Kuna jambo ambalo mwenzenu linanitatiza kwa kweli na hapa nahitaji ushauri wenu.
Jirani na mahali ninapoishi amehamia dada mmoja mwanajeshi, na nyumba anayokaa imezungushiwa ukuta na ina nafasi ya kutosha watoto kucheza hata mpira, sasa huyu dada kaanzisha darasa la kufundisha watoto kucheza KARATE wakiwemo mabinti wa hapa mtaani kwetu.
Awali mimi sikujua kama huyo dada Mwanajeshi anafundisha mazoezi ya kucheza KARATE hivyo mama Ngina aliponiomba ruksa kwamba anataka kujiunga na mazoezi ya kujenga afya nilimkubalia bila kinyongo maana mimi ni mpenzi sana wa mazoezi ya kujenga afya na huwa namsisitiza tuwe tunakimbia uwanjani pamoja lakini akawa hataki, sasa baada ya kuniomba kwamba anajiunga na darasa na maozezi ya kujena afya nikamkubalia, lakini jana nimerudi mapema kutoka kazini nikasikia kelele zinazofanywa na wacheza karate hapo kwa huyo jirani yetu nikaona nifanye udadisi ili kujua ni kitu gani kinaendelea, nilipochungulia getini nikamuona mama Ngina anajifunza kucheza KARATE, nikashangaa kweli.........
Aliporudi nyumbani nikataka kumuuliza lakini moyo wangu ukasita. Ukweli ni kwamba mimi na mama Ngina huwa tunatofautiana, lakini hatujafikia hatua ya kushikana zaidi ya kupishana lugha. Sasa kwa kitendo chake cha kujifunza hayo makitu ameniweka roho juu maana nachelea siku tukitofautiana anaweza kunipa za uso......
Hebu nishaurini nimkataze kucheza hayo makitu au nikae kimya nimuache aendelee kujiweka fit........