Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 38,352
- 88,797
ULE MWISHO UTAKAPOFIKA
Anaandika Robert Heriel
Mtibeli
Nilipoanza kuhesabu siku zangu zilizobaki, niligundua kwamba nilikuwa nimeishi maisha yangu yote nikihesabu siku nilizokuwa nazo.
Sasa niko kitandani.
Mwili wangu umekuwa kama Gofu ambalo mwenyewe anajua i
Limeanza kupasuka. Miguu haina nguvu kama zamani. Mikono inatetemeka ninapojaribu kuinua kikombe. Macho yangu yameanza kunisaliti na kumbukumbu kupepesuka, lakini ajabu ni kwamba akili yangu bado inakumbuka mambo ambayo ningependa iyasahau.
Ninatazama dari.
Kuna nyakati ninahisi kama dari hiyo ndiyo anga langu la mwisho.
Ninajua nitakufa.
Lakini Sijui nitakufa lini.
Lakini najua.
Na labda hiki ndicho kitu pekee ambacho mwanadamu hujua kwa uhakika, lakini huishi kana kwamba hajui.
Mlango wa chumba nilipokuwa unafunguliwa.
“Babu?”
Alikuwa mjukuu wangu. Kijana mdogo mtoto wa binti yangu.
Anaingia taratibu, akifuatwa na mama yake. Anakuja pembeni ya kitanda na kukaa karibu yangu.
“Babu, unaumwa?”
Ninamwangalia na kutabasamu.
“Uzee si ugonjwa, mwanangu.”
“Basi ni nini?”
Ninavuta pumzi ndefu.
“Ni ukumbusho kwamba muda haukusubiri.”
Ananiangalia bila kuelewa.
Watoto huwa wanafikiri wazee wanajua kila kitu. Hawajui kwamba sisi wazee tulijifunza mengi baada ya kuumia.
Nilimshika mkono.
“Unajua mwanangu, kuna makosa ambayo mtu huyaona ukiwa mdogo, lakini ukifika mwisho wa safari ndipo unagundua yalikuwa makosa makubwa.”
“Ulikosea sana, babu?”
Nilicheka.
“Nilipatia pia.”
“Ulipatia nini?”
“Nilipatia pale niliposikiliza moyo wangu. Nilikosea pale nilipodhani kwamba nilikuwa na muda mwingi.”
Kimya.
Hapo nikageuka kuangalia dirishani.
Nje kulikuwa na watoto wakicheza.
Nilitabasamu.
Nilikuwa nimewahi kuwa mtoto kama wao.
Nilikuwa nimewahi kukimbia bila kujua kwamba siku moja miguu yangu ingeshindwa hata kunipeleka chooni.
Nilikuwa nimewahi kuamka asubuhi nikiwa na mipango mingi.
Nilikuwa nimewahi kusema, kesho nitafanya.
Kumbe kesho ni deni ambalo si kila mtu hulipwa.
Nikafumba macho.
Na hapo ndipo maisha yangu ya zamani yakaanza kupita mbele yangu kama filamu.
Nilimwona yule Robert wa zamani. Aliyejiita Mtibeli. Yule mwandishi machachari.
Kijana.
Mwenye nguvu.
Mwenye hasira za ukamilifu
Mwenye ndoto za mafanikio.
Mwenye kiburi cha maarifa.
Mwenye tamaa ya hekima.
Mwenye upendo
Lakoni Mwenye makosa mengi ambayo nilitamani niyasahau. Lakini je?
Nilimtazama kwa muda mrefu.
Nikajiuliza:
Kama ningekutana na huyu kijana leo, ningemwambia nini?
Ningemwambia asikimbilie kila kitu.
Ningemwambia si kila anayekupinga ni adui yako.
Ningemwambia si kila anayekusifia ni rafiki yako.
Ningemwambia mali ni muhimu, lakini usiuze utu wako ili uipate.
Ningemwambia mwanadamu anaweza kujenga nyumba kubwa na bado akaishi ndani ya moyo mdogo.
Ningemwambia usiwadharau wazee. Kwa sababu siku moja utakuwa mmoja wao.
Na ningemwambia jambo moja ambalo ningetamani kulijua mapema:
Usiishi maisha yako kwa ajili ya kuwafurahisha watu ambao hawatakuwepo siku ya hukumu yako.
“Babu?”
Nilifungua macho. Mjukuu wangu alikuwa bado amekaa pale.
“Kwa nini umenyamaza?”
Nikamwangalia.
“Nilikuwa naongea na mtu.”
“Na nani?”
“Na mimi mwenyewe wa zamani.”
Alicheka.
“Mimi sikuelewi, babu.”
“Utakuja kuelewa.”
“Lini?”
“Utakapokuwa mzee.”
“Na mimi nitakuwa mzee?”
“Ndiyo.”
“Na wewe utakuwa wapi?”
Swali lile lilinipiga kuliko maumivu yoyote ya mwili.
Nilimtazama bila kujua kama ningeweza kummaliza.
Nikanyamaza nisijue ninamjibu vipi.
Kwa sababu kuna maswali ambayo ukweli wake ni mzito kuliko jibu lake.
Nikageuka na kutazama dirishani tena.
Jua lilikuwa linazama.
Na nilijua kabisa kwamba siku moja, wala si mbali sana, jua lingezama bila mimi kuliona.
Nilikuwa nasubiri.
Sio wageni. Wala watoto.
Sio madaktari.
Nilikuwa nasubiri ule mwisho ambao kila mwanadamu huukwepa kwa maneno, huukimbia kwa mawazo lakini hawezi kuukwepa kwa vitendo.
Mwisho wangu.
Na pamoja na mwisho huo, kulikuwa na swali moja ambalo nilikuwa nimebeba maisha yangu yote:
Baada ya kila nilichofanya, kila nilichosema, kila nilichoandika, kila nilichojenga, kila nilichoharibu, na kila nilichopenda, nitakapofika mwisho, nitapokea nini?
Ahadi?
Au hukumu?
Nilifumba macho tena.
Safari hii sikutaka kuzungumza na mtu.
Nilitaka kusikiliza.
Kwa sababu kuna wakati katika maisha ya mwanadamu ambapo maneno yote huisha.
Na hapo ndipo ukweli huanza.
***********

Ule mwisho utakapofika...
Nilirudisha mkono wangu kifuani.
Moyo ulikuwa ukipiga taratibu.
Pigo moja. Puuuh!
Kimya.
Pigo lingine. Puuuh!
Kimya. Kisha mapigo mawili. Puuuh! Puuh!
Nilisikiliza.
Niliwahi kuandika kuhusu kifo mara nyingi.
Nilizungumzia kuhusu maisha kana kwamba nilikuwa nimeyamaliza.
Nilizungumza kuhusu mwanadamu, tamaa, upendo, mamlaka, fedha, ndoa, vita, Mungu, dunia, ujinga na hekima.
Lakini leo nilikuwa nimelala hapa, mzee, nikisubiri kile nilichokuwa nimekiandika kwa miaka mingi.
KIFO!
Nilicheka peke yangu.
Kumbe kuna vitu ukiviandika sana, siku moja vinakuja kukutokea na kuvitolea hesabu wewe.
Nilipokuwa kijana sikujua kwamba siku moja ningefikia umri huu. Nilijua nitazeeka. Lakini nilijua hivyo kwa akili tu.
Kama mtoto anavyojua kwamba shule ipo, lakini hawezi kufikiria siku atakayokuwa mwalimu.
Nilikuwa kijana. Nilikuwa na nguvu. Nilikuwa na muda. Na nilikuwa na kalamu.
Hiyo kalamu ndiyo iliyonifanya niishi maisha ambayo watu wengi hawakuyajua.
Ujana wangu mwingi niliutumia kuandika. Wakati wengine walikuwa wakitafuta burudani, mimi nilikuwa natafuta sentensi.
Wakati wengine wakitafuta pesa na utajiri mimi nilikuwa kwenye shimo la ufahamu.
Wakati wengine walikuwa wakilala, mimi nilikuwa najiuliza maswali ya hekima.
Wakati wengine walikuwa wakizungumza kuhusu maisha yao, mimi nilikuwa nikichunguza maisha ya wengine na matukio ya ulimwengu.
Nilikuwa naangalia watu wakigombana na kujiuliza:
Kwa nini mwanadamu hupigana na mtu anayempenda?
Nilimuona tajiri akimnyanyasa maskini na kujiuliza:
Kwa nini mali humfanya mtu ajione bora kuliko mwanadamu mwingine?
Nilimuona maskini akimchukia tajiri na kujiuliza:
Je, chuki yake ingeisha kama angepewa mali?
Nilimuona mtu akipenda.
Nikamuona huyohuyo mtu akisalitiwa.
Nikajiuliza:
Je, upendo ni udhaifu au ni ujasiri wa kukubali kuumizwa?
Nilikuwa na maswali mengi.
Na kalamu yangu ilikuwa mahali pa kuyaweka.
Sikuandika kwa sababu nilikuwa najua kila kitu.
La.
Niliandika kwa sababu nilikuwa sijui.
Kuandika kulikuwa njia yangu ya kuhoji dunia. Kuongea na dunia. Kufikiri na dunia. Kubishana na dunia.
Kila nilichoandika kilikuwa kama kuyaambia maisha:
"Hebu simama kidogo. Nataka nikuchunguze. Nataka tutete"
Nilikuwa nikikaa na karatasi mbele yangu kwa saa nyingi.
Baadaye teknolojia ikanifanya nikae na simu na laptop muda mwingi. Nikisoma na kuandika. Nikiperuzi na kupost.
Wakati mwingine nilikuwa naandika sentensi moja tu.
Nikiisoma. Nakuifuta
Naiandika tena.
Naitazama.
Kisha najiuliza kama kweli nimeeleza kile nilichokuwa nachotaka kusema.
Wakati mwingine maneno yalikuwa yakija mengi kiasi kwamba nilishindwa kuyaandika kwa kasi.
Wakati mwingine nilikaa mbele ya ukurasa mtupu kwa muda mrefu.
Ukurasa ule ulikuwa kama maisha.
Unaangalia mbele. Huoni kitu.
Lakini ndani yako unajua kuna kitu kipo au kinaweza kuwepo.
Na ndipo nilipojifunza moja ya hekima kubwa ya maisha:
Ukurasa mtupu haumwogopeshi mwandishi kwa sababu hauna kitu; humwogopesha kwa sababu unaweza kuwekwa kitu chochote ndani yake. Ndivyo sisi waandishi hofu yetu ilipo.
Maisha nayo yalikuwa hivyo.
Nilipoanza siku yangu, siku nilipozaliwa ukurasa ulikuwa mtupu.
Niliijaza kwa matendo.
“Babu?”
Nilifungua macho.
Mjukuu wangu alikuwa bado pale.
“Ulikuwa unaandika nini zamani?”
Nikatabasamu.
“Vitu vingi.”
“Vitabu?”
“Ndiyo.”
“Uliandika vitabu vingapi?”
Niliangalia upande wa pili wa chumba.
Kulikuwa na kabati lililojaa vitabu.
Baadhi vilikuwa vyangu.
Baadhi vilikuwa vya watu wengine.
Niliviona kama makaburi madogo ya mawazo.
“Siwezi kuhesabu tena.”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu nilipokuwa kijana nilikuwa nikihesabu nilivyoandika. Nilipokuwa mtu mzima nilianza kuhesabu nilichotaka kuandika. Sasa ni mzee, nahesabu yale ambayo sikuyasema.”
Mjukuu wangu akakaa kimya.
Kisha akauliza:
“Babu, uliwahi kujuta kuandika?”
Hapo nilijikuta Nacheka.
“Ndiyo.”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu wakati mwingine kalamu yangu ilisema ukweli ambao watu hawakutaka kuusikia.”
Nikavuta pumzi.
“Lakini sikujuta kuwa mwandishi.”
Nilimtazama machoni.
“Hilo silijuti.”
Nilipokuwa kijana nilidhani mwandishi anaandika vitabu.
Baadaye nikagundua mwandishi haandiki vitabu tu.
Anaandika ushahidi.
Anaandika historia. Anaandika kumbukumbu ya simulizi
Anaandika maumivu yake na yajamii. Anaandika mambo ambayo watu waliishi lakini hawakujua kuyaeleza.
Anaandika maswali ambayo watu waliogopa kuyauliza.
Anaandika mambo ambayo wengine wanayaficha.
Na wakati mwingine anaandika mwenyewe bila kujua kwamba anajiweka kwenye simulizi yake mwenyewe.
Niliandika kuhusu wazee.
Sikujua siku moja ningekuwa mzee.
Niliandika kuhusu vijana. Sikujua siku moja ningewatazama vijana kama ninavyowatazama sasa.
Niliandika kuhusu wazazi. Sikujua siku moja ningekuwa babu na watoto wa watoto wangu wangekuja kuniuliza kuhusu maisha.
Niliandika kuhusu kifo. Sikujua siku moja ningelala kitandani nikikisubiri. Hilo ndilo jambo la ajabu zaidi nililokuja kulielewa.
Mwandishi anaweza kutumia maisha yake yote kuandika kuhusu mwisho, bila kujua kwamba kila ukurasa anaouandika unamsogeza kwenye mwisho huo.
Nilikuwa naandika usiku.
Huo ulikuwa muda wangu. Dunia ikiwa kimya, ndipo mawazo yangu yalikuwa yakipiga kelele. Yakibisha katika ufahamu wangu.
Nilipenda usiku kwa sababu watu waliponyamaza, akili yangu ilianza kuzungumza.
Niliwahi kuandika nikiwa na furaha.
Niliwahi kuandika nikiwa nimekasirika.
Niliwahi kuandika nikiwa nimevunjika moyo.
Niliwahi kuandika nikiwa na matumaini.
Niliwahi kuandika nikiwa nimekata tamaa.
Lakini kila mara nilipoandika, nilihisi kama nimepunguza mzigo mmoja moyoni.
Ndiyo maana sikuacha.
Maisha yaliponipiga, niliandika.
Watu waliponielewa vibaya, niliandika.
Waliponielewa vizuri, niliandika.
Niliposifiwa, niliandika.
Nilipodharauliwa, niliandika.
Niliposhindwa, niliandika.
Nilipofanikiwa, niliandika.
Kumbe bila kujua nilikuwa nikihifadhi vipande vya nafsi yangu mwenyewe
Leo hii nikitazama nyuma, naona kijana yule alikuwa anajenga kaburi la kumbukumbu yake mwenyewe.
Kila kitabu kilikuwa jiwe.
Kila makala ilikuwa jiwe.
Kila sentensi ilikuwa jiwe.
Kila methali ilikuwa jiwe.
Na sasa nimefika mahali ninajiuliza:
Nani atakayezisoma baada yangu?
Mjukuu wangu aliniuliza:
“Babu, vitabu vyako vitabaki?”
Nikanyamaza.
Swali hili lilikuwa kubwa kuliko umri wake.
“Vitabu vinaweza kubaki.”
“Na wewe?”
Nikamwangalia.
“Siwezi.”
Akatabasamu kwa huzuni.
“Kwa nini?”
“Kwa sababu kila mwanadamu ana muda wake.”
Nikamshika mkono wake. Kisha nikanong'ona
“Usijaribu kuishi milele, mwanangu.”
Akanitazama kwa mshangao.
“Kwa nini?”
“Kwa sababu utashindwa kuishi leo.”
Nilimwambia:
“Watu wengi wanataka kuacha jina litakalodumu milele, lakini wanasahau kuishi maisha yanayostahili kukumbukwa.”
“vipi wewe ulitaka jina lako likumbukwe?”
Nilitabasamu.
“Nilitaka maneno yangu yawasaidie watu kufikiri.”
“Na kama wakikusahau?”
Nilikunja uso kidogo.
“Basi watanifanyia haki.”
“Haki?”
“Ndiyo.”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu hakuna mwanadamu anayepaswa kuwa kumbukumbu ya milele.”
Nilitulia. Kisha nikasema:
“Ukipata mtu aliyekusaidia siku moja ukamsahau, hilo si jambo baya. Cha muhimu ni kwamba msaada ule uliendelea kuishi ndani yako.”
Niligeuka upande wa kitanda. Mwili ulikuwa mzito.
Nilitazama mikono yangu.
Mikono hii ndiyo ilishika kalamu.
Mikono hii ndiyo iligeuza kurasa kuwa kitabu. Maneno kuwa makala.
Mikono hii ndiyo iliwahi kushika mikono ya watu niliowapenda.
Mikono hii ndiyo iliwahi kubeba watoto.
Mikono hii ndiyo iliwahi kufanya kazi.
Na sasa ilikuwa inatetemeka.
Nilijiambia:
Mwili una mwisho, lakini matendo yana safari ndefu.
Lakini hata maneno yanaweza kufa. Yanaweza kutoweka.
Hata vitabu vinaweza kupotea.
Hata jina linaweza kufutika. Na kusahaulika
Hata sanamu inaweza kuanguka.
Hata historia inaweza kubadilishwa.
Kwa hiyo, nilijiuliza:
Ni kitu gani mwanadamu anaweza kuacha ambacho hakifi kabisa?
Sikupata jibu mara moja. Baadaye nikagundua.
Mwanadamu huacha athari. Mtu anaweza kufa, lakini namna alivyomfanya mwingine ajione inaweza kubaki.
Unaweza kufa, lakini mtoto uliyemfundisha anaweza kuendelea kufundisha. Unaweza kufa, lakini wazo ulilopanda linaweza kuendelea kukua.
Unaweza kufa, lakini tendo lako moja la wema linaweza kubadilisha maisha ya mtu ambaye hata hukuwahi kumjua.
Hapo ndipo nilipoelewa:
Mwanadamu haishi kwa muda aliokaa duniani pekee. Anaishi pia kwa athari aliyoiacha baada ya kuondoka.
Mara nyingi wageni walikuja kuniona. Wengine walikuja kwa sababu walinipenda.
Wengine kwa sababu walikuwa na maswali na walihitaji majibu.
Wengine walikuja kwa sababu walitaka kusikia kutoka kwa mzee ambaye alijulikana kwa hekima.
Wengine walikuja ndio walikuja wale waliokuwa wakinichukia, wakiutazama mwisho wangu kama ushindi wao waliousubiri kwa miaka yao yote.
Na nilipofika umri huu, niligundua kitu. Mzee akikaa kimya, watu hudhani hana cha kusema. Nilikumbuka wazee wangu wakati nikiwa kijana. Nikaelewa. Lile swali nililowahi kuwauliza, mababu, Babu Heriel Chambua, Babu Furahael Tenga, Babu Clifford Tenga, Babu Robert Kalalu, na Mabibi zangu, Bibi Nasemba Tenga, Bibi Lightness Kalalu, Bibi zilpa Tenga. Na leo je?
Leo ni zamu yangu. Nami ni mzee
Majibu naenda kuyaandika. Kimya cha mzee...!
Lakini mara nyingi mzee anayekaa kimya ana historia ambayo haiwezi kusemwa kwa siku moja.
Nilikuwa nimeishi muda mrefu.
Nilikuwa nimeona watu wakija na kuondoka.
Niliwaona vijana waliokuwa na nguvu wakawa wazee.
Niliwaona matajiri wakapoteza mali.
Niliwaona maskini wakiwa dhalili wakainuka.
Niliwaona wenye kiburi wakinyenyekezwa na maisha.
Niliwaona wanyenyekevu wakifika mbali.
Nilijifunza kwamba maisha hayana tabia ya kubaki upande mmoja milele.
Leo unaweza kuwa juu.
Kesho unaweza kuwa chini.
Leo unaweza kucheka.
Kesho unaweza kulia.
Leo unaweza kuwa unayeshauri watu. Kesho unaweza kuhitaji ushauri kutoka kwa watu.
Usimdharau mtu kwa sababu yuko chini; hujui kesho yake.
Na usimwabudu mtu kwa sababu yuko juu; hujui mwisho wake.
Siku moja mwanamke mmoja mzee, rafiki yangu wa zamani, alikuja kuniona.
Akakaa pembeni ya kitanda.
Alinitazama kwa muda mrefu.
“Robert,” alisema.
“Naam.”
“Umechoka?”
Nikacheka. Huku nikimtazama.
“Umeniona?”
“Ndiyo.”
“Nimechoka.”
Kisha akaniuliza
“Unaogopa?”
Swali hilo lilinifanya ninyamaze.
Nilitazama dirishani. Mwanamke huyu niliyeishi naye tangu tukiwa vijana, alinifahamu kama kijana jasiri, nisiyejua kuogopa. Na nikiogopa basi hiyo ingekuwa ndani ya sinema tuu. Ndiye huyo Binti Kimoso. Mke wangu. Mwanamke wa zamani.
Yule mwanamke niliyemfanya kuwa wakipekee.
Macho yake yaliniangalia.
Kisha nikasema:
“Siogopi kifo kama ninavyoogopa kufika mwisho bila kuelewa nilichokuwa nikikitafuta.”
Alitikisa kichwa.
“sasa umeelewa ulichokuwa ubakitafuta?”
Nikatabasamu.
“kwa Sehemu.”
“Sehemu gani?”
“Kwamba maisha hayakuwa swali la mimi kuishi kwa muda gani.”
Nikavuta pumzi.
“Lilikuwa swali la nilifanya nini na muda niliopewa.”
Alikaa kimya. Nikaendelea:
“Nilipokuwa kijana nilitaka kujua maana ya maisha. Nilipokuwa mtu mzima nilitaka kubadilisha maisha. Sasa ni mzee nikagundua kwamba kwanza nilipaswa kuyakubali maisha jinsi yalivyo.”
“Na mwisho?”
“Mwisho ndiyo mwalimu mkubwa. Mwalimu mwenye upole anayefundisha mwanafunzi mwenye huzuni nyingi. Huzuni ya kuagana na wapendwa wake"
Usiku ulipoingia, nyumba ilitulia.
Nilisikia sauti za watu nje kama kawaida lakini haikuwa kawaida mwisho unapokaribia. Kila kitu huwa cha thamani mwisho ukifika"
Mtu moja akifunga mlango. Mwingine akizungumza kwa simu.
Watoto akicheka na kulia
Kisha kila kitu kikaanza kutulia.
Nilijua kesho kutakuwa na maisha. Watu wataamka. Wataenda kazini. Wengine watabaki nyumbani.
Wengine watapendana. Wengine watachukiana.
Wengine watazaliwa. Wengine watakufa.
Wengine wataandika.Wengine watasoma.
Wengine watajenga. Wengine watabomoa.
Dunia itaendelea.
Hilo ndilo jambo ambalo mwanadamu hulisahau: Dunia haikomi kwa sababu wewe umefika mwisho.
Nilifumba macho.
Niliona maisha yangu tena. Niliona ujana wangu.
Niliona kalamu yangu.
Niliona karatasi na vitabu.
Niliona watu.
Niliona makosa yangu.
Niliona mafanikio yangu.
Niliona wale niliowapenda.
Niliona wale niliowaumiza.
Niliona wale walioniumiza.
Na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, sikutaka kuhukumu yeyote. Nilitaka kusamehe. Hata kujisamehe mimi mwenyewe.
Kwa sababu niligundua kwamba mtu anapofika mwisho, huwa hana muda tena wa kubeba chuki. Chuki ni mzigo wa safari.
Na safari yangu ilikuwa karibu kuisha.
Nilifungua macho.
Mjukuu wangu alikuwa amelala kwenye kiti karibu na kitanda.
Nilimtazama.
Nikajiambia:
Huyu bado ana safari ndefu.
Nikafikiria mambo yote ambayo ningependa kumwambia. Lakini nikagundua kwamba siwezi kumwambia yote.
Kwa sababu baadhi ya hekima hazifundishwi kwa maneno. Zinafundishwa na maisha yenyewe.
Nikamnong'oneza:
“Usiogope mwisho, mwanangu.”
Hakunijibu.Aliendelea kulala.
Nikatazama dari. Moyo wangu ukapiga tena.
Pigo moja. Puuh!
Kimya.
Pigo lingine. Puuh! Kabla ya pigo la tatu;
Nikajiuliza:
Je, hili ndilo pigo la mwisho?Sikujua.
Kisha polepole, nikahisi miguu ikipotea katika mwili wangu. Ni kama haokuwepo.
Kisha kiuno na tumbo vikayeyuka.
"Kama huu ndio mwisho wangu. Nani atakaa pembeni yangu?"
Polepole nuru ya macho ikaanza kufifia. Sikujua kama ni Usingizi au ndio KIFO chenyewe.
Kifo yule Rafiki yangu wa zamani. Ambaye aliniahidi atakuja kunichukua.
Hatimaye kukawa giza. Kisha kimya.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa...!
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaa.