Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

Kwa wale wote mnaofuatilia simulizi hii nawaombeni mniwie radhi ni majukumu yananibana kwani nipo huku JNHP mradini. ila kwa Sasa nitaimalizia kwa ipo mwishoni bado vipande vichache. Msikose kuchungulia

Lakini pia Mimi siuzi hadithi na yule aliyekuja PM na kunitukana, naomba ajue kuwa nimejisikia vibaya sana, na Mimi siishi kwa kuuza stori, Bali nimeshare nanyi kwaajili ya kiburudisho na kujifunza.

keisangora Manyanza ram Boogman makorere Numbisa Mkushi w jani moneytalk hewizet MR KUO na wengine wote niliowasahau.
Aisee msalimie Eng,David.nimepamiss corona
 
SEHEMU YA TISINI NA NNE

Asubuhi na mapema Samson aliamka mapema lengo aanze kazi ili walau kujiweka kwenye mazingira mazuri asije akaonekana huwa mvivu, lakini baada ya kutoka nje alishangaa kumuona Mama yake mzazi akiwa ameshaamka, wakiwa na dada wa kazi Sarah wakitimiza majukumu ya kazi asubuhi ile.

Mama shikamoo, mbona umeamka mapema sana, ni Bora ungeendelea kupumzika tu hizi kazi tutafanya Mimi na aunt Sarah. aliongea Samson akishangazwa namna mama yake alivyojihimu.

Haina shida mwanangu wala hakuna maana kulala wakati tayari kumekucha, nimeona ni afadhali niamke tu, lakini mwanangu Jana Kuna kauli nimeisikia toka kwa shemeji yangu (Mzee Mgaya)japokuwa alikatishwa na mkewe lakini tayari nilimwelewa,
Wanasema yule mtoto wa yule Binti ni wa kwako? unajua haya masuala yamesababisha nikose usingizi kabisa kwani Kila nikiwaza nimekosa majibu. Najua nitaambiwa lakini wewe ni mwanangu napaswa nikusikilize kwanza wewe.
aliweka kituo mama mzazi wa Samson huku akimwangalia Samson Kwa kumkazia macho.

Wanasema ni mtoto wangu ila Mimi naendelea na masomo yangu kama kawaida. alijibu kifupi Samson.

(Mama yake Sam akacheka kwa kumuhudumia mwanaye) Kisha akaendelea....

Wanasema akina nani, kwahiyo wewe huna uhakika kama ni mwanao? Hivi wewe mtoto mbona unakosa akili timamu ya kulinganisha maisha haya ya wenzetu na maisha ya kule kijijini kwetu.
Halafuuuu mmmmh nashindwa kuelewa kwakweli, kwanza Kuna barua tulipokea tangu mwezi wa tisa kuhusu malalamiko ya huyu Mama lakini hatukuitilia maanani tukahisi labda ni mgongano wa kawaida na hata nilivyoambiwa nije nilipuuza.

Lakini pia mwezi wa kumi na moja tulipokea simu kutoka kwa baba yako mkubwa Mzee Mgaya, kiukweli masikitiko yaliyoandikwa mule yalitunyong'onyesha kiasi cha baba yako kuniruhusu nije maana yeye kabanwa na shughuli za shamba. lakini tayari mwanga nimeshapata , halafu wewe unaniambia eti wao wanasema kuwa ni mtoto wako kwakuwa wewe hujui siyo.
Mama yake Sam aliongea kiasi cha kuifanya sauti iwe juu, ila Samson alimsihi mama yake atulie.

Heeeeh shoga yangu mbona mapema tena, kwanza habari za uchovu, nilitegemea ulale dada yangu lakiniiiiiiii... alishindwa kumalizia sentensi yake Mama Kulwa huku akijifunga nguo zake vizuri.

Hakuna haja ya kufanya kazi dada yangu wewe, wewe pumzika tu tunaye mtu ambaye yupo kwa kazi za hapa. aliongea mama Kulwa na kuingia na mgeni ndani.

Samson alibaki nje, huku akiwa na wasiwasi fulani juu ya maneno ya mama yake mzazi, aliendelea na mishe zake huku akiwa ana hamu ya kumuuliza mama yake habari za kijijini japo alijua mama akipata full mkanda wa habari zake, basi amani itapotea.

Breakfast time ilifika huku watu wote wakiungana kwenye meza moja, kasoro mama Kulwa na mama yake Samson ambao walikuwa pamoja muda wote wakiongea na kucheka mambo fulani huku Samson akitamani angekuwepo mahali walipo ili asikie kinachoongelewa lakini haikuwezekana.

Hebu toa hivyo vyombo, siyo kila kitu afanye Sarah wakati mwingine inabidi wewe mwenyewe ujue Nini unapaswa ufanye acha kuwa mvivu.
Mzee Mgaya aliongea kwa ukali kiasi cha kumshangaza Samson akitaka kujua Nini kinaendelea.

Baada ya muda watu wote walikuwa pale sebuleni wakiwa na kikao cha dharula ambacho kiliitishwa na mzee Mgaya kwaajili ya kumweleza mgeni tabia za mwanaye Samson.

Kwanza nikushukuru kwa mara nyingine shemeji yangu kwa kuacha shughuli zako na kuamua kuja kuitika wito wetu hakika ni jambo zuri sana, lakini moja kwa moja kwakuwa ni haraka kidogo ningeomba mke wangu aeleze kile alichodai Jana si vizuri kukwambia lakini nadhani huu ni muda sahihi kuweza kufahamu mambo ya kijana wetu.
Mzee Mgaya alifungua kikao kile.

Unaelekea mwaka wa nne tangu tumpokee huyu mtoto, lakini alivyonikinai utasema tumekaa naye miaka zaidi ya kumi,
Samson ni kijana mpole tu ukimwangalia lakini ni mtu mwenye kujisahau sana, ni mtoto ambaye anaweza kurudia kosa moja zaidi ya mara tano kwa muda mfupi, mwaka wa kwanza nilikaa naye miezi michache lakini tukakosana, ikabidi aende kwa mke mwenzangu ambako Nako kulimshinda akaona ni nafuu hapa kwangu, lakini kosa kubwa alilofanya ni kutuletea hiki kiumbe ,
Hakika ni dharau kubwa na aibu aliileta kwenye familia hii, nadhani mengi nimekueleza lakini si vibaya nikarudia.

Kutokana na kuwa ni mzazi wa kwanza huyu Binti alininyanyasa sana kiasi cha Mimi kusitisha baadhi ya kazi zangu yote kuhakikisha afya na usalama wa huyu Binti.
Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi, na mambo nimeyaona , Samson amenipa somo nimelea watoto wangu mpaka Sasa ni wakubwa Lakini hawajawahi kuwa na makosa ya kujirudiarudia kama huyu.
Nimegeuka mlezi wa mtoto maana kama unavyomuona huyu Binti umri wake, hajafikia kutambua dalili zozote za mtoto kuwa kwasasa anataka nini au nini, mtoto akilia na yeye analia kwahiyo unajua jinsi gani nahitaji kuwa karibu na huyu Binti,
aliweka kituo mama Kulwa.

Kisha mama yake Samson akajibu.....

Na Mimi nawashukuru kwa kuweza kukaa na huyu kijana mpaka Sasa, lakini niwashukuru zaidi kwa uvumilivu wenu juu ya yote yaliyojitokeza kwa huyu (akitaja tusi)
Mmeweza kudharau na kukuta ni lazima muishi naye japo kwa kumsukuma, Kisha akamgeukia Samson,

Kwani mwanangu una malengo gani mpaka muda huu maana tabia na mwenendo wako umenistua na umetutia aibu Mimi na baba yako tuonekane tulikulea vibaya kiasi cha wewe kuwa si mwenye kusikia, je una mawazo gani juu ya hatma yako?
mama Samson aliuliza.

Mimi nitaendelea na shule kama kawaida Sina mpango wala njia nyingine zaidi ya kuwaza shule, kwani tayari nawashukuru walezi wangu wameweza kunitafutia shule nzuri ambayo itanikuza kitaaluma.
alijibu kiufupi Samson.

Siyo shule ambayo itakukuza kitaaluma, ni kwamba tuligundua shule unayosoma hutakiwi na ndiyo maana tukaamua kukuhamisha mapema vinginevyo ungefukuzwa kabisa. dada yangu, mwanao tabia yake imeenea mtaa mzima kwanza hakuna anayemtaka kuanzia huko shuleni kwao, walimu hawampendi kutokana na tabia zake Lakini yote hayo sisi tulisamehe na kuchukulia kama ni ya kawaida. alidakia mama Kulwa.

***************************************

Samson baada ya kusoma nyuso za wakubwa wake aliamua kupiga magoti katikati huku akianza kuwaomba msamaha Mzee Mgaya na mkewe kisha akamuinamia mama yake mzazi na kukiri makosa yake yote, huku akiahidi kubadilika.

Jamani binafsi Mimi namsamehe ni kijana, ni mtoto wetu pia ni hatua za makuzi yake , watoto hawawezi kufanana kila mmoja huwa na namna yake ya ukuaji hivyo binafsi nikitakie utekelezaji mzuri kwa uliyoahidi mbele yetu. aliongea Mzee Mgaya huku kauli ikiungwa mkono na watu wote mle ndani.

Baada ya hapo stori za kawaida zilifuata huku furaha, utani na mengine ya kufurahisha yakiendelea huku wakipokezana mtoto wa Rahma Kila saa ila Kila wakikutanisha macho Kati ya Samson na mama yake mzazi, Kuna kitu Samson aligundua mama yake alijikaza tu mbele ya wenyeji wake na lakini inaonesha alikuwa na donge likimkaba akionesha kutoridhishwa na yale aliyoambiwa,na namna yalivyoisha.

Samson na mama waliendelea kukwepana hususan Samson alikuwa anaona aibu hata kumuuliza mama yake habari za kijijini, alitamani afanye hivyo lakini aligundua mama hataki kuongea naye chochote ikabidi afanye habari zake.

Siku iliisha na Samson aliamini Kila kitu kipo sawa, lakini baadaye baada ya kupata chakula cha jioni waligawana vyumba kama kawaida na yeye damson kuingia ndani kwake, lakini baada ya kama masaa mawili huku usingizi Ukiwa unamchukua alisikia mlango ukigongwa, aliamka na kufikiri ni Rahma huku akiwa kashajiandaa kumpa makavu yake kwanini amuaibishe mbele ya uwepo wa mama yake.

Lakini baada ya kufungua alikutana na sura ya mama yake mzazi,

Mama vipi mbona ni usiku Kuna shida gani? aliuliza Samson

Mama hakujibu badala yake aliingia ndani na kufunga mlango Kisha akatoa fimbo yake ambayo inaonesha aliindaa tangu mchana, mfano wa bakora, akaanza kumshushia kipigo Kizito Samson akiwa hachagui pa kupiga licha ya Samson kupiga makelele ya kuomba msamaha na msaada lakini mama yake hakuonesha hata chembe ya huruma , mama Kulwa, Rahma pamoja na Sarah walionesha wameshafika mlangoni na kumsihi mama Samson aamuache mwanaye lakini hakusikia,
Mama mwenye nguvu za kijijini mwenye kutumia jembe la mkono zaidi ya miezi mitatu kuanzia kulima, kupalilia mpaka mavuno, alikuwa akitoa dozi kwa mwanaye ambapo Samson alijikunja mithili ya mtu aliyepoteza tumaini.

Licha ya mama Kulwa kumbembeleza mgeni wake kuwa amuache mwanaye atamuumiza lakini hali ilikuwa mbaya, ni Samson mwenyewe baada ya kugundua kuwa akijilegeza atakufa alifungua mlango kwa taabu huku akikimbilia sebuleni ambapo paji la uso na sehemu zingine za kichwa zilikuwa zikivuja damu. Maana haikuwa fimbo ya kawaida.

Watu wote watatu mama Kulwa, Rahma na Sarah walimwanfalia mama yake Samson kwa uoga huku akiwapita na kuingia kwenye chumba chake huku akimuita mama Kulwa Kwa ishara.

Pole vipi umeumia sana? Au tukupeleke hospital. Rahma alimwambia Sam huku akimfuta damu, na Sarah naye akiwa anafuta damu zilizodondokea sakafuni. Mama yake Sam kuona vile Rahma anamfuta damu Samson, alirudi kwa kasi na kuanza kumshambulia Rahma huku akitoa matusi mazito sana.

Jamani leo imekuwaje na hivi Mume wangu hayupo nawezaje kuituliza hii hali,halafu dada huyu Binti ni mgonjwa mgonjwa hajatengamaa bado utamuumiza.
alilalamika mama Kulwa huku akishindwa la kufanya kumuokoa Rahma ndani ya mikono ya mama yake Samson.
 
Muhehe kapandisha mori
 
SEHEMU YA TISINI NA TANO

Mzee Mgaya alifika asubuhi na mapema akitokea kwa Tausi, akaacha gari lake nje kabisa ya fence pengine ilikuwa asalimie tu Kisha aendelee na mambo yake,

Habari za hapa Sam, Mzee Mgaya alisalimia.

Nzuri tu shikamoo baba. alijibu Samson lakini Mzee Mgaya alikuwa akimwangalia Samson Kwa umakini huku akionesha kushangaa.

Wewe vipi huko usoni imekuwaje tena, umevamiwa? na mara nyingi nimekuwa nikikukanya kuhusu tabia ya kuzurula usiku.
aliongea Mzee Mgaya kana kwamba anajua kilichomsibu Samson, lakini kabla Sam hajajibu , mama Kulwa alikuwa anatokea chumbani kwake huku akionesha ana furaha fulani.

Kuvamiwa? avamiwe na nani huyu kapigwa na mama yake jana usiku Mimi nimeogopa hata kuamua maana mwanamke mwenzangu alikuwa mbogo,nisingeweza kumkaribia. alifafanua mama Kulwa huku tabasamu Pana likionekana Kila alipomwangalia Samson.

Kwani Sam alifanya kosa gani tena,
Maana nimeondoka hapa naacha Kuna amani kabisa. aliendelea kuhoji Mzee Mgaya huku akigundua Samson mkono wake wa kulia kaushikilia na akiwa na majeraha sehemu za mbavu pamoja na uvimbe sehemu nyingi.

Hebu kwanza chezesha huo mkono, kwani umeumia sana mwanangu,kwani ulimkosea Nini mama? mzee Mgaya alimuhurumia Samson

Jana tulikuwa vizuri tu hakuna jambo lolote alilokosea Sam, isipokuwa tangu huyu mwenzangu apewe taarifa kuhusu tabia za Sam alikosa raha huku akionesha hasira za wazi nadhani hali hiyo ilipelekea kufanya maamuzi haya.Na si huyu tu na Rahma naye kalia usiku mzima maana na yeye kapigwa sana tu ni baada ya kumsogelea Samson kumpa pole ndipo alipojitafutia maumivu na yeye. aliongea mama Kulwa huku akionesha kufurahi mno kwa kitendo cha mama Samson kuwaadhibu wale watoto.

Hebu kamuamushe huyo Binti naye nimuone maana huyu Samson kaumia sana , na bado siku chache aripoti shule, anawezaje kwenda na hali hii, halafu mke wanguuuu, umefanya kosa kubwa sana kumuacha huyo shemeji afanye maamuzi haya, angeua je, unadhani Nini kingeendelea? alilaumu mzee Mgaya.

Njoo mama njoo hebu futa machozi basi, enheee niambie ilikuwaje mkaumizwa kiasi hiki? Pole mwanangu, halafu mke wangu hebu fanya mpango niwapeleke Hawa hospital. alishauri Mzee Mgaya.

Mara mama yake Samson alionekana akija usawa walipo akina Mzee Mgaya huku akionesha ametoka kuamka muda si mrefu.

Habari za asubuhi shemeji, alisalimia Mzee Mgaya.

Nzuri tu shemeji yangu, nimetoka kule kwa mdogo wenu nikaona nije kuwasalimu Kisha niendelee na majukumu mengine lakini pia mdogo wako Tausi anakukaribisha sana, anasema atajisikia vibaya kama utaondoka bila kufika kwake. aliongea Mzee Mgaya huku akijichekesha.

Sawa shemeji yangu kwasababu nadhani Leo tulipanga na huyu dada yangu (Mama Kulwa) twende mjini tukaangalie baadhi ya vitu Kisha tutapitia stengi kukata tiketi kwaajili ya safari ya kesho, natamani ningekaa kidogo ila huu ni msimu wa kilimo kijijini kwetu hivyo nalazimika kurudi mapema na pia mdogo wako unamjua alivyo na mdomo ikiwa nitazidisha siku ambazo tulikubaliana. alifafanua mama mzazi wa Samson huku wote wakicheka.

Mimi Nina wazo nadhani kuzidisha siku moja siyo mbaya , nadhani siku ya leo tungeenda kwa Tausi halafu tupitie mjini tukaangalie baadhi ya vitu halafu kesho upumzike huku jioni yake tukikata ticket kwaajili ya safari na wewe uondoke kesho kutwa eeeh usiwe na haraka hivyo dada yangu bado Nina stori na wewe. alishauri Mama Kulwa.

Ni kweli shemeji hata Mimi Nina mizigo ya kumpa mdogo wangu (baba yake Samson)
Na sijaiandaa bado hivyo tungekuomba utuvumilie. aliongeza mzee Mgaya na Mama yake Sam akakubali kwa shingo upande .
Kisha Mzee Mgaya akaondoka na wale watoto Samson na Rahma akiwapeleka hospital.

**************************************

Sasa Doctor mimi nadhani ungenisaidia tu, hawa vijana wangu Wana maumivu makali hapo walipo hivyo nakuomba nipo chini ya miguu yako fanya uwezalo ili wapate unafuu. aliongea kwa upole Mzee Mgaya akimuomba daktari awatibu wale watoto.

Halafu mzee nadhani ni vyema ukawa mwelewa, nikwambie mara ngapi unielewe?
Hiyo ni shambulio kama huyo mtoto wa kiume mkono wake unaonesha umepata madhara makubwa na we wewe unakiri wamepigwa, Sasa jambo ni dogo sana tunalobishana hapa ni kiasi cha wewe kwenda kituo cha polisi ukachukue PF3 kisha watatibiwa Wala hamna shida, nadhani nimeeleweka, okoa muda Nina wagonjwa wengi wanahitaji tiba hivyo siwezi ongea na wewe muda wote huo. daktari aliongea huku akionesha hataki masihara wala mazoea na kazi yake.

Labda nikwambie tu ukweli Doctor Hawa hawajapigwa na mtu baki Bali ni mwanafamilia ambaye ndiye mama wa yule mtoto wa kiume na ni mgeni pale nyumbani kwangu , hivyo kitendo cha kwenda polisi huoni kama tutatengeneza matatizo zaidi , tafadhali Dr. Nisaidie katika hili eeenhee tutalindana Wala hakuna shida, yule Nia yake ilikuwa ni kuwaonya tu lakini akajikuta anazidisha adhabu labda kwa kutokujua, si unajua tena ndugu zetu waishio vijijini sheria nyingi hawazijui. aliongea Mzee Mgaya huku akijipendekeza kwa yule Daktari.

Mzee nikikutazama ulivyo na unavyotaka ni vitu viwili tofauti,

Huyu kijana mbona ni mtu mzima tayari Ina maana hawezi kuonywa kwa mdomo mpaka apigwe Tena kwa kuumizwa kiasi hicho,wote tuna watoto na tunawaadhibu wakikosea lakini ..............
Huyu aliyefanya hivi anadhani ndiyo watamuelewa akipiga kiasi cha kutaka kuua, hebu angalia mkono wa huyu kijana ulivyovimba na hapo nadhani X-rays itahusika. Halafu wewe kirahisi tu unataka usaidiwe, hebu ondoka bwana usiniharibie siku, hizi kazi Zina miiko na taratibu zake au unataka kuniharibia kazi. Daktari aliongea kwa ukali huku Mzee Mgaya akiondoka na vijana wake kwa aibu. akaelekea polisi.

Samahani mdogo wangu nadhani imekuwa bahati kukutana na wewe bila uwepo wa askari wengi,
Hawa watoto wamepigwa Jana na mama yao sasa nimeenda hospital wamenigomea kabisa kutoa tiba , angekuwa doctor Chacha yule angenisaidia lakini Kuna daktari mwembamba hivi mgeni nadhani yaani mgumu kuelewa sijapata kuona. aliongea Mzee Mgaya.

Nadhani yuko sahihi kaka, bila PF3 inakuwa ngumu , halafu na wewe unaogopa nini si ni kiasi Cha kuchukua karatasi tu na kwenda nalo hospital? aliuliza yule afande huku akipekua makaratasi yake na taratibu za kuandika majina zianze.

Kwani kaka na huyu ni Binti yako. aliuliza yule afande huku akimtazama
Rahma.

Huyu ni Binti wa kazi wa pale nyumbani anaitwa Rahma.alijibu kifupi mzee Mgaya.

Mtoto wa kimanga Mali yenyewe kabisa hii , Nina kijana wangu kamaliza chuo na tayari ana kazi yake nadhani huyu angemfaa kabisa na kijana wangu huwa ananiambia hata mke msomi mwenzake anataka wife materia hivyo huyu anamfaa kabisa kijana wangu. afande alionesha hatanii kuongea vile.

Samson mwili ulimsisika huku maumivu yakipotea na donge la wivu likimkaba.

Haaaa jamani afande hebu nipatie hizo karatasi Mimi niondoke yaani ratiba zangu nyingi zinakwama Leo na muda nao unakimbia sana. aliongea Mzee Mgaya huku aliangalia saa yake ya mkononi huku akikata tamaa maana huenda ratiba zake zilivunjika kutokana na masuala ya akina Samson.

Walipata tiba, wakufungwa bandage alifungwa lakini pia Samson hakuvunjika mkono kama daktari alivyosema kabla hajampima Bali ilikuwa ni uvimbe wa kawaida tu,
Walifunguliwa geti huku mama yake Samson akiwa kashaambiwa habari kibao zenye kumuhusu Samson hivyo jazba ikawa zaidi ya ile ya Jana, hakutaka kujua tiba Wala Nini alimrukia Samson huku alitaka kumpiga kwa mara nyingine, lakini Mzee Mgaya alisimama imara.

Haaaaa!! shemeji kama ni adhabu si ulimpa jana, utazua mambo yasiyo ya lazima muache amekuelewa huyu.nafikiri ni makuzi yake tu ikifika muda ataacha Kila kijana ana uelewa na makuzi yake.mimi mwenyewe natambua haya ndiyo maana bado Nampa nafasi ya kukaa naye vinginevyo ningekuwa nimeshamrudisha siku nyingi
aliongea Mzee Mgaya huku akishindwa kumuelewa shemeji yake kwani ana nini.huku akimkata jicho baya mkewe mama Kulwa kwani aligundua ndiye mwenye kuchochea moto ule

Wewe mtoto ni mjinga tena mpumbavu haswa, ni nani mwenye moyo wa kukusaidia ambaye ataweza kuishi na mtu wa aina yako, utachokwa wewe mtoto Hawa watashindwa kukusaidia.
Mtoto umasikini unautaka na kuukaribisha mwenyewe unawezaje kuishi na taahira asiye na akili?
Wakati wazazi wako tunajua fika kuwa wewe una akili timamu?
Umetuaibisha na kutudhalilisha wazazi wako huku ugenini hakika sitaki hata kukuona.mtu gani naambiwa unafanya makosa yenye kujirudia huku ukikosa adabu wewe wa kumgongea huyu mtoto Malaya mbele ya wazazi wako?licha ya kuonywa ukarudia kosa huku mkipeana ujauzito? Loooh
aliongea mama yake Samson kwa uchungu huku machozi yakimtoka .

Rahma alimuomba Mzee Mgaya amsaidie ampeleke kwa Tausi akakae huko hadi mama yake Samson atakapoondoka maana aliona watapigwa wachakae.huku mama Kulwa akishindwa kuficha furaha yake kwa yanayoendelea

Itaendelea..................
 
SEHEMU YA TISINI NA SITA

Baada ya masaa kadhaa kupita huku Samson akiwa anamkwepa mama yake wasikutane kwani hasira yake ilikuwa bado haijaisha.Hivyo Samson akaamua kukaa nyuma ya nyumba huku akiwa na Review fulani mkononi akijisomea labda kwa kupoteza muda.

akiwa pale alishangaa kuona mama yake akimfuata kwa mara nyingine, alitamani kukimbia lakini haikuwezekana, akawa tayari kwa lolote lile akijua kipigo kinafuata kwa mara nyingine hivyo akawa kakubali lolote na liwe huku akihema Kwa uoga sana.

Usiogope mwanangu, wewe ni mtoto pekee wa kiume kwenye tumbo langu, na pia ni mtoto ambaye familia Ina Imani na wewe, dada zako wote hawajasoma ,na hapa napokuambia dada yako Jane tayari kaolewa na kijana mmoja mtoto wa mzee..(akitaja jina)ambapo Samson alimjua.

Na kaolewa kwa shinikizo la baba yako ambaye alianza kumsumbua Jane kuwa kwanini haolewi wakati tayari ana umri mkubwa, nilijitahidi kuzuia hili suala hasa ukizingatia Jane naye alimkataa yule kijana kwakuwa siyo chaguo lake kama alivyodai, lakini tulizidiwa nguvu baada ya baba yako kuhoji kuwa kama alikuwa hamtaki kwanini anakula pesa za yule kijana. alifafanua mama mzazi wa Samson.

Kwahiyo da Jane kaolewa?
aliuliza Samson.

Ndiyo japo nadhani hana furaha na ndoa ile kwani ndani ya miezi kadhaa tumeshasuluhisha ugomvi mara nyingi, na huku dada yako akionesha ana makosa Kila mara.huwezi amini Jane kaweka tumaini lake kwako, akihisi wewe unaweza kuikomboa familia na tukajikuta tupo kwenye nafasi na maisha mengine zaidi ya haya tunayoishi. Hata dada yako mdogo naye anasumbuliwa na baba yako kuwa aolewe , baba yako anadai hawezi kulea mabinti wakubwa ambao walitakiwa kuwa kwenye nyumba zao. Naye huyo haishi kukutaja wewe, akiona ni mkombozi na mtetezi wao.

Cha ajabu nimefika hapa napewa kesi na mashitaka meeeeengi yaani Kila tunachokiwaza tukiwa kule ni tofauti na nilichosikia mwanangu?
Kwani unataka kuwa nani?
Au turudi nyumbani ili ukalime?
Maana hakuna cha maana unachokipigania kwenye masomo yako zaidi nakuona kama mzigo kwa wenyeji kwani hata wao wanaonesha wamekuchoka sana, tena sana tu.
Hata hicho kitabu nadhani umekishika kwasababu nipo Mimi kwasababu nimesikia huna tabia hiyo. Samson wewe ni mtoto wa kiume pekee kwenye tumbo langu, huwa na vile hujafanana na baba yako huku ukifanana na Mimi huwa nahisi na akili utakuwa kama Mimi na laiti ungechukua hata moja ya kumi ya akili na mawazo yangu pengine ungefikiri mara mbili ni nini kilikuleta mjini.

Ni wewe Samson
Ambaye tulipanga na kukubaliana tuchukue mitihani yako hasa ile ambayo ulifanya vizuri tukabandika kwenye Kuta dhaifu ya nyumba yetu lengo tumshawishi baba yako mkubwa ili akusaidie, ni kweli alirudi japo alilewa lakini aliweza kupitia baadhi ya makaratasi na kujiridhisha kuwa atakusaidia. Lengo letu lilitimia huku familia nzima ikikuombea na ikiweka tumaini kwako.

Lakini bado ulitokea ugumu baada ya jina lako kuuzwa kwa watu wengine, Lakini namshukuru shemeji yangu alipambana hadi akafanikiwa,
Samson kwani mwanangu unataka kuwa nani kwenye maisha yako na huu ulimwengu?
alimaliza kwa mfumo wa swali mama yake Samson.

Samson aliinuka na kumkumbatia mama yake huku akilia kwa sauti kama mtoto mdogo,

Mama nisamehe, mama nisamehe nahitaji baraka zako, nahitaji huruma na nafasi ya mwisho, mama niombee msamaha kwa dada zangu, niombee msamaha kwa mama Kulwa, naomba fanya hivyo mama nahitaji kusoma, naomba nipewe nafasi ya mwisho. Samson alilia kwa sauti huku akimng'ang'ania mama yake kwa nguvu akihisi anamuacha.alihisi Dunia inamuelemea huku kimbilio pekee akiwa ni mama yake.

Mama Kulwa alisikia sauti ya kilio ikabidi aje aone kuna nini.

Jamani ndugu yangu mbona unamuadhibu Kila mara huyo mtoto kwanini. Mama Kulwa aliuliza huku akionesha kukerwa Sasa na tabia ya mama yake Samson, lakini alipowakaribia zaidi aligundua wapo kwenye amani na Samson analia kwa hisia zake tu akaamua kuwaacha tu na kurudi ndani.

Baada ya muda mama Samson alimfuta mwanaye machozi kwa kitenge chake huku Samson akiwa kapiga magoti.

Mwanangu nakupenda sana, najua ujana umepelekea yote haya ila NAKUSAMEHE. na kumbuka umekiri makosa na umeniahidi kutorudia naomba uzingatie masomo yako, hii ni kwa faida yako na familia yako utakayoijenga , pengine Mimi nitakuwa nikeshakufa unadhani Mimi nafanya haya kwaajili yangu?
Tazama dada yako kaolewa na yule kijana masikini kabisa unadhani ni lini watajikomboa na umasikini, kwa kile kilimo cha mkono?

Samson alimuelewa sana mama yake, na aliendelea kuuliza habari za kijijini kwao huku alikijibiwa vyema na mama yake, walipiga stori kibao pale nyuma ya nyumba ya Mzee Mgaya Kisha wakarudi ndani na kumkuta Sarah pekee, kwani mama Kulwa alipumzika na Rahma muda wote alikuwa anajifungia ndani kwa kumuogopa mama yake Samson.

Mama nataka nikuoneshe mitihani yangu tangu kidato cha kwanza mpaka cha tatu. aliongea Samson kwa furaha baada ya kugundua mama yake amesamehe na kuachilia.

Sasa mwanangu samuuuu, hata ukileta Mimi nitaelewa nini, kusoma sijasoma. alijibu Mama yake Sam.

Hapana najua umeishia darasa la saba Nina Imani utaelewa tu, Samson aliileta mitihani yake , yaani burungutu la makaratasi, Kisha wakawa wanapekua huku Sam akimuonesha namna ambavyo hafanyi utani shuleni.

Na hapa mama nikwambie, baba mkubwa kanitafutia shule nyingine nzuri zaidi tena imejizolea sifa za kufaulisha japokuwa siyo ya miaka mingi. Samson alimwambia mama yake.

Sawa, Mimi nitazidi kukuombea na pia wewe uache tabia zisizoendana na maadili yanayotakiwa.

Samson alimwangalia Mama yake Kisha wote wakatabasamu huku furaha ya mama Samson ikirudi vilivyo, kumbe wakati wapo pale nje , mama Kulwa na Rahma walikuwa mlangoni wakishangaa mtu na mwanaye wamepatana saa ngapi?
Kwani kila mmoja alifurahia ile hali.

Mama Kulwa alisogea taratibu huku akitabasamu akiwaangalia watu wale kwa zamu, yaani mwanamke mwenzangu wewe ulivyokuwa msichana sijui ulikuwaje, maana mmmmh na sura ya Sam mtoto wa kiume ndiyo hii je hao wakike watakuwaje? aliuliza mama Kulwa huku wakigonga mikono na mama yake Samson wakicheka.

Basi huwezi amini watoto wakike wamefanana na baba yao eti, ni huyu tu alifanana na Mimi. alijibu Mama yake Sam.

Wakati huo Rahma naye alikuwa anasogea taratibu mahali walipo wale watu watatu huku akiwa makini kama mama Samson akitaka kuleta timbwili yeye akimbilie ndani, lakini aligundua mama Hana kinyongo na habari zote zimeisha.

Wewe Binti kamlete huyo mtoto nimuone maana Mimi ndiye mkweo rasmi, nataka nione ni wa kwetu au umembambikia mtoto wangu. aliongea kwa utani mama yake Samson.

Lakini jina anaitwa Jackline , nimeamua kumpa jina langu vipi inakuwaje, maana mwenye mjukuu kamili umefika. alitania mama Kulwa.

Usijali hilo jina kwanza ni zuri tu, lakini pia ulistahili , kwani uvumilivu wako kwa Hawa watoto licha ya kuwa walikutia aibu na kukuudhi lakini bado ukawakumbatia, bado ni upendo na uvumilivu usiopimika kwanza nikupongeze na nikushukuru sana. Huyu atabaki na hilo jina lako.
aliweka kituo mama mzazi wa Samson.

Mzee Mgaya alirudi akashangaa namna familia ilivyokuwa na furaha siyo Sam Wala Rahma, si Mama Kulwa Wala mama yake Sam, wote walikuwa wanaongea huku wakionesha furaha sana, huku Sarah akiwa bize akitimiza wajibu wake. Mzee Mgaya aliwaangalia wote kwa zamu Kisha akatabasamu na kuingia chumbani kwake.

Itaendelea.......................
 
Moto uendelee

Sent from my SM-N950U using JamiiForums mobile app
 
Nimerudi rasmi kuchukua nafasi yangu.....
20230325_014255.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom