Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Duh, pamoja na wadhifa wako wote, bado kiinglishi kinakupiga chenga!


Kama CCM imeshindwa kuwapata viongozi mpaka ikawaamini watu kama akina MCHEMBA kuwapa unaibu katibu mkuu sasa unadhani CCM inaelekea wapi, akina Jerry Slaa eti ndiyo viongozi wa CCM inatisha hawa wanachokijua ni kujiendekeza kwa zidumu fikra za mwenyekiti lakini si watu wa strategy ndiyo maana wanachokiweza ndicho hicho mnachokishuhudia, hakuna zaidi. wenye kujua nini cha kufanya wanaangalia tuu.
Poleni sana CCM mmechemsha kabisa kwa safu yenu ya uongozi mliyonayo, inaonekana kabisa kwamba maji yapo shingoni chochote mnachodhani kitawaokoa mnakidaka, ndiyo ilivyo kwa kila mfa maji, watanzania hatuwatakiiiiiiiiiiii !!!!!!!!!! ????????????????? @@@@@@@@@@@@@
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.

Yakweli hayo Mwigulu?
 
Kuhusu ukweli wa yeye kuongea na Nyakalungu ameshasema , japo hajatamka mojakwamoja.Kitu anachotaka kutuaminisha ni kwamba alikuwa anamshauri Nyakalungu kuhusu, kufanikiwa ktk siasa bila kuwa na fedha, biashara pamoja na masomo.Mimi naamini wapo watu wengi wa kutoa ushauri mzuri kuhusu hayo maswala zaidi ya huyu mwigulu. Kwanini mwigulu, kwanini sio Mnyika, sio prof Baregu, kwanini sio Dr. Slaa au watu wengine ambao hata kama sio wana-CHADEMA, basi pia wasiwe maadui wa chama.Kwa mtazamo wangu mimi,mbali na maadui wakubwa wa nchi yetu kama umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi, pia kuna maadui watu ambao ni sampuli ya huyu mwigulu nchemba, watu kama hawa hatupaswi kuchangamana nao kabisa.
 
unadhani kunasiku atawaza maendeleo haitakuja kutokea hata siku moja, umwambiwe kunamganga sehem fulani atamtafuta mpaka ampate mwanga huyu.
 
Well hata kama ungemkimbia bado sio jambo la mjadala!
 
Sijui hata unachokisema ni nini?. Kwanza umefahamu kama mimi ni Mura kwa maana kwamba Mura kwenye R wanaweka L na hii ni kutokana na rafudhi zao, vivyo hivyo kwa makabila mengine.

Hata Waingereza ambao point yako unaipeleka huko huwa wanatumia S wakati Wamarekani (USA) mara nyingi wanatumia Z kwenye kiingereza.

Hata rafudhi za Waingereza wenyewe zinatofautia, kuna Cockney, Geordie, Scouse, Brummie n.k

Huyo unayemsema anaweza kukufukuza kazi kwa sababu ya rafudhi hafai hata kuwepo kwenye hiyo position kwa sababu kama angekuwa amenawa uso kwa kutembelea sehemu na nchi mbali mbali hata asingefikiria kitu kama hicho achilia mbali kuandika barua ya kukuachisha kazi.

Ni afadhari ajue kama hajui kuliko kujifanya anajua kumbe hajui.
Nakubaliana na wewe mkuu,lakini naomba ufanyie mazoezi matumizi ya r na l kwa sababu hapo tena umerudia neno "rafudhi "mara mbili badala ya "lafudhi" pia "afadhari" badala ya "afadhali" ili kuepusha ukosoaji mwingine wa vitu vidogovidogo,mimi naheshimu ufahamu wako katika mambo anuai ingawa hotofautiana nawe katika utetezi wako kila CCM inapoelekezewa tuhuma
 
bora hata ungemfuata ukamsalimie maana kuanzia 2015 atakua matawi ya juu hata kumwona kwa mbali hutamwona
 
Ni kweli umekimbia bhana acha soga hizo....toa sababu sasa kama kinachosemwa hapa ni uongo
 
Hiyo kwenye RED na wewe ni nini?. Usipende kuwanyoshea wenzio vidole haraka haraka. Sisi ni binadamu na mapungufu ndiyo yanayotufanya tuwe wanadamu. Siwezi kukwambia hilo ni pungufu la kimantiki kwa sababu uwezo huo sina.

Ni angalizo tu.
,
Mkuu M,Mtoi yuko sahihi kwa kiswahili fasaha kusema "Kakio" ni sawa na kusema "Kaka Yako",ni kama kufupisha maneno,nduguyo,mwanao,dadayo,rafikiyo nk
 
Kakio ndiyo nini?

Hivi na wewe ni Chadema? Mohamedi na Chadema wapi na wapi? Bora ungebaki chama chako cha zamani CUF.

Kasome kiswahili vizuri,ukitaka kusema "kaka yako" kwa namna sawa na kusema "nduguyo,mwanao,rafikio"unasemaje?
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.

Sijakupata hapo kwenye red unamanisha nini?
 
Kwa nini mnatumia jina bandia (Mwigulu Nchemba ) kum-address huyu mtu? Jina lake sahihi ni Lameck Madelu. Wisdom begins with calling a person by his correct name-Lameck madelu!!!
 
Mwigulu Nchemba utawapa vijana mawazo gani wewe? Ya mgando au yaliyoyeyuka? Huna haiba wata heshima kihivyo!! Labda utafute wachemfu kama wewe!!! Au unataka kuwafundisha manners zipi wakati wewe huna? Bora ungekaa kimya usije tuchafulia hali ya hewa hapa!! Kashughulikie matatizo yenu huko na anguko la Elimu na shida ya maji tanzania nzima!! Nakushauri uishauri CC mkamuombe Mnyika na Mbatia Msamaha ndipo kieleweke. Shughulika na makubwa na si madogo kama uliypost hapa!! Husafishiki!! Labda tutumie maji taka kukuchafua zaidi.
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia. Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.

Mhe. Mwigulu Nchemba vijana wageni waliofukuzwa CHADEMA na kuingia ccm wakapewa kipaumbele cha kutembezwa kila kona kufanya mikutano wakati kuna vijana wa UVCCM ambao wana uwezo mkubwa kuliko hao vijana.Pia hao ambao wameenda CCM kufuata pesa afu wanapewa heshima ya kutumia jasho la chama kwa kufanya mikutano kitu ambacho kinawavunja moyo walio kipigania chama cha dhidi ya chadema,unasemaje juu ya hilo?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom