Gis expert
Member
- Jan 11, 2014
- 28
- 6
ukiona za mwenzako zinanyolewa basi za kwako tia maji. jipange!
Kuna jambo ambalo mwenzenu
linanitatiza kwa kweli na hapa nahitaji ushauri wenu.
Jirani na mahali ninapoishi amehamia dada mmoja mwanajeshi, na nyumba
anayokaa imezungushiwa ukuta na ina nafasi ya kutosha watoto kucheza
hata mpira, sasa huyu dada kaanzisha darasa la kufundisha watoto kucheza
KARATE wakiwemo mabinti wa hapa mtaani kwetu.
Awali mimi sikujua kama huyo dada Mwanajeshi anafundisha mazoezi ya
kucheza KARATE hivyo mama Ngina aliponiomba ruksa kwamba anataka
kujiunga na mazoezi ya kujenga afya nilimkubalia bila kinyongo maana
mimi ni mpenzi sana wa mazoezi ya kujenga afya na huwa namsisitiza tuwe
tunakimbia uwanjani pamoja lakini akawa hataki, sasa baada ya kuniomba
kwamba anajiunga na darasa na maozezi ya kujena afya nikamkubalia,
lakini jana nimerudi mapema kutoka kazini nikasikia kelele zinazofanywa
na wacheza karate hapo kwa huyo jirani yetu nikaona nifanye udadisi ili
kujua ni kitu gani kinaendelea, nilipochungulia getini nikamuona mama
Ngina anajifunza kucheza KARATE, nikashangaa kweli.........
Aliporudi nyumbani nikataka kumuuliza lakini moyo wangu ukasita. Ukweli
ni kwamba mimi na mama Ngina huwa tunatofautiana, lakini hatujafikia
hatua ya kushikana zaidi ya kupishana lugha. Sasa kwa kitendo chake cha
kujifunza hayo makitu ameniweka roho juu maana nachelea siku
tukitofautiana anaweza kunipa za uso......
Hebu nishaurini nimkataze kucheza hayo makitu au nikae kimya nimuache
aendelee kujiweka fit........
utakoma nakuambia unaonaga raha kumfanya mwenzako mlinzi wako.
Bravo mama ngina tena akimaliza hapo anajifunza :boxing: :boxing:
mwambie dadangu anichukulie fomu ya usajili!!
ndo dawa yenu nyie!
na wewe kajifunze boxing ngoma iwe ndroo la sivyo utakul za uso mda si mrefu
Mimi nina aleji na ugomvi siwezi kabisa kujifunza hayo makituMzee na we chuku a fomu, au ni maalum kwa wanawake na watoto peke yake... exclusive
Na we jiunge hapo hapo ujiweke tayari kwa lolote
shikamoo Mtambuzi...
mimi nasubiria thread yako ya "mama ngina kanivunja shingo".....
mwache ajifunze ili siku mkivamiwa na majambazi awe msaada mkubwa.....
kwani amekwambia anajifunza kupigana ili akupige? anafanya kwa afya, mtie moyo utafurahia minyumbuliko itakavyo ongezeka. ila sasa na wewe ufanye ya kwoko asije akafika mwisho akawa fit wewe tumbo kuleee, sec 30 pumzi imekata.
ahahahahaha muonee huruma huyu mzee!
maisha yake yatakuwa magumu muda si mrefu!
amu unajua sikuelewi ujue.... hivi wewe uko upande gani...?utakoma nakuambia unaonaga raha kumfanya mwenzako mlinzi wako.
Bravo mama ngina tena akimaliza hapo anajifunza :boxing: :boxing:
amu... halafu weweeeee....
Mwanamke ni mwanamke tu.. Hata akienda boxing....
Hujahitimu bado??
Nilidhani wewe ndiye teacher...above sterling!!
Babu DC wa 2014!!
wewe sasa naona unashabkia shari. Unajua hiyo makitu bora ajifunze mwanaume na siyo mwanamke.....
Mimi nina aleji na ugomvi siwezi kabisa kujifunza hayo makitu
wewe hunitakii mema ungemuona jinsi anavyoruka yang kibadachi wala usingenishauri nmsogelee
wala sitaki na wala sina wazo la kujifunza karate
namba sikupi na wala sikushauri ujifunza, mwenzi hapa nakuna kichwa maana siijui siku wala saa
eti anafanya kwa afya...! Ni nani alikwambia kwamba karate ni mazoezi ya afya, wewe kweli hujui
bora wewe umeona wengine hapa wanashabikia wala hawajui hatari iliyoko mbele yangu
amu unajua sikuelewi ujue.... Hivi wewe uko upande gani...?
amu... Halafu weweeeee....
mi kuna mtu atanipeleka kwa bensouda muda si mrefu!!Hahaha babu usimtishe paw wangu buree. Mi nna ak47. Afu majuzi nimemsikia anaongelea sijui leseni ya silaha, UN inabidi ipunguze majeshi ya sudani ya kusini wengine waje wakakae uani kwetu. Vita inanukia
Hebu nishaurini nimkataze kucheza hayo makitu au nikae kimya nimuache aendelee kujiweka fit........
Ninyi si mwili mmoja kaka, muulize dhumuni la hayo mazoezi ni nini haswa?
Ila kama ulikuwa umezoea kumchapa makofi nadhani hata usimuulize maana anaweza kuanzia homework kwako...
Ninyi si mwili mmoja kaka, muulize dhumuni la hayo mazoezi ni nini haswa?
Ila kama ulikuwa umezoea kumchapa makofi nadhani hata usimuulize maana anaweza kuanzia homework kwako...
hapo kwenye something different hapo!haaaaapo hapo!!Mtambuzi karate is about
- Self-Defense
- Fitness
- Confidence
- Coordination
- Focus
- Discipline
- Something Different -usiwe na shaka...hatakuwa mmbabe...