Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Sungusungu ungetamani sana iwe hivyo lakini utasubiri sana. Kura hazitapigiwa jf. Kwa iramba hakuna mtu atafikia hata nusu ya kura zangu.

labda za maruhani...........we ni zero kabisa subiri kiama chako...laana tupu damu za watu zinakutafuna nilikutafuta sana igunga sikufanikiwa just hold on.....
 
Sungusungu ungetamani sana iwe hivyo lakini utasubiri sana. Kura hazitapigiwa jf. Kwa iramba hakuna mtu atafikia hata nusu ya kura zangu.

Kwani Iramba ulishindaje??? Fahamu jinsi ulivyoshinda na ndivyo hivyo utakavyoshindwa.

Hustahili kuwa mbunge kabisa wewe.
 
Acheni chuki mwigulu ni muwakilishi halali anawakilisha watu kibao wa jimbo lake ww unayesema hakustaili kuwa mbunge unamuwakilisha nani inawezekana hta familia yko haikuamini uiwakilishe
 
Unasema hudhani kama alikuona,mara alipita kwa kasi na hakuwa na attention na watu...sasa tena ulimwonaje kama alipita kwa kasi?
 
Hivi tukiacha utani, ni kweli kutoka moyoni mwako Mwigulu unaweza kumsalimia kwa dhati ya moyo wako Dr. Slaa? maana huwa unamtukana na kumdharau sana!
 
Jambo ambalo unapaswa kufahamu ni kuwa ww bado una umri mdogo na unasafari ndefu sana kisiasa! naamini watu wengi wanaweza kuwa wanakueleza ama watakueleza jambo hili. no body knows about tommorow.
 
Haihusiani chochote Albert Einstein wakati anaenda Marekani alikuwa hawezi kiingereza vizuri na alikuwa anatoa hotuba na kufundisha kwa kiingereza kibovu kuliko hicho cha huyo 1st class Economist alichokiandika na Albert Einstein alikuwa ni 1st class Physicist kama ukipenda!


Yaan unadiriki ku m compea Mwigulu na Einsten!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Kweli Zero za Kawambwa hazikuanza leo
 
Kwangu wewe(mwigilu) ni moja kati ya wanasiasa vituko hapa nyumbani, samahi lakini
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.
Ni kweli hukumkimbia ndio, bali ulikua unatembea wakati unamkwepa!!
 
Mwigulu,
Hapo kwenye nyekundu na blue mbona zinakinzana? Nikisoma between lines naona kama ulimuona Dr. Slaa (angalia kwenye blue), ndiyo maana unasema kulikuwa na watu wengi na hata attention hakupata. Wakati huo huo unasema (kwenye nyekundu) kwamba hukumwona Dr. Slaa. Pole sana kwa kujichanganya.
sikuwa na mpango wa kulog in lakini comment yako imenifanya nilog in ili nikupe like LOL
 
Mh. Mwigulu wanaokushambulia hapa ni watu wanaoamin ktk uchama kuliko taifa,kwao wao yeyote anayetishia uhai wa chama chao ni adui na uzuri ni kwamba silaha yao ya matusi na kejeli hapa jf haiathiri fikra za waliokuchagua na wanaoendelea kukuamini.na kwa wanachama wa chama cha mapinduzi hakuna fitina itayopakwa mafuta tukaipokea ili uachie ngazi wapate kupumua.wamepoteza umaarufu wanachachawa.
 
Iramba tunajua kuwa Baba yeti Mwigulu no mwiba WA upinzani. Kwetu sisi no mbunge WA kihistoria. Ameleta heshima kwa miss mfupi
 
Humu kuna vituko,sasa umkimbie kwani ana mapembe.
Ndiyo ,jamaa sio handsome kivile,hata kama anatisha(i mean muonekano)ndo kweli mtu amkimbie?

muonekano wa nini, kwani anachumbiwa, hiyo ndiyo sura ya kiume siyo ya 'kike-kike'
 
Kwa nini unajitokeza unaposhambuliwa binafsi wakati kuna mambo mengine mengi yenye maslahi ya taifa huyazungumzii. Mfano kama mchumi kwa nini usizungumzie kupanda kwa gharama za maisha; unga sembe ni gharama kuliko hata unga wa ngano. Tunahitaji fikra zenu kama ni pevu zijidhihirishe kwenye maslahi mapana ya taifa na mustakabali wake na si hizi hoja dhaifu ambazo hazima manufaa kwetu.
Swala la wewe kumkimbia au kutomkimbia sio issue ya kuzungumza maana haikuongezei wala kukupunguzia kitu.
 
Mwinuka unahoja ya msingi lakini elewa kiongoz alitoa majibu. Kama ni la hoja mngeweka thread yenye issues then mmwite kiongoz kufafanua. Nijuavyo angekuja na hoja ya unga maji sukari mngesema jibu tuhuma. Humu vichwa maji vingi kuliko mambo ya msingi kama hayo unayofikiria
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli
na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.

kwa hapo mwanzo kabisa, Kumbe thread zote huwa unaziona eh???? haya tuachane na hayo, twende kazi;
Hapa naona wengi wamepaona ila mi nakazia tu kama ilivyokua kwa baba rizi, kwahiyo ndugu Nchemba, hukukimbia bali uliondoka sema kwa mwendo kasi kwa vile ulikua na ratiba zao za kutoka na mwendo kasi pale ukishtukiwa sio???

na kama una uhuru wa kuteta na mtu yeyote na wa chama chochote, maana yake ulikua na Nyakarungu sio???

hapo kwamba hukumwona Dr. Slaa kwa vile alipita bila attention ya watu na ulikua na watu wengi naomba niruke manake hata yule wa form 4 ya juzi anakucheka, labda niulize tu kwani yeye Dr. sio mmoja kati ya hao watu wengi???? haya, tuendelee na story, na hayo uloyasema sijui kama yametoka kwenye moyo wako ama kwenye kongosho, eti unawashauri namna ya kuingia kwenye siasa bila ya kutumia hata senti 5??
wewe kwenye budget ya nchi umeshindwa hata kuchangia ile contigency fund itumike namna gani alafu ndo wa kushauri hayo uloyasema???
shame, kwenye kipengele cha elimu, wacha ni take a comercial break kidogo, hivi ungekua na huo upeo wa kuwashauri juu ya elimu ungeweza vipi kuzima ile hoja ya mbatia??? na hoja nyingi tu za Mbunge wako wa Ubungo???
embu kapige cha Arusha afu urudi hata kutuimbia taarabu kama zile za kwenye kampeni. na hiyo afya ya taifa unategemea itoke wapi kama watu wake ndo full assasination??????

labda kwa vile tu upo off line, ukirejea naomba unambie umri wako bro, mwenyewe nataka nikuombe ushauri namna yakufanya biashara halali kama zile za Dr. Ulimboka Kule Mabwepande, gues kulikua na mkwanja wa kutosha. hope hutonibania tips. Shame on you ccm and members.

ni maswali tu bro ningependa tujadili kwani namimi ni kijana kama wale ulokua nao pale kwenye "bila attention ya watu"
 
Back
Top Bottom