Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

Kongole mwandishi wetu
Tumejifunza mengi...
-ndoa/mahusiano
- kujituma kazi kwa bidii
-kuishi vizuri na ndg,jamii nk
-biashara na uwekezaji
_imani/dini kuishika kama Rahma

Yangu ni hayo ndg wanajamii ....mbarikiwe sana
 
Nashukuru. Nimebakiza stori moja ya bm6 baada ya hapo sintosoma Hadithi humu. Mana zinanichukulia my mental energy of thinking about them. Haya maisha yako Sana. Hata namie Ni Kama Samson Ila ingawa matukio yanatofautiana
 
Dah kumbe namie nna roho ndogo mbona nimesikitika sana mzee mgaya jmn...mkuu ulisema hiki kisa kina mahusiano na mimi na boss wangu nimeshindwa kuhusihanisha kbs kindly do the necessity bas
Kila binadamu mwenye roho nzuri ya huruma lazima asikitike.

Kuhusu kutofanana kwa stori ni sahihi, kwenye stori zote mbili Kuna vitu vingi vimepunguzwa ili kukwepa wahusika wanaomjua Samson wasihusianishe stori,

Yote kwa yote ni kuhakikisha simulizi inaleta ladha kwa msomaji
 
Asante sana Jack Daniel tumekuwa pamoja mwanzo mwisho wale wenzangu na mim wa episode mbiri wanataka michango wanalo la kujifunza kwenu watunzi nguli humu Jf
Ahsante
Suala la michango mnaweza kuchangia kwasababu waandishi wengine ni kazi zao na ndipo anapata riziki
 
Hongera jack kwa kazi nzuri.storry ilikuwa nzuri sana na kulikuwa na mengi yakujifunza
 
Ahsante
Suala la michango mnaweza kuchangia kwasababu waandishi wengine ni kazi zao na ndipo anapata riziki
Sasa si bora uione kweli hii ni kazi hata nikiambiwa changia nachangia simulizi imekaa kimchongo mchongo mtu anakuambia ni true story😂😂😂 wakati huo mi mwenyewe msomaji naona haya ni mambo ya kubuni kabisaaaaaa
 
Sasa si bora uione kweli hii ni kazi hata nikiambiwa changia nachangia simulizi imekaa kimchongo mchongo mtu anakuambia ni true story wakati huo mi mwenyewe msomaji naona haya ni mambo ya kubuni kabisaaaaaa
Ndiyo hivyo tena unajikuta ni mraibu wa stori hivyo unapaswa ulipie.
 
It takes some of my mental energy that could be used in another activities that gonna add value for me
Ni uamuzi mzuri ili kudeal na shughuli nyingine kuliko kujipa arosto ambazo zitakufanya ushindwe kufanya mambo yako kwa usahihi
 
SEHEMU YA MWISHO

Masomo yaliendelea vizuri kwa Samson hata mwalimu mkuu ambaye alikuwa na wasiwasi na Samson akimtaka arudie darasa, alianza kuwa na Imani naye sana tu , Samson aliungana na ndugu zake wale mapacha ambao waliunda utatu fulani mzuri sana kiasi cha kuwashawishi na wengine.

Kitabu na wao, wao na kitabu.
Hii ilipekekea kuwa mfano wa kuigwa hata na wanafunzi wenzao ingawa kulikuwa na vichwa pale darasani kiasi cha Samson kushindwa kuelewa kwani wanafunzi wengine hutumia ubongo huuhuu au Kuna namna nyingine, lakini yote kwa yote Kila mtu alijikuna anapofikia.

Tabia ya mtu ni kama ngozi kuivua inakuwa haiwezekani,
Kuna siku moja Samson alipata kuvutiwa na msichana fulani pale shuleni, akaanza kutupa ndoano zake, Kila msichana wa watu akikataa yeye Samson akawa hakati tamaa, basi siku moja nyakati za usiku walikubaliana wakafanye tendo la kibiologia nyuma kabisa karibu na yalipo majiko ya kupikia ndipo walipofumwa na mwalimu aliyekuwa doria huku akiwatembezea bakora za kutosha. Kwakuwa neno lile Samson hakutaka lienee shuleni pale akaomba msamaha sana huku akitoa rushwa kidogo kwa yule mwalimu na kukubaliwa, lakini licha ya hivyo bado taarifa zilienea kwa baadhi ya wanafunzi ambao walimsema Samson na kumsimanga sana tu, ukawa mwisho wa tabia za kishenzi akaamua kudeal na masomo yake.

Baada ya shule kufunga mwezi wa sita wote watatu walirudi nyumbani na kukuta Kuna mabadiliko kidogo, kuanzia housemaid mpya, lakini pia Samson alishangaa kuona mtoto wake yupo na house girl Kila muda ikabidi aulize,

Mama vipi Rahma yuko wapi mbona simuoni? aliuliza Samson.

(Kwanza mama Kulwa aliguna kisha akaendelea)
Rahma katoroka,
Ilikuwa hivi Kwanza aunt yako Sarah aliaga kwakuwa mkataba wake uliisha kwani nilimchukua kwaajili ya uangalizi wa Rahma akiwa na mtoto mdogo, hivyo alidai anarudi nyumbani ambako Kuna mchumba wake na anaenda kuolewa. Hivyo nikamruhusu aondoke huku nikimkalisha kikao Rahma kuwa Sasa mtoto kakua hivyo anapaswa kufanya kazi zote hapa nyumbani ndipo alikubali huku nikigundua ni kwa shingo upande kwani tangu Samson uondoke alikuwa mnyonge. alifafanua mama Kulwa.

Lakiniiiiiii mmmmh yule mtoto basi tu, Kuna siku nilirudi toka mjini nikakuta hajaandaa chochote humu ndani, hata nilipomwambia Mzee wenu alidai kama nashindana naye basi naweza kumruhusu aondoke lakini kwa moyo wangu wa kibinadamu sikutaka kumfukuza Rahma wangu. mama Kulwa alifafanua Kisha akaendelea....


Baada ya miezi kadhaa kupita Rahma aliniambia kuwa anahitaji kubadili jina la mtoto wake, ikabidi nimuulize kwanini?
Akadai yeye tangu mtoto apewe jina lile hakuwa radhi kwani lipo jina linaloshabihiana na Dini yake ambalo mtoto anataka apewe.
Kiukweli sikumjibu kwani kuhusu yeye kuwa mdini natambua siku nyingi sana hivyo nilimwacha tu.

Baada ya siku mbili hivi wakati narudi toka mjini kwenye biashara zangu nilimkuta kijana fulani aliyevalia kanzu akiwa na muonekano wa kiustadhi,lakini yule kijana baada ya Mimi kuingia naye alitoka muda huo huo. Ikabidi nimuulize Rahma kwanini anaingiza watu ndani mwangu bila uoga Kuna kuibiwa , Kuna kupelelezwa na mengine mengi sana lakini Rahma alichukia na kuondoka usiku huohuo shahidi Mzee Mgaya ambaye alimuona anaburuza begi licha ya kumuita hakutaka kusimama basi Mzee Mgaya aliingia ndani kuja kuniambia hizi habari lakini tulipotoka hatukuiona sura ya Rahma hadi leo hii , akatuachia tu huyu mtoto ambaye nilipata naye taabu hivyo hivyo lakini MUNGU ni mwema mtoto anaendelea vizuri.
Mama Kulwa aliweka kituo.

Kitendo cha kuambiwa Rahma alitoroka kilimtingisha kidogo Samson kwani alimpenda sana lakini hakukuwa na namna ndiyo hivyo alikubaliana na hali.

Kuhusu wazazi wako tunawasiliana nao mara kwa mara, na wanakuombea sana. Na pia Tausi hatunaye mwanangu hivi una taarifa?
Maana Kuna siku Mzee Mgaya alikuja hakuwapa habari hii? aliuliza mama Kulwa.

Samson. Hakuwa na majibu akabaki anaangalia tu, ndipo mama kulwa akafafanua.

Tausi alifariki kwaajili ya gari, ambapo alikuwa anaendesha mwenyewe tena ikiwa ni siku ya kwanza tu tangu anunue akalivamia Lori lililokuwa limepaki pembeni mwa barabara ndipo ukawa mwisho wa uhai wake.
Lakini pia mwanangu Catherine (Cathy) yule sijui hela kapata wapi kwasasa anaishi maeneo wanakoishi watu wazito huko kiufupi hata hapa hajawaji kuja na mawasiliano yetu ni hafifu.alifafanua mama Kulwa ambaye anaonesha alimmiss Samson. Kuliko hata wanaye kwani walikuwa wanapiga stori akimsimulia mambo mbalimbali.

Na pia mwezi wa nane Kuna shughuli nzito hapa maana kaka yako Jose anaoa, japo huyo mchumba sijamuona ila sijapenda aina ya kazi yake nasikia ni mwanasheria kama alivyo kaka yako Sasa hofu yangu mwanangu asifunikwe maana Hawa mabinti wasomi haswa Hawa ma lawyer huwa Wana masharti sana kwenye ndoa, mama Kulwa alionesha hajapenda chaguo la mwanaye Jose.

Hapana mama Mimi nadhani kaka Jose anajua kikubwa heshima na uaminifu Kati Kati yao nadhani wenyewe wanajuana vizuri. alijibu Samson Kwa uelewa wake.

Mmmmh ngoja tuone na tatizo mwanangu hashauriki yule, alilaumu Mama Kulwa.

***************************************Baada ya Samson. Kuhitimu kidato cha nne alirudi nyumbani kama alivyoambiwa na wazazi wake kuwa arudi kijijini afanyiwe tambiko fulani ili kunyoosha mambo yake kama ilivyo kwa makabila mengi nchini. japokuwa hakuwa na Imani na mambo yale lakini aliheshimu wito na maamuzi ya wazazi wake, alikaa zaidi ya wiki kadhaa akiwa anasikilizia matokeo pia ndipo aliporudi mjini baada ya kusikia ataendelea na masomo yake ya kidato cha tano bila wasiwasi.

Cha ajabu wakati anafika nyumbani muda ya usiku kama saa tatu kwenda saa nne alishangaa uwepo wa magari mengi pamoja na wingi wa watu ndipo aliposikia kuwa Mzee wake aliyempa msaada, aliyemfutia ujinga japokuwa hakuwa amemaliza , yaani James Mgaya alikuwa amefariki huku majirani na marafiki wakidai walikuwa wanakunywa wote pombe hata alipodondoka walidhani ni pombe zimemzidia lakini ukweli ni kwamba Mzee Mgaya alikuwa kaaga Dunia.

Samson alilia, akalia na kulia mtu pekee mtetezi na mwenye misimamo yake alikuwa hayupo Tena Samson alijua mwisho wake ndiyo ule. Lakini baada ya taratibu za matanga na mengineyo Joseph James Mgaya alimuita Samson kwenye grocery moja iliyo karibu na nyumbani kwao mazungumzo yakawa hivi.

Samson mdogo wangu nimetambua ulivyolia na ulivyomnyonge mpaka muda huu kutokana na kuondoka kwa Mzee wetu, baba yetu Mzee Mgaya lakini nikutoe wasiwasi Mimi hapa ni mbadala wa mzee Mgaya nitajitahidi kusimamia miradi yake na mambo yake ikiwemo wewe kutimiza ndoto zako hivyo naomba usijisikie vibaya.

Kwa kuondoa shari na migongano ambayo itajitokeza wewe utasoma nje ya Dar es salaam jitahidi kuwa kwenye mstari mnyoofu na maadili mema. yalikuwa ni maneno ya Jose akimfariji Samson.

Kifupi Samson alisoma mpaka chuo kikuu akifanikiwa kupata Degree Moja ya uhandisi huku akipewa ushirikiano na kaka yake Jose,mengine alijiongeza mwenyewe kama ilivyo kwenye mbanga, mishe na habari za kujiongeza town, huku wenzake wakifeli haswa Dotto ambaye alichagua biashara mapema. Hujui Kulwa akiishia kuwa mwalimu wa sekondari.
Mama Kulwa alifariki kipindi Samson akiwa ana kazi, ameoa na ana mtoto mmoja.

Kuhusu wazazi kamili wa Samson wote wapo hai mpaka muda huu , MUNGU awalinde na awazidishie maisha marefu.

Stori ya kweli ya maisha ya Samson, huku majina yaliyotumika humu yakiwa fake ili kuwakwepa watu wa karibu kuunganisha matukio.
Huu ni mwisho wa simulizi yetu.
Hongera ndugu msomaji kwa kuifuatilia Hadi mwisho.

Pia niwaombe radhi kwa kushindwa kuileta muda na wakati sahihi. Tusameheane.
Nikipata muda na wakati wenye utulivu nitaleta simulizi nyingine lengo ni kuburudika na wanajamvi.

Alamsiki.


Sent using Jamii Forums mobile app
moneytalk beb umeshapita ?
 
Nashukuru. Nimebakiza stori moja ya bm6 baada ya hapo sintosoma Hadithi humu. Mana zinanichukulia my mental energy of thinking about them. Haya maisha yako Sana. Hata namie Ni Kama Samson Ila ingawa matukio yanatofautiana
Mkuu habari
Naomba nitag kwa story ya bm6
 
Mkuu habari
Naomba nitag kwa story ya bm6
Am not fan such. Just subscribe. My mind only it's working best when am concentrating at one task in my hand.
So hapa inabidi niiweke kichwani kuwa siku akituma nakukumbusha. It's kind of mind/mental job like any other physical job sema Sasa kwa vile Ni mental haionekani kuwa Ni kazi. Ni sawa na kumpatia mtu ushauri wa kisheria,kihasibu ama kihandisi,ama unasovu swali fulani watu hawaoni kuwa umefanya kazi Ila mpaka nibebe mawe ndio dunia iamini kuwa Nimefanya kazi Mana nitachoka nitatoa jasho.

Kwako itabidi niweke wazo kwenye mind na kuliweka Ni kazi kwangu. Huwa napenda free life.
 
Pongezi kwako Eng.jack.vya kujifunza ni vingi.haswa Kwa mzee mgaya.,ametuwakilisha wanaume vzuri.yapo mengi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom