UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 30
- 25
LICHA ya kuwapo kwa maofisa wa Serikali wenye dhamana ya kulinda ustawi wa watoto kikatiba, kisheria na kisera, idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi mkoani Shinyanga inaendelea kuwa kubwa.
Uchunguzi wa Nipashe uliofanyika kwa takriban miezi mitatu umebaini kuwa watoto wengi wamekimbilia kuishi mitaani wakitafuta riziki, huku wengine wakiacha shule na kuzima ndoto zao kutokana na kukosa mahitaji ya msingi kutoka kwa wazazi au walezi wao, yakiwamo chakula, mavazi na vifaa vya shule.
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, kupitia vifungu vya 6(1)(d), 7 na 9, inasisitiza haki ya mtoto kulelewa na wazazi wake, kupewa jina na utaifa, pamoja na kupata mahitaji ya msingi ikiwamo chakula, malazi, mavazi, matibabu, chanjo, elimu na haki ya kucheza na kuburudika.
Hata hivyo, utekelezaji wa vifungu hivyo mkoani Shinyanga umekuwa changamoto, hali iliyosababisha watoto kukosa haki zao za msingi ikiwamo malezi na elimu, na wengine kukimbilia kuishi mitaani katika maisha ya dhiki.
Sheria hiyo inaelekeza wazi kuwa wazazi na walezi wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanapata haki zao zote, ikiwamo kupelekwa shule, kufuatiliwa mienendo yao na kupewa malezi bora.
Mtoto Baraka Jonas (11), mkazi wa Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, anasema wazazi wake walitengana akiwa mdogo na hakuwahi kuandikishwa shule. Anasema baada ya kuishi na baba yake bila kutimiziwa mahitaji ya msingi, aliamua kukimbilia mitaani akiona ndipo kwenye usalama kwake.
Mtoto mwingine, Inno Abubakari (10) wa Kitangili, anasema anaishi na babu yake asiyejiweza na hajawahi kupelekwa shule, na hivyo ameamua kuishi mitaani ili kujitafutia mahitaji yake.
Anasema, Babu yake hajiwezi, hivyo yeye ndiyo anamlea, ambapo akipata chochote mtaani anampelekea na maisha yanaendelea.
“Mimi nimezoea kuishi mtaani, napata chochote kuliko nyumbani ambako hakuna hata chakula, ila nikipata huku chochote nampelekea na Babu yangu” anasema Inno.
Naye Abubakari Shabani (10), mkazi wa Busulwa, anasema alikatisha masomo akiwa darasa la tatu kutokana na kukosa mahitaji ya shule baada ya kuishi na shangazi yake.
“Napenda kusoma ili nitimize ndoto ya kuwa mwalimu, lakini nimeshindwa kutokana na njaa na kukosa mahitaji ya msingi ya shuleni” anasema Abubajari.
Mzazi Halima Nziku, anasema ugumu wa maisha ndiyo una changia kushindwa kuwalea watoto wao katika misingi bora, na kushindwa kuwatimizia mahitaji ya msingi ikiwamo elimu.
Anasema, wanafahamu kuwa jukumu la kumlea mtoto nila mzazi, lakini kutokana na ugumu wa maisha wanashindwa kutekeleza wajibu wao kwao, na kuwaacha wakajitafutie ridhiki wenyewe huko mitaani.
“hakuna mzazi ambaye anapenda mtoto wake akaishi huko mitaani ni ugumu tu wa maisha,” amesema Halima.
Nkwangu Madelanha, na Bibi ambaye ametelekezewa mjukuu na mtoto wake na hajui alipokimbilia, na kwamba hua hamtumii hata hela ya matunzo.
Anasema, kutokana na kuwa na hali duni ya maisha, ili mlazimu kumuacha mjukuu wake aende mitaani kutafuta ridhiki na mahitaji yake mingine.
“Mimi nimemaliza nguvu za kufanya kazi sinauwezo tena, sasa huyu mjukuu wangu nitamleaje, na sina hela ya kumnunulia mahitaji ya shule, Mama yake hajulikani alipo na hatumi chochote, acha tu aende mitaani, na akipata hua ananikumbuka Bibi yake analeta chochote, lakini shuleni ndiyo basi tena,” anasema Nkwangu.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano, anakemea tabia ya wazazi kutelekeza wajukuu kwa wazee, akisema hali hiyo ndiyo chanzo kikuu cha watoto kuishia mitaani na kuacha shule.
Anasema wazee hawana nguvu tena ya kulea wajukuu, bali wao ndiyo wanapaswa kutunzwa, lakini cha ajabu wanapewa mizigo tena ya kuishi na wajukuu, na matokeo yake wanashindwa kuwatunza na kuwatumizia mahitaji yao ya msingi na wengine kuacha masomo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Busulwa Pastory Kishiwa. Anasema wao kama viongozi wamekuwa wakiwarudisha baadhi ya watoto kwa wazazi wao, ambao wanabahatika kuwafahamu, na kwamba wengi wanaishi na Bibi na Babu zao, na hali zao ni duni kimaisha.
“siku za masomo hua naona watoto wengi wakiwa mitaani, na baadhi ambao hua tuna bahatika kuwafahamu wazazi wao, tunawakamata na kuwarudisha, ukiwafikisha nyumbani mzazi wake ana kuambia hana uwezo wa kumtunza sababu ya ugumu wa maisha, baada siku mbili unamuona tena mitaani,” amesema Kishiwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Sanjo, Moshi Ngoyeti, anasema watoto wengi wamekuwa wahawafiki shule na kuishia mitaani, huku wengine wakijihusisha na vitendo vya wizi.
“Siku moja kuna watoto wawili walikuwa wana dhurura mitaani hawakwenda shule, nikaletewa taarifa wamempora mtoto mmoja sh.1,000. ambaye alikuwa ametumwa dukani, tuliwakamata na kuwapeleka wa Bibi yao, tukambana huyo Bibi akasema mwanaye yupo Dodoma, akatupa namba ya simu, tukampigia akawaijia watoto wake,”amesema Ngoyeti.
Anasema, hatua ambayo wamekuwa wakiichukua wao kama viongozi wa serikali ya Mtaa wa Sanjo, ni kutoa elimu kwa wazazi kupitia mikutano ya hadhara namna ya kuwalewa watoto wao na kuhakikisha wanafika shuleni.
Anaongeza, mbali na kutoa elimu hiyo, pia wamekuwa wakifanya doria kwa kushirikiana na Jeshi ka Jadi Sungusungu, kuwa kamata watoto wote ambao hudhurura mitaani hovyo siku za masomo, na kisha kwenda nao hadi kwa wazazi wao ili wawapeleke shuleni.
Kaimu Afisa Elimu Taaluma Idara ya Msingi Manispaa ya Shinyanga Ally Liuye, anasema watoto wengi huishi na Bibi zao, na ndiyo maana husindwa kumaliza shule, kutokana na kuishindwa kutimiziwa mahitaji yao.
“Mfano mwaka 2025 watoto waliosajiliwa kufanya mtihani darasa la saba walikuwa 4,959, lakini waliofanya matihani ni 4,908 na wanafunzi 51 hawakufanya mtihani,”amesema Liuye.
Anataja takwimu hizo kwa mchanganuo wa jinsia, kuwa wasichana waliosajiliwa kufanya mtihani darasa la saba mwaka huo 2025 walikuwa 2,670, na waliofanya mtihani 2,651, huku 13 hawakufanya mtihani, na kwa upande wa wavulana walisajiliwa 2,289, waliofanya 2,651, na 38 hawakufanya mtihani huo.
“Mikakati ambayo serikali tunaipanga kupitia idara ya elimu, ni kufanya mikutano na wazazi kwenye shule, ili kuhimiza uchangiaji wa chakula shule, ili watoto wawe wanakunywa hata uji tu, hii itasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi na kutoacha masomo,”amesema Liuye.
Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Manispaa ya Shinyanga Nyanjulwa Kiyenze, anasema ugumu wa maisha umekuwa kikwazo cha familia nyingi kushindwa kutimiza mahitaji ya watoto wao.
Amesema, wao kama dawati hilo, wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi kujiunga na vikundi vya ujasiriamali, ili wapate mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri na kujikwamua kiuchumi, ambayo asilimia nne hutolewa kwa wanawake na vijana. huku asilimia mbili hutolewa kwa watu wenye ulemavu.
Anataja takwimu za mikopo ya asilimia 10 ambayo tayari wameshaitoa kwa kipindi cha kuanzia (2021-2025), kuwa wameshatoa sh.bilioni 1.2, wanawake wameshawapatia sh.milioni 553.7, vijana milioni 581.3 na watu wenye ulemavu milioni 89.2.
“Mikopo hii ina msaada mkubwa kuwainua wananchi kiuchumi, mfano kwa upande wa wanawake wazee, wanaweza kufuga hata kuku, bata, na mbuzi, mifugo ambayo itawasaidia kutimiza mahitaji ya familia zao,” amesema Kiyenze.
Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo, anasema watoto wasipolindwa na kutunzwa katika malezi bora, kunaweza kuzalisha kizazi kibaya cha vijana kisichokuwa na maadili zaidi hata ya “Gen Z.”
Anasema, hatua ambayo wataichukua ili kusaidia watoto hao, watakaa kikao na Maafisa Maendeleo ya Jamii, Ustawi, kutafuta suluhu ya tatizo hilo, ikiwamo kuwasaka watoto wote na kuwarudisha kwa wazazo wao au walezi, pamoja na kutenga fedha za kuwanunua mahitaji ya shule.
Ameongeza, pia watawawezesha wazazi wao mitaji kupitia mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri isiyo na riba, ili wapate mitaji na kufungua biashara ndogo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, Desemba 25, 2025 wakati akila Krismasi na watoto wanaoishi Mazingira Magumu Manispaa ya Shinyanga, ameagiza apewe orodha ya watoto hao ambao wanasoma shule, ili awanunulie mahitaji yote ya shule pamoja na kuwakatia bima za afya, ili wawe wanatibiwa bure na kuwapa ahueni walezi wao.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Frola Ignas, amesema katika Manispaa hiyo kuna jumla ya watoto 336 ambao wanaishi mazingira magumu, wakiume 172 na wakike 164.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, anataja takwimu za mkoa mzima za watoto ambao wanaishi mazingira magumu kuwa ni 99,939 na wanaoishi mitaani ni 612, na wengine hutoka Mikoa ya Kagera, Ngara, Kigoma na nchi za jirani.
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inasema ifikapo mwaka huo, kuwepo na maisha yenye staha, usawa na utu, kwa Watanzania wanaotarajiwa kufikia zaidi ya milioni 118, na kwamba lengo hilo linatarajiwa kufikiwa kupitia malezi na makuzi bora ya watoto, ambapo kwa Shinyanga inaweza kuwa kikwazo kwa dira hiyo kufikia malengo hayo.
ANDIKO LA: Marco Maduhu, SHINYANGA
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.