Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Asubuhi nimesikia kwenye uchambuzi Danny Mwakalinga sijui inakuwaje hapo Masa na Sikonge?

Mkuu, soma maelezo ya Engineer hapo juu. Kama anachosema huyo jamaa ni kweli basi ni vema TUSUBIRI hiyo riport maana hapo hakuna atakayesema KASINGIZIWA. Hivyo wote tuache papara na TUSUBIRI.
 
Na wewe acha kamba.

Kuwa na simu mbili za Ericsson zenye kunasa sauti na kupiga picha siyo big deal kwa dunia hii. Sasa angelikutwa na Iphone au Blackberry?

Ukitaka kumuuwa mtu siku hizi huhitaji kutumia kisu. Inatosha kumpa Zombe type visenti kidogo na umekwisha. Polisi wanafanya kazi hiyo safi kabisa na wanakukingia kifua. Kwa sasa anatembea na Waandishi wa IPPMEDIA kibao na ilisemwa tangu mwanzo.

Kwa ni siri kuwa Mwakyembe kaolea uchagani? Huko ukweni si ndiyo familia ya Mengi? Mwamba ngoma ndugu yangu, huvutia kwake......

Halafu jina la kijana aliyekuwa na simu mbili za Ericsson linaleta utata sana. Walau ingelikuwa Sony-Ericsson ningeliona ni simu ya kisasa. Mie nilifikiri Ericsson wameshakufa na kuamua kufunga ndoa na Sony? Hii miandishi OVYOOO KABISAAA..

Halafu kukutwa na KISU si kuwa umekuwa muuwaji. Huyu jamaa anaweza kuwa alikimbia kwa kuogopa kipigo kutoka kwa vijana wa CCM wanaofahamika kwa kibano chao cha nguvu. Wakati POLISI wanasema tunaendelea na uchunguzi, wao tayari wameshamhukumu? Ningelikuwa mie ningeliwashtaki kwa kunipakazia kuwa NILITAKA KUMUUWA Mwakyembe.

na Mwakyembe mwenyewe, wewe mwanasheria mzima unakuwa kama Mtei? Ukibanwa useme aliyepewa hizo milioni 400 ili kukumaliza, utaonyesha? Watu wamevurunda wenyewe na sasa kipindi cha malipo kinakaribia mtu anaanza kutafuta kisingizio. Nani alikuambia utowe AHADI kibao kama Muungwana? Mwakani utaubeba msalaba wa ahadi HEWA.

Hapo ndipo tulipo fikishwa na wahandisi wetu wa habari. Wanajua tunameza kila kitu bila kutafakari hivi kweli inaingia akili mtu aende kumdhuru mbunge kwenye mkutano wake akiwa na wafuasi wake kwa kutumia kisu cha mkunjo? IPP wanaji dhalilisha sana kwa kukumbatia ujinga kama huu.

Yana mwisho haya - Rashid kwenye KULI
 
Habari ya leo kwenye Nipashe inasema kuna message nyingi zenye ujumbe mzito kutoka kwa Vigogo Mbeya zinazoashiria kwamba kijana alikua anafanya kazi maalumu. Zaidi, inasema kwamba kuna fedha hupitia mikoa ya kaskazini (ARSHA ?), lakini zikiwa na chanzo chake nje (?). Naamini kwamba mwandishi hawezi kuandika uongo utakao mletea shida baadaye. Hii ni habari ya kipelelezi, inabidi tuifuatilie. Hivi Kyela kuna chama cha upinzani chenye nguvu? Nadhani ni wakati mzuri Bro. Mwakalinga na Dr. Mwakyembe wakapambanishwa kwa vyama tofauti. hapo tutaona nani ni nani. Vinginevyo tuachieni Kyela yetu ya amani........
 
Mpwa check spelling una maana George?

Una matatizo na George Mwakalinga, hilo tunalijua. Huyo kijana ni Daniel Mwakalinga (Dan) na ndiye alikuwa ana record hiyo public meeting baada ya kutumwa na ndugu zake ili kuweka ushahidi kwasababu Dr. Mwakyembe alikuwa anaropoka majungu mengi sana huko vijijini kwamba Mwakalinga kahongwa milioni 400 na katumwa na mafisadi.

Wakaamua kwamba kama anasema ukweli basi afanye hivyo wakati anakuwa recordrd. Huyo kijana wote pale wanamfahamu maana weekends husimamia kuonyesha mipira kwenye big screen kwenye ukumbi wa Mwakalinga na vijana karibu wote wa Kyela huenda kuangalia mipira hapo.

Waliamua aende mtu ambaye anajulikana ili kusiwe na kisingizio cha kwamba walimtuma mtu kwa siri. Walipomwona wakambeba na mambo mengine ndio kama nilivyoandika hapo juu.

Sasa wamezua lingine wanasema kwenye simu kulikuwa na sms za mawasiliano na vigogo. Ni kigogo gani atawasiliana na huyo kijana?

Pia kitu kingine ambacho NIPASHE wamechemsha ni kwamba hiyo simu ilifikishwa polisi ikiwa imesha battery kwahiyo polisi Kyela walishindwa kusoma kilichoandikwa. Baadaye mwenye simu akaambiwa apeleke charger na RCO akaondoka na simu kwenda Mbeya. Kwahiyo hakuna polisi Kyela aliyesoma hizo sms kinyume na Nipashe wanavyodai.

Waliosoma hizo sms ni hao wapambe wa mheshimiwa pamoja na mheshimiwa mwenyewe.

Wacha tusubiri taarifa na ukweli wote utajulikana tu.
 
Mpwa check spelling una maana George?

Daniel Mwakalinga ni huyo kijana inasemekana alitekwa nyara na Wapambe. Huyu ni MPELELEZI anayetumia vifaa vya kisasa kabisa yaani simu ya ERICSSON (OLD SCHOOL) kwa kurekodi picha na sauti.

Kama angelikuwa Mwakalinga George, angelikuwa na vifaa lattest kutoka China ambavyo hata wapelelezi wa Tanzania hawana na huko ni kifaa cha kawaida kabisaaa watoto wanatumia mitaani.

Hebu cheki hii kalamu. Hii ndiyo walitumia kumrekodi Waziri Masha.

LUX-Camera%20pen.jpg
 
Mwakyembe siri yafichuka

Na Mwandishi wetu
5th September 2009

headline_bullet.jpg
Mtuhumiwa akutwa na ujumbe wa kummaliza kisiasa
headline_bullet.jpg
Wadaiwa uliandaliwa na vigogo mbalimbali nchini

Mwakye%282%29.jpg

Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe.

Siku tatu baada ya kutiwa mbaroni, Daniel Mwakalinga, anayeshukiwa kuandaa njama za kumdhuru Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, ujumbe uliokutwa kwenye simu yake unadaiwa kuwahusisha vigogo wa Mkoa wa Mbeya katika maandalizi ya kummaliza kisiasa.

Hatua ya ujumbe mfupi uliokutwa kwenye simu ya mtuhumiwa, unadaiwa kuweka hadharani majina ya vigogo hao wanaohusika na njama hizo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakituhumiwa kumhujumu kisiasa.

Taarifa za polisi zinadai kuwa ujumbe mbalimbali uliokutwa kwenye simu za mtuhumiwa zilizochukuliwa kwa uchunguzi, zinawahusisha moja kwa moja vigogo kadhaa wa CCM na serikali ya Mkoa wa Mbeya kuhusika na njama hizo.

“Sms (ujumbe) hizi zinathibitisha taarifa ambazo tumekuwa nazo kwa siku nyingi...anahusika na vurugu zote za kisiasa zinazotokea Kyela kwa lengo la kumdhoofisha Dk Mwakyembe,” kilidai chanzo chetu kutoka polisi.

Licha ya chanzo hicho kushindwa kutoa undani wa sms hizo, mmoja wa wasaidizi wa Dk Mwakyembe (jina linahifadhiwa), alidai kuwa aliweza kuona baadhi ya ujumbe huo baada ya kumfikisha mtuhumiwa polisi.

Pia zinaonyesha mtiririko wa fedha kutoka nje ya nchi kupitia moja ya mikoa ya Kaskazini kabla ya kuwafikia walengwa mkoani Mbeya.

Mmoja wa wanaotishiwa ni mwandishi wa habari Richard Kilumbu

Ujumbe mwingi unatoa taarifa kutoka kwa mtu wanayemwita 'mzee' na nyingine zinamtaja kigogo mmoja wa mkoa moja kwa moja.
ambaye anadaiwa kumuunga mkono Dk Mwakyembe.

Taarifa za mtandao huo zinadai, mmoja wa wapambe wa kigogo huyo na wapigadebe wa mwanamtandao anayeishi nje ya nchi, tayari anafanya kampeni kuwania ubunge mwenyewe.

“Hawa na kundi lao wanaendesha kampeni kali vijijini za kujinadi sambamba na kundi la ... kwa Kyela hakuna cha muda rasmi kuanza kampeni maana wote hawa wana baraka zote za kigogo wa Serikali mkoa na CCM,” alidai mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya. Majina na sms hizo kwa sasa tunayahifadhi.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa walidai kuwa, hali tete ya kisiasa imesababishwa na uamuzi wa makosa au makusudi kuteua mtu ambaye ana uhasama na mbunge.

Hoja hiyo inaungwa mkono na wazee na vijana na kwamba, lawama zote za kudhurika kwa mbunge wao zitabebwa na serikali.

“Mbona haijafanya hivyo kwa majimbo mengine? Kyela tu! Mbunge wetu kakosea nini?” alihoji Mzee Kandambili Malundi, mkazi wa Ikolo.

Taarifa zilizotufikia jana jioni zilidai kuwa mwandishi wa habari, Richard Kilumbo, tayari amefungua jalada la malalamiko polisi kuhusiana na sms anazopata kutoka wanamtandao hao.

Akizungumzia matukio hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alisema jana jioni kuwa vielelezo vya Mwakalinga vimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Nipashe ilitaka kujua iwapo simu ya Mwakalinga nayo inashikiliwa, hivyo RPC Nyombi alikuwa na haya ya kujibu: "Nimekueleza kwamba vielelezo vyote ya mtuhumiwa vinashikiliwa nadhani unaelewa maana ya kusema hivyo."

CHANZO: NIPASHE

Hivi kumbe George Mwakalinga katumwa au anaungwa mkono na Mhe. Mwakipesile? huo si ndo mtandao wa mafisadi?
 
Habari ya leo kwenye Nipashe inasema kuna message nyingi zenye ujumbe mzito kutoka kwa Vigogo Mbeya zinazoashiria kwamba kijana alikua anafanya kazi maalumu. Zaidi, inasema kwamba kuna fedha hupitia mikoa ya kaskazini (ARSHA ?), lakini zikiwa na chanzo chake nje (?). Naamini kwamba mwandishi hawezi kuandika uongo utakao mletea shida baadaye. Hii ni habari ya kipelelezi, inabidi tuifuatilie. Hivi Kyela kuna chama cha upinzani chenye nguvu? Nadhani ni wakati mzuri Bro. Mwakalinga na Dr. Mwakyembe wakapambanishwa kwa vyama tofauti. hapo tutaona nani ni nani. Vinginevyo tuachieni Kyela yetu ya amani........

Nyumbu,

Hiyo habari ya NIPASHE leo ni uwongo kwa aslimia zaidi ya 90.

Ni kigogo gani mjinga kiasi hicho atakuwa anamtumia sms kijana mdogo na kibarua tu pale Kyela mjini?

Hakuna sms za aina yoyote kama hizo wanazozisema. Kuna kitu Engineer kaandika hapo juu ambacho ni ukweli. Hiyo simu ilizimika ikiwa mikononi mwa wapambe wa Mwakyembe kabla ya kufika polisi Kyela na mpaka RCO anaichukua hakuna polisi wa Kyela aliyekuwa amesoma sms ndani ya simu hiyo. Alisema ataenda kui charge Mbeya na ndipo angesoma hizo sms. Ukiachia mawasiliano ya kawaida ya Mwakalinga na vijana wake wa Kyela hakuna habari za kigogo yeyote.

Wanachofanya NIPASHE ni mwendelezo wa habari za kupika kama jana walivyosema mheshimiwa alitaka kuchomwa kisu.

Kwa habari hii ya leo Mwakalinga ameshawaambia wanasheria wake Dar kuishitaki IPPMEDIA kwa uzushi na kutaka kuleta machafuko Kyela.

Kuweni na subira na ukweli utajulikana muda sio mrefu.
 
Hapo ndipo tulipo fikishwa na wahandisi wetu wa habari. Wanajua tunameza kila kitu bila kutafakari hivi kweli inaingia akili mtu aende kumdhuru mbunge kwenye mkutano wake akiwa na wafuasi wake kwa kutumia kisu cha mkunjo? IPP wanaji dhalilisha sana kwa kukumbatia ujinga kama huu.

Yana mwisho haya - Rashid kwenye KULI

Masatu,
Safari hii mtu lazima AFIKISHWE mahakamani kwa huu upuuzi. Mtu huwezi kuandika UPUPU namna hii. Unatunga uongo na mwisho unaanza kuuamini mwenyewe. Hii inanikumbusha ile kesi ya Omar Mahita alipoita waandishi wa habari na kuonyesha USHAHIDi wa visu vya CUF. Visu vyenyewe kama ushahidi eti vimepakwa rangi ya bendera ya CUF - too low. Na ukweli ukawa kwamba yeye ndiyo alikuwa kinara wa kutuma vijana wake. Si ajabu baadaye Zombe akanogewa na akaendeleza hayo mambo.

Mwisho watasema hicho kisu cha mkunjo kimeletwa kutoka nchi za nje. Ngoja tusubiri riport na kama kweli walimteka na kumpeleka kwa Mbunge basi itabidi Mwakalinga atafute MAWAKILI ili hili swala LIISHE. Na hawa jamaa wa IPPMEDIA itabidi na wao wapandishwe kizimbani vilevile kwa kumpakazia. Nina imani mawakili wengi watataka kuishika hii kesi maana ukishinda against IPPMEDIA, basi chart yako ITAPANDA SANA.
 
Hivi kumbe George Mwakalinga katumwa au anaungwa mkono na Mhe. Mwakipesile? huo si ndo mtandao wa mafisadi?

Mkuu,
Mbona husomi habari? Mwenyewe umetutumia na wala hujasoma? Ovyo kabisaa. Unaweka maswali wakati jibu umeweka mwenyewe?

Akizungumzia matukio hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alisema jana jioni kuwa vielelezo vya Mwakalinga vimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Nipashe ilitaka kujua iwapo simu ya Mwakalinga nayo inashikiliwa, hivyo RPC Nyombi alikuwa na haya ya kujibu: "Nimekueleza kwamba vielelezo vyote ya mtuhumiwa vinashikiliwa nadhani unaelewa maana ya kusema hivyo."
 
Kyela hii ni aibu sana, imekuwaje tumefikia hapa? Kama kweli mbunge anamteka kijana na kumpeleka nyumbani kwake, hilo litakuwa kosa kubwa sana.

Hii habari iliwekwa hapa Jumatano, watu tukaona majungu mpaka walipotoa Nipashe jana.

Mwakyembe mbona anakuwa na watu wa IPPMEDIA kwenye mikutano yake yote Kyela ikiwemo hii anayofanya sasa. Kama hii habari ni kweli alitaka kuuliwa, iweje hao waandishi wasiitoe habari muhimu kama hii siku hiyo hiyo ya Jumatano au hata Alhamisi?

Nafikiri hili jambo litaishia kuwa kama lile la Iringa tu; watu watageuziana vibao mpaka ukweli wote upotee.

Itabidi RPC awe makini sana maana mwanya wowote Dr. Mwakyembe atautumia.

Kwa taarifa nilizo nazo mimi Dr. kule jimboni ana hali ngumu sana, huenda anaamua kutumia hata njia za ajabu ili aonewe huruma kwamba anaandamwa na mafisadi.
 
Natanguliza shukrani ndugu yangu!

Nitakupa story baadaye kuhusiana na Mayasa niliyekuwa naye Jeshini. Mkuu nimechoka na siasa za bongo hasa ukizingatia yaliyotokea week inayoisha hii.

Kila laheri

Masa

Masa,

Huu wimbo nimeupata ONLINE. Unaweza kuupata kwenye PLAYLIST ya George Mwakalinga kama inavyoonyesha kwenye hiyo site. Wimbo wenyewe ni wa 43 kwenye hiyo GeorgeMwakalinga Playlist. Na ili uuvute inabidi uwe na realplayer program ambayo ni free of charge (i hope unayo). Wakati unapiga ukisogeza alama ya mouse, itatokea symbol ya realplayer na ukibonyeza itakuuza wataka kushusha, hapo wee shusha. Ila itaupeleka kwenye mafaili ya Real player. Anyway na jina itaita George Mwakalinga hapo itabidi ukabadili. Ila mwisho kipande kimekatwa, pole sana. Nikipata mwingine ntakutumia ila kwa leo anzia hapa.

http://www.mixpod.com/playlist/18425796 (wimbo wa 43).

Ukishavuta, sema basi asante kwa George Mwakalinga..... hi hiiiii 🙂

NB: Masa, UJUMBE WANGU NIMEU-EDIT. Ila umeni-quate so badili na wako pia ili usije changanya watu hapa nikawa kama vile nakuchonganisha na watu...... Tupo pamoja.
 
Last edited:
Masa,

Huu wimbo nimeupata ONLINE. Unaweza kuupata kwenye PLAYLIST ya George Mwakalinga kama inavyoonyesha kwenye hiyo site. Sijui kama utachukua maana naona humpendi saana Mwakalinga. Anyway kazi kwako. Wimbo wenyewe ni wa 43 kwenye hiyo GeorgeMwakalinga Playlist. Na ili uuvute inabidi uwe na realplayer program ambayo ni free of charge (i hope unayo). Wakati unapiga ukisogeza alama ya mouse, itatokea symbol ya realplayer na ukibonyeza itakuuza wataka kushusha, hapo wee shusha. Ila itaupeleka kwenye mafaili ya Real player. Anyway na jina itaita George Mwakalinga hapo itabidi ukabadili. All in all, jinamizi la MWakalinga litakuwa na wewe siku nzima na sijui itakuwaje wakati unasikiliza huku ukijua huu wimbo nimeiba kutoka kwa Mwakalinga. Ila mwisho kipande kimekatwa, pole sana. Nikipata mwingine ntakutumia ila kwa leo anzia hapa.

http://www.mixpod.com/playlist/18425796 (wimbo wa 43).

Ukishavuta, sema basi asante kwa George Mwakalinga..... hi hiiiii 🙂

Mpwa Sikonge

Thanks a lot, nitaweka thanks kwa Mtanzania si ana mahusiano na George! Nimeutafuta sana huu wimbo....! Jamaa anakipaji cha kutunga RIP Marijan Rajaabu!

Nitamsupport George kama nilivyosema awali naona hamtaki nielewa, aache kuwa pandikizo la mafisadi jamani....simchukii yeye kama yeye...ni ile tabia aliyoonayo ya kutumika. Mwakalinga come up and stand on ur feet....wacha nifaidi Mayasa.......asante Sikonge na napata shida kusema fisadi George Mwakalinga!

Asante napata Mayasa siku nzima
 
Hii stori mbona haijakaa vizuri. Yaani ukitaka kumuuwa mwanasiasa humuvizii kimya kimya nyumbani kwake au hotelini bali unamufuata kwenye mukutano wa hadhara ambapo kutakuwa na mamia au ma-alufu ya watu ambao wamekuja kumusikiliza huyo mwanasiasa. Ili iweje? Kama habari hizo ni kweli basi mimi nasema kuwa huyo muuwaji amepungukiwa na akili! Badala ya kumupeleka jela, mupelekeni kwenye hosipitali ya vichaa!

It doesn’t even pass the smell test, let alone any detailed scrutiny of the events that “really” took place at the meeting that is supported by more than a single media source. Reporters in Tanzania can easily be bought and it does to require a lot of cash to do it, in case you don’t already know this. It is a widely accepted thesis that for a little cash, some Tanzanian newspaper reporters can and are often used to lavish glory and praise on their paymasters who are usually politicians that are seeking to promote a particular point of view for political gain of course. But more often than not, reporters are used to demonize and destroy their paymasters’ political opponents. I hope you are not as naïve as to realize for the very first time that these troubling developments have crept into the Tanzanian political landscape.

If you are good at connecting dots (there won’t be a prize for getting it right🙂 you will undoubtedly reach the conclusion that I personally came to, that is to say, the Dear Dr. and his Kyela entourage and disciples are getting desperate and this is only September 2009, God help us come September 2010!. Until this event, I was a strong supporter of the good Dr. but he is beginning to show a dark and vicious side will put him in a bad light in the public eye, political hero or not. Tanzanians voters of this and future generation will not be easily fooled by political stunts so don’t underestimate our intelligence.

But I also have to confess; if it’s any consolation to the Dear Dr, I am not from Kyela so I won’t be given the opportunity to express my disgust at the ballot box for their politics but I am deeply troubled nonetheless as a human being and a Tanzanian. That’s why I have decided to use this forum to speak up now while I can and you should do the same. The mantra that “desperate times call for desperate and drastic measures” certainly applies here in spectacular fashion. Pretty sad!
Join Date: Mon Aug 2009
Posts: 11
Thanks: 0
Thanked 5 Times in 4 Posts
Rep Power: 0
MLIKUWA MKISOMA KAMA WAGENI SASA MMEJIUNGA
 
Nyumbu,

Hiyo habari ya NIPASHE leo ni uwongo kwa aslimia zaidi ya 90.

Ni kigogo gani mjinga kiasi hicho atakuwa anamtumia sms kijana mdogo na kibarua tu pale Kyela mjini?

Hakuna sms za aina yoyote kama hizo wanazozisema. Kuna kitu Engineer kaandika hapo juu ambacho ni ukweli. Hiyo simu ilizimika ikiwa mikononi mwa wapambe wa Mwakyembe kabla ya kufika polisi Kyela na mpaka RCO anaichukua hakuna polisi wa Kyela aliyekuwa amesoma sms ndani ya simu hiyo. Alisema ataenda kui charge Mbeya na ndipo angesoma hizo sms. Ukiachia mawasiliano ya kawaida ya Mwakalinga na vijana wake wa Kyela hakuna habari za kigogo yeyote.

Wanachofanya NIPASHE ni mwendelezo wa habari za kupika kama jana walivyosema mheshimiwa alitaka kuchomwa kisu.

Kwa habari hii ya leo Mwakalinga ameshawaambia wanasheria wake Dar kuishitaki IPPMEDIA kwa uzushi na kutaka kuleta machafuko Kyela.

Kuweni na subira na ukweli utajulikana muda sio mrefu.

He he heee! Ha ha haa! Bwa ha ha haaaaa!
Ndio maana naipenda JF. The home of great thinkers! Surely, there are some great sinkers!
 
Story za wakati ule za Simba na Yangu kurusha njiwa na wachezaji kuruka ukuta ndio sasa zinatumika kwenye siasa za Bongo. ...no wonder, the country is so poor kwa sababu inaongozwa na story za vijiweni...viongozi wetu wanahitaji TBS....
 
Kyela hii ni aibu sana, imekuwaje tumefikia hapa? Kama kweli mbunge anamteka kijana na kumpeleka nyumbani kwake, hilo litakuwa kosa kubwa sana.

Hii habari iliwekwa hapa Jumatano, watu tukaona majungu mpaka walipotoa Nipashe jana.

Mwakyembe mbona anakuwa na watu wa IPPMEDIA kwenye mikutano yake yote Kyela ikiwemo hii anayofanya sasa. Kama hii habari ni kweli alitaka kuuliwa, iweje hao waandishi wasiitoe habari muhimu kama hii siku hiyo hiyo ya Jumatano au hata Alhamisi?

Nafikiri hili jambo litaishia kuwa kama lile la Iringa tu; watu watageuziana vibao mpaka ukweli wote upotee.

Itabidi RPC awe makini sana maana mwanya wowote Dr. Mwakyembe atautumia.

Kwa taarifa nilizo nazo mimi Dr. kule jimboni ana hali ngumu sana, huenda anaamua kutumia hata njia za ajabu ili aonewe huruma kwamba anaandamwa na mafisadi.
Kama kuna mtu asiyempenda Dr basi huyo ni fisadi au ni sehemu ya mafisadi. Kwa nini bambumbile na wenzako mnataka kuwachonganisha wana Kyela kwa Watanzania wachukiao mafisadi? Kwa TAARIFA YENU Dr akitaka kugongea jimbo lolote Mbeya atapeta kwa kura kama alizozipata Mbowe kwenye mkutano wa jana. Acha uzushi na uchonganishi,wakati Dr akisoma ripoti ya RICHMOND mlikuwa wa kwanza kumpongeza leo kwa sababu ya njaa zenu(kuhongwa na mafisadi) mnamgeuka. Mtakufa na njaa zenu kumbukeni WALIOZOEA VYA KUCHINJA VYA KUNYONGA HAWAWEZI.
 
Nyumbu,

Hiyo habari ya NIPASHE leo ni uwongo kwa aslimia zaidi ya 90.

Ni kigogo gani mjinga kiasi hicho atakuwa anamtumia sms kijana mdogo na kibarua tu pale Kyela mjini?

Hakuna sms za aina yoyote kama hizo wanazozisema. Kuna kitu Engineer kaandika hapo juu ambacho ni ukweli. Hiyo simu ilizimika ikiwa mikononi mwa wapambe wa Mwakyembe kabla ya kufika polisi Kyela na mpaka RCO anaichukua hakuna polisi wa Kyela aliyekuwa amesoma sms ndani ya simu hiyo. Alisema ataenda kui charge Mbeya na ndipo angesoma hizo sms. Ukiachia mawasiliano ya kawaida ya Mwakalinga na vijana wake wa Kyela hakuna habari za kigogo yeyote.

Wanachofanya NIPASHE ni mwendelezo wa habari za kupika kama jana walivyosema mheshimiwa alitaka kuchomwa kisu.

Kwa habari hii ya leo Mwakalinga ameshawaambia wanasheria wake Dar kuishitaki IPPMEDIA kwa uzushi na kutaka kuleta machafuko Kyela.

Kuweni na subira na ukweli utajulikana muda sio mrefu.

labda nami niulize ni kibarua gani huyu tena kijana mdogo wa kyela anaweza kuwa na mwakili wake dar akawaambia waishtaki IPPMEDIA?au kuna mwakalinga mwingine yupo nyuma ya huyu mwakalinga kibarua?
vinginevyo naaza kuamini mwakyembe amefanya kazi ya ziada kuleta maendeleo mpaka vibarua wa jimbo lake wana wanasheria wao
big up sana mwakyembe kwa hilo.
 
Back
Top Bottom