Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.
Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.
Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.
Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.[/QUOTEkiri kuwa ]
Anhaaaaa......!afadhali mwenyewe umekiri ya kuwa uliluwa katika eneo lilotajwa, na ni kweli kuwa ulikuwa una mazungumzo na bwana Nyakarungu!
Kwa jinsi ulivyokosa staha kichwani mwako na jinsi unavyoteswa na mafanikio ya CHADEMA kisiasa hapa nchini, lazima watu wenye akili tukutilie mashaka...
Kuna jambo unataka kulipika kwa kumtumia huyo kijana!