DIAMOND:
@Officialbabalevo WEWE KUANA MWENZANGU NA NAHESHIMU NAFASI YAKO ILA UNAPOELEKEA. UNANILAZIMISHA KUKAA MBALI NA WEWE MAANA UNAFANYA. NIHISI KUNA AGENDA. NISIOLJUA UNANITENGENEZEA. @mbosso_ UNAHAKI YA KUTOPENDEZWA, KUCHUKIA NA KUREACT KWA NAMNA YOYOTE UNAYOHISI NI SAHIHI UNAPOKOSEWA ILA NAOMBA USINUJUMUISHE KWENYE UJINGA WA BABA LEVO NA NADHANI TUSHALIONGEA HILI SI MARA MOJA WALA MBILI TENA KWA USHAHIDI NA MIFANO. NAWAHESHINU NAOMBENI HESHIMUNI HESHIMA NINAYOWAPA, ILA KAMA MNA AGENDA NISIOIJUA KUPITIA KIVULI CHANGU, NA MIOYO YENU INAWAMBIA NI SAHIHI MNAYOYAFANYA, HAYA ENDELEENI
MBOSSO:
Mimi na Baba Levo Wapi na Wapi, Hatukutani , Hatufanyi Kazi Pamoja , hatushindi Pamoja na Wala Hatusafiri Pamoja .. Tusizunguke Mbuyu .. Mtu Pekee Wa Kumkanya Baba Levo ni Wewe Bro Sio Mimi.. Na Ukiamua Kumkanya Serious Ataacha Tu.. (nimetumia Neno Serious sio Kumkanya na baadae kwenda Kumchekea Kwenye Coment ig) Sijawahi Kukuvunjia Heshima Na Sitakuja Kukuvunjia Heshima .. Mchango Wako Kwenye Maisha Yangu Ni Mkubwa Mno nikisema Leo Nikukosee Hata Mwenyezi Mungu Hawezi kunibariki .. Heshima yangu kwako ni mpaka siku nakufa ..
DIAMOND:
Naona unalazimisha kuhitilafiana na mimi nikuongezee mwendo, okay wacha nikuridhishe...kwanza kabisa sikutaka mitandao nilikupigia simu na kukutumia messages na tulipokutana niliongea na wewe kwa hekima na ushahidi namna gani nimekua sipendezewi na nimekua nikimsema baba levo anachokifanya tena nikikuonesha kwa ushahidi na nikikuambia kuwa hakina faida kwangu zaidi ya kunitia tu ubaya!..lakini pia nilikuambia msanii anapotoka kwenye lebo usitegemee wote watakua na reaction za kufanana, wengine watakua na reaction mbalimbali, kuna wengine wanaweza wakawa wanareact vitu ambavyo sio vizuri kwa maumivu ya kukupenda tu kuona dah ndugu yetu kwaio katoka kwenye team...
Nikakuambia jitahidi kutumia busara maana hayo ni mambo ya kawaida na unapaswa kujua binadam wako hivyo usipokua makini utaona kila mtu katumwa na diamond then utaishia kunichukia na kugombana na mimi bila sababu...na nikakutolea mfano hai kua ata wewe alipotoka rayvanny ulikuja nyumbani kwangu na hasira kuniambia maneno kedekede ya kumchukia rayvanny na ulipinga kabisa nisifanye nae nyimbo ya “nitongoze” na wala nisishirikiane nae kwa lolote ... Nikakuambia hapana si vyema, mtu kutoka kwenye lebo sio uadui ni jambo la kawaida kuna time itafika ata wewe utapaswa pia kutoka kwa lebo kuanza maisha ya kujitegemea... Haikuishia hapo na kila nilipofanya nae bwimbo ulinuna na mara zote kuchukia kwanini nampasupport kazi zake!
Pili: baba levo nimtu mzima mwenye familia na watoto juu, hivyo ki hekima nina kiwango cha kumwambia kitu, anapoamua kuendelea inamaana hapo ni yeye kadhamiria na jukumu langu ni kuonesha sikubaliani nalo hadharani na akizidi kujiepusha nae , nandiomaana umeona nimefanya hayo kwa hekima ya kusema sina msemaji lakini pili yalipozidi nikamuambia ndugu yangu unalazimisha nikupunguze, unless otherwise ulikua unataka nimwamabie kwa userious gani labda nimpige makofi au nimpeleke polisi?.....
Tatu: nitakua ni mpumbavu kuamini ya kua kila analosema mwijaku katumwa na alikiba ama harmo kisa anafanya kazi nao ama wakati mwingine kusafiri nao. Nadhani point unayoificha ni kua vijana mkitokaga wasafi ata mfanyiwe wema gani mnapendaga kujitaftishaga vibifu ushuzi na kujitilisha huruma muonekane kama mnaonewa ili kupata vishabiki maandazi vinavyoichukia wasafi!
Kwenye maelezo yako unaforce kunijumuisha ukidai tunakuonea wivu... Yani mie nikuonee wewe wivu kwa kitu gani haswa...halaf mie itanisaidia nini haswa? Yani niache kupambana na harakati zangu za kuona natoboa vipi duniani nikae kitako nakupangia njama wewe? Yani kwa lipi labda?? Na kisha itanisaidia nini labda?? Nitake sifa kupitia pawa??? Pawa imehit kuliko nyimbo ya sele nchini? Je sele ulitandika pekeako? Uliona popote nimeenda kujisifu??
Hodari, nadekezwa, maajab, tamu, ova watakubali, tamba, moyo, sina nyota, baikoko, shetani, shida, assalaam, ulikua wapi, yataniua, yes, sonona, nimekuzoea, sina nyota...??? Takribani asilimia 90% ya nyimbo zako zote kama kuna nyimbo ambayo niliandika kwa kiwango kidogo basi labda asilimia 20% ila takriban nyimbo zako zote nimeandika kuanzia silimia 40% , 50% zingine nimeandika hadi asilimia 90% viitikio, verses, michezesho na kadharika na zilihit kila kona, wapi ushanisikia najisifiahilo?? Sanasana naonekanaga kama wewe ndio unaniandikia mie nyimbo wakati uhalisia mie ndio nimekuandikia nyimbo zako nyingi tena kuliko wewe ulizoshiriki kwangu...!
Umetoka wasafi licha ya sivakutoza ata shilingi mia nilikua nakudai milioni miatatu, ishirini na tatu na laki mbili na hamsini (323, 250,00/=) ya kukukopesha toka mfukoni mwangu... Na vyote nilikuachia nikakuambia mdogo angu huo ni mchango wangu kwako kaanzie maisha... Then unasema nakuonea wivu, kisa kitu gani asa ep? Ep ya bongo fleva, nyimbo ambazo zimejaa ndani kwangu kibao sitaki kuzitoa kwakua hazitakua na msaada kimataifa naishia kugawa nyimbo na kuwaandikia watu...
Au wivu wa nini labda pawa? Pawa ambayo kila anaepost anapost kipande changu? As matteer of fact ngoma ya pawa si tulitfanya ukiwa ushatoka lebo wasafi, kama ningekua na roho mbaya studio si ningejikausha tu, but niliona nyimbo haiko sawa nikaamua kusaidia upate ngoma kali ikafanye vizuri, na situ melody na maneno juuv!...je chorus yako ya pawa ulikua unaimba vile? No! Nikakusaidia kutengeneza chorus itayohit na kuingiza sauti juu
umekamilisha ep umekuja home tunashauriana namna ya promotion, logo ya khan music, tareh ya kurelease ep, media coverage na kila kitu ili nawe ep yako ikafanye vizuri, leo ukaseme nakuonea wivu yani nilikua na sababu ipi ya kuweka mawazo yangu kwenye ep ikiwa ushatoka wasafisasa, au nakuonea gere yani kwa hit hit ipi labda unayofikiri wewe ilohit kuliko komasava, wah, inama, baba lao, number one, jeje, african beauty etc...!
Achana na mabongo fleva ya kina mbagala, ukimuona, zuwena, sikomi yenye maviewers ya mpaka milioni 70 youtube, makolabo from yope, love you die, tetema, enjoy etc? Yani nikuonee wivu kwa kipi labda ambacho mie nakitamani kwako?? Mziki ni safari ndefu mdogo angu usikubali kupumbazwa na wajinga ukagombana na watu wenye upendo wa kweli kwako na kukupambania pindi wengi hawakuthamini!...si walikua wanakukataa na kusema huna uwezo kipaji anacho aslay na daftari kaondoka nalo, leo umekua wa maana sana eeh? Jifunze kuijua dunia na watu wake! Jifunze kujua wanafiki na watu real kwenye maisha!
Nimeamua maisha ya kukaa kimya ata panapokua na uongo wa kias gani unaenezwa dhidi yangu, hivyo naombeni niacheni nibaki kwenye mstari huo! Msinichokoe!w".... Kwenye hii tasnia sidhani kama kuna mwanamuziki aliesaidia wanatasnia mmoja mmoja kunizidi mimi, kuanzia wenye ukaribu mpaka wasio na ukaribu, kuanzia maisha binafsi hadi kazi...... Wanaomba misaada kwa siri nawasaidia wakifika kwenye hadhara wanatakaga kuonekana wao wako against na mimi ili kuwafurahisha maadui zangu, then naambulia kulipwa kutengenezewa chuki, unafiki, uongo wa kila namna ilhali mimi ndio nawasaidia wao...
Kwakua mwenyez mungu kanijalia busara, naamuaga vyote kuviacha tu na kuwapa nyie ushindi ili muonekane nyie ndio wema, nyie ndio mna roho nzuri, mimi ndio mbaya, nina roho mbaya, nawafitini na mabaya yote!!! Vyote hivyo nimeamua kuvipokea na kuamua kudeal tu na maisha yangu, sasa ombi langu... Jitahidini walau kuheshimu kukaa kimya kwangu! Maana ninapoelekea ntaonge vitu ambavyo hamtopenda jamii na watu wenu wavijue!
LAST AND NOT THE LEAST! SITAKI SHUKRANI, CREDIT WALA HESHIMA YA MS*NGE YOYOTE! KWENYE CHOCHOTE! ILA TU ONYO! NATUMIA HEKIMA, BUSARA NA UVUMILIVU MKUBWA KUJIEPUSHA KWA KUKAA KIMYA NA KUAMUA KUDEAL TU NA MAMBO YANGU!...HIVYO MNAPOONA NIMEKAA KIMYA NAOMBENI JITAHIDINI KOHESHIMU UKIMYA WANGU!" MAANA MIE NIMWEHU KWELIKWELI NA SINAGA HABARI UJUE! NA SIO LEO TOKEA ENZI ZA MAGAZETI YA SHIGONGO, ASK ABOUT ME!!!
MBOSSO:
Kaka yangu mpendwa ..., Ukipata wasaa Soma andiko langu la Jana Kuhusu BABA LEVO kwa utulivu na umakini sana bila hata KUPANIC nakuomba soma tena kwa Utulivu na umakini sana bila kupanic.. Utanielewa vizuri sana Mdogo wako..
Sijawahi Sema unanionea Wivu wala Siwezi Sema Unanionea Wivu.., Wewe ni msanii Mkubwa sana kwangu na ni kiongozi bora kwenye safari yangu ya Mziki hadi Mimi kuwa hapa.. Unionee Wivu Kwa haka ka Ep Kamoja au Kawimbo ka moja ambacho kitapita msimu wake na Nyimbo Nyingine za Wasanii Wengine zitakuja na zitafanya vizuri ..? Umenizidi Kila kitu how come unionee Wivu, Umekuwa msaada Mkubwa kwangu vipi unionee Wivu .. ..? Haiwezekani na Najua hauna Roho hiyo ..
Hizi kauli za Wivu Zinazojijenga kwako ni Nguvu ya Shetani anayetaka Kukufanya unichukie na unione nimebadirika na Pengine uniweke Kwenye upande wa Adui Kwako “Wakati adui alolijenga hili amekaa pembeni anatutazama huku akitabasamu .. Mimi ni Yule Yule Mdogo wako Mbwana Yusuph Kilungi ambae Nimekuwa mtiifu Kwako Kwa Miaka Yote Tangu unijue .., Ulishiriki Sehemu kubwa ya kazi zangu na Kwenye Kila Jambo Lako nilishiriki Kwa Kujitoa Kwa asilimia 100 .. Pengine sio kwa kipato ila kwa nafasi Yangu uliyonipa uliona kujitoa kwangu kwako na kwa Wasanii wenzangu ..
“Ukiwa Msanii Wa Wasafi ni Kawaida Msanii kuadika wimbo wake Mwanzo mwisho yeye mwenyewe na kuuleta kwako kwa ajili ya marekebisho.. kwa sababu Ww ni kiongozi, Muandishi mzuri sana na mzoefu kuzidi mimi.. hukufanya hivyo kwangu tu ni kwa wasanii wote wa wasafi wazamani hadi wa sasa .. Kwa sababu lengo ilikuwa kupata kitu kizuri kwa faida ya msanii na label pia . Kwa njia rahisi maana Yake umeshiriki Kwenye Kazi zangu Zote, na wasanii wenzangu wote tuliokuwa wasafi Binafsi nashukuru Sana
Nasisitiza Kama nilivyosema Kwenye Post Yangu Ya Jana Sijawahi kukuvunjia Heshima , na sitakuja kukuvunjia Heshima.. Mchango Wako kwenye maisha Yangu hi Mkubwa Mno Nikisema Leo nikukosee Hata Mwenyezi Mungu haiwezi kunibariki
Nimekuwa nikikutafuta mara kwa mara kukusisitiza Umkanye Baba Levo Na jibu lako unanambia mdogo wangu mpotezee , nimpuuzie nilikuwa nakuelewa ila Sasa ni Too Much na Je, Ulikuwa unashindwa nini Kumwambia Tu Akaacha Hizi Drama ..? Kwamba hakusikilizi hata wewe Boss wake ..? Post zako za Leo zinakaa Vibaya sana na utafanya watu wataamini ni kweli ulikuwa unamtuma .. Na mbaya zaidi unaonekana kama una vitu kwa muda mrefu moyoni ila hukupata nafasi nzuri ya Kuvitoa .. Sababu tumepigishwa shot UMEPANIC .. UKaona nafasi Ndo Hii
Kukuaminisha kuwa mm ni mwenye heshima kwako hautaona post Yangu au Kusikia sehemu Yoyote Nikisema au kuorodhesha idadi ya Nyimbo zako nilizowahi kuhusika Kwenye Uwandishi au Kuchangia Melodies au Mawazo Yoyote Bro wangu .. Ulikuwa unaniita tangu Nipo ya Moto Band na kuja kwako na wakati mwingine Studio kushiriki uwandishi wa kazi zako .., (nitaishia hapa) Na Baada ya kuingia wasafi , kazi za wasanii wenzangu wa wasafi , Ep na Album nilizoshiriki Kuandika au mawazo yangu .. Sito Taja Orodha Na sio Hizo hata Ambazo nilishiriki Kuandika na wakaimba wasanii Wenzangu wasafi .. Sitataja Orodha hata wimbo Mmoja Kaka Yangu wa #Wasafi sitotaja NAKUAHIDi Sababu nakuheshimu na nathamini Mchango wako Kwenye Maisha Yangu .. ni mkubwa mno kuzidi haya mambo yakusaidiana wimbo.. Heshima Yangu Kwako ni Hadi Siku Nakufa Wallah
Kuna siku itatokea haina jina .. utakaa Ukiwa Peke yako Kaka yangu Utatafakari na utapata jibu kuwa matatizo haya yote sio Mimi .. “Tatizo ni Kijana wako Huyo.. “
DIAMOND:
MDOGO ANGU ACHA KUZUGA HILILA LEO SI NDIO ULIKUA UNALITAKA, OKAY NIMEKUPA KATENGENEZEE ELA....NISHAWAZOEA NYIE WASANII HAMNAGA JEMA ATA MFANYIWE NINI, MKISHATOKAGA WASAFI TU AKILI ZENU ZINAWAMBIA SASA KINACHOFATA NI KUANZISHA UADUI NA WASAFI, KUJITILISHA HURUMA ZA KINAFKI KWA WATU KAMA VILE MNAOEWA KUMBE LENGO NI KUTAFTA TU KIBIFU NA DIAMOND ILI KUPATA TREND ZA KIJINGA ZA KUSHINDANISHWA NA DIAMOND !... NDIOMAANA KWENYE KILA JAMBO UNAKAZI YA KUNIJUMUISHA MIMI TU, DIAMOND, DIAMOND, YANI KILA NINAVYOJITAHIDI KUKUONESHA TENA KWA USHAHIDI KUWA SISAPOTI HUO UJINGA UNAOFANYIKA NA KUYAKEMEA HADI HADHARANI, WEWE BADO UMEKAZANA TU DIAMOND DIAMOND... YANI MIE NIACHE KUFOCUS NA NATOBOAJE DUNIANI NIFOCUS NA WEWE, HIVI UNAWAZA SAHIHI KWELI?
MARA SJUI NAZUNGURUKA MBUYU, MARA NATAKIWA KUMKANYA, YANI KUMKANYA BABA LEVO NILITAKIWA NIMFANYAJE LABDA KWAKO WEWE NDIO IMEKAA KUMKANYA? NIMPIGE BUNDUKI AU? NIMPELEKE POLISI AU NIMCHAPE FIMBO AMA!?? BABA LEVO NI MTU MZIMA MWENYE FAMILIA NA WATOTO JUU, HIVYO KI HEKIMA NINA KIWANGO CHA KUMKATAZA JAMBO , ANAPOAMUA KUENDELEA KUFANYA INAMAANA HAPO SASA KADHAMIRIA YE MWENYEWE NA JUKUMU LANGU NI KUONESHA SIKUBALIANI NA HILO, TENA HADHARANI...NA NDIO SABABU YA KUWEKA POST YA KUWA “SINA MSEMAJI, MSIAMINI LOLOTE ANALOSEMA MTU KUHUSU MIMI KAMA SI MIMI” ....AKIZIDI INANIPASA KUEPUKANA NAE NA NDIOMAANA NILIPOONA MAMBO YA JANA NILIMUAMBIA KWAMBA KWANINI UNALAZIMISHA NIKUPUNGUZE, SASA SIJAJUA WEWE MWALIMU WA NIDHAMU ULIKUA UNATAKA NIMWAMBIE KWA USERIOUS GANI LABDA NIMTEKE AU NIMRUSHIE BOMU? ACHENI KUTAFTA HURUMA ZA KINAFKI NA TRENDY ZA KIPUUZI MTANDAONI, MAISHA NI SAFARI NA HAUJUI NANI ANAWEZA KUFAA KESHO!