Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Kukimbia ilikuwa muhimu maana Dr Slaa Nyundo iliyowashinda Waajemi.
 
Mwigulu Nchemba,

Bora umejitokeza kuweka sawa ili swala Dr Slaa bana sasa umkimbie kwa sababu gani.
 
Jamani acheni siasa kwanza. Mkienda mwendo huu mtakuwa mnaenda siko. Nawaombeni watu wawe na uhuru wa kukutana na kuongea na mtu yeyote. Ikitokea wana mitizamo tofauti basi isiwe chanzo cha kujadiliana mambo mengine. Maisha si siasa peke yake. Hata Mh. Dr. Slaa kuna wakati aliishi na mtalaka wake ambaye alikuwa ni mwana CCM na yeye Slaa akiwa bosi wa CDM.
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.
Uandishi na jinsi ulivyojenga hoja kwenye huu uwongo unaotuandikia hapa unajidhalilisha mkuu. Ningekuwa mimi ndio wewe ningesema tu "Kuna mtu ameniibia password yangu" tungekuelewa kuliko huu uwongo unaojaribu kuutetea.

Mwigulu Nchemba,

Bora umejitokeza kuweka sawa ili swala Dr Slaa bana sasa umkimbie kwa sababu gani.

Kaka wewe nawe husomeki kwa usahihi kama jinsi kakio Mwigulu anavyo someka. Rudi hapo juu usome vizuri akili ikiwa imetulia uone jinsi ombwe la ki-mantiki linavyo jidhihirisha.
 
Mwigulu Nchemba,

Bora umejitokeza kuweka sawa ili swala Dr Slaa bana sasa umkimbie kwa sababu gani.

Kwa sababu ni mwiba kwa CCM. Hata M/kiti wako anajua na kulikiri hilo!!!! MAGAMBA wanapo muona mahali alipo, ni sawa na kuwaambia MAGAMBA WASHIKE NYETI ZA SIMBA ALIYEJERUHIWA". Kitu ambacho hakiwezekani.
 
Kaka wewe nawe husomeki kwa usahihi kama jinsi kakio Mwigulu anavyo someka. Rudi hapo juu usome vizuri akili ikiwa imetulia uone jinsi ombwe la ki-mantiki linavyo jidhihirisha.

Hiyo kwenye RED na wewe ni nini?. Usipende kuwanyoshea wenzio vidole haraka haraka. Sisi ni binadamu na mapungufu ndiyo yanayotufanya tuwe wanadamu. Siwezi kukwambia hilo ni pungufu la kimantiki kwa sababu uwezo huo sina.

Ni angalizo tu.
 
Mwigulu,
Hapo kwenye nyekundu na blue mbona zinakinzana? Nikisoma between lines naona kama ulimuona Dr. Slaa (angalia kwenye blue), ndiyo maana unasema kulikuwa na watu wengi na hata attention hakupata. Wakati huo huo unasema (kwenye nyekundu) kwamba hukumwona Dr. Slaa. Pole sana kwa kujichanganya.

Mara nyingi kwenye Ukweli Uwongo ujitenga!
 
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.

sasa wewe gamba kama unasema ukumuona dr....uliona vipi kama hakupata atensheni ya watu??kama sio umbea unakusumbua mtoto wa kiume
 
Kwa sababu ni mwiba kwa CCM. Hata M/kiti wako anajua na kulikiri hilo!!!! MAGAMBA wanapo muona mahali alipo, ni sawa na kuwaambia MAGAMBA WASHIKE NYETI ZA SIMBA ALIYEJERUHIWA". Kitu ambacho hakiwezekani.
jama,sio slaa huyuhuyu aliekua anamkwepa JK hadi kwenye misiba akawa anajitahidi wasikae nae karibu hadi watu wakasema tena humuhumu jf?
 
Hizi siasa za majitaka ziko katika vyama vyote vya siasa Tanzania. Inashangaza pale watu wanaangalia kwa jicho moja wakati siasa kwa Tanzania zina uozo kifkra na kimtazamo.

Hakuna Maraika kwenye siasa za Tanzania. Vyama vyote ni wale wale.

great words.....ubarikiwe....
 
Back
Top Bottom