Simba kuanzia Hatua ya 2 CAFCL, kukutana na mshindi wa mechi kati ya Power Dynamos na African Stars

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553


Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepangwa, Simba itaanzia Raundi ya Pili kwa kucheza na mshindi wa mechi kati ya Power Dynamos (Zambia) dhidi ya African Stars (Namibia)

Yanga itaanzia Raundi ya Kwanza kwa kukipiga na ASAS ya Djibouti, timu itakayoshinda itaingia Raundi ya Pili na kukutana na timu itakayoshinda kati ya Otoho ya Congo dhidi ya Al Merrikh ya Sudan

KMKM ya Zanzibar itaanzia Raundi ya Kwanza kwa kukipiga na St. George ya Ethiopia, mshindi wa hapo atacheza dhidi ya Bingwa Mtetezi Al Ahly ya Misri.

Mechi za Raundi ya Kwanza zitachezwa Agosti 18–19 na marudio ni Agosti 25–26, 2023, Raundi ya Pili ni Septemba 15–16 na marudio ni Septemba 29–30, 2023, baada ya hapo inafuata Hatua ya Makundi.
 


Droo ya hatua za awali za mashindano ya CAF zinaendelea muda huu. Fuatilia hapa yanayojiri kutoka kwenye droo hiyo ambapo timu za Tanzania zitahusika pia.

Simba itaanzia hatua ya pili ya michuano ya CAFCL na inaweza kukutana na timu moja kati ya hizi;
  • Bumamuru
  • Green Mamba
  • Big Bullets
  • Power Dynamos
  • African Stars
  • Dragon FC
  • Bendje

Hamna timu hapa
 


Droo ya hatua za awali za mashindano ya CAF zinaendelea muda huu. Fuatilia hapa yanayojiri kutoka kwenye droo hiyo ambapo timu za Tanzania zitahusika pia.

Simba itaanzia hatua ya pili ya michuano ya CAFCL na itakutana na mshindi wa mechi kati ya timu za Power Dynamos na African Stars.

Basi kwenye Simba Day Power Dynamos itaficha silaha na makucha yake. Simba mna bahati sana..
 
Back
Top Bottom