SEHEMU YA TISA
Masoud na wenzake wawili walirudi kutoka kituo cha polisi huku wakiwa wamebaini vitu vingi sana,
Kwanza hakuna sura hata moja waliyoiona Kati ya zile zilizokuja kwao Jana yake. lakini pili polisi walionekana kushituka na majambazi hao wanaoonekana kwanza ai wenyeji wa mji ule.
Huku wakitoa Rai kwamba kama vijana waishio Kambi ile wapo wengi, wanao uwezo wa kuwazunguka kama watarudi Tena ili wajae kwenye mikono ya sheria, lakini pia wakaonya kuwa huyo kijana apelekwe kwao na wao wawe na tahadhari.
*********************************
Watu kutoka sehemu mbalimbali katika Kijiji cha kwa kina mzee Mgaya walikusanyika huwa taarifa za uwepo wa mganga wa jadi mwenye uwezo wa kumrudisha Samson,
Kila mmoja alikuwa na hamu na shauku ya kutaka kuona maajabu hayo ambayo kiuhalisia hayawezekani.
Michango ya kuweza kununua kondoo ili kazi ianze Mara moja ilifanyika haraka sana, watu walichanga si kwakuwa Wana pesa nyingi Bali ni kwasababu walitaka kuiona sinema ambayo ingeweka kumbukumbu na rekodi isiyofutika ya mtu kupotea kimazingara na kurudishwa.
***********************
Saa kumi na moja alfajiri Masoud na Samson walikuwa kwenye bus au gari la abiria lifanyalo safari zake Madibira to Mafinga, lengo washuke kijiji cha jirani na washike njia kuelekea nyumbani kwa kina Samson , huku wengine wakiwa wanaagana Kisha kushika njia ya kuelekea kambini kwao.
Mida ya saa nne za asubuhi watu waliahirisha shughuli zao za kulima katika msimu ule wa mwezi wa kumi na mbili, wengi waliacha kazi zao huku wakielekea kwa akina Samson huku idadi ikiongezeka kama vile Kuna msiba.
Wakati watu wengi wakiwa wameyazunguka yale mafiga matatu huku chungu kikubwa kikiwa kinachemka nyama iliyochanganyika na dawa fulani huku pembeni ya kile chungu kukiwa na pembe kubwa ya mnyama wa porini ambaye hakufahamika ni mnyama gani, huku mganga akiwa katulia tu pembeni kazi ya kuchochea moto ilifanyika na wasaidizi wake ambao walifanya manuizi Kila baada ya dakika tano wakipuliza ile pembe kama ishara ya kumuita Samson.
Ilifika muda kama saa tano hivi mganga aliinuka kwenye kiti Chake na kuizunguka ile nyumba huku akiwa na kioo kilichozungushiwa shanga zikionekana ni chafu yaani zimefungwa zamani sana, aliendelea kumulika huku na huko kisha akageukia mlimani akiwa ameganda kwa muda huku akitamka maneno fulani ya majigambo kwa sauti mithili ya wachungaji wanavyoombea watu.
Watu wote walikuwa makini wakifuatilia Nini kitajiri kwenye lile zoezi.
Mama wa kijana aliyepotea hebu sogea hapa, aliamrisha mtaalamu yule.
Mama Mgaya alisogea kwa unyonge akapiga magoti kama alivyoelekezwa ikaletwa nyama ile iliyochanganyika na dawa akaambiwa kwakuwa yule ndiyo mama mzazi wa muhusika anatakiwa awe wa kwanza kula nyama ile akafanya kama alivyoagizwa.
Aje na baba halali wa mtoto aliyepotea.
Mganga aliagiza tena.
Alisogea mzee Mgaya akiwa na koti lake kuukuu kabla hajatia kipande Cha nyama mdomoni mganga alimuuliza swali.
Je, wewe ni baba halisi wa mtoto?
aliuliza mtaalamu.
Swali lile Mzee Mgaya hakutegemea swali lile akabaki anacheka cheka tu Kisha akatingisha kichwa kuashiria ni mwanae wa kumzaa.
Sikiliza mzee wangu manuizi ya dawa niliyofanya inawalenga wazazi halali tu, kama huyu si mwanao pengine mke wako alizaa nje ya ndoa na wewe ukaona kwakuwa kitanda hakizai haramu ngoja nilee tu, ndugu yangu hapa hupaswi kula hii nyama maana utapata matatizo.
aliongea yule mtaalamu akawafanya watu wacheke huku mzee Mgaya akiwa na huzuni, kwani hakujua afanyaje.
Mama Mgaya aliropoka kwa sauti kali akimweleza mganga kuwa huyo ni baba halisi wa watoto wake wote anaowaona hakuna mtoto wa kumtilia mashaka hata kidogo. hivyo asingependa kudhalilishwa.
ni kweli maneno ya mtaalamu yule yalimdhalilisha mama Mgaya na hata mzee Mgaya pia.
Basi zoezi la kula nyama liliendelea kwa Kila mwanafamilia huku mtaalamu akiagiza kila Mmoja ale kwani mtu ambaye watamuona alikuwa sehemu isiyo ya kawaida hivyo unapoangalia kitu kilichokuwa kwenye ulimwengu mwingine unapaswa kula ile nyama watu wote waligombania nyama ile huku hatua zingine za kumrudisha Samson zikiendelea.
Samahani mtaalamu muda unazidi kwenda vipi zoezi litachukua muda gani hadi kurudi kwa huyo kijana?
aliuliza mwenyekiti wa Kijiji ambaye alitoa kibali Cha kufanyika shughuli ile iliyowakusanya watu wa Kijiji kile.
Wewe tulia hii kazi ni nzito Mimi hapa huyu kijana najaribu kumuangalia kwenye vyombo vyangu namuona kabisa tena amekonda sana na hapa hiyo nyama waliyokula wazazi wa huyu kijana inaanza kushindana na mizimu na ninavyoona mizimu inakaribia kushindwa na kwa muda wa siku kama tatu atarudi. alijibu mganga huku baadhi ya watu wenye akili timamu wakishindwa kuridhika na majibu yale.
Mganga aliendelea kufanya vitu vyake huku watu wakiwa na Imani kubwa sana ya kurudi kwa Samson .
Lakini kitendo Cha mganga kubainisha wazi kwamba kwa mujibu wa vipimo vyake Samson aliko amekonda sana na pia matumaini ya kurudi ni siku tatu baadaye
Familia ya nzima iliumia mno tena sana .
******************************
Masoud na Samson walijikuta wanachelewa kufika kutokana na gari kuharibika njiani maeneo ya kijiji fulani kinaitwa Igomaa, siyo Igoma ya mwanza Lakini, walisubiri matengenezo ya gari bila mafanikio yeyote hadi saa tatu za asubuhi hatimaye wakakubaliana waanze kupiga mguu wakajikuta wanatumia muda mwingi njiani.
Mida ya saa nane mchana waliikaribia nyumba ya akina Samson huku wakishangaa kundi la watu wanaoonekana umbali wa mita mia mbili hivi.
Wewe dogo unasema pale ndiyo nyumbani kwenu , mbona kama hamna usalama pale.
aliuliza Samson huku akipunguza hatua za kutembea maana hisia zake zilimtuma tofauti.
Ndiyo pale ndiyo nyumbani na sijui Kuna Nini pale, alijibu Samson huku wakizidi kuikaribia nyumba yao.
Mara majirani wanaomtambua Samson wakiwa pembeni pembeni ya nyumba walimuona Samson akiongozana na watu wawili watu wazima wasiowafahamu .
Jamani Samson mwananguuuuuuuu ilikuwa ni sauti ya jirani Mmoja mwanamke ambaye alikuwa wa kwanza kushindwa kujizuia watu wote waligeuka kuwaangalia wale wageni huku wakipigwa na butwaa zito lililokosa majibu, wapo waliojaribu kukimbia wakidhani ni mzimu lakini walirudi baada ya kuona kijana wa watu ni mzima wa afya.
Watu walilia kwa kupokezana haikujulikana ni machozi ya aina gani ila Kila mtu alilia kwa namna yake huku mama yake Samson akiwa kazimia muda mwingi tu baada ya watu kunyamaza, walimgeukia mganga/mtaalamu wakiwa na nyuso zilizoashiria shari, huku mganga akiwa kabadilika sura na ana uoga ndani yake.
Itaendelea..........................