Sielewi Mama Ngina anataka kufanya nini...!

Sielewi Mama Ngina anataka kufanya nini...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,442
Kuna jambo ambalo mwenzenu linanitatiza kwa kweli na hapa nahitaji ushauri wenu.

Jirani na mahali ninapoishi amehamia dada mmoja mwanajeshi, na nyumba anayokaa imezungushiwa ukuta na ina nafasi ya kutosha watoto kucheza hata mpira, sasa huyu dada kaanzisha darasa la kufundisha watoto kucheza KARATE wakiwemo mabinti wa hapa mtaani kwetu.

Awali mimi sikujua kama huyo dada Mwanajeshi anafundisha mazoezi ya kucheza KARATE hivyo mama Ngina aliponiomba ruksa kwamba anataka kujiunga na mazoezi ya kujenga afya nilimkubalia bila kinyongo maana mimi ni mpenzi sana wa mazoezi ya kujenga afya na huwa namsisitiza tuwe tunakimbia uwanjani pamoja lakini akawa hataki, sasa baada ya kuniomba kwamba anajiunga na darasa na maozezi ya kujena afya nikamkubalia, lakini jana nimerudi mapema kutoka kazini nikasikia kelele zinazofanywa na wacheza karate hapo kwa huyo jirani yetu nikaona nifanye udadisi ili kujua ni kitu gani kinaendelea, nilipochungulia getini nikamuona mama Ngina anajifunza kucheza KARATE, nikashangaa kweli.........

Aliporudi nyumbani nikataka kumuuliza lakini moyo wangu ukasita. Ukweli ni kwamba mimi na mama Ngina huwa tunatofautiana, lakini hatujafikia hatua ya kushikana zaidi ya kupishana lugha. Sasa kwa kitendo chake cha kujifunza hayo makitu ameniweka roho juu maana nachelea siku tukitofautiana anaweza kunipa za uso......

Hebu nishaurini nimkataze kucheza hayo makitu au nikae kimya nimuache aendelee kujiweka fit........
 
Usitie shaka la msingi kaa kimya tu hayo mazoez yanaweza kuwa msaada wa baadae katika familia au pia anaweza kuwa mstari wa mbele kupambana na vibaka tofauti
 
sa kama wanaume wanaruhusiwa na wewe kajiunge bila kumwambia mkutane mazoezin sawa baba ngina
 
kwani amekwambia anajifunza kupigana ili akupige? anafanya kwa afya, mtie moyo utafurahia minyumbuliko itakavyo ongezeka. ila sasa na wewe ufanye ya kwoko asije akafika mwisho akawa fit wewe tumbo kuleee, sec 30 pumzi imekata.
 
Punguza hasira mwl Mtambuzi anza na huyo mdada mwanajeshi😛😛

Umenikumbusha kitu mkuu,

Kuna huu usemi wa Tata Madiba...."Stay closer to your enemy and within the circles of your friends".

Nadhani hiyo ndiyo dawa yao hawa ndugu zetu....Kukaba hadi penalty...hata likiingia goli usijilaumu!

Babu DC in 2014!!
 
utakoma nakuambia unaonaga raha kumfanya mwenzako mlinzi wako.
Bravo mama ngina tena akimaliza hapo anajifunza :boxing: :boxing:


Hii hii tabia ya nyie wadau zetu kugombelezeana inamaanisha nini amu??

Huwa nashangaa Mmama anavyoweza kuhangaika kuvalisha katoto ka jirani ili akisioneshe mtaji kwa umma....hata kama hawafahamiani na mama wa mtoto...lol!!

Babu DC wa 2014!!
 
Last edited by a moderator:
Hii hii tabia ya nyie wadau zetu kugombelezeana inamaanisha nini amu??

Huwa nashangaa Mmama anavyoweza kuhangaika kuvalisha katoto ka jirani ili akisioneshe mtaji kwa umma....hata kama hawafahamiani na mama wa mtoto...lol!!

Babu DC wa 2014!!

women supporting each other.
Tyta embu kapicha kidogo mama ngina keshahitimu black belt.
Ha ha ha nacheka sana Mtambuzi ole wako ujichanganye.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom