SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
Baada ya muda fulani mzee Mgaya alikuwa na Samson, kwenye gari huku akiwa na mawazo juu ya mkewe mkubwa kuwa na mawazo mabaya kwa Tausi.
Mama Kulwa sijui yupoje yaani, miaka yote kumsingizia Binti wa watu kuwa anamroga, yaani utu uzima wake wote anashindwa kuwa na busara na kuyaacha haya yapite? Hata kama ana chuki moyoni mwake maana asilimia nyingi wake wenza huwa hawapendani, lakini ndiyo aoneshe chuki hadharani vile kiasi Cha kuwazuia watoto wasiende kwa mama yao mdogo?
Hii chuki na mbegu mbaya anayoipanda baadaye itakuja kuisambaratisha familia nafikiri kuna haja ya kufanya kitu kabla mambo hayajaharibika. aliwaza mzee Mgaya huku akikata kona kuingia barabara kubwa.
Kwa upande wa Samson yeye shingo ilikuwa na tabu ya kugeuzwa Kila muda, kutokana na kushangaa majengo makubwa ambayo hakuamini macho yake huku Dar es salaam aliyokuwa akisimuliwa ikiwa tofauti na anavyoiona.
Walipokelewa vizuri na Tausi huku, akionesha tabasamu zuri la upendo kwa wageni wake.
Jamaaani my husband karibuni, karibu tena, bila shaka huyu ndiye mgeni wetu Samson.
aliongea kwa mbwembwe huku wageni wakikaribishwa moja kwa moja kwenye meza ya Chakula.
Eeeeeh uko vizuri mwenzangu ulijuaje kama Nina njaa maana nimejikuta nazunguuuuka mjini hata breakfast sikupata.
aliongea Mzee Mgaya huku akiwa na pupa ya kujipakulia mwenyewe kile Chakula .
Lakini my haya yote sikufanya kwa bahati mbaya uliniambia kwamba utakuja na wageni, Tena uliniambia na akina Kulwa watakuja , vipi mbona ....... alijikuta anashindwa kumalizia sentensi yake huku akimwangalia mumewe kwa makini.
Akina Kulwa unawafahamu, hivyo mgeni ambaye ilikuwa lazima afike hapa ni huyu kijana Samson.
alijibu Kwa mikato.
Unajua nimeandaa Chakula kingi kwa kuzingatia idadi ya watu, kwakuwa uliniambia mwenyewe, kwahiyo hiki kinaenda kuharibika tu masikini.
aliongea Tausi huku akilifunua Hotpot lake na kuangalia jinsi Chakula kilivyokingi.
Hivi ni vyakula tu mke wangu, yaani unasikitika hizo kilo mbili zako za mchele? Mwaka fulani kwenye birthday ya my first born niliwahi kualika watu kwenye tafrija ndogo iliyohusisha mambo mawili kwanza ulikuwa birthday yake, pili alikuwa katoka kumaliza chuo hivyo tukamfanyia kasherehe fulani,
Majirani walialikwa, na watu wengi mbalimbali lakini ilipofika saa tano asubuhi ukatokea msiba mzito wa jirani yangu marehemu mzee
(akimtaja jina)
Basi watu wote tulisitisha zoezi la tafrija majirani wakaondoka kuelekea mita kama miatano tu ulipo msiba, hata Mimi na mama Kulwa tuliiahirisha tafrija yetu tukaelekea kwenye msiba ule wa mtu mzito, hakuna aliyekuwa na hamu hata ya kula Tena.
aliweka kituo mzee Mgaya
Nakumbuka sana, Kuna baadhi ya watu wachache walichomoka msibani na kuja kugonga geti ili mwanao awapakulie chakula nasikia walikula na kusaza lakini bado asilimia themanini ya Chakula kiliharibika. aliongeza Tausi akionesha tukio analikumbuka vizuri.
Baada ya kumaliza kula utambulisho uliendelea,
Mke wangu huyu ni mtoto wa mdogo wangu kabisa, na kutokana na kuridhishwa na matokeo yake ya mitihani mbalimbali nilijikuta nashawishika kumsaidia mdogo wangu, lakini pia kumsaidia huyu mwanangu (akimpigapiga mgongoni Samson)
Japokuwa kulikuwa na changamoto kubwa sana kwenye uhamisho wake ni baada ya walimu wake kufanya uhuni fulani ambao Mimi bila kushirikisha watu wakubwa huenda tusingefanikisha jambo hili.
Na wewe samson, huyu ni mke wangu mwingine maana nasikia uliniulizia kule mbona sijarudi, ni kwamba ukiona sionekani kule basi nipo huku.
Samson alitikia kwa kichwa akionesha kukubaliana na pia aligundua upendo fulani wa kweli toka kwa tausi, alijikuta akipapenda ghafla kwa Tausi japo mandhari na uzuri wa nyumba kule kwa akina Kulwa ni kuzuri zaidi, lakini alipapenda kwa Tausi.
Samson, Mimi ni mama yako mdogo naitwa Tausi, nadhani si vyema sana kukutajia jina langu lakini nitafanyaje Sina mtoto mtaani kote hapa wananiita kwa jina langu,
Kuwa na amani kama Kuna msaada wowote utahitaji hata Ukiwa kule usisite kuniambia,kama Nina uwezo na naafford........
Alikatishwa baada ya mzee Mgaya kumminyia jicho ili aache kuweka mambo mengi wazi, maana angemchanganya Samson, hivyo wakabadili stori.
Mke wangu wiki hii nataka walianza shule Hawa najua sitakuwa bize sana nataka kuanza kukagua miradi yangu yote, maana nashangaa hakuna hata anayeleta hela na pia ni siku nyingi sijatembelea mashine zangu za uzalishaji wa mbao (Sawmill) mbaya zaidi nasikia kuwa wateja wameongezeka wanaleta mizigo nadhani huu ni muda muafaka wa kuwa karibu tunaibiwa ujue. alitania mzee Mgaya huku akiinuka kwenye kiti chake na kutoka nje.
Baada ya kutoka nje mzee Mgaya Tausi aliitumia fursa ile kutaka kumpeleleza Samson mambo fulani ikiwemo kushawishi ahamie kwake,
Sawa mama, ila Mimi kumbuka si mwenyeji wa mji huu, hata ukisema nirudi kule kwa mama mkubwa Wala hata sijui naanzia wapi, kuja huku nitakuja ila lazima niwe na mwenyeji.
alijitetea Samson.
Sasa mke wangu Mimi naondoka na kesho nawapeleka akina Kulwa huko shuleni kwao tayari kwa kuanza maisha mapya, najua hawatakuwa wapweke kwakuwa wapo wawili, ila nitawamisi wanangu. alisema Mzee Mgaya bila kujua kama anazidi kumuudhi Tausi ambaye huwa hapendi umtambie suala la watoto mbele yake.
Mimi naona mke wangu nikuage na Leo sitarudi hapa nataka niamkie kule iwe rahisi kupunguza foleni barabarani, wakaingia kwenye gari na Samson tayari wakirudi ndani.
Tausi ni mwanamke fulani anajiamini sana kuanzia mtaani hadi kazini kwake, ila kuwa alone kulimtesa sana, na yote hayo alijua mchawi wake ni mama Kulwa alishindwa kujua ni lini atapata mtoto kitendo Cha mke mkubwa kupata watoto mapacha huku yeye akiwa Hana mtoto, aliumia sana,alimuona mchawi wa maisha yake ni mama Kulwa
alihitaji kuwa na mtu angalau wa kulinda nyumba yake, na kwa mtazamo wake aliona Samson kijana aliyetambulishwa muda si mrefu angemfaa.
Kwa upande wa mama Kulwa naye alijua mchawi wa maisha yake ni Tausi, kitendo Cha yeye kupata watoto kwenye umri mkubwa tena mapacha aliona ni baraka toka kwa MUNGU mwenyewe lakini ni kipindi ambacho alizisikia maneno mengi ya shombo toka kwa tausi akiitwa mchawi.
Mzee Mgaya alipiga honi kutaka afunguliwe mlango Mara baada ya kukaribia geti la nyumba yake, alishangaa kuona geti likifunguliwa na mkewe ambapo si kawaida..
Haya baba naona umeenda kwa changudoa wako, umepewa ulichopewa lengo uje utuangamize humu ndani, haya kama unachakufukia, fukia baba. Najua unampenda sana yule aliyeharibu kizazi kwa umalaya wake na leo hii unataka kuwaua wanangu ili umfurahishe yule kahaba Sasa nakwambia niuwe Mimi kwanza kuuuutwa nzima unazurura Mara uende huku Mara huku una Nini wewe baba Kulwa ? aliendelea kubwata yule mama ambaye hata kitenge alichovaa kilimvuka na kubaki na gauni lake tu.
Mama vipi twende ndani mama yangu kwani Kuna nini, alihoji dada wa kazi huku akimtoa boss wake na kuingia ndani , wakati huo Mzee Mgaya alimpuuza tu, anamjua wazi ni mlevi wa pombe alitambua vyema kama atakuwa kaonja, hata wanae wakina Kulwa walichukulia kawaida tu maana wanalijua gubu la mama yao.
Kwa upande wa Samson alikuwa na hofu kubwa sana, alimuona rasmi mama yule alivyo mkali sana, alizidi kutetemeka huku akiingia ndani kwa uoga.Mama Kulwa alikuwa ni nusu kichaa hasa akikasirika,aliwaza namna atakavyoishi naye akajikuta ana kibarua kikubwa Cha kuhakikisha hamuudhi yule mama, ambaye ni nesi mstaafu aliyefanya kazi miaka mingi hospital ya taifa Muhimbili .Samson akajikuta anaanza kuona mahali pale ni kwa moto
Itaendelea......... ............