Sifa wanazopewa viongozi hawastahili ni wajibu wao kutekeleza wanayoyafanya, siasa ni mchezo mchafu umejaa laana, unyanyasaji na dhulma

vanus

JF-Expert Member
May 27, 2017
1,158
2,864
Afrika ni bara lenye laana, limejaa watu wa ovyo sana haswa hawa wanaojiita chawa.

Imagine unapambana usiku na mchana unatengeneza pesa alafu una-mteua mtu asimamie mali na pesa zako na unamlipa mwisho wa mwezi.

mtu huyo anaenda dukani anakununulia kiatu kwa pesa zako, kwa upumbavu ulionao kichwani unaanza kuruka kwa vigelegele nderemo na vifijo na kumpa sifa ambazo hakustahili

yeye ndie alibidi akusifu wewe kwa kuwa na uwezo wa kuchapa kazi, kutengeneza pesa, kumteua yeye azisimamie na kumlipa mshahara kwa mwezi.

Mbaya zaidi tukaona mambo hayaendi sawa, tukaamua kumtea mtu mwingine wa katikati kwa ajili ya kutusemea na kutuombea pesa zetu.

Yaani mtu ambae nimemteua kwa ajili ya kusimamia pesa na mali zangu, ameshindwa kutekeleza wajibu wake kwa wakati inabidi nimtafute mtu mwingine wa kunisemea, kuniombea pesa zangu.

Mtu huyu wa kunisemea nina mlipa mshahara ambao unazidi kipato changu, posho na mshahara vinamlewesha anaungana na mkubwa kuendelea kutafuna jasho langu kwa kutembelea gari za kifahari pasipo umuhimu wowote.

cha kusikitisha zaidi wanatengeneza nguvu kazi, vijana machachari walio feli darasani na kuwapa mafunzo makali ili kuja kutunyanyasa, kutupiga virungu kwa kutetea haki zetu na ufujaji wa pesa za wavuja jasho

Viongozi inabidi watuombee kwa Mungu tuishi maisha marefu, wapambanaji, wavuja jasho, bila sisi wasingeishi maisha ya kifahari na kutunyanyasa.

Wasingeweza kuwapeleka watoto wao cambridge schools wakati wa kwetu wakisoma shule za kajamba nani.

Afrika tuamke, hakuna kiongozi ambae anabeba box marekani wala ambae anakoroga zege mtaani kuongeza pato la taifa, ni sisi wananchi wavuja jasho lakini hatujipongezi sisi, tunawapa sifa watu ambao tunawalipa mwisho wa mwezi.
 
Back
Top Bottom