Sikujua kumpoteza Baba ni kugumu hivi

Sikujua kumpoteza Baba ni kugumu hivi

Tangu baba yangu afariki, ilinchukua miaka 15 maumivu kupungua........
Inauma zaidi ukipata matatizo unamkumbuka yeye ata kama hayahusiani...ukinyanyapaliwa unamkumbuka yeye........

Inauma zaidi kama aliwaacha hamna kitu....kama yeye ndo alikua tegemezi

Kama kila siku marafiki zake walikuja kumtembelea nyumbani...hutawaona tenaaaa...watakata mguu

Lakini atatokea rafiki yake mmoja atawasaidia mpaka meisho wa dahariii
 
Babangu alizaliwa tarehe 28/12/1958 na alifariki juzi tarehe 25/12/2017 kwa ajali.

Kwa hakika katika maisha yangu yote hili ni pigo la pili baada ya pigo la aliyekua mpenzi wangu lakini naona hili ni zito kuliko.

Siwezi kulala usingizi bila kulia katikati ya usingizi.
Siwezi kula bila kumfikiria na wakati mwingine hata chozi hunitoka.

Kwa siku hizi 5 tu Naona Dunia ni ngumu kuliko chochote. Niwaangaliapo ndugu zangu naona wao wana afadhali kuliko mimi. Najitahidi ku behave kama wao lakini nashindwa.

M/Mungu amrehemu baba yangu na kumpunguzia adhabu ya kaburi. Nimejikuta nataka kubaki kijijini ili nilione tu kaburi lake kila siku lakini inanibidi nirejee kwenye familia yangu.
Pole sana
 
Pole sana mwanandugu.
Sisi tu mavumbi na mavumbi tutarudi na kila nafsi itaonja umauti na kila aliyezaliwa na mwanamke naye atakufa.

Jitaidi kumwombea sana na wewe Umwombe Mungu akujalie kusahau na jitaidi kujiweka bize na usikae mwenyewe.

Poleni sana wanafamilia.
 
There are moments when troubles enter our lives and we can do nothing to avoid them.
But they are there for a reason. Only when we have overcome them will we understand why they were there.....Pole mkuu
 
Pole sana my dear

Maumivu ya msiba ayajuae mfiwa pekee. Msiba unauma sana tena sana hakuna cha kuulinganisha nao. Maumivu yake ni ya milele.

Unaweza onekana nje unatabasamu ila moyo unalia machozi ya damu na hata ukisema ulie nje bado watu watakusema unajiendekeza hakuna ajuae maumivu ya mtu kila mmoja ana maumivu yake kwa kipimo chake.
View attachment 663409 View attachment 663410
Nimechukua hizi article zako mpenz, [emoji120]
 
Babangu alizaliwa tarehe 28/12/1958 na alifariki juzi tarehe 25/12/2017 kwa ajali.

Kwa hakika katika maisha yangu yote hili ni pigo la pili baada ya pigo la aliyekua mpenzi wangu lakini naona hili ni zito kuliko.

Siwezi kulala usingizi bila kulia katikati ya usingizi.
Siwezi kula bila kumfikiria na wakati mwingine hata chozi hunitoka.

Kwa siku hizi 5 tu Naona Dunia ni ngumu kuliko chochote. Niwaangaliapo ndugu zangu naona wao wana afadhali kuliko mimi. Najitahidi ku behave kama wao lakini nashindwa.

M/Mungu amrehemu baba yangu na kumpunguzia adhabu ya kaburi. Nimejikuta nataka kubaki kijijini ili nilione tu kaburi lake kila siku lakini inanibidi nirejee kwenye familia yangu.
Pole dear ndiyo njia yetu sote hakika tutakufa tu.Hakuna njia nyingine tutakayopita kutoka hapa duniani zaidi ya kifo Muombe Mungu akupe faraja ya kipekee ila nawe ukijiweka tayari maana hatujui siku wala saa ya kifo.Mimi huwa najipaga moyo kuwa kama kuna kukutana na kukumbukana basi tutakutana na wapendwa wetu.Na mara nyingi napoaga mpendwa wangu nikifika pale kwenye Jeneza naangalia na moyoni nasemaga na mimi siku moja ntalala hapo.
 
Pole mnoo mamy naelewa sana maumivu ya kumpoteza mzazi Mungu akufanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu ulichonacho
 
Back
Top Bottom