Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Ndugu wanampira nimepitia maoni yenu yote na kugundua kuwa baadhi ya wachangiaji wamenibatiza kuwa utopolo kwa sababu wanazozijua wao. Mimi nimefungua huu uzi kama angalizo kwa TFF kwamba ikiwa hawatakuwa waangalifu Yanga wanaweza wakawatokea puani kama wataamua kuwakazia. Nina sababu lukuki na baadhi nimeishazitoa hapa lakini hakuna mtu anayenisikiliza. Napenda kujitoa kwenye kundi la utopolo ambalo baadhi yenu mmeamua kuniweka. Andiko hili nimelitoa kama mchambuzi sio kama mwanamsimbazi au mwanautopolo. Naomba nieleweke hivyo.

Sababu au dukuduku zinazonifanya niwe na wasiwasi kuhusu haya niliyoyaandika hapa ni hizi zifuatazo:

1. Kama Yanga walikuwa na makosa kutopeleka timu kiwanjani mbona hawakuadhibiwa? Kwa sababu hii, wanaweza wasipeleke timu tena tarehe 3/7 na TFF au serikali hawawezi kuwafanya lolote kwa kuwa kama wangekuwa na makosa wangechukuliwa hatua za kinidhamu tangu siku ile walipogoma kupeleka timu kiwanjani.

2. Kwa kuwa TFF hawakuwapa adhabu immediately maana yake ni kwamba hiyo adhabu (kama ipo) tayari imeisha expire. So, TFF hawawezi kuwaadhibu Yanga wala kuwapa pointi Simba na ikiwa watafanya hivyo, Yanga watawakaanga mapema sana.

3. Pesa za mashabiki walioingia kiwanjani kutazama mechi zitarejeshwa lini? Kumbuka hata waziri mkuu amewahi kuongelea jambo hili lakini TFF wameziba masiko yao viazi.

4. Gharama za maandalizi kwa timu zote mbili zitalipwa na nani na lini? Timu zote mbili tayari wameandaa bill ya maandalizi ijapokuwa bado hawajaiwasilisha rasmi TFF.

5. Kitendo cha serikali kulazimisha mechi isogezwe mbele kwa sababu za kipuuzi kabisa maana yake ni kuwa serikali imeingilia mambo ya mpira kinyume na sheria za FIFA. Kwa maana hii, kama Yanga wakiamua kupeleka hili jambo CAS au FIFA na kulishupalia kisawasawa, TFF hawana pa kutokea.....watafungiwa tu....na kisha Yanga watalipwa mabilioni ya dola kama fidia kwa usumbufu. Tatizo kuna baadhi ya watu hawajui hili, wao wanajua sheria za TFF tu. Wanashangaza :oops: :oops: :oops: :oops:

Ni hayo tu.
 
Hapo nimekuelewa vizuri sana mkuu. Lakini Simba walishindwa kupeleka timu baada ya Yanga kuondoka kiwanjani. Wangepeleka timu icheze na nani wakati Yanga wameishasepa kitambo? Na pia hapakuwepo na marefa wa kuchezesha mchezo.
Sheria inasema muda wa mchezo ukikaribia ingiza timu uwanjani, na baada ya muda wa mchezo kufika subiria nusu saa uwanjani kama.timu haijaingia uwanjani ondoa timu uwanjani na inahesabika mpinzani hajafika mchezoni, Yanga waliondoa timu saa 17:30 hapo Simba anahesabika amekimbia mechi.
 
Hiyo sentesi ya mwisho una authority?

Kuhusu kanuni ya kubadilisha muda wa mchezo, kanuni ina exception ya emergence,(nenda kaisome yote, usiishie njiani) ambapo kukiwa na emergency hata kama imebaki dk moja mchezo unaweza sogezwa mbele au ratiba kubadilishwa. Una uhakika asilimia ngapi serikali itashindwa kudhibitisha kua kulikua na emergency?

Kuhusu serikali kuingilia michezo haipo hivyo unavyofikilia. Kuna baadhi ya mambo na baadhi ya sababu zinaweza fanya serikali ikaingilia. Kwa mfano, kipindi cha corona ni nani alitoa tamko ligi isimame???
Mechi inaweza kuahirishwa au kusohezwa mbele chini ya masaa 24 kama tu

■ Kuna tishio la kigaidi au bomu uwanjani

■ Hali ya hewa kutoruhusu mchezo kuchezwa.

■ Majanga ya ya kidunia kama tetemeko la ardhi au kimbunga kikali.

Lakini siyo nje ya hapo
 
Tatizo simba huyu ameenda pole mno hadi ataikosa nyama au atakuta imeioza. Tazama nchi zote duniani ligi zao zimefika tamati lakini ligi hii ya TFF inatarajiwa kufika tamati mwaka ujao. Haya ni maajabu ya dunia ndugu yangu Bujibuji .
Vipi ligi ya Misri?
 
Mechi inaweza kuahirishwa au kusohezwa mbele chini ya masaa 24 kama tu

■ Kuna tishio la kigaidi au bomu uwanjani

■ Hali ya hewa kutoruhusu mchezo kuchezwa.

■ Majanga ya ya kidunia kama tetemeko la ardhi au kimbunga kikali.

Lakini siyo nje ya hapo

Kanuni imesema emergency ambayo TFF wanalidhia kuwa ni dharura na muhimu. Si hizo tu.
Tukubali kulikuwa na hali ya kukariri badala ya kuelewa kanuni.

Kwa hiyo ikitokea uwanja unawaka moto au kubomoka, mechi itaendelea kwa kuwa haijatajwa?
 
Wakikwambia kulikuwa na shughuli ya kiserikali hivyo watu wa usalama wakaelekezwa huko kwanza na hawakuwa na watu wa kutosha kuangalia usalama uwanjani, kwenye shughuli ya kiserikali na jamii kwa pamoja. Wewe una lipi la kupinga?
Hiyo shughuli ya kiserikali ilikuwa ni ya ghafla au ilipangwa muda mrefu?

Kwani kulikuwa na ugumu gani wa kutoa ahirisho la mechi siku moja kabla?
 
Jambo wakuu!

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha. Naomba niwatonye jambo moja la hatari linaloinyemelea soka ya Tanzania endapo TFF hawatachukua hatua zinazofaa kuepushia mbali hatari hii.

Mechi iliyopita kati ya Simba na Yanga ilishindikana kuchezeka baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kugoma kupeleka timu kiwanjani kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni zinazoendesha ligi kuu (VPL). Huenda kweli madai yao yalikuwa na mashiko ndio maana hadi leo hawajachukuliwa hatua zozote za kinidhamu kama ilivyo kawaida. Na kwa bahati mbaya, hadi leo hakuna mtu yeyote (sio serikali, TFF, bodi ya ligi au wizara ya michezo) aliyetoa sababu za msingi za kuahirishwa kwa mechi ile, licha ya kwamba Yanga wanainyooshea kidole TFF kwa kuvuruga muda wa mchezo bila sababu zinazoeleweka.

Mimi sio mtu wa mpira kiviiiiile lakini nadhani Yanga wapo sahihi kwa asilimia 90% kwa kuwa TFF wameshindwa kuwaadhibu kwa kugomea mchezo au kutoa maelezo kuhusu kadhia nzima. Nina wasiwasi mchawi ama yupo ndani ya TFF au bodi ya ligi. Ndio maana wanashindwa kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe ili kuepuka aibu. Pia wanakwepa kudaiwa fidia na timu za Yanga na Simba kwani awali timu hizi zililalamika kutumia gharama kubwa za maandalizi ya mchezo husika na hivyo kutaka aliyeharibu mchezo kuwalipa fidia.

Jambo jingine linalowaumiza vichwa TFF ni kuhusu mamilioni ya fedha za mashabiki walizokusanya kama viingilio. Je, fedha hizi zinarejeshwaje kwa wahusika na watawatambuaje? Tukumbuke kuwa tiketi za mashabiki zilichanwa kabla ya kuingia kiwanjani.

Utamu wa utata huu unaanzia hapa. Sikiliza kwa makini. Kwa muijbu wa sheria na kanuni za TFF, ili timu itangazwe kuwa bingwa wa ligi ni lazima iwe imecheza jumla ya mechi 34 kwa msimu huu wa ligi (2020/2021). Hii ni kwa sababu kuna jumla ya timu 18 katika ligi, ambapo kila timu ikicheza dhidi ya timu zote (home and away) inapaswa kukamilisha jumla ya mechi au michezo 34.

Lakini mwelekeo unaonyesha Yanga hawapo tayari tena kupeleka timu kucheza dhidi ya Simba. Viongozi wao wameishasema tena na tena kwamba wao wameishacheza huo mchezo na hawako tayari kupeleka timu kiwanjani kwa namna yoyote ile. Kwa maana hiyo, ikiwa Yanga wataendelea na msimamo huu maana yake ni kuwa, mpaka msimu unamalizika Simba watakuwa wamecheza jumla ya michezo 33, hivyo kukosa uhalali wa kisheria kukabidhiwa kombe la ushindi. Na kwa kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa hata Simba wakicheza michezo 33 wana uwezo wa kuchukua kombe, Yanga wamewatega TFF walikoroge walinywe. Wanawasubiri wausage mtama wabugie wenyewe!

Movie nzima iko hivi: endapo TFF wataogopa kuwakabidhi Simba kombe lao kwa kuogopa kuadhibiwa na Yanga, basi serikali itaingilia kati ili Simba wakabidhiwe kombe kwa nguvu na kinyume cha sheria za FIFA. Ifahamike kwamba sheria za FIFA zinakataza serikali kuingilia mambo ya michezo na adhabu ya papo kwa papo itakayotolewa ni kuifungiwa kwa TFF, hivyo kupelekea ligi yetu kufutwa na timu zetu kutoshiriki mechi za kimataifa. Aidha, Yanga nao watakimbilia mahakamani kuwashitaki TFF kwa kuwakabidhi Simba kombe kinyume cha sheria. Hapa sasa movie itakuwa imefikia patamu sana. Matokeo yake TFF watapigwa rungu ya pili na FIFA kwa kusababisha masuala ya soka kupelekwa mahakamani. Yanga wanafanya hivi kwa makusudi ya kuwakomoa Simba (watani wa jadi) ama kwa kujua au kutokujua madhara yake ya ujumla kwa mpira wa Tanzania.

The ultimate END of this fantastic movie is that TFF will be banned forthwith by FIFA and Simba will not be crowned the championship of VPL this season. Kwa hiyo sasa nchi itaingizwa kwenye migogoro ya FIFA moja kwa moja na ligi ya VPL itasahaulika duniani. Wapenzi wa mpira katika nchi hii wajiandae kisaikolojia kutazama mashindano ya ndondo. Hakutakuwa na mashindano ya VPL msimu ujao.

Nawasilisha.​
Hili jambo sioni kama litafika huko. Siku ya mchezo timu ambayo haifiki uwanjani hupewa adhabu na iliofika hupewa ushindi. TFF na board ya ligi ni mbuzi wa kafara ktk mchezo wa kwanza ulio ahirishwa. Mhusika ni serikali kupitia wizara ya michezo ilio ona ni busara kusogeza mbele mchezo ili watanzania washuhudie uzinduzi wa kitabu cha 'baba' na 'mwana' kumzawadia gari.
.
 
Hili jambo sioni kama litafika huko. Siku ya mchezo timu ambayo haifiki uwanjani hupewa adhabu na iliofika hupewa ushindi. TFF na board ya ligi ni mbuzi wa kafara ktk mchezo wa kwanza ulio ahirishwa. Mhusika ni serikali kupitia wizara ya michezo ilio ona ni busara kusogeza mbele mchezo ili watanzania washuhudie uzinduzi wa kitabu cha 'baba' na 'mwana' kumzawadia gari.
.
Huoni kuwa, kwa kauli yako hii, TFF ni wapuuzi wa kupindukia? Kwanini TFF walikubali kuahirisha mchezo kwa sababu FEKI kama hii?
 
Mjinga ww ambae unadandia treni kwa mbili huu uzi uliandikwa jana usiku na sehem ya team aliweka team 20 uliwa waliouona mapema so unakua boyaboya tu
Wewe ni 'mjinga', na kiasi mjuaji. Mbona kaandika timu zipo 18? Kuandika timu itacheza michezo 34 hujaelewa?
 
Mjinga ww ambae unadandia treni kwa mbili huu uzi uliandikwa jana usiku na sehem ya team aliweka team 20 uliwa waliouona mapema so unakua boyaboya tu
Afu wee jamaa mbona unashupalia sana hii hoja wakati kila mtu anajua ligi ina timu 18? Sawa tumekuelewa. Hebu changia hoja sasa.
 
Subiri tarehe 3 tuutoe huo mwiko matakoni 100% najua mtaleta team
Mbona wee chalii unapenda kuandika matusi kiasi hiki? Hivi huwezi kuchangia hoja bila kuweka matusi? Bora tu shule zifunguliwe mrudi shule mkapambane na walimu wenu tumewachoka.
 
Mnazingua sana mnajikuta viazi mnaleta tu nyuzi ambazo hazina mashiko sisi tunategema jf kukuta vitu smart sa nikikutana na huu utopolo nashindwa kujizuia
Mbona wee chalii unapenda kuandika matusi kiasi hiki? Hivi huwezi kuchangia hoja bila kuweka matusi? Bora tu shule zifunguliwe mrudi shule mkapambane na walimu wenu tumewachoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom