Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA KUMI NA SITA

Mwanangu hebu amka, amka Samson nakwambia, ama kweli ng'ombe wa maskini hazai, amka chukua mbegu ya mahindi humo twende nazo shambani.
Yaani dada zako wanakuwa wa kwanza kuamka kuliko wewe mtoto wa kiume, hebu acha ujinga, wewe ni mkulima tu , na kilimo hikihiki ndiyo utakufa nacho. Maana toka uambiwe mpango wa kwenda mjini na huyo baba yako mkubwa basi hata kazi hutaki. aliongea Mama Mgaya katika harakati za kumwamsha mwanae.

Samson aliamka akiwa mnyonge sana akanawa uso na kuelekea shambani huku wazazi wake wakija nyuma wakipiga stori.

Ujue mke wangu naona una Imani sana na kaka yangu kuhusu yale aliyoyasema kuhusu Samson, labda nikwambie tu kuwa wewe humjui yule, Mimi yule ni ndugu yangu namjua kuanzia utosi hadi unyayo (akimaanisha anamjua vyema)

Mara oooh nitamsomesha huyu mtoto, Mara oooh nitawajengea nyumba nzuri, yaani Kila kitu anaongea yeye, na hakuna mtekelezaji pale, no kwamba Hawa kuku tunaomchinjia Kila siku anakula nyama basi anajiikuta anatoa ahadi za uongo, yule ni muongo sana, ni ndugu yangu lakini usimwamini haraka kauli zake,ohhooooh.
aliweka kituo mzee Mgaya.

Lakini baba Samson, kama kweli angekuwa muongo angekubali kupoteza nauli Hadi wilayani kuulizia matokeo? Yaani nauli ipotee kirahisi tu. alihoji mama Mgaya.

Mke wangu, wewe mtu mwenye sifa, mwenye kupenda kujikweza,mwenye kutaka kuonekana, humjui. anaweza kutumia gharama kubwa sana ili atimize lengo lake kutaka kukubalika.
Kwanza nishamchoka Bora aondoke tu, ananizurulisha tu, kazi zangu haziendi hata mke mwenzio huko kashaanza kunilaumu kuwa nafanya kazi upande mmoja lakini pia hata Mimi naona kabisa ninavyofeli hivyo lazima nikatae tu na safari hii siendi sehemu yoyote yule msumbufu tu.
alilaumu mzee Mgaya huku wakiwa wanakaribia kufika shambani kwao.

Mama Mgaya hakuwa na neno yeye alimshukuru MUNGU kwa Kila kinachoendelea akiamini huenda si riziki ya Samson.

Mwambie Samson, aendelee kuchimba mashimo, na dada zake watupie mbegu. aliamrisha Mzee Mgaya kwa ukali.
Halafu wewe Samson nakuona upo taratibu sana, hebu changamka usiniletee ujinga wako, hebu hakikisha mistari inanyooka sawa , wewe ndiye mwanangu pekee wa kiume halafu tena nikupeleke ukakae kwa watu. weeeee haiwezekani wewe ni mrithi wa haya Mashamba yangu , Hawa dada zako muda wowote wanaolewa.
Wewe ndiye mwenye kuendeleza jina langu. aliweka kituo mzee Mgaya.

Maneno yale yalimtisha na kumuhuzunisha Samson, alijikuta analia lakini hakuwa na namna mbaya zaidi hata baba yake mkubwa haoneshi Nia kama ilivyokuwa mwanzo.

Mama Mgaya alitambua muonekano na mawazo ya Samson, akajikuta anatoa kicheko cha kumuhurumia akiamini ndoto za mwanangu hazitimii.

***********************************HoHodi, hodi humu ndani, ilikuwa ni sauti ya James Mgaya, akibisha hodi kwenye nyumba ya mwl mkuu,

Nani, hebu nisubiri navaa, alijibu mwalimu yule huku akijifunga nguo ya kitenge , akatoka nje akashangaa kumuona yule mgeni ambaye alimuona Jana kwa mzee Mgaya.

Karibu, una shida gani baba. aliuliza

Ni kweli Nina shida ila ni vyema tungekaa maana ni maelezo marefu.
alijibu mzee Mgaya mkubwa huku akikaribishwa ndani.

Wakati huo mwl mkuu yule bado alikuwa hajiamini, maana huwa si rahisi kutembelewa na ugeni hasa nyumbani kwake mbaya zaidi hamfahamu.

Samahani baba, Leo ni Mara ya tatu nakuona, mlikuja na baba yake Samson kuulizia matokeo na Jana nilikuona pale pale vipi Kuna shida gani. aliuliza yule mwalimu kwa shauku ya kutaka kujua.

Naitwa James Mgaya ni ndugu wa damu kabisa na baba yake Samson. alijitambulisha.

Ooooohooo sawa ni kweli mnafanana baadhi ya vitu hata masikio yenu mnafanana, vipi wewe ni mdogo wake eeeeh. aliuliza mwalimu.

Hapana yule ni mdogo wangu Tena nimemzidi miaka kumi nzima na hapa Kati tuna dada yetu ambaye nimemzidi miaka sita nzima. alifafanua

Haaaa dah basi ulivyo unaonekana kijana kabisa, maana siamini kama umemzidi umri Baba yake sam.labda ni kazi ngumu zinamzeesha
Ehhee na unaishi wapi maana inaonesha hauishi hapa kijijini kwetu. aliuliza mwalimu.

Naishi jijini Dar es salaam, tangu miaka kama thelathini iliyopita, akaanza kujitambulisha vitu vingi sana James Mgaya kiasi Cha mwalimu kugundua kuwa kumbe anaongea na mtu mwenye uzito wake.

Safari hii mwalimu hakuwa na wasiwasi kwani, alishamtambua mgeni kwa kiasi fulani, ambaye ni mtulivu kwenye kuongea lakini pia ana mvuto........
Licha ya dharau za mwalimu yule kwa wanaume wengi lakini huyu alipenda hata akae tu.

We mzee unasema umepigana hadi vita vya Uganda? taratibu usije umbuka Mimi mume wangu ni mtoto wa marehemu (jina kapuni) huyo marehemu alipigana vita hivyo akiwa mmoja wa wanajeshi wanaoheshimika kwenye nchi hii, huyo ndiye kamuinspire mume wangu kuingia jeshini. Je, huyo mkwe wangu unamfahamu? aliuliza mwalimu yule.

Nimeshakwambia nimepigana vita hivyo, Ina maana huniamini mwalimu?
Huyo marehemu mkweo alikuwa mwanajeshi wa kawaida sana, ila alionesha ubunifu mkubwa akiwa jeshini, ikiwemo ushapu, uharaka wa kutengeneza vitu, kama mahema, lakini pia kuwa na uwezo wa kutambua aina za silaha, alikuwa anajua hiyo ni silaha gani hata ambazo jeshi letu halikuwa nazo.
Lakini pia alikuwa fundi, licha ya Idd Amin kubomoa daraja mzee yule alikuwa mwepesi wa kubuni na kufanikisha kujenga temporary bridge hali iliyofanya aaminike jeshini na baada ya kuisha vita ni mmoja wa wanajeshi waliopata vyeo vya juu.
alifafanua mzee Mgaya.

Hapo sawa nimeamini ni kweli,Sasa karibu maana tumeongea porojo nyingi bila kuuliza shida iliyokuleta, aliongea mwalimu yule ambaye alivaa kinyumbani nyumbani.

Unasema mumeo ni mwanajeshi, yupo wapi kwa Sasa maana watu tunaogopa fumanizi ndugu yangu. alijihami mzee Mgaya.

(Huku akicheka)hapana bwana Mr hayupo yupo nje ya nchi kusoma hivyo usiwe na hofu. wakati hayo yakiendelea kililetwa Chakula na Fulani kama chai ya asubuhi wakajikuta wote wanajumuika kula huku wakipiga stori.

James Mgaya, ujue jina lako si geni kwangu, nimejikuta nazidi kukumbuka zaidi, ni kwamba Mara ya mwisho mwezi uliopita nilichukua barua Za sanduku letu, nikamtumwa mwalimu wangu aipeleke kwa ndugu yako si hilo tu, pia Kuna telegram ya hela ilitumwa mwaka Jana ikiwa inaenda kwa ndugu yako huyo huyo Hadi nilijiuliza nani katuma hela nyingi hivi , ilikuwa takribani lakini moja na nusu, si kawaida ujue. alitamia yule mwalimu mkuu wote wakacheka.

Hata shida iliyompeleka pale James Mgaya alisahau, hata mwalimu alijikuta amesahau kuuliza Nini kimemleta pale yule jamaa badala yake walijikuta wanatamaniana wazi wazi, James ni mmoja wa wanaume wakware tangia zamani huwa hapendi kupitwa na mwanamke mzuri,Licha ya umri kusogea lakini bado alikuwa yumo.

Mwalimu Agness, au Anyes kama walivyomuita wanakijiji wa pale alijikuta anababaika na mwanaume mmoja mzee wa mjini, anayejua kuchana nywele zake vizuri, anayejua kuvaa, suti ya bluu iliyonyooka kwa pasi ya mkaa yenye kijogoo inayopatikana kwa akina Samson, ilitosha kuonesha na kudhihirisha umaridadi wa James Mgaya. lakini kubwa lilimvutia mwalimu mkuu ni perfume ya kiume toka uarabuni ambayo mzee Mgaya alinunua kwa wapemba huko Zanzibar.

Ilifanya Kila muda mwalimu amwangalie mzee James Mgaya, na Kila walipogongana macho mwalimu aliangalia pembeni huku akionesha hajiwezi.

James Mgaya mkongwe, mwanasaikolojia aligundua ile hali akaamua kupiga ndege wawili kwa jiwe moja, yeah alijua fika huyu ndiye aliyeuza jina la Samson kwa watu wengine hivyo atambembeleza Hadi atajua ukweli na atasaidia kurahisisha matokeo ya kijana wao kupatikana, la mwisho kabisa angefaidi uzuri na utamu, wa penzi la mwanamama yule.

Mwalimu alimuaga mzee James akiingia chumbani huku, akiwa tayari mwili wake upo kwenye hali isiyoridhidha, ni mwanamke, ni mwanadamu, anakula ana afya njema, kubwa zaidi hajakutana na mwanaume kwa muda mrefu, lakini hatimaye alimpata mtu ambaye huenda akakidhi haja zake.
Akajikuta anaapa kwamba lazima aoneshe mitego yake Kisha akatoka akaja sebuleni.

Samahani mgeni tumeshindwa hata kukupokea briefcase yako, aliongea yule mwalimu kwa madaha.

Mzee James akajikuta ananyang'anywa mkoba wake Kisha ukawekwa kando, alielewa somo huku akijitahidi kuwa mwepesi na kumrahisishia somo mwalimu yule, alipanga kuwa lecture wa muda kwa yule mwalimu.

***********************************
Mke wangu mpaka saizi saa nane watu tumeenda shamba tumerudi lakini ndugu yangu hata hajarudi, huyu kaja kuzurura mke wangu yaani hata haeleweki kaja kufanya nini
Sasa wewe kwenda kwa mwalimu mkuu kuomba matokeo, hadi saizi, Mimi mke wangu nibishie tu lakini ukweli utaujua tu kaka yangu kabahatika tu kuwa na hela lakini Kuna mambo huwa yanamshinda sana alilaumu sana mzee Mgaya.

Milango ya mafanikio itafunguka kwa Samson? au ataishia kuwa mkulima wa jembe la mkono kama anavyosema baba yake?

Itaendelea..........
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA

Hatimaye mzee James Mgaya na mwalimu Agness walijikuta, wamevunja amri huku mwanamke akiwa na kaaibu fulani ka kike

Samahani mwalimu, nadhani toka nifike hapa sijasema kilichonileta, lakini pia hata wewe hujaniuliza, lakini hilo si jambo baya, ni kwamba nimekuja ili unipe ushirikiano wa kupata jina la mwanangu mtoto wa mdogo wangu, inavyoonesha amefaulu tena kwa alama nzuri hivyo basi hivyo tumeambiwa tuanzie kwenye ngazi yako, ukiwa kama mwl wake. aliongea kwa kukaza macho mzee James.

Aaaammm sasa, mbona kama tunarudia haya masuala , jamani huyo mtoto kama kafaulu wote tungejua Kila kitu kipo wazi, huu ukakasi mnaoupata ni kwamba huyo kafeli, jamani ndugu yangu unakwama wapi kulitambua hili?
Unakaribia kuvunja furaha yetu, naomba ujue kuwa umenifurahisha sana mtu mzima mwenzio hivyo hebu tuenjoy na penzi letu kwanza, hayo mengine tutayashughulikia sawa baba. aliongea mwalimu Agness, huku akionesha mahaba ya wazi kwa mzee James.

Sawa, ila Mimi sijaja kwaajili ya kufanya kilichofanyika, hizo ni nguvu za shetani tu zimetuzidia, ila kwakuwa hujataka kuonesha ushirikiano kwenye hili basi Mimi naomba uniruhusu niondoke,. aliongea Mzee James huku akiinuka kutaka kuondoka.

Ha ha hapaaana, hebu ningoje kwanza nakuja. aliongea mwalimu yule huku akiingia chumbani kwake.

Huyu mzee vipi mbona king'ang'anizi?
Jamani, kwani baba yake Samson si yupo? Kwanini huyu mzee anajifanya kimbelembele kutaka matokeo ya kijana wao.
au nimkatishe tamaa zaidi nimwambie anajisumbua tu, hatapata anachokihitaji,
huyu dawa yake ni kumdharau tu, wenye mtoto wametulia hawana shida, lakini yeye kashikilia hili suala..............

Lakini sipaswi kumdharau maana sijui ana wadhifa/cheo gani, na anasema ni mstaafu wa jeshi la wananchi, najua wastaafu wengi huwa bado wana nyadhifa serikalini,
mmmmh hapana napaswa kuwa makini na jambo hili linaweza kuleta matatizo baadaye. huyu atachoongea inabidi nimsikilize.
aliwaza sana akiwa chumbani yule mwalimu.

Mwalimu samahani naomba uniruhusu niondoke maana nachelewa. aliongea Mzee James huku akiwa nje ya zile nyumba za kota za kijijini zisizokuwa na uzio.

Hapana mzee nakuja, alijibu mwl Agnes huku uso Ukiwa wenye hofu kubwa (huku akijichekesha)
Kwahiyo mzee wangu unaelekea wapi , aliuliza mwalimu.

Hapa silali tena kwenye hiki Kijiji, maana hata bwanamdogo nishamuaga kuwa lazima nifike mkoani kwaajili ya kulitimiza hili, na nilipita kwako hapa kusudi unipe ushirikiano lakini hata hivyo si mbaya nitajua huko huko. aliongea kwa kujiamini mzee James huku namna ile ikizidi kumpa woga mwalimu Agness.

Lakini unajua kama kesho ni Christmas Ofisi hazitokuwa wazi? pia hata keshokutwa bado ofisi hazitokuwa wazi, hebu jaribu kufikiria kwanza. alishauri mwl mkuu

Haya yote nayajua ila nitakaa huko huko hadi pale ofisi zitakapokuwa wazi, naamini Kila kitu kitakaa sawa kwasababu naenda kufanya vitu vingi tofauti tofauti. alijibu mzee James.

Mwalimu Agness tumbo lilimkata akajikuta Hana la kufanya, Maana aligundua kuwa yule mzee ana Nia ya kumsomesha Samson na hatanii hata kidogo akajikuta anaropoka.

Basi twende wote huko mkoani mzee mwenzangu, aliongea mwalimu huku akijichekesha kwa uoga.
Hata James Mgaya alishangaa kuona mtu anataka kuongozana naye, akamuashiria kwa kichwa kuwa amekubaliana naye.

***************************************
Mzee Elias Mgaya au baba yake Samson, aliiaminisha familia yake kuwa harakati anazofanya kaka yake ni batili Wala hazitakuwa na manufaa yoyote, hii ilichochea na kujenga Imani kwa wengine kuwa haiwezekani

Aliyasema hayo kwasababu hakuwa na uwezo wa kumsomesha mtu hivyo kama Samson asingeenda shule basi kwake ingekuwa poa tu
. na hata Samson mwenyewe tayari alianza kumwelewa baba yake. aliona wazi jinsi ndoto zake zinavyokwenda kuzimika lakini hakuwa na namna, akakiri kwamba ng'ombe wa maskini hazai na pia hakutamani tena kwenda popote eti kutafuta kazi au kibarua chochote,

Maana taabu na shida alizozipata kule jumlisha matusi, kejeli toka kwa watu ambao ni kama hawajazaliwa na mwanamke kwa namna wanavyotukana, akaona Kwa umri wake Bora aendelee kukaa tu pale nyumbani kwao.

Siku inayofuata ilikuwa ni sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo.
Basi kama ilivyo shamra shamra Duniani kote, ndivyo ilivyokuwa kwenye Kijiji cha akina Mzee Mgaya.

Wakati mzee Mgaya akiwa kwenye kilabu fulani Cha pombe za kienyeji, alifuatwa na jamaa fulani huku akiulizwa kaka yake ambaye huwa anaongozana naye yuko wapi, ikabidi amjibu kuwa kasafiri.

Asafiri? asafiri wapi wakati watu tumemuona Jana akiingia sehemu moja nyeti kabisa, na hatukumuona akitoka, na hata Leo hii ndugu yako yupo kwa mwalimu mkuu kafungiwa ndani,na katika huu msimu wa sikukuu watu wengi wanarudi makwao, huwezi jua mume wa yule mwalimu anarudi saa ngapi, huoni kama ndugu yako yupo hatarini?aliongea yule mmbea kwa uchungu.

Maneno yale yakuonekana kaka yake yupo tu pale kijijini kwao akiendekeza umalaya, yalimuhuzunisha mno Mzee Mgaya huku akirudi nyumbani na kumsimulia mkewe.

**************************************
Siku ya sikukuu James Mgaya licha ya kupata changamoto kutokana na ulinzi uliopo alikuwa nyumbani kwa mkuu wa wilaya wakipiga stori kwani walikuwa wanafahamiana kipindi kirefu sana, tangu akiwa jijini Dar es salaam kabla hajahamishiwa mkoani

Ndugu yangu vipi tena sikukuu kubwa kama hii umekuja kula huku kuliko kutulia nyumbani na watoto wako, maana si wenzako tunatamani tungerudi nyumbani, lakini kwa nafasi na kubanwa na shughuli nyingi za ujenzi wa taifa tumejikuta tumenasa hapa hapa. alitania mkuu wa wilaya

Ndipo James Mgaya alipofunguka masuala ya Samson kuanzia mwanzo mpaka mwisho, huku akiweka wazi A to Z.huku akiweka wazi dharau alizowaletea afisa elimu.

Haya mambo yamekuwa mengi hususani mikoa ya nyanda za juu kusini, masuala ya kuibiwa na majina na kupewa wanafunzi wengine yamekuwa ni matukio ya kawaida
Na nashukuru sana kwa wewe kujitolea kuweza kufuatilia shida hii , kama kweli kijana wenu ni miongoni mwa waliofaulu basi naamini hili tutaliweka sawa, ila naongea na wewe kirafiki tu isije kuwa mtoto wenu kafeli ila mnataka kuchafua watu tu, alionya yule mkuu wa wilaya.

Baada ya mazungumzo yale mafupi, mzee Mgaya alirudi kwenye nyumba ya wageni akaweka documents zake huku akiisubiria kesho aliyoahidiwa kuwa wakutane kwenye ofisi za mkuu wa wilaya na si nyumbani kama alivyokwenda, akatoka huku akitafuta baa nzuri ili atulize mawazo.

***************************************
Tukirudi kwa mwalimu Agness, mwalimu mkuu wa shule iliyopo Kijiji kile, alikuwa ndani kwake huku akiwa kakosa amani na raha, aliwaza na kuwazua, alijua fika kuna bomu litalipuka na akajishauri kuwa hapaswi kuwa kimya na akisema asubiri anaweza kuipoteza kazi Sasa Cha kufanya ni kuwahi yaani kwenda wilayani ili akawaruke baadhi ya watu ambao aliwajua yeye mwenyewe.

Chakula kwake hakikuwa kinashuka vizuri Kila akimkumbuka mzee James namna alivyoshupalia jambo lile akaona huu ni msala.

**************************************Mke wangu kilasiku nakuambia tabia ya ndugu yangu lakini wewe unamwona mstaaraaaaaabu!!
Yule ni mshenzi, huwezi amini taarifa nilizokuwa nazo hapa ni kwamba yupo tu kwa mwalimu Anyes, Kuna Nini tena. aliongea mzee Mgaya huku akitoa kicheko cha masikitiko.

Sasa mwalimu mkuu ndiye mtu anayeleta vikwazo vya mwanetu, Sasa shemeji anavyoenda hukoooooo........
Kuna mafanikio kweli, si atasema tu kuwa ameshindwa!!! aliongea kwa mshangao mama Mgaya huku akimwangalia mumewe.

Unashangaa nini, si ulikuwa unamwamini , Mimi namjua kaka yangu ohoooooh. alifurahi sana mzee Mgaya akiamini Sasa ataonekana mkweli kwa familia yake.

Siku ya pili mwalimu mkuu, alikuwa kwenye ofisi za afisa elimu huku akimsubiri kwa muda mrefu licha ya kuambiwa atatokea muda si mrefu.

Enhee mbona bado sikukuu zinaendelea halafu tunaitana Tena ofisini vipi, na umebahatika Wala nisingekuwepo mji huu,
Na unaitwa nani vile, aliuliza afisa Elimu akijifanya kumsahau,..

Aaaah mkuu Mimi ni mwalimu Agness nipo shule ya (jina kapuni)
Nimekuja ili turekebishe jina la mwanafunzi aitwaye Samson Elias Mgaya maana kuna mjinga ananiumiza sana kichwa, tafadhali naomba tuwape jina lao, alishauri mwl Agnes.

Aaaah hasa na wewe mwalimu yule mlugaluga anakusumbua nini, yule si mshamba tu au vile visuti vyake vimekuchanganya? yule Hana lolote kwakuwa eti anakaa Dar es salaam ndiyo atutishe sisi wasomi, Mimi nilishamuonya asikanyage hapa. aliongea kwa maringo na kwa kujiamini yule afisa Elimu.

Mkuu usidharau jambo hili navyokwambia yule mtu kaja hukuhuku na kasema tukizingua anaenda mkoani kabisa. aliweka wazi mwalimu Agness.

(Huku akicheka)
Hana jeuri hiyo, kumbe ndivyo wanavyowaambieni na kuwatisha huko, Sasa mwambie huu moto haiwezi kwanza yule Mr anakuja kesho kukamilisha taratibu za uhamisho wa mwanaye aliyepewa jina la Samson hivyo wewe kuwa na amani.

Wakati akiongea na kuleta majigambo hayo alipokea ugeni mzito kwake alikuwa ni mkuu wa wilaya akiwa na wengine wanne akiwemo James Mgaya.

Itaendelea..............
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Baada ya kushangazwa na tukio la wazazi wawili kuja kutaka matokeo ya jina moja, afisa elimu aliwaruhusu wote kwamba waende na warudi baada ya siku tatu.

Samahani ndugu afisa, Mimi ni kaka wa huyu ambaye ndiye mwenye mtoto, tumekuja hapa ili kufanya mpango wa kumuhamisha maana nataka nikamsomeshe Mimi.
aliongea James Mgaya.

Sawa, nimekuelewa ila mrudi baada ya siku tatu naamini mtapata majibu sahihi, tunahitaji kuweka wazi huu mkanganyiko nachojua mimi nimakosa ya kibinadamu tu yamefanyika ila naamin tutarekebisha wala msiwe na shaka. aliongea kwa lugha rafiki yule afisa kiasi cha Mzee Mgaya na kaka yake kuridhika na majibu yale kisha wakaondoka.

Mzee Mgaya ambaye ndiye mwenye mtoto hakuweza kugundua chochote kuhusu mkanganyiko wa ufaulu wa mwanae ila kaka yake alijua mapema na alifahamu kuwa hakuna jambo la bahati mbaya badala yake Kuna namna inatumika kudidimiza vipaji vya watu maskini, akapanga kulivalia njuga lile suala.

Unajua Nini ndugu yangu, hapa inabidi tufanye juu chini tuhakikishe tunapata haki yetu haiwezekani kipaji na haki ya mtoto wetu ikanyang'anywa na wajanja wachache halafu sisi tukafumbia macho, si kweli hata kidogo. alisema kaka wa mzee Mgaya.

Walifika nyumbani jioni sana wakiwa wamechoka kiasi, lakini baada ya kupumzika James Mgaya alipata wazo, akaona ni bora aongee na mtoto mwenyewe aone kama anapenda shule au la. Ikabidi amtege kwa maswali kadhaa.

Wakiwa wawili tu Samson na baba yake mkubwa wakiwa hatua kadhaa kutoka nyumba ilipo, walianza mazungumzo kama ifuatavyo,

Unajua mwanangu, Kila mwanadamu hapa Duniani kaumbwa na kipawa/au kipaji chake, kwa mfano mimi tangu zamani nikiwa mdogo nilipenda kazi ya ualimu, wapo waliopenda udaktari, wapo maafisa kilimo na mifugo kana yule mzee mwenye nyumba nzuri kule bondeni (akionesha na kidole Cha shahada nyumba ilipo)

Lakini wapo ambao wao hawajasoma lakini Wana pesa na Wana maisha mazuri tu, kwamaana ya walitumia vipaji vyao ambavyo wanavyo, kufika walipotarajia, au kwa lugha nyingine kutimiza ndoto zao.

Je, wewe Samson unahisi kipaji chako ni kipi, na malengo yako ni yapi? aliuliza yule mzee.

Mimi hapa kwanza sijui kipaji changu, ila nikiwa shuleni, Kuna mratibu wa Elimu aliwahi kuniambia kwamba nisome sana kwani Nina kipaji kikubwa, ila hakuniambia ni kipaji gani.Lakini pia baadhi ya walimu waliniambia kuwa kama nitasoma naweza kuja kuwa kiongozi mkubwa
sana. alijibu Samson.

Unadhani kwanini walikwambia unaweza kuwa kiongozi, ulifanya nini Hadi ukaambiwa hivyo?
aliuliza baba mkubwa wa Samson.

Nikiwa darasa la tano nilikuwa Monitor wa darasa , Sasa basi ikitokea wanafunzi wenzangu wamepigana nilikuwa nawaamulia na nawashauri waache mchezo wao mbaya bila kuwapeleka kwa walimu.

Lakini pia kulikuwa na mwalimu wa darasa letu alikuwa mkali sana,
Sasa siku moja akaja na attendance kwaajili ya kuwaadhibu wanafunzi watoro, basi kutokana na hofu waliyokuwa nayo wanafunzi wenzangu niliamua kuwaombea msamaha kwa mwalimu, nikimwambia awasamehe hawatarudia tena.

Lakini mwalimu alikasirika sana akaniambia kwanini namfundisha kazi anawezaje kuwasamehe wanafunzi wasiokuwa na nidhamu, Sasa adhabu ya hawa utabeba wewe nifuate ofisini, nilimfuata Kisha nikashambuliwa na walimu nikapigwa sana nikarudi darasani nikiwa kawaida tu. alifafanua Samson

Kwahiyo hapo sifa ya uongozi inakujaje hapo? aliuliza yule mgeni

Mwalimu mkuu msaidizi aliniita kesho yake akaniambia kwanini nilikubali kuadhibiwa kwa kosa ambalo si langu, nikamjibu kuwa huwa sipendi kuona mtu akifanyiwa jambo baya mbele yangu.

Unajifanya Nelson Mandela eehh, utakuja kufa shauri yako, ila nimependa misimamo yako soma sana huenda ukaja kuwa kiongozi Bora baadaye, Samson anaelezea yale aliyoambiwa na mwalimu wake.

Sawasawa, unaonekana una upeo mzuri ila hujanijibu ni kipi ukiambiwa ufanye Sasa hivi, utafanya kwa usahihi?aliuliza yule mzee.

Kwasasa sijui labda ningesoma kwanza nitajua mbele kwa mbele. alijibu Kwa kifupi Samson.

Unaonaje nikikupa mtaji ufanye biashara. aliuliza kimtego Yule Baba yake mkubwa.

Mimi kwanza sijawahi kufanya biashara, japo naipenda sana , ila baba kwanini hayo nisingeyafanya baada ya kusoma na kuwa na elimu?
Kwasababu hata walimu wetu walituhimiza tusome sana wakidai mtu Ukiwa na Elimu unaweza fanya mambo kirahisi zaidi tofauti na asiyesoma. alijibu Samson

Hadi hapa baba mkubwa wa Samson alishajua kuwa samsoni anapenda shule, na alifurahi kwasababu walipanga kuhakikisha Kila kitu kinakaa sawa kuhusu kutaka kudhulumiwa jina la mtoto wao, lakini alitaka ajiridhishe kwanza , maana wasije kuhangaika na mtu ambaye pengine hapendi shule.

Lakini mwanangu nakuona upo vizuri kichwani, Nini kilipelekea ukatoroka hadi kuwaweka wazazi wako kwenye wakati mgumu,? aliulizwa Samson

Lakini hakuwa na majibu ya swali hili badala yake aliomba msamaha tu hasa ukizingatia ndiye atakayetoa msaada, ikabida Samson awe mpole

Siku tatu baadaye kama kawaida, kama walivyoambiwa waje walikuwa kwenye ofisi ile huku wakitazamana na afisa elimu, akiwa siku hiyo kabadilika akiwa Hana tabasamu zuri.wakasalimiana.

Mnajua nyinyi labda niwaweke wazi tu kuwa yale matokeo ya mwanzo yalikosewa kumbe, hivyo tumefanya kazi kubwa kuwasiliana na wenzetu waliopo ngazi ya mkoa hatimaye tumeletewa matokeo mengine ambayo yanaonesha mtoto wenu kwa bahati mbaya hayupo kwenye list ya waliofaulu. niwape pole tu kwa usumbufu. aliongea huku akionesha hajapenda ujio wao.

(James Mgaya akicheka)
Samahani afisa unadhani ni rahisi kutuambia maneno hayo hebu kuwa na aibu hata kidogo basi kwanini Kila siku mnatufanya wajinga naomba nipate barua ya kuweza kufuatilia matokeo ya mwanetu huko huko mkoani. aliongea kwa jazba bila uoga ndugu wa mzee Mgaya.

Sasa mzee Ina maana huniamini au kwanza usilete ujuaji kwenye ofisi yangu nitakufunga. alitishia yule afisa elimu huku akivua miwani yake.

Ni mpambano wa vita mpya kati ya James Mgaya na afisa elimu.
Je, nani atashinda huu mpambano. Usikose sehemu ijayo.
Haya Mambo wakurya walichezewa mno na wajaluo na wajita. Mana wazee wetu walijua kufuga ng'ombe. Sasa bana Kaka zetu enzi na baba zetu miaka iyo ya 60/70/80 wakimaliza majina wanachukua hao walimu wanayauza kwa wenye pesa ama wenye muamko wa kusoma wanaenda kusoma.
Yaani kweli hii dunia iache ivyo. Sisi wote Ni wanyama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom