kufika chini kwani alitokea mwanaume na kumdaka

Na mwanaume huyo hakuwa mwingine bali ni jimmy

"Sara, asante kwa kunipa taarifa" jimmy alishukuru kwa moyo wa dhati kabisa akimlenga yule mwanamke aliyekuwa amekaa na alikuwa ni rafiki yake na monica

"anytime" akimaanisha muda wowote

Monica baada ya kuona aliyemzuia asidondoke ni kaka yake ndio alizidisha kulia ni kama vile jimmy amefungua maji ya bomba kwani alilia sana kiasi cha jimmy kupatwa na wasiwasi na kumgeukia Sara akitaka maelezo

Sara alimpa ishara ya kwamba amevunjwa moyo yaani mapenzi ndiyo yanayomliza

"Unajua mapenzi ni ya ajabu sana, na sijawahi kuyaelewa. Unatoa moyo wako, uaminifu wako, yaani kila kitu ili mwisho wa siku uje kulipwa na maumivu? Mapenzi ni kama mchezo flani hivi ambao sheria zake hazijawahi kueleweka

Love's a bullsh*t you know?" aliongea monica huku machozi yakimtoka

"I hear you, kila neno, maumivu yatokayo kwenye moyo wako, nayaelewa na siwezi kukaa hapa nikikuangalia tu ni lazima nimshikishe adabu huyo mpuuzi ila unapaswa kujua mapenzi ndivo yalivyo, kuna muda yankuacha na maumivu, maswali na majeraha ya moyo ambayo huchukua muda kupona

Lakini sikia.... Hutakiwi kuwa mnyonge hivi na kulialia unapaswa kujikaza. Sio mapenzi yanayokuumiza bali ni mpuuzi mmoja anacheza na hisia zako. Cha kufanya ni kusahau tu na kuanza upya you're still of worth something true" alimfariji dada yake na kumpa moyo na kwa kiasi flani alifarijika

"Nilidhani labda utaanza kunifokea na kunisema" monica aliongea

*na kweli ningekufokea sema tu muda haukuwa sahii" alijiwazia na kuishia kumpa tabasamu tu

"ata kama ningekufokea kesho ungesahau tu" aliongea na kumfanya monica atabasamu

"Twende nyumbani mama anatusubiri kwaajili ya kula" aliongea jimmy akiwa ameshaanza kupiga hatua na monica alianza kumfata kwa nyuma kama kifaranga, ungedhani labda jimmy ndio kaka mkubwa kutokana na mwili wake pamoja na urefu.

Wakati anakaribia mlango wa kutokea aligongana na mwanamke aliyekuwa akiingia kwenye bar hiyo, haikueleweka ni makusudi ama kutokuwa makini kwa mwanamke yule mpaka kugongana mabega

"Samahani dada" licha ya kosa kutokuwa lake jimmy aliomba radhi na kuuelekea mlango

"Subiri kwanza kijana unaenda wapi?" aliongea yule mwanamke

"Naondoka" jimmy alijibu lakini alipofika mlangoni aliweza kuzuiwa na mabaunsa wawili wakisimama mbele yake

Alikuwa ni aina ya wale wanawake wenye mashauzi sana, maringo meengii na kujiona wa matawi ya juu sana kiasi kwamba aliwadharau binadamu wenzake aliowaacha mbali kimaendeleo

"Si umeombwa radhi na wewe" Monica aliingilia kati ni kama vile sio yeye aliyekuwa akilia dakika chache nyuma

"Haitoshi"

"hehehe eti haitoshi, unajiona nani kwani?"

"Na wewe ni nani wa kuingilia yasiyokuhusu" aliongea mwanamke yule akisindikiza na sonyo kama la jini kabula

"kwa taarifa yako huyo ni kaka yangu hivyo yananihusu bibiye halafu inaonekana wewe ndio mwenye kosa ni wewe ndiye uliyemgonga mwenzio halafu na bado ukaombwa msamaha ety" haitoshi" screw you!

"Inatosha Monica, unatakaje ili tumalizane haraka?" jimmy alimtuliza dada yake kisha kuuliza

"piga magoti"

"Unasema?"

"Nimesema piga magoti kwani we kiziwi?" aliongea na kumfanya jimmy aachie tabasamu ambalo ni monica pekee alilielewa



TO BE CONTINUED..........

Though kuna makosa madogo ya uandishi lakini sio mbaya ninaeleweka na nitazidi kujirekebisha kadri diku zinavyozidi kusonga

Ndugu wasomaji wa simulizi za kusisimua mnikaribishe writer katika ulimwengu wenu nipate nafasi ya kuwaburudisha☺️

NB: Simulizi bado haijakamiliks inaendelea na nitakuwa nashushs kwa vipande vitatu(kipande kimoja kwa siku. J5, Alh na J'mosi)
Kazi nzuri
 
Bt Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 12: Najua unaitwa Biancalina

Jimmy alikuwa akijisikia vizuri sana baada ya kushiba kifungua kinywa, afya yake ilikuwa imara hakuona ulazima wa kutumia dawa lakini hakutaka kufanya mambo yawe magumu kwa upande wa nurse hivyo alikubali kumeza vidonge kishingo upande

Baada ya hapo alimuuliza nurse utaratibu wa kuondoka maana hakuona umuhimu wa kubaki hospitalini ilihali tatizo limekwisha isha, suala la kukaa hospitalini wiki nzima kama daktari alivyosema hakutaka kuliingiza akilini

"Samahani, nurse. Ningependa kujua utaratibu wa kutoka hospitalini. Nadhani afya yangu imeimarika kwa sasa" aliongea Jimmy

"Mr Jairo, naelewa unavyotamani kuondoka, lakini hali yako bado haijaimarika ipasavyo. Daktari alipendekeza upumzike kwa wiki moja"

"Nashukuru kwa kujali, lakini kwa kweli najisikia vizuri kabisa. Sioni sababu ya kuendelea kukaa hapa"

"Naelewa, lakini wakati mwingine dalili zinaweza kurudi ghafla. Kukaa hapa kwa muda mfupi zaidi kunatupa nafasi ya kukuangalia na kuhakikisha hutopata matatizo yoyote hapo baadae. Ni kwa afya yako."

"Ondoa wasiwasiniko sawa nachotaka ni kurudi nyumbani na kuendelea na maisha yangu ya kawaida sina hamu ya kukaa hapa"

"Sitokulazimisha kama umeamua, hata hivyo ingependeza umsubiri daktari akague afya yako kwa mara ya mwisho"

"Kama ni hivyo sina neno, mradi niondoke tu basi"

"Sawa, nitaandaa nyaraka zinazohitajika. Utahitaji kusaini fomu ya kutoka" aliongea nurse huyo na kuondoka kwenda kumuita daktari na kuandaa fomu za kusaini

"Una uhakika hali yako ni shwari? Isije ukazimia huko njiani ukanitwika mzigo wa kukurudisha tena hospitani" aliongea mrembo Bianca

"Mrembo wasiwasi wa nini? Kuwa na imani kidogo na imimi... Niko sawa"

"Sawa"

Dakika mbili Daktari aliweza kuja kwenye chumba hiko na koti lake jeupe, alikuwa ni mzee kiasi, mwenye kitambi na mfupi.

"Habara za asubuhi bwana Jimmy Jairo" alisalimia daktari huyo alipoingia

"Nzuri dokta, Jimmy linatosha"

"Sawa Jimmy, nurse hapa ameniambia unataka kuondoka leo"

"Ndio, nadhani sina sababu ya kuendelea kukaa hapa hospitalini, afya yangu imeimarika"

"Ni jambo jema kusikia una afya njema, lakini kabla Sijakuruhusu uondoke, ningependa kufanya uchunguzi wa mwisho kuhakikisha kila kitu kiko sawa" aliongea Daktari huyo na Jimmy alikubaliana naye kufanya vipimo vya mwisho

Daktari alifanya vipimo, alisikiliza mapigo ya moyo, aliangalia shinikizo la damu na kumuuliza Jimmy maswali macheche na aliweza kurithika na afya yake.

Nirse aliingia mkononi akiwa ameshikilia fomu za kusaini pamoja na kalamu alienda moja kwa moja kumpatia Jimmy, naye alisaini fomu hizo na kumrudishia.

Alichukua prova jeupe na kulivaa lenye maandishi mbele yasomekayo "Be Bold, Be You" pamoja na kitabu chake kisha alimsogelea nurse karibu na kumnong'oneza masikioni

"Naona kuna njemba ilifurahia usiku wa jana. Natumai kuta hazikuteseka sana!" alinong'ona na kumfanye nurse huyo atamani apotee kichawi kuficha aibu yake lakini isingewezekana, aliishia kuangalia chini kukwepa kumuangalia usoni na Jimmy aliishia kutabasamu tu

"Asanteni nyote kwa huduma nzuri sana" Jimmy alitoa shukrani zake ambazo ni daktari pekee aliitikia

Jimmy aliongozana na Bianca kuondoka hospitalini, ile wanatoka nje ya chumba tu macho kwa macho na walinzi ilionekana walikuja na Bianca na waliishia nje ya mlango ni vile tu wakati Jimmy anamuita Bianca hakuweka umakini kuangalia

Safari hii walikuwa ni makini mno ni wazi kwamba hawakutaka lile kosa kujirudia, walipomuona Jimmy walitoa salamu zao kwa ishara isitoshe bila yeye ingekuwa ni habari nyingine kabisa wala wasingekuwa hapo walipo

Walikwenda mpaka chini ya ghorofa na kwenda sehemu ya maegesho ya magari na mbele yao kulikuwa na gari tatu nyeusi, moja ikiwa ni Toyota Alphard G nyingine zikiwa ni Land rover defender

Jimmy na Bianca waliingia kwenye Alphard huku walinzi walinzi wakiingia kwenye land rover na safari ya kuondoka hospitalini humo ilianza

Njiani kwenye msafara wa magari hayo ndani ya Alphard kulikuwa kimya sana, ukiachana na dereva ambaye yuko bize na kuendesha gari wawili hao walikuwa kimya wakitazama mandhari kupitia dirishani

"Jim" hatimae Bianca alivunja ukimya

"Naam" aliitikia

"Una miaka mingapi?" bianca alimuuliza

"ishirini na mbili kwanini unauliza? " Jimmy alijibu

"Hamna nataka kukujua zaidi" aliongea Bianca huku akiangalia pembeni na Jimmy alitabasamu

"Kama una maswali mengine uliza tu mrembo nitakujibu yote kwa usahihi" Jimmy aliongea kwa kutabasamu

"Okay, ulijifunza wapi kucheza piano?"

Jimmy alitoa tabasamu baada ya kuulizwa swali hilo kisha alijibu "Nimefundishwa na mzee wangu, aliniambia tu anataka kunifunza mwanzoni sikuwa nataka kwasababu niliona ni usumbufu na kujiumiza vidole tu lakini baada ya kushuhudia akicheza "Moonlight sonata" nilivutiwa sana na ndiyo nikakubali"

"Moonlight sonata? Ndiyo ule uliokuwa ukicheza kule Mall?" Bianca aliuliza

"Ndio, unataka nikufundishe?" Jimmy alitingishakichwa kukubali na kumuuliza kama anataka amfunze

Bianca alitingisha kichwa kukubali na kutabasamu, lilikuwa ni tabasamu lenye kutoa nuru usoni, tabasamu lilipendezesha sura yake na kuwa mrembo maradufu hali iliyofanya mapigo ya moyo wa Jimmy kwenda kasi.

"Usiwaze mrembo hilo hesabia tayari ombi lako limekubaliwa" aliongea Jimmy na kimya kifupi kilifuata

"Vipi mbona huniulizi swali? Hutaki kunijua? " Bianca alipngea baada ya kuona Jimmy yuko kimya

"Najua unaitwa Biancalina Johnson Merizesta, una miaka ishirini, Una jina zuri sana lenye maana ya" Little white one" Bianca ni neno la kiitaliano lenye maana "white" na lina lenye maana ya "little" ni jina zuri sana linaloashiria usafi na upole kitu ambacho kwako ni kweli, sijui wazazi wako walifikiria nini kukupatia hilo jina lakini hawakukosea" Kwa maelezo haya ilitosha kumfanya Bianca mashavu yake kuwa mekundu kama nyanya, asikudanganye mtu wanawake wanapenda sana kusifiwa.

"Umejuaje naitwa Biancalina?" Bianca aliuliza na Jimmy aliishia kumuonyesha ishara kwamba ni kaka yake ndiye aliyemwambia

"Kipi kingine unajua kuhusu mimi?" Bianca aliuliza

"Sijui mengi sana ila nitakwambia machache niyajuayo"

"Najua rangi yako pendwa ni nyeupe, tangu mara ya kwanza kukuona ulivaa gauni jeupe, ulipanda gari rangi nyeupe, hereni ulizovaa masikioni ni nyeupe kitu ambacho hadi sasa umevaa hereni nyeupe, na katika mavazi uvaayo haikosekani rangi nyeupe, mfano hata hapo umevaa T-shirt jeupe, raba nyeupe mkoba wako ni mweupe, haishangazi hata prova uliloninunulia ni jeupe" aliongea kitaalamu sana na hakuwa akidanganya, kama ni kujitafutia point mbele ya mrembo huyo itoshe kusema amepata pointi za kutosha

Upande wa dereva alikuwa akitoa tabasamu kisirisiri tu, alitamani yeye ndkyo angekuwa Jimmy akimwaga voko mbele ya mrembo kama huyo ambaye ni ndoto ya kila mwanaume rijali kuimiliki, alijiambia kama ni bahati basi Jimmy anabahati za kutosha

"Japokuwa mimi sio mtaalamu wa mambo ya afya lakini kupitia elimu yangu ya darasani nadhani unasumbulia na ETD-Eustachian Tube Dysfunction(Mrija wa Eustachian)

ETD ni ugonjwa wa masikio ambapo mrija wa Eustachian unapoziba au kushindwa kufunguka ipasavyo, husababisha mabadiliko ya shinikizo la hewa(pressure) kwenye sikio, na matokeo yake ni kusikia kwa shida au kusikia kwa kupungua na kuongezeka, maumivu ya masikio na kadhalika

Sababu kuu za hali hii ni maambukizi kama vile mafua au sinusitis, mzio (allergies), au mabadiliko ya ghafla ya shinikizo la hewa (mfano ukiwa kwenye ndege au maeneo yenye miinuko mikubwa). Wakati mwingine, ni kwa sababu tu mirija ni myembamba, ndiyo maana watoto huwa na matatizo ya masikio mara nyingi zaidi kuliko watu wazima.

Mpaka msafara huo wa magari matatu unafika getini mwa Apartment aishiyo Jimmy, Jimmy alikuwa amezungumza mengi sana na alishuka na kumkaribisha Bianca aingie ndani lakini aligoma akisema siku nyingine kwamba kuna sehemu anawahi

Jimmy hakuuliza ni wapi aendako zaidi alishukuru kwa kila kitu na baada ya msafara huo kuondoka aliingia ndani mpaka kwenye floor yao

Hakukuta mtu ndani ikiashiria kwamba Mamaye na dadaye wapo kwenye shughuli zao za kila siku.
Muda ulikuwa ukisoma saa tatu na jimmy aliona ni mapema sana na hakuwa na cha kufanya na wazo la kumjia akilini mwake ni kulala tu maana usiku wote wa jana hakulala kabisa.

Aliwasha feni ya ya sebuleni, alivua prova na kujitupa kwenye kochi na alifumba macho kama utani tu na dakika tano mbele alikuwa ametulia tuli akiufurahia usingizi wake

Masaa mawtano mbele muda ukiwa ni saa nane na dakika kadhaa Jimmy aliamka kutoka usingizini kutokana na kengele ya mlango ikiashiria kwamba kuna mgeni alikuwa akibisha hodi

Aliamka kivivu na kujivuta mpaka mlangoni na kuufungua

"Unalala sana bro nakupigia simu hupatikani" alikuwa ni Cid na aliingia ndani kama kwao na kwenda kukaa kwenye kochi

Na Jimmy sasa ndio anakumbuka simu yake iliharibika akiwa kwenye purukusheni na wale maninja wa Yami no Senshi na aliishia kutingisha simu kwa masikitiko, alikipenda sana kiswaswadu chake lakini kwa bahati mbaya hakipo tena mikononi mwake

"Nadhani nilisahau kukutaarifu kwamba sina simu anyway nini kimekutoa huko mpaka huku ukiwa serious hivyo" aliongea Jimmy akienda kuketi kwenye kochi pia

"Nimekupigia simu hupatikani, nimekuja hospitali sikuoni ndiyo kuambiwa umeondoka, yani siku moja bbaada ya kuamka kwenye coma?"

"Miujiza bro, sala zanu zimejibiwa msisahau kupeleka sadaka za shukrani kanisani" Jimmy alitania na Cid aliishia kucheka

"Kabla ya kukuambia kilichonileta nina maongezi mengine pia" Cid aliongea akiwa serious

"Masikio yangu yako wazi bro ni wewe kuamua uanze kuongea saa ngapi"

"Jimmy mimi ni rafiki yako?" Cid aliuliza akitaja na jina kabisa, Jimmy alishamzoea kusikia akimuita bro hivyo kutaja jina lake aliona kweli yupo serious

"Ndio kwanini unauliza swali kama hilo?"

"Unajua bro licha ya mimi na wewe urafiki wetu ni wa muda mfupi lakini ninakuchukulia kama mwanafamilia na familia yako ni familia yangu pia?"

"Unataka kusema nini?"

"Nacho maanisha ni kwamba usinifiche upatwapo na matatizo iwe ni familia au wewe binafsi"

"Lipi nimekuficha bro?" aliuliza Jimmy makusudi licha ya kujua aliachomaanisha

"Unaona sasa bado unajifanya hujui, familia yako imetekwa lakini ukanificha licha ya kuniomba msaada, nilipokuja kugundua hilo nimeona unanichukulia poa.. You took me granted"

"Ni kwamba tu sikutaka kukusababishia matatizo"

"Nimenusurika kufa mara mbili bro na ni wewe uliyeniokoa hivyo ni haki yangu kukusaidia acha kutumia ngao ya matatizo"

"Kama nilikaribia kupoteza uhai unadhani ningekushirikisha ungetoka salama? anyway yameshapita tugonge yajayo"

"Lakin......"

"Next time sitokuficha usiwaze aya niambie hiko kingine kilichokuleta unikatie usingizi wangu" Jimmy alimkatisha

"Kesho ni siku yangu ya kuzaliwa hivyo nakualiksa wewe pamoja na familia yako nyumbani kuungana nasi kwenye siku muhimu kwangu"

"Ooh hongera sana bro unafikisha mingapi?

" Ishirini na tano"

"Aah kumbe wewe ni kaka yangu kabisa asee, sema nini braza sina maokoto ya kukuletea zawadi"

"Zawadi haina umuhimu kikubwa uwepo wako tu, inatosha" aliongea Cid akiangaza huku na huko ndani ya nyumba

"Monica yuko wapi?" aliuliza

"Yupo chuo anapiga ung'eng'e"

"Chuo gani bro?"

"Ebu acha maswali ya ajabu ajabu kaka kwanini usimuulize wewe akirudi"

"Unazingua sana kaka hata hivyo sikai sana" aliongea Cid akinyanyuka

"Vaa hilo prova tuondoke" Cid alichukua prova lililopembeni ya kochi na kumrushia.Jimmy

"Wapi tena?" Jimmy aliuliza na Cid aliishia kutabasamu tu asimwambie kitu

°°°°°°°°°

Kesho asubuhi na mapema jimmy alikuwa amewahi kuamka na aliketi chini sakafuni chumbani mwake mkao wa kufanya tahajudi kifua wazi akifumba macho yake na kuvuta pumzi nyingi ndani na kuzishusha taratibu

Pembeni yake kukiwa na kitabu cha kale kimefunuliwa kurasa kadhaa

"Huu ni upuuzi sasa!" aliongea kwa kukunja ndita, ilionekana ni mara yake ya kufanya tahajudi

Katika kitabu kile kimeandikwa kwamba kabla ya kutumia kanuni!/maarifa yaliyomo anatakiwa awe na nguvu/imara, yaani kimwili, kiakili, kihisia na kiroho na ili kufikia kuwa na nguvu kiroho anatakiwa kwanza kuwa na nguvu kimwili, kiakili na kihisia ndipo iwe rahisi kwake kuwa na nguvu kiroho

Kuhusu suala la kuwa na nguvu kimwili halikuwa na shida yoyote maana tayari alikuwa nazo kwa kujifua zaidi ya miaka kumi, shida inakuja kwenye kiakili na kihisia sasa na mojawapo ya njia ya kuifuata ni kufanya tahajudi

Hawezi kuwa imara kihisia pasipo akili yake kutulia, kanuni inasema inahitajika akili na hisia kubalance

Picha linaanza kila akijaribu kutuliza akili yake inamuwia vigumu na kuanza kuwaza vitu vya ajabu ajabu akilini kibaya zaidi makelele ya kunguru kulialia vilichangia

Aliachana nayo na kufungua kurasa nyingine na kusoma na aliachia tabasamu

"Sio mbaya hii njia ni rahisi sana ngoja nijaribu" alijisemea na kunyanyuka kisha kuchukua nguo ya juu nyepesi na kutoka humo chumbani hakusahau kitabu chake pia

"Unaenda wapi?" ilikuwa ni sauti ya mama yake ambaye alikuwa akifanya usafi wa ndani baada ya kumuona Jimmy akiukaribia mlango wa kutokea

"Aah mama kumbe umeamka mapema, shikamoo!"

"Marahaba mwanangu wapi alfajiri yote hii" aliitikia salamu na kuuliza maana lilikuwa ni jambo la kushangaza kwa Jimmy kuamka mapema tena saa kumi na moja

"Nakwenda kufanya mazoezi"

"Sawa mazoezi mema!" alimtakia heri na kuendelea na kazi zake

Muda mchache mbele Jimmy alikuwa amesimama akiitazama bahari iliyoko mbele ya macho yake



TO BE CONTINUED..........
 
BY Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 13: Upuuzi wa jambo matokeo yake ni hasara


Upuuzi wa jambo au kitu fulani kiwe kidogo au kikubwa siku zote matokeo yake huwa ni hasara

Kupuuza jambo ni kutotaka kujifunza na kuujua ukweli!/siri zilizopo, ni sawa kuujipofusha na mwisho wa siku ni hasara, Historia imetuonyesha jinsi upuuzi/ujinga ulivyosababisha vita, mateso na kadhalika. Yote hayo ni kwa kujitakia
Na hiki ndicho Jimmy anachokwenda kukifanya

Sorcerer kwa lugha yetu ya kibongo tunaita mchawi mkuu, Sorcerer ni mtu mwenye nguvu za kichawi za asili, ambazo iwe kwa kuzaliwa nazo, damu ya ukoo, laana/baraka au uhusiano wa moja kwa moja na chanzo cha uchawi.Uchawi wao hutiririka moja kwa moja kutoka kwao, na huweza kurithishwa kwa njia nyingi sana na Salazar Solren Soledad alikuwa ni mchawi mkuu ambaye nguvu zake amemrithisha Jimmy hivyo ni sawa kusema Jimmy ni Sorcerer pia.

Kwa maelezo ya kitabu ni kwamba Sorcerers nguvu zao zimo ndani yao hawahitaji kutumia dhana yoyote ya kichawi ni kunena au kuamua tu na maajabu yanatokea "they just will it in existence"

Lakini kuamua tu haitoshi inahitajika imani, nia na hisia kwa muhusika ili kuleta matokea, bila hivyo uchawi hutofanya kazi

Kwa kawaida wachawi wakuu wana nguvu kubwa mno kadri wanavyopanda level lakini mara nyingi hukosa udhibiti wa nguvu zao na ili kuweza kuwa na udhibiti wa nguvu zao inahitajika kuwa imara, kimwili, kiakili, kihisia na kiroho

Sorcerer hupanda levo kwa kutumia "Mutation magic" nguvu zao huendelea kukua na kubadilika kulingana na mazingira au hali ya kihemko.

Mutation magic(Uchawi wa mabadiliko) ni aina ya nguvu isiyotabilika inayolenga kubadilisha mwili, akili kwa njia zisizo za kawaida, Kadri sorcerer anavyokuwa na nia thabiti, ndivyo mabadiliko yanavyokuwa makubwa zaidi.

Zipo level tano za Mutation magic kwa Sorcerer ambazo ni 1.Awakening(Kuamka) , 2.Shifting blood(Damu inayobadilika) 3.Breakthrough(Kiini cha mabadiliko) 4.Forbidden(kupaa kwa ukengeufu) 5.Supreme(Ukuu)

Ili kuweza kuamsha nguvu iliyondani yake na kupanda level anapaswa kuwa imara kimwili, kiakili, kihisia na kiroho lakini Jimmy anapuuza na kufanya jaribio kwa sababu tu ya kusoma kwenye kitabu nguvu ya "willpower" kwa Sorcerer

Willpower ni nguvu ya kiakili/uamuzi inayompa mtu uwezo wa kupinga vishawishi, kushinda changamoto, na kuendelea kufuata lengo lake licha ya vikwazo. Inahusiana sana na azimio, nidhamu, na udhibiti wa nafsi

Kwa mchawi, willpower ndiyo msingi wa uchawi. Wakati watu wa kawaida wanategemea nguvu za mwili, mchawi hubadilisha uhalisia kwa kutumia akili/uamuzi na roho yake. Uwezo wao wa kuendesha nishati, kutamka maneno ya uchawi, na hata kubadilisha miili yao hutegemea nguvu yao ya willpower

Jimmy alisimama mbele ya bahari na kunyoosha mikono yake kuelekea baharini

"Aqua Dominus" Jimmy alitamka neno hilo la kilatini lenye maana ya "Lord of the waters" na ghafla upepo ulianza kuvuma kwa kasi kadri muda unavyozidi kwenda

"Rise, Furious Sea! Hear my voice and ascend to the sky"(Inuka bahari kwa ghadhabu, isikie sauti yangu na upae angani) aliyaamuru maji ya baharini kuinuka kama wimbi la tsunami lakini ghafla alihisi kupatwa na uchizi na alianguka chini akipiga magoti na kutema damu mdomoni na hali ile ya upepo kuvuma kukoma

Hakuishia kutema damu tu alianguka chini na kuanza kutetema kama mtu mwenye kifafa na kutoa povu mdomoni. Hayo ndiyo yalikuwa madhara ya kupuuza vitu vidogo vidogo

Baada ya dakika mbili Jimmy aliinuka kwa kujilazimisha mwili ukiwa umeishiwa nguvu, akili nayo ilichoka na alijihisi kama nafsi yake inavutwa na sumanku na aliishia kujiambia kweli anayo safari ndefu sana

Alijikongoja mdogo mdogo kurudi nyumbani na alipofika mara baada ya kusukutua mdomo alijitupa kitandani kulala kuupumzisha mwili wake

°°°°°°°°°°

BLACK SITE

Upande mwingine muda huo kwenye maeneo ya siri yanayotumiwa na mashirika ya kijeshi au kijasusi kwa ajili ya mahojiano na mateso kwawatuhumiwa kulikuwa na watuhumiwa wanne wote wakichezea kichapo na kuteswa mateso makali sana kwenye chumba cha giza chenye mwanga hafifu

Sauti za mijeredi, ngumi mateke na miguno ya maumivu ilisikika ndani ya chumba hiko
Miili ya hao watuhumiwa ilikuwa imejaa alama za micharazo na makovu nyuso zao zilikuwa zimevimba kwa kutandikwa makonde zisiweze hata kutambulika ni za jinsia gani.

Walikuwa wakipewa mateso na wanajeshi wenye miili sugu iliyokomaa kama zege na wenye roho ya kikatili sana

"Fungua mdomo we mshenzi utuambie nani aliyekutuma kwenda kutekeleza mauaji kwa wale wanafamilia. Nani aliyekupa amri? Unadhani unaweza kuingia tu na kuua watu wasio na hatia bila kukutana na madhara?" aliongea mjeshi jitu jeusi tii lenye sura baya na lips za pink kupitiliza kana kwamba alipaka lip stick ya pink

" Familia ni yako? Wale watoto bado wako hai hivyo unapoteza muda wako" aliomngea Rico akiguna kwa maumivu

"Bado unaongea upuuzi we mshenzi" mjeshi alimaka na kumtandika ngumi ya tumbo

"Kama unadhani tutatoa siri kwa kunguni wachache kama nyie basi unakosea" Rico aliendelea kukaza

"Hahaha! We ain't gonna say a damn thing soldiers!" aliongea mwingine huku akitoa kicheko kilichochanganyika na maumivu

Ilionekana baada ya polisi kushindwa kuwahoji na kupata majibu ya kwanini walitelekeza mauaji yale kule shopping mal ilitoka amri kutoka juu kwamba hao watuhumiwa wakabidhiwe jeshi lakini nako mwendo ulikuwa ni ule ule tu, licha ya kuwa ni watu wakawaida lakini walikuwa na mafunzo ya kuvumilia mafunzo makali

Mara mlango wa chumba ulifunguka na sauti ya viatu kutembea ilisikika na kusimama karibu na hao wahalifu

"Inaonekana hamtaki kutoa ushirikiano" ilikuwa ni sauti ya mtu huyo akitoa tabasamu lenye uovu ndani yake
Alikuwa ni Jenerali John Merizesta mkuu wa majeshi ya nchi

"Haha! Even the general himself is here, but let me make myself clear....."

"..... That you won't say a damn thing right?" Jenarali alimsaidia kumaliza sentensi

"If that's the case then lets see how long you're going to shut damn mouth!" aliongea Jenerali na alipomaliza kauli hiyo waliingia wanawake wanne wakibeba sahani kubwa juu kukiwa na dildo za kutosha

Wahalifu wale macho yaliwatoka na kukunja ndita.
Jenerali alikwenda kuketi pembeni kwenye kona akiangalia saa yake, sekunde tano tummoja wa wahalifu wale alikurupuka

"Nitasema nitasema!" aliongea kwa sauti na Jenerali aliishia kutoa tabasamu na kumpa ishara aongee

°°°°°°°°°°

Muda ulisonga kwa kasi mpaka kufikia jioni ya saa kumi na moja, hali ya hewa ikiwa imetulia sana Jimmy na wanafamilia wenzake walikuwa wamejiandaa vizuri, walivaa wakapendeza

Jana yake wakati Cid anamwambia waondoke walikwenda kununua nguo za kuvalia hiyo siku, Jimmy hakuona haja ya kununuliwa nguo yeye na wenzake lakini Cid hakutaka kumsikiliza alienda mbali kumwambia achague size za ndugu zake kitu ambacho Jimmy hakujua, ni kwa kubahatisha tu aliweza kuwachagulia nguo nzuri zilizowatosha

Aliwachagulia magauni marefu rangi tofauti, monica kijani kibichi, na mamaye rangi ya njano na ziliwapendeza huku yeye akivaa Shati lenye mikono mirefu lisilo na kola rangi ya zambarau iliyokolea aliyochomekea upande mmoja wa kushoto kwenye jeans nyesi iliyombana vyema iliyoishia kwenye vifundo "dont-touch-my-shoe" na rubber nyeupe kama theluji, hakika alipendeza

Muda si mwingi gari la kuwachukua kuwapeleka mahali husika lilifika, lilikuwa ni gari jeusi Cadillac Escalade new model

Majirani waliwaonea sana wivu huku wakiwasindikiza na macho mpaka wanaondoka eneo hilo

"Kweli bahati humjia kila mtu kwa wakati wake" aliongea mmoja wa majirani baada ya wao kuondoka

"Acha kujifariji kijana mimi na uzee wangu wote huu sina bahati. Bahati haimpati kila mtu" aliongea jirani mwingine mzee hivi

"babu kama ni una gundu, nenda kaogee maji ya baharini kuondoa hilo gundu mzee"

Lisaa limoja na dakika kadhaa gari la kifahari Escalade lilionekana likikatiza mitaa ya masaki na kwenda kusimama kwenye uzio mrefu wenye geti kubwa.
Baada ya kupiga honi na geti kufunguliwa gari liliingia ndani kwa mwendo wa taratibu Monica na mama walikuwa wakishangaa mazingira ya humo jinsi kulivyopendeza na kuvutia macho, ni Jimmy pekee hakuwa akishangaa sana kwasababu haikuwa mara yake ya kwanza kufika eneo hilo.

Gari lilienda sehemu maalumu ya kuegeshea magari, picha linakuja magari yote yaliyoegeshwa hayakuwa ya kitoto, niagari yenye gharama sana

Walishuka na kupokelewa na kijakazi wa humo na waliongozwa mpaka upanfe wa nyuma wa jumba hilo la kifahari.

Nyuma kulikuwa na uwanja mkubwa sana ukiwa umepambwa na vitu vya thamani pamoja makundi makundi ya meza na vit, palipambwa pakapambika na kupendeza kama ilivyo kwenye kumbi zitumiwazo kufanya hsrusi na sherehe.

Kulikuwa na watu pia wamekwishafika kwa kualikwa.
Upande wa Cid mara baada ya kuona Jimmy na wanafamilia wameshafika eneo hilo alikwenda kuwapokea

"Hatimae mmefika karibuni kwenye siku yangu muhimu sana" aliwakaribisha

Mama Jimmy hakuja mikono tupu alikuwa na bosi la zawadi hivyo alimpatia

"Hongera sana kijana japo umetushtukiza sana lakini sio mbaya, pokea zawadi kutoka kwangu" aliongea Mama Jimmy na kumpatia zawadi

"Asante sana mama, vp na wewe umeniletea zawadi? " Cid alimgeuka monica na sura ya matarajio

"Hata kama mimi ni bahili lakini siku za kuzaliwa ni muhimu sana, kuandaa zawadi ndogo sio shida" aliongea monica akiingiza mkono wake kwenye mkoba na kutoa kiboksi kidogo chembamba umbo la mstatili na ndani yake kulikuwa kuna cheni rangi ya dhahabu yenye nyota, ilikuwa ya bei chee 30k lakini yenye kupendeza macho

Jimmy aliipokea kwa mikono miwili na tabasamu huku akitanguliza na shukrani kisha akamwangalia Jimmy

Jimmy naye alipoona anaangaliwa aliishia.kumpa jicho la "Bro si ulisema hakuna umuhimu wa mimi kuja na zawadi"

Baada ya mapokezi mazuri walikwenda kutafuta sehemu ya kuketi wakimuacha Cid kuendelea kupokea wageni na kuwakaribisha

Kila meza ina vitivinne, walitafuta meza eneo la mwisho ambalo walikwenda kukaa, tangia wafike hapo walikuwa wakiangaliwa sana pengine ni kwasababu hawakutambulika, wengi wao walikuwa ni wafanya biashara, vibosile, watu wenye pesa zao n.k

Muda si mrefu aliongezeka mru ambaye aliteka umakini wa watu wengi, alikuwa ni mwanake mrembo aliyevalia gauni jekundu lenye mpasuko upande mmoja wa paja, skuna nyeusi, pia umbo lake halikuwa la kudharauliwa wahuni wanaita umbo nsamba nane. Licha ya hivyo hakuna aliyethubutu kumsogelea kwa kumhofiamaana hakuna asiyemjua Sophia, mwanamke kauzu na nyodo juu.

Alienda kuketi mahali pa peke yake asijali macho ya watu wanaomwangalia. Upande wa Jimmy aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko, alikuwa akiwasikitikia wanaume marijali kwa kuwa waogaalijiambia mwanamke ni mwanamke tu hata awe katili kiasi gani akiwa kitandani ni mwendo wa miguno na kuomba poo akipelekewa moto kisawasawa

Muda ulisogea mpaka kufika saa moja watu wakiwa tayari wameshajazana kwenye vit, Hatimae birthday ya kijana Cid ilianza
Upande wa walipokaa wakina Jimmy alijitokeza Bianca haiukeleweka amepitia wapi lakini alikuwa kwenye meza yao na alivuta kiti kukaa na kukamilisha idadi ya watu wanne kwenye meza

"Shikamoo! Mama" aliamkia Bianca na mama Jimmy aliitikia salamu kwa bashasha na kumsifia amependeza hali iliyomfanya atabasamu na kuzipokea sifa hizo.

Jimmy naye hakuwa nyuma kumwaga sifa na baada ya maongezi mafupi waliweka umakini mbele

Cid alichukua Mic na kusimama mbele ya watu wote waliohudhuria siku hiyo kisha alisafisha koo na kuanza kuongea

"Good evening, everyone! First of all, I just want to say a huge thank you to each and every one of you for being here tonight. It truly means a lot to celebrate this special day surrounded by family, old friends, and even some new ones.

Turning 25 is a big milestone, and looking back, I realize how lucky I am to have such amazing people in my life. Your love, support, and presence tonight make this day even more special. So, from the bottom of my heart—thank you!

Now, before we officially start the ceremony, I’d like to take a moment to introduce someone very special. We haven’t been friends for that long, but I can say with certainty that he’s one of the most incredible people I’ve ever met.

Two years ago, I was in an accident. There were many people around, but only one person stepped forward to help me—and that was him. At the time, I didn’t even know his name, but his kindness left a lasting impression on me.

Fate, however, had other plans, and recently, we crossed paths again—this time under even more intense circumstances. During a terrifying terrorist attack, he once again stood by my side, proving not just his bravery but his loyalty as a friend. And today, I can say I’m truly grateful to have met him not just him, but also his wonderful family.

So, as a way to kick off tonight’s celebration, I’d like to invite my friend up here to sing a song for us before we begin. Let’s give him a big round of applause. Hey Jimmy come up here" aliongea kwa kingereza kwasababu kulikuwa na wazungu pia akimaanisha

"Habari za jioni, nyote! Kwanza kabisa, nataka kusema asante sana kwa kila mmoja wenu kwa kufika hapa leo. Inanifanya niwe na furaha sana kusherehekea siku hii maalum nikiwa nimezungukwa na familia, marafiki wa muda mrefu, na hata marafiki wapya.

Kutimiza miaka 25 ni hatua kubwa maishani, na ninapotazama nyuma, natambua jinsi nilivyo na bahati kuwa na watu kama ninyi katika maisha yangu. Upendo wenu, msaada wenu, na uwepo wenu hapa leo vinafanya siku hii iwe ya kipekee zaidi. Kwa hivyo, kutoka moyoni mwangu, asanteni sana!

Sasa, kabla hatujaanza rasmi sherehe hii, ningependa kumtambulisha mtu maalum sana. Hatujakuwa marafiki kwa muda mrefu, lakini kwa hakika naweza kusema kwamba yeye ni mmoja wa watu wa kipekee niliowahi kukutana nao.

Miaka miwili iliyopita, nilipata ajali. Kulikuwa na watu wengi karibu, lakini ni mtu mmoja tu aliyesimama na kunisaidia na huyo ni yeye. Wakati huo, sikujua hata jina lake, lakini ukarimu wake ulinigusa sana.

Hata hivyo, hatima ilitaka tupatane tena hivi karibuni lakini safari hii ilikuwa kwenye tukio kubwa zaidi. Wakati wa shambulio la kigaidi, alionyesha tena ujasiri wake na kuwa upande wetu, si tu kama anayetoa msaada bali pia kama rafiki wa kweli. Na leo, naweza kusema bila shaka kwamba namshukuru Mungu kwa kuniletea rafiki kama huyu, pamoja na familia yake nzuri.

Kwa hivyo, kama njia ya kuanza sherehe hii rasmi, ningependa kumwalika rafiki yangu hapa mbele ili atuimbie wimbo kabla ya kuanza sherehe. Tumpigie makofi makubwa! Oya Jimmy njoo hapa" huku akimpungia mkono na watu wote kumgeukia wakitaka kumuona huyo jimmy huku wakipiga makofi
Monica na mamaye pia walikuwa na sura zenye maswali baada ya kusikia neno "tukio la kigaidi" lakini iliwabidi waweke kiporo suala hilo na kupamba nyuso zao kwa tabasamu

Mwanzoni Jimmy hakuwa na habari na speech hiyo lakini baada ya kusikia ameingizwa kwenye speech aliishia kukunja sura tu Alijiuliza ina maana kumsisitiza kote kule apendeze kumbe ndiyo kuja kumtangaza mbele ya watu kibaya zaidi alimtaka kwenda kuimba.



TO BE CONTINUED........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom