TFF wanazidi kujipambanua kwamba Simba ni Kijana wao mpendwa

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Natoa kama Rai mashabiki wa Yanga hamna budi kuomba sana kwa ajili ya timu yenu maadui ni wengi mnoo mje na ndani ya uwanja na wanafanya kazi kwa kushirikiana kuhakikisha malengo yenu hayatimii.

Adui kwa kwanza mkubwa wa Yanga ni TFF, TFF ipo kwa lengo la kuhakikisha yanga inaharibu lakini kwa maombi na sala za wanayanga timu yao bado inafanya vizuri, nani anakumbuka gemu ngumu za Yanga back to back lakini bado yanga ikavuna pointi zote, nani anakumbuka Aucho kupigwa ban ili akose michezo muhimu lakini bado Yanga ikatusua.

Kali zaidi ni hii ratiba ya sasa ukiangalia ratiba Simba ndio ana viporo vingi ila bado ratiba inampa upendeleo, nlitegemea Simba ndio aanze kucheza gemu zake kwanza halafu Yanga ndio wafwate ila imekua kinyume.

Nani anakumbuka gemu ya Azam na Simba ilivyopigwa danadana lengo tu Tff waliona upepo wa Simba sio mzuri wakawapa muda wa kujipanga na kufanya sajili ili tu kuwatengenezea mazingira mazuri ya ushindi, kumbuka hapo yanga alicheza na Azam, Singida utd, Simba bado akaenda tanga kucheza na vijukuu vya Simba Kostali united.

Yanga imecheza leo, Kesho inapanda ndege inakwenda Mbeya kumbuka watashukia Songwe na safari ya basi mpaka mbeya wakati huo Kesho Simba anacheza na Azam Mwanza then anacheza na Geita utd pasipo na Shaka Tff watawabana Geita utd wachezee Mwanza so Simba hatosafiri na kupata faida ya kupunguza uchovu haya yote yanamtengenezea mazingira Simba..

Ukiangalia Afcon inayoendelea Wachezaji wawili muhimu wa Yanga Nondo na Bacca walitumika sana karibia mechi zote walicheza ila ajabu bado ratiba ya Azam confederation cup walianza kucheza Yanga ilihali Tff wakifahamu wachezaji wa Yanga wametoka kwenye majukumu mazito ya kitaifa.

Kama hilo halitoshi ukiangalia mazingira ya marefa bado wanaibeba SImba kuna tukio gemu na Mashujaa kule Kigoma Kibu D alichezewa rafu refa akatenga tuta leo the same same event kachezewa Yao refa kapeta.

Hakika matukio ni mengi ntajaza server ya JF tu ila Tff watambue kwa tabia hii ya kuipendelea Simba ni ngumu sana kuja kupata timu nzuri ya taifa tutaendelea kudemadema tu
 
Tusiogopo yanga ratib Ni nyepesi Sana wacha tuanze mechi zetu mapema tuwadubiri yanga Ina kikosi kipana kuxidi timu zote ,yanga Muda wowote anakupa matokeoo mazuri

Na kesho Azam atamuoa kbsa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom