Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA TISINI NA NANE

Hakuna aliyekuwa na furaha na amani kwa wakati ule, si mama yake Samson, wala Samson mwenyewe,
Hata Sarah na Rahma walionesha unyonge fulani, kwani waliogombana walikuwa Top leaders kwenye ile familia, hivyo Kila mmoja alimuomba MUNGU hali ile ipite.

Mzee Mgaya alitoka ndani akiwa na hasira sana huku akimpita mama yake Samson kama hamuoni vile, akaja usawa wa gari lake akafungua mlango wa siti za nyuma na kutoka na makaratasi fulani lengo aingie nayo ndani kwa mkewe, lakini mama Kulwa tayari alikuwa nje, huku akionesha ana hasira zisizo za kawaida.

Weeeee baba, usinitanie, tena nataka unyooshe maelezo vizuri, sihitaji makaratasi, bali nahitaji pesa.
Huwezi kunizuga wala kunifanya mjinga, ili amani ipatikane nahitaji unioneshe kiasi cha pesa nilichokutajia, kisha tutamaliza kesi yetu, hakuna haja ya kuzungushana.mwaka unaisha huu na kumbuka uliniahidi mwenyewe kuwa mwisho wa mwaka utaweka kile kilichopatikana kwa msimu mzima, umepata tenda za kutengeneza vitu kwenye taasisi kubwa tu, hivyo sihitaji senti nahitaji pesa.
aliweka kituo mama Kulwa akionesha anahitaji pesa toka kwa mumewe japo haikujulikana ni kiasi gani.

Mzee Mgaya aliwaangalia mama Samson na mwanaye, namna walivyoonesha kusononeka, ilimuwia vigumu kuendeleza ugomvi japo uso wake ulionesha hasira za wazi, alirudisha makaratasi yale kwenye gari huku akipiga ngumi nzito kwenye moja ya siti, ni hasira ambapo alishindwa cha kufanya haswa mbele ya mgeni mama yake Samson.

Sasa unapiga hilo gari ili iweje, wewe nipige Mimi Wala usijizuie maana hoja zangu, matakwa yangu hayana maana ndiyo maana nimefikia hatua ya kukuudhi , Mimi sijachukia wewe kufanya mambo yako na Tausi, unaweza hata kumjengea Jumba la kifalme (kasri)Mimi sitauliza wala kuonesha hisia mbaya Bali ni pale utakaponitimizia ulichoniahidi basi. Nataka unioneshe kiasi cha pesa taslimu iwe Cash, usiniambie zipo wapi mara wapi.
mama Kulwa aliongea kwa kujiamini kiasi cha kumtisha mama yake Samson maana tangu amfahamu hajawahi kumuona akiwa kwenye hali ile.

Mzee Mgaya alicheka sana, tena sana siyo kicheko cha kawaida, Bali kicheko cha majonzi na huruma kwa maisha anayopitia. Kisha akawasha gari na kumuashiria Samson apande Kisha wakaondoka huku wakiacha maneno mengi aliyoongea mama Kulwa japokuwa hawakuyasikia vizuri.

Mzee Mgaya aliendesha gari taratibu huku akiwa hajui anaenda wapi huku muda mwingine gari likihama njia yote ni hali aliyokuwa anapitia, hatimaye wakapark gari kwenye Pub moja ambayo haikuwa na watu wengi, wakaamua kukaa nje karibu na maua fulani mazuri huku Samson akiwa na shauku ya kutaka kumuuliza Mzee Mgaya maswali kadhaa.

Waliita vinywaji visivyolewesha kisha Samson akaanza kujimiminia ile soda huku Mzee Mgaya akiwa katulia tu, huku akicheka peke yake kila mara.

Samahani baba pengine sipaswi kujua habari zako nyingi lakini kwakuwa mmekwazana na mama mkubwa pale najikuta napenda nifahamu kwani mama Kulwa kakwazika na nini?
aliuliza Samson.

Mwanangu wakati mwingine napenda sana maisha wanayoishi wazazi wako, yaani wanaheshimiana kiasi cha Mimi kuwaonea wivu, yaani juu ya kuwa hawana kitu lakini , sijawahi kushuhudia wala kusikia habari kuwa labda wamegombana, ni ngumu, sisemi kuwa hawagombani lakini Mimi na mke wangu tumezidi na si Mimi Bali ni huyu mama yako asiyekua yaani sijui anajionaje ila yote namuachia MUNGU.
aliongea Mzee Mgaya akiwa hata soda hajaifungua kwani huenda aliagiza kwa kutimiza masharti ya eneo husika.

Hivi kumbe mama Kulwa mlienda naye kwa mama yako mdogo Tausi siyo? aliuliza Mzee Mgaya.

Ndiyo ila aliondoka mapema sana kwani alisema anajisikia vibaya.
alijibu Samson.

Mzee Mgaya alicheka kidogo Kisha akaendelea..........

Mwanangu najua kuna vitu vingine sipaswi kukwambia lakini haina budi wewe ni kijana sasa, ni mtu unajua baya na zuri ni lazima nikwambie tu baadhi ya mambo, ni kwamba bila shaka unaukumbuka ugomvi wa mwaka jana Kati ya Mimi na mama yako mkubwa.mzee Mgaya aliongea huku akimwangalia Samson.

Sam akatingisha kichwa kuonesha anakumbuka.

Mwanangu na ndiyo maana huwa nakushauri usome kwa bidii zote yaani ujitoe nguvu na akili zako zote ziishie kwenye masomo, maana Kuna watu wanakuombea ushindwe ili wapate cha kuongelea, pia nataka ujue kuwa Kuna siku niliita wazee pale kwangu watusuluhishe, baada ya mama yako kusema hela natumia vibaya hususani wewe, akidai nasomesha mtu mwenye laana, na ambaye ni ngumu kuonesha matunda ya uwekezaji unaofanyika, unasahau Kuna siku ulifukuzwa, na bahati nzuri ndiyo siku narudi, Sasa kile kipindi ndicho mke wangu alitaka wewe ufukuzwe na baada ya wazee kumuuliza ili Aishi na Mimi kwa amani anataka nini , aliwajibu kuwa wewe uache shule siyo uhame nyumbani kwake, la hasha uhame yaani isitumike shilingi yoyote yenye kukuhusu wewe.

Hivyo Mimi na uzee huu nilitumia busara kuwa siwezi kumuacha mke wangu kwa mambo ya kipuuzi na pia siwezi kukufukuza wewe, kisa ujinga wa mtu mmoja, Imani yangu ni Moja juu ya wewe kutuonesha nidhamu mbovu mara kadhaa lakini najua una kitu kichwani kwako kipo kitu.
aliweka kituo mzee Mgaya.

Sasa baba niambie ulifanyaje ili nisifukuzwe, na pia wewe na mama maisha yenu yakiendelea vizuri. aliuliza Samson.

Samson umekua na hakika najivunia kwa Sasa , umeuliza swali zuri ambalo nililisahau,
Ni kwamba nilitumia mbinu ya kumuahidi kiasi fulani cha pesa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, na hiyo pesa ipo na ningemuonesha lakini tatizo ameuliza kwa njia ya dharau huku akishinikiza aione Leo leo na Mimi kama mwanaume siwezi kupelekwa kihivyo. Yaani kuona kile kibanda cha Tausi tayari akaona pesa itakuwa imepotea, badala ya kutulia aulize kwa heshima yeye ananiropokea na hata hivyo tarehe ambayo tulipanga haijafika. Pia hela hizo zipo kwenye account ambayo hata nikifa leo yeye ataziona tu kwani taarifa zangu zote anajua hakuna kitu nimemficha, kwani mama Jose ana nini lakini.
aliongea kwa sauti Kali Mzee Mgaya huku akigonga ile meza iliyodizainiwa
Kwa mtindo wa culture ikifanana natumbwi.

Oyaa wewe James vipi muda wote naona uso wako umesawajika nini kinakusibu, na shida yako ni hela tu hakuna namna yaani na tatizo lako wewe muoga, na utakufa masikini, au ndiyo umeshatidhika na maisha yako eeeh. aliongea kwa dharau yule jamaa ambaye umri unafanana na mzee Mgaya kwani wote walikuwa na mvi nyingi za uzee ili tofauti yao ni kwamba huyu mwingine alijiweka kiujana kwani alikuwa kavaa kaptura na vest huku shingoni kukiwa na cheni kadhaa Samson alimkumbuka kuwa ni bwana wake Cathy.

Sikia wewe nipo na mwanangu na sikuzote huwa nakuonya upunguze utani haswa ukinikuta na watoto wadogo kama hawa, aliongea Mzee Mgaya akionesha kukerwa na maneno ya jamaa.

Wewe James vipi bwana, Mimi nakwambia ukweli unadai nakutania ona sasa umepaki land cruiser hapa yaani gari za kwendea safari za mbali mikoani huko wewe unakuja nazo huku wewe vipi au nikuuzie hii yangu, kwanza hela zenyewe unazo. aliendelea na tambo yule jamaa.

Kufumba na kufumbua yule jamaa alipigwa ngumi kwenye paji la uso akaangukia kule, kwenye kokoto huku akivuja damu, Mzee Mgaya akataka kukimbia lakini akazuiwa na baadhi ya watu pale.

Weeee Mzee unaenda wapi nani unataka kumwachia kesi, yaani uuue halafu utuachie msala hebu tulia hapo. Mzee Mgaya alitii amri.

Mzee Mgaya kazua balaa kwenye pub alipoenda kupunguza mawazo,

Mama Kulwa anataka aoneshwe pesa na mumewe na haelewi chochote,

Muda wa Samson kuripoti shule unakaribia, itakuwaje?

Kumbuka Kuna mgeni mama yake Samson naye anatakiwa arudi kijijini.

Itaendelea...............................
 
SEHEMU YA TISINI NA TISA

Yule bwana wake Cathy aliamka na kujifuta damu huku akitoa maneno ya vitisho kwa Mzee Mgaya kuwa atamjua yeye nani Kisha akaliendea gari lake la kisasa kwa miaka ile na kutokomea.

Meneja wa sehemu ile alimfuata Mzee Mgaya na kumtaka naye aondoke akidai anaidharaulisha pub yao halafu, kwa umri wake na maamuzi aliyoyafanya haviendani.

Sikiliza Mzee hii ni biashara na tupo hapa kutafuta pesa, ila pesa zako sizihitaji , siyo kwa leo tu , nikwambie tu kuwa tunakuomba usithubutu kukanyaga hapa tutakuja kuleteana matatizo, sitosita kukuitia polisi ikiwa utalazimisha kuja hapa. aliongea yule kijana huku akimsukuma Mzee Mgaya.

Mtoe nje mshamba huyu, yaani sehemu ya kuja kurefresh mind yeye anakuja kuleta timbwili lake yaani Mzee mzima hajielewi , ama ni kubwa jinga hili zee?

Kwanza hata hatujawahi kumuona hapa,yaani kuja leo tu mara anaanzisha balaa.
walitukana baadhi ya watu waliokuwa pale huku Samson akiona aibu ya mwaka.

Mzee Mgaya aliendesha gari kwa fujo huku Samson akiomba MUNGU gari lisije pinduka, hatimaye walifika nyumbani kwao, huku Sarah akiwafungulia geti, Mzee Mgaya hakuingiza gari ndani badala yake aliingia Kisha akaongea masuala fulani na Sarah huku akiangalia saa yake ya mkononi. Kisha akampa maagizo Samson.

Dada yako sijui aunt yako nimeshampa maelekezo, na pia umuage mama yako mwambie Mimi nitakuja kesho asubuhi, halafu pia asifunguliwe geti mtu yeyote hata kama mnamfahamu labda awe wa muhimu sana.
aliongea Mzee Mgaya huku akionesha ni mwenye wasiwasi hata shati alilokuwa kachomekea vizuri lilikuwa limechomoka upande mmoja huku akiwa hata hajui Kisha akawasha gari na kuondoka kwa high speed.

Vipi mlienda wapi maana tulikuwa na wasiwasi maana ni usiku huu ,na hivi unayaonaje haya maisha mdogo wangu,au wamerogwa hawa?halafu ujue mama Kulwa hataki kulala ndani yupo kwenye gari lake? aliongea Sarah akionesha kuchoshwa na maisha yale .

Mmmmh mama yangu yuko wapi kwanza, halafu ujue baba kazua msala huko tulikotoka sijui itakuwaje yaani. aliongea Sam akiwa anafunga vizuri geti dogo.

Weeeee eti nini?
Yaani ya hapa hayajaisha bado mabichi kabisa , halafuuuuuu .. Sarah alijishika kiuno Kisha wakaanza kutembea kuja usawa wa parking ya magari.Wakawaona mama Kulwa na mama yake Samson wakiongea jambo huku mama yake Samson akimsihi mwenzake kuwa waingie tu ndani na mambo yale yataisha tu.

Shoga yangu huyu mzee ananifanya Mimi kama kinyago chake Sasa nataka atambue kuwa Mimi ni mke wake na yeye ni mume wangu, Tena tukioana miaka mingi enzi za utineja wetu, hawezi kuendesha mambo kiholela halafu nimkalie kimya, sema ni wewe wala usijisikie vibaya Hawa wanaume bila kuwashtua shtua huwa hawaeleweki. aliongea mama Kulwa huku safari akionesha hasira zimepungua.

Kwanza yuko wapi maana nakuona Sam tu, baba yako yuko wapi?
aliuliza mama Kulwa.

Alikuja mpaka hapa nadhani alikuwa ananileta Mimi tu ila kaondoka tena. alijibu Samson.

Mbona humwambii habari zote?
Ohooo , nasikia kapiga mtu huko, eti kampiga nani vile?
aliuliza Sarah.

Samson alijibu huku akionesha hataki zile habari zimfikie mama Kulwa wala mama yake kwani zingewahuzunisha lakini kwakuwa Sarah alishamwaga mchele basi Samson ikabidi aeleze full mkanda.

Jamani, jamani baba Jose, kwahiyo hasira za hela ambayo aliniahidi Kisha akaamua kutumia na Tausi, na nikimuuliza anashindwa kunipa majibu kamili, kaamua kwenda kuleta matatizo zaidi.
Hivi mnamjua vizuri huyo mtu aliyepigwa?
Si mtu mwenye huruma hata kidogo, yaani kifupi mume wangu kajitafutia matatizo. aliongea mama Kulwa akionesha kumlaumu mumewe kwa kitendo alichokifanya.

Hivi anaweza kwenda polisi eeh, maana Mzee kaagiza tusifungue geti ovyo ovyo. aliongeza Sarah.

Nani aende polisi, ni afadhali angeenda huko ingekuwa afadhali mtu mwenyewe anatafutwa na hao polisi, yaani baba Jose kanunua matatizo mengine kabisa Hilo jitu analoishi nalo Cathy nalijua kuanzia biashara zake na maisha yake Kila kitu kwake ni cha magendo, hivyo nadhani mmeshanielewa namzungumzia mtu wa aina gani. hapa dada yangu nikwambie ukweli nachojua mume wangu hana pesa, na Sina uhakika kuwa Samson atasoma ikiwa Mzee Mgaya ametafuta battle na lile jamaa.
mama Kulwa aliongea huku akitoa kicheko cha kejeli.

Mama Samson na mwanaye waliangaliana Kisha mama mtu akatabasamu,
Ni tabasamu ambalo lilibeba maumivu, kukata tamaa na masikitiko juu ya stori wanazopewa kuhusu hatima ya Samson.

**************************************

Kesho asubuhi na mapema honi ya gari lililoonekana kuwa siyo la Mzee Mgaya ilisikika, lakini kutokana na kuonywa wasifungue geti basi Kila mmoja aliingiwa na uoga lakini mama Kulwa kwakuwa alimtambua ni nani basi akafungua.

Msichana mwenye nyodo na kibri akiwa kavaa suruali na raba vyote ni vya mazoezi aliingia kwa dharau huku akimsalimia mama Kulwa na kuanza kutoa vitisho fulani.

Hivi mama Kulwa umesikia habari za my kupigwa na mumeo, hivi Mzee Mgaya kwa huwa anasumbuliwa na nini lakini kwasababu amemuumiza mwenzie na ukisikia sababu yenyewe, inashangaza.

Mtu Sina biashara Wala kazi ya kueleweka hapa mjini halafu mnaniumizia yule mtu mnataka niishije? Halafu Mzee Mgaya......... Cathy alishindwa kumalizia sentensi yake baada ya kusikia honi ya gari la Mzee Mgaya ambaye aliingia akiwa na begi fulani dogo akiwa kaongozana na vijana fulani ambao wanafanya kazi kwenye Karakana yake.

Sarah na Samson nadhani Jana Kuna maelezo niliwapa, vipi kwanini mmekaidi maagizo yangu, aliongea kwa ukali Mzee Mgaya bila hata salamu.

Na wewe Binti humu ndani kwangu unatafuta nini, Mimi ni masikini naishi kimasikini hata akili na mipango yangu ni ya kimasikini. Hawara yako si tajiri Wala Hana kitu kama ambavyo huwa anajinasibu, labda atakuwa hajui maana nzima ya neno utajiri. sihitaji mazoea na mke wangu na nyumbani kwangu .
nakuomba utoke nisije nikafanya mambo yasiyofaa jamii ikaniona sifai.
Mzee Mgaya aliongea kwa ukali huku Kila mmoja akimuogopa kwa muda ule hata mkewe mama Kulwa alikuwa kimya asiongee chochote.

Mzee Mgaya aliwakaribisha wale vijana wake ndani wakaongea ndani ya muda fulani Kisha wakatoka huku wakiwa na furaha kiasi fulani.
Ila hakuna aliyejua wamefanyiwa kitu gani. Kisha Mzee akaiamuru familia yake yote iingie ndani waongee, ilikuwa ni amri hakuna aliyepinga.

Itaendelea..................
 
Daah..! Huyu mzee mgaya ni kama profesa wa juakali aisee
 
SEHEMU YA MIA MOJA

Mzee Mgaya akiwa na sura ya kiume huku weusi wake ukizidi kudhihirisha msimamo wake, hakutaka kukaa kwenye Kochi kama wengine walivyokaa badala yake alivuta kiti chake cha mbao cha kawaida mithili ya office chair. Akaanza kuongea kwa msisitizo sana.........

Katika safari ya maisha kila mwanadamu anapenda kutimiza na kutimiziwa mahitaji yake kama ilivyo kawaida kwa watu wengi.

Lakini je, mazingira yanaweza kuruhusu upate unachotaka?

Au hali inaruhusu ufanye unachotaka?

Kila binadamu ana akili na upeo wake, Kila binadamu ana uwezo na kiasi fulani cha kufikiri, hivyo migongano ambayo hutokea kwenye familia na jamii nzima ni hali ya kutofautiana kimtazamo, kimsimamo na kimaamuzi, huwezi kumfurahisha Kila mtu na huwezi kutimiza Kila kitu Duniani .
Unaweza kuacha urithi kwa watoto wako wa kuwazaa, yaani Mali nyingi mno lakini bado ukalaumiwa , kwanini uliacha Mali za design fulani.
Hayo ndiyo maisha ya walimwengu

Sasa kwa mifano hii naomba kwanza niwaombe radhi familia nzima kwa yaliyotokea jana nadhani wengi mmeshangazwa na kitendo cha Mimi kufanya vitendo vilivyoonesha ni kukosa msimamo lakini ni mambo ya kawaida wala yasiwashtue sana. Kisha akamgeukia mkewe..........

Mke wangu sina haja ya kukuelezea sana umuhimu wangu kwako, isipokuwa naweza kusema wewe ni shina lililobeba matawi , maua na matunda yote yanayopendeza na kuning'inia ,umenipa heshima ya ukubwa wa uzao wangu katika jumla ya watoto wangu watano, huku kukiwa na watoto watatu wakiume, ni heshima kwangu na jina langu la ukoo wa MGAYA.
Nakupenda mke wangu na ahadi niliyokuahidi iko pale pale nadhani baada ya kikao hiki tutamalizana.
aliongea Mzee Mgaya huku akimkazia macho mama Kulwa, Kisha akamgeukia mama yake Samson,

Shemeji najua umechoshwa na kushangazwa kidogo na yanayoendelea au uliyoyasikia, pia kule kwetu kijijini ni nadra sana kuona mambo haya na yote ni kutokana na uchache wa watu, na kumbuka huku ni mjini mambo ni mengi watu ni wengi pia hivyo usishangae kuona yanayoendelea, japokuwa si vizuri kwa yaliyotokea lakini nakuomba shemeji yangu usijisikie vibaya. aliweka kituo mzee Mgaya.
Mama Samson hakujibu chochote zaidi ya kutabasamu tu, huku akionesha unyonge na furaha au tabasamu la kulazimisha.

Kisha Mzee Mgaya aliinuka na kuingia chumbani huku mama Kulwa akimfuata, watu wote walitawanyika huku Samson akiwa karibu na mama yake kumfariji fariji ili asiwe mpweke, baada ya dakika kadhaa mama Kulwa alitoka akiwa mwenye furaha sana, yaani ile furaha ya kupitiliza.

Eeh shoga hapa ningeomba ujiandae twende mjini kwaajili ya kwenda kuangalia baadhi ya vijizawadi, Kuna kiasi cha pesa katoa shemeji yako, lakini pia na Mimi Nina zawadi zangu haswa kwa mabinti zangu (akimaanisha dada zake Samson wa kijijini) .
Mama yake Sam alishangaa visa vya mama Kulwa na mumewe namna wanavyocharurana na kupatana haraka mno, alibaki kushangaa tu,mama Kulwa alitoa maagizo kuwa wao lunchtime watapata huko huko mjini hivyo Sarah asiwahesabie Chakula.

Wakiwa kwenye gari mama Kulwa akiwa kwa usukani, pembeni mama yake Samson na siti ya nyuma Samson ambaye alikuwa naye akishangaa baadhi ya majengo ambayo tangu afike hajawahi kuyaona vizuri, stori zilinoga mama Kulwa alikuwa anaongea huku ikionesha Mzee Mgaya kamtimizia mkewe ahadi yake.

Hapa kwanza tupitie huko kwenye maji mengi, (baharini)tukashangae shangae kidogo, kisha tutarudi nikakuoneshe vijibiashara vyangu maana shoga yangu una haraaaaka ya kuondoka hivyo inabidi leo leo tuzunguke Kila mahali japo nahisi muda hautatosha na tukumbushane safari ya mwisho ni kwenda stendi kukata tiketi sawa Samson? Mama Kulwa alisisitiza huku akimtaka Samson awakumbushe pale watakaposahau.

Walizunguka sana na gari huku mama yake Samson akishangaa zaidi baada ya kufika kwenye duka la kwanza la mama Kulwa kukiwa na wauzaji zaidi ya wawili akamkanyaga mwanaye Samson, Kisha wakaangaliana,

Mmmmh mwanangu, kumbe Hawa watu Wana pesa eeeh , Sasa huyu mama yako mkubwa alikuwa anasikitika nini, eti pesa hazioni wakati kumbe ana biashara yake nzuri kabisa jamani, aliongea kwa kunong'ona mama yake Samson.

Mama yangu, Hawa watu si haba Wana maisha mazuri tu mbona, na Kuna duka lingine lipo nyuma ya hili, nalo ni la kwake, pia ungekuwa na muda ningekuonesha na miradi ya Mzee Mgaya kifupi wapo vizuri tu.
Samson alifafanua.

Mwanangu hawa watu inatakiwa uwatumie vizuri, usicheze na shule kumbuka hivi vyote unavyoviona ni Mali za watoto wao, hivyo wewe tumia mwanya huu uliopewa kuweza kutimiza ndoto zako Hakika hii nafasi hupaswi kuipoteza baba yangu , Wala si kwa manufaa yetu Bali ni wewe kwenye maisha yako.
Hebu tizama Mali zote hizi dukani lakini bado huwa analalamika hana hela. Samson na mama yake walikuwa wakiongea kwa sauti za chini Kisha wakanyamaza baada ya mama Kulwa kuwa anakuja walipo.

Shoga yangu hapa ndipo ofisini kwangu, nazugazuga hapa maana inabidi tutafute vijisenti ili siku Mzee Mgaya akirudi kijijini basi tuweze kulima kisasa zaidi, eti si nasikia naye ana mashamba yake tena ekari nyingi eeeh? aliongea kwa utani mama Kulwa.

Waliingia duka la pili ambalo hili lilikuwa dogo lakini lililopendeza mno, likisheheni bidhaa za kike tu, mikoba na viatu na baadhi ya vitu vinavyohusiana na wanawake, walinunua baadhi ya vitu pale huku Samson akishangaa kwanini mama Kulwa anunue vitu kwenye duka lake, yeye alihisi angechukua tu bure si kwake? labda hakujua maana ya biashara kwa wakati huo. Kisha wakaingia kwenye maduka ya nguo na kuteketeza pesa nyingi kiasi cha mama yake Samson kushangaa moyo wa mama Kulwa kwani hatabiriki, Kuna muda anaonekana ana roho mbaya, mara Kuna muda ni kama mtu mwema lakini yote kwa yote mama Samson aliwashukuru sana.

Samson aliweka mabegi kwenye buti la gari Kisha wakaingia kwenye hotel, kubwa na yenye vyakula vya gharama, huku Samson na mama yake wakishangaa pesa inayolipwa lakini yote kwa yote walifurahi kwani ilikuwa ni sehemu ya utalii kwao, baada ya hapo gari ilielekea stendi kwaajili ya kupata tiketi ya kusafiria na Kisha wakarudi nyumbani.

Walishangaa kukuta Kuna gari ya kifahari imepaki pale nje kwao, lakini mama Kulwa aliingiza gari ndani wakashuka Kisha wakashangaa kumuona Cathy na bwana wake wakiwa wanapeana mikono na mzee Mgaya kuonesha kuna mambo walikuwa wakiongea na wakionesha wamemaliza. Cathy alisalimiana na Mama Kulwa Kisha wakaondoka.

Mume wangu hawa walifuata nini, aliuliza mama Kulwa.

Huyu ni mpuuzi tu, alikuja kuniomba msamaha kwenye mambo yake ya Jana nadhani alilewa ndiyo maana alinikashifu sana lakini tumemaliza, ni mtu nilimsaidia na kumpa michongo mingi kipindi hicho, baadaye akajiingiza kwenye kuuza motors used akizitoa nje na kuingiza nchini, na hapa ndipo alipoanza kufanikiwa , lakini pia ana madili mengi yasiyozungumzika yote kwa yote Mimi ni Moja ya watu muhimu kwake, nadhani huko aliko akili imekaa sawa ndiyo maana amekuja kuomba msamaha. alifafanua mzee Mgaya.

Mmmmh sawa mambo yenu mnajua wenyewe, Sasa mume wangu sisi tumeshaandaa mizigo yetu vipi wewe ulisema una mizigo kwaajili ya mdogo wako vipi umeiandaa ili tuunganishe kwenye mizigo yetu?
aliuliza mama Kulwa.

Mizigo ipo utaikuta juu ya kabati la nguo, alijibu kiufupi Mzee Mgaya.

Siku iliisha watu wakiwa na furaha sana, hasa mama yake Samson ambaye mawazo yake yote yalikuwa kwenye safari ya kesho maana alishachoka visa vya pale, huku akiwa anaongea na Rahma kuwa siku moja awatembelea kijijini kwao ili ampeleke mtoto wakamtambike kwenye mizimu yao.
Rahma alicheka huku akionesha utayari kuwa ipo siku ataenda.

Walipata Chakula Cha usiku Kisha wakafanya Sala fupi ili kumuombea mama yake Samson asafiri salama salimini, ili akasherehekee vizuri siku ya kumpokea masihi, ambaye siku yake ya kuzaliwa huadhimishwa Duniani kote Kila tarehe 25 December, hakika ulikuwa ni usiku mzuri na wenye baraka kwenye familia ya mzee Mgaya.

Je safari itakuwepo? Maana ya MUNGU mengi. Ungana nami kwenye mwendelezo.

Itaendelea................................
 
Aah sasa hapo mwishoni mbona unatutisha tena
 
Kama huwezi kusoma mpak mwisho kaa kimya au nenda kacheze na watoto wenzio kibaba na kimama mpike pike mcheze rede

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
SAwa shogangu ntakuja kukuungia tela tucheze..hivi huwa mnaachiwagwa funza matakoni wanakua wanawachonyota au matakoni mnawashwa kujibu msioulizwa au jamani wanaume wakiwa wanawasiliana wamama mkae mchochewe ukuni muive mazafanta
 
Leta mwendelezo sasa
 
Mmmmh mkuu .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom