- Thread starter
- #81
Habari zenu wakubwa. Shikamooni. Nimekaa kimya kwa mda wote huo ni kwasababu sina simu. Nimemsubiri aliyenayo ndo nimeweza kuingia internet. Kiukwel mwaka jana nilisoma QT na mungu akajaalia kufaulu. Hivyo mwaka huu ninatakiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne. Nimeshindwa kujisajili kutokana na shida kadhaa zilizotokea baina yangu. Mtu niliyekuwa namtegemea tayar ameshatangulia. Hapo awali ktk post yangu hapo juu niliandika kuwa naenda kulipia nikiwa na ref no pamoja na form ya matokeo ya QT. Ni kweli ila nimefanya makosa kwa kufikiri kuwa natumia reference ile ya form two kumbe sivyo inatakiwa nilipie tena centre ili nipate reference no nyingine. Samahani kwa wote, nimepata maelekezo haya zaidi baada ya kuongea na mmoja kati ya walimu na kunipa maelekezo kwa undani.