Ujinga wa mapenzi ulivyonitesa shule (advance level)

washasimu

Member
Feb 25, 2024
7
2
Hellow

Kwa majina naitwa washasimu washasimu ni mtoto wa tatu kwenye familia yetu kati ya watoto wa 5 na hii ndio historia yangu kwa ufupi

MAISHA YANGU YA UTOTO

Maisha yangu ya utoto kati ya miaka 7 mpaka 13 kifupi yalitawaliwa na furaha kiujumla kwa sababu nilikuwa huru sana kuchagua marafiki na watu wa kucheza nao baba na mama yangu wote walikuwa wafanya biashara so mama anaondoka asubuhi na kuludi jioni baada ya kutoka kwenye Mishe zake na baba pia ni hivyo hivyo so nilikuwa huru sana kwenda mitaa yoyote ile kucheza na ikifika jioni naludi nyumbani naoga na kuendelea na maisha mengine katika umri huo nilikuwa napata uangalizi mkubwa sana kutoka kwa kaka zangu na rafiki wa kaka zangu so pamoja na uhuru wote lakini nilikuwa under guidance kifupi nilikuwa ni mtoto mwenye tabia njema sikuwahi tukana mtu matusi ya nguoni(hususa ni viungo vya uzazi) na niliogopa sana na pia mimi mwenyewe nilikuwa najilinda sana na makundi mabaya sababu baba na mama kila siku walikuwa wananionya

MAISHA YA SHULE

Nilianza shule mwaka X(kipindi ambacho Kikwete alikuwa yupo madarakani) sikusoma vidudu nilianza tu darasa la kwanza Hii ulinipa shida sana hasa katika maendeleo yangu ya shule coz nilikuwa sijui kusoma wala kuandika na kwaio iliniwia vigumu sana kufauru katika darasa la kwanza kipindi nipo darasa la kwanza nilikuwa na mwili mdogo sana kwaio nilikuwa naonewa na wale wakubwa ukiongeza na kutokufauru shule nikajikuta naichukia shule kiujumla hapo ndipo nikaanza kushinda porini katika umri mdgo kabisa nakumbuka ulikuwa ni mwezi wa 4 ndipo nilipoanza kushinda porini

Maisha ya kushinda porini yaliendelea mpaka mwezi wa 8 hapo bado sijui kusoma wala kuandika kuna siku nimekaa porini nimejificha nashangaa wanafunzi wenzangu wanakuja upande wangu wakiwemo na wale ambao huwa nashindaga nao porini mimi baada ya kuwaona wale washkaji zangu nikajua hakuna noma yoyote huwenda tumeongezeka idadi kumbe wametumwa na mwalimu wa darasa waje kunikamata baada ya kunikamata nikapelekwa kwa mwalimu wa darasa siku ile nilikula sana bakora na kesi ikafika nyumbani pia nikala bakora za kutosha hapo ndio nikapewa uangalizi maalum nyumbani pamoja na shule

Nyumbani nilipewa uangalizi wa kutopewa uhuru ule kama mwanzo kama nataka kucheza au kutoka nje basi niwe na kaka zangu mbali na kaka zangu siluhusiwi kwenda zaidi zaidi nibaki ndani na dada wa kazi

Shule nilipewa uangalizi na mwalimu wa darasa muda wote anataka niwepo darasani pia nikakabidhiwa mtu wa kunifundisha kusoma na kuandika alikuwa ni dada mmoja hivi mweupee anaitwa Aisha(jina halisi)

Maisha ya shule yaliendelea na Aisha alikuwa kila siku ananifundisha kusoma na kuandika coz yeye ndio alikuwa kinara wa darasa kipindi hicho na nilikuwa namuelewa sana coz alikuwa ananifundisha kwa uporeeee


Maisha yakaendelea nikaanza kuimprove katika swala zima la elimu baada ya miezi mi 2 nikawa najua kusoma na kuandika kiasi sikuwa zoba kama mwanzo ikafika mwezi wa 11 tukafanya mtihani wa kufunga shule nilikuwa wa 57 kati ya wanafunzi 74 na Aisha alikuwa ndio wakwanza rafiki zangu ambao nilikuwa naludi nao nyumbani mmoja alikuwa wa 5 mwingine wa 7 mwingine wa 12 so njiani walikuwa wananicheka mimi tu hii iliniuma sana nikajiapiza kuanzia darasa la 2 nitawanyosha

Likizo ile ya mwezi wa 12 nilitumia vizuri sana kwa kujifunza kusoma na kuandika kwa ufasaha hii kazi alikuwa anaifanya kaka yangu mkubwa alinifundisha kwa moyo wote
Nilivoelewa kusoma na kuandika akaanza kunifundisha na hesabu za kawaida zile za la kwanza pamoja na za la pili LIKIZO IKAISHA HIVO


MAISHA YANGU YA DARASA LA PILI MPKA LA SABA

Baada ya kurudi shule baada ya likizo kuisha nilibadilika sana Aisha ndie alikuwa desk mate wangu so alinifanya nipende shule pia hata darasani nikawa sishikiki tena kama sitakuwa wa kwanza basi wa pili wa kwanza Aisha tumepokezana hizi namba na Aisha mpka darasa la 5 hapa ndio wakaibuka vipanga wengine so competition ikawa kubwa but haikunizuia kuitetea namba yangu

Tulipo fika darasa la sita Aisha akahama shule na mkoa pia( baba yake alikuwa ni asistant lecture wa moja ya chuo kikubwa hapa Tanzania) so nikabaki mwenyewe

Nakumbuka kwenye competition za mitihani ya jumamosi na shule jirani nilikuwa nawaburuza sana shule jirani hasa kwa masomo kama sayansi na maarifa ya jamii nilikuwa sishikiki but hisabati nilikuwa siipendi so sikuwa na uhakika wa kuongoza pamoja na English japo kuna muda nilikuwa nawaburuza kwa masomo yote


Nilipofika darasa la saba niliendelea kukiwasha matokeo ya darasa la saba nilipata wastani wa A nikafauru moja ya shule kubwa pale jijini kwetu



Itaendeleaaaa
 
A%20Message%20Of%20Faith.jpg
 
Hellow

Kwa majina naitwa washasimu washasimu ni mtoto wa tatu kwenye familia yetu kati ya watoto wa 5 na hii ndio historia yangu kwa ufupi

MAISHA YANGU YA UTOTO

Maisha yangu ya utoto kati ya miaka 7 mpaka 13 kifupi yalitawaliwa na furaha kiujumla kwa sababu nilikuwa huru sana kuchagua marafiki na watu wa kucheza nao baba na mama yangu wote walikuwa wafanya biashara so mama anaondoka asubuhi na kuludi jioni baada ya kutoka kwenye Mishe zake na baba pia ni hivyo hivyo so nilikuwa huru sana kwenda mitaa yoyote ile kucheza na ikifika jioni naludi nyumbani naoga na kuendelea na maisha mengine katika umri huo nilikuwa napata uangalizi mkubwa sana kutoka kwa kaka zangu na rafiki wa kaka zangu so pamoja na uhuru wote lakini nilikuwa under guidance kifupi nilikuwa ni mtoto mwenye tabia njema sana sikuwahi tukana mtu matusi ya nguoni(hususa ni viungo vya uzazi) na niliogopa sana na pia mimi mwenyewe nilikuwa najilinda sana na makundi mabaya sababu baba na mama kila siku walikuwa wananionya

MAISHA YA SHULE

Nilianza shule mwaka X(kipindi ambacho Kikwete alikuwa yupo madarakani) kiukweli sikusoma vidudu nilianza tu darasa la kwanza Hii ulinipa shida sana hasa katika maendeleo yangu ya shule coz nilikuwa sijui kusoma wala kuandika na sikusoma vidudu kwaio iliniwia vigumu sana kufauru katika darasa la kwanza nakumbuka kipindi nipo darasa la kwanza nilikuwa na mwili mdogo sana kwaio nilikuwa naonewa na wale wakubwa ukiongeza na kutokufauru shule nikajikuta naichukia shule kiujumla hapo ndipo nikaanza kushinda porini katika umri mdgo kabisa nakumbuka ulikuwa ni mwezi wa 4 ndipo nilipoanza kushinda porini

Maisha ya kushinda porini yaliendelea mpaka mwenzi wa 8 hapo bado sijui kusoma wala kuandika Nakumbuka kuna siku nimekaa porini nimejificha nashangaa wanafunzi wenzangu wanakuja upande wangu wakiwemo na wale ambao huwa nashindaga nao porini mimi baada ya kuwaona wale washkaji zangu nikajua hakuna noma yoyote huwenda tumeongezeka idadi kumbe wametumwa na mwalimu wa darasa waje kunikamata baada ya kunikamata nikapelekwa kwa mwalimu wa darasa nakumbuka nilikula sana bakora siku ile na kesi ikafika nyumbani pia nikala bakora za kutosha na hapo ndio nikapewa uangalizi maalum nyumbani pamoja na shule

Nyumbani nilipewa uangalizi wa kutopewa uhuru ule kama mwanzo kama nataka kucheza au kutoka nje basi niwe na kaka zangu mbali na kaka zangu siluhusiwi kwenda zaidi zaidi nibaki ndani na dada wa kazi

Shule nilipewa uangalizi na mwalimu wa darasa muda wote anataka niwepo darasani pia nikakabidhiwa mtu wa kunifundisha kusoma na kuandika alikuwa ni dada mmoja hivi mweupee anaitwa Aisha(jina halisi)

Maisha ya shule yaliendelea na Aisha alikuwa kila siku ananifundisha kusoma na kuandika coz yeye ndio alikuwa kinara wa darasa kipindi hicho na nilikuwa namuelewa sana coz alikuwa ananifundisha kwa upore

Basi bana nikaanza kuimprove katika swala zima la elimu baada ya miezi mi 2 nikawa najua kusoma na kuandika kiasi sikuwa zoba kama mwanzo ikafika mwezi wa 11 tukafanya mtihani wa kufunga shule nakumbuka nilikuwa wa 57 kati ya wanafunzi 74 na Aisha alikuwa ndio wakwanza nakumbuka rafiki zangu ambao nilikuwa naludi nao nyumbani mmoja alikuwa wa 5 mwingine wa 7 mwingine wa 12 so njiani walikuwa wananicheka mimi tu hii iliniuma sana nikajiapiza kuanzia darasa la 2 nitawanyosha

Likizo ile ya mwezi wa 12 nilitumia vizuri sana kwa kujifunza kusoma na kuandika kwa ufasaha hii kazi alikuwa anaifanya kaka yangu mkubwa coz alikuwa ananipenda sana so alinifundisha kwa moyo wote
Nilivoelewa kusoma na kuandika akaanza kunifundisha na hesabu za kawaida zile za la kwanza pamoja na za la pili LIKIZO IKAISHA HIVO


MAISHA YANGU YA DARASA LA PILI MPKA LA SABA


Kiukweli baada ya kurudi shule baada ya likizo kuisha nilibadilika sana Aisha ndie alikuwa desk mate wangu so alinifanya nipende shule pia hata darasani nikawa sishikiki tena kama sitakuwa wa kwanza basi wa pili wa kwanza Aisha tumepokezana hizi namba na Aisha mpka darasa la 5 hapa ndio wakaibuka vipanga wengine so competition ikawa kubwa but haikunizuia kuitetea namba yangu

Tulipo fika darasa la sita Aisha akahama shule na mkoa pia( baba yake alikuwa ni asistant lecture wa moja ya chuo kikubwa hapa Tanzania) so nikabaki mwenyewe

Nakumbuka kwenye competition za mitihani ya jumamosi na shule jirani nilikuwa nawaburuza sana shule jirani hasa kwa masomo kama sayansi na maarifa ya jamii nilikuwa sishikiki but hisabati nilikuwa siipendi so sikuwa na uhakika wa kuongoza pamoja na English japo kuna muda nilikuwa nawaburuza kwa masomo yote


Nilipofika darasa la saba niliendelea kukiwasha nakumbuka matokeo ya darasa la saba nilipata wastani wa A nikafauru moja ya shule kubwa pale jijini kwetu



Itaendeleaaaa
Wewe ni ke au me?

Kama ni me utakuwa na matatizo, maana Unasound kama ke.
 
Let's goooo


Baada ya mimi kufauru vizuri na kuchaguliwa katika moja ya shule bora pale mkoani kwetu baba yangu alifurahi sana kwani mimi pekee katika mtaa wetu ndio nilipata daraja kubwa na kuchaguliwa katika shule hiyo nzuri so mzee aliniahidi zawadi ya kunisomeaha shule nzuri na ya gharama kama zawadi kwangu kwa kumuheshimisha


Ulipofika mwezi wa kwanza nikaripoti shule ambayo nilichaguliwa na nikasoma kwa muda wa mwezi mmoja tu then mzee akaniamisha na kunipeleka shule moja ya private iliyopo mkoa X kusini mwa Tanzania shule hii ilikuwa inasifika kwa uwezo wake wa kufaulisha wanafunzi so hata ada yao ilikuwa kubwa kidogo( kwa uwezo wa familia yetu) nakumbuka baba aliniambia alikuwa analipa zaidi ya 2,300,000 kwa mwaka nikaanza maisha katika shule hiyo mpya

Uwezo wangu kwa mala ya kwanza ulionekana kuwatishia walionekana vipanga wa darasa kwa wakati huo(shule ilikuwa na utaratibu wa kufanyisha monthly test) kwani test za kwanza tu nilipata wastani wa 92 nikawa wa pili wa kwanza alikuwa na wastani wa 98 maisha yakaendelea kusonga

Kiuhalisia mimi nilikuwa ni mtu mpole na asiyependa kuongea na watu wengi yaani mimi muda mwingi nilikuwa napenda kukaa peke yangu na kufanya vitu pekee yangu but nilikuwa muongeaji sana kwa watu niliowazoea kingine moja ya ulevi wangu mkubwa ilikuwa ni mziki nilikuwa napenda sana mziki

Maisha yakaendelea katika hayo makazi mapya yaliyojaa watu wengi ambao siwajui so muda mwingi nilikuwa nipo peke yangu term ya kwanza ikaisha nilifaulu vizuri sana ya pili nayo ikaisha nikaua tena pepa ya tatu ikaisha nikaua kama kawaida

Kipengele kikaja kwenye term ya nne hapo nilikuwa na marafiki wachache sana kama wawili tu nakumbuka katika term ya nne nilikuwa nimemiss sana kusikiliza mziki na sikuwa na njia yoyote ya kusikiliza but kuna jamaa mmoja alikuwa na mabraza zake wa madarasa ya juu ambao walikuwa watukutu so walikuwa wanamiliki redio na memory card na kila weekend lazima waluke Uzio wa shule na kwenda mtaani kufanya yao ikiwemo na ku burn nyimbo kwenye memory card so kila wimbo mpya walikuwa wanao hii ilinivutia sana kuona wana nyimbo nyingi mpya to cut the story nilijiunga kwenye kundi la hao jamaa na ndio wakawa rafiki zangu wapya japo watu walikuwa wanajiuliza inakuwaje mimi mtu mpole na manage kuongea na kuishi na hao watukutu kumbe mimi ni muongeaji zaidi ya wao coz nilikuwa naongea sana nikisha mazea mtu term ya nne nilifaulu vizuri but sio ile ya kutisha

Nilipofika form two urafiki wetu na wale jamaa watukutu ukawa umekwiva so muda mwingi nilikuwa nashinda nao nikaanza kutokuingia darasani nikaanza kuruka uzio wa shule na kwenda kwenye miziki mtaani sisi tulikuwa tunaita (mapini) walimu walijaribu kunionya lakini ilikuwa kazi bure coz nilikuwa napenda ninachofanya walijalibu kumshilikisha mzee kuhusu mwenendo wa tabia yangu mzee alikuwa anashauli nipigwe tu na walimu na walimu walikuwa wananipiga kweli lakini sikuacha tabia zangu na performance yangu ikaanza kushuka kama kimondo

Mtihani wa mock nakumbuka nilipata division 4 ya 29 na wenye 4 tulikuwa wa 5 tu hivyo tukakaa na uongozi wa shule wakatuwekea program maalumu ya kutufanya tufaulu kila jioni tulikuwa tunaenda library ya shule tunapewa past paper tunafanya then kesho yake tunasahihishwa kwa tulichokosea Hii ilisaidia coz mtihani wa mwisho(necta) wote tulifaulu na mimi nilipata division 2 ya 20


Darasa la form two likawa limeisha kihivyo huku ni nikiwa miongoni mwa wanafunzi vilaza darasani

Tuliingia form 3 maisha ya utukutu yakaendelea ikawa haipiti siku mbili hatujaluka Uzio wa shule walimu walikuwa wakitukamata wanatuadhibu tu then wanatuacha tukahisi hawana cha kutufanya zaidi ya kutuadhibu kwa viboko coz tayari tulikuwa Masugu hapo tulikuwa wa 3 ambao tupo form 3 na wengine 6 wapo form 4. Kuna siku ilikuwa mwezi wa pili ile tunaluka tu ukuta kwenda nje tunakutana na mwalimu mkuu msaidizi pamoja na mwalimu wa nidhamu na scout wa shule wanoko walishatuchoma kwa walimu so walimu walichofanya ni kutuvizia coz waliochoshwa na tabia zetu tukapelekwa kwenye ofisi ya mwalimu wa nidhamu tulikula sana bakora siku hiyo na kesi ikafika kwa mkuu wa shule bodi ya shule ikakaa kikao na kwa sababu tulionekana ni wanafunzi watukutu wakakubaliana tufukuzwe shule kikao kilikaliwa Ijumaa na kuna mwalimu mmoja alikuwa na urafiki na wale ma bro wa form 4 ndio aliyekuja kuwapa taarifa so wote zikatufikia kuwa j3 hatuna shule na simu zishaanza kupigwa majumbani kwetu


Ikafika j3 tukaenda asemble kama kawaida yakatolewa matangazo ya kawaida then tukatawanyishwa hakuna lolote liliongelewa kuhusu sisi so tukahisi bro alituchota tu hakuna kitakachotokea kesi imeisha

Ikafika saa 6 kengele ya dharula ikagongwa hapo tukashtuka tukaangaliana na wanangu then tukaelekea eneo la asemble ile nafika tu namuona mzee kasimama asemble nilishtuka nikajisemea moyoni nimeisha

Akapanda displine master akaongea sana kuhusu swala la nidhamu na kutukumbusha sheria za shule na adhabu zake kwa wataozivunja then akamkaribisha headmaster

Headmaster akatuita majina yetu na kutuambia tusogee mbele wote tukapanda asemble then headmaster akakumbushia sheria za shule na kutuambia kuwa sisi tumezivunja(walituongezea na kosa la kuvuta bangi japo haikuwa kweli) so adhabu ilikuwa ni viboko vi 5 mbele ya wanafunzi na wazazi na uongozi wa shule pamoja na kufutwa shule

Hatukuwa na la kubisha coz tulikuwa wadogooo mbele ya wazazi tukapigwa bakora zetu 5 then wazazi wakapewa nafasi ya kuongea nakumbuka mzee aliongea kwa uchungu sana na kuwahusia wanafunzi wengine wasituige sisi chozi lilinitoka siku ile kwa yale maneno ya mzee akilaumu kuwa alipoteza tu pesa zake

Shule tukafukuzwa kihivyo nikaludi nyumbani na mzee wangu kwenye gari hakuna aliemuongelesha mwenzake



Itaendeleaaaa kabla ya saa 5 usiku
 
Advance level ndio nini? That sentence doesn't make any sense in any language.

Alafu nashangaa sana watu wengi wanaojiita wasomi wanashindwa kutofautisha obvious improper grammar kati ya "Advance Level" na "Advanced Level"

Ni Advanced Level. Neno Advance Level halina maana wala tafsiri.
 
Advance level ndio nini? That sentence doesn't make any sense in any language.

Alafu nashangaa sana watu wengi wanaojiita wasomi wanashindwa kutofautisha obvious improper grammar kati ya "Advance Level" na "Advanced Level"

Ni Advanced Level. Neno Advance Level halina maana wala tafsiri.
Sasa si unamuona mwenyewe kilaza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom