Simba 10 wauawa Ngorongoro, yadaiwa ni kisasi baada ya Simba kuwala punda wawili wa wafugaji

Simba 10 wauawa Ngorongoro, yadaiwa ni kisasi baada ya Simba kuwala punda wawili wa wafugaji

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,842
Reaction score
5,152
Taarifa za awali kutoka eneo la Ndutu, Kata ya Endulen, Wilaya ya Ngorongoro, zinaeleza kuwa leo Septemba 19, 2026, simba wapatao 10 wameuawa katika tukio linalodaiwa kuhusishwa na kisasi baada ya simba hao kuwala punda wawili wa wafugaji katika eneo hilo.

Taarifa zinaonesha kwamba awali simba waliokuwa wamekufa hadi saa 4:00 asubuhi walikuwa watano. Taarifa za baadaye zinaeleza kuwa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 10.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, simba hao wanadaiwa kulishwa mzoga wenye sumu, katika tukio linalodaiwa kufanywa na baadhi ya wafugaji baada ya tukio la kuuawa kwa punda wao lililoripotiwa kutokea Septemba 17, 2026.

Jeshi la Polisi pamoja na askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamefika eneo la tukio na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo na kuwabaini wote waliohusika.

Tathmini ya awali imeibua madai mengine kwamba uharibifu huo unaweza kuwa na lengo la kusababisha uhaba wa maji na hivyo kutengeneza mazingira ya kudai kuruhusiwa kwa mifugo kuingizwa katika maeneo ambayo yamewekewa zuio kwa sababu za uhifadhi.

Mamlaka zinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa kadiri taarifa zilizothibitishwa zitakavyopatikana.

FB_IMG_1789853201537.jpg
FB_IMG_1789853199526.jpg
 
Back
Top Bottom