Simulizi: Milango ya mafanikio

Jack Daniel

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
2,146
10,380
SEHEMU YA KWANZA.(utangulizi)

Sam, saam , samsoniii, huko unakoenda hakikisha unakula huko huko, maana huwezi kunisumbua kila siku , kwanini husikii weee mtoto Sasa nikwambie tu kuwa leo hakuna kula hapa nyumbani. nakwambia rudi sam, rudiii au unataka nimwambie baba yako akija, umesahau alichokufanyia Mara ya mwisho
Wewe, weeeeeeeeeh.

Yalikuwa ni maneno ya mke wa mzee
Mgaya, au mama yake na Samson, akimtaka mwanaye arudi ili aendelee na kazi za pale nyumbani kwao kuliko kwenda kuchunga ng'ombe wa watu tu, wakati wao hawana hata ng'ombe mmoja.

Lakini maneno yale wala hayakuweza kusaidia chochote maana Samson alizidi kutokomea porini akifuata kundi kubwa la ng'ombe kutoka kaya tofauti tofauti.huku jambo pekee lililo kuwa linampeleka Samson kule ni sinema za bure, yaani ng'ombe wanapopigana.

Iko hivi , tukiacha wafugaji wakubwa kama wamasai,wamang'ati na wasukuma, wapo baadhi ya makabila wengi wanafuga ng'ombe, mbuzi, kondoo na hata kuku, ni kawaida tu kukuta karibu Kila kaya Ina mifugo, utakuta hapa Kuna ng'ombe ishirini, hapa kumi na tano sehemu nyingine hata ng'ombe zaidi ya hamsini.

Lakini pia wapo watu wanaoazima ng'ombe wa mtu kwa lengo la kujipatia mbolea(samadi) kwaajili ya kukuzia mazao mbalimbali,
Yaani mtu unakaa na ng'ombe zaidi ya ishirini wa mtu lengo ni maziwa na mbolea, japo hata hayo maziwa huwa siyo mengi kutokana na aina ya ufugaji, kwani si wa kisasa.

Basi wakati mifugo kama ng'ombe wanakutana malishoni(nyikani) huwa Kuna kutambiana kwa madume au mafahali kutoka vikundi tofauti tofauti huku kukiwa na wale mafahali wanaojulikana kabisa kuwa ni unbeaten yaani wanatisha kwa kupigana.

Ni mchezo mzuri na watoto wengi wa vijijini huwa wanaenjoy sana kuangalia mapambano ambayo kwa kweli huwa yanaburudisha japo ni hatari maana huwa Kuna ng'ombe wenye hasira pale anapopigwa au anaposhinda hivyo ule ushindi wake humfanya aone anamudu Kila kiumbe.

Wenye mchezo wao Wala huwa hawapati taabu yaani wakiona mpambano ushaanza wanapanda juu ya miti huku wakienjoy game Bila wasiwasi, huku yule mwenye ng'ombe aliyeshinda akiheshimika kana kwamba kapigana yeye na Kuna wakati mnamaindiana kiasi Cha kuzichapa wenyewe.

Ni mchezo mzuri sana hasa ukiwakutanisha mafahali wale ving'ang'anizi inachukua muda wa lisaa au masaa mawili huku wafuatiliaji wakichukua points ni fahali yupi anajua vichwa na yupi anajua kutumia pembe zake vizuri, hakika ni mchezo unaovutia watoto wa vijijini, lakini pia hata sare hutokea. Kivipi?

Ni pale ng'ombe wanapochoka na kubaki wanaangaliana na Lila mmoja kushika njia yake wakiendelea kula majani, au ni pale waangaliaji wanapochoka yaani burudani inatosha, mshindi hapatikani , au Giza linaingia wanaachanishwa huku mkipanga namna ya kukutana siku nyingine.

Ni mchezo mzuri sana, wakati waliozaliwa mjini wakiinjoi mapambano ya akina Evander na akina Tyson, M. Alli watoto wa kijijini Wana namna yao ya kufurahi.

Samsoni ni mtoto pekee wa kiume kwenye familia ya watoto wanne wa mama mgaya huku yeye akiwa watatu kuzaliwa, huku kwa baba yake wakiwa ni wengi maana mzee mgaya alikuwa na wake wawili.

Miaka ya 1996 alianza darasa la kwanza kijijini kwao akiwa na umri wa miaka kumi, umri ule haukuwa kikwazo sana maana Elimu ilipewa kipaumbele sana hasa maeneo ya vijijini huku sera ile ikichagizwa na serikali mpya ya hayati B. W. Mkapa.

Hivyo watendaji na wenyeviti walihimiza watoto wote waanze darasa la kwanza huku wengine wakiwa na umri mkubwa zaidi ya Samsoni, basi samsoni alijitahidi sana kusoma kwa mbinde na uvumilivu wa hali ya juu kwani changamoto kubwa ilikuwa ni umbali kutoka huko mashambani anakoishi Hadi kijijini ilipo shule yao.

Alijitahidi Hadi pale alipohitimu shule ya msingi akiwa na umri wa miaka kumi na Saba, alimaliza na umri huo ni baada ya kufeli darasa la nne akalazimika kurudia darasa.basi baada ya kumaliza Elimu ya msingi hakukuwa na matarajio yoyote kwa labda ataenda Sekondari, si wazazi wake Wala si yeye mwenyewe ambaye aliwaza hatima ya aendelee shule ya upili au awe na mishe zingine.

Miaka kumi na Saba kwa mtoto ambaye kakulia kijijini huwa haha mature bado tofauti na aliyekulia mjini, basi balehe ilimfanya Samsoni awe mbishi, kiburi, jeuri na asiyependa kazi za pale nyumbani kwao, badala yake ni kwenda kucheza mpira wa makaratasi, au kwenda kuangalia mapigano ya ng'ombe huko malishoni.

Kwakuwa baba yake alikuwa na nyumba mbili {wake wawili}basi mama Mgaya alijikuta anapata kazi kubwa ya kuhandle kijana wake ambaye alikuwa akimgomea kazi nyingi ikiwemo kutokujijali yeye mwenyewe, maana hata kuoga yaani usafi unaohusu mwili wake samsoni ilikuwa Hadi akumbushwe vinginevyo na baridi la mkoani inaweza kupita siku kibao hajaoga.

Basi siku moja baba yake Samson mzee Mgaya alirudi nyumbani akitokea kwa mke mdogo, alifika pale huku akiegesha baiskeli yake aina ya Avon ukutani, huku akisikia makelele ndani yaliyoashiria hakukuwa na amani. Sauti alizitambua ni Samson na mama yake.

Vipi jamani Kuna Nini? Enhhhee mama Jane Kuna Nini na mwanao?
Aliuliza mzee mgaya. (Huku akimdaka Samson ambaye alitaka kupenya pale mlangoni akimbie)

Kaa chini wewe. aliamrisha Mzee Mgaya.

Afadhali umekuja, Tena ni kama MUNGU kakuleta Mimi nimechoka baba nimechoka, hebu muangalie mwanao, mtazame mavazi na nguo zake, haogi, hafui hapo alipo ukiingia ndani kwake hakutamani , Wala huwezi amini kama analala binadamu. Naomba nisaidie mwanao anatia aibu, nasema Bora hata alivyokuwa shule kuliko anavyoshinda hapa maana anazidi kuniongezea mawazo nashindwa kujua kwani nilimzaa mtoto wa aina gani.

Alilalamika mama Mgaya huku akizidi kumpalia makaa Samson, maana alijua fika tabia ya mzee Mgaya, akianza kupiga mtoto haangalii wapi anachapa.
Inajulikana kuwa samsoni hasikii vizuri kutokana na Kofi alilowahi kupigwa na baba yake kwa tuhuma za kusababisha pancha kwenye baiskeli yake.

Kitendo hiki kilimuuma mama Mgaya kwamba kwanini ampige mtoto mdogo kama anapigana na mtu mzima, na kupelekea mtoto akawa hasikii vizuri.

Lakini siku hiyo Wala hakujali aliamua liwalo na liwe maana samsoni alizidi ukorofi.

Mzee Mgaya alivuta kiti akakaa, akamsogeza Samson karibu na alipokaa akamwangalia kama sekunde kadhaa hivi bila kusema chochote Kisha akajiinamia chini huku akicheka kwa kumuhurumia Samson.

Itaendelea......................
 
SEHEMU YA PILI.

Mwanangu Samson, nakuonea huruma sana kwa aina ya maisha yako unayoenda nayo, nakuomba ubadilike mwanangu, unatambua fika hali halisi ya maisha yetu kwamba sisi wazazi wako ni masikini.

Sasa iweje umpe kazi mama yako Kila siku anaongea na wewe mtu mmoja, kwanini?
Hapo ulipo si mtoto tena ni mvulana mkubwa ambaye unategemewa, yaani naamini wewe ni msaada mkubwa pindi nikiwa sipo, lakini ya MUNGU mengi naweza kutangulia kufa hata leo nawaacha watoto wangu wengi tu lakini nyinyi wa kiume ndiyo nguzo pekee ya kuongoza hata hao dada zenu.

Badilika mwanangu, sitaki niwe nagombana na wewe kila wakati, ifike mahali nikuheshimu kama mwanangu na utuheshimu kama wazazi wako.

Yalikuwa ni naneno machache ya mzee Mgaya ambapo kwanza mama Mgaya mwenyewe alishangaa lakini pia hata Samson, maana kwa mkono mwepesi wa maamuzi wa mzee yule hakuna aliyefikiri kuwa ataongea maneno matupu bila makofi au viboko, ila kwa siku Ile alikuwa kawaida.

Siku ya pili kulikucha Samson akiwa anafanya kazi ya kuhamisha matofalu toka kwenye tanuri kuleta karibu na msingi uliochimbwa, karibu na nyumba yao kwaajili ya ujenzi, ni kazi ambayo alikuwa anafanya basi tu,labda kwakuwa baba yake alikuwepo.

Mara Kuna kijana jobless ambaye ni Rika la samson ila yeye aliacha shule kitambo sana, alipita karibu na anaposomba tofali Samson.

Oyaaaah Sam vipi, naona unapiga kazi mwanangu, dah sema Nini mi hata siwezi weee, we mitofali kama hiyo unajitwisha kichwani, kwanini usingetumia hata toroli Samuuuu?

We acha tu na hapa nilipo sijui Nina mkosi gani yaani tangu nimalize shule wananitumatuma tu, Mara fanya hiki Mara hili ili mradi wanione nafanya kazi, sijui haya mateso yataisha lini. alijisemea Samson.

(Hahaha) tatizo wewe Sam muoga sana, kwanza nikuulize, kwani hao mafundi ujenzi si wanalipwa? aliuliza yule kijana.

Wanalipwa ndiyo, na hapa nikifikia hatua fulani kwenye kusogeza tofali, nimeambiwa nijaze Yale mapipa ya maji Sasa jamaa yangu huu si uonevu kweli huu?yaani kulipwa walipwe wengine kazi nifanye Mimi kweli? alihoji Samson huku akionesha kukerwa sana na ile kazi.

Waliendelea kuongea mambo yao ya kipumbavu huku wakishawishiana mambo ya hovyo kulingana na umri wao, foolish age.

Mida ya saa kumi na mbili jioni familia nzima ilikuwa Barazani ikipunga upepo, mama Mgaya akavunja ukimya,

Hongera mwanangu Leo umefanya kazi kubwa na nzuri sana,

Weee kweli kabisa mama leo kaka Sam kafanya kazi nzuri wote tumeona jamani,. walidakia Dada zake Sam huku wakionesha kufurahi. Lakini Cha ajabu licha ya pongezi zote Sam alikuwa kakunja ndita kwa hasira akionesha hahitaji sifa wala pongezi zozote, uzuri hakujibu kitu .

Kwahiyo umekasirika, we mjinga nini, unadhani ukinikasirikia ndiyo hutatumwa Tena, muone kwanza sura yake, Mimi ni mama yako mpumbavu wewe na hapa ulipo kila kazi unayostahili utafanya, sijui unajiona nani humu ñdani, au kwakuwa Jana baba yako kaamua kukuacha hajakutia bakora? Naunajua Nini kingetokea . aliongea mama yake Samson kwa hasira huku samsoni mwenyewe akikimbilia ndani.

Usiku wa siku ile Samson aliwaza mambo mengi sana, alihisi ananyanyaswa, anaonewa.
Akawaza na kuwazua, akapata jibu kuwa njia pekee ya kuepukana na Yale yote ni kutoroka, ulikuwa ni msimu wa kuandaa Mashamba ya mpunga huko mbeya, kwahiyo maeneo ya Madibira, Rujewa ilikuwa ni moja ya sehemu ambazo angeelekea kwakuwa zinasifika kwa upatikanaji wa vibarua.

Aliwaza anatokaje nyumbani na nauli Hana, akapata wazo la kukamata kuku ili akauze apate nauli.
Asubuhi ilifika watu wote wakawa wanajiandaa kwaajili ya kuelekea kanisani, huku Samson akiachwa nyumbani.

Samson alifurahi sana kwakuwa ilikuwa ni opportunity nzuri ya yeye kubeba vitu vyake atoroke, akawaza sehemu rahisi ya kwenda na ni karibu ni Madibira, maana huko pia Kuna ndugu wanaishi huko hivyo akiulizia ulizia anaweza kuwapata, akachukua kibegi Chake akakibana mgongoni huku makwapani akiwa kabana kuku wawili .

Hakutembea sana,akakutana na mnunuzi wa kuku ambaye alikuwa na tenga lake kwenye baiskeli akiokoteza kuku kwa majirani , yule mnunuzi aliwachukua wale kuku kwa bei ya chini Sana labda kwasababu muuzaji alikuwa ni mtoto tena asiye mzoefu wa kuuza.

Sikia dogo Hawa kuku kwanza wanaumwa, na Mimi najua huu msimu wa kilimo wengi wanauza kuku hivyo kama huridhiki na bei niliyokutajia basi. aliongea kwa mbwembwe yule mnunuzi.

Samson kusikia vile hakuwa na ka kufanya kwasababu kwanza hawezi kurudisha kuku, akikuta wazazi wake wamerudi atasema alikuwa anawapeleka wapi, pia bei aliyoambiwa kwa kuku wote nauli ilitosha kumfikisha sehemu husika na chenji inabaki akauza hivyo hivyo kwa hasara.

Akasogea kwenye kituo akakwea gari kuelekea alikopanga.
Huku nyuma mama Mgaya na mabinti zake walirudi toka kanisani ila licha ya kutokumkuta Samson hawakushituka, kwakuwa ni kawaida yake kwenda kucheza mpira au kwenda kuangalia mapigano ya ng'ombe huko malishoni.

Hakuna aliyekundua upungufu wa kuku kwa haraka haraka, naana kila mtu alikuwa busy na Mambo yake, baada ya kazi za hapa na pale Dada yake Sam aitwaye Jane, alihoji.

Jamani wenzangu, hivi kaka Sam mpaka saizi mbona si kawaida?
Maana tayari Giza linaingia.aliuliza Jane

Wee Kaa kimya huyu Leo atanitambua maana sijui Mimi ananichukuliaje huyu bila kuchapwa haelewi Sasa Leo atanitambua. alidakia mzee Mgaya huku akizunguka nyuma ya nyumba yao kuchuma fimbo .

Dakika, Mara masaa yalikatika huku hofu, wasiwasi kwa Kila mmoja ukichukua nafasi yake. Mume wangu ni saa tano kasoro hii mwanangu hajarudi atakuwa wapi? Ni mtoto yule ujue mmmh mwenzangu Mimi hata sielewi. alianza kulalamika mama Mgaya

Atarudi tuu mke wangu, we unadhani awe wapi yule, usikute yupo kwa marafiki zake. alitoa jibu jepesi mzee Mgaya. japo hata yeye tayari alishaingiwa na wasiwasi, maana siyo kwa usiku ule.

Kwa marafiki zake? Marafiki gani, tangu lini mwanangu ukaona kalala kwa mtu?
aliongea kwa ukali na hasira mama Mgaya huku akitoka nje.

Itaendelea....................
 
SEHEMU YA TATU

Samson alifika kwenye barabara ya vumbi akisubiri gari la abiria, ambapo Mara kadhaa alilazimika kurudi mita chache toka usawa wa barabara kutokana na vumbi linalotokana na maroli yanayopita Kila muda.

Wewe mtoto,karibu lisaa tena nakuona hapa umekaa kwani unamsubiri nani?

Aliuliza Babu mmoja aliyekuwa kabeba jembe na panga akionekana katoka kusafisha Mashamba yake.

Hapa Mimi nasubiri gari babu nataka inayoelekea Madibira. alijibu samsoni.

(Akicheka kwa nguvu)
Mjukuu wangu usiku huu wa saa mbili wewe unasubiri gari utaipata wapi, eeeeh

Mimi mwenyewe natembea usiku huu kwasababu natoka kuchoma moto majani kwenye shamba langu, nimefanya hivi kwasababu nilishindwa kuchoma mchana kwa kuhofia usalama, maana moto unaweza kunishinda nikajikuta naunguza mapori.halafu pia mwaka huu kunaonekana kutakua na mvua nyingi............

Samahani mzee wangu , naweza kupata usafiri wowote hata maroli tu. aliongea Samson ambaye alionekana kukerwa na kuchoshwa na stori za babu yule.

Ah hata Mimi sijui ila kwa muda huu sidhani kama unaweza kupata Gari.halafu hapa utoke si salama kuendelea kukaa hapo labda ukakae kule juu karibu na shule.
aliongea kwa kukatisha tamaa yule mzee.

Samson, aliondoka taratibu akipandisha barabara inayoelekea usawa wa shule ya msingi ya kijiji kile, akiwa amekata tamaa huku akiwa anaanza kujuta kwa maamuzi yake ya kutoroka, akawa anawaza muda ule angekuwa kalala nyumbani kwao.

Wakati akiwaza hayo Kuna basi moja lililokuwa linakuja kwa kasi huku ule mwanga wa taa ukimuumiza macho Samson, alianza kupungia mkono, kwa fujo, lakini gari lilimpita likaenda kusimama mbele kama mita mia mbili, baada ya kugundua limesimama akaanza kulikimbilia huku moyo Ukiwa na amani kiasi fulani.

Weee Dogo vipi , unasimamishaje gari kwenye down (mteremko)?
Kwanza unaenda wapi wewe? aliuliza jamaa mmoja aliyeonekana yupo smart kuanzia mavazi Hadi sura yake.

Mimi naelekea Madibira. alijibu haraka haraka Samson.

Yule jamaa alimkubalia Samson kwa kutingisha kichwa.

Samson alipepesa macho huku na huko hakuona abiria yeyote zaidi ya yule aliyekaa karibu naye, na pia kulikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa anaongea sana, pamoja na dereva aliyeonekana kama anafokewa Kila saa.
Jumla wakawa wanne pamoja na Samson kwenye lile bus.

Unajua nini Dogo, Mimi hili gari Wala hata sikupanga kununua wala nini, na Mara kadhaa nimekuwa nikikwambia biashara ya mabasi tuwaachie wenye pesa zao lakini dogo hata hunielewi kabisa yaani. aliongea yule jamaa aliyeonekana ni mmiliki wa lile gari ambalo lilikuwa linaendeshwa na mdogo wake.

Sasa bro Mimi huwa nakushangaa sana yaani kitu kikileta matokeo mazuri huwa huna tatizo lakini kikiharibika lawama unaniangushia Mimi, hayo ni manyanyaso bro Mimi nikwambie tu ukweli, aliongea Kwa masikitiko makubwa yule dereva

Lakini shemu sisi na kaka yako hatukulaumu tatizo ni kwamba madereva uliowapa kazi siyo waaminifu, kama kaka yako kakupa kazi ya kusimamia magari yote manner maana yake kakuamini, Lakini wewe badala ya kuangalia taaluma, unaangalia uswahiba, sijui urafiki . Mambo hayo kwenye kazi hakuna, Routes zote tulizopeleka gari zetu zina abiria was kutosha na tushafanya tathmini muda mrefu tu.

Lakini faida hakuna shemu, unataka tukueleweje sisi, au unafikiri tunapata faida kuuubwa, eeh hapana.
aliongea yule mwanamke ambaye alionekana ana sauti kuliko hata mumewe.

Sasa ndugu yangu nisikufiche naenda kuosha hizi gari zote pamoja na zile zilizotangulia , maana mtaalamu kasema kazi ifanyike ndani ya siku hizi mbili tu kwahiyo kesho utafuata gari la mwisho kwaajili ya kuosha (kuzindika) hivi vyombo maana hali siielewi kabisa,. alisisitiza kaka mtu.

Hapana huyu Mimi simtaki aendelee kusimamia kwenye magari yetu, huyu yeye arudishwe kwenye Mashamba ya mpunga ,maana trekta zishaanza kazi huko. aliongea mke wa jamaa anayeonekana ni mkali sana Hana huruma.

Safari iliendelea huku Samson akiwa anasikiliza mazungumzo Yale ambapo hayakuwa na amani, huku akiwaza usiku ule anaenda kufikia Kwa nani Lakini pia ni mgeni wala haijui hiyo Madibira inafananaje, akajikuta ana mtihani mbele yake.

Baada ya muda Fulani wale watatu waliacha mazungumzo yao wakawa wanaongea kawaida haswa jamaa na mkewe, maana yule dereva alionekana kukasirika Kwa tuhuma anazoangushiwa, kwahiyo akawa anadili na gear tu.

We kijana ujue saizi ni usiku sana kwani unaenda wapi,.
aliuliza yule mwanamke.

Naelekea Madibira, kutafuta kazi.
alijibu Samson.
Na kusababisha watu wote wacheke.

Mmmmh weee usinitanie, kwahiyo kama tusingekuchukua sisi ungesafiri na nini maana usiku huu hakuna usafiri tena, kwanza unaitwa nani?
aliuliza yule mwanamke.

Naitwa Samson Mgaya. alijibu Kwa woga.

Una umri gani, na una tafuta kazi gani? alizidi kuulizwa maswali

Nina miaka kumi na Saba, natafuta kazi yeyote. alijibu Samson.

Una wazazi au mlezi, maana Kwa umri wako mtu anakuachiaje ?
Aliuliza yule mama

Ninao na wapo nyumbani. alijibu Samson.

Mume wangu, Dunia haiishiwi vituko yaani umri wa mtoto huyu Kuna watu wanamruhusu mtoto akatafute kazi, kweli, huyu si mtoto bado huyu . alilaumu yule mwanamke huku mumewe akawa hajamjibu chochote.

Oyaa wewe dogo tushafika hapa Mkunywa, shuka maana sisi tunaelekea nyumbani.
aliongea dereva huku akiwaamsha kaka na shemeji yake , labda Wana maamuzi juu ya yule mtoto.

Sasa mwanangu unasema huijui Madibira, hii ndiyo MD yenyewe na hapa ni Center panaitwa Mkunywa, shuka basi dogo uangalie ustaarabu mwingine, sawa? aliongea yule mwanaume anayeonekana ni mmoja wa wenye hela si haba.

Hivi mume wanguuuu jaribu kuwa na huruma hata kidogo basi, ashakwambia hapajui hapa bado tunamtelekeza jamani? aliongea yule mwanamke.

Sasa unataka kusemaje, kwanza hapa penyewe tumefanya msaada mkubwa , kumleta huku , kumbuka sisi tunatakiwa kurudi nyuma zaidi ni huku pembeni Nyamakuyu, umesahau tulikubaliana Nini mke wangu? Tulisema hata nyumbani hatutakiwi kufika haoa mjini.

Usijifanye una huruma sana, kama wazazi wake wamemruhusu mtoto mwenye umri huu, eti kwenda kutafuta maisha basi wanamwamini, hebu tujaribu kufanya mambo yetu kwanza.
aliongea yule jamaa huku akimuamrisha mdogo wake ageuze gari iangalie ilikotoka tayari kwa safari.

Jamani wenzangu,saa hizi ni saa Saba usiku, Mimi kama mwanamke , ni mzazi, siwezi kukubali huyu mtoto nimuache peke yake, lazima niende naye nyumbani, sikupanga kulala lakini acha nikalale, weee haiwezekani ndugu zanguni, kama wazazi wake walimruhusu, niseme tu kuwa walikosea sana . aliongea yule mama huku akimshika mkono Samson aingie kwenye gari liwapeleke nyumbani kwake.

Dakika tatu ni mbali walifika kwenye nyumba moja nzuri iliyokuwa karibu na mto wenye makelele unaowasaidia wakulima wa pale.

Lakini mke wangu kumbuka alichosema mtaalamu, unajua tunakosea masharti lakini, kumbuka alisema tunatakiwa tufike wote kama tulivyoelekezwa. alilaumu yule jamaa

Wewe huku mwelewa mtaalamu, alisema tufike wote siku ya kazi kwanza bado gari moja ile Canter ya mizigo inabidi shemeji aifuate kesho tuje tuoshe kwa pamoja, hivyo Mimi nitakuja kesho huko. aliongea kwa kujiamini yule mwanamke huku akipokelewa na wasichana wengi wanaokaa pale.

Haya basi si tunaondoka, aliongea mume mtu Kisha akatokomea na gari.

Samson alikaribishwa ndani, akakaa sebuleni huku akishangaa sehemu nzuri kama ile yaani hajawahi kuona akawa anashangaashangaa tu.

Sasa hapa mwanangu tutalala na njaa maana hakuna aliyekuwa na taarifa juu ya ujio wetu hivyo jikaze asubuhi si mbali utakula tu mwanangu, twende nikakuoneshe pakulala,

Samsoni akaoneshwa chumba, kikubwa ambacho alishangaa chumba kile kwanini hakina mtu anayelala huku akiletewa mashuka mawili mazuri yanayonukia huku akijifunika moja na moja akaweka pembeni kwani hakujua kazi yake, kumbe lilikuwa la kutandika.

Usiku ule aliwaza sana, jinsi watu walivyo na roho mbaya,

Sasa pale walitaka kuniacha sijui hata ningelala wapi , na kama huyu mama asingenichukua pengine ningekuwa Niko pale chini ya miembe. aliwaza Huku akijilaumu sana kubwa zaidi huko nyumbani wanawaza Nini hakujua akahisi Kuna LAANA ndani yake.

Usingizi ulimpitia saa ngapi, hakujua ila alishangaa kuona mwanga nje, kupitia vioo vizuri akaamua kutoka nje , akawajuta wasichana watatu wanaoonekana kumzidi wakiwa wanaosha vyombo huku pale nje pakiwa pamepaki matrekta na vifaa vingi vibovu.

Alishangaa kuona jua limetoka kumbe kumekucha muda mrefu sana

Wale wasichana baada ya kumuona Samson waliangaliana Kisha wakacheka sana, tena sana .

Samson hakujua wanacheka Nini,alitamani awaulize yule mama wa Jana yuko wapi, lakini aibu za shamba zilimtawala.
Njaa nayo haikuwa nyuma, tumbo lilidai chochote kitu, lakini hakuwa na jinsi , hela alikuwa nayo lakini wapi akanunue walau mkate , hakujua.

Saa tatu..... saa nne...... hadi saa Saba njaa ilimtafuna sawasawa Samson. alitoka nje ya kile chumba kuelekea sebule ilipo akawakuta wale wasichana wanakula Chakula ambacho nacho kilikuwa mwishoni, alimezea mate ile harufu ya wali lakini hakukaribishwa badala yake wale wasichana walicheka kila wanapomwangalia huku wakiwa hawamsemeshi jambo lolote.

Samson kijana mwembamba aliyekosa mwili Wala huwezi kudhania kama ana miaka kumi na Saba, alianza kumkumbuka mana yake mama Mgaya , ni Samson ambaye hata akilala huamshwa ili ale, lakini siku Ile ilikuwa historia kwake.

Mama aliyemleta Jana , hakujua kaenda wapi, nani amuulize hakujua maana watu hata hawaoneshi ushirikiano.

Alirudi kule chumbani akaanza kulia,
Akijua kabisa ulimwengu unamfunza.

Itaendelea.............................
 
shukran mkuu
 
SEHEMU YA NNE

Asubuhi na mapema kulikucha, ratiba za kazi zilivunjika kwa mzee Mgaya, huku akitengeneza baiskeli yake, tayari kwenda kutoa taarifa juu ya kupotea kwa mwanaye.

Kuhusu mama yake Samson au mama Mgaya yeye alikuwa haongei chochote hali iliyopelekea watu wakawa makini naye maana ukimya wake hawakuuelewa, si dada zake wote walinyongea, walinyeshewa Kila mtu sura ilikuwa ya huzuni, fimbo ambayo mzee Mgaya aliichuma kwaajili ya kuja kumuadhibu, aliichukua akaivunja vunja huku akiwa kasawajika sana usoni.

Jua lilizidi kutoka lakini hakuna aliyehisi njaa, mama Samson alipita kwa majirani wote na marafiki wa Samson akiulizia mwanaye lakini hakupata majibu sahihi, Kila mtu alitoa jibu lake huku wengine wakitoa majibu ya uongo kwaajili ya kuomba rushwa ya pesa.

Mama Samson alirudi nyumbani mida ya saa nane mchana huku akiwa kaishiwa nguvu kabisa.

Mama, mama, mama yangu pole sana, tunakuomba ule Chakula mama, tumejaribu kupeleleza kwa baadhi ya marafiki wa kaka Sam tumeambiwa kaenda mjini kwa mjomba, hivyo usijali mama kaka Sam yupo salama kabisa.
Alisisitiza Jane bint Mgaya akimtaka mama yake ale,

Si kweli kwamba waliambiwa Samson kaenda kwa mjomba wao hapana bali ilikuwa mbinu ya kumtaka ale chakula.

Lakini si mama Mgaya, alielewa mbinu za wanae akawaangalia huku akitoa kicheko cha masikitiko.kwa kuwaona wanahangaika bure

Mzee Mgaya aliingia huku akiwa na majirani kadhaa, wakimfariji na kuahidi kutoa ushirikiano juu ya upotevu wa Samson
Wageni walikaribishwa ndani huku wale wenye asili ya ulevi wakijifanya wanajua alipo lengo wapate vijisenti wakalewe pombe ya kienyeji ya mahindi almaarufu "komoni".

Turudi alikofikia Samson

Kijana alilia, akalia na kulia huku, akikosa tumaini kabisa juu ya hatima ya maisha yake kwa siku hiyo,
Muda kama saa tisa alasiri, Samson alisikia sauti ya yule mama wa Jana ikimuita akakurupuka huku akisahau hata viatu vyake labda ni kwasababu ni sauti ya mtu anayemtegemea

Alifika pale akamuamkia yule mama ambaye mchana ule alikuwa anamuonya vyema, si Samson si yule mama Kila mmoja alimtambua mwenzake vizuri.

Pole sana mwanangu nasikia hujakula, chochote ngoja tule maana hata Mimi Nina njaa sana, aliongea yule mama ambaye alikuwa anampakulia Samson Chakula huku samson mwenyewe akishindwa kujua kwani kimepikwa saa ngapi.

Taratibu wakaanza kula huku yule mama akimsisitiza Samson asione aibu ale atakavyo,
Na Samson akawa anapiga ipasavyo.

Uliniambia unaitwa nani vile mwanangu?

Naitwa Samson mama. alijibu

Sawa, kazi gani wewe unaiweza vizuri unahisi hiyo ukipewa haikusumbui?

Kazi yoyote kulima, kuchota maji hata kuchunga ng'ombe Mimi naweza, alijibu Samson.

Hahaha, we mtoto usinichekeshe bwana, mbona mwili wako na hizo kazi tofauti sana. Shule umemaliza mwaka gani? aliuliza

Nimemaliza mwaka huu. Alijibu Samson.

Sawa, ila kwa umri wako Mimi ningeshauri kama wazazi Wana uwezo wangekupeleka Sekondari maana Elimu ndiyo msingi wenyewe, kwasasa hata mheshimiwa Rais wetu wa Sasa Mkapa anasisitiza hilo kuliko kuchagua hizo kazi unazitaka, kazi zipo utazikuta baadaye ukiwa na Elimu yako.

Baada ya kumaliza kula waliendelea na stori za hapa na pale huku Samson akizidi kuwa mjanja zaidi maana aligundua kama akiwa lazy lazy atapitwa na vingi.

Kwani mama Hawa kina dada ni wanao? aliuliza Samson

Ni swali ambalo yule mama hakulitarajia ila alijibu Samson kwa upana zaidi.

Sawa, kwanza Mimi naitwa Mrs Shayo, yule uliyekaa naye siti moja kwenye gari ni mume wangu, na ndiye Shayo mwenyewe na yule aliyekuwa anaendesha gari ni shemeji yangu, yaani mdogo wake mume wangu.

Ila sisi siyo wakazi wa hapa, tunaishi Iringa mjini, na hata watoto wetu wanaishi huko huko, Hawa unaowaona ni wafanyakazi wangu wapo wengi sana, na siyo Hawa tu wapo na wanaume wengi ambao wao wapo Kambi yaani wameshika kazi ya msimu mzima huko mashambani. aliweka kituo

Kwahiyo hapa siyo kwako. Aliuliza Samson

Kwanini unauliza hivyo Sam.

Umesema unaishi Iringa na familia yako nzima ipo huko, Sasa hapa ni Kwa nani Tena, aliuliza lile swali la kipumbavu Samson.

Yule mama alimwangalia Samson kitambo kidogo, akachanganya na zake akigundua ni mtoto wa kijijini au yule asiyejichanganya sana na watu, akamjibu

Hii ni nyumba yetu tuliinunua kwaajili ya kufikia pindi tukiendesha kazi za shamba, hata hivyo Leo nilijihimu kwenda huko ndiyo maana hukuniona nilienda kuangalia mipango inaendaje huko.
aliongea yule mama huku akitambua anazungumza na mtu wa aina gani.

Sasa kesho inabidi uende kazini kule shamba kazi yako itakuwa ni kuwapikia vijana na wafanyakazi wa kule maana , wamelalamika kuhusu kubanwa na kazi hali inayopelekea wanakula muda umeenda mno. aliongea yule mama.

Samson kusikia kapata kazi kwanza alifurahi sana, maana hitaji lake lilikuwa kazi na kazi akawa kapata.

Sasa mama kwani hatuwezi kwenda Leo ili kesho niamkie kazini ? aliuliza kwa pupa Samson.

Hapana we tulia kwanza kesho nitakupeleka nikakukabidhi huko Leo pumzika tu, lakini unaweza kupika Chakula gani na Chakula gani.?

Naweza sana ugali, wali siwezi. alisema ukweli Samson.

Sawa, lakini kumbuka kule unaenda kupika Chakula Cha wanaume zaidi ya nane kwahiyo jitahidi mwanangu sawa , maana nayajua mazingira yao, ila kwakuwa naenda na Mimi nitawaambia kabisa kuwa muwe mnasaidiana.aliweka kituo.

Samson alifurahi sana , maana alishashiba , alishapata uhakika wa kazi kwahiyo akawa kasahau kuwa kafikaje hapo, hakujua ni dhahma gani kaacha nyumbani, yeye alifurahi na yake.

Saa nne kamili walikuwa shamba huku Mama Betty kama wanavyomwita wale wafanyakazi,
Akiitisha kikao kidogo Cha dharula.

Jamani kwanza poleni sana na kazi, lakini niwapongeze si mbaya kazi inaenda vizuri kabisa,

Ila sijapenda tabia ya kuwasha moto kwa Diesel, jamani Jana kwa macho yangu mtu anamimina karibu Lita nzima kwaajili ya kuwasha moto kweli ndugu zanguni, ni haki kweli hiyo, sijapenda na hata Mr (mume wake) akisikia hili sidhani kama atakubaliana nalo.

Hayo tuache kuna malalamiko juu ya kula , yaani watu wanakula muda umeenda, niseme kilio chenu nimekisikia na tayari nimekuja na kijana ambaye huyu hatafanya kazi yeyote ile badala yake kazi yake itakuwa ni kupika tu, atalipwa kwa kazi hii sawa jamaniii? akiuliza

Wote walionekana kumuunga mkono huku wakifurahi maana wengine ile adha ya kupeana zamu kupika walikuwa hawapendi hivyo wakaona huu ni mteremko.

Hebu wasalimie wenzio humu wengine ni kaka zako, wengine ni kama baba zako kabisa sawa?

Samson aliwasalimia huku, akijichangamsha asikae kiunyonge.

Baada ya kumaliza utambulisho ule kundi la watu kama kumi Kila mtu akaendelea na majukumu yake huku yule mama akiingia kwenye land Rover yake na kurudi Madibira.

Samson akaanza kuwasha moto huku akiangalia ule uwingi wa watu kijasho kikimtoka maana hana uzoefu wa kupika ugali wa watu wengi, alitenga msufuria ambao unaonekana huwa hata hauoshwi
Vizuri akaanza makeke yake, lakini kabla hata ugali haujaiva alishangaa watu wamesharudi huku wengine wakimuhimiza aharakishe kwakuwa wananjaa walimkera sana lakini hakuwa na la kufanya,

Kejeli, matusi ya nguoni ilikuwa ndiyo lugha inayotumika kule huku samsoni akishangaa watu kutukana namna ile bila woga

Oyaa we kicheche malaya, huo ugali haujaiva tu bado,na ole wako utupikie ugali mlaini kama tupo hospital , tunataka ugali mgumu sawa wewe dogo.

Watu wakawa wanamsimamia Tena akiwa anapikia juani, jua la utosi lilimpata sawa sawa , jumlisha moto wa jikoni jumlisha maneno na dharau za majamaa, Masaa matatu aliyaona kama mwaka.

Alikosa kujiamini, alikosa nguvu, aliingiwa na woga, akajikuta Hana la kufanya,

Kuna jamaa mmoja alikuwa pembeni haongei ila aliona namna Dogo alivyoelemewa akaamua kumsaidia,

Oyaa wee Masoud eeh mbona unaleta huruma za kijinga?au hujui huyo analipwa kwa kazi hiyo umesahau boss kasemaje , hebu toka hapo we mwehu.

Walimrushia matusi mwenzao lakini Wala hakujali,

Muwe na huruma jamani Huyu bado ni mtoto Wala hii kazi hajaizoea tumsaidie, aliongea yule masoud huku akimpa moyo Samson kuwa avumilie tu Yale ndiyo maneno yao.

Samson alionesha unyonge na hofu kubwa.

Milango ya mafanikio, simulizi mpya,

Enjoy yourself

Itaendelea...............
 
SEHEMU YA KWANZA.(utangulizi)

Sam, saam , samsoniii, huko unakoenda hakikisha unakula huko huko, maana huwezi kunisumbua kila siku , kwanini husikii weee mtoto Sasa nikwambie tu kuwa leo hakuna kula hapa nyumbani. nakwambia rudi sam, rudiii au unataka nimwambie baba yako akija, umesahau alichokufanyia Mara ya mwisho
Wewe, weeeeeeeeeh.

Yalikuwa ni maneno ya mke wa mzee
Mgaya, au mama yake na Samson, akimtaka mwanaye arudi ili aendelee na kazi za pale nyumbani kwao kuliko kwenda kuchunga ng'ombe wa watu tu, wakati wao hawana hata ng'ombe mmoja.

Lakini maneno yale wala hayakuweza kusaidia chochote maana Samson alizidi kutokomea porini akifuata kundi kubwa la ng'ombe kutoka kaya tofauti tofauti.huku jambo pekee lililo kuwa linampeleka Samson kule ni sinema za bure, yaani ng'ombe wanapopigana.

Iko hivi , tukiacha wafugaji wakubwa kama wamasai,wamang'ati na wasukuma, wapo baadhi ya makabila wengi wanafuga ng'ombe, mbuzi, kondoo na hata kuku, ni kawaida tu kukuta karibu Kila kaya Ina mifugo, utakuta hapa Kuna ng'ombe ishirini, hapa kumi na tano sehemu nyingine hata ng'ombe zaidi ya hamsini.

Lakini pia wapo watu wanaoazima ng'ombe wa mtu kwa lengo la kujipatia mbolea(samadi) kwaajili ya kukuzia mazao mbalimbali,
Yaani mtu unakaa na ng'ombe zaidi ya ishirini wa mtu lengo ni maziwa na mbolea, japo hata hayo maziwa huwa siyo mengi kutokana na aina ya ufugaji, kwani si wa kisasa.

Basi wakati mifugo kama ng'ombe wanakutana malishoni(nyikani) huwa Kuna kutambiana kwa madume au mafahali kutoka vikundi tofauti tofauti huku kukiwa na wale mafahali wanaojulikana kabisa kuwa ni unbeaten yaani wanatisha kwa kupigana.

Ni mchezo mzuri na watoto wengi wa vijijini huwa wanaenjoy sana kuangalia mapambano ambayo kwa kweli huwa yanaburudisha japo ni hatari maana huwa Kuna ng'ombe wenye hasira pale anapopigwa au anaposhinda hivyo ule ushindi wake humfanya aone anamudu Kila kiumbe.

Wenye mchezo wao Wala huwa hawapati taabu yaani wakiona mpambano ushaanza wanapanda juu ya miti huku wakienjoy game Bila wasiwasi, huku yule mwenye ng'ombe aliyeshinda akiheshimika kana kwamba kapigana yeye na Kuna wakati mnamaindiana kiasi Cha kuzichapa wenyewe.

Ni mchezo mzuri sana hasa ukiwakutanisha mafahali wale ving'ang'anizi inachukua muda wa lisaa au masaa mawili huku wafuatiliaji wakichukua points ni fahali yupi anajua vichwa na yupi anajua kutumia pembe zake vizuri, hakika ni mchezo unaovutia watoto wa vijijini, lakini pia hata sare hutokea. Kivipi?

Ni pale ng'ombe wanapochoka na kubaki wanaangaliana na Lila mmoja kushika njia yake wakiendelea kula majani, au ni pale waangaliaji wanapochoka yaani burudani inatosha, mshindi hapatikani , au Giza linaingia wanaachanishwa huku mkipanga namna ya kukutana siku nyingine.

Ni mchezo mzuri sana, wakati waliozaliwa mjini wakiinjoi mapambano ya akina Evander na akina Tyson, M. Alli watoto wa kijijini Wana namna yao ya kufurahi.

Samsoni ni mtoto pekee wa kiume kwenye familia ya watoto wanne wa mama mgaya huku yeye akiwa watatu kuzaliwa, huku kwa baba yake wakiwa ni wengi maana mzee mgaya alikuwa na wake wawili.

Miaka ya 1996 alianza darasa la kwanza kijijini kwao akiwa na umri wa miaka kumi, umri ule haukuwa kikwazo sana maana Elimu ilipewa kipaumbele sana hasa maeneo ya vijijini huku sera ile ikichagizwa na serikali mpya ya hayati B. W. Mkapa.

Hivyo watendaji na wenyeviti walihimiza watoto wote waanze darasa la kwanza huku wengine wakiwa na umri mkubwa zaidi ya Samsoni, basi samsoni alijitahidi sana kusoma kwa mbinde na uvumilivu wa hali ya juu kwani changamoto kubwa ilikuwa ni umbali kutoka huko mashambani anakoishi Hadi kijijini ilipo shule yao.

Alijitahidi Hadi pale alipohitimu shule ya msingi akiwa na umri wa miaka kumi na Saba, alimaliza na umri huo ni baada ya kufeli darasa la nne akalazimika kurudia darasa.basi baada ya kumaliza Elimu ya msingi hakukuwa na matarajio yoyote kwa labda ataenda Sekondari, si wazazi wake Wala si yeye mwenyewe ambaye aliwaza hatima ya aendelee shule ya upili au awe na mishe zingine.

Miaka kumi na Saba kwa mtoto ambaye kakulia kijijini huwa haha mature bado tofauti na aliyekulia mjini, basi balehe ilimfanya Samsoni awe mbishi, kiburi, jeuri na asiyependa kazi za pale nyumbani kwao, badala yake ni kwenda kucheza mpira wa makaratasi, au kwenda kuangalia mapigano ya ng'ombe huko malishoni.

Kwakuwa baba yake alikuwa na nyumba mbili {wake wawili}basi mama Mgaya alijikuta anapata kazi kubwa ya kuhandle kijana wake ambaye alikuwa akimgomea kazi nyingi ikiwemo kutokujijali yeye mwenyewe, maana hata kuoga yaani usafi unaohusu mwili wake samsoni ilikuwa Hadi akumbushwe vinginevyo na baridi la mkoani inaweza kupita siku kibao hajaoga.

Basi siku moja baba yake Samson mzee Mgaya alirudi nyumbani akitokea kwa mke mdogo, alifika pale huku akiegesha baiskeli yake aina ya Avon ukutani, huku akisikia makelele ndani yaliyoashiria hakukuwa na amani. Sauti alizitambua ni Samson na mama yake.

Vipi jamani Kuna Nini? Enhhhee mama Jane Kuna Nini na mwanao?
Aliuliza mzee mgaya. (Huku akimdaka Samson ambaye alitaka kupenya pale mlangoni akimbie)

Kaa chini wewe. aliamrisha Mzee Mgaya.

Afadhali umekuja, Tena ni kama MUNGU kakuleta Mimi nimechoka baba nimechoka, hebu muangalie mwanao, mtazame mavazi na nguo zake, haogi, hafui hapo alipo ukiingia ndani kwake hakutamani , Wala huwezi amini kama analala binadamu. Naomba nisaidie mwanao anatia aibu, nasema Bora hata alivyokuwa shule kuliko anavyoshinda hapa maana anazidi kuniongezea mawazo nashindwa kujua kwani nilimzaa mtoto wa aina gani.

Alilalamika mama Mgaya huku akizidi kumpalia makaa Samson, maana alijua fika tabia ya mzee Mgaya, akianza kupiga mtoto haangalii wapi anachapa.
Inajulikana kuwa samsoni hasikii vizuri kutokana na Kofi alilowahi kupigwa na baba yake kwa tuhuma za kusababisha pancha kwenye baiskeli yake.

Kitendo hiki kilimuuma mama Mgaya kwamba kwanini ampige mtoto mdogo kama anapigana na mtu mzima, na kupelekea mtoto akawa hasikii vizuri.

Lakini siku hiyo Wala hakujali aliamua liwalo na liwe maana samsoni alizidi ukorofi.

Mzee Mgaya alivuta kiti akakaa, akamsogeza Samson karibu na alipokaa akamwangalia kama sekunde kadhaa hivi bila kusema chochote Kisha akajiinamia chini huku akicheka kwa kumuhurumia Samson.

Itaendelea......................
kmbe kuna kitu uku jmn na wala hamsemi sijapenda
 
SEHEMU YA TANO

Siku ya tatu baada ya kupotea kwa Samson, kulikuwa na kikao kifupi majira ya saa saa mchana. ilikuwani namna ya kujadili ni hatua zipi zichukuliwe ikiwemo kwenda kuripoti kituo Cha polisi ambacho kipo mbali sana yaani kinapatikana wilayani.

Ni kama kilomita hamsini toka kwenye Kijiji cha akina samsoni hivyo ilitakiwa wajitolee watu kama watatu waende kuripoti.

Majonzi na hali ya huzuni ilitawala kuanzia kwa wazazi wenyewe hata kwa majirani, lakini pia hata mke mwenza wa mama mgaya naye alihuzunika kupotea kwa mtoto wa mke mwenzake, japokuwa huwa haelewani sana, lakini kwa siku hiyo lilikuwa tukio la kusikitisha kwa kila binadamu mwenye moyo wa huruma.

Maagizo toka kwa katibu wa Kijiji kama walivyokuwa wanaitwa kipindi kile, yaliamua hatma ya hatua zipi zichukuliwe. Watu walitawanyika huku Kila mmoja akiahidi kutoa ushirikiano kwa hali na mali lakini pia wapo ambao walienda mbali zaidi wakiwaza labda Samson kafichwa na wachawi kama ambavyo huwa inatokea mtu kujikuta kapotea kimazingara , wakaanza kushushiana tuhuma wao kwa wao , hali iliyozua tafrani huku mwenyekiti na katibu wake, wakionya watu waache mawazo yale mabaya kwani ni kuchochea upotevu wa amani.

Badala yake wakaripoti kwenye jeshi la polisi, kwa kupata msaada zaidi.

Hapana, Mimi sikubali na sitakubali , kwanza Mzee Mgaya umezidi upole mno, hebu fikiria , umegundua Nini juu ya yule bibi wa kule karibu na mtoni,? aliuliza kijana mmoja jobless anayeamini sana ushirikina.

Aaah kwa kweli kijana Mimi sijagundua jambo lolote kwani vipi?
alihoji Mzee Mgaya.

Yule bibi kwanza ni mchawi kufuru, ni mchawi aliyekosa aibu, watu wengi wamekuwa wakimtuhumu kwa kugeuza watu misukule kimazingara hivyo Mimi akili ya kupotea kwa dogo Wala haiji yule yupo kuleeeee,.bibi ana roho mbaya sana yule,mtu gani hakai hata na mjukuu, aliongea kijana yule huku akioneshea Ile nyumba kuu kuu kwa kidole.

Ila kweli, kwanza hata hapa kwenye kikao hajaja, yaani ni yeye pekee, hajashiriki mmmmh mbona kama naanza kuamini amini.hapa Kuna namna inabidi akili zetu zifanye kazi mtatupa nauli bure kwenda sijui polisi sijui wapi lakini bado sidhani kama mtafanikiwa hebu ndugu zanguni jaribu kusikiliza maoni ya watu ohoooooh. aliongeza mwanamke mmoja akizidi kupigilia msumari kwamba yule bibi huenda anahusika juu ya upotevu wa Samson.

Watu wote walitawanyika, ikabaki familia husika.

Mke wangu, mama Jane, kwanza naomba upunguze unyonge, nafikiri ni muda wa wewe kuamua Moja tuungane tumtafute mtoto wetu na siyo kulia kila saa haisaidii Wala hutapata muafaka wowote. alishauri mzee Mgaya.

Sawa mume wangu , ila tunafanyaje kuhusu nauli maana kumbuka hata wale watakao tusindikiza uko bado watategemea nauli zetu kuwapeleka na kuwarudisha kwahiyo nikiangalia akiba hapa bado hata haitoshi kwa watu watatu , tunafanyaje mume wangu? aliuliza mama Mgaya.

Kuku si wapo tutakamata kuku kadhaa, tuuze tupate kuongezea panapopungua. alishauri mzee Mgaya

Hodi, hodiii humu ndani,
sauti ya mzee mwanamke ilibisha hodi,

Karibu sana bibi, karibu.
Alikaribisha Jane huku akikunjua mkeka fulani na kumkaribisha yule bibi, ni yule aliyetoka kutuhumiwa na majirani muda si mrefu kuwa ni mchawi wa kutupwa na hata upotevu wa Samson huwenda ana husika Moja kwa Moja.
Jambo zuri ni kuwa familia ya mzee Mgaya kuanzia wazazi hata watoto wao hawakuamini sana zile tuhuma zinazomhusu yule bibi hivyo walimkaribisha kwa moyo wa upendo tu.mzee Mgaya na mkewe wakatoka chumbani walikokuwa wanajadili mambo yao kuja
Kumsikiliza yule bibi.

Ohoooh Bi.Maria, habari za siku jamani, mbona unapotea sana, ni takribani wiki ya tatu Sasa hatujaonana bi, Maria. aliongea kwa kujichangamsha mzee Mgaya.

Jamani mwenzenu naumwa, yaani miguu inaniuma sana, hivyo muda mwingi nakuwa nimelala tu na hata hivi majuzi nilijikaza nikaenda huko Parokiani nikaonane na sista mmoja wa kizungu ambaye aliniahidi atanipa dawa, nashukuru MUNGU dawa zinanisaidia kwa kweli naendelea vizuri japo miguu bado inasumbua yaani haiumi ila imevimba tu.
aliongea bi Maria huku akionesha miguu iliyoonesha kujaa jaa.

Ndugu zangu kwanza poleni na hili nalosikia la kupotelewa na mtoto wenu, maana nilikuwa nje nafua nguo zangu ndipo akapita jirani mmoja alinilaumu kwanini sijaja kwenye kikao Ina maana sijui juu ya upotevu wa mtoto kwenye Kijiji chetu, nimemshangaa akinilaum wakati Mimi hizo taarifa Sina. aliongea Kwa masikitiko Bibi Maria kama wanavyomwita.

Kwanza Mimi sidhani kama unasitahili lawama,na hata sisi kweli tumeghafirika kutokana na kuvurugwa juu ya upotevu wa mtoto wetu ikawa ngumu kumtaarifu mtu mmoja mmoja. lakini achana nao hao vijana ni walevi tu nisamehe Mimi mzee wangu. aliongea Mzee Mgaya kwa huzuni huku akilaumu wale vijana wanaoenda kuparamia wazee wa watu kwa tuhuma zisizo na ushahidi.

Sawa, ila poleni sana kwa tatizo lenu, lakini niwe mkweli siku ya jumapili nikiwa natoka mission kwa yule sista kuchukua dawa mida ya saa kumi na Moja nilimuona mtoto wenu akiwa kakuambatia kuku wawili akiwa anatembea haraka haraka akielekea Kijiji cha jirani (akitaja jina la kijiji)
mimi nilijua labda mmemtuma mahali , lakini baada ya kusikia muda mfupi kuwa kapotea nikaona nije nipate taarifa zaidi. aliweka kituo yule bibi.

Kengele za hatari ziligonga kichwani kwa mzee Mgaya, akatoka nje haraka huku akiomba aletewe punje za mahindi, akaanza kupiga mluzi aliowazoesha kuku wake kuwaita, baada ya kuwarushiarushia mahindi wale kuku , mabinti zake ambao muda wote walibaini kutokuwepo kwa majogoo wadogo wawili,.

Baba wale jogoo wawili wekundu hawaonekani kwenye kundi, ndipo walipojiridhisha juu ya upotevu wa kuku wakaanza kuunganisha matukio.

**************************
Turudi kwa samsoni.

Watu wote walianza kula ule ugali huku Samson akiwa hajazoea kukaa na wahuni, basi maneno ya shombo yalimtia hasira sana, akawa hata hamu ya kula hana.

Kwahiyo we dogo ndiyo unasusa kula, susa susaaaaa ndugu yangu, Mimi ninachojua utakula mwenyewe . aliropoka jamaa mmoja.

Huku wakila kwa pupa ule ugali na dagaa wenye mchanga mwingi lakini wala majamaa hawakujali, baada ya kumaliza Kila mtu alirejea kwenye kazi yake huku wakimuamrisha Samson atenge maharage kwaajili ya jioni,

Samson hakuweza kuzoea ile hali muda mwingi alijikaza huku akijizuia asilie akachukua sufuria kubwa akaweka maharage kwa kipimo alichoambiwa, akabandika jikoni huku akikaa pembeni akiwaza na kuwazua.

Mida ya saa kumi na Moja majamaa walianza kurudi,huku Kila mtu akioga kwa namna yake, wapo waliochukua zile ndoo za Chuma wakiogea wapo waliooga walikotoka, lakini kubwa zaidi Samson alishangaa jibaba jitu Zima likivua nguo mbele yake bila aibu likijirusha mferejini huku likijipakaza sabuni uchi wa mnyama , hali ile kulingana na mazingira aliyokulia Samson lilikuwa jambo la kustaajabisha.

Oyaaa Jay eeh, tabia gani ya kuvua nguo mbele ya mtoto, hivi huoni kama unajidhalilisha ndugu yangu?
alilaumu jamaa aitwaye Masoud aliyeonekana mstaarabu kuliko watu wote kwenye ile kambi.

Na wewe Ostaz Nini bwana, mtoto, mtoto, Mimi nina watoto hapa, huyo angekuwa mtoto angekuja huku we vipi bwana, aliongea yule Jay huku akiwa kapakaa sabuni kuanzia usoni Hadi unyayoni lakini hata wanawake waliokuwa wanapita kwenye ile njia Wala hawakustuka Wala kujali , inaonekana walishazoea.

Baadaye watu wote waliondoka kwenda kuzurura kwenye pombe na mademu kama ilivyo kawaida watu wa makambini.
Pale walibaki watu wawili tu, Samson na Masoud.

Baadaye Samson aliingia ndani, akamkuta Yule masod yupo bize akiwa anaswali, japo Samson hakujua mtu yule anafanya nini maana licha ya kumuongelesha, hakujibiwa akatoka nje.

Baadaye Masoud alitoka nje ya lile banda,.

Kwani we anko ulikuwa unafanya nini maana nimekuita hukunijibu? aliuliza Samson

Kwanza yule jamaa akacheka sana Kisha , akamuuliza Samson.

Wewe ni Dini gani, mwanangu?

Mimi ni Dini yangu ni mroma, alijibu Samson.

Hapana, sema hivi Mimi ni mkiristo na dhehebu langu ni Roman Catholic. alimsahihisha . Ikabidi wacheke wote maana Samson mwenyewe kweli alijua kakosea.

Na Mimi nilikuwa naswali, na Mara nyingi ukinikuta kwenye hali ile usiniongeleshe sawa. alimuonya Samson huku wakiendelea kupiga stori za hapa na pale

Sasa mwanangu, hapa ugali tusipike mwingi maana navyojua wale majamaa watarudi wamelewa hakuna mlaji hapa hivyo punguza hayo maji.

Masoud ni jamaa mmoja muislamu na mchamungu ambaye anamuonea huruma Samson kwani ni rika la wanaye aliowaacha huko mkoani Pwani alikozaliwa hivyo anamuona kama mwanaye.

Samson naye anagundua Kambi nzima wote Wana akili zinazofanana , mtu pekee aliyemuona ana busara ni Masoud anamchukulia kama baba yake. waliendelea kupiga stori huku
yule jamaa akisonga ugali.

Kwani wewe unafanya kazi gani kwa hapa? Maana nilikuona umelala tu? aliuliza Samson

Ok, sawa Mimi ni dereva wa trekta hili hapa ila limeharibika.
Mazungumzo yao yalikatishwa na gari ndogo iliyopark pale usiku ule wa saa mbili usiku. huku Masoud mwenyewe akishangaa.

Itaendelea......................
 
SEHEMU YA SITA

Wakati Masoud na Samson wakiendelea, kuishangaa ile gari ndogo ambayo ilikuwa na mwanga hafifu, hatimaye walishuka wanaume wawili huku mmoja akionekana mzee sana, kwani sura yake na hata nywele zake ziliakisi vile.

Pia mwingine alikuwa kijana wa makamo mkakamavu anayeonekana mtu wa mazoezi akiwa kavaa kapelo iliyofunika macho yake hali iliyopelekea asionekane sawa sawa,.

Habari za hapa ndugu zetu,
Walisalimia Mara tu baada ya kushuka kwenye gari.

Ni salama tu, karibuni.
Alijibu Masoud huku akionesha wasiwasi fulani kuhusu ujio wa watu wake kwani kule mashambani huwa si rahisi kuonekana kwa gari ndogo, hasa nyakati za usiku.

Ahsante sana, naitwa Ray naishi Mbeya mjini, alijitambulisha yule ambaye ni kijana zaidi.

Naitwa Komba, au watu wengi wananiita Babu K. alijibu yule mzee huku akiwa anatafunatafuna vitu tangu afike pale.

Samahani sana jamani sisi tunatokea Mbeya tunamtafuta kijana mmoja ambaye ni mjukuu wangu, alitoroka nyumbani tangu mwezi uliopita , na kwa upelelezi wetu, tumegundua yupo Madibira hii, Sasa kwa muda wa wiki moja Sasa tupo pale Mkunywa tukiwa tunafanya upelelezi juu ya wapi alipo mtoto wetu .

Na tumeambiwa yupo Kambi hii ndiyo maana tukatoka kule kijijini kuja huku mashambani, hivyo tungeomba ushirikiano wenu.
Aliongea yule mzee Komba kwa kuamrisha akionesha ana Imani moja kwa moja kwamba mjukuu wake yuko pale.

Sawa mzee wangu, anaitwa nani huyo mjukuu wako, na pia una vielelezo vyovyote toka polisi au hata serikali za mitaa, na hata picha yake labda ? aliuliza Masoud huku akiwaangalia kwa makini.

Wale jamaa waliangaliana huku wakionesha wamekerwa na maswali ya Masoud.

Kwahiyo hakuna kijana yeyote mgeni kwenye Kambi hii?
aliuliza kwa ukali kidogo yule jamaa mwingine aliyejitambulisha kuwa ni Ray.

Kaka nishasema leteni vielelezo, vya kumtafuta huyo mtu, na kwanza hapa hakuna kijana mgeni wote tunajuana hapa kambini, alijibu Masoud huku kengele za hatari ziligonga kichwani mwake akijua Hawa watu si wazuri.

Masikini Samson hakujua lolote linaloendelea , aliendelea kuchochea vinavyopikwa huku akijiona hahusiki na yanayoendelea pale.

Sauti za walevi zilisikika kwa mbali huku wengine wakitukana, wengine wakiimba wengine wakirushiana matusi ya nguoni baina ya vibarua wenzao wanaoishi kwenye makambi mengine, waliendelea kukaribia zaidi kwenye kambi yao hatimaye wakafika kabisa.

Heeeeh vipi bro Masoud,
Au Masoud jah mwenyewe, vipi dogo kashasababisha , tumeambiwa na boss kuwa huyu ndiyo kila kitu kwahiyo tunaamini msosi tayari, aliropoka jamaa mmoja.

Waliendelea kumzomea zomea Samson huku wakiwa tungi sana. Na hili liliwafanya wale wageni watambue kuwa pale Kuna kijana mgeni.

Wakati tayari Chakula kile local kilipakuliwa huku watu wakila kwa fujo yaani bila utaratibu maalum kwani Chakula hakikuheshimiwa maana huyu kachuchumaa , huyu kasimama huyu kapakua sahani yake kashikilia mkononi ili mradi fujo tupu yaani.

Wale majamaa walikuwa wanateta kidogo pembeni baadaye wakamuaga Masoud wakaondoka kwa kasi sana.

Hakuna mtu aliyewashitukia wale wageni maana wote walikuwa na pombe kichwani, lakini Masoud pekee alitambua kuwa wale watu si wazuri.

Kwanini? ni kwasababu,
Hawakuwa na vielelezo

Muda wa kulala Kila mtu alitafuta sehemu yake, na kulala lakini Masoud aliendelea kukaa tu pale nje huku akiwaza na kuwazua, akili ilikuwa imevurugika huku akijiuliza, wale wamejuaje kama hapa Kuna kijana mgeni?

Na wanamtafuta wanini?

Lakini hata hivyo siwezi kujisumbua kumuwazia huyu kijana wa nini?

Mimi mwenyewe nina familia yangu na majukumu kibao sidhani kama ni sahihi kuendelea kujitwisha mizigo na matatizo yasiyonihusu, kama umri kama huu wazazi wake wamemruhusu aje huku? Potelea mbali.

Alitafuta sehemu yake ya kulala akiegesha tu , japo alilazimisha kupata usingizi Mara kadhaa lakini hakupata hata lepe la usingizi,. Akili yake ilimwambia dogo lazima atatekwa, Kila akijilazimisha kutokukubali ile hali, lakini kengele zilikuwa zinamwambia wale jamaa lazima watarudi kwa Mara nyingine ili wamchukue Samson.

MUNGU ni mwema alilowaza Masoud, ndilo walilowaza majamaa , alitamani awaambie wafanyakazi wenzie juu ya mashaka aliyonayo lakini akaona hakuna mwenye akili ya kuweza kujali maisha ya mtu. akaamua kupiga kimya .

Alichukua tochi yake ya betri mbili kubwa ya kizamani akaanza kumulika mulika, kila Kona ya lile banda akaona Kila mtu kalala fofofo huku Samson akiwa mwisho kabisa tena chini kwani hakuwa kajifunika shuka, na pia alisukumizwa na jamaa mmoja na kujikuta kalala chini, lakini bado alikuwa kalala fofofo.
Ama kweli usingizi ni nusu ya kifo.

***********************
Maelezo ya bi Maria kuhusu kumuona Samson, yalitosha kumshawishi Mzee Mgaya na familia yake kujua ni hatua zipi za kuchukua, akili za Kila mmoja iliamini Samson katoroka, kasoro mtu mmoja tu, mama yake Samson, huyu hakutaka kuamini kama Samson, ana akili au wazo la kutoroka, badala yake aliwaza mengi, kama si kifo basi itakuwa kapotea katika mazingira ya kishirikina kama Imani za watu wengi was Kijiji kile zilivyokuwa zinawaambia.

Sasa baba Jane, tunafanyaje kuhusu suala hili la mwanangu , unataka kuniua, unataka nife Bila kumuona mwanangu, nakuomba sana fanya Kila linalowezekana, nipate tu majibu sahihi.

Kama amekufa nijue nalia machozi ya aina gani, kama kafichwa napo nijueeeh. alilalamika mama Mgaya huku akizidisha majonzi kwenye familia yake wakajikuta wanaangua kilio kikubwa familia nzima, hasa pale mama Mgaya alipotaja kifo, Kila mmoja si mabinti zake si mume wake walijikuta mioyo inapiga pah.

Walikumbatiana huku wakilia, na Mzee Mgaya naye alikimbilia chumbani huku akijizuia kiume asilie maana hali ya hewa ilichafuka kwenye ile familia.

Sasa nafanyaje Mimi, namtafutia wapi huyu mtoto, familia nzima inaniangalia na kunitegemea kuwa naweza kuleta majibu sahihi,
Lakini polisi nao wametoa maelezo na ushauri ambao bado sioni kama una msaada, hata nilipojaribu kuwalazimisha , walinikoromea na kuniambia nisubiri jeshi lifanye kazi yake, hata nikirudi huko bado sitapata majibu sahihi.
alifikiria Mzee Mgaya hatimaye chozi lilimdondoka Bila kujua, akajikuta kajifuta haraka sana asijulikane kuwa naye alilia.

Samson aliitesa vilivyo familia yake, lakini pia wahuni, wajuba na wachuna ngozi ambao walitambua kuwa ni mgeni tangu alipotua pale mkunywa mjini Madibira, waliendelea kujaribu bahati yao.
Maskini Samson hakuna hata alilolijua kuwa anawindwa ili akauawe.

Tukutane sehemu ijayo................
 
SEHEMU YA SABA

Masoud hakujua ni saa ngapi alipitiwa na usingizi, ila alishtushwa na muungurumo wa gari nje, ya Banda lao, akafikicha macho kidogo akaona Kuna mwanga nje akapata hofu kiasi.

Ikabidi amuamshe mshikaji fulani akamweleza anachohisi nje, na bahati nzuri baadhi ya majamaa pombe zilishawatoka wakajikuta karibu wote wanaamka kasoro Samson, labda ni ule usingizi wa kitoto.

Aisee jamani mbona hivyo usiku huu Kuna Nini ndugu zangu? Mbona siyo kawaida kupiga stori usiku huu wa manane. aliuliza chapombe mmoja ambaye ile komoni ilishaisha ikawa yuko active tu muda ule.

Kuna gari ipo hapo nje, nadhani hawana Nia nzuri hawa watu kwahiyo
tunaomba tuchukue tahadhari kidogo Cha msingi tuwazingire ili
Tujue wanataka nini.
alishauri Masoud.

Basi watu wote wakakurupuka wakatoka na mapanga na baadhi ya local weapons, chaajabu walikuta gari la polisi ambalo lilikuwa linaunguruma bado.

Baada ya kuona wenyeji wametoka huku Kila mmoja akiwa kashika silaha ya jadi, wale Askari feki walifungua milango ya gari ya nyuma wakatoka, huku dereva akiwa kwenye usukani wake akiangalia nje.

Nyinyi vipi tunajua mi maaskari lakini kwanini mje mpark gari bila kutuamsha mlikuwa mna maana gani?aliropoka jamaa mmoja.

Wewe kaa kimya, Tena wote wekeni mapanga yenu chini, mchuchumae na mikono juu, waliamrisha wale maaskari huku Masoud na timu yake wakitii sheria bila shuruti,.

Hamuwezi kuishi na mtoto mdogo ambaye kwao anatafutwa,
Wazazi wake wanamtafuta huyu mtoto mwezi wa pili sasa na nyinyi mmemficha huku, mna maana gani au tuwachukue wote tukawasweke ndani. alitishia afande mmoja.

Wakati mabishano Yale yakiendelea tayari Samson alishaamka akawa anatoka nje huku akifikicha fikicha macho apate kuona vizuri.

Wale maaskari feki baada ya kumuona walitazamana kwa muda, Kisha wakaanza kutoa mikwara.

Oneni jamani huyu ni kijana mdogo kabisa huyu, na ndiyo huyu huyu ambaye anatafutwa na wazazi wake huyu tunaondoka naye kwaajili ya kumrudisha nyumbani kwake,na yeyote aliyempa kibarua huyu tutampeleka mahakamani.

Dogo hebu sogea huku upande kwenye gari,mtoto mdogo unakuja kujificha huku wewe ulipaswa kuwa Sekondari. Serikali hii ya Mkapa inasisitiza wahitimu wote wa shule ya msingi wanatakiwa kujiunga na shule ya upili, hivyo huyu tunaondoka naye. aliongea yule afande kwa vitisho.

Huyu haondoki, huyu haendi sehemu hapa tunauana , aliongea mbabe mmoja ambaye anafahamika kwa jina la "Chongo".
Hakuwa na makengeza ila aliitwa hivyo

Nyie siyo maaskari kama ni kweli tunaomba vitambulisho vyenu, pia tunaomba picha ya mtoto mnayemtafuta, kama ni huyu kweli pili tunaomba historia fupi ya huyu dogo tuna Imani waliowatuma wamewapa details za mtoto huyu.
aliongeza Masoud ambaye alikuwa timamu zaidi.

Yote uliyosema braza Masoud, Imani yangu ni kwamba Hawa ni majambazi tu kwasababu Mimi nimezaliwa Madibira, nimekulia hapa na naishi hapa hapa katika mfululizo wote wa maaskari wanaoletwa hapa nawafahamu, Madibira ni Kijiji kidogo tu, huku tukiwa na kituo kimoja tu Cha polisi hivyo haiwezekani Mimi Kati ya Hawa maaskari wanne nikashindwa kumtambua hata mmoja.Chongo muhuni wa kipindi hicho aliongea kwa kujiamini sana.

Chongo ni mtu aliye kuwa anaogopeka pale Madibira kwa ujasiri wake wa kupigana, na fujo nyingi, huku kubwa zaidi ikiwa ni ujangili wake, alikuwa muwindaji haramu ambaye alistaafu, ni baada ya kuona mbinu za maaskari pori zimekuwa za kisasa akaona asije kufa mtu, akaamua kugeukia mishe zingine.

Tuendeleee.......

Wale maaskari walipoona wanabanwa na wanazidiwa waliingia kwenye gari lenye plate number fake waliondoka huku wakitishia kuwa watarudi Tena uchunguzi ukikamilika na ole wao mtoto atoroshwe.

Samson yeye kama yeye aliona ile ishu ni ya kweli, kwamba huwenda wale jamaa wametumwa na wazazi wake.

Baada ya kuondoka wale Askari feki, watu wote walikuwa timamu huku wakichochea moto na kuuzunguka ule moto huku Masoud akiwasimulia kisa kizima tangu gari la kwanza lenye watu wawili , yaani Ray na Komba alipowatilia mashaka.

Dah Masoud uko makini sana, hivi tungekuwa wote huwa tunatoka na dogo akabaki peke yake, si wangemkomba kweli? aliongea Chongo, huku wote wakitikisa vichwa vyao kwa masikitiko wakimuonea huruma dogo.

Sasa bila mjadala dogo inabidi arudi home , au mnasemaje wadau? aliuliza Chongo.
Kila mmoja akaonesha kukubaliana na wazo lile.

***************************
Asubuhi na mapema mzee Mgaya alimpokea mgeni, hakuwa mgeni kwa Kila mwanafamilia, ila ni kwakuwa hakuwa akikaa pale, si mwingine bali
Dada yake na mzee Mgaya au shangazi wa akina Jane.

Walipeana pole za hapa na pale huku wakifarijiana kwa namna nyingi.

Dada yake na mzee Mgaya anakaa Kijiji cha jirani, kama kilomita kumi hivi, na jambo kubwa alilokuja nalo lilikuwa ni kuleta taarifa ya mtaalamu anayepatikana kijijini kwao ambaye angeweza kuwafanyia dawa ili Samson arudi, huku akionesha ana Imani kubwa sana na mganga huyo wa jadi kwani ana jina na historia kubwa sana kwenye kazi yake.

Itaendelea...........................
 
SEHEMU YA NANE

Masoud na wafanyakazi wenzie waliendelea kuota moto ule huku tayari upande wa mashariki nyota ya alfajiri ikionekana vyema kuashiria tayari kumekucha.

Kila mmoja alikuwa makini sana kutokana na kilichotokea muda si mrefu lakini pia wengi wao waliingiwa na hofu kubwa sana wakijua kabisa usalama ni sifuri.

Jamani ndugu zanguni, leo huyu dogo tunatakiwa tumrudishe nyumbani tufanye Kila linalowezekana afike japokuwa Mimi Sina pesa yoyote ya kuweza kumchangia huyu dogo. alisema yule mbabe Chongo huku akijitoa kwenye mambo ya pesa. alifahamika vizuri sana kwa ubahili.

Jamani kwani Kuna Nini mbona sielewi, Mimi nimekuja kufanya kazi na bosi alisema nitalipwa baada ya siku thelathini, Sasa hata siku kumi bado sijafikisha mnataka nirudi. Kwanini? aliuliza Samson.

(Watu wote wakacheka)
Kwa kumuhurumia maana hatari yenyewe ilimhusu yeye.

Sikia Dogo hapa unatakiwa urudi nyumbani haraka iwezekanavyo maana nyumbani kwenu unatafutwa na sisi hatuwezi kukaa na mtu ambaye kwao hajaaga vizuri Cha msingi leo tunasitisha kazi zote tunakusindikiza wewe. alipigilia msumari Masoud Kisha watu wakaingia bandani mwao kuvaa nguo zenye unafuu wakaanza safari ya kurudi Madibira kwa miguu.

Kutokana na Mashamba kule yapo kwenye vitalu vyenye namba, na wao walikuwa namba kumi ni mbali zaidi kutoka mji ulipo, walifika eneo moja kwenye intek za maji , yaani ulipo anzia mradi wa maji yaendayo Mashambani ilikuwa saa mbili za asubuhi , waliendelea kupiga mguu hadi kwenye daraja la Chuma lililojengwa na wakoloni, wakalivuka like daraja, na tayari walikuwa karibu na kata ile ya Madibira wilaya ya Rujewa mkoa wa Mbeya.

Kutokana na hofu iliyowakuta kule shamba kambini, walishauriana kuwa kwa usalama Zaidi wakaripoti polisi, japo kulikuwa na mabishano ya nani aende huko maana Baadhi ya majamaa walikataa kwenda kituoni wakiogopa rekodi zao chafu, hasa Chongo ambaye alikuwa akiishi kama Digi kutokana na tabia zake mbaya wakajikuta kwenda polisi ni kama mbwa kumfuata chatu alipo.

Basi sikilizeni ndugu zangu, hapa hakuna shida Mimi na wenzangu Hawa wawili tutaenda kuripoti polisi na wewe Chongo na wengine mtafute gari lolote hata la mizigo mumpandishe dogo arudi kwao.alishauri Masoud.

Hapana, huyu hapandishwi kwenye Lori peke yake Bali anatakiwa apelekwe Hadi kwa wazazi wake na wewe Masoud ndiyo ambaye pengine unaaminika kuliko yeyote hapa, hivyo nenda karipoti polisi, Kisha urudi, sisi utatukuta nyumbani kwa boss. aliongea kwa kujiamini Chongo, wakakubaliana.

Watatu wakaenda kuripoti polisi juu ya usalama wao na wengine wakielekea kwa boss wao ili wakasubiri mrejesho kwa boss wao.
Hakukuwa na simu kwakuwa Teknolojia ilikuwa bado hasa maeneo mengi ya vijijini, hivyo hakukuwa na mawasiliano yeyote Kati ya wafanyakazi na boss wao.

***********************************
Watu takribani ishirini na tano walikuwa nyumbani kwa mzee Mgaya wakimsikiliza mganga ambaye kwa utaalamu wake alidai
Samson hayupo mbali na maeneo yale na yuko porini kwenye milima huko.

Basi watu wote walipigwa na butwaa kusikia kumbe mtoto, kijana, na ndugu yao yupo tu milimani siku zote hizo, anakula nini, anakunywa Nini, anaishi vipi, yalikuwa ni mawazo ya Kila mmoja huku wakiamsha hisia mpya, wenye machozi ya karibu walilia kabisa.

Sasa mbona bi. Maria kasema alikutana na Samson, akiwa anaelekea njia za barabarani huko?
Alihoji Binti mkubwa wa mzee Mgaya aitwaye Jane.

(Huku akicheka sana)
Kwanza naomba kujua aliyesema alikutana na huyo kijana njiani ni nani? alihoji yule mganga.

(Wote wakajibu)
Wakioneshea nyumbani kwa mzee au bi. Maria.
Anaishi kuleeeeeeeeeeeh ni bibi Fulani hivi.

Ah mshasema ni mzee pengine hakuona vizuri na macho yake ya uzee. alisema mzee Mgaya

Sawa, Mimi vipimo vyangu, vinaniambia mtoto yule anasumbuliwa na mizimu ya upande wa wewe baba (Mzee Mgaya)
Mizimu hiyo ni kwamba kwa miaka mingi mmekuwa hamfanyi matambiko na kutoa kafara , mnapuuza sana hivyo basi mizimu ile imeanza kuwadai, hivyo ili mpate kujua imeamua kufanya hivyo kwa kumpoteza kijana wenu ili mpate kuikumbuka mizimu hiyo ya mababu zenu. aliongea kwa kujiamini yule mtaalamu.

Watu wote waliokuwa pale wakashangilia wakionesha Imani kubwa na mganga huyo machachari, aliyerithi mikoba toka kwa Babu yake.
Pia dada yake na mzee Mgaya ambaye ndiye aliyemleta mganga alikuwa mstari wa mbele kuwaaminisha watu wote kuwa yule ni mganga haswa.

Baada ya maelezo Yale ya mtaalamu, waliomba kujua gharama za kuweza kumrudisha kijana wao.

Kwanza hapa kunatakiwa vifaa, kwakuwa zoezi litachukua siku mbili,
Moja kwakuwa kijana ana umri mdogo kunatakiwa apatikane kondoo achinjwe kwaajili ya kuiomba mizimu iturudishie kijana wetu, lakini pili kwakuwa hamjawahi kufanya tambiko lolote kwaajili ya kuiomba mizimu muishi salama, kutatakiwa apatikane ng'ombe dume mkubwa kama zawadi kwa mizimu ili kuiridhisha isiwasumbue tena.

Pili Mimi kama mtaalamu nitakayefanya kazi hii nitatakiwa kupewa ng'ombe jike mmoja ambaye hajawahi zaa kama malipo ya kazi yangu lakini kama ng'ombe hakuna nipewe hata hela thamani ya huyo ng'ombe. alikamilisha maelezo yale mtaalamu huku mzee Mgaya na familia yake wakishindwa kujua la kufanya kutokana na umasikini uliokithiri, hakuwa na ng'ombe, mbuzi Wala kondoo zaidi ya kuku anaofuga.

Wakati hayo yakiendelea alikuja mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya kijiji kile akiwa na bahasha mkononi. kama kawaida alikuwa anaheshimika wakasalimiana na mzee Mgaya Kisha akamwita pembeni.

Mzee Nina mzigo wako huu, nilienda Jana wilayani zilipo ofisi za posta hivyo nimekuta barua zimerundikana kwenye sanduku la Kijiji chetu , hata hii yako inaonekana Ina wiki mbili tangu ifike, aliongea mwalimu yule mstaarabu.

Mzee Mgaya alifungua akaisoma , akaielewa vizuri , akaagana na mwl mkuu akabaki pale akitafakari jambo kwa muda, ni barua toka mjini Dar es salaam, ikitokea kwa kaka yake first born ambaye anaishi jijini Dar es salaam.

Ni kaka yake alikuwa anamtaarifu kuwa atakuja kijijini hapo kwaajili ya kuwasalimia maana ni karibu miaka kumi hawajawahi kuonana.hivyo Christmas akapanga aje kula kijijini

Mzee Mgaya alifurahia ile habari huku akionesha kufurahi ujio wa kaka yake ambaye kwa tarehe iliyoandikwa kwenye barua angefika siku mbili tu baadaye,lakini furaha yake ilikatishwa Kila akimkumbuka mwanaye Samson. Akarudi akaungana na baadhi ya watu wakimsikiliza mtaalamu ambaye walimwamini kwa asilimia nyingi.

Itaendelea...............................
 
SEHEMU YA TISA

Masoud na wenzake wawili walirudi kutoka kituo cha polisi huku wakiwa wamebaini vitu vingi sana,
Kwanza hakuna sura hata moja waliyoiona Kati ya zile zilizokuja kwao Jana yake. lakini pili polisi walionekana kushituka na majambazi hao wanaoonekana kwanza ai wenyeji wa mji ule.

Huku wakitoa Rai kwamba kama vijana waishio Kambi ile wapo wengi, wanao uwezo wa kuwazunguka kama watarudi Tena ili wajae kwenye mikono ya sheria, lakini pia wakaonya kuwa huyo kijana apelekwe kwao na wao wawe na tahadhari.

*********************************

Watu kutoka sehemu mbalimbali katika Kijiji cha kwa kina mzee Mgaya walikusanyika huwa taarifa za uwepo wa mganga wa jadi mwenye uwezo wa kumrudisha Samson,
Kila mmoja alikuwa na hamu na shauku ya kutaka kuona maajabu hayo ambayo kiuhalisia hayawezekani.

Michango ya kuweza kununua kondoo ili kazi ianze Mara moja ilifanyika haraka sana, watu walichanga si kwakuwa Wana pesa nyingi Bali ni kwasababu walitaka kuiona sinema ambayo ingeweka kumbukumbu na rekodi isiyofutika ya mtu kupotea kimazingara na kurudishwa.

***********************
Saa kumi na moja alfajiri Masoud na Samson walikuwa kwenye bus au gari la abiria lifanyalo safari zake Madibira to Mafinga, lengo washuke kijiji cha jirani na washike njia kuelekea nyumbani kwa kina Samson , huku wengine wakiwa wanaagana Kisha kushika njia ya kuelekea kambini kwao.

Mida ya saa nne za asubuhi watu waliahirisha shughuli zao za kulima katika msimu ule wa mwezi wa kumi na mbili, wengi waliacha kazi zao huku wakielekea kwa akina Samson huku idadi ikiongezeka kama vile Kuna msiba.

Wakati watu wengi wakiwa wameyazunguka yale mafiga matatu huku chungu kikubwa kikiwa kinachemka nyama iliyochanganyika na dawa fulani huku pembeni ya kile chungu kukiwa na pembe kubwa ya mnyama wa porini ambaye hakufahamika ni mnyama gani, huku mganga akiwa katulia tu pembeni kazi ya kuchochea moto ilifanyika na wasaidizi wake ambao walifanya manuizi Kila baada ya dakika tano wakipuliza ile pembe kama ishara ya kumuita Samson.

Ilifika muda kama saa tano hivi mganga aliinuka kwenye kiti Chake na kuizunguka ile nyumba huku akiwa na kioo kilichozungushiwa shanga zikionekana ni chafu yaani zimefungwa zamani sana, aliendelea kumulika huku na huko kisha akageukia mlimani akiwa ameganda kwa muda huku akitamka maneno fulani ya majigambo kwa sauti mithili ya wachungaji wanavyoombea watu.

Watu wote walikuwa makini wakifuatilia Nini kitajiri kwenye lile zoezi.

Mama wa kijana aliyepotea hebu sogea hapa, aliamrisha mtaalamu yule.

Mama Mgaya alisogea kwa unyonge akapiga magoti kama alivyoelekezwa ikaletwa nyama ile iliyochanganyika na dawa akaambiwa kwakuwa yule ndiyo mama mzazi wa muhusika anatakiwa awe wa kwanza kula nyama ile akafanya kama alivyoagizwa.

Aje na baba halali wa mtoto aliyepotea.
Mganga aliagiza tena.

Alisogea mzee Mgaya akiwa na koti lake kuukuu kabla hajatia kipande Cha nyama mdomoni mganga alimuuliza swali.

Je, wewe ni baba halisi wa mtoto?
aliuliza mtaalamu.

Swali lile Mzee Mgaya hakutegemea swali lile akabaki anacheka cheka tu Kisha akatingisha kichwa kuashiria ni mwanae wa kumzaa.

Sikiliza mzee wangu manuizi ya dawa niliyofanya inawalenga wazazi halali tu, kama huyu si mwanao pengine mke wako alizaa nje ya ndoa na wewe ukaona kwakuwa kitanda hakizai haramu ngoja nilee tu, ndugu yangu hapa hupaswi kula hii nyama maana utapata matatizo.
aliongea yule mtaalamu akawafanya watu wacheke huku mzee Mgaya akiwa na huzuni, kwani hakujua afanyaje.

Mama Mgaya aliropoka kwa sauti kali akimweleza mganga kuwa huyo ni baba halisi wa watoto wake wote anaowaona hakuna mtoto wa kumtilia mashaka hata kidogo. hivyo asingependa kudhalilishwa.
ni kweli maneno ya mtaalamu yule yalimdhalilisha mama Mgaya na hata mzee Mgaya pia.

Basi zoezi la kula nyama liliendelea kwa Kila mwanafamilia huku mtaalamu akiagiza kila Mmoja ale kwani mtu ambaye watamuona alikuwa sehemu isiyo ya kawaida hivyo unapoangalia kitu kilichokuwa kwenye ulimwengu mwingine unapaswa kula ile nyama watu wote waligombania nyama ile huku hatua zingine za kumrudisha Samson zikiendelea.

Samahani mtaalamu muda unazidi kwenda vipi zoezi litachukua muda gani hadi kurudi kwa huyo kijana?
aliuliza mwenyekiti wa Kijiji ambaye alitoa kibali Cha kufanyika shughuli ile iliyowakusanya watu wa Kijiji kile.

Wewe tulia hii kazi ni nzito Mimi hapa huyu kijana najaribu kumuangalia kwenye vyombo vyangu namuona kabisa tena amekonda sana na hapa hiyo nyama waliyokula wazazi wa huyu kijana inaanza kushindana na mizimu na ninavyoona mizimu inakaribia kushindwa na kwa muda wa siku kama tatu atarudi. alijibu mganga huku baadhi ya watu wenye akili timamu wakishindwa kuridhika na majibu yale.
Mganga aliendelea kufanya vitu vyake huku watu wakiwa na Imani kubwa sana ya kurudi kwa Samson .

Lakini kitendo Cha mganga kubainisha wazi kwamba kwa mujibu wa vipimo vyake Samson aliko amekonda sana na pia matumaini ya kurudi ni siku tatu baadaye
Familia ya nzima iliumia mno tena sana .

******************************
Masoud na Samson walijikuta wanachelewa kufika kutokana na gari kuharibika njiani maeneo ya kijiji fulani kinaitwa Igomaa, siyo Igoma ya mwanza Lakini, walisubiri matengenezo ya gari bila mafanikio yeyote hadi saa tatu za asubuhi hatimaye wakakubaliana waanze kupiga mguu wakajikuta wanatumia muda mwingi njiani.

Mida ya saa nane mchana waliikaribia nyumba ya akina Samson huku wakishangaa kundi la watu wanaoonekana umbali wa mita mia mbili hivi.

Wewe dogo unasema pale ndiyo nyumbani kwenu , mbona kama hamna usalama pale.
aliuliza Samson huku akipunguza hatua za kutembea maana hisia zake zilimtuma tofauti.

Ndiyo pale ndiyo nyumbani na sijui Kuna Nini pale, alijibu Samson huku wakizidi kuikaribia nyumba yao.

Mara majirani wanaomtambua Samson wakiwa pembeni pembeni ya nyumba walimuona Samson akiongozana na watu wawili watu wazima wasiowafahamu .

Jamani Samson mwananguuuuuuuu ilikuwa ni sauti ya jirani Mmoja mwanamke ambaye alikuwa wa kwanza kushindwa kujizuia watu wote waligeuka kuwaangalia wale wageni huku wakipigwa na butwaa zito lililokosa majibu, wapo waliojaribu kukimbia wakidhani ni mzimu lakini walirudi baada ya kuona kijana wa watu ni mzima wa afya.

Watu walilia kwa kupokezana haikujulikana ni machozi ya aina gani ila Kila mtu alilia kwa namna yake huku mama yake Samson akiwa kazimia muda mwingi tu baada ya watu kunyamaza, walimgeukia mganga/mtaalamu wakiwa na nyuso zilizoashiria shari, huku mganga akiwa kabadilika sura na ana uoga ndani yake.

Itaendelea..........................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom