KISA CHANGU: Mara ya kwanza kuvuta bangi nilienda kumuomba ushauri mwalimu kuwa nataka kujiua

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
479
665
JF salaam,

Ni miaka takribani 17 tangu kituko hiki nikifanye nikiwa O Level kweli bangi inawenyewe. Nikiwa na marafiki zangu watano mi nikiwa 6 kati yao wa3 walikuwa wanakula bangi na darasani wanafanya vyema sana yaani tano bora muhimu wawemo.

Hili lilitufanya tuwaze sana na jamaangu wa karibu sana tumuite Mr cobra. Japo class hatukuwa wabovu kivile
lkn kilichokuwa kinatuuma ni sisi kuwa mbali na kushika no mbaya darasani tofauti na wao ambapo mara zote kujisomea tulihusika pamoja nao kila leo na kila kipindi.

Ni kipindi kimoja tu ndo hatukuhusika nao wale jamaa yaani wakienda kuvuta bangi. Japo kuna muda walikuwa wanavuta tukiwa pamoja hasa usiku nk.

SIKU NAVUTA BANGI MIMI NA MR COBRA

Basi baada ya kuwaza sana na mbele yetu kulikuwa na mitihani inakuja ilibidi sasa nasi tuvute. Mr cobra alinambia kama ukoo wenu hakuna wavuta bangi utawehuka lakini sikuzingatia hilo.

Yeye alisema kwao wavuta bangi wako hivo sio issue, muda ukafika tulikuwa class mida ya lunch
tukatumia muda huo kwenda kutimiza azima yetu. Wenyeji wetu wakatuelekeza namna ya kuiandaa wakituambia hakikisha mbegu haibaki hata moja.

Waliona tunachelewa jukumu wakalibeba wao kuandaa iliandaliwa kama misokoto3 mikubwa halafu huko mbele umevimba kama mwanamke mwenye mimba.

Fegi likawashwa na mwanetu mmoja akavuta kama pafu mbili hivi akanipatia. Vile navuta pafu la kwanza sikuona shida yoyote ile nikapiga pafu kama 4 ndipo nikaona naanza kuzunguka.

Nikiwaangalia jamaa zangu nawaona wananizunguka nikaamua kukaaa chini kwa muda. Baada ya dk kadhaa nilianza kucheka sana kwa sauti kubwa , jamaa zangu kuona nacheka wao nao wakaanza kucheka hapo sasa walinipa kampani ya kucheka kidogo nijikojolee kwa kicheko.

Muda kidogo tukaenda darasani lakini ardhi nilikuwa naiona kama imeumka yaani iko juu hivyo tembea yangu
ilikuwa tofauti sana natembea nanyanyua mguu nyuzi90 wenzangu mbavu sio zao wanacheka mbaya hasa wazoefu wetu. tukaingia darasani niakenda kukaa nyuma kabisa muda huo nimetafuna iliki na big g baada ya kukaa ulinipitia usingizi mzito sana.

Nikiwa nimelala fofofo darasdani nilishitukia nacharazwa kiboko mgongoni na mwalimu. Nilimind sana yule ticha. Nikachukua begi langu bila kumuongelesha kitu chochote nikaenda hadi ofisini kwa second master wetu alikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana.

Aliponiona nalia kitu ambacho hakuwa kuniona aliniuliza salama? Nikamwambia hapana nimepigwa kiboko na mwalimu fln nimekuja KUKUOMBA USHAURI NIKAJIUE.

Mwalimu alishituka sana nakuogopa mno akampigia Hmaster akaja waakanzqa kunihoji nikatoa sababu hata hazieleweki. sababu pekee niliyotoa na iliyoeleweka nikupigwa wakati mimi naumwa kichwa na ninaumwa kizunguzungu.

Mwalimu akaitwa aliyenipiga akahojiwa na akaambiwa anaona bora akajiue. Mwalimu alijitetea kama mtoto mdogo. Jamaa yangu mmoja machale yakamcheza ikabidi aje ofisini na kuwaomba walimu aongee namimi faragha kweli tukatoka nje. Tulipofika nje aliuliza moja oyaah umetuua kwa maticha au? Nikamwambie waaambie twende geto nikalale kwanza nahisi kizunguzungu. Mwalimu akawasha pikpiki yake haoo hdi geto.

Muda sio mrefu wahuni wenzetu wakaja wanacheka mbaya, japo mwalimu aliendelea kuwa karibu sana na mimi akiniona sina furaha tu lazima aniite ofisini kwakwe, kuhusu Mr cobra nitaandika kwenye comment

Mwisho: huo ndo ulikuwa mwanzo na mwisho wa kuvuta bangi.
 
_20240303_235638.JPG
 
Mr Cobra yeye hakupatwa na manyanga mengi sana kama mimi , yeye alipoona imepanda alitoroka hadi akaenda kwenye geto lake ila akiwa njiani akiri ilimtuma avue nguo zake ili awe mwepesi akabaki kwenye pensi pekee hadi geto

Muda huo jasho kali likimtoka alipofika akatupia mlangoni nguo zake za shule na kuuchapa usingizi balaa
 
Aina hii ya Vijana, Wana Mchango Mdogo Sana Katika Taifa

Rest Easy Mwendakuzimu Jiwe

Hii Nchi ina vijana vya hovyo sana aisee
mkuu hayo ni mapito tu na ulimbukeni , nilitokako huko. cha ajabu jamaa yetu mmoja saivi ni dr mzuri tu na bado anavuta kila tukikutana ananikumbusha hata leo kanipigia simu ndo nikaleta na huu uzi hapa

mwinine ni mwalimu wa science mzuri yule wa3 pamoja na mr cobra sijui hata walipo hadi leo
 
Hongera kwa kuamua kuwa Huru kuliko Freeman. Maana Truth is the only option to Original freedom.

Hao wanaokuzomea nadhani Kuwa muwazi kwao ni msamiati mgumu. Mimi ninachojua washkaji wengi na marafiki zetu wamegawanyika ktk magroup mawili tuu makubwa.

Wanaokula ganja huwa so direct and Real men, ila wasiokula ndio wengi huingia kwenye magriup yale yanayolalamikiwa.. mfano anaesnitch wenzie, mnafiki, mchawi, mwongo, mwizi, msaliti nk.

Ninafungua mlango wa kukosolewa kwa ushahidi na utafiti. Ktk hii fact yangu.
 
Hongera kwa kuamua kuwa Huru kuliko Freeman. Maana Truth is the only option to Original freedom.

Hao wanaokuzomea nadhani Kuwa muwazi kwao ni msamiati mgumu. Mimi ninachojua washkaji wengi na marafiki zetu wamegawanyika ktk magroup mawili tuu makubwa.

Wanaokula ganja huwa so direct and Real men, ila wasiokula ndio wengi huingia kwenye magriup yale yanayolalamikiwa.. mfano anaesnitch wenzie, mnafiki, mchawi, mwongo, mwizi, msaliti nk.

Ninafungua mlango wa kukosolewa kwa ushahidi na utafiti. Ktk hii fact yangu.
Ahante mkuu tulivuka hatua hiyo
 
Back
Top Bottom