Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

Yes ni kweli niko free, baada ya kutoka mkoani nilikokuwa hata hivyo Niko home tu Kuna kijihoma kinanisumbua , nadhani hali ya hewa natamani tungepiga vyombo pamoja ila niko likizo kidogo na hivi vitu

Kwasasa Nina muda wiki nzima hivyo stori itawekwa vipande viwili kila siku
Ugua pole ndugu .
Ila pata muda ukapime ujue nini shida.
 
Samahani si kwamba siheshimu makubaliano mkuu ila ratiba zimeingiliana, hata hivyo jioni kama kawaida mzigo utakuwa hewani
Mkuu Mungu akubariki sana kwa jibu lako la unyenyekevu kwa huyo mdau hopefully inaweza kumsaidia kubadirika kimtazamo. Be blessed Man
 
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA

Heheeeheee mume wangu, nilikwambia mimi, ooh unamsingizia, Mara bado hajui lolote huyo, Sasa ndiyo huyu hapa usiku wa manane kaja kumgongea huyu Binti, simuelewi, samsoni hueleweki baba. Haya danganya, ongopa lolote. aliongea mama Kulwa huku akijifunga kitenge chake vizuri na mzee Mgaya akawa kashafika.

Hebu wewe mpuuzi Kaa chini kwanza, saa Saba hii unatafuta nini huku? na ujue mke wangu huenda wote walipanga hawa, haiwezekani mtu hujaongea naye halafu uje kugonga mlango haiingii akilini, hebu wewe Binti toka huko ndani, njooni huku.

Wote wanne wakaja hadi sebuleni huku mama Kulwa akiwa anatoa vicheko vya kejeli Kila mara huku ikionesha kachukia kuliko maelezo,

Tafadhali Samson nilizisikia habari zako siku nyingi sana, lakini nikawa nazipuuzia, pole sana mwanangu najua tayari umejipunguzia uaminifu kwa kiwango kikubwa sana.

Halafu nikwambie tu kuwa huu siyo utaratibu wa maisha yetu, yule Jose uliyemuona pamoja na ndugu zako wote hawajawahi kutuvunjia heshima hata kidogo hata kuwahisi tu, achilia mbali kuja kugonga mlango bila heshima.

Hebu mama Kulwa kaniletee mkanda wangu kule ndani maana haya lazima tuyamalize usiku huu huu. aliongea Kwa kumaanisha Mzee Mgaya akiwa na hasira sana.

Hapana mume wangu huyu ni mtoto wa wazazi wenzetu, mama mzazi wa Samson amelala huko kijijini, hatujui njozi ndoto zake ziko vipi, hapana sishauri umpige, huyu ashauriwe tu na kama itashindikana, basi tutafanya utaratibu wa kumrudisha kwao. aliongea mama Kulwa huku akimsogeza Rahma aje kwenye mwanga.

Huyu naye nina wasiwasi naye sana tu kwasababu, ile siku mke wangu hawa watoto nusura watulaze nje, tena ilikuwa ni saa moja tu jioni, lakini tulikaa zaidi ya nusu saa, gonga geti Mara kadhaa watu hawasikii, tukafikia kuwaza vibaya, lakini hata tulipowauliza majibu yao bado yalikuwa ni mepesi sana, Kwa maana hiyo Hawa Wana mahusiano, Sasa hii hali Mimi siwezi kuiruhusu hata kidogo.kwanza huyu Binti kuanzia kesho sitaki kumuona. alichimba mkwara Mzee Kisha Rahma akadakia.

Samahani sana baba, Sasa Mimi naingiaje mwenye Hilo kosa la Samson, hebu baba yangu kama Mimi ningekuwa nimeongea na Samson aje ndani kwangu, si ningeacha mlango wazi ili akifika asipate taabu, Mimi Sina mahusiano na samson baba, hata baada ya mlango kugongwa Mimi nilihisi ni mama, kwakuwa ndiye mtu pekee hunigongea na si mwingine.
alijitetea Rahma.

Mama Kulwa alimtazama mzee Mgaya Kwa jicho linalotaka amwelewe Binti wa watu kwani kile alichosema kina mashiko,

Yaani nilitegemea unajisomea ndani na kupumzika ili kesho uendelee na ratiba zako kumbe wewe una hangaika kutaka ku............. Mzee Mgaya alishindwa kumalizia sentensi yake akaanza kumpiga mateke Samson bila kuchagua wapi anapiga , ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kipigo alichopata Samson ambaye kwanza hakutarajia maana alishatetewa na mama Kulwa lakini haikusaidia kwani alichapwa vibaya , licha ya mama Kulwa kuingilia Kati lakini alishachelewa, kwani Samson aliumizwa vibaya kwa muda mfupi sana

Baba Jose mume wangu, haya unayoyafanya unajitafutia matatizo kwa ndugu zako, ije kuonekana sisi tunashirikiana kumuumiza mtoto wa watu, kama akitushinda mrudishe kwao huenda na shule inamshinda, Hadi kuyafanya haya hakuna mwanafunzi hapa. alizungumza mama Kulwa huku Mzee Mgaya akiwa bado ana hasira anataka kuendelea kumpiga Samson. lakini mama Kulwa alimkumbatia Sam kwani kipigo alichopata kilitosha.

Kesho ukirudi toka shule nitakuwa na kikao na nyinyi wawili (Samson & Rahma)
Halafu kuna picha inanijia, juu ya ugomvi wenu wewe Binti na mama yako mdogo hata hivyo, Mimi naenda kumalizia usingizi wangu haya yataongelewa kesho. aliongea mzee to Mgaya huku akimtishia Samson kila muda akaingia zake ndani huku akiongea peke yake maneno ambayo hayakusikika na mtu yeyote

Nendeni vyumbani kwenu Mimi huyu namjua anaweza kurudi na kuanzisha jambo upya,. aliongea mama Kulwa Kisha Samson akaingia naye chumbani kwake huku akigundua mguu wa kulia kwenye nyama za paja kumeumia kiasi Cha kujikuta anachechemea kwani aliumia vibaya, baada ya teke la kushtukizwa kutua sawasawa.

Alijilaza huku akimlaumu Rahma kwa kutoacha mlango wazi,

Huyu naye kama alikuwa hataki niende si angesema tu, tumekubaliana vizuri lakini Cha ajabu kafunga mlango, Sasa kaniaibisha nitawezaje kuaminika tena, na nipo hatarini kupoteza hii nafasi ya Mimi kusoma, kwani hata akinirudisha kule, kijijini nitasoma shule gani kwani zote zipo mbali, si umbali tu hata
Zingekuwa karibu, amgesomeshwa na nani akajikuta anatakiwa kesho awe wa kwanza kuomba msamaha.
aliwaza Sam, huku akijikuta ni mkosaji

********************************* Samson aliamka asubuhi na mapema lengo asionekane na yeyote lakini alishangaa kumkuta mama Kulwa pale sebuleni akiwa na Rahma.
Mmmmh kwani Hawa hawakulala? alijiuliza Samson asipate jibu ,
 
SEHEMU YA HAMSINI NA SABA

Samson alimsalimia mama Kulwa, huku akishangaa uwepo wa watu wale asubuhi ile.

Nadhani jana ulimsikia baba yako kuhusu kikao tutakachofanya na wewe ukirudi shule, lakini kwasababu tunazozijua sisi tumeona tuongee muda huu. aliongea mama Kulwa huku akimkazia macho Samson.

Sasa mama mimi si nachelewa shule maana huu muda naona kama unaenda hivi wazee wangu.
alijitetea Samson kwasababu aliona kuanza kuyajadili mambo yale asubuhi, ni kujichelewesha na kuzua mambo mengi zaidi.

Wewe hebu Kaa kimya na utulie kwa shule gani unayoiwahi tena, kwani nani kamwambia bado unaendelea na masomo , hapa wewe unarudishwa kwa wazazi wako mkoani halafu wao ndiyo watakutafutia shule, kama watakuja kukurudisha shule hii hii na wakakupangia sehemu nyingine sawa ila Mimi siwezi tena, mwanangu Jose alishauri kuwa na uhamishiwe shule wanayosoma akina Kulwa lakini kwa tabia yako hiyo wewe utasoma shule hizi hizi halafu utajilinganisha aliyesoma high school na wewe na mwenye taaluma nzuri.aliongea Mzee Mgaya akiwa anatoka ndani na kulisogelea kabati fulani lililokuwa pale sebuleni na kuvuta droo huku akionekana kutafuta kitu.

Mke wangu kwani zile karatasi zangu za vibali vya maliasili pamoja na leseni viko wapi maana natafuta sivioni na bila hivyo vitu ninakoenda nitakuwa najisumbua tu. aliweka kituo mzee Mgaya

Baba Jose na wewe, Jana si ulisema nikuwekee kabisa kwenye begi lako , inakuwaje tena unasahau?
aliuliza mama Kulwa.

Aaah ni huyu mpumbavu ndiye ananichanganya yaani, aliongea huku akirudi kuketi kwenye kiti baada ya kuambiwa vitu anavyotafuta vipo.

Nikianza na wewe binti naomba kujua wewe mligombana Nini na Tausi, maana nimejaribu kufikiria nikahisi huenda mke wangu Tausi aliwashtukia nyinyi na Samson,
Na ndipo mlipoanza kukwaruzana, hebu niambie kwanza
mzee Mgaya hakuwa na masikhara hata kidogo.

Baba haya ulishaniuliza na siku nyingi nikakwambia Mimi sijui nilichomkosea mamdogo, na hata yeye ulimuuliza ukadai hajakupa jibu la kueleweka, kiufupi Mimi sijui
alijibu kifupi Rahma.

Nikirudi kwa wewe Samson nakupa nafasi ya mwisho ya kukaa ndani mwangu, hata hivyo naomba nikirudi nikute umeandika maelezo ambayo yataonesha hutarudia tena tabia hiyo halafu nitaisoma nikiridhika na ulichokiandika basi nitakwambia usaini halafu hiyo karatasi nitakaa nayo Mimi maana wewe umeshakuwa kijana ambaye unapaswa uheshimiwe kwa namna fulani mambo ya kupigana pigana eti, unaonywa hayo siyawezi badala yake ukirudia kosa karatasi uliyoiandika mwenyewe ndiyo itakayokurudisha kwenu, aliongea Mzee Mgaya huku akimuomba mkewe funguo za gari ili aondoke awahi kwenye mambo yake.

Na Mimi mume wangu naomba niongezee jambo la mwisho kama alivyoambiwa usiku ule kuwa tumeishi na madada wa kazi chungu mzima , yaani ni wengi Kila mmoja akiishi hapa kwa wakati wake, lakini watoto wetu wa kiume hawajawahi kuonesha vitendo vya utomvu wa nidhamu hata kidogo waliishi kwa kuheshimiana mno, Sasa mwanangu unapaswa ujiangalie sana vinginevyo ndoto zako zitaishia njiani. aliongea Kwa sauti ya upole na ya kumuhurumia Samson huku Mzee Mgaya akitingisha kichwa kukubaliana.

Wakamruhusu Samson aondoke, huku tayari jua likiwa limetoka,
Samson alianza kwenda shule kwa kukimbia akiwa kachelewa kweli kweli, akafika shuleni kwao akiwakuta walimu watatu wakiwa wanaongea huku nje kukiwa hakuna mwanafunzi hata mmoja kuashiria wote wapo madarasani,

Wewee, hebu njoo kwanza hapa, unakuja shule muda huu hii ni shule ya baba yako? aliuliza mwalimu fulani wa kike aliyefahamika kwa jina la madam S. alisifika kwa ushambenga sana na hakuwa na huruma.

Hata ingekuwa ya baba yake ndiyo aje muda anaoutaka yeye, hebu piga magoti wewe, Tena huyu anakaa nyuma tu hapo kwa yule mama mweupe yule Daktari, aliongea mwalimu fulani aliyeonesha anapajua anapokaa Samson.

Ahaaaaaah, eti mwalimu hapo si ndipo tulipoambiwa mwalimu Sadick kazua balaa, mwalimu naye alifuata Nini jamani vijanamke vya mitaani , vichokoraa tu ndo vimemponza ona sasa anaona aibu hata kuja shule. aliongea yule madam S huku akiangua kicheko cha nguvu.

Hapana, tena hapana, mwalimu Sadick si tunamfahamu hana mambo hayo hao walimsingizia tu, nasikia huyo ni Binti wa kazi, Sasa mwalimu Sadick aje kutembea na madada wa kazi hawahawa tunaowajua haiba zao huku wengi hata kuoga hadi wakumbushwe,. waliongea wale walimu wakiume wawili wakipinga kuwa mwenzao hangefanya vile,
Masikini hawakumjua Binti mrembo Rahma, mwenye sura nzuri huku akiwa ni msafi kupitiliza kiasi Cha kuwachanganya baadhi ya wanaume wakware huku wengine wakiwa wanajiheshimu kutokana na umri wao kuwa mkubwa, na wapo ambao wakikutana na Rahma basi walikuwa wanatangaza ndoa tu

Wapo wafia Dini ambao walimlaumu, Rahma kuwa kwanini anaishi na watu wa Dini nyingine ilhali yeye ni Dini nyingine, lakini yeye Rahma hakuwasikiliza kwani uhuru aliopewa pale kwa mama Kulwa ulikuwa mkubwa, ikiwa ni pamoja na kutengewa chumba cha kuswalia na kumpa ruhusa Kila ijumaa ili akajumuike na wenzie, huku familia ya mama Kulwa ikiwa ni ya kanisani .

Hebu toka hapa, muone kwahiyo umelewa kusikiliza maongezi yetu, mjinga wewe, walimfukuza Samson kama mbwa huku akiingia darasani mwao akimkuta mwalimu ashaanza kipindi.

Heeeeh wewe ndo unaingia muda huu kwenye kipindi changu utaelewa Nini, mwalimu huyu hakutaka maelezo ya Samson badala yake alimchapa fimbo nne na matusi juu,
Wajinga nyie yaani unaingia muda huu umeambiwa hapa ni sokoni, kwamba kwakuwa linafungwa jioni naweza kwenda muda wowote,mpumbavu wewe. alitukana yule mwalimu.na kuendelea na kipindi chake.

*************************************
Muda wa mapumziko kama ilivyo kawaida wanafunzi walisukumana wakitoka nje na kwenda kutafuta vyakula ambavyo vilikuwa vinauzwa na kinamama shuleni pale, huku wanafunzi watukutu wakiingia mtaani kwaajili ya mambo yao.

Lakini Samson alibaki darasani akiwaza mambo mengi sana,
Kwanza alijutia kosa lake sana tu,

Kama Mzee Mgaya kitendo cha kugonga mlango kamaindi na kunipiga vile tena asubuhi kaamka na mambo yale yale, je akija kusikia nililala na mkewe Tausi si ataniua kabisa, eeeh MUNGU nisaidie hii hali inipite, alikumbuka namna alivyotukanwa na kuambiwa kama akishindwa kuishi pale basi wazazi wake ndio watakaomsomesha,
Maneno yale yalimuumiza sana.

Aliufikiria umasikini wa kutupwa wa wazazi wake, alimkumbuka baba yake Mzee Elias Mgaya, mtu ambaye alikuwa anazeeka kuliko kaka yake kutokana na kazi ngumu za kijijini ikiwa ni namna ya kupambana na umasikini waliokuwa nao,
Ni kweli msaada aliopewa wa kuweza kusomeshwa angalau shule za kufuta ujinga alishukuru huku maneno aliyoyataka Mzee Mgaya kuwa Samson atajilinganisha mwenyewe Kati ya aliyesoma high school na yeye nani atakuwa Bora.
alijikuta anaumia sana kila alipokumbuka maneno haya.

Ina maana hii shule ninayosoma haiwezi kunitoa? Ina maana napoteza muda tu? lakini mbona nasikia Kuna watu kibao wamefaulu vizuri sana tu wakitoka shule hii hii?

Hapana nitaongeza juhudi tu, nitahakikisha natoboa nikiwa Hapa hapa nitakaa mbali na mwanamke yeyote yule nadhani nafasi niliyopewa ni ya mwisho yule mzee Mgaya nikifanya masikhara nitafukuzwa kweli, ngoja nitasoma kwa bidii Kila kitu kitakaa sawa tu, aliongea kwa hisia Samson huku akigonga meza kwa nguvu kiasi Cha kuwashitua wanafunzi wenzie waliokuwa wanarudi toka kwenye break.

Wewe Sam vipi unachanganyikiwa?
Jamani tukamwambie mwalimu mkuu kuwa Kuna mtu anapandisha mashetani huku, aliongea mwanafunzi fulani comedian aliyeitwa Zena, na kuwafanya wanafunzi wote wamcheke Samson.

Itaendelea............................
 
Shukrani boss tunasubiri muendelezo pindi upatapo muda.
 
Mkuu tukumbuke hata kidogooo tu
Mkuu Clkey napenda sana tuburudike pamoja kuhusu mwendelezo wa simulizi hii, lakini nawajibika sehemu nyingi, hivyo kujikuta nachoka sana na kukosa muda , ila kesho panapo majaliwa tutaamka na vipande viwili.
Kumbuka inahitaji utulivu kuandika ili angalau kuleta ladha kwa msomaji
 
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE

Hata muda wa kwenda nyumbani ulipofika Samson alikuwa mzito kwenda nyumbani alitamani angekaa tu darasani kwaajili ya kujisomea, lakini hata hivyo angeelewa nini?
Mawazo na hofu ya kuacha shule vilimsumbua sana.

Wanafunzi wenzake walitawanyika huku yeye akirudi darasani kwaajili ya kuzugazuga ili kupoteza muda ili afike nyumbani usiku,

Oyaa Sam mbona huoneshi kuondoka vipi, Mimi nadhani ni vyema ungeenda kula kabisa maana si tuliambizana turudi baada ya kula? Fanya hivyo mwanangu basi maana tunaweza kupishana, wewe unaenda sisi tunarudi tutakuwa tunafanya nini? aliongea mwanafunzi mmoja kutoka lile group la Samson kama walivyokubaliana warudi baada ya kula waje kujadili mambo yao.

Haina shida, Mimi mtanikuta humu humu, nyie nendeni tu. alijibu kifupi Samson.

Yule mwanafunzi alimwangalia Samson, kitambo kidogo Kisha akasema,
Unajua wee Sam tumegundua Leo huna furaha kabisa tatizo ni Nini, kwasababu hata muda wa mapumziko hukutoka, na hujala chochote muda ule, na saizi eti huendi nyumbani, kwani una Nini Sam. Unajua kundi letu Kuna baadhi wamedai tukupige chini na nafasi yako achukue mtu mwingine, lakini Mimi nimekutetea kuwa huenda hayupo sawa. aliweka kituo yule mwanafunzi huku akimwangalia Sam kwa umakini.

Watu bwana Sasa wanitenge kwenye kundi Mimi kosa langu nini, aliuliza Samson.

Wanakuona kama una kisirani sana, wewe mwenyewe jiangalie, Leo utakuja tutacheka tutafurahi tutasoma kwa pamoja, kesho utakuja Ukiwa tofauti ukionekana umenuna, nani umemnunia inakuwa haieleweki, na tulichogundua kutoka kwako Samson ni mademu, hususan yule msichana mnayekaa naye, Sasa nadhani kila anapokuzingua na wewe inapelekea kupoteza baadhi ya mambo fulani.demu kashakukataa ndiyo maana upo hivyo, na haya mambo ya kuchanganya mapenzi na masomo yatakugharimu.
Sam huo ndiyo ukweli, wapo wasiojua lakini baadhi kwenye kundi letu tushajua, na omba hizi taarifa zisifike kwa walimu nahisi utakuwa hatarini zaidi . alizidi kupigilia msumari yule mwanafunzi mwenzie.

Unasikia wewe Mimi sijawahi kuwaza wanawake, Mimi nimepokea taarifa mbaya, toka kijijini kwetu ndiyo maana unaona Niko hivi, sawa hakuna shida kama mmeamua kunizushia mnayoyajua nyinyi badala yangu Haina shida.
Samson alijifanya amekasirika huku yale aliyoambiwa yakimchoma kama mwiba maana kulikuwa na ukweli unaofanana
Aliinuka na kubeba begi lake, huku akipiga hatua kuelekea nje, alitamani angekuwa anakaa mbali ili achelewe kidogo maana hakutaka kufika mapema, lakini hakukuwa na jinsi tayari alikuwa anaangaliana na geti la nyumbani kwao muda mfupi tu.

Aligonga Kisha akasikia hatua za mtu kuja kufungua,
Rahma alifungua mlango Kisha akatabasamu baada ya kumuona Samson, lakini Samson hakutaka mazoea akasalimia kisha akawa anaenda ndani huku moyo Ukiwa bado unadunda dunda maana alijua kama wazee watakuwepo basi maada itazaliwa upya lakini hakuona dalili za uwepo wa mtu tofauti na Rahma, akamgeukia Rahma na kuuliza, vipi wazee wapo?

Hawapo, baba tangu alivyoondoka asubuhi, na mama naye kaenda mjini nadhani dukani kwake, alipita Cathy hapa wakachukuana wakaondoka, alijibu Rahma.
Lakini kaka Sam pole sana kwa mambo yaliyotokea jana, yaani nimewaza sana nakujikuta Mimi ndiye msababishaji, nilijisahau mwenzio, nikajikuta nimeweka komeo bila kujua kuwa utakuja, naomba nisamehe sana, lakini pia usijali Mimi nipo Kila kitu kitakuwa sawa, aliongea Rahma kwa hisia huku Samson akiwa anamwangalia kwa macho yanayoonesha hapendi anachoambiwa.

Akaingia ndani pitiliza hadi chumbani kwake, akawa anapanga vitu vyake huku akikumbuka kuwa aliambiwa aandike barua ya maelezo yanayoonesha hatarudia aliyoyafanya. Akatafuta karatasi nzuri huku akibuni maneno mazuri anayohisi yatawashawishi wazazi wake,

MUNGU nisaidie niokoe na hii hali nayopitia , nitaishije Sasa Ina maana narudi kijijini bila kutimiza ndoto zangu? na hili naliona lipo wazi muda wowote nitaanguka, ama kweli ng'ombe wa masikini hazai hata akizaa huzaa dume. lengo mambo mazuri yasiendelee, wakati akiwaza yale sauti ya Rahma ilisikika toka sebuleni.

Sasa kaka Sam ina maana huli Chakula leo, njoo basi Kuna mtu anakuita huku,
Samson alitoka huku akiwa na shauku ya kumjua huyo anayemuita lakini hakuona mtu,

Nani ananiita , aliuliza Samson.

Wewe kula kwanza Sam , hakuna anayekuita mimi nakuonea huruma mdogo wangu, nakuita mdogo wangu kwasababu Kwa umri wako Mimi nimekuzidi miaka saba, najua sura yangu hii inawafanya watu wanione mtoto, ila Mimi ni mkubwa,
Halafu Sam usijali Mimi mchana nimeongea na mama kuwa wewe huna tabia hizo na hujawahi kufanya mambo hayo ila ni shetani tu, na mama kaelewa. Rahma aliendelea kuongea huku akiwa hajibiwi lolote na Samson, hata baada ya kumaliza kula Samson alirudi chumbani kwake

Wewe Sam njoo kwanza mama aliacha maagizo hapa, kule jiko la umeme limeharibika sijui Kuna Nini, hivyo alisema ukirudi umfuate fundi aje arekebishe, nadhani angenituma Mimi lakini ana sababu ambazo zinapelekea asinitume.

Samson hakujibu kitu, yaani hakutaka kuongea na Rahma hata ule ukaribu hakutaka alifungua geti na kuingia mtaani akimfuata yule fundi ambaye alimkuta ofisini kwake akiwa anabishana mwanamke anayeonekana ni mkewe.

Sasa mke wanguuu, hali ni ngumu naomba unielewe , yaani huwezi amini tangu nafika hapa saa mbili asubuhi hakuna mteja aliyekuja hata mmoja eeh, hivyo Sina kitu mpaka saa kumi na mbili hii na ni Bora nifunge tu maana muda umeisha nimeshindwa kupokea wateja mchana watakuja usiku? alijitetea yule fundi kwa mkewe ambaye alionekana kafuata hela.

Wewe dogo vipi unasikiliza maongezi ya watu hebu Kaa pembeni basi , kwanza hata husalimii halafu unasogea hapa huna adabu nini wewe, aliongea yule fundi kwa ukali.

Hapana bro mimi nimeambiwa nikufuate,jiko letu limesumbua twende ukaliangalie, aliongea kivivu Samson.

Ahaaaaa basi sorry dogo ngoja nichukue vifaa,alijibu Kwa pupa yule fundi.

Unaona mke wanguu Mimi nilikwambia lazima uwe na Imani, MUNGU ndiye muweza na mpaji wa vyote, ona sasa riziki imekuja jiooooni kabisa, basi tangulia nyumbani kipenzi changu Mimi narudi Sasa hivi, aliongea yule fundi wakiangaliana na mkewe huku wote wakitabasamu.

Mmmh kweli hii ndiyo Dar es salaam, Ina maana bila Mimi kumtafuta wangeishije sasa, yaani maisha haya acha tu. Samson alijiwazia moyoni.

Walifika nyumbani fundi akaoneshwa kazi huku akiianza kwa mbwembwe zote Samson akiwa pembeni akimwangalia tu, ndani ya dakika kadhaa fundi alimaliza kazi huku, akisubiri malipo.

Da Rahma uko wapi, fundi amemaliza kazi yake huku njoo umlipe wewe si ndiye uliyeachiwa maagizo yote.aliita Samson

Rahma alikuja akamkabidhi pesa yule fundi ambaye uso wake ulionesha amefurahi sana, huenda malipo yalikuwa makubwa kuliko kazi.

Wakati Samson akimsindikiza fundi ili atoke na yeye afunge geti, fundi alianza mambo yake,

Aisee dogo hivi huyo dada unamuitaje, maana mwenyezi MUNGU anaumba jamani yupo vizuri sana Mashallah ,unaweza kuniitia niongee naye kidogo.
Fundi alianza kizidisha ufundi maana alianza kukimbilia mambo ambayo hayajamleta pale.

Oyaa bro eeeh, hebu wewe wahi bwana mkeo atakuwa anakusubiri, aliongea Samson huku akifunga geti.akarudi chumbani kwake na kuanza kuandika barua ya maelezo ili pindi Mzee Mgaya akirudi amkabidhi

Itaendelea...........................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom