Sifikiri kama ni mara ya kwanza

Mkuu, tatizo sio kwamba ulikuwa unatania, tatizo ni mipaka ya huo utani. Jukwaa la jokes sio leseni ya kuwabeza au kuwadharau watu.

Umesema ulikuwa utani, sawa. Lakini kama uliwakwaza watu kiasi hicho, badala ya kushangaa β€œkwa nini povu?”, jiulize kama utani wako haukuvuka mipaka.

Na kujitetea leo kwa kusema β€œnilikuwa natania” hakubadilishi maneno uliyoyaandika jana. Si kila kinachoitwa utani kinakosa madhara. πŸ˜…
 
Niweke sawa , sijitetei kwa lolote , wala sina wakuomba msamaha hapa , dhumuni langu ni jokes tu kama nilivyo ponda masela wenye vitambi pia πŸ˜…
 
Kesho ngoja nilete bonge la Uzi unaokataa mazima uwepo wa mademu wakali humu.

Demu atakayeubishia Uzi wangu sharti awake picha yake mjongeo na atuambie mahala anakokaa, la sivyo hoja yake ni batili.

Aidha, hao ambao hutokwa na povu waje na uthibitisho wa wazi unaonesha kama JF kweli Kuna pisi Kali.
 
Ni udikteta wa ajabu sana kwamba unapaswa kudai eti ni wazuri πŸ˜ƒ nasoma mapovu yao nawaona wajinga tu
 
Ni udikteta wa ajabu sana kwamba unapaswa kudai eti ni wazuri πŸ˜ƒ nasoma mapovu yao nawaona wajinga tu
Halafu wanatoa povu nasikia ni wa kiume. Hii ndo kusema kuwa nao ndio wale watembeao na vioo kwenye mikoba?! πŸ€”
 
Niweke sawa , sijitetei kwa lolote , wala sina wakuomba msamaha hapa , dhumuni langu ni jokes tu kama nilivyo ponda masela wenye vitambi pia πŸ˜…
Sawa mkuu, kama ulikuwa unatania hakuna anayekulazimisha kuomba msamaha. πŸ˜… Hoja yangu ilikuwa tu kwamba jokes nazo zina mipaka. Kumponda mwenye kitambi ni utani unaomhusu mtu binafsi, lakini unapolenga kundi zima na mwonekano wao, ni kawaida baadhi ya watu kuuchukulia kama dharau.
 
Yeah nakubali mno , ila niliyotoa ni maoni yangu tu, na kimantiki vita yote ni kupingana na maoni ambayo ni mali ya mtu binafsi , ndio maana nikabaki kimya kuhesabu idadi ya wapumbavu tu
 
Niweke sawa , sijitetei kwa lolote , wala sina wakuomba msamaha hapa , dhumuni langu ni jokes tu kama nilivyo ponda masela wenye vitambi pia πŸ˜…
Ushawakojoza wadada wa JF bhana, hakuna cha jokes wala nn 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…