Sikonge,
Hii habari mimi niliituma moderators wa JF wakasema ni majungu.
Ni kwamba huyo kijana alikamatwa akiwa ana record mkutano wa mbunge kwa kutumia simu. Baada ya hapo wakamfungia kwenye gari, kisha wakampeleka nyumbani kwa mbunge Ikolo na kuanza kumpekua, wakamnyang'anya simu, wakasoma sms zote.
Walimkamata saa nane mchana lakini wakamfikisha polisi saa mbili usiku wakati huo tayari jeshi la polisi limeshaanza kumtafuta.
Walipoona balaa wakazua case ya kwamba alikuwa na mwenzake ambaye alikuwa na kisu na walitaka kumdhuru mbunge. Polisi hata wamejua kisu kilinunuliwa wapi mjini. Ni yale yale ya ajali ya Iringa na kusingizia kugongwa na lori kwa nyuma.
Kwa taarifa za chini chini, RCO na kundi lake wameshathibitisha kwamba ni uwongo mtupu na sasa wanaandaa taarifa ambayo kila mtu anaisubiri kwa hamu maana kuna mtu atafungwa safari hii.
Huwezi kumteka kijana na ukampeleka nyumbani kwako na kumtesa masaa sita wakati hiyo kazi ni ya polisi, tena polisi wenyewe wako sio mbali na hapo mkutano ulipokuwa unafanyika. Hayo yote yanafanywa mbunge anashiriki, mtu ambaye inatakiwa aongoze kwa kulinda sheria.
Nipashe hawataji muda kwasababu haiingii akilini umkamate mtu aliyetaka kumuua mbunge saa nane na umfikishe polisi saa tatu usiku.
Wengine hapa tumetulia na uwongo huu utaumbuliwa mno. Someni na nipashe ya leo muone waliyoyaandika. Ni magazeti ya Mengi yanatumiwa vibaya na watu ambao wanataka wabaki madarakani kwa njia zote. Kila mtu anasubiri RPC wa Mbeya anonge.