Sikujua kumpoteza Baba ni kugumu hivi

Sikujua kumpoteza Baba ni kugumu hivi

Pole sana Dada! Mwenyezmungu amrehem inshallah!
Unaweza mfariji huko aliko Kwa kutenda mema Kwa ajili yake,eg toa sadaka,chimba kisima Kwa jamii,nk, yaan fanya jambo jema ambalo ni endelevu lenye thawabu/ malipo Kwa Muumba,huku ukielekeza hizo thawabu kwake.

Kweli kufiwa na Baba n jambo linaloumiza,sana,na halisahauliki.
Mi nakumbuka nilifiwa na Baba tangu 1998,nikiwa form two,nilikua shule,halafu siku 5 kabla ya kifo chake alinisubiri road,/njiani ili anisalimie na kunipa pocket money,tulikua tunatoka Mikumi National Park(study tour),lakini hatukuonana. Alitusubiri mpaka sa 4usiku akarudi nyumbani kulala. Sisi tulipita pale mida ya saa 5,usiku.
Hiyo ilikua ni siku ya jumamosi.
Ilipofika jumanne,nimefuatwa shuleni na Mgeni kutokea kijijini kwetu,naambiwa unaitwa,nje,(nilikua class),toka na vitu vyako vyote, nikasafiri hadi nyumbani,ile nafika tu,nashuhudia umati wa watu wamejaa uwanjani kwetu.
Nauliza,naambiwa Baba yako amefariki Jana usiku,na leo ni kuzika.
Niliumia sana,siku ile sikulia sana,lakini nilipata maumivu makali sana,nilipomaliza form 4,sasa natakiwa kwenda Ndanda high school,kuanza form 5,.
Huezi amini ni miaka 19,sasa tangu nimeondokewa na Baba,lakini mpaka leo taswira hunijia,take Baba,
Ninamuona ndotoni,na kuzungumza nae Mara kadhaa. Machungu ninayo mpaka sasa.
Allah mrehem Baba,na umuangazie nuru ktk giza la kaburi,inshallah!
pole sana[emoji29] japo mda umepita... maneno yako yapo flani ivi yamenifanya hadi niwazie(kuimagine) mambo mabaya..Mungu aepushie.RIP mzee
 
Pole Sana Dada,

Kufiwa na mtu wa karibu, Mtu umpendae, Mtu ambaye kwako unamuona kama nguzo pekee hapa duniani Si kitu kidogo.

Hakuna unachoweza kufanya zaidi, Hakuna Mtu dunia hii anayeweza kukupunguzia Machungu ya kufiwa na Baba yako.

Pole pekee hazitoshi kutuliza Maumivu na Uchungu ulionao Moyoni.

Mie nishapitia hatua hiyo ngumu maishani, Nafahamu maumivu uliyonayo.

Itakuchukua muda,Akili na Mwili kutulia na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Kamwe usiminye hisia zako za uchungu, Unapojisikia kulia lia hasa inasaidia kuondoa uchungu ule wa ndani kabisa,

Ni kipindi Kigumu Sana, Na ndio wakati sahihi zaidi wa kuzidi kumuombea huko aendako.

Pole sana.
 
Mwenyezi Mungu akutie FARAJA na AMANI moyoni mwako ,akuondolee maumivu yako yote ya msiba wa baba yetu
 
Pole sana my dear

Maumivu ya msiba ayajuae mfiwa pekee. Msiba unauma sana tena sana hakuna cha kuulinganisha nao. Maumivu yake ni ya milele.

Unaweza onekana nje unatabasamu ila moyo unalia machozi ya damu na hata ukisema ulie nje bado watu watakusema unajiendekeza hakuna ajuae maumivu ya mtu kila mmoja ana maumivu yake kwa kipimo chake.
images(2).jpg
images(1).jpg
 
Babangu alizawa tarehe 28/12/1958
Alifariki juzi tarehe 25/12/2017 kwa ajali
Kwa hakika katika maisha yangu yote hili ni pigo la pili baada ya pigo la aliyekua mpenzi wangu lakini naona hili ni zito kuliko
Siwezi kulala usingizi bila kulia katikati ya usingizi.
Siwezi kula bila kumfikiria na wakati mwingine hata chozi hunitoka
Kwa siku hizi 5 tu Naona Dunia ni ngumu kuliko chochote,niwaangaliapo ndugu zangu naona wa wana afadhali kuliko Mimi najitahidi Ku behave kama wao lakini nashindwa
M/Mungu amrehemu baba yangu na kumpunguzia adhabu ya kaburi, nime jikuta nataka kubaki kijijini ili nilione tu kabuli lake kila siku lakini inanibidi nirejee kwenye familia yangu.
Pole mkuu kwa kipindi kigumu unachopitia..kuna hali ambayo uko nayo kwa sasa muda mwingine unahisi huamini kwa kilichotokea naelewa situation uko nayo kwa sasa because nimeipitia...hiyo hali huwa inapotea taratibu baada ya mwezi utajikuta unaanza kukubali ukweli kuwa mzee hayupo duniani na kadri siku zinavyoenda utajikuta umezoea na kuona basi kazi ya mungu haina makosa.ila kwa haraka ni ngumu kuzoea.piga moyo konde muombee baba apumzike kwa amani na mW mungu ampunguzie adhabu za kaburi ukumbuke kumfanyia dua na kumtolea sadaka mzee wako...kila mzazi anayetangulia amali yake pekee duniani ni watoto wake hasa pale unapomtolea sadaka nakumuombea dua apate kupunguziwa adhabu ya kabur.

Qullnafsi dharikat mauti..........hakika kila nafsi itaonja umauti.

Pole sana mkuu
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
Nahisi alifurahia kuachiwa mali za urithi
 
Kwann mkuu, au ulifurahia kuachiwa mali za urithi?
Hata kama ulizaliwa mtaani huna baba usilete mzaha ktk jambo hili fahamu kuwa mali sikila kitu wapo walioachiwa Mali lkn zimegeuka mateso makubwa sijambo la kuleta mizaha hili kuwa makini na unacho zungumza
 
Hata kama ni mzee na alikuwa anakutegemea hii habari haielezeki ni isubiri siku yakukute Mimi ilikuwa 2015 Disemba lkn najikuta hataleo ni napata uchungu usio elezeka ninapo mkumbuka japo mimi ni mtu mzima wa miaka 50 sasa
Kuna umri ukifika utakiwi kuamkia wewe unakuwa wakupokea tu salamu .na mpaka mzazi wako akifikia huko hakuna namna hata wewe mtoto unaona pia ni kheri apumzike hakuna namna.

Nimewaza tu.japo kweli hakupunguzi machungu ya kufiwa na MTU huyo.all in all pole sana
 
Pole sana mpendwa ,unajua wakati fulan mwanadamu anaitajika kua na Nguvu ya kukubali !! Nguvu ya kusahau kilichotokea ili kuweza kusonga mbele..

Ona, mawazo mengiii husababisha ubongo kuzalisha appetite suppressing hormone, hiii hupelekeaa kushuka kwa kiwango cha Cortisol na serotonin mwilin mwetu and the same time Adrenaline hormone humwaga nyingi mwilin , sasa matokeo yake,, mwili wote unajiona upo ktk maumivu ,, na kwsababu mwil upo ktk maumiv ,Kinachotokea unajikuta unajitahidi sana kutafuta Survivability nasio uponyaji wala matumain and Finally HATA CHAKULA HUTOWEZA KUKILA ,SABABU NACHO KINAKUPA PHYSICAL PAIN !!!

Nasababu huli chakula ,, Tumbo linalazimika Kumwaga Acid yake ambayo mwisho huishia kukwangua kuta za tumbo na utumbo na baada ya Muda utapata Madonda Tumbo ambalo linakua tena ni Pigo LA Tatu.

Nikuombe mpendwa ,,, sote tumepoteza wazazi Wetu, tumepoteza wapenzi ,ndugu na rafiki ,,tumepoteza watu ambao mwanzo hukuitaj ipite hata sekunde moja bila kumwona au kusikia sauti yake,, but what we gonna do ????? We have been born and raised with a Limit ,the point of no return itabakia kuwepo tu ..

Mmhhh mpendwa ,, kwann sasa mapito yako yakuamlie maisha ?? Yaharibu maisha ? Yakutie ktk matatizo makubwa zaidi ??.

Embu bana usiwe ivo ,, you are strong ,I say you are always strong na utabaki kua strong ,, I hope you can walk through that storm , I hope you can stand on the top of mountain nakusema "hakika nimeweza".

I hope you are such person who believe that ,the challenges are there to strengthen our conviction.

I hope you are strong to the extent that ,you believe Challenges are not there to run us over.

I hope u mwanamke imara who believe that , after the storm ,Comes fair weather.

I trust in you that ,you are such woman who believe after Sorrow ,Comes joy !!.

My dear ,, usiumie sana mapito ,you are strong , nawala hamna ambacho ndugu najamaa wamekuzidi ..

Take it from me ,,, *Every seed knows its time , So stay strong mama , the Sun will shine in your yard too*.
Nice words[emoji8]
 
Kuna umri ukifika utakiwi kuamkia wewe unakuwa wakupokea tu salamu .na mpaka mzazi wako akifikia huko hakuna namna hata wewe mtoto unaona pia ni kheri apumzike hakuna namna.

Nimewaza tu.japo kweli hakupunguzi machungu ya kufiwa na MTU huyo.all in all pole sana
Huwezi kumuombea mzazi afe eti kisa umri uwepo wake tu ni kuwaweka nyinyi karibu kwawale mnaokimbia majukumu ndio mnaona akizeeka bora afe huku mkisahau kuwa mmezaa vitoto vyenu mkarushia huko ili mlelewe
 
Back
Top Bottom