Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA KUMI NA NANE

Karibu mheshimiwa, karibu sana.
alikaribisha afisa elimu huku akionesha unyenyekevu fulani kwa mkuu wa wilaya.

Ahsante sana,tumekaribia.alijibu mkuu wa wilaya yule.

Waliingia ofisini mule huku vijana walibaki nje ya ofisi ile, mle ndani wakawa watu wanne, yaani
Mkuu wa wilaya,
Afisa elimu,
Mwalimu Agness na
Mzee Mgaya.

Ndugu afisa elimu wetu, najua tuna sikukuu hii kubwa ambayo inatufanya tupumzike na familia zetu majumbani . lakini pamoja na hilo bado tunahitajika kwenye hizi ofisi ili kutoa huduma kama watumishi wa umma na huu ndiyo utumishi wenyewe hivyo usishituke na ujio wangu. aliongea DC na kuweka kituo.

Bila shaka mheshimiwa, najua ni lazima tufanye hivyo Kila panapobidi.
aliongea yule afisa Elimu huku kijasho chembamba kikimtoka maana kitendo cha kumuona Mzee Mgaya pale akajua tayari mambo yameharibika.

Nimekuja huku kutatua au kuweka wazi mkanganyiko wa majina ya mtoto wa huyu mzee, maana matokeo yanaonesha amefaulu, lakini Kuna taarifa na matokeo ya shuleni kwao yakionesha hajafaulu, wakati ngazi ya mkoa na wilaya jina lipo Sasa tunaomba ndugu Ofisa tuondolee hii sintofahamu.DC akaweka kituo.

Afisa elimu aliinuka huku akiwa tayari hayupo sawa , akalisogelea kabati fulani lililokuwa na mafaili mengi akawa anajaribu kutafuta kitu ambacho hata yeye hakujua anatafuta Nini. Ile hali mheshimiwa DC alitambua akaona anaenda kuaibika mtu, akaamua kuwatoa watu wengine nje ili waongee wawili, hivyo mzee Mgaya na mwalimu Agness wakaambiwa watoke wataitwa.

Unajua ndugu yangu, wewe ni Ofisa mkubwa unayeaminika sana, kitendo mlichokifanya ni Cha aibu na pia ni kuidhalilisha wilaya, kunidhalilisha Mimi nionekane sifai, sifanyi kazi, lakini pia ni kuiabisha wizara ya Elimu na baraza lake la mitihani.
Kwa namna nikujuavyo sikufikiria kama utakuwa hivi, Sasa bila kupoteza muda naomba taarifa sahihi za ufaulu wa jina la Samson Elias Mgaya.nimeamua kukustahi kwa kuwatoa nje wageni lengo usipate aibu lakini Kila kitu kipo wazi. Aliongea kwa ukali DC.

Samahani, tena samahani sana mheshimiwa DC, jambo hili nililetewa likiwa lishafanyika na Kuna mwalimu mmoja ambaye umemtoa nje Sasa hivi ndiye ambaye anajua mlolongo mzima alijitetea yule afisa ili msala usiwe wake pekee.

Akaitwa mwalimu Agness, na kuingia ndani.

Wewe ni nani na unahusika vipi na kadhia ya mkanganyiko wa majina ya wahitimu, aliuliza kwa kukaza macho mheshimiwa DC.

Mimi naitwa mwalimu Agness, ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi(jina kapuni).alijibu

Kwahiyo kazi yenu ni kugeuza geuza majina ya wanafunzi kwa kuwaambia wamefeli wakati si kweli huoni kama ni kitendo kibaya sana kinachangia kudidimiza vipaji vya watu wengine huku wakishindwa kutimiza ndoto zao kwaajili yenu nyinyi msio waaminifu?

Sasa tuko hapa na tambueni kuwa siku zinazidi kwenda yaani shule zitafunguliwa na si siku nyingi nachokuombeni ni kwamba tunahitaji matokeo halali ya Samson Mgaya. aliweka kituo mheshimiwa DC.

Afisa Elimu na mwalimu Agness waliangaliana kwa uoga huku wakishindwa waanzie wapi, maana kama joto lilikuwa joto kweli kweli.

Mkuu wa wilaya aliinuka huku akiwapa muda wa masaa sita wawe wameshakamilisha Kila kitu.
Kisha wakaondoka na gari wakatokomea.

Aiseeeh yaani tangu ulivyoniambia Jana nilidhani labda watakuwa wamechanganya majina tu, kumbe kweli, nitahakikisha nakula nao sahani moja maana hatuwezi kuiendekeza hii hali tutaonekana watumishi wazembe, aliongea kwa uchungu DC akimwambia mzee Mgaya.

Ni kweli, haya mambo yapo siku nyingi sana lakini nadhani ni wakati muafaka kukomesha hii tabia, na nikuombe kitu mheshimiwa, ni kwamba huyu mtoto namuhamisha kwahiyo nahitaji vielelezo vyote vitakavyo hitajika ili tukifika mjini Dar es salaam kusiwe na longolongo nyingine. alisema James Mgaya.

Hilo halina shida, kwanza nashukuru, kwa kuweza kusaidia kuibua huu uozo, unadhani ni watu wangapi wananyanyasika na hawana pa kusemea, lakini pia nikupongeze kwa kubeba jukumu la kusomesha mtoto wa ndugu yako, ni wachache wenye moyo huo. aliongea yule mh, DC huku wakigonga mikono na kucheka.

***************************************

Mwenzangu hapa inabidi tufanye haraka, tambua hakuna jambo ambalo litawezekana bila kuwepo mratibu wangu lakini pia yule tajiri unayemuita kaka yako inatakiwa apatikane tumweleze hali halisi asije akaona kama tunamzunguka, Aliongea afisa elimu huku akiwa na hofu kubwa wakatoka kuelekea nyumbani kwa mratibu Elimu ambaye alikuwa ni wa tarafa ila akiwa anatumia ofisi moja na afisa elimu wa wilaya.

Walitoka kwa miguu wakitembea hadi kwa mratibu wakamkuta akiwa na tafrija ndogo nyumbani kwake , akawakaribisha ndani.

Vipi ndugu yangu afisa, pamoja na kukualika Mara mbili mbili lakini nimeshangaa huyu mtu mbona hatokei? Lakini si mbaya bado hujachelewa sana, karibuni sana.
aliongea maneno yale yule mratibu akidhani afisa kaja kwasababu ya mwaliko kumbe alikuwa na mambo mengine kabisa.

Mwenzangu hayo achana nayo, mambo yameharibika, Tena unayemuona hapa ni mwalimu Agness katoka huko kijijini kwaajili ya kuja kuweka sawa Yale masuala, Sasa basi naomba kujua kama zile taratibu za uhamisho wa jina la Samson ambaye anatakiwa akasome Kilimanjaro vipi zimekamilika? Maana tunahitaji kuzitengua, huwezi amini mheshimiwa DC katoka ofisini kwangu muda si mrefu,kutoa vitisho na katoa six hours only tuwe tumeshakamilisha na kama unavyomjua Hana dogo kabisa. aliongea yule afisa huku akitetemeka.

Sawa, nimekusikia ila sikufanya kitu kwasababu uliniambia kuwa watu walikuja kudai jina hili hivyo tukashauriana tusifanye chochote, Hadi watu wale wapotezee, hivyo bado hata hivyo yule tajiri bado anaulizia taratibu zikoje maana tunamchelewesha anahitaji kupeleka taarifa kamili. aliongea mratibu huku nae akiwa kanyongea tayari hata furaha ya tafrija aliyoiandaa ilitoweka alishakuwa kikaangoni.

Afisa elimu alishusha Presha baada ya kusikia kumbe mratibu hakuwa kafanya chochote, ikabidi waongozane warudi ofisini safari hii wakiwa watatu,

Sasa mwalimu Agness, tulikwambia unapocancel jina na mtahiniwa hakikisha unaangalia yule wa kwenye familia masikini ambaye Hana uwezo wa kumsomesha mwanae, sasa wewe umeenda kinyume unaona aibu tunayoipata, na kazi zetu zipo hatarini ujue. alilaumu yule mratibu.

Wewee huwezi amini hii ni familia choka mbaya sana, lakini Kuna ndugu yao katoka mjini wewe mratibu hujamuona , ni mjuaji mno nimejaribu mbinu nyingi kumkatisha tamaa lakini haijasaidia kitu.
alijibu mwl Agnes.

Jamani haya malumbano Wala hayasaidii Mimi hapa nawaombeni mkamilishe hizo taratibu ili yule jamaa akija aje achukue barua yake na mkumbuke kuwa anamuhamisha hivyo bado Kuna kuandika habari za uhamisho ila hadi waje wenyewe.

Wote watatu baada ya kuweka mambo safi walijikuta Kila mmoja akiwaza lake, hakuna aliyemuongelesha mwenzie,
Hakuna aliyeisikia njaa ikimuuma
Kila mtu aliwaza namna walivyorisk kazi zao,walikuwa kwenye mawazo sana wanaume wawili na mwanamke mmoja.

************************************
Mzee James Mgaya alikuwa nyumbani kwa DC, wakiwa wanavuta vuta muda ufike ili wakachukue ripoti kwa afisa elimu.Walikuwa wanakunywa mvinyo huku wakipiga nyamachoma zilizotengenezwa kiufundi sana.

Kula nyama ndugu yangu, kula.
Ujue mwanzo nikipata taabu sana pindi naingia kwenye mkoa huu nilikuwa sili nyama zingine zaidi ya kuku , maana najua sifa ya wenyeji,wanaweza kukuchanganyia na nyama zingine. aliongea mheshimiwa DC kiutani na kumfanya mzee Mgaya acheke sana.

Baada ya kufanikiwa kuchukua barua ya ufaulu wa Samson pamoja na taratibu zote za uhamisho, ambazo zilimfanya akae wilayani kwa takribani siku nne, hatimaye alirudi huku akiwa na furaha sana, alivuta picha namna atakavyopongezwa na familia ya mdogo wake kwa kufanikisha Yale ambayo walidhani hayawezekani.

Baada ya kufika aliwakuta wote wakiwa nyumbani wamepumzika baada ya kazi nyingi za kutwa nzima kama ilivyo desturi ya shughuli za kilimo vijijini. alishangaa kuona watu hawamchangamkii kama siku za nyuma, ikabidi avunje ukimya.

Kwanza poleni na kazi ndugu zanguni, na pia tunapaswa kumshukuru mwenyezi MUNGU kwa kuwezesha kufanikisha suala la Samson. niseme tu hatimaye Samson anakaribia kujiunga na kidato Cha kwanza. aliweka kituo

Kaka, hapana mwanangu haendi sehemu wewe kama unaondoka , nenda tu niachie mwanangu, Mimi baba yake Nina Kila kitu Nina Mashamba, wala hayana mwenyewe mtu pekee atakayelima na kuyaendeleza ni Samson. aliongea Baba yake Samson akiwa hatanii.

Ni kweli shemeji, tumejadili tumeona wewe nenda tu huyu tutabaki naye. alikazia mama Mgaya.

James Mgaya aliwaangalia wote kwa zamu huku akiwahurumia, alitikisa kichwa kwa masikitiko, alikaribia kukata tamaa, akamuita Samson Kisha akamuuliza,

Mwanangu unapenda shule?
Samson hakujibu ila alikuwa aliwaangalia wazazi wake , kana kwamba ndio waliomuuliza, huku baba yake akiwa bize na kuchonga mpini wa jembe na mama yake akiwa anasuka kikapu.

Samson baba mkubwa si kakuuliza?
Mjibu basi, aliongeza Jane dada yake Samson.

Samson alitikisa kichwa kuonesha hataki shule.
Sumu aliyoimwaga baba yake Samson ilikuwa Kali kiasi Cha kuibadilisha familia yake na kuwa na msimamo wa kijinga.

Itaendelea...............
 
umetukumbuka,shukran mkuu
 
Unadhabi wote hawana kazi za kufanya kama wewe
Afuu hii ni burudani Wala hatumlipi anafanya kwa upendo tuu ashakwambia ana majukumu kibao Kaa kwa kutulia
Jamaa ni injinia wa Tanroad huyo kwahiyo majukumu yanambana halafu mnaopenda Simulizi sio kila mwandishi ni jobless humu
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA

Usiku wa siku hiyo, James Mgaya hakupata usingizi mapema, alisikitishwa na aina ya maamuzi ya ndugu/mdogo wake. alishangazwa na maamuzi ya shemeji yake ambaye mwanzo alikuwa kipaumbele mwanae asome.

Alishangazwa pia na mtoto mwenyewe {Samson} maana mwanzo alionesha kupenda shule lakini kwanini anakataa?
Haikumpa tabu ya kugundua nani kaeneza na kumwaga sumu ile. alifikiria mambo mengi sana.

Hadi inafika saa saba usiku, alijikuta yupo macho akaamua kutoka nje, maana tayari alikuwa na hasira sana,

**Nimehangaika kwenda wilayani Kila mara, nimepoteza hela zangu nyingi kwaajili ya nauli za hapa na pale, mbaya zaidi Kuna shughuli nyingi zinakwama nyumbani kwangu , nikiwa nacheleweshwa na suala la mtoto huyu.
Hakika najua kwa yote niliyoyafanya sikutegemea kama nitapigwa mateke wakati nafanya jambo zuri kwa manufaa ya mtoto wao .
alijiwazia James Mgaya.

Alianza kuizunguka nyumba ile ambayo imeezekwa kwa makuti Lakini pia ilikuwa fupi mno, alikumbuka maneno ya mdogo wake aliyomwambia kwamba urithi wa mwanaye ni Mashamba pamoja na vile vibanda alijikuta anacheka Tena kwa sauti kubwa tu huku akimuhurumia sana mdogo wake kwa kuwa na mawazo ya kijima. wakati anawaza kurudi ndani, Baba yake Samson alitoka,

Nimesikia vishindo nje, nikaona nitoke, maana nilikuwa na wasiwasi tusije kuibiwa mifugo yetu bure, kumbe ni wewe kaka, vipi tena usiku huu wa manane unafanya nini nje?
Mbona unanitisha kaka.
aliuliza baba yake Samson ambaye alikuwa kavaa kitenge Cha mkewe huku akishika panga mkononi tayari kwa ambalo lingetokea.

Najisikia vibaya nahisi nina homa ndiyo maana nikatoka nje, ila najisikia nafuu. James Mgaya alijitetea wakarudi ndani.

Asubuhi ilipofika mzee James Mgaya aliwaita familia nzima,

Ndugu yangu,
Shemeji yangu,
Lakini pia wanangu wote nawaomba niwaambie jambo moja kuhusu umuhimu wa Elimu.

Watu wanafanya juu chini kuhakikisha wanaisaka Elimu kwa udi na uvumba, na ndiyo maana wapo ambao wapo tayari kutoa gharama kwa kununua majina ya wanafunzi waliofaulu kusudi yawasaidie kufika walipofika.

Hata maadui watatu aliowahi kuwazungumzia hayati baba wa taifa hili, maadui wote wanasababishwa na umasikini, na hata haya maisha mnayoishi nyinyi hapa kijijini ni mabaya na yasiyofaa kabisa ingawa nyinyi mmeyazoea.
Nimejitolea kuwasaidia, nimepambana na kuhatarisha kazi za watu kwaajili yenu, leo hii ndugu yangu unakosa hata aibu, kwa kunikataa wazi wazi,
Wakati nafika hapa mliniambia kuwa mtoto alitoroka na kwenda kusikojulikana, yote haya yanasababishwa na umasikini uliokithiri kwenye hii nyumba, wewe mtoto kama huyu anawezaje kuhangaika na vibarua?

Ila nisiongee sana, nimewaita ili niwaage, nilikuja kwaajili ya nyinyi ndugu zangu tule sikukuu kwa pamoja, nilihitaji kufurahi na nyinyi lakini haikuwa hivyo nilijitia huruma ambazo ziliniponza nikajikuta hata sikukuu inanikuta nje ya sehemu niliyoilenga na kuikusudia, naomba mnisamehe kama Kuna sehemu nimewakwaza katika kipindi chore nilichokaa, niseme tu kuwa Mimi ni binadamu tu, ujuaji wangu kama unavyoniita mdogo wangu umeniponza. aliongea kwa hisia sana James Mgaya.

Hapana shemeji Wala wewe huna kosa Bali ni mtoto wetu ambaye alibandika matokea yake ya mitihani mbalimbali, kusudi lake lilikuwa uone ili umsaidie, ni kweli ulianza kutupambania, lakini anayeinyong'onyesha familia na kuikatisha tamaa familia ni mume wangu.
aliongea bila uoga mama Mgaya.

Baba yake Samson hakuwa na lakusema aliona tu aibu akawa anatizama chini tu.

Hapa hakuna mjadala shemeji naomba umchukue Samson , sisi tunakuamini, angekuwa mtu Baki nisingekubali akae na mwanangu lakini Mimi Nina Imani na wewe , mama Mgaya alizidi kakazia.

Na wewe ndugu yangu unasemaje, au unanihakikishiaje , maana shemeji si mzazi pekee anayeamua nahitaji kusikia ruhusa yako. alisema James Mgaya.

Mimi Sina shaka ila nahitaji usalama wa mwanangu tu basi hakuna lingine, .alisisitiza mzee Mgaya au baba Samson.

***********************************
Mzee Mgaya na kaka yake walitoka wakielekea kwa baadhi ya majirani akiwa anaaga tayari kwa kusafiri mchana ule ili wakalale Mafinga mjini au wilayani.

Nafasi mama Mgaya aliitumia kuongea na Samson.

Samson mwanangu,
Unaondoka hapa familia nzima inajua unaenda kusoma , hatuhitaji kuja kupokea kesi na malalamiko kwamba husomi, kumbuka Leo watu hawaelewani kwaajili yako, hata mazungumzo yao yamejaa unafiki , baba yako kakuruhusu kishingo upande tu, hivyo ili utuaminishe na kututoa wasiwasi inatakiwa ukasome kwa bidii.

Lingine unaenda mjini sehemu ambayo ina watu wa Kila aina, Kuna watu wema na wazuri , lakini wapo makatili wasiojali utu na ubinadamu wa mtu hivyo kuwa makini sana kosa dogo utajikuta unagharimu maisha yako.

Samson nakujua mwanangu una tabia ya udokozi , unakumbuka ulikutwa unaiba miwa kwenye shamba la bibi maria? aliongea Mama Mgaya.

Lakini ulisamehewa kwa kuwa wanakijiji wanakujua wewe ni mtoto wa nani, Sasa mjini ni tofauti kule ukiiba unapigwa na utakufa mwanangu, naomba kazingatie kilichokupeleka. (aliongea Mama Mgaya akiwa ananyoosha nguo za Samson na kuziweka kwenye kibegi fulani kikuukuu, kwaajili ya safari.

Nimesahau kuhusu kuishi na wenye nyumba, Sam, Sam mwananguuuu,
Tambua unaenda kuishi na mama mwingine siyo Mimi, Mimi nikikutuma huwa unanigomea, lakini Kuna muda nakuacha tu Sasa kama unataka milango yako ifunguke ili ufanikiwe kwa lililokupeleka tafadhali ukawe na heshima na adabu.

Kule hakuna mama yako wala dada yako, na baba yako unamuacha hapa unaondoka na huyu baba mkubwa na nadhani unamjua alivyo mkali, Sasa ukamletee za kuleta, watoto wake mwenyewe wanamuogopa, sembuse wewe Samson.

Maneno yale yalimtisha Samson na kumtetemesha, hasa suala la udokozi alijijua ana hiyo tabia hivyo akapanga kuacha kutamani kitu Cha mtu mjini ingawaje hakujua mji unafananaje.

Itaendelea...............

Sent using Jamii Forums mobile app
 
moneytalk
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom