Habari za asubuhi, ni siku nne tu ndizo zilizobakia. Kiukweli inaniathiri kwa mawazo niliyonayo. Nimesoma kwa shida hapo awali na leo mwishoni nafikia kukata tamaa kwa kukosa kulipia mtihani. Tarehe 31 ndio mwisho wa kulipia. Sijui nini hatma yangu kiukweli. Wapo walioniambia najidhalilisha na wapo waliotaka niwape reference no lakini kimya mpaka leo. Wacha nijidhalilishe kwakuwa ni mhitaji kweli. Na laiti ningekuwa wa kudanganya nisingekuwa naendelea kujidhalilisha kama wengi wasemavyo. Nina shida kweli ndugu zangu. Endapo nikishindwa kati ya siku ya leo au kesho, sitaweza tena. Nawaomba kwa dhati ndugu zanguni... Nawaomba sana.