Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

Simulizi ya kifantasia: Solo king: ancient legacy

By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 14: Nina ndoto tofauti ya kutimiza, kuimba kutabaki kuwa hobby yangu


Macho yalikuwa ni mengi sana yakiangalia upande wa meza waliyokaa Jimmy na wanafamilia wake.

Jimmy aliupamba uso wake kwa tabasamu na kusimama akielekea mbele alikoitwa akisindikizwa na macho ya wengi kana kwamba ni supa staa kumbe ni mshikaji mmoja tu ambaye bahati humuangukia mara kwa mara

Mbeleni kulikuwa ni kijukwaa kidogo ambacho Cid alisimama, Jimmy alipomkaribia alikumbatiana nae kishkaji kwa bega moja na kabla hajaachia mkono alimnong'oneza

"That’s a wonderful speech, but why me?" (Hio ni hotuba nzuri sana lakini kwanini mimi) alimnong'oneza na Cid aliishia kumtolea tabasamu tu na kumpatia Mic

Alikusanya ujasiri na kusafisha koo yake vizuri kisha kusogeza mic karibu na mdomo tayari kwa kuongea

" Sio mbaya nikiruka salamu na utambulisho maana tayari wote mnajua naitwa Jimmy kama nilivyotambulishwa, Pia ningependa kumshukuru rafiki yangu kwa maneno mazuri aliyosema kunihusu. Ukweli ni kwamba, sikufanya yote hayo kwa kutegemea shukrani au malipo nilifanya kwa sababu ilikuwa jambo sahihi kufanya.

But you know, life works in many mysterious ways, Back then, I had no idea that the person I helped would one day become a close friend, niwe mkweli tu kama rafiki sijaja na zawadi kwenye siku yake maalum kwa sababu ya kukosa maokoto haha" Jimmy aliongea kiswainglish akitoa na kicheko na kufanya baadhi yao kucheka wengine kutoa tabasamu kisha aliendelea

"Kwakuwa ameniomba na kunitaka hivyo sio mbaya nikachukulia kama zawadi yangu kwake naona haitakuwa haki kumkatalia"

Jimmy alirudishia mic Cid, uzuri maandalizi yalishafanyika kitambo kulikuwa na kinanda jukwaani pamoja na guitar na vifaa vingine vya muziki kwaajili ya band zilizoalikwa kutumbuiza

Alikwenda na kuchukua guitar(gitaa) moja rangi ya chungwa brand ya Corodoba C5, ni gitaa iliyoundwa kwa mtindo wa jadi wa Kihispania na lina bracing ya feni, inayosaidia kutoa sauti yenye nguvu na endelevu.

Alivuta stuli ndefu iliyojukwaani na kuketi juu yake akikunja nne kisha kuiweka gitaa vyema tayari kwa kuicheza, alikuwa katika utulivu wa hali ya juu sana

Na mdogo mdogo alianza kuchezesha vidole na sauti nyororo ilisikika vyema masikioni mwa watu huku akiimba wimbo aujuao yeye, alikuwa akicheza mtindo flani wa mziki wa gitaa uitwao "Cavatina"

Cavatina ni mtindo ulioundwa na mwana muziki wa filamu kutoka uingereza aitwaye Stanley myers miaka ya 1960s, ni mtindo wa muziki unaowakilisha hisia na kujieleza, ni mtindo wa taratibu wenye kuukonga moyo wa yeyote asikilizaye, hasa kama msikilizaji ni mpenda nyimbo za taratibu

Sababu ya Jimmy kuamua kucheza huo mtindo ni kwasababu ya wimbo aliokuwa akiimba, ni wimbo uliokuwa ni kama storytelling flani hivi, ni kama alikuwa akihadithia alivyokutana na Cid na hakutegemea kama wangekuja kuwa marafiki siku za mbeleni kwa njia ya kuimba, pia wimbo uliokuwa na shukrani ndani yake. Ukiniuliza ni shukrani gani mimi sijui.

Sauti nayo ilikuwa ni nzuri na yenye kuvutia sana, kwa jinsi alivyokuwa hapo jukwaani ni kama supa staa flani hivi akitumbuiza kwenye birthday ya Cid.

Upande wa Monica na mama yake walikuwa kwenye mshangao, ilikuwa ni mara yao ya kwanza kumshudia jimmy akiimba na kucheza gitaa kwa ustadi sana, upande wa Bianca naye alikuwa akimtazama Jimmy kwa hisia mchanganyiko isieleweke anahisi nini moyoni

Mpaka anakuja kumaliza kuimba watu walimpigia makofi wakionyesha kumkubali na Cid aliyekuwa pembeni yake alimsogelea na kumpongeza huku akimnong'oneza masikioni

"Leo lazima wadada wakugombanie bro yaani kwa staili hii sidhani kama umewaacha salama mioyoni mwao" alinong'ona Cid

Basi baada ya hapo sherehe ilianza kama kawaida, nisiongelee sana yaliyotokea ila kifupi sherehe hiyo ilikwenda vizuri, watu walikula wakashiba na blah blah blah

"Mdogo wangu sikujua kama una kipaji kiasi hiki" aliongea Monica baada ya kumaliza kula

Jimmy hakujisumbua kumjibu badala yake yeye alikuwa akibebe tonge la pilau na kulisindilia mdomoni hakuwa na haja ya kutumia kijiko, mkono wake wa kulia ulimtosha kabisa kushughulika na msosi

"Wewe Jimmy hivi ushibi? Ni sahani ya tano hio kama sikosei?" aliongea mama yake akimshangaa mwanae maana hakuwahi kumuona akila chakula kingi kiasi

"Na mchana alikula sahani tatu huyu" Monica alichomekea

"Hata mimi sielewi mama najikuta tu nina njaa" aliongea huku akiendelea kula chakula huku Bianca akimshangaa asitie neno lolote

Mara katika meza yao aliongezeka mtu mwingine, alikuwa ni Sophia na haikueleweka amekuja kufanya nini hapo.

"Samahanini nahitaji maongezi na huyu kijana" aliongea Sophia akimnyooshea kidole Jimmy

Jimmy sasa ndiyo alikuwa akimalizia tonge la mwisho la pilau na baada ya kumaliza alichukua maji ya chupa yaliyokuwa kwenye meza na kunywa yote mfululizo huku sauti ya maji kupita kooni ilisikika, alipomaliza alinyanyuka na kwenda kunawa kisha kurudi

"Oh mimi? Haina shida kwahiyo tunaongea wapi au ni hapahapa?" aliliza Jimmy na Sophia aliongoza njia

"Nitarudi" Jimmy aliwaambia wenzake na kumfuata Sophia nyuma

"Vijana wa siku hizi hawanaga muda wa kusalimia wakubwa zao" aliongea Mamaye kwa kutingisha kimasikitiko baada ya Jimmy na Sophia kuondoka, Monica na Bianca waliungana naye kusikitika

Watu walikuwa wakimuangalia Jimmy ambaye alikuwa akimfuata Sophia kwa nyuma, nadhani walikuwa wakijiuliza imekuwaje mpaka kijana huyu akiongozana mrembo Sophia ilihali wao hata ujasiri wa kumsogelea hawakuwa nao

Walienda mpaka ndani ya nyumba na kwenda sebuleni

"Unaonaje tukasahau yaliyopita.... Jimmy" Sophia aliongea baada ya kuketi kwenye sofa na kumpa Jimmy ishara aketi

"Usiwaze sana mimi huwa siwekagi vinyongo kwenye vitu vidogo" Jimmy aliongea baada ya kukaa

"Oh sawa... Sijui kama unanifahamu ila sio vibaya kujitambulisha, Naitwa Sophia Merizesta na ndiye dada mkubwa na mzaliwa wa kwanza kwenye hii familia" aliongea akijitambulisha

"Unajua lengo la mimi kukuleta mpaka hapa?" Sophia aloiliza

"Umesema unahitaji maongezi na mimi" aliongea Jimmy akijiambia huyu bibie ni kama baba yake tu kuzunguka zunguka tu badala ya kwenda kwenye point

"Yes nataka tuongee biashara, lakini kabla ya kuanza ningependa kutoa shukrani zangu kwa uliyoyafanya, sikudhani mtu yule tuliyekutana bar na kutofautiana angekuwa ndiye mwokozi wa ndugu zangu, I owe you one" aliongea Sophia

Japokuwa Sophia alikuwa ni mwanamke mwenye kujisikia sana lakini likija suala la familia yake alikuwa ni tofauti na yule mwenye nyodo, alikuwa akiwajali ndugu zake ni sawa na kusema kwa nje anaonekana mgumu sana ila ndani ni mwepesi hivyo aliguswa na wema wa Jimmy

"Nilishasema sikufanya yote nikitegemea shukrani au malipo yoyote hivyo suala la wewe kuwa na deni sahau isitoshe mtu yeyote angefanya vile"

"Kama nilivyosikia kuwa wewe ni mgumu sana kama kwa mama yangu ulikataa shukrani sidhani kama kwangu utakubali pia, anyway tuzungumze biashara"

"Nakusikiliza" Jimmy aliuliza

"It's an offer, just then I saw you perform on stage out there and I have to say you truly are a talent, A raw natural talent that my industry is always looking for. And I happen to be in a position to offer you an opportunity that most people would dream of.ā€ aliwasilisha Ofa yake kwa kingereza safi cha kwa mfalme Charles III akimaanisha "Ni ofa, mara tu nilikuona ukitumbuiza kwenye jukwaa huko nje na lazima niseme ukweli wewe ni talanta, Kipaji cha asili ambacho tasnia yangu inatafuta kila wakati. Na nimetokea kuwa katika nafasi ya kukupa fursa ambayo watu wengi wangeitamani.ā€

"I hear you" Jimmy aliitikia akimaanisha anamsikia

"I run Sonic Bloom Records We’re one of the biggest labels in the country, responsible for shaping some of the top artists in the industry. We provide the best producers, world-class management, and a platform that guarantees success." (Ninaendesha Sonic Bloom Records Sisi ni mojawapo ya lebo kubwa zaidi nchini, inayohusika na kuunda baadhi ya wasanii wa juu katika tasnia. Tunatoa watayarishaji bora zaidi, usimamizi wa kiwango cha kimataifa na jukwaa linalohakikisha mafanikio) aliisifia label yake na kuendelea

" I see potential in you. If you sign with us, we’ll take your music to heights you never imagined. Your name, your voice it could be everywhere" akimaanisha Naona uwezo ndani yako. Ukijiunga nasi, tutaupeleka muziki wako katika kiwango ambacho hukuwahi kufikiria. Jina lako, sauti yako vitasikika kila mahali.

"ā€œI appreciate the offer, But I’m not interested.ā€ alikataa kistaarabu

" Usiwe na haraka jipe muda wa kufikiria hii fursa adimu sana kwa vijana kwenye tasnia ya muziki" Sophia alijaribu kumshawishi tena

"Naelewa lakini nimeshafanya uamuzi sio kwamba sipendi hapana nina ndoto tofauti ya kutimiza, kuimba kutabaki kuwa hobby yangu" Jimmy aliongea

Sophia alitabasam na kuongea "Endapo utabadili mawazo mlango wetu upo waz" kisha alinyanyuka na kumpa mkono ishara ya "handshake" naye alinyanyuka na kuupokea

"Wewe kijana yaani unikatalie kote kule lakini leo unalegeza kwa mwingine au kwasababu mimi ni mzee" ilisikika sauti ya mwanamke na kweli alikuwa ni mwanamke ambaye kwa kumuangalia alikuwa kwenye miaka ya mid 60s

Alikuwa katika tabasamu pembeni yake kulikuwa pia na mwanamke mwenzake ambaye bila shaka alikuwa ni mwanamama Velora

"Haha kumbe upo huku?" Jimmy aliuliza huku akijichekesha

"Nilikuona mda sana tu ila si unajua mambo ya koneksheni kijana" aliongea mwanamke yule

"Oh Kumbe ila sio mbaya vipi hali yake bibi?" Jimmy alimjulia hali

"Sio mzima mimi umenikatalia ofa yangu halafu unamkubalia mshindani wangu" aliongea mwanamama yule

"Hamna msimamo wangu ni ule ule tu kupeana mikono kusipe presha sana bibi utazeeka vibaya mno"

"Ma Jack unamjua huyu?" Mwanamama velora aliuliza

"Ndio huyu mtoto ana vipaji vingi sana hata familia yake haijui nishambembeleza sana lakini wapi" aliongea Ma Jack akisikitika na kuwaeleza alivyomjua

Ma Eliasi ni mama yake Sara na ambapo Sara ni mtoto wa pili kwake, Sara ni rafiki yake na Monica na kupitia Sara aliweza kumfahamu Jimmy

Alikuwa ni mfanya biashara wa Real Estate na Music industry nchini Tanzania na biashara yake ya muziki mshindani wake mkuu ni Sophia na ofa aliyokuwa akijaribu kumshawishi Jimmy akubali ni kuwa Producer wa label yake huku akimuahidi mshahara mnono lakini bila mategemeo alikataliwa kwa kisingizio kilekile alichomwambia Sophia

Hata Jimmy kule hotelini alipocheza piano mualiko alioupata ulikuwa ni kutoka kwa Ma Jack ambaye jina lake halisi ni Mrs Rose bayeye na jina lake maarufu kwa kumiliki label ya muziki nchini lilifahamika kama Bibi machina hivyo haikushangaza kwa Jimmy kumuita Bibi, hata hivyo alikuwa ni Bibi kweli, ni kule kufosi tu kuonekana kama kijana kwa kupaka mavipodozi

"Sikutegemea ile siku ungetoroka bila kuaga" alilalama Bibi machina alikuwa akimaanisha ile siku hotelini ambapo aliondoka alipokutana na Cid lakini Jimmy aliishia kujichekesha tu na kumwambia kwamba alijisahau kutokana na njaa

Wakati wakiendelea kuzungumza kirafiki Cid, Bianca, Monica na Mamaye waliongezeka. Muda ulikuwa umeenda sana na ilikuwa ni saa sita wengi wa waliokuja kusheherekea walikuwa washaondoka

"Bro nilikuwa nakutafuta kumbe umejificha huku na wazee" Cid alitania na aliishia kukatwa jicho na Bi machina pamoja na mama yake

Mara walionekana walinzi watatu wakiingia taratibu wasije wakaiangusha piano kubwa ya mbao ambayo walikuwa wameibeba, walienda kuiweka sehemu ambayo walielekezwa na ilikuwa humohumo sebuleni

"Leo mnashinda hapa kwakuwa muda umeenda, kuna vyumba vingi vya wageni na nishaongea na wenzako na wamekubaliana nami" aliongea Cid akimuangalia Jimmy

"Lakini kabla ya kwenda kulala lazima utupigie songi moja matata sana ili tulale vizuri au sio ndugu zangu" aliongea Cid akiwageukia wakina Monica na Bianca nao walitingisha kichwa kukubaliana nae

Monica alitaka kushuhudia umahiri wa mdogo wake kwenye kucheza piano maana alishachoka na ngojera za Cid za kumsifia na ndio alitaka kuona kwa macho yake na sio kuishia kusikia tu

Alijiambia hata kama Jimmy aliweza kucheza gitaa haimaanishi na piano ataweza, kifupi Monica alikuwa ni kama mafarisayo tu yaani mgumu kukubali licha ya kushuhudia kipaji mojawapo cha ndugu yake. Kati ya gitaa na piano, gitaa ni ngumu sana hasa kwa wanaoanza kujifunza tofauti na wacheza piano, sasa kama kitu kigumu amekiweza kwanini kirahisi isiwezekane? Ni vile tu aliamua kuwa mgumu kukubali

"Bro ina maana zawadi yangu haikutosha?" aliongea Jimmy huku akikunja sura aliona huyu rafiki yake ni msumbufu sana

"Kwanini usituburudishe kidogo Jimmy nataka kujionea kipaji chako kwenye kucheza piano" aliongea mwanamama Velora na wote walitingisha kichwa kukubaliana naye isipokuwa Sophia tu na walinzi

Jimmy aliishia kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha, alianza kujilaumu kwanini hakuondoka mapema, kingine alikuwa ameshiba sana hivyo alihitaji kupumzika

Alikubali kishingo upande na kwenda kukaa kwenye piano, na wengine wote walikwenda kukaa kwenye sofa wakitega masikio yao

Ile Jimmy anataka kuanza tu zilisikika sauti za vishindo vizito vilivyomshtua kila mtu

"BAM! BAM! BOOM!



TO BE CONTINUED.............
 
By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 15: Imani


Vilikuwa ni vishindo vizito kutokea nje ya nyumba hiyo, hata Jimmy naye alishtuka na kujiuliza kuna nini huko? Wale walinzi watatu walianza kutoka nje kwa tahadhari wakiwa tayari wameshachomoa siraha zao tayari nyuma wakifuatiwa na Jimmy na wengine wote

Walipofika nje waliweza kushuhudia tukio la kutisha sana na la kikatili, walinzi watatu waliokuwa wakilinda nje wawili walikuwa wamepigizwa kwenye kiasi cha chuma kubonyea na mmoja alipizwa kwenye ukuta kiasi cha kusababisha nyufa kadhaa

Kibaya zaidi kulikuwa na viumbe vitatu vya ajabu vikiwanyonya damu kiasi cha ngozi zao kukauka mpaka wanapoteza uhai, Jimmy alipata msisimko wa ajabu sana ambao hakuwahi kuhisi hapo kabla

Ni kama hisia zake zilikuwa zikimwambia kwamba hao viumbe ni hatari sana

Walikuwa ni viumbe wenye umbo kama binadamu wa kawaida lakini hawakuwa binadamu, macho yao yalikuwa ni meupe yaliyokosa mboni nyeusi, sura zilikuwa za kutisha zilizochafukwa na damu, mikono yao ilikuwa na kucha ndefu kama jini kabula na haikueleweka wametokea wapi na imekuwaje wakafika hapo, lakini jambo la uhakika uwepo wao ulitibua amani

Upande wa mama yake Jimmy, Bianca na Bibi machina walikwisha zimia kitambo kwa mshituko walioupata walipowaona, wengine walikuwa na woga usio na kifani, Cid mwili mzima ulikuwa ukitetemeka kama vibrator ni bahati tu hakujikojolea, hakuwai kufikiria Ipo siku atakuja kushuhudia tukio kama hilo maishani mwake,, Monica aliyemdaka mama yake alikuwa akitetemeka pia kwa woga huku machozi yakimtoka kama mfereji wa maji, Sophia aliyemdaka Bibi machina na Mwanamama Velora nao pia walitawaliwa na hofu

Ni Jimmy na walinzi pekee walijikaza lakini mioyo yao haikuacha kudunda kwa kasi, ni wazi wao pia walikuwa na woga lakini kama wanaume waliamua kujipa ujasiri lakini ujasiri wao haukutosha

"Firee!! Motooo!! Unguaa!" Nyie mashetani ungueni kwa moto wa mbinguni!! Fire!! Imeandikwa........ ""Cid alianza kuwakemea na kusoma vifungu vya biblia akitegemea kupata matokeo lakini hakuna kilichotokea zaidi ya kuonekana anapiga makelele usiku

"Mnazubaa.. nini nyie wapuuzi fyatunieni risasi mnataka tufe?" Cid alifoka kwa sauti yenye mtetemeko, alikasirika mashetani kuvamia kwenye siku yake maalumu, alitaka kuwatukana lakini aliona ni kheri kukaa kimya

Walinzi bastola waliziona nzito sana, mikono yao ilikuwa ikitetemeka hata ule ujasiri wa kufyatua hawakuwa nao

Wale viumbe taratibu walianza kuwasogelea, kila hatua waliyokuwa wakipiga ndiyo ule msisimko aliokuwa akihisi Jimmy ulikuwa ukiongezeka, alipatwa na hisia za woga na hisia zingine za ajabu zisizoeleweka

Alikumbuka mara kadhaa alikuwa akiangalia taarifa ya habari na kusikia kwamba kuna vifo visivyoeleweka hutokea usiku na miili kuonekana kukauka kana kwamba wamekamuliwa damu na palepale akili yake ilifanya kazi
I
"Ingieni ndani kubaki hapa sio salama" kwenu" aliongea Jimmy akiwaamuru wote waingie ndani

"Unataka kufanya ni. ... " Monica kabla hata hajamaliza sentensi yake alizimia na ni wazi Jimmy alifanya hivyo akiwa na kusudi lake.

"Nyie walinzi wapelekeni hawa ndani na asitoke mtu" aliongea Jimmy akimaanisha ndugu zake na wengine na walitaka kuongea lakini walipewa ishara na Cid kwamba wasikilize wanachoambiwa na walitii na kufanya kama walivyoambiwa na alibaki yeye pamoja na Cid

"Na wewe Ingia ndani" aliongea Jimmy akimwambia Cid

"Lakini kama unataka kufa baki na mimi" Cid alihisi ubaridi kwenye uti wa mgongo kwa kauli hiyo

Wale viumbe walikuwa umbali wa kama mita mbili hivi na waliposimama na kufumba na kufumbua uso kwa uso na wakina Jimmy, ilikuwa ni spidi ya ajabu sana

Jimmy kwa spidi alimtandika teke Cid lililomrusha mbali na waliposimama, ilikuwa ni kumuokoa asije kudhurukia na Jimmy hakujali atamfikiriaje alijiambia wakisalimika hapo atamuomba radhi

Hakujali tena kuhusu uimara wa akili sijui roho alijiambia liwalo na liwe nakwenda kutumia huo uchawi, potelea mbali kanuni ya uimara yupo kwenye mlango kifo, aliona ni bora kuumia kuliko kufa kabisa

Jimmy baada ya kujaribu kufanya lile jaribio na kushindikana, alipumzika kidogo na kuendelea kusoma kile kitabu kuhusu mbinu mbali mbali za uchawi wa kunena

Sorcerers huzaliwa na willpower thabiti lakini si wote ni baadhi yao, alikuwa akijua willpower yake ni dhaifu mno alikuwa kwenye levo ya kwanza ya willpower, Fragile mind(akili dhaifu) na njia ya kuwa thabiti ni kuongeza kiwango cha willpower kupitia majaribio na mateso
Mchawi bila willpower ni sawa na upanga usio na makali

Kupitia mapambano makali, wachawi huongeza kiwango chao cha willpower na kuwa na uwezo wa kushinda vizuizi vikubwa zaidi na na kadri willpower inavyokuwa kubwa na thabiti ndivyo hupanda level na hilo Jimmy alikuwa amelisoma kupitia kitabu
Ni kupitia mapambano makali na mateso na willpower kuongezeka ndiyo hupanda level za uchawi wa mabadiliko(mutation magic) kutoka ya chini kwenda ya juu, ni sawa kusema viwango vya willpower vinahusiana na kupanda level kwa mchawi mkuu(Sorcerer)

Jimmy yeye hata level ya kwanza tu ya uchawi hajafika, ifahamike licha ya kurithishwa nguvu hizo za ajabu haimaanishi amekuwa na nguvu kama mrithi wake, hapana. Alichoingiziwa ni nguvu tu iliyolala na jinsi ya kuziamsha ni kupitia juhudi zake mwenyewe kufuata muongozo na kanuni na kujifunza maarifa yaliyoko kitabuni

Baada ya Jimmy kumpiga teke Cid na kumrusha mbali na alipo hakusubiri hata sekunde moja alitamka maneno "Descend, burden of the heavens. Heavy Storm!" alinena kwa kingereza akimaanisha "Shuka, mzigo wa mbingu, Dhoruba nzito!"
Uchawi wa kunena haijalishi unatumia lugha gani ilimradi lugha utumiazo zina maana moja na uliyokusudia na zimetamkwa kwa usahihi. Uchawi unafanya kazi.

Palepale upepo mkali kama dhoruba ulitokea katikati yao Jimmy na wale viumbe ilitokea pressure kubwa kama ile isababishwayo na mlipuko wa bomu na kuwarusha wote hao jimmy akienda kaskazini na kujipigiza kwenye ukuta na wale viumbe walirushwa kusini na kwenda kujipigiza kwenye magari na ilisikika milio ya BOOM! BAM! BAM! "

Upande wa Cid alipigwa na bumbuwazi asiamini macho yake kwa kile alichokishuhudia

Upande wa Jimmy alipojipigiza kwenye ukuta alitoa mguno wa maumivu na kutema damu mdomoni, ni kwasababu alikuwa dhaifu sana kutumia nguvu hizo ndiyo maana na yeye alipata madhara pia. Kilichofanya nguvu kufanya kazi ni ile imani thabiti aliyokuwa nayo ya kwamba anaweza na kuwa tayari kwa lolote

Imani ni moja ya misingi ya mchawi ukiachana na willpower, yaani ile kujiamini ndani ya nafsi yako kwamba inawezekana bila kuwa na shaka yoyote na ndipo matokeo hutokea kwenye uchawi wa kunena, ukinena bila imani ni sawa tu na kufyatua bastola ambayo hakuna risasi ndani yake na hilo Jimmy alilijua na ndiyo aliyotumia ili kuleta matokeo

Hata hivyo nguvu haikuwa kubwa kiasi kile kutokana na kutokuwa imara kwake, licha ya kuonekana kwa macho ya kawaida ni nguvu kubwa ila kichawi shambulio lile lilikuwa bado dhaifu

Wale viumbe licha ya kurushwa na kujipigiza kwenye magari hawakuonekana kupatwa na madhara, zaidi walinguruma kwa hasira sana, ilionekana kwao ni dharau kuweza kushambuliwa shambulio lile tena kwa binadamu dhaifu kama huyu

Kufumba na kufumbua wote walikuwa mbele ya Jimmy, upande wa alipokuwa Cid hakuonekana, ilionekana alikwenda kujificha hakutaka kubaki tu akishuhudia rafiki akifa halafu mwisho wa siku naye auawe, Japokuwa alitamani sana kusaidia lakini huo uwezo hakuwa nao, kitu pekee alichoona ni kujificha tu kuokoa uhai wake

Mmoja wa wale viumbe wa ajabu alishika shingo Jimmy na kumnyanyua kiasi cha kuning'inia, Jimmy hakuwa na nguvu mwilini, baada ya shambulio lile alikuwa dhaifu mno ni kama nguvu zake zote aliwekeza kwenye lile shambulio.

Kitu pekee alichobaki ni kufurukuta tu lakini juhudi zake hazikuzaa matunda na yule kiumbe aliyemkaba alipanua mdomo wake wenye kutoa harufu mbaya iliyoambatana na harufu ya damu. Alikuwa na meno yaliyochongoka kama ncha kali. Kutokana na kiu yake ya damu alisogeza mdomo wake akitaka kumng'ata shingo. Na kumnyonya damu na wale wengine mmoja alishika mkono wa Jimmy wa kulia mwingine wa kushoto wakidhamiria kumnyonya damu kupitia kiwiko cha mkono

Lakini kabla hawajatimiza kusudi lao ilitokea nguvu ya ajabu iliyowarusha mbali wale viumbe na Jimmy kudondoka chini akikohoa na kuvuta hewa kwa tabu. Aliangalia upande wa wale viumbe na kukuta wamechomwa na mkuki wote kwa pamoja kama vile mshikaki na mkuki mkubwa wenye urefu wa mita saba na sasa Jimmy ndiyo alielewa kumbe ilikuwa ni nguvu ya mkuki na hakuacha kushangaa na kujiuliza ni nguvu kiasi gani iliyotumika?

Ulikuwa ni mkuki ujulikanao kama "sarissa" ni moja ya mikuki mirefu sana katika historia, uliotambulishwa na mfalme Philip II wa Macedonia na kutumiwa na "Phalanxes" wake wa kimasedonia
Phalanxes in wanajeshi wa zamani katika mstari wa mstatili wenye ngao na mkuki kwa ajili ya ulinzi na kufanya adui iwe ngumu kupenya

Jimmy aliona kuendelea kuzubaa na kushangaa haitaleta maana yoyote na aligeuza tena shingo lake kuangalia upande mkuki ulipotokea na hapo sasa aliweza kuona kuona kundi la watu

Lilikuwa ni kundi la watu nane wakivalia mavazi staili tofauti lakini zenye rangi moja , rangi nyeusi na hawakuwa wengine bali ni lile kundi lijiitalo HIDDEN SUPREMACY

Kati ya watu nane wa katikati alionekana mwanamke akinyoosha mikono kwa staili ya kurusha mkuki na ilionekana ndiyo aliyefanya shambulizi lile

Alikuwa ni yule mzungu mwenye nywele rangi ya fedha, alifahamika kwa jina la Freya

"Kuna nguvu ya ajabu nimehisi ikitokea mahali hapa au hisia zangu zinanidanganya?" aliongea Ben alifunga kitambaa kwenye paji la uso, alionekana ndiye bishoo kuzidi wote na hakuna aliyejisumbua kumjibu

"Boy you're lucky we're not that late otherwise....." aliongea Freya alipomkaribia Jimmy akimaanisha kwamba anabahati hawajachelewa sana vinginevyo... (akiacha sentensi yake ielee hewani, nadhani alimaanisha marehemu)

"Thanks for your help and compliment little girls" aliongea Jimmy akitabasamu akimaanisha asante kwa msaada na pongezi msichana mdogo.
Ni wazi hakupenda kuitwa "boy" hivyo alirudisha shambuliza kistaarabu

"Haha! Nimempenda bure huyu jamaa" aliongea Ben ikionyesha wazi alikuwa akimkejeli Freya kwa njia isiyo ya moja kwa moja

"Oh my dear mother Theresa!" aliongea Ben akimwambia Freya huku akinyoosha mikono upande wa wale viumbe walipo na alikuta wamejichomoa kwenye ule mkuki

"Hawa punda ni wabishi sana kufa" aliongea mwingine mwenye mwili uliotuna kama baunsa aliitwa Mzube.

"Blazing fist!" Ben aliongea kwa nguvu na palepale mikono yake aliyoikunja ngumi ilianza kuwaka moto wa njano na alifyatuka kwa spidi kama risasi na kwenda kumtandika ngumi ya kichwa mmoja wa wale viumbe na kumpasua kichwa kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana

Spidi yake ya ajabu na mikono yake kuwaka moto bila kuonyesha ishara ya kuungua ilimshangaza sana Jimmy na kujiuliza hawa watu ni wakina nani

Ben alifanikiwa kumuua mmoja wa wale viumbe na kubaki wawili na kuanza kupambana na wale wengine lakini ilimuwia vigumu kupambana nao, sababu ya yeye kuweza kumuua mmoja wao ni kwasababu lilikuwa ni shambulizi la kushtukiza hivyo walijiandaa baada ya mwenzao kufa, walinguruma kama simba na mpambano kuchukua ukurasa mpya

Ulikuwa ni mpambano kati ya binadamu na viumbe wawili vya kutisha wajulinao kama wanywa damu

"Nyie washenzi ebu acheni kunishangaa njoeni mnisaidie" Ben alimaka baada ya kuona wenzake wanazubaa tu bila kufanya chochote maana aliona anakwenda kuzidiwa

"Unapaswa kujua msaada sio haki ya binadamu, usiposaidiwa usichukie ukiona unakwenda kufa na hakuna anayekwenda kukusaidia unachopaswa ni kusali sala ya mwisho kwa Mungu umuaminiye pengine utatokea muujiza na kuokoka kwenye kifo" aliongea Freya

"Nyie watu sijui bifu lenu litaisha lini" aliongea Caren muhabeshi na aliamua kuchukua hatua kwenda kusaidia

Kama chui alichomoka pale alipo kuelekea mahali pambano linatokea kwa mtindo wa Zig zag na kabla hajakaribia lilionekana panga refu mkononi haikuueleweka imekuaje akaonekana na panga mkononi ilihali mwanzo hakuwa na siraha yoyote

Panga lile lilimlenga shetani mmoja mmoja upande wa moyo lakini kabla kusudi lake halijatimia alionekana kushtukiwa na yule kiumbe na alilikwepa

"Shit!" alilaani baada ya shambulizi lake kushtukiwa

Wale viumbe walionekana ni wagumu sana kufa na utashi wao wa kuelewa mambo licha ya kutoongea ni kama mazombi vile yenye akili nyingi.

Kiumbe mmoja alionekana kupiga kelele ya ajabu yenye kuumiza masikio na wale wengine waliobaki waliishia kukunja ndita tu kana kwamba wamemezeshwa dawa chungu

"Pumbavu! Huyu punda anaita wenzie!" Mzube alifoka kwa hasira

"Hehehe ndio raha sasa angalau tuchangamshe mwili, nilikuwa nimeboreka sana" mmoja wao aliongea kwa mchecheto, alikuwa ni mwanaume mrefu hivi mwenye upara aliitwa Joshua

Jimmy aliishia kukunja ndita tu baada ya kusikia kauli hiyo, alijiambia kama hao wanaoitwa "punda" wakiongezeka, itakuwaje kwa familia yake iliyoko ndani na hawajui hata nini kinaendelea huku nje, aliona kabisa usalama ni mdogo



TO BE CONTINUED............
 
By Samuel jk_Euphoria

SOLO KING: ANCIENT LEGACY

CHAPTER 16: Damu inayobadilika


Bila ya kueleweka wametokea wapi, mashetani vichaa waliongezeka kutoka pande tofauti idadi yao ikiwa si chini ya ishirini, wakiwazingira kundi la HIdden Supremacy na Jimmy.


Walikuwa wakitoa harufu mbaya kama ya uozo iliyoambatana na damu,Jimmy alitamani kutapika kwa kichefuchefu alichojisikia,alijiambia mizoga ina afadhali,ilikuwa ni harufu kali kana kwamba hawakuoga zaidi ya miaka mia moja


"Kijana Ifanya juu chini uondoke hapa,mahali hapa si salama" aliongea Joshua lakini ni kama kauli yake haikuwa na maana kwa Jimmy. Ataondokaje ilihali wamezingirwa na viumbe vyenye sura ya kutisha,mbaya zaidi sura zao zilivyowaangalia ni kama wamefurahi kupata vitowea baada ya njaa ya muda mrefu,wataachaje sasa kitoweo kimoja kitoroka ilihali idadi yenyewe haikuwatosha


Jimmy aliangalia huku na huko na alipatwa na ahueni baada ya kuona Cid hayupo mahali hapo vinginevyo angekuwa na kazi nyingine ya kuhakikisha bwana huyo anakuwa salama.


Upande wa Ben na Caren waliweza kufanikisha kazi yao ya kuwaua wale mashetani wasiojulikana ni viumbe wa aina gani zaidi ya kuwaita wanywa damu kutokana na ukatili wao wa kunywa damu za wanadamu wa kawaida wasio na hatia


"Let the show begin!"Joshua aliongea kwa mchecheto kwelikweli na palepale nguo zake zilichanika na mwili kutun na ndani ya ngozi yake damu yake ilionekana kuchenka kiasi cha kutoa kama mabujabuja mwili mzima na ghafla alibadilika kutoka kuwa binadamu na kuwa mnyama,Simba mwenye manyoya meusi mwili mzima,alikuwa ni simba dume afananae na Jaguar


Jimmy hakuwa mjinga aliishia kukodoa macho na kutamka maneno 'ninyi ni wachawi!"


Alikuwa amesoma kuhusu level za uchawi wa mabadiliko,kila kitu na kuhifadhi ubongoni,Joshua alikuwa ni mchawi katika levo ya pili ya uchawi wa mabadiliko,levo ya shifting blood


Katika level hiyo ya pili mchawi huweza kujibadili umbo lake na kuwa kiumbe kingine, lakini suala la koumbe.wa aina gani hutegemea na nguvu alizonazo muhusika(mchawi) katika level hiyo


Damu Inayobadilika ni ngazi ya uchawi wa mabadiliko inayomruhusu mchawi kubadilisha muundo wa mwili wake, mifupa, misuli, na hata mifumo ya ndani kwa kudhibiti damu yake katika kiwango cha seli. Huu ni uwezo wa nadra na hatari sana kwa sababu unasukuma mwili kupita mipaka ya kawaida, ukimfanya mchawi awe mwenye mabadiliko makubwa


Mtumiaji anaweza kubadilisha mwili wake kwa madhumuni tofauti iwe kwa mashambulizi, ulinzi, au kuishi katika mazingira magumu.


lakini pia kuna ukomo wa matumizi na ni ndani ya dakika kumi,akizidi hapo hutawaliwa akili yake na kushindwa kuidhibiti na nafsi yake kutekwa ambapo mwisho wa siku anakuwa kama mwehu na kufanya matendo yasiyo ya kibinadamu, na muhusika akishindwa kuidhibiti akili yake na nafsi katika hali ya kutawaliwa hubadilika na kuwa kiumbe cha ajabu na si binadamu tena na hayo ndiyo madhara ya Damu inayobadilika. Na hata kama akifanikiwa kutumia uchawi huo ndani ya hizo dakika kumi bado mchawi huyo atakumbwa na madhara ya, uchovu, upungufu wa damu na kupoteza nishati nyingi.na kama sio kuhisi kizunguzungu huzimia kabisa


Jimmy licha ya kusoma yote kuhusu hayo alichukulia kama hadithi tu iliyoandikwa kumhamasisha mhusika ajifunze na hakutaka kuamini masuala ya binadamu kubadilika lakini baada ya kushuhudia usiku huo aliishia kumeza mate mengi na kujiambia kweli dunia ina mambo mengi sana ya ajabu na alikuwa akiyashuhudia baadhi yake live bila chenga, kufikiria vile swali jingine lilimjia kichwani mwake na kujiuliza ina maana na hao viumbe pia ni wachawi waliobadilika na kupateza ubinadamu wao kutokana na madhara ya Damu inayobadilika? Lakini hakupata jibu


Mzube naye alibadilika na kuwa fisi mkubwa mweusi, hakuwa peke yake na wengine pia walibadilika na kuwa wanyama wa ajabu wenye manyoya meusi tii. Isipokuwa kwa Ben, Caren na Freya ambao wao hutumia siraha, lakini hali ile ilimuogopesha sana Jimmy


"Kijana unaweza kupambana? " Caren alimuuliza Jimmy na Jimmy alitingisha kichwa kukubali


"Shika hiyo" alimrushia upanga wake na Jimmy aliudaka


"Tafuta upenyo uondoke hapa nitakusaidia" Caren alimwambia baada ya kumrushia upanga wake


Walianza kushambuliana kundi la wanyama weusi na viumbe vya ajabu na kama Caren alivyosema aliwezesha kwa Jimmy kutoka katika duara lile walilozungukwa


Lakini Jimmy hakuondoka, hakutaka kuondoka akiiacha familia yake nyuma na rafiki zake wapya sehemu hatari kama hiyo


Alienda kusimama mlangoni mwa Jumba hilo la kifaharivakishuhudia mtanange wa ajabu, wakipelekana huku na huko na sauti za vishindo zikitawala masikio yake. Palepale alipata wazo la kuwatorosha wenzake walioko ndani kuondoka sehemu yenye hatari bila kushtukiwa na swali liljia je atawatoroshaje?


Alifikiria namna ya kuwatorosha bila kushrukiwa lakini hakuna njia aliyoipata na alikasirika kuona hana msaada wowote.


Mara alihisi anaangaliwa na kweli alikuwa sahihi na kulikuwa na lishetani limoja lililochoropoka kwenye uwanja wa vita likiwa limechoka na kujeruhiwa sehemu kadhaa za mwili wake na alikuwa akimsogelea lakini safari hii spidi ilipungua tofauti na mwanzo na hiyoo ni kwasababu ya majeraha na uchovu


Jimmy kuona vile ule uchovu wake ulimpotea na hari ya kupambana ilimvaa, hakutaka kuona likimjeruhi na kuingia ndani na kuwajeruhi wengine pia hakutaka kuona miaka yake kumi ya kujifua kimazoezi na mbinu mbalimbali ilikuwa ni ya bure. na alikaa mkao wa kupambana akinyoosha upanga upanga kumuelekea shetani hilo


Alitabasamu na shetani lilimjia kwa spidi na alitegemea hilo na kabla hajamsogelea Jimmy aliruka sarakasi kumkwepa na kwenda kutua upande mwingine


Shetani lilinguruma kwa hasira baada ya kuona limeshinfwa kumkaribia na ile anageuka upande alioko Jimmy uso kwa uso na upanga uliokuwa kwenye kasi


"Shwaaa!!" ulikuwa ni mlio wa kuchanwa kwa ngozi na alikuwa ameuchanja uso wa shetani yule na damu kuruka hewani


Lishetani lilinguruma mlio uliochamganyika na maumivu na hasira kwa wakati mmoja kwa fujo kama zote alianza kurusha mashambulizi bila mpangilio maalumu


Jimmy alikuwa akijitahidi kumkwepa na kwa wakati mmoja asimfikie huku akirudisha mashambulizi
Walikuwa wameachana umbali mdogo tu wa mita mbili, na Jimmy alikuwa akitumia mbinu aliyofunzwa na Master wake Mzee Momochi


Iliitwa "two meter distance combat" yaani alikuwa akipambana na adui wakiwa mita mbili nna hakuna kupunguza urefu wala kuongeza, alikuwa akizingatia sana miondoko ya adui, akipiga hatua moja kumsogelea naye hupiga hatua moja nyuma ili urefu wa mita mbili ubaki palepale


Walikuwa wakipigana kwa kwenda mbele na kurudi nyuma lakini mita zilikuwa ni zilezile hakuna kupungua wala kuongezeka, na ndani ya dakika saba aliweza kumchana chana sehemu ntingi za mwili wa shetani huyo kiasi kwamba hakuweza hata kuendelea kushambulia na kuishiwa nguvu kwani damu nyingi zilikuwa zikivuja na aliishia kusimama kwa kulegea


"Kufa wewe shetani!" Jimmy alipiga ukelelr akisindikiza na shambulio la upanga kwa nguvu zake zote


Sauti ya utenganisho wa kichwa cha shetani yule na mwili wake ulisikikika na damu kurukaruka hewani.


Jimmy alihema kwa nguvu kwani alichoka na alikuwa amechafukwa na damu kwenye nguo zake mpya na mikononi.


Upande wa Freya aliweza kushuhudia kila kitu kuanzia mwanzo wa mpambano kati ya Jimmy na shetani lile, mwanzoni alitaka kwenda kusaidia lakini alisitisha alipoona Jimmy anaweza kudili na alikuwa akiangalia pambano. Hakuwa peke yake mwenyye kushuhudia


Iliwachukua dakika nne kundi la Hidden Supremacy kuweza kumalizana na wale mashetani na walibaki kutazama pambano la dakika saba kati ya Jimmy na shetani lile ambalo muda huo halikuwa na uhai


Kati ya hao nane ni watatu tu wasio uchi, wengine wote walikuwa uchi baada ya kurudi katika maumbo yao na hawakujali sana ilionekana ni kama walishaizoea hio hali


Cid ambaye alikuwa amejificha ndani ya gari aliweza kutoka huku jasho likimtiririka licha ya usiku huo kuwa na baridi, alikuwa akitetemeka, ni dhahiri kwamba aliweza kushuhudia kila kitu kilichotokea, alitembea kwa tabu mpaka kumkaribia Jimmy, kila hatuaaliyopiga mguu ulitetemeka


"Bro hawa ni wakina nani?" Cid aliuliza kwa kunong'ona alipomkaribia Jimmy akiwanyooshea mkono kundi lile


"We unadhani ni wakina nani kama sio wachawi?" Jimmy aliongea


"Kwahiyo tunafanyaje?" aliuliza na Jimmy alifikiria


"Kijana kwanza kabisa sisi sio wachawi, kuhusu sisi ni wakina nani hilo sitokujibu hatujaja hapa kujieleza" aliongea Mzube


Jimmy aliishia kuweka sura ya kimaswali yaani wameongea kwa sauti ya chini lakini ameweza kusikiwa licha ya umbali waliokuwepo


"Kama ni hivyo niambieni mmekuja kwa lengo gani?" Jimmy aliuliza lengo, lakini ndani ya kichwa chake alikuwa akiwaza, alijiuliza kama sio wachawi ni wakina nani ilihali mbinu walizotumia ni za kichawii? au ndio kujifunza mbinu bila kujua wanachojifunza ni uchaw? Licha kujiuliza hakuwa na jibu


"mbona kila kitu kipo wazi, sisi ni taasisi inayodili na punda kama hawa" aliongea Mzube akiwatafsiri wale viumbe kama punda


"Wanaitwa punda sababu hawana akili, kazi kunguruma ilihali midomo wanayo, anyway natumai yaliyoshuhudiwa leo yataishia hapahapa" aliongea mwanamke mwingine akitoa na tabasamu


"wewebmpuuzi kutwa nzima ni uchokozi kwani huwezi kukaa kimya" aliongea Caren


"Nashindwa kujizuia na sauti yake tamu, shida ni mchoyo sanana sauti yake" Ben alijibu akitabasamu na Freya aliyekuwa kimya muda wote aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko


"Hehe! Hatimae umeongea, inapendeza sana ukiongea na sio kutukalia kimya kwa sura ya utanisiku nzima, mrembo kama wewe kutususia haipendezi" Ben aliongea


"Kazi yetu imeisha hapa sisi tunaondoka" aliongea mwanaume mfypi na mnene aitwaye Beka na kweli walianza kuondoka


"Subiri" Jimmy aliita na Caren alipogeuka alimrushia upanga wake na kutoa Ishara ya shukrani kwa kutingisha kichwa mara moja na baada ya hivyo walitokomea kwakuruka ukuta wa fensi


°°°°°°°°°°


Ndani ya nyumba sebuleni kila mtu alikuwa na wasiwasi na kile kinachoendelea nje, hakuna hata mmoja aliyekuwa na mudi ya kukaa kwenye sofa zaidi ya watatu waliolazwa kwenye sofa wakiwa hawana fahamu, walinzi nao walikuwa makini sana na tayari kwa lolote


Mara mlango mkuu wa kuingilia ulifunguliwa na walinzi walinyoosha bastola zao kuelekea mlangoni, nyuso zao zikiwa makini


Walishusha baada ya kugundua ni Cid na Jimmy na walishukuru kuona wako salama na kitu cha kwanza ni kutaka kujua nini kiliendelea huko nje


Ili kutoleta maswali mengi ni mishtuko isiyo na lazima Jimmy aliishia kuwadanganya kwamba walikuwa wakiwagombania na walipigana wenyewe kwa wenyewe ambapo mwisho wa siku walikufa wote kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, Cid aliamua kuunga mkono uongo wa Jimmy maana isingeleta maana hata akiwaambia ukweli, zaidi sataonekana ni waongo alijiambia sasa si bora kusema uongo kuonekana muongo kuliko kusema ukweli halagu uonekane muongo.


Jimmy alipoulizwa kuhusu kuchafukwa na damu alitunga uongo mwingine aliypujua yeye ambao watauamini na walimuamini, Walinzi hawakuwa wajinga licha ya kujua ni uongo lakini walijiongeza na kukubaliana na uongo kishingo upande. Walielewa hakutaka kusababisha hofu zaidi na maswali mengi, maana hoofu waliyonayo iliwatosha


"Mimi sitaki usumbufu wa polisi, mambo ya kuhojiwa wiki nzima na kusaidiwa uchunguzi sitaki na sidhani kama wataniamini hata nikiwaambia ukweli na huo uchunguzi hawatapata majibu wala suluhu" aliongea Jimmy


"Kwahiyo unashauri tufanyeje?" alouliza Cid


"Tunahitaji kusafisha na kuichoma moto hiyo miili ya kishetani kufuta ushahidi" Jimmy altoa wazo lililomjia kichwani na kukawa kimya sebule nzima


Nusu saa mbele Jimmy pamoja na walinzi walikuwa sehemu yenye miti mingi sana wameikusanya miili ya mashetani isiyo na uhai kwa makundi makundi na kuwa makundi manne, walikuwa wamesimama mbali na miili ile, umbali wa kama mita kumi na tano


Mikononi walishikilia madumu yenye mafuta ta petroli na walikuwa tayari wameimwagia miili ile mafuta ya kutosha na Mlinzi mmoja mkononi mwake alikuwa na lighter, aliiwasha na kutupa chini na moto uliwaka na kusafiri kwa kasi kutokana mafuta ya petrol kuelekea sehemu ile yenye makundi na kuunguza miili ile.


Baada ya kuridhika na kazi ile waliingia ndani ya gari walilokuja nalo na kuondoka mahali hapo





TO BE CONTINUED..........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom