Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Mzee Mgaya na kaka yake walikuwa kwa ndugu yao fulani, wakipanga taratibu za kwenda kuzuru/kutembelea makaburi ya wazazi wao huku kaka yake na mzee Mgaya akikusudia kufanya tambiko fulani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.

Akiamini waliolala pale yaani wazazi wake wanaweza kumsikiliza na yeye akanyoosha mambo fulani, ila wazo lile lilikuja kukosa nguvu baada ya kila mmoja kumkumbuka mganga ambaye alitaka kuwatapeli kuhusu tukio la kupotea kwa Samson.

Unajua ndugu yangu Mimi moja kwa moja kutokana na migongano kazini kwangu huko mjini, dhumumi langu kubwa lilikuwa ni kuja kufanya shughuli ya kutambika ili kunyoosha mambo fulani, lakini Kila nikiangalia na kukumbuka tukio lenu naona kama mambo haya tuyaache yapitwe na wakati tu. alishauri yule mgeni kaka wa mzee Mgaya.

Baada ya kushauriana kuwa waachane na yale mambo lakini walishika njia ya kurudi nyumbani huku wakiongea masuala mbalimbali.

Hivi ndugu yangu unajua wewe katika watoto wako wote hawajasoma na hawana elimu, na inabidi utambue kuwa Dunia ya Sasa tunakoelekea inawahitaji wasomi zaidi. ili kurahisisha maisha , je una mpango gani kuhusu kijana wako Samson maana wale dada zake hakuna namna tena Kwa umri wao hawawezi kuendelea na Elimu yeyote. alihoji yule mgeni.

Unachoongea ndugu yangu ni kweli hata Mimi natamani sana hasa huyu mwanangu Samson asome, lakini uwezo kaka. alijitetea mzee Mgaya.

Uwezo upi kwamba huwezi kumsomesha mwanao au yeye hana uwezo wa kuafford masomo, maana kama ni ada Mimi sidhani kama kweli wewe ndugu yangu unakosa ada ya kulipia kweli kwenye shule hizi za kawaida, si ipo ile shule yenu mpya kule wilayani Wala Haina hata gharama na ni ya kutwa, inakushindaje? aliuliza kaka yake na mzee Mgaya huku akikazia sana lile suala.

Unajua wewe kaka unaongea tu, wewe mwenzangu una kipato kikubwa watoto wako wakubwa karibu wote umewasomesha, jaribu kulinganisha hali yangu na yako Mimi nadhani hakuna anayependa watoto wake wasisome ila tatizo ni umasikini uliopindukia.alikaza mzee Mgaya huku akiwa hapendi kejeli za kaja yake kumlazimisha vitu ambavyo yeye hana uwezo navyo.

Waliendelea kuzunguka, wakakikuta kilabu fulani Cha pombe za kienyeji wakaingia huku wengi wao wakimshangaa yule mgeni, waliomkumbuka walisalimiana kwa heshima huku wakifurahia kumuona yule mgeni, basi alichofanya yule mgeni alimuita mama muuza pombe akamwambia awape pombe watu wote waliokuwa mle ndani.

Watu wote walifurahia sana wakaanza kubwia zile pombe kwa fujo huku wakimshukuru sana yule mgeni, hata yeye alizikumbuka sana pombe za asili ya kwao hivyo akazipiga kisawa sawa , huku wote wawili wakishika njia ya nyumbani kwa mzee Mgaya wakirudi wakiwa wamelewa kiasi.

Muda wa saa mbili za usiku walifika nyumbani huku Kila mmoja akiwa Hana hamu ya kula yaani ile pombe ni kama huwa inashibisha, hivyo Kila mtu akaamua kulala tu.

Kitendo cha wao kurudi usiku kilimuhuzunisha Samson ambaye alibandika matokeo yake ya mitihani
lengo baba yake mkubwa ayaone lakini wakawa wamerudi wamelewa halafu ni usiku akanyongea sana Samson.

Mama Mgaya alitambua ile hali ya mwanaye akamfuata akampoza poza tu huku akimpa moyo kuwa atamwambia shemeji yake hitaji la mwanae, basi siku hiyo ikaisha

Kutokana na pombe nyingi za kienyeji zilimchukua kaka yake na mzee Mgaya, akajikuta anachelewa kuamka, wakati huo wenyeji walishaamka kitambo wakiwa wanalimalima nje ya nyumba yao kama ilivyo kawaida ya watu wa kijijini Mashamba kuwa karibu tu na nyumba.

Mgeni aliamka mida ya saa mbili na nusu huku akitoka nje na kuangaza macho na kuwasalimia wenyeji wake kwa kupunga mikono
Alishangazwa na makaratasi mengi yaliyobandikwa kuzungushwa kwenye ukuta wa nyumba ikabidi ayasogelee na kuanza kusoma karatasi moja moja.

Wakati akiendelea kufuatilia Yale makaratasi familia nzima ilikuwa inamuangalia huku Samson akiwa ana furaha zaidi maana lengo lake lilitimia kwa kiasi kikubwa akawa ana furaha sana.

Wakati huo Mzee Mgaya na mkewe waliacha shughuli zao huku wakirudi ndani ili kumuandalia mgeni maji ya kuoga lakini na chai pia

Yule mgeni aliganda sana pale, akiwa anaangalia hatua moja ya karatasi baada ya jingine.

***************************
Kwa majina kamili anaitwa James Mgaya ni kaka wa kwanza kwenye familia ya marehemu Victory Mgaya ambaye alikuwa Jumbe, yaani kiongozi fulani wa eneo kutokana na muundo wa serikali ya kikoloni.

Hivyo wakati huo waingereza wakiendesha shule fulani za misheni walikuwa wanachukua kijana mmoja mmoja kwenye Kila familia, kutokana na wadhifa wa uongozi wa mzee Mgaya marehemu ikabidi achukuliwe kijana wake anayeitwa James akawa anasomeshwa kwa msaada wa wamisionari, alisoma hadi darasa la nne akafanya mtihani akafaulu akaendelea na masomo ya middle school mpaka darasa la nane.
akiwa na elimu kubwa tu kwa kipindi hicho.

Akarudi kijijini kwake akabahatika kuwa ni mmoja wa walimu wa shule ya kijijini kwao kutokana na uhaba wa walimu kwa kipindi hicho , wakiwa wanajulikana kama walimu wa UPE
(Universal Primary Education)
alifundisha kwa takribani miaka mitano akijulikana kwa jina la mwl James Mgaya huku wanakijiji wakifurahi kumpata mwalimu ambaye ni mzaliwa wa hapo.

Baadaye akafuatwa na shirika fulani la kidini likimtaka afanye kazi kwenye shirika lao rasmi , hivyo wakahamia Dar es salaam, lakini baada ya kufika mjini mambo yalibadilika lile shirika likapoteza dira huku yeye akiwa tayari ana wenyeji na connection kibao hivyo akajiunga kwenye moja ya shirika la reli hapa mjini.

Kwenye shirika la railway hakukaa sana baada ya kutokea kwa vita vya Uganda na Tanzania, akachaguliwa kuwa mmoja wa jeshi la akiba kwa kipindi hicho (alikuwa na sifa au la haikujulikana mapema)

Basi baada ya vita vile kumalizika James alikuwa kwenye wakati mzuri na mnufaika mzuri sana hivyo mambo yakaanza kumnyookea, huku akioa na kuanzisha familia rasmi.
Basi tangu hapo akawa ni mtu muhimu kwenye ukoo na familia nzima kiujumla.

*****************************
Kaka yake na mzee Mgaya aliangalia yale maendeleo ya Samson akagundua kuwa mtoto ana kitu kichwani ila huenda hana sapoti akamuita Samson pamoja na wazazi wake akiwalaumu kwanini kijana anaonesha alikuwa na maendeleo mazuri Sasa kwanini hawaoneshi mpango wa kumpeleka Sekondari.

Wazazi wa Samson walijitetea kuhusu kipato huku wakimuomba kama ana uwezo basi amsaidie.

Yule mgeni aliwaza kitambo kidogo Kisha akawaambia kuwa inabidi aende wilayani akaangalie matokeo yake ili mipango ya kumuhamisha shule iendelee. Ilikuwa taarifa nzuri sana kwa mzee Mgaya na familia yake huku wakimuomba MUNGU afanikishe mpango wao.

Je, atafanikiwa, tukutane sehemu ijayo.
 
moneytalk umeshapta hapa ?
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

James Mgaya alimaliza kuangalia maendeleo yale aliyoyabandika Samson, aligundua kuwa kijana ana uwezo kama akiandaliwa mazingira mazuri roho ilimuuma akamgeukia mdogo wake,(yaani baba yake Samson)

Ndugu yangu, pole sana Sasa tunafanyaje kwenye hili maana huyu afaulu asifaulu inatakiwa atafutiwe shule aendelee na masomo . alishauri yule mgeni.

Ni kweli kaka, japo Mimi sijawahi kufuatilia maendeleo ya mwanangu kwasababu hata Elimu ya miembeni tu sijapitia hivyo sijawahi kujua uwezo wa mtoto wangu yeyote yule.
aliongea ukweli wake mzee Mgaya huku akicheka cheka kwa aibu

Mama Mgaya, Samson mwenyewe na ndugu zake walikuwa washaacha majembe yao wapo tu pale uwanjani wakiwa kimya huku Kila mtu akiomba kwa namna yake ili MUNGU atie wepesi.

Hebu njoo mwanangu sogea, James Mgaya alimwita Samson huku akimuonesha umbo moja kwenye somo la hesabu akimwambia kuwa duara Zima huwa lina nyuzi 360°
Hivyo nusu duara ni 180°.kwanini yeye aliandika ni nyuzi 90°?
Japokuwa mwalimu wake alimpa tiki kwenye jibu lakini haikuwa sawa.
Au hautaki kuwa Injinia mwanangu lazima ujue hesabu zote kwa usahihi kwani kile unachosoma Leo ndicho utakachokiishi kwenye kazi na maisha kiujumla. Hata hivyo lazima nikuchukue tu ukaanze shule mjini hakuna namna. alimalizia yule kaka yake na mzee Mgaya.

Watu wote waliokuwa pale walifurahi sana tena sana hususani Mama Mgaya maana alichokuwa anakiomba kimetimia hivyo ikawa ni furaha kwa Kila mwanafamilia hakika walifurahi mno huku furaha ya Samson ikiwa haipimiki, siyo tu kwakuwa anaenda kuanza masomo ya Sekondari bali ni kwenda kujionea jiji la Dar es salaam ambalo alikuwa akilisikia tu.

******************************
Muda wa saa nane mchana Mzee Mgaya na kaka yake walikuwa nyumbani kwa mwl mkuu wa shule ya Kijiji kile wakiwa na lengo moja kuhusu taratibu za kumuhamisha Samson lakini kwanza matokeo yake.

Kwanza nawashukuru sana kufika hapa kwangu kwaajili ya kutaka taarifa muhimu za mtoto wenu ni wazazi wachache sana wenye kufuatilia masuala haya wengi wanadhani kazi hii ni ya walimu pekee hapana, ni lazima tushirikiane wote kuhakikisha maendeleo ya mwanafunzi husika. alimalizia yule mwl mkuu mwanamke ambaye wanakijiji walikuwa hawampendi kutokana na dharau zake alizonazo kujiona Bora kuliko mtu yeyote.

Sawa Mimi naitwa James Mgaya ni ndugu wa damu na huyu baba yake Samson, lengo kubwa ni kutaka kufuatilia matokeo ya kijana wetu kama kafaulu au la. aliuliza yule mgeni na kumfanya yule mwalimu achukue funguo zake na kuwaambia wamfuate hadi shuleni maana Kila kitu kipo ofisini kwake .
Baada ya kufika mwalimu yule alichukua faili fulani na kulipekua huku wakipiga stori.

Enhee wenzangu nilisikia huyu kijana alipotea katika mazingira ya kutatanisha , vipi mlimpataje? aliuliza yule mwalimu.

Ukweli mwalimu kijana wetu ni msumbufu tu, alitutia hofu, akatutia aibu sana tu , ni kwamba alitoroka ila baada ya maisha kumshinda huko akarudishwa. Alijibu mzee Mgaya akafanya wote watatu wakacheka sana.

Sasa mzee niwe mkweli na muwazi kijana wenu wala hakuwa mzuri sana darasani, kwa maana ya si mmoja wa wanafunzi ambao nategemea kama watafaulu. aliongea yule mwalimu huku akibinua midomo kuonesha dharau kwa Samson akiwa na imani kuwa hawezi kufaulu.

Jambo lile lilimsikitisha sana mzee Mgaya akiona kuwa mwanaye hana bahati.

Mimi hapa nilikuwa na wanafunzi sabini na nne, waliofanya mtihani ni wanafunzi arobaini na nane tu, na kwa taarifa nazozisikia ni kwamba tuna wanafunzi saba tu waliofaulu arobaini na Moja wote wamefeli, aliongea yule mwalimu mkuu huku akitoa kicheko cha kejeli akimaanisha hana uhakika kama Samson atakuwa miongoni mwa waliofaulu.

Unasema ulikuwa na wanafunzi sabini na nne uliotarajia wafanye mtihani yaani ishirini na sita nzima uliwapoteza, ukajikuta una wanafunzi arobaini na nane tu, waliotahiniwa lakini pia kwanini wafaulu Saba tu? aliuliza kaka yake na mzee Mgaya

Swali lile lilimuudhi yule mwl mkuu wa kike, unajua baba jukumu la kulinda nidhamu ya mwanafunzi si la walimu pekee, laiti tungekuwa tunashirikiana baina ya walezi na walimu naimani suala la nidhamu lisingesumbua. alijitetea yule mwalimu.

Na kwanini wafaulu wanafunzi wachache Ina maana taaluma hakuna, wafaulu Saba? alizidi kuhoji yule mzee Mgaya mkubwa.

Suala hilo usitulaumu sisi, hujiulizi kwanini hawa Saba wamefaulu, Ina maana watoto wenu ndiyo wazito sisi wala hatuna tatizo.
alijibu mwl yule ambaye alikuwa mkali wanafunzi wenyewe walimuogopa.

Mzee Mgaya na kaka yake waliaga wakiwa hawajaridhika na majibu ya mwalimu yule, lakini Imani ya baba mkubwa wa Samson iliamini Samson yuko vizuri kichwani, kinachochangia ni taaluma ya shule ile kuwa chini.

**************************************
Ilikuwa ni wakati ambao Samson alikuwa na mama yake akipokea nasaha mbalimbali,

Mwanangu, bila shaka unaziona jitihada za baba yako na huyu mgeni ni jinsi gani wanakupigania, Sasa jua kabisa unakoenda unaenda kukutana na baba mwingine si huyu uliyemzoea, utakutana na watu wa Kila aina huko mjini, jitahidi kuwa makini heshimu Kila mtu, lakini usimwamini mtu haraka haraka,

Unaenda kukutana na mama mwingine, sisemi kwamba labda watakuwekea roho mbaya hapana nachelea kusema unatakiwa kupunguza kiburi, ujeuri na visa vyako kama ulivyotoka kutufanyia hapa siku chache zilizopita.

Samson alimsikiliza mama yake kwa umakini huku akijitahidi kutokumuangusha, ni kwamba Yale aliyokutana nayo kipindi katoroka yalitosha kumpa somo kuwa maisha siyo marahisi kama alivyodhani.na hii ilichangia kiasi kikubwa Samson kupenda shule.

********************************
Mzee Mgaya alisikitishwa sana na namna mwalimu mkuu alivyowajibu na kuwakatisha tamaa, lakini kaka yake yeye Imani yake ilikuwa kwa Samson, aliamini yule mtoto akitafutiwa shule nzuri atafanya vizuri .

Kesho yake iliwakuta kwa afisa Elimu wa wilaya yao, walipokelewa vizuri na Ofisa yule mchangamfu na mkarimu, wakaeleza shida yao kuwa ni kupeleleza matokeo ya kijana wao.

Ok, ok mjue wakati huu unakaribia sikukuu tulipaswa tupumzike lakini suala la wazazi kuja Kila siku kuulizia matokeo ya watoto wao limetufanya tuwe tunakuja ofisini Mara kwa Mara. aliongea yule afisa Elimu aliyeonekana ni muongeaji mzuri sana.

Mmesema namba pamoja na jina la mtahiniwa ni lipi? aliuliza yule afisa Elimu.

Kiukweli hatuijui namba ila kwa majina ya mtoto anaitwa Samson Elias Mgaya, aliongea kaka wa mzee Mgaya ambaye alikuwa anajiamini sana.

Afisa yule alitoka akiwaacha wageni akaingia kwenye chumba fulani akarudi huku akitabasamu.
Baba wa mtoto ni yupi ? aliuliza yule afisa.
Ni Mimi alijibu mzee Mgaya huku akijipiga kifuani kwa kujitambulisha.

Hongera sana bwana mwanao kafaulu tena mwaka huu shule yenu imeweza kufaulisha tofauti na miaka yote Kuna takribani wanafunzi 18.
Wamefaulu, na mwanao amefaulu kwa daraja zuri sana ndugu zanguni.
aliongea huku akionesha kufurahi yule afisa.

Lakini jambo la kusema shule imefaulisha watoto 18 wakati mwalimu wa shuleni kwao aliwaambia ni wanafunzi Saba tu walishangaa wakajikuta mzee Mgaya na kaka yake wanaangaliana.

Mara akaingia mheshimiwa fulani ambaye alijitambulisha wakaungana na akina mzee Mgaya kama sehemu ya wenye shida ya ofisi ile.

Nimekuja kuchukua fomu za uhamisho wa mwanangu ambaye anatakiwa mwezi wa kwanza akaanze kidato Cha kwanza huko Moshi mkoani Kilimanjaro. aliongea yule jamaa huku akijiseti kwenye kiti vizuri.

Sawasawa bila shaka mzee, alijibu yule afisa Elimu huku akiangalia vitu kwenye computer iliyo mbele yake, lakini pia akiwa anaangalia kwenye mafaili fulani yaliyokuwa mbele yake akiwianisha vitu.

Anaitwa nani mzee wangu, aliuliza afisa yule.

Anaitwa Samson Elias Mgaya. alijibu yule mzee bila wasiwasi.
Hali ile ilifanya afisa elimu, na akina mzee Mgaya washtuke sana, kwanini jina la mtoto wao litajwe na mtu mwingine,

Samahani mzee, Hawa unaowaona hapa wamekuja kuangalia matokeo ya mtoto wao anayeitwa kwa jina ulilotaja Sasa mbona siwaelewi kuhusu huu mgongano.

Yule mzee alipigwa na butwaa baada ya kusikia wale ndiyo wenye jina la ukoo wa akina Mgaya, akaanza kubabaika kuongea huku afisa yule akiwa anamtizama kwa umakini mkubwa sana.

Lakini kengele za hatari ziligonga kwenye kichwa Cha James Mgaya ambaye alishajua kinachoendelea pale. Je, Nini kitajiri baada ya wazazi wawili kutaka matokeo yenye jina moja nani yupo sahihi?

Usikose sehemu ijayo

Itaendelea ...................................
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Baada ya kushangazwa na tukio la wazazi wawili kuja kutaka matokeo ya jina moja, afisa elimu aliwaruhusu wote kwamba waende na warudi baada ya siku tatu.

Samahani ndugu afisa, Mimi ni kaka wa huyu ambaye ndiye mwenye mtoto, tumekuja hapa ili kufanya mpango wa kumuhamisha maana nataka nikamsomeshe Mimi.
aliongea James Mgaya.

Sawa, nimekuelewa ila mrudi baada ya siku tatu naamini mtapata majibu sahihi, tunahitaji kuweka wazi huu mkanganyiko nachojua mimi nimakosa ya kibinadamu tu yamefanyika ila naamin tutarekebisha wala msiwe na shaka. aliongea kwa lugha rafiki yule afisa kiasi cha Mzee Mgaya na kaka yake kuridhika na majibu yale kisha wakaondoka.

Mzee Mgaya ambaye ndiye mwenye mtoto hakuweza kugundua chochote kuhusu mkanganyiko wa ufaulu wa mwanae ila kaka yake alijua mapema na alifahamu kuwa hakuna jambo la bahati mbaya badala yake Kuna namna inatumika kudidimiza vipaji vya watu maskini, akapanga kulivalia njuga lile suala.

Unajua Nini ndugu yangu, hapa inabidi tufanye juu chini tuhakikishe tunapata haki yetu haiwezekani kipaji na haki ya mtoto wetu ikanyang'anywa na wajanja wachache halafu sisi tukafumbia macho, si kweli hata kidogo. alisema kaka wa mzee Mgaya.

Walifika nyumbani jioni sana wakiwa wamechoka kiasi, lakini baada ya kupumzika James Mgaya alipata wazo, akaona ni bora aongee na mtoto mwenyewe aone kama anapenda shule au la. Ikabidi amtege kwa maswali kadhaa.

Wakiwa wawili tu Samson na baba yake mkubwa wakiwa hatua kadhaa kutoka nyumba ilipo, walianza mazungumzo kama ifuatavyo,

Unajua mwanangu, Kila mwanadamu hapa Duniani kaumbwa na kipawa/au kipaji chake, kwa mfano mimi tangu zamani nikiwa mdogo nilipenda kazi ya ualimu, wapo waliopenda udaktari, wapo maafisa kilimo na mifugo kana yule mzee mwenye nyumba nzuri kule bondeni (akionesha na kidole Cha shahada nyumba ilipo)

Lakini wapo ambao wao hawajasoma lakini Wana pesa na Wana maisha mazuri tu, kwamaana ya walitumia vipaji vyao ambavyo wanavyo, kufika walipotarajia, au kwa lugha nyingine kutimiza ndoto zao.

Je, wewe Samson unahisi kipaji chako ni kipi, na malengo yako ni yapi? aliuliza yule mzee.

Mimi hapa kwanza sijui kipaji changu, ila nikiwa shuleni, Kuna mratibu wa Elimu aliwahi kuniambia kwamba nisome sana kwani Nina kipaji kikubwa, ila hakuniambia ni kipaji gani.Lakini pia baadhi ya walimu waliniambia kuwa kama nitasoma naweza kuja kuwa kiongozi mkubwa
sana. alijibu Samson.

Unadhani kwanini walikwambia unaweza kuwa kiongozi, ulifanya nini Hadi ukaambiwa hivyo?
aliuliza baba mkubwa wa Samson.

Nikiwa darasa la tano nilikuwa Monitor wa darasa , Sasa basi ikitokea wanafunzi wenzangu wamepigana nilikuwa nawaamulia na nawashauri waache mchezo wao mbaya bila kuwapeleka kwa walimu.

Lakini pia kulikuwa na mwalimu wa darasa letu alikuwa mkali sana,
Sasa siku moja akaja na attendance kwaajili ya kuwaadhibu wanafunzi watoro, basi kutokana na hofu waliyokuwa nayo wanafunzi wenzangu niliamua kuwaombea msamaha kwa mwalimu, nikimwambia awasamehe hawatarudia tena.

Lakini mwalimu alikasirika sana akaniambia kwanini namfundisha kazi anawezaje kuwasamehe wanafunzi wasiokuwa na nidhamu, Sasa adhabu ya hawa utabeba wewe nifuate ofisini, nilimfuata Kisha nikashambuliwa na walimu nikapigwa sana nikarudi darasani nikiwa kawaida tu. alifafanua Samson

Kwahiyo hapo sifa ya uongozi inakujaje hapo? aliuliza yule mgeni

Mwalimu mkuu msaidizi aliniita kesho yake akaniambia kwanini nilikubali kuadhibiwa kwa kosa ambalo si langu, nikamjibu kuwa huwa sipendi kuona mtu akifanyiwa jambo baya mbele yangu.

Unajifanya Nelson Mandela eehh, utakuja kufa shauri yako, ila nimependa misimamo yako soma sana huenda ukaja kuwa kiongozi Bora baadaye, Samson anaelezea yale aliyoambiwa na mwalimu wake.

Sawasawa, unaonekana una upeo mzuri ila hujanijibu ni kipi ukiambiwa ufanye Sasa hivi, utafanya kwa usahihi?aliuliza yule mzee.

Kwasasa sijui labda ningesoma kwanza nitajua mbele kwa mbele. alijibu Kwa kifupi Samson.

Unaonaje nikikupa mtaji ufanye biashara. aliuliza kimtego Yule Baba yake mkubwa.

Mimi kwanza sijawahi kufanya biashara, japo naipenda sana , ila baba kwanini hayo nisingeyafanya baada ya kusoma na kuwa na elimu?
Kwasababu hata walimu wetu walituhimiza tusome sana wakidai mtu Ukiwa na Elimu unaweza fanya mambo kirahisi zaidi tofauti na asiyesoma. alijibu Samson

Hadi hapa baba mkubwa wa Samson alishajua kuwa samsoni anapenda shule, na alifurahi kwasababu walipanga kuhakikisha Kila kitu kinakaa sawa kuhusu kutaka kudhulumiwa jina la mtoto wao, lakini alitaka ajiridhishe kwanza , maana wasije kuhangaika na mtu ambaye pengine hapendi shule.

Lakini mwanangu nakuona upo vizuri kichwani, Nini kilipelekea ukatoroka hadi kuwaweka wazazi wako kwenye wakati mgumu,? aliulizwa Samson

Lakini hakuwa na majibu ya swali hili badala yake aliomba msamaha tu hasa ukizingatia ndiye atakayetoa msaada, ikabida Samson awe mpole

Siku tatu baadaye kama kawaida, kama walivyoambiwa waje walikuwa kwenye ofisi ile huku wakitazamana na afisa elimu, akiwa siku hiyo kabadilika akiwa Hana tabasamu zuri.wakasalimiana.

Mnajua nyinyi labda niwaweke wazi tu kuwa yale matokeo ya mwanzo yalikosewa kumbe, hivyo tumefanya kazi kubwa kuwasiliana na wenzetu waliopo ngazi ya mkoa hatimaye tumeletewa matokeo mengine ambayo yanaonesha mtoto wenu kwa bahati mbaya hayupo kwenye list ya waliofaulu. niwape pole tu kwa usumbufu. aliongea huku akionesha hajapenda ujio wao.

(James Mgaya akicheka)
Samahani afisa unadhani ni rahisi kutuambia maneno hayo hebu kuwa na aibu hata kidogo basi kwanini Kila siku mnatufanya wajinga naomba nipate barua ya kuweza kufuatilia matokeo ya mwanetu huko huko mkoani. aliongea kwa jazba bila uoga ndugu wa mzee Mgaya.

Sasa mzee Ina maana huniamini au kwanza usilete ujuaji kwenye ofisi yangu nitakufunga. alitishia yule afisa elimu huku akivua miwani yake.

Ni mpambano wa vita mpya kati ya James Mgaya na afisa elimu.
Je, nani atashinda huu mpambano. Usikose sehemu ijayo.
 
Duh.imekuwa fupi sana Na ni nzuri mno.kwani inafundisha pia.hongera mwandishi ila. Jitahd utuongozee epsod mzee
 
moneytalk
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO.

Taarifa za kuonekana kuwa Samson amefaulu ila jina lake limeuzwa liliihuzunisha sana familia ya mzee Mgaya, Mama Mgaya alijikuta anamuonea huruma mwanaye akijua kuwa haiwezekani tena, hata Samson mwenyewe alinyongea huku akishindwa hata kula vizuri, anaikosa shule, lakini anakosa kwenda Dar es salaam jiji kubwa kuliko yote Tanzania, sehemu anayoisikia kwa watu tu huku akijenga taswira anayoijua yeye kuwa Dar es salaam inafananaje.

Muda huu mzee Mgaya na kaka yake walikuwa kwenye klabu moja cha pombe za kienyeji wakiwa lengo kubwa si kulewa bali ni kujadili namna ya kufuatilia matokeo ya kijana wao.

Ndugu yangu, kwanza nikushukuru kwa jitihada ulizozifanya hadi kufikia hapa na nashukuru kufahamu utapeli na tabia mbaya zinazofanywa na walimu hakika hili limenifumbua macho sikuwa najua,
Lakini mimi nikuombe kitu kimoja tu kwamba kila kitu hupangwa na MUNGU lakini pia Kila mwanadamu na riziki yake,
Wanasema kisicho riziki hakiliki, au siyo kaka, lakini wanasema riziki haivutwi na kamba.
aliongea baba yake Samson huku akijichekesha kupalilia kauli zake.

Una maanisha nini kusema hivyo,
aliuliza kaka yake na mzee Mgaya.

(Akicheka cheka)
Mimi nakuonea huruma ndugu yangu naona kama muda unaenda, lakini pia gharama za usafiri Kila Mara nazo si haba, lingine tumemuona fika mtu ambaye tunagombania jina anaonekana ni mtu mzito unadhani hili linawezekanaje? Tunaweza tumia muda mwingi na gharama kubwa na tusifanikishe zoezi ketu hivyo naona tuache tu haya mambo. mzee Mgaya aliweka kituo.

Kwanza siamini kama maneno haya yanatoka kwenye kinywa chako mdogo wangu, yaani Mimi ndiye nilitakiwa kuonesha kukata tamaa kwakuwa ndiye ninaye toa pesa, lakini pia Nina kazi chungu mzima zinanisubiri mjini, lakini naamua kukusaidia kwa moyo tu ili mwanao asome, maana maisha na kadri miaka inavyosonga Dunia inawahitaji wasomi hata kazi ya kufagia maofisini, Sasa mbona sikuelewi ndugu yangu. aling'aka kaka wa mzee Mgaya.

Na ukizingatia walikuwa wanakunywa pombe wakajikuta wanazozana muda mrefu sana huku wakiinuka kushika njia ya kurudi nyumbani.

Mida ya jioni saa kumi na moja alikuja mwanamke fulani wa makamo nyumbani kwa akina Samson, si mgeni machoni mwao, na ukizingatia hakuna mwanamke mwingine kwenye Kijiji kile anavaa vizuri kuliko yeye , wakamtambua akiwa bado yupo mbali alikuwa ni mwl mkuu wa shule iliyopo kwenye Kijiji kile, si kawaida mwalimu yule kutembea kwenye nyumba za watu, ni kutokana na dharau alizokuwa nazo.

Hodi wenyeji wa nyumba hii,
alibisha akiwa bado yupo mbali.

Karibu, karibu sana mwalimu,alikaribisha mama Mgaya huku akimkaribisha ndani.

Akhaa!! siingii ndani mwenzangu nileteeni tu kiti nikae hapa nje. alijibu mwalimu yule, huku Kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kujua ana shida gani.

Jamani wenzangu kumbe mna kuku wengi hivi mama Mgaya, yaani hata siku moja kusema ngoja tumpelekee mwalimu naye akale nyama ndugu zanguni? sisi walimu hasa mimi tunatakiwa tutunzwe na nakumbuka kipindi naletwa huku niliambiwa Kuna watu wakarimu sana, lakini nimetimiza miaka nane Sasa Sijaona watu wachoyo na wenye roho mbaya kama wanakijiji wa hapa, jamaniiiiii
Nitasimulia. aliongea kwa dharau yule mwalimu.

Hapana mwalimu, kukupa kuku mmoja wala siyo shida tatizo mmiliki mwenye kuku wake yaani hapa anamjua hadi kifaranga wa mwisho hivyo wakipungua ni kesi ya jinai, aliongeza mama Mgaya wakajikuta wote wanacheka.

Wakati huo sauti za watu ambao zinaonesha ni mazungumzo yasiyo ya amani zilikuwa zinakuja huku zikiwa zimetambulika tayari ni nani na nani, hatimaye mzee Mgaya na kaka yake walifika huku wakifikia nje wakiwa wanashangaa ujio wa mgeni ambaye huwa si rahisi kutembea kwenye majumba ya watu

Karibuni jamani, maana mimi mmenikuta hivyo inabidi niwakaribishe ninyi, aliongea kwa madaha yule mwalimu mkuu huku macho yakigongana vema kabisa na James Mgaya, huku Kila mmoja akimkumbuka mwenzie vizuri.
Wakasalimiana.

Jamani kabla ya giza halijaingia kwanza niwashukuru wote kwa kuweza kutukutanisha , aaah lengo langu kubwa ni kuja kuongea na ninyi kuhusu mzigo wa lawama mnaotaka kuniangushia kuhusu kijana wenu samweli sijui Samson?

Wote wakamjibu anaitwa Samson Elias Mgaya.

Enheeeeeeh, huyu mtoto tayari ananinyima Mimi usingizi, yaani mzee Mgaya na familia yako mnanitwisha mzigo usionihusu, kwanini lakini, jamani? aliongea yule mwanamke huku akipandisha sauti kuwa ya juu.

Jamani waliofaulu, wamefaulu.
Samson hajafaulu, na siyo Mimi niliyemfelisha, siyo Mimi niliyemkosesha majibu ili afeli, kubwa zaidi Mimi sijasahihisha mitihani yake kwamba labda nilimfelisha makusudi,
Matokeo yamekuja, huku Mimi nikiwa kama mwalimu mkuu nikipenda wangefaulu hata darasa Zima, kwani hii itanipa sifa nzuri zaidi mimi. Sasa nasikia mmeenda hadi wilayani kufuatilia matokeo kwanini lakini tunachafuana bila sababu?
aliongea huku akimkazia macho baba yake Samson.

Aaaammm unajua mwalimu sisi tulienda kuhakikisha tu lengo letu si kwaajili ya kukuchafua bali ni kutaka kujua matokeo ya mwanetu tu, alijitetea mzee Mgaya huku akionesha anamuogopa yule mwalimu, na si yeye tu asilimia nyingi ya wanakijiji kile walikuwa wanamuogopa sana yule mwalimu hasa kwakuwa huwa anaonekana eti, msomi lakini pia ni mke wa mwanajeshi mwenye cheo kikubwa jeshini jambo lile lilimuongezea kujiamini sana mwalimu yule.

Akaendelea........

Wanafunzi waliofaulu wanajulikana, na kama tungekuwa na uwezo huo tungefaulisha wanafunzi wote hata Samson angekuwepo, aliongea yule mwalimu huku akiwa anaaga na kutaka kuondoka.

Wakati wa mazungumzo na lawama zote alizotoa mwalimu, Mzee Mgaya mkubwa alikuwa kimya Wala hakuchangia chochote kile, alikuwa anamsoma tu yule ticha huku akivutiwa na uzuri wa yule mwanamke jinsi alivyo na shepu matata hakika alipendeza sana, lakini pia alikuwa hadhi yake!!

Tangu afike kwenye Kijiji kile kutoka mjini hakuona mwanamke mwenye hadhi ya kutembea na yeye licha ya kuwa anapenda sana ngono mzee yule, akajua kabisa ataikaribisha sikukuu ya Christmas na mwaka mpya akiwa na mwalimu yule. pombe za kienyeji zilimlewesha akajikuta badala ya kuchangia mada ya Samson yeye anamthaminisha yule mwalimu.

Jamani mzee Mgaya, naomba kuku mmoja jamani hata kusema mwalimu wetu naye akajisikie vizuri, mnajua wazi Kijiji chenu hakina butchers za nyama yeyote.
alisema kwa kudeka mwalimu yule Mrefu, mwenye rangi na shepu safari hii akiwa kasimama huku Mzee Mgaya mkubwa udenda ukimtoka kwa yalikuwa ndiyo mambo yake

Bila kuuliza kwakuwa ilikuwa Giza linaingia kuku washaingia bandani, alitumwa Samson, atafute jogoo fulani wa wastani akapewa mwalimu yule, hakika alifurahi sana.

Kesho tunakuja kula wote mwalimu, aliropoka mzee Mgaya mkubwa huku mwalimu yule akigeuka na kumwangalia mwanaume mwenye ngozi ya mafuta, na pia ni mrefu mwili mkubwa na kaunda suit yake iliyomkaa vyema. Wakajikuta hawaongei Bali wanaangaliana huku wanatabasamu Kati ya mwalimu na James Mgaya.

Wakubwa wakaelewa, huku mwalimu hakujibu neno akaaga akiwa anasindikizwa na mama Mgaya Hadi mbele kidogo, Kisha mwalimu akarudi nyumbani kwake maeneo ya shule zilipo nyumba za walimu

Usiku ule mzee Mgaya aliwaza namna ambavyo kaka yake anataka kumtia matatizoni kwa kulazimisha Samson aonekane kafaulu huku hajafaulu kama mwalimu mkuu anavyodai, akapanga asubuhi yake atamchana makavu.

James Mgaya yeye kutokana na kulewa sana alijikuta anawaza ngono tu, akapanga hawezi rudi Dar es salaam bila kutembea na yule mwalimu lazima iwe hivyo tumeumbiwa sisi namkosaje huyu ticha? alijiwazia Kisha akalala.

Mama Mgaya, roho ilimuuma sana ilimkereketa, maneno ya tambo za mwalimu mkuu, yalimkatisha tamaa kibaya zaidi si mume wake Wala shemeji yake aliyeonekana hata kusimama na kuweka msimamo wameishia kunyamaza huku akipewa na zawadi ya kuku juu.

Ina maana ndoto za mwanangu hazitimii? Lakini mbona Sam anapenda shule jamani, hata nikikaa naye anawaza shule tu, halafu macho waliyoangaliana Kati ya mwalimu mkuu na shemeji yake yalimkatisha tamaa akaona hapa hakuna mfuatiliaji kama watu wanatamaniana tena?

Kwa upande wa mwalimu mkuu aliwaza sana huku akimkumbuka yule mgeni, alikuja hapa ofisini siku si nyingi, halafu anaonekana ana maisha mazuri, sijui anaishi mkoa gani, Mimi mwenyewe sijakutana na mume wangu mwaka sasa, tangu aende nje ya nchi kusoma, licha ya kuniambia mwezi uliopita atarudi Dar es salaam Kisha atakuja Hadi hukuuuuu hakufanya hivyo aliishia kambini kwao tu Kisha nikasikia kuwa alirudi tena masomoni, najua alipenda kuja huku ila ilishindikana kutokana na amri za wakubwa wake.
Mmmmh hizi kazi zina changamoto sana. aliwaza akiwa kitandani mwalimu yule

Kwa hadhi yake hakuona mwanaume yeyote wa kutembea na yeye wote katika Kijiji kile aliwaona hawana hadhi licha ya afisa kilimo na mifugo kumsumbua sana, lakini bado alimuona hamfai ila siku ile baada ya kukutana na mzee Mgaya mkubwa alijikuta anadata.

Asubuhi ilifika mzee Mgaya mkubwa pombe zilimuisha , hakutaka Tena kuwekewa maji na shemeji yake akiona si heshima akaweka akaenda bafuni akajiswafi huku akiwa na wazo moja kabla sikukuu hazijafika awe kashashughulikia suala la Samson.
Alisahau ya Jana licha ya kukumbuka baadhi ya vitu ila mengi alisahau.
alivaa akiwa tayari na safari ya kwenda mkoani akiwa na documents kadhaa ambazo Kila anaposafiri hutembea nazo ili kuwatisha na kuwaonesha wadhifa wake wanaomdharau .

Kaka vipi tena, wapi asubuhi hii.
aliuliza baba yake Samson.

Wewe acha ujinga , wewe tulia Lima fanya kazi zako mimi naenda mkoani nitarudi kesho na shemeji naomba baadhi ya vyeti vya kijana huyu, aliamrisha James Mgaya kwakuwa ile familia aliimudu.

Lakini shemeji kwanza taarifa kama hizi lazima zianzie shuleni aliposoma wale Wana data zake nyingi, ni vema ungeongea na mwalimu aliyekuja Jana kwanza yeye ndiye anayefahamu. alishauri Mama Mgaya.

James Mgaya akamuunga mkono shemeji yake huyo , huku akibadili uelekeo akienda kwa mwalimu mkuu, akiwa vizuri tu, pombe zimemuisha na kasahau kama alimtamani yule mwalimu.

Nini kitajiri akimkumbuka/wakikumbukana.

Itaendelea.............
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom