hasa kwa mke mdgohahaahaa nimecheka sana hapo mke mkubwa anaposema haya baba kama anakitu chakufikia fukia tu baba,mzee mgaya nae mjanja tu kijijini ila mjini hana sauti kwa wake zake
mkubwahasa kwa mke mdgo
Wanawake Wana roho mbaya mno yaani mbaya Tena na Ni nusu mashetani.akiliangalia rundo la nguo, akiangalia jua limeisha , akaona kazi ipo, huku akijiuliza kwa yule dada w
Aisee, pole sana Sam, lkn utatoboa tu jipe moyo, though I wish ungekuwa unajua njia ya kwenda kwa tausiSEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Siku mbili baadaye akina Kulwa na ndugu yake waliondoka rasmi pale nyumbani kwao, ikiwa ni mwanzo wa maisha mapya huko boarding hali iliyofanya nyumba ipooze lakini pia ikiwa na watu wachache.
Sasa mwanangu kwanza inatakiwa kesho wote twende kanisani, nazungumzia hivyo kwasababu Kila jambo lolote ili ufanikiwe lazima uwe na Imani, na si Imani tu lazima kuwe na msingi kwanza, kesho kutwa unaanza rasmi safari ya masomo ya upili, (secondary) lazima ujue kuwa utakutana na changamoto kadhaa kwenye safari ya masomo yako, pia walimu,na hata wanafunzi wenzako.
Kwenye maisha huwezi kuwa sawa kwenye Kila jambo, na si Kila binadamu anawaza kama uwazavyo wewe, hivyo lazima ujue kuwa wakati mwingine kutofautiana mawazo na wenzako si kwamba hawana akili au wewe si mwelewa hapana, Bali unatakiwa kuwa kwenye mstari wa uadilifu na Imani.
Tukirudi hapa nyumbaniiiiiii, mmmmh
Mwanangu nimekutoa kijijini kwa lengo moja tu, wewe na shule,
Kwenye harakati za kuisaka na kuipambania Elimu si jambo jepesi, milango yake ni migumu, changamoto ni nyingi , hivyo naomba ujitahidi kupuuza baadhi ya mambo ya hapa nyumbani, hasira zako za kijijini achana nazo hapa watu watataka ususe Kisha wakurudishe kijijini hivyo usiwe mwenye kukata tamaa au kuwa mnyonge kuwa kawaida.alimalizia mzee Mgaya huku akijimiminia konyagi kama vile maji.
Maneno yale hayakumwingia wala kumgusa Samson, badala yake alifikiria labda ni maneno ya kilevi tu
Muda huo aliingia chumbani akawa, anavichungulia vitu vyake ambavyo muda si mrefu katoka kununuliwa muda si mrefu.
Hakika vilipendeza sana machoni pake, hasa sare ambayo ilishonwa vyema huku ikiwa inamtosha vizuri akashindwa kujua waliwezaje kujua saizi yangu ikiwa fundi hakunipima? Akapanga nguo zake vizuri Kisha akashika begi zuri kabisa ambalo ndilo litakuwa la kubebea madaftari na vifaa vyake.
Mara akasikia sauti ikiiita ikiwa inakaribia kabisa kuja usawa wa chumba chake, aliisikia vyema alikuwa ni mama yake mkubwa.
Weee kijana vipi upo chumbani muda huu unaumwa? aliuliza yule mama.
Hamna nilikuwa napanga vitu vyangu . alijibu kiuoga Samson.
Sawa, hebu njoo huku sebuleni, Kuna jambo nahitaji kuongea na wewe.aliongea mama Kulwa, mama ambaye ni mzuri wa sura lakini ni ile inayoamrisha muda wote.
Sikiliza mwanangu Samson, hapa kwasasa kwenye hii nyumba tupo watu watatu tu, nasema hivyo kwakuwa baba yako huwa hakai hapa siku zote,lakini pia akina Kulwa kuonana pengine Hadi likizo au tuwatembelee sisi wenyewe, labda kama Kuna tatizo.
Sasa basi naomba tugawane majukumu, ya kikazi muda wa kurudi shule unajulikana, na kizuri zaidi shule ipo karibu sana , hivyo ni rahisi kufanya mambo yako na Kisha kupata muda wa kujisomea .
Naomba ufahamu kuwa utakapofanya kazi za hapa nyumbani haraka na kwa weledi basi ndivyo utakavyopata muda wa kupumzika pamoja kujisomea.
Hapa babaaaaa inatakiwa kuosha vyombo, pia kusafisha mazingira,kupunguza maua na kazi zingine nyingi, tulikuwa na mpango wa kumuweka shambaboy lakini , tumekosa Cha kumlipa kwasababu gharama nyingi zimekuja kwako, masuala ya uhamisho, ada na makorokoro kibao . yote ni kwasababu ya kukusaidia wewe , uandaliwe maisha bora ya baadaye,
Je, kwa mtu aliyejitolea vitu vyote hivyo, wewe unashindwaje kumsaidia? aliulizwa Samson akawa Hana majibu zaidi ya kujiinamia chini.
Basi hata hivyo Mimi nadhani umenielewa vizuri sana , tunaweza hata kuanza kwa vitendo, na kwakuwa dada kashaosha vyombo wewe nifulie tu hivi vitambaa vyangu Wala hata si vichafu sana.
**************************************
Siku ya jumatatu ya kuripoti shule ilifika huku Samson, akiwa mwanafunzi aliyekamilika, nywele zilizokatwa vyema, mavazi nadhifu, kiufupi alikuwa na appearance ya kimjini.
Samson alienjoy sana kwa ile siku ya kwanza, vile walimu mbalimbali walivyojitambulisha Kila mtu aliyepita akijitambulisha kwa namna yake, wapo waliokuwa kama comedian na utani utani mwingi ikiwa ni mbinu ya walimu kuwaweka sawa wanafunzi hususani wale wa form one.
Samson kupitia ujanja wake alijikuta anaelewana na baadhi ya wanafunzi kadhaa huku wengi wakitambua kuwa katoka mkoani kwani hata lafudhi yake haikuwa ile ya pwani.
Muda fulani aliingia mwalimu mkuu wa shule, ambaye alikuwa na visa na vichekesho vingi kiasi Cha kuwavunja mbavu watoto wale,
Naitwa mwl Yasin, Mimi ndiye mwalimu mkuu wa hii shule, lakini pia Mimi ni mwalimu wa Sayansi,
Bila shaka hapa wote ni wageni,
What is science?
Aliuliza swali la kiingereza huku Samson akishangaa kuona Kuna baadhi ya wanafunzi wamenyoosha mikono kuashiria wanalijua Hilo swali.
Akainuka Binti mmoja ambaye aliielezea ile maana vizuri kwa kiingereza, huku Samson akipigwa na butwaa , kuona mbona wao hawakufundishwa shuleni kwao, hata hivyo hakujua kitu inaitwa Pre_form one hivyo alikuwa na haki kutokujua ile definition.
Mwalimu mkuu akaendelea,
Maisha ni Sayansi Kila kitu kinafanyika kwa Sayansi, ukitaka uishi vizuri na watu lazima uijue Sayansi.
Ukitaka kuwa mchungaji, Sheikh au mhubiri mzuri lazima uifahamu Sayansi, Sayansi imechukua asilimia nyingi sana kwenye maisha yetu.sayansi tutakayosoma hapa si hii mliyokaririshwa kwenye tuitions za vichochoroni. Bali tunahitaji wahandisi, marubani na ma architecture na hata wanasiasa, kwakuwa siasa inahitaji Sayansi ndani yake.
What is physics?
Aliwashtua kwa kuuliza swali bila kutarajia
lakini bado Kuna wanafunzi walinyoosha mikono, kuashiria wanajua, ndipo Samson alipogundua kuwa mle darasani hasa mkondo wake ule Kuna watu vichwa sana ila akaweka Imani tu kwamba haya maswali yote lazima watafundishwa na atahakikisha anakuwa level za wale wanafunzi ambao wengi aligundua wanajuana na wanaviswanglish sana kuonesha watakuwa vichwa darasani.
Jioni alirudi nyumbani huku akiwa kapania kupambana na kuhakikisha anakuwa mmoja wa wanafunzi bora kama ilivyokuwa kijijini kwao.
Dah, kweli MUNGU wa ajabu, karibu sana baba yangu, hapa nilikuwa nawaza hii shughuli ya kufua nawezaje kumaliza mimi,
Yaani Bora wenye washing machine maana Ina kuwa rahisi, lakini umasikini huu baba yako mkubwa hela zote zimeishia kuwaandalia wanafunzi.
aliongea bila breki Wala kusalimiana yule mama.
Samson alipitiliza Hadi chumbani kwake, akabadilisha vitu vyake, akatoka huku akiwa na njaa, akiliangalia rundo la nguo, akiangalia jua limeisha , akaona kazi ipo, huku akijiuliza kwa yule dada wa kazi anafanya kazi gani?
Itaendelea.............



Kali sana kuliko muvi
Beb njoo kitu chako tayari huku moneytalkSEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
Maisha ya shule kwa Samson, hayakuwa mabaya sana, alizidi kuipenda shule, huku akijipatia umaarufu fulani wa kuulizauliza maswali kwa walimu hasa pale ambapo anakuwa hajaelewa vizuri.
Jambo hili liliwaudhi baadhi ya wanafunzi wavivu Darasani kwao, kwani ilisababisha mwalimu aendelee na ufafanuzi fulani, huku wengine wakijiona wanachoshwa tu wakimuona Samson ana kiherehere.
Miezi sita baadaye, Samson alikuwa akiongea na baba yake mida ya jioni wakiwa kibarazani wakiwa wanakumbushana mambo fulani,
Enheee, hebu niambie mwanangu shule unaionaje.
aliuliza Mzee Mgaya.
Nashukuru MUNGU mambo ni mazuri japo changamoto hazikosekani baba. alijibu Sam bila uoga wowote.
Changamoto tena mwanangu, ni zipi hizo? aliuliza Mzee Mgaya.
Unajua baba, kwenye mitihani ya muhula wa kwanza huu hapa mategemeo yangu nilidhani huenda nitakuwa kwenye nafasi nzuri za juu hasa kwenye mkondo wetu, lakini wapi, yaani nimepata alama A, somo moja tu, mengine B, lakini pia Kuna masomo mengine nimepata D kabisa baba. alifafanua Samson.
Haaaaaa kwanza nikupe hongera kwa maendeleo mazuri,lakini hiyo ndiyo unaiita changamoto! Hapana mwanangu wewe cha msingi ni kuongeza juhudi tu, utafaulu. alimpa moyo kijana wake.
Unajua nini baba, yaani pale shuleni sijui watu wapoje, Kuna watu hawasomi kwa wakati, pia ni watundu sana, yaani wakorofi wakorofi mno, huku wakiwa wanapewa adhabu Mara kwa mara, Kuna kipindi nikawa nadhani labda hawapendi shule, lakini Cha ajabu wamekuja kuwa kwenye nafasi nzuri za juu huku mmoja akipata alama A tu karibu kila somo, hii imenishangaza sana. alimalizia Samson.
(Mzee Mgaya alicheka sana)
Sikiliza mwanangu Samson, Sasa lazima ulijue jiji, lazima ujue kuwa umekutana na vipaji visivyozuilika, Ukiwa kule nyumbani kijijini ulisoma na watu wa jamii moja, yaani Mila na tamaduni zinazofanana, lakini hapa mjini unakutana na watu wa asili na jamii mbalimbali, Kuna watu waelewa na wajuzi wa mambo, kutokana na mazingira waliyolelewa.
Cha msingi nachokiona kwako ni kwamba naona una maendeleo mazuri tu, Cha msingi unapaswa kujiangalia wewe kama wewe, na kujihakikishia kupata marks zenye kuridhisha kwenye masomo yako, usijipe Presha kwa kujilinganisha na wengine. aliweka kituo Mzee Mgaya.
Haaaaaa jamani baba Kulwa, mazungumzo gani mnayoongea muda wote kana kwamba hamjawahi kuonana, unamchelewesha bwana, Kuna kazi nimemtuma huyo,
Mtu mwenyewe unamuona mziiiito hata kuujua mji hadi hii leo hata sokoni ni muoga kwenda, bado hajapajua, na dada yake(housemaid) nimemtuma sokoni.
Hivyo yeye nataka anisaidie, kuweka mazingira sawa hapa nguo zote ni chafu, na vyombo kama mnavyoona Mimi mwenyewe hapa Presha yangu inanisumbua nahitaji kupumzika, wewee Sam endelea na kazi na kumbuka dada yako akirudi atafikia kuandaa Chakula Cha jioni, hivyo kazi za leo zote zinakuhusu baba,. alisisitiza mama Kulwa.
Mzee Mgaya aliingia ñdani akipitiliza hadi chumbani kwake akitafakari mambo fulani,
Alikumbuka namna alivyoongea na kijana wake muda mfupi uliopita, alifurahi kuona kwanza anapenda shule, na Imani yake aliona tayari angefika mbali, alikiona kipaji kilichopo kwa Samson, akagundua kijana yupo smart sana licha ya manyanyaso kadhaa anayopitia lakini bado haoneshi unyonge wowote. aliwaza kumuhamisha shule ili asome high school kama akina Kulwa lakini Kila akimuwaza mkewe alijua atapinga kwa nguvu zake zote na ugomvi wake hauwezi kuisha milele. akaamua kutulia tu.
Alifurahishwa sana na maendeleo mazuri ya Samson.
Alitamani kumwambia mkewe ampunguzie kazi kijana wake huyo, lakini picha ya majibu ambayo angepewa aliiona akaamua kukaa kimya tu.
************************************
Siku moja wakiwa kitandani mzee Mgaya alizungumza na mkewe akiwa anamuaga.
Mke wangu, ile Safari yangu ya kwenda China imekaribia, kwahiyo nitumie fursa hii kukuaga mapema, maana safari ni wiki ijayo. mzee Mgaya alimwambia mkewe.
Kwani uliniambia unafuata nini vile, baba Kulwa, aliuliza kana kwamba hajui.
Nafuata mashine zangu za uchakataji wa magogo kwenye karakana yangu, unajua pale Kuna mashine nyingi ndogo ndogo zinakosekana hivyo, hivyo wateja wakija unakuja kazi zao zinakuwa zinaishia nusunusu, lakini pia napishana na hela nyingi inaniuma sana, Kuna mashine ya kuranda, mbao, kupiga msasa, na nyingine nyingi sina hivyo nataka niongeze ili karakana yangu ikamilike.
alizungumza Mzee Mgaya.
Wewe mwanzo uliniambia utaagiza, Kisha utazipokea bandarini kama ilivyokuwa kwa vifaa vingine, kwani lazima kwenda baba Kulwa?
Unajua mke wangu wewe unaongea tu, kitu Cha kuagiza kina karaha sana , kwanza niliwahi kufanyiwa ushenzi wa kuletewa bidhaa isiyoridhidha, pili muda unakuwa mwingi, sijajua makosa yako huko au bandari yetu, na Kuna jamaa yangu kaagiza mashine za kukoboa mpunga akaletewa vitu tofauti, hivyo safari hii naenda mwenyewe . alikazia Mzee Mgaya.
Wewee labda umdanganye mtoto mdogo, wewe unapenda sana kuzurura, yaani hapo unaenda na Tausi, unapenda sana starehe mume wangu kana kwamba hukuzifanya utotoni, na sijui Tausi alikufanyia dawa gani, looooh yule mtoto, aseme Nini asifanyiwe, na safari zako nyingi lazima uongozane naye, au ndiyo mmeahidiana mje kufa wote si ndiyo.
aliongea bila breki mama Kulwa.
Hayo maneno gani mke wangu, umri huu Mimi nifanye mambo hayo ya kipuuzi, hebu kuwa na adabu na heshima sisi ni wazee umri wetu siyo wa kuoneana wivu wa kijinga namna hiyo, Mimi nafuata mizigo yangu ili nije kuleta upinzani, kazini kwangu, hapa nilipo nimestaafu tayari, mafao yangu nimejaribu kuyahamishia kwenye uwekezaji mwingine, na matunda yake unayaona , ni biashara ambayo hela ipo, Sasa masuala ya kutokuaminiana kwenye umri huu....... unanitisha mke wangu.
Wewee baba wewe hebu nilale miye, kwani ukisafiri na Tausi Kuna kosa gani. Nyie nendeni nawatakieni safari njema. alizungumza mama Kulwa na kujifunika shuka gubigubi akimaanisha hataki tena stori.
Mzee Mgaya alikasirika sana, alitamani amwambie kitu mkewe lakini haikuwezekana, maana alitambua kufanya hivyo watakesha hadi asubuhi maana alimjua vyema mkewe, lakini ukweli ni kwamba kwenye safari alikuwa peke yake , kuambiwa atakuwa na Tausi, ilimuuma kiasi, hakutaka kuonekana mwenye upendeleo.
Tukirudi kwa Samson, mzee Mgaya aliona mabadiliko ya kijana wake kwa muda mfupi, aliona si vyema sana kwa mtoto wa kiume kufua nguo hasa za kike, kwake haikumpendeza sana
Ingekuwa ni mfanyakazi Baki , nisingeona shida sana, si analipwa?
Lakini huyu ni mwanangu, ni mtoto wa ndugu wa damu, tunachomfanyia Leo huyu anakiona, hatakuja kuwa na uhusiano mzuri na sisi ikiwa nitaacha afanyiwe ushenzi akapanga kuongea na mkewe asubuhi.
Kama kawaida mishe na majukumu kwa kila mmoja akitimiza majukumu yake huku mama Kulwa akiwa mtu wa kujihimu sana, lengo ni kuwaamrisha vijana wafanye kazi kwa usahihi.
Mzee Mgaya alitoka nje akiwasha gari lake na kuliacha likiunguruma kwa muda na yeye kurudi ndani, Kisha kitambo fulani akarudi kulizima.
Mke wangu, hivi unamuonaje Samson, tangu siku ya kwanza anafika na hii leo, aliuliza Mzee Mgaya.
Nimuoneje, namuona kawaida. alijibu Kwa mikato mama Kulwa.
Hamna mke wangu, kanenepa bwanaa wewe huoni alivyoongezeka Hadi urefu, yaani huenda zilikuwa shida tu kijijini, lakini Dar es salaam imempenda.aliongea huku akijichekesha.
Yes, ni kweli tena na chunusi za balehe naona si haba, anazidi kuwa mbaba Samson.
aliongeza mama Kulwa Kisha wakagonga mikono na mumewe huku wakicheka.
Sasa mke wangu Mimi Nina ombi moja , nadhani ni vyema tukampunguzia Samson majukumu ili apate muda wa kujisomea,
Awaze kazi, awaze masomo mshika mawili moja humponyoka.
Kumbuka watoto wetu akina Kulwa tumewapeleka shule ambayo muda wote wanakuwa wao na kitabu na kitabu na wao,
Hebu tufanye hivyo kwa Samson, sisemi asifanye kazi mke wangu unielewe, nasema apinguziwe majukumu. akaweka kituo mzee Mgaya.
Kwahiyo unahisi tunamtesa au vipi mume wangu,
aliuliza huku akiwa kaminya midomo ya dharau.
Hapana, nataka apate muda mwingine wa kujisomea, tuna dada wa kazi tena analipwa , kwanini hizo kazi asifanye yeye, hapana kuanzia leo ni marufuku kwa Samson kufua nguo za mtu mwingine tofauti na za kwake, amri hii naitoa Mimi kama mume, na baba wa familia.
aliongea kwa sauti kubwa na Kali huku akionesha hatanii.kiasi Cha Samson na yule dada wa kazi kusikia vizuri.
Mama Kulwa aliingia chumbani akaenda bafuni akajiswafi, baada ya muda fulani akatoka akiwa kapendeza sana, nywele zake ambazo huwa hazisukwi bali zinachanwa huku zikiwa zinameremeta, licha ya kuwa tayari alikuwa na mvi kichwani kutokana na umri, lakini bado alipendeza sana,
Suti yake ya kike ya wamama watu wazima ilimkaa vyema sana, huku mguu akivaa viatu vya wazi visivyo na visigino virefu, vinafanana na mkoba aliobana kwapani, akiwa ananukia vizuri, alitoka nje huku watu wote wakishangaa anaenda wapi, hata Mzee Mgaya alishangaa alijua labda mkewe kaingia chumbani kutuliza hasira zake hakuwa akijua kuwa anatoka.
Mke wangu wapi unaenda, halafu hayo Maigizo yako tutakuja kuachana ukubwani ujue hakuna lisilowezekana. aliwaka Mzee Mgaya.
Licha ya kupewa vitisho mama kulwa hakujali wala hakujibu akafungua mlango wa geti na kupotelea mtaani, haikujulikana anaenda wapi.
Huyu anajifanya mtoto au Binti wa miaka ishirini na roho mbaya yake Sasa safari hii nitamkomesha, mzembe wa fikra huyu.
alilaumu mzee Mgaya.
Itaendelea........... ......................
Mbona unauza kazi za watu bila ruhusa yao una shida gani aiseee hujui hilo ni kosa
Naam, nimeitikaEngineer kama Engineer.
Beb njoo moneytalkSEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
Mzee Mgaya alirudi ndani na kupitiliza hadi chumbani, aliangalia picha fulani ni ya siku nyingi sana, ambayo yupo yeye na mkewe.
Aliangalia namna mkewe alivyotoa tabasamu Pana kwenye picha ile huku akikumbuka vyema kuwa hata hivyo hiyo siku waliyopiga picha hiyo kama alivyoamrishwa na mkewe, ni siku ambayo pia alipokea taarifa mbaya toka kijijini kufuatia kifo cha mama yake mzazi.
Hivyo mara nyingi huwa anapendekeza picha ile itolewe ukutani kwani ilibeba kumbukumbu mbaya kwenye maisha yake, lakini mkewe huwa anagoma akidai Ina kumbukumbu nzuri kwake, kwani ni siku ambayo alipokea taarifa nzuri ya kupandishwa daraja na nyongeza ya mshahara, huku akipewa mualiko wa kwenda uingereza.
Huyu mwanamke najuta hata kumuoa, na sijui shetani gani alisema nikubali, hakuwa chaguo langu kabisa huyu, namlaumu sana afande (jina kapuni) yeye ndiye aliyenishawishi, Mara ohh ni mwanamke mzuri , Mara ni mwenye Elimu yake hivyo mtajenga familia Bora, Mara ohh ni mrefu kama wewe hivyo mtapata kizazi bora na chenye kupendeza, lakini ukweli huyu mwanamke ana roho mbaya sana, ni mke wangu, atabaki kuwa mke wangu si tumezaa watoto wengi tu, lakini mmmmh
Misiba mingapi imetokea kwetu lakini yeye hakutokea,
Kila matatizo yanayotokea kwenye familia yangu huwa anaishia kutoa pole tu, lakini si kwenda.
Aliwaza mzee Mgaya akiwa ndani kwake Kisha akatoka nje akamkuta Samson amekaa chini akionekana mwenye mawazo.
Wewe Samson mbona umejiinamia hapo unawaza Nini, ni huyo mama yako? Bado hujamzoea tu.
Wewe ni mtoto wa kiume jaribu kudharau baadhi ya mambo.
Aliongea kwa sauti ya kuamrisha mzee Mgaya huku akijaribu kumuweka sawa Samson hapo hata yeye ilimuuma mno ila hakutaka aonekane dhaifu kwa mkewe.
Alimuita dada wa kazi na kumuaga huku akimtaka Samson aingie kwenye gari lake na wakaondoka
Sasa baba hivi mama atakuwa kaenda wapi, maana kaondoka akiwa na hasira vileeee............. aliuliza Samson huku akishindwa kumalizia sentensi yake.
Ahhh yule mama yako ndivyo alivyo Wala usijali, najua kaenda wapi, najua, najua sana tu. alijibu huku akiendesha gari kwa high speed kiasi Cha kumtisha Samson.
Na pia Samson hapa tunaenda kwa mamako mdogo kule Temeke, Sasa tafadhali sana, asije akakupeleleza
Mara vipi unaishije, Mara sijui nini, maana Tausi namjua huwa anajifanya Bora wakati naye ana matatizo yake mengi tu, hivyo ya kule yaache kule kule, aliongea Mzee James huku akiwa anamaanisha.
Samson aliishia kushangaa tu huku akiwa hajajibu chochote,
Hatimaye wakafika nyumbani kwa Tausi wakapokelewa vizuri huku Samson akiona aibu kidogo kutokana na uzungu wa Tausi kwa mume wake .
Stori ziliendelea pale sebuleni huku utani na vicheko vikitawala pale sebuleni, angalau Sasa hata Samson alianza kuchangamka,
Enhee niambie mwanangu Samson naona Dar es salaam imekupenda, yaani ni tofauti na miezi kadhaa iliyopita, aliongea kwa bashasha Tausi.
Ni kweli mama nadhani mji umenipenda, ila masomo yamenipenda zaidi, na nimeyapenda sana, nafikiri tunapendana. alijibu Samson na kuwafanya watu wote wacheke mle ndani huku Mzee Mgaya akifurahishwa na majibu ya Samson , maana aliona kwasasa anajiamini tofauti na yule samsoni mwenye aibu.
Ila kama ni hivyo wewe Samson una moyo mkuu sana, maana uishi pale halafu unenepe, weeeeeeeeh acha nikusifu tu, aliongea Tausi.
Mzee Mgaya ikabidi amkate jicho fulani la kuonesha hajapenda kinachoongelewa.
Unaniangalia kwa jicho baya ili iweje, kwani uongo? mama Kulwa ana roho mbaya bwanaaaa, madada wa kazi wangapi, wameondoka pale, huko kazini kwake je, na kwenye biashara zake mbona watu wanalalamika Hana huruma na wenzie? Haaaa
Acha niongee bwana.
Tausi, aliropoka mambo mengi huku akijua wazi Mzee Mgaya hatomfanya chochote.
Mzee Mgaya aligwaya,hakusema chochote mapungufu ya mkewe mkubwa aliyajua lakini hakupenda azungumziwe vibaya na mtu yeyote yule, pia hakupenda tabia ya Tausi badala ya kuongea mambo yake lazima amuongelee mke mwenzie, lakini hakulaumu sana, kwakuwa alijua visa vyao.
Wakati akiwaza hayo kuna kijana mdogo aliingia, akionesha kutumwa jambo fulani kwa Tausi.
Mara baada ya kukaribishwa akae walishangaa kuona wanaonesha kufahamiana na Samson,.
Vipi Samson naona mnaangaliana huku mnatabasamu vipi unamfahamu huyu?
aliuliza Mzee Mgaya.
Ndiyo, tunasoma darasa moja na mkondo mmoja, anaitwa Abdallah au almaarufu Dullah, alifafanua Samson
Haaaaaaaa kumbe Dullah unasoma shule anayosoma Samson, jamaaaaniii , unajua napenda sana Samson akae hapa,ila changamoto ni kwamba ni mgeni anaogopa kupotea , hata hivyo ni kama MUNGU kawakutanisha hapa. aliongea Tausi huku akionesha kufurahi sana akampa yule kijana mzigo wake Kisha akaondoka.
Dah unaona sasa Sam,kumbe Dullah anasoma shule na darasa moja kwanini asiwe kampani yako , ili uishi huku, nadhani itakuwa poa sana, utakuwa hupotei tena au unasemaje baba na chumba chako kipo utaishi safi kabisa. aliongea Tausi akionesha anataka Samson akae kwake.
Wakati stori hizo zikiendelea mzee Mgaya yeye alikaa kimya huku akionesha hapendi zile stori.
Siku nzima Mzee Mgaya na Samson walishinda kwa Tausi huku furaha zikizidi mle ndani, walikula wakaangalia tamthilia kwa pamoja mithili ya watu waliopo kwenye sinema.
Watu watatu walitosha kuichangamsha nyumba vilivyo,
Baadaye jioni sana, mzee Mgaya alimuaga Tausi kuwa anamrudisha Samson huku yeye usiku wa siku hiyo atakuwa hapo,
Mida ya saa moja jioni Mzee Mgaya na Samson walikuwa kwenye gari wanarudi.
Unajua Nini mwanangu Samson, mama Kulwa ni mke wangu Mimi tuna zaidi ya miaka arobaini tunaishi pamoja, hivyo namfahamu vyema , lakini pia huyu mama yako mwingine naye tuna miaka mingi tu tupo wote Sasa basi Mimi nimekutoa kijijini nimekuleta kwa mama Kulwa, Mimi si mjinga najua ni sehemu sahihi ambayo itakufaa , Yale unayoyaona ni changamoto za kawaida tu, natamani kuongea na wewe vitu vingi lakini umri wako......... yaani basi tu.
Aliongea Mzee Mgaya kwa uchungu.
Yule manako Tausi usione anakuchangamkia vile ukaona labda anakupenda sana, ukajikuta unashawishika kukaa kwake hapana, ukikaa nae ndipo utamjua ana tabia gani, hivyo usihadaike na ngonjera zake
Aliongea Mzee Mgaya akionesha kumtisha Samson ili awe na msimamo mmoja.
Hatimaye walifika nyumbani wakafunguliwa geti, wakamkuta mama kulwa kalala kibarazani
Vipi mama yako kachafuka hivyo, Kuna Nini, aliulizwa housemaid.
Kaletwa na taxi tangu saa kumi, ila hawezi kuingia ndani, anasema amechoka sijui kapatwa na nini, maana Kila nikisema nimsaidie anasema nimuache,
Alisema dada wa kazi akimwambia boss wake mzee Mgaya.
Mzee Mgaya alimsogelea mkewe, akakutana na harufu ya pombe kali, akawa ameshajua Nini kimempata akamuinua kwa nguvu na kumrudisha ndani.
Niache, niache nakwambia baba Kulwa kwanini lakini , wewe si una mkeo Tausi, na una wanao akina Samson? Sasa unataka Nini kwangu?
Alilalamika mama Kulwa, lakini haikusaidia kitu bado aliburuzwa kwa lazima Hadi chumbani.
Itaendelea..................
Hii ipo based on a true story, haijatungwa, kama ulisoma stori inayoitwa
MIMI NA BOSS WANGU
Basi Ina uhusiano na hii.