Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Mkuu Mtanzania[ Malafyale] nadhani wewe ni mzoefu wa siasa za mkoa huu, na hili la wilaya ya Chunya unalionaje? Naamini unaifahamu Chunya vizuri sana, kuna kitu gani kinachokwaza maendeleo huko ilihali wilaya ina rasilimali kibao?

Bulesi,

Inabidi nikiri kwamba siijui Chunya kabisa. Afadhali hata Mbozi nimewahi kufika na kukaa kwa muda lakini Chunya hata kuikanyaga sijawaji.

Mimi najua zaidi Mbeya, Rungwe, Kyela na Ileje.
 
Mkuu Mtanzania[ Malafyale] nadhani wewe ni mzoefu wa siasa za mkoa huu, na hili la wilaya ya Chunya unalionaje? Naamini unaifahamu Chunya vizuri sana, kuna kitu gani kinachokwaza maendeleo huko ilihali wilaya ina rasilimali kibao?

Heshima mbele mkuu....Tatizo la Chunya kuwa nyuma kimaendeleo hata mimi silijui hasa maana ukiangalia kadiri muda unavyozidi kwenda wilaya ndo inazidi kurudi nyuma kimaendeleo..angalia maeneo kama Lupa Tingatinga,Makongolosi,Mkwajuni,Matundasi,Saza hata na Chunya mjini maeneo haya yalikuwa yanakuja juu sana kimaendeleo katika miaka ya 80 na 90 mwanzoni lakini ukienda sasa hivi utashangaa jinsi kulivyochakaa,Saza,Mkwajuni,Matundasi na Makongolosi miaka nenda rudi kumekuwa na dhahabu nyingi tu,mtu unategemea kwamba utajiri huu wa dhahabu ndo ingekuwa kichocheo cha maendeleo katika wilaya hii lakini ndo kwanza wilaya yazidi kudidimia kimaendeleo..Lupa kwa miaka mingi tu wamekuwa ni wakulima wazuri wa zao la Tumbaku lakini pamoja na tumbaku Lupa nayo ndo hivo tena yazidi kurudi nyuma kimaendeleo...Kwa miaka ya nyuma vijiji vya Kanga,Galula,Tete,Mwambani,Mbuyuni,Totowe,Isanzu na Maleza vilikuwa ni maarufu sana kwa ulimaji wa zao la Pamba watu wa maeneo haya walianza kunufaika na kutajirika kwa kilimo cha Pamba lakini baada ya serikali kusimamisha kilimo cha Pamba katika maeneo haya hali ikaanza kuwa mbaya maana hakukuwa na zao mbadala ambalo lingechukua nafasi ya Pamba...Pia Chunya kuna Ziwa Rukwa ambalo lina samaki wengi tu lakini cha ajabu ni kwamba mpaka sasa wavuvi bado wanatumia njia duni katika uvuvi wao,boti za uvuvi ni za kuhesabu,wananchi wa vijiji vinavyopakana na ziwa Rukwa vya Sazafosi,Mbangala,Maleza na Udinde wakiwezeshwa kwa kupewa/kukopeshwa nyenzo za kisasa za uvuvi wanaweza wakasaidia katika kuleta maendeleo ya wilaya ya Chunya,Pia Chunya kuna utajiri mkubwa wa miti ya asili ya mbao ya mninga katika maeneo ya Kambikatoto,Ngwala,Mafyeko,Matwiga,Kininga,Mkola nk,vilevile kuna hifadhi ndogo ya asili ya Rungwa,kuna mlima Kwimba...Kwa kweli Chunya kuna Rasilimali nyingi mno,tatizo ni viongozi wameshindwa kuwa wabunifu juu ya nini kifanyike katika kuzifanyia kazi rasilimali zilizopo ambazo kama zingetumika ipasavyo Chunya ingekuwa mbali sana kimaendeleo...Viongozi wilayani wameshindwa kuwatafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao wangeweza kuja kuwekeza kwenye sekta za madini,kilimo na uvuvi...Mji mdogo kama wa Mkwajuni ulikuwa na tawi la Benki ya NMB lakini tawi hilo lilishafungwa(bila sababu yoyote ya msingi) miaka mingi tu majengo tu yamebaki pale(nasikia yameuzwa) so watu wa vijiji kama Kanga,Iseche,Mbala,Mkwajuni,Totowe,Saza,Maleza,Mbuyuni,Galula,Gua,Udinde,Mbangala,Miembeni na Patamela inabidi wasafiri mpaka Chunya mjini kwa ajili ya huduma za kibenki katika benki ya NMB tawi la Chunya ambako ni mbali mno...Inasikitisha kwa kweli
 
sehemu kubwa ya tanzania mambo ndo hivyohivyo.

serikali ingeidentify sehemu kadhaa na maliasili zilizopo sehemu hizo ambazo kama zingetumika vizuri zitasogeza mbele maendeleo ya watu wa eneo hilo. halafu cha kufuata ingekuwa kutoa mafunzo/utaalamu, nyenzo (vifaa) na mitaji. hii ingefanyika kwa mtu mmoja mmoja au kwa vikundi.

na viongoz wa kuteuliwa wangekuwa wanapimwa ni kwa kiasi gani wameweza kutumia rasilimali za eneo husika ktk kuwaletea watu maendeleo.

kwa mfano, bos mwakipesile ilikuwa aulizwe (kwenye interview) kama anujua mkoa ule na rasilimali zilizopo kule na mazingira yake. ingetakiwa aonyeshe jins gani anaweza kuwaongoza watu wa mbeya kutoka ktk umaskini

kama kitu kama hiki kisingefanyika kwa wakuu wa mikoa bas angalau kingefanyika ktk ngaz ya wilaya

na mazingira yangetengenezwa ili mtu akiharibu asisingizie serikali kuu au mtu yeyote
 
Heshima mbele mkuu....Tatizo la Chunya kuwa nyuma kimaendeleo hata mimi silijui hasa maana ukiangalia kadiri muda unavyozidi kwenda wilaya ndo inazidi kurudi nyuma kimaendeleo..angalia maeneo kama Lupa Tingatinga,Makongolosi,Mkwajuni,Matundasi,Saza hata na Chunya mjini maeneo haya yalikuwa yanakuja juu sana kimaendeleo katika miaka ya 80 na 90 mwanzoni lakini ukienda sasa hivi utashangaa jinsi kulivyochakaa,Saza,Mkwajuni,Matundasi na Makongolosi miaka nenda rudi kumekuwa na dhahabu nyingi tu,mtu unategemea kwamba utajiri huu wa dhahabu ndo ingekuwa kichocheo cha maendeleo katika wilaya hii lakini ndo kwanza wilaya yazidi kudidimia kimaendeleo..Lupa kwa miaka mingi tu wamekuwa ni wakulima wazuri wa zao la Tumbaku lakini pamoja na tumbaku Lupa nayo ndo hivo tena yazidi kurudi nyuma kimaendeleo...Kwa miaka ya nyuma vijiji vya Kanga,Galula,Tete,Mwambani,Mbuyuni,Totowe,Isanzu na Maleza vilikuwa ni maarufu sana kwa ulimaji wa zao la Pamba watu wa maeneo haya walianza kunufaika na kutajirika kwa kilimo cha Pamba lakini baada ya serikali kusimamisha kilimo cha Pamba katika maeneo haya hali ikaanza kuwa mbaya maana hakukuwa na zao mbadala ambalo lingechukua nafasi ya Pamba...Pia Chunya kuna Ziwa Rukwa ambalo lina samaki wengi tu lakini cha ajabu ni kwamba mpaka sasa wavuvi bado wanatumia njia duni katika uvuvi wao,boti za uvuvi ni za kuhesabu,wananchi wa vijiji vinavyopakana na ziwa Rukwa vya Sazafosi,Mbangala,Maleza na Udinde wakiwezeshwa kwa kupewa/kukopeshwa nyenzo za kisasa za uvuvi wanaweza wakasaidia katika kuleta maendeleo ya wilaya ya Chunya,Pia Chunya kuna utajiri mkubwa wa miti ya asili ya mbao ya mninga katika maeneo ya Kambikatoto,Ngwala,Mafyeko,Matwiga,Kininga,Mkola nk,vilevile kuna hifadhi ndogo ya asili ya Rungwa,kuna mlima Kwimba...Kwa kweli Chunya kuna Rasilimali nyingi mno,tatizo ni viongozi wameshindwa kuwa wabunifu juu ya nini kifanyike katika kuzifanyia kazi rasilimali zilizopo ambazo kama zingetumika ipasavyo Chunya ingekuwa mbali sana kimaendeleo...Viongozi wilayani wameshindwa kuwatafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao wangeweza kuja kuwekeza kwenye sekta za madini,kilimo na uvuvi...Mji mdogo kama wa Mkwajuni ulikuwa na tawi la Benki ya NMB lakini tawi hilo lilishafungwa(bila sababu yoyote ya msingi) miaka mingi tu majengo tu yamebaki pale(nasikia yameuzwa) so watu wa vijiji kama Kanga,Iseche,Mbala,Mkwajuni,Totowe,Saza,Maleza,Mbuyuni,Galula,Gua,Udinde,Mbangala,Miembeni na Patamela inabidi wasafiri mpaka Chunya mjini kwa ajili ya huduma za kibenki katika benki ya NMB tawi la Chunya ambako ni mbali mno...Inasikitisha kwa kweli

Nimezaliwa kijiji cha Makongolosi. Nimesoma shule ya msingi Makongolosi, nimesoma O level Lupa then nikahamia Mkwajuni. A level nikatoka wilaya ya Chunya, nikasoma Njombe kabla ya UDSM. Na sasa nipo Finland for Masters of Science in Technology. Wazazi wangu ni wazawa wa Chunya. Hivyo basi mimi ni mwanachunya.

Ninakubaliana na wewe kwa maelezo yako lakini Naomba utueleze, specifically Makongolosi, kwanini Unasema maendeleo ya mwaka 1980s na 90s ni mazuri kuliko ya Sasa??
 
Mbalawata,nami pia nimeishi Makongolosi,kimsingi nimesema maeneo haya yalikuwa yanakuja juu sana kimaendeleo,ukiangalia kasi ambayo Makongolosi ilikuwa inakuja juu kipindi cha miaka ya 80 mwishoni na 90 mwanzoni kama kasi ile ingeendelea Makongolosi sasa hivi ingekuwa habari nyingine mzee,mwaka jana nilikuwa Tz likizo na nikapita Makongolosi,Mwaoga(kumechakaa sana),Matundasi na Chunya mjini ukweli ni kwamba hakuna chochote cha kujivunia kuwa Makongolosi imeendelea,nakumbuka enzi zile mtu ukifika Makongolosi unakuwa kama umefika mjini palikuwa pazuri kuliko hata Chunya wilayani,Enzi za EDEN lodge,PARADISE na SUKUMALAND,Watu kama akina ERASMO MKONGOMA alipopata hela si unaona kanymba kale kazuri alikokajenga???,kubali kataa lakini mimi kwa mtizamo wangu naona Chunya yazidi kurudi nyuma kimaendeleo
 
Mbalawata yawezekana twafahamiana,angalia PM
 
Sasa ndugu yangu nimekuelewa kuwa unazungumzia kasi ya maendeleo katika wilaya yangu ya Chunya. Ni kweli kabisa kasi haiwezi fananishwa na ya miaka 90s na 80s (Japo kuwa mimi ni wajuzijuzi tu - only 27 years old). Kuna kipindi niliwai mwambia mheshimiwa mmoja kuwa HIVI LENGO LA SERIKALI KATIKA KUENDELEZA WILAYA YA CHUNYA LIPOJE? AU SERIKARI INATAKA WILAYA YA CHUNYA IWE MAKUMBUSHO ILI IFIKAPO MIAKA YA MBELE WAWE WANASEMA TANZANIA MWAKA 1960S MPAKA 2020S ILIKUWA HIVI (wakionesha kidole wilaya ya Chunya). Dhahabu zipo, je wanaochimba ni akina nani? Wakishazipata wangapi wanaendeleza wilaya ya chunya, na wangapi wanatoka wilaya ya chunya na kwenda wilaya zingine? Nakubali tunautajili kama ulivyoeleza, but we are poor!!!!!!!!!!
Asante
 
Ndo hivyo mkuu,GEITA na KAHAMA kuna dhahabu kama ilivyo Chunya,na Chunya dhahabu imeanza kuchimbwa tangu kipindi cha mkoloni,sasa linganisha maendeleo ya Chunya na yale ya Kahama na Geita ndo utapata jibu...
 
Mbalawata angalia PM yako kuna ujumbe nimekutumia,maana yaonekana tunafahamiana sana..
 
Nimezaliwa kijiji cha Makongolosi. Nimesoma shule ya msingi Makongolosi, nimesoma O level Lupa then nikahamia Mkwajuni. A level nikatoka wilaya ya Chunya, nikasoma Njombe kabla ya UDSM. Na sasa nipo Finland for Masters of Science in Technology. Wazazi wangu ni wazawa wa Chunya. Hivyo basi mimi ni mwanachunya.

Ninakubaliana na wewe kwa maelezo yako lakini Naomba utueleze, specifically Makongolosi, kwanini Unasema maendeleo ya mwaka 1980s na 90s ni mazuri kuliko ya Sasa??

Mbalawata angalia PM yako kuna ujumbe nimekutumia,maana yaonekana tunafahamiana sana..

Nimeona PM kuna ujumbe wako. Nimejibu

Hizi ndizo siasa za Mbeya zenyewe! Teh!! teh!! teh!! teh!!
 
Hizi ndizo siasa za Mbeya zenyewe! Teh!! teh!! teh!! teh!!

Heshima yako mkulu,sidhani kama kuna tatizo kwa watu wanaofahamiana kukutana humu na kutumiana PM,vitu vingi tu kuhusu siasa za Mbeya vimeelezwa hapo juu na ikatokea kwa bahati tu kwamba mimi na Mbalawata twafahamiana,so siasa za Mbeya zitaendelea tu kuwepo mkulu(kama zilivyoainishwa hapo juu hivi vingine ni vijimambo tu...be blessed,,
 
Hakuna tatizo kabisa, wala sijakulamuni aisee, labda umenielewa vibaya tu.

Kama mheshimiwa Mbalawata atagombea ubunge wa Chunya nadhani sasa hutashindwa kumpa kura yako, teh!!! teh!!!! teh!!!!

Take it easy.
 
Nimekusoma mkulu,Mbalawata akigombea lazima nimpe kura yangu bwana 😀😀...be blessed mkuu
 
Hakuna tatizo kabisa, wala sijakulamuni aisee, labda umenielewa vibaya tu.

Kama mheshimiwa Mbalawata atagombea ubunge wa Chunya nadhani sasa hutashindwa kumpa kura yako, teh!!! teh!!!! teh!!!!

Take it easy.

Masikini Mbalawata, ataweza kweli????
 
Wakuu,

Nimeona hii inahusu Chunya. Sijui ni kweli au ndio siasa zimeanza kwa ajili ya 2010.

Jimbo changa la Songwe lajikongoja kuhimili mikikimikiki ya maendeleo
Oscar Mbuza
Daily News; Monday,December 29, 2008 @20:05

Jimbo changa la Songwe lajikongoja kuhimili mikikimikiki ya maendeleo
Jimbo la Songwe ni jimbo changa lililotokana na kugawanywa kwa lililokuwa Jimbo la Chunya. Kwa pamoja jimbo la Songwe na lile la Lupa yana ukubwa wa kilometa za mraba 29,219, sawa na asilimia 46 ya eneo lote la Mkoa wa Mbeya.

Jimbo la Songwe linaundwa na kata za Gua, Ngwara, Kapalala, Mbangala, Mkwajuni, Mbuyuni, Kanga, Galula na Totoe, huku likiwa na tarafa mbili za Kwimba na Songwe.Mbunge wa Jimbo la Songwe ni Dk. Guido Sigonda, ambaye alifanikiwa kulitwaa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Awali Mbunge wa Jimbo hilo alikuwa Paul Ntwina.

Dk. Sigonda, mmoja wa waliokuwa walinzi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania enzi hizo, alifanikiwa kutwaa taji hilo, baada ya kushinda katika kura za maoni na katika Uchaguzi Mkuu.

Alipita bila kupingwa na kuwa mmoja kati ya wagombea wachache wa ubunge waliopita bila kupingwa. Wakazi wa upande wa Bonde la Songwe, waliomba kuwa na jimbo linalojitegemea, kwa madai kuwa hatua hiyo ingeweza kuharakisha maendeleo yao ya kiuchumi na kijamii, kuliko ilivyokuwa awali ambapo upande huo wa Songwe na upande wa Chunya mjini, walikuwa katika jimbo moja.

Wakati sasa karibu miaka kumi inakaribia tangu uamuzi huo ufanywe, wakazi wengi wa upande wa Bonde la Songwe wanasema kupatikana kwa Jimbo la Songwe kumewezesha kufanyika kwa mambo mengi ya maendeleo kwa muda mfupi, kutokana na Mbunge wao kusimamia vilivyo utekelezaji wa shughuli hizo za maendeleo.

Hali halisi ya maisha Mji wa Mkwajuni ndiko yaliko Makao Makuu ya Jimbo la Songwe. Ni mji uliochangamka kutokana na kuwa na pilikapilika nyingi za kimaisha na hasa uvuvi kutokana na mji huo kuwa jirani sana na Ziwa Rukwa.

Kuwapo jirani kwa Ziwa Rukwa na pia kuwapo kwa Bonde la Songwe ambalo linatokana na Mto Songwe unaoingia katika Ziwa Rukwa kumefanya eneo hilo kuwa na shughuli kubwa mbili za uvuvi na kilimo na kuwaingizia wakazi wa maeneo hayo fedha za kujikimu kimaisha na kimaendeleo.

Wakazi wa Jimbo la Songwe pia ni wafugaji wazuri wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na mifugo ya aina nyingine. Kama ilivyo katika maeneo mengi nchini, hali ya maisha katika Jimbo la Songwe ni ya kawaida. Hali ya usalama ni ya wastani, Songwe pia imekuwa ikiandamwa na matukio ya ujambazi ya hapa na pale.

Kwa ujumla ujambazi unaojitokeza wilayani Chunya ni ule wa kutumia silaha ambapo majambazi huteka magari na kupora mali za wananchi. Hata hivyo lipo tatizo lingine kubwa kwa upande huu wa Jimbo la Songwe nalo ni la kuwapo kwa matukio ya ugomvi wa mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.

Ugomvi huu hutokea kwa msimu hasa wakati wa kiangazi ambapo wafugaji hupeleka mifugo yao mashambani kabla wakulima hawajamaliza kuvuna mazao yao. Hali ilikuwa mbaya zaidi Julai mwaka huu ambapo yalitokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Mapogoro na kusababisha vifo vya watu watatu.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Fatuma Kimario, anasema tatizo hilo wameliona na tayari wamelichukulia hatua. "Wilaya imepitisha sheria ndogo ya hifadhi ya mazingira na kutoa maelekezo kwa vijiji kuchagua uongozi wa jadi wa wakulima na wafugaji utakaoshirikiana na serikali za vijijini kusimamia sheria hizo," anasema.

Mkuu huyo wa Wilaya anasema Wilaya kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama imekuwa ikisimamia sheria kwa kuwachukulia hatua kali wahusika wa mapigano hayo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Kama ilivyo kwa wenzao wa Lupa, hali ya maisha ya wananchi wa kawaida wa Jimbo la Songwe pia si ya kuridhisha sana kwani wengi wao ni masikini. Hii pia ni changamoto kwa Mbunge Dk. Sigonda. Takwimu za pato la mkazi wa Songwe ni Sh 168,350 kwa mwaka. Hii ni sawa na pato kwa mwaka kwa majirani zao wa Lupa ambao wao wanajivunia utajiri wa madini ya dhahabu.

Mkazi wa Mkwajuni, Isihaka Minzi anasema chanzo kikubwa cha umasikini kwa wakazi wa Jimbo la Songwe ni ukosefu wa elimu unaowafanya kushindwa kubuni mikakati ya uhakika ya kujipatia na kuzitumia ipasavyo fedha wanazozipata.

"Kipato kinapatikana, tunakamata pesa kidogo lakini bado hatujui tunaweza kuzizalisha vipi ili tuweze kuondokana na lindi hili la umasikini. "Nadhani viongozi wetu wanawajibika kutusaidia kutupa elimu ya ujasiriamali ili tuweze kujikwamua kiuchumi," anasema Minzi.

Hali ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya si mbaya kwani rekodi zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2007/2008, wilaya hiyo ilikisia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 1.039, ikiwa ni mapato ya ndani ingawa iliweza kukusanya Sh milioni 927.664 sawa na asilimia 89.2. Katika mwaka wa fedha wa 2008/2009, halmashauri hiyo inakisia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 1.158, ikiwa ni mapato yake ya ndani.

Katika Jimbo la Songwe upo mchanganyiko wa wananchi wa kawaida na watumishi wa serikali na taasisi nyingine za serikali na zisizo za serikali zikiwamo pia taasisi za dini. Hata hivyo Chunya ina upungufu kiasi wa watumishi wenye taaluma mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Fatuma Kimario, anakiri wilaya hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa watumishi. Anasema kati ya watumishi 1,920 wanaohitajika kulingana na ikama, ni watumishi 1,349 tu ndio waliopo hivi sasa ikiwa ni sawa na asilimia 70 ya mahitaji. Anasema hatua hii inafanya wilaya nzima ya Chunya kuwa na upungufu wa watumishi 570 sawa na asilimia 30.

Uchunguzi umebaini sababu mbalimbali zinazosababisha watumishi kushindwa kuripoti katika maeneo ya kazi wanayopangiwa wilayani Chunya, sababu kubwa ni imani kwamba Chunya ina mazingira magumu.

Hatua hii imekuwa inafanya watumishi wenye sifa kutojitokeza kuomba kazi pindi nafasi za ajira zinapotangazwa kutokana na mtazamo huo hasi. Wapo pia wafanyakazi ambao wameripoti lakini kutokana na mazingira yalivyo wanaomba uhamisho kwa kutoa visingizio mbalimbali kama vile ndoa au matatizo ya afya, lakini ukweli ni kwamba hawataki kufanya kazi Chunya.

Mkuu wa Wilaya anasema serikali imeliona suala hilo la upungufu wa watumishi na inaweka mikakati ya kukabiliana nalo. Anasema moja ya mikakati ni kuweka makisio ya maombi ya ajira toka serikalini. Hatua hii imefanikisha wilaya hiyo kuidhinishiwa ajira ya watumishi 251 mwaka huu wa 2008/2009.

Wilaya imeandaa mpango wa motisha kwa watumishi, mfano kuwapatia huduma ya usafiri watumishi waliopo maeneo ya mbali wakati wanapofuata mishahara benki ambayo ipo Chunya mjini. Motisha nyingine inayotolewa kwa watumishi wilayani Chunya ni kulipiwa pango la nyumba kwa wakuu wa idara, lakini pia kuwajengea nyumba watumishi, kuwapatia baiskeli watendaji wa vijiji, pikipiki maofisa ugani, watendaji kata, tarafa na maofisa wa afya.

Mwamko wao katika elimu Kipaumbele cha Serikali ya wilaya ni kutoa elimu bora katika mazingira bora na ya kuvutia. Ipo mikakati ya kuridhisha ya kuendeleza elimu ya awali, elimu ya msingi na elimu ya sekondari. Wakazi wengi wa Jimbo la Songwe wanasifu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mbunge wao katika kuhakikisha kuwa miradi ya uendelezaji wa elimu inafanikiwa katika Jimbo lao la Songwe.

Atanas Mbawala wa Mkwajuni anasema yapo mabadiliko makubwa katika uboreshaji wa sekta ya elimu jimboni humo ingawa anasema yapo matatizo ya hapa na pale. Kwa ujumla Wilaya ya Chunya ina madarasa ya awali 155, yenye jumla ya wanafunzi 4,109. Madarasa hayo yapo kwenye shule za msingi 87. Mkuu wa Wilaya hiyo anasema shule za msingi 12 zilizobaki zitaanzisha madarasa ya awali mwakani ili kufanya shule zote za msingi kuwa na madarasa ya awali.

Kwa upande wa shule ya msingi, Chunya ina shule 99 zenye jumla ya wanafunzi 47,647. Uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi umekuwa ukiongezeka. Kwa ujumla kazi hiyo imefikia kiwango cha asilimia 94.5. Mkuu wa Wilaya, Kimario anasema kiwango cha ufaulu tangu mwaka 2005 hadi 2007, kimekuwa kikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 60.

Anasema mwaka 2006, kiwango hicho kiliongezeka kwa zaidi ya asilimia 60. Anasema mwaka huu ni mategemeo ya wilaya hiyo kwamba kiwango hicho cha ufaulu kitaongezeka hadi kufikia asilimia 80 na wanafunzi wote wataendelea na elimu ya sekondari. Zipo kasoro katika ukuaji wa elimu katika Wilaya hiyo ya Chunya, kasoro kubwa ikiwa ni wanafunzi kukatiza elimu baada ya kuanza masomo, sababu kubwa ikiwa ni mimba na utoro.

Uchunguzi umebaini kuwa chanzo kikubwa cha watoto wa kike kukatiza masomo ni kutokana na kujiingiza katika shughuli za kiuchumi na hasa uchimbaji wa madini ya dhahabu, kilimo cha tumbaku, uvuvi na ufugaji. Kutokana na kushamiri kwa uchimbaji mdogo wa dhahabu yapo madai kuwa wanaume wachimbaji wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi kwa fedha na kuwakatiza masomo.

Wavuvi na wafanyabiashara wa samaki pia wanatajwa kuwa wamekuwa wakichangia utoro kwa wanafunzi kutokana na kuwashirikisha katika biashara hiyo lakini pia kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike na hivyo kuwasababishia mimba.

Mkuu wa Wilaya anasema ipo kasoro nyingine katika elimu wilayani humo ya wilaya kukabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 588, nyumba za walimu 966, matundu ya vyoo 1,413, madawati 7,671, viti 1,592, meza 1,575, stoo 103 na ofisi za walimu 79. Upo mkazo wa kukabiliana na kasoro hizo.

Wilaya nzima ya Chunya ina jumla ya shule 19 za sekondari, kati ya hizo 17 ni za serikali na shule mbili ni za Jumuiya ya Wazazi. Hali hii ni tofauti na mwaka 2005 wakati wilaya hiyo ilipokuwa na shule tano tu za sekondari.

Pamoja na matatizo ya hapa na pale lakini uongozi wa Serikali ya Wilaya hiyo upo katika mpango wa kuanzisha kidato cha tano katika shule za sekondari za Kiwanja na Maweni mwakani. Mkuu wa Wilaya anataja hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na kasoro katika elimu ya sekondari kuwa ni shule za kutwa kuwa na mabweni ili kuepusha vishawishi vibaya kwa wanafunzi.

Mkakati mwingine ni kila shule ya sekondari kuwa na maktaba za muda wakati mpango wa kudumu ukiendelea kutekelezwa, wananchi kuendelea kuhimizwa kujenga na kuendeleza shule na kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya wanaowapa mimba wanafunzi.

Changamoto katika sekta ya afya Wilaya ya Chunya ina hospitali mbili, moja ya serikali na nyingine ya dhehebu la Katoliki. Vipo vituo vya afya viwili na zahanati 34. Kwa mujibu wa Kimario wilaya hiyo ina upungufu wa vituo vya afya 21 na zahanati 38.

Anasema zipo jitihada za makusudi zinazoendelea kufanyika ili kukabiliana na uhaba huo kwa kutumia nguvu za wananchi na msaada kutoka serikali kupitia mpango kabambe wa kila kijiji kuwa na zahanati yake. Wilaya hiyo haiko nyuma kuendeleza Mfuko wa Afya ya Jamii ili kuleta unafuu wa tiba miongoni mwa wananchi na kuendeleza mapambano dhidi ya Ukimwi.

Wilaya hiyo imeendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kupima virusi vya Ukimwi kwa hiyari tangu Oktoba wakati mpango huo ulipozinduliwa rasmi mkoani Mbeya. Hata hivyo hali ya afya jimboni humo si ya kuridhisha sana. Ingawa ipo hospitali ya wilaya, bado si ya kuridhisha sana, majengo pamoja na huduma zinazotolewa na hospitali hiyo si za kuridhisha sana.

Sekta ya maji Wilaya hii ya Chunya ni miongoni mwa wilaya kame nchini inayotegemea maji kutoka vyanzo vya maji vilivyo chini ya ardhi. Asilimia 95 ya vyanzo vya maji ni visima. Kati ya idadi hiyo ya visima, visima vifupi ni 67 na visima virefu ni 42, jumla inayofanya wilaya nzima kuwa na visima 109.

Vyanzo vingine vilivyopo ni maji ya mtiririko ambavyo ni vya miradi sita tu ya maji katika wilaya nzima. Kati ya visima virefu 42 vilivyopo wilayani Chunya, visima vinne viko katika Mji wa Chunya ambavyo kwa pamoja vina uwezo wa kutoa maji kiasi cha meta za ujazo 153 kwa siku, sawa na asilimia 14.2 ya mahitaji halisi ya wakazi wapatao 18,000 wa Mji wa Chunya, wenye jumla ya mahitaji ya meta za ujazo 1,080 kwa siku hivyo kufanya wastani wa huduma ya maji kuwa asilimia 34 tu.

Mkuu wa Wilaya anakiri kuwapo kwa upungufu huo mkubwa wa maji kwa kusema kuwa hali ya huduma ya maji katika Wilaya ya Chunya ni ya kiwango cha chini sana ambapo ni asilimia 35.5 tu ya wakazi wa wilaya hiyo ndio wenye uhakika wa kupata huduma ya maji.

Anasema tatizo la maji ni miongoni mwa kero kubwa za wananchi waishio mjini na vijijini. Katika juhudi za kutatua tatizo hilo la maji, Kimario anasema wilaya imefanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahusisha wadau kama Mamlaka na Kampuni za Tumbaku na mashirika ya VECO na DADS ili kusaidia kuwaokoa wakazi wa Chunya.

Wadau wengine wanaohusishwa ili kuweza kuokoa jahazi hilo ni Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Wizara yenyewe ya Maji na Umwagiliaji ambao kwa pamoja wanasaidia kuchimba visima vifupi na virefu katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Anasema hata hivyo bado wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa upatikanaji wa maji safi na salama. Anaiomba serikali kuipatia wilaya hiyo ili kupunguza tatizo hilo sugu. Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inakiri kuwapo kwa tatizo hili la maji lakini inasema jitihada mbalimbali zinafanyika ili kulikabili.

Hadi hivi sasa kila Kata ina kisima cha maji ingawa hakikidhi mahitaji halisi ya wananchi. Sekta ya kilimo Kwa ujumla wake Wilaya ya Chunya, ina hekta 230,050 zinazofaa kwa kilimo. Anasema kati ya hizo, hekta 117,955 zinalimwa kwa sasa na hekta 3,900 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji ingawa ni hekta 1,150 zinazotumika kwa umwagiliaji mdogo mdogo wa asili katika vijiji vya Ifumbo, Ngwala, Matwiga, Totowe na Mwambani.

Mkuu wa Wilaya anasema ili kufanikisha malengo ya kulima hekta 9,500 katika msimu huu, wilaya hiyo inaendelea kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo. Tumbaku ni zao kuu la biashara katika Wilaya ya Chunya. Zao hili linachangia zaidi ya theluthi moja ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa mwaka.

Uzalishaji wa mazao ya chakula ulipanda kutoka tani 105,050 kwa mwaka 2006/2007 hadi kufikia tani 244,150 kwa mwaka 2007/2008, hatua hii ikiwa inatokana na kuongezeka kwa mvua. Kwa mwaka 2007/2008, mahitaji ya mbolea viwandani yalikuwa tani 650. Hata hivyo kiasi kilichotolewa kilikuwa tani 473.12 tu kupitia mpango wa mbolea ya ruzuku ya serikali.

Ili kufanikisha malengo ya kilimo, wananchi walihamasishwa kutumia mbolea za asili ambapo tani 412,200 zilitumika. Kama ilivyoelezwa awali, wakazi wa Jimbo hili la Songwe wanao utajiri mkubwa zaidi wa kuwapo kwa Bonde la Songwe ambalo lipo katika maeneo ya jirani na mji mdogo wa Mkwajuni.

Ni katika bonde hilo, ndipo Mto Songwe, unaingia ndani ya Ziwa Rukwa, na kufanya eneo lote la bonde hilo kuwa lenye rutuba na linaloweza kufaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa msimu wote wa mwaka, hatua inayoweza kuwapatia fedha nyingi.

Hata hivyo wakazi wa Mkwajuni, walimwambia Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira aliyewatembelea hivi karibuni kwamba, wananchi wa maeneo ya jirani na bonde hilo hawanufaiki na urithi huo. Wanasema kutokana na Mto Songwe kuwa mali ya nchi mbili za Tanzania na Malawi, wakazi wa pembezoni mwa mto huo hawaruhusiwi kufanya shughuli yoyote ya kilimo kando kando ya mto huo na hivyo kushindwa kuitumia ipasavyo fursa hiyo.

Hata hivyo, Wassira anawatoa wasiwasi wakazi hao kwa maelezo kwamba serikali inaangalia uwezekano wa kupitisha sheria itakayowaruhusu kufanya shughuli za kilimo kidogo kando kando ya Bonde hilo la Songwe ili waweze kujikimu kiuchumi.

"Ingawa wataalamu wa Tanzania na Malawi wapo katika mchakato wa kutathmi matumizi ya maji ya Mto Songwe kwa manufaa ya pande zote mbili, lakini serikali inaangalia uwezekano wa kuwaruhusu wakulima kulima kilimo kidogo kidogo," Waziri Wassira aliwaambia wakazi hao.

Endapo wakazi hao wataruhusiwa kujishughulisha na kilimo kidogo kidogo kama vile cha mbogamboga na matunda katika bonde hili, bila shaka hali zao za maisha zitabadilika na bila shaka wataweza kujikwamua katika hali ya umasikini uliokithiri walionao hivi sasa.

Mbali ya bonde hilo lakini pia kuwapo kwa Ziwa Rukwa katika sehemu hii ya Wilaya ya Chunya, bado ni kichocheo kingine cha maendeleo kwa wakazi wa eneo hili. Hizi ni baadhi ya fursa ambazo kama watazitumia ipasavyo, wakazi wa Wilaya hii kongwe ya Chunya watapiga hatua kubwa katika kujiletea maendeleo yao binafsi, kaya na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Wassira akiwa katika jimbo hilo, aliwaagiza watendaji wa serikali wilayani humo kuhamasisha matumizi ya mbolea ya Minjingu. Wassira alisema ni mbolea ya Minjingu pekee ndiyo itakayoweza kuwakomboa wakulima ili kufikia ndoto ya Mapinduzi ya Kijani, mkakati ambao umelenga katika kuongeza uzalisha wa mazao ya kilimo kwa eneo dogo.

Ingawa kilimo cha pamba hakipo tena katika Wilaya ya Chunya, kutokana na kuibuka kwa mdudu mharibifu lakini jitihada za Dk. Sigonda zimewezesha wakulima waliokuwa wanadai malimbikizo ya fedha za mauzo ya pamba miaka zaidi ya kumi iliyopita sasa kuwa na uhakika wa kulipwa fedha zao.

Kwa mujibu wa Wassira tayari zaidi ya Sh milioni 500 zimefikishwa katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ili kuwalipa wakulima wanaodai. Sekta ya maendeleo ya jamii Mkuu wa Wilaya ya Chunya Kimario anasema wilaya hiyo imeendelea kutoa elimu sahihi ya sera za maendeleo ya jamii, jinsia na watoto.

Anasema dhana ya ushirikishwaji jamii inaendelea kusisitizwa katika kubaini mahitaji, kupanga na kuchangia maendeleo mbalimbali katika jamii kwa kuzingatia usawa wa jinsia katika uamuzi. Anasema ili kuharakisha maendeleo tarajiwa katika jamii, wilaya hiyo kupitia kwa wadau mbalimbali imeweza kutambua watoto 7,828 walio katika mazingira magumu na kuweka mipango ya kuwasaidia ikiwamo kuwaendeleza kielimu kwa kuwalipia ada na kuwapatia vifaa vya shule.

Pia wilaya hiyo inahamasisha vijiji kuwa na akaunti kwa ajili ya kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu. Jitihada hizo zimezaa matunda katika vijiji vinne ambavyo tayari vimefungua akaunti. Kimario anasema wilaya hiyo ina Mfuko wa Kusomesha watoto waliopo katika mazingira magumu, ambao kwa mwaka huu wa fedha umetengewa Sh milioni 15 kwa kazi hiyo.

Kwa upande wa mikopo, Kimario anasema halmashauri hiyo imetoa mikopo kwa vikundi 28 vya wanawake yenye jumla ya Sh milioni 27 kuanzia mwaka 2006/2007 hadi mwaka 2007/2008 ili kuwezesha uendeshaji wa miradi ya kiuchumi iliyoainishwa katika mipango ya maendeleo ya vikundi husika.

Hadi sasa jumla ya asasi 12 zimeanzishwa zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi, hifadhi ya mazingira, elimu ya watu wazima, haki za watoto, wanawake, wazee, walio na ulemavu na vijana.
 
Mto Songwe unatajwa katika kuweza kuinua kipato cha wakaazi wa Jimbo la Songwe iwapo mto huo utatumika katika kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo mto huo ambao unamwaga maji yake katika Ziwa Rukwa una umuhimu kwa nchi mbili, Tanzania na Malawi. Kwani unamwaga maji yake ndani ya Ziwa Malawi/Nyasa vilevile.

Kabla ya kuendelea kujadili hili kuna memba yoyote mwenye ufahamu wa mto huu, unaanzia wapi?

Iwapo una manufaa kwa nchi mbili, je kuna mpango wowote wa kuwa na kamisheni ya pamoja kati ya Tz na Malawi ili kuona kuwa mto huo unatumika kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili pasipo kuwepo na ugomvi?
 
Hamna lolote hakuna anayemtafuta mwenzake huko mbeya isipokuwa wambeya ni WAMBEYA kuna watu wanaishi kwa kungonganisha vichwa vya wasomi hawa kwa bahati mbaya they are not inteligent enough kuweza kubaini haya.ukimuuliza mwakipesile kwa nini unawachukuia hawa wezako hana jibu ukiwauliza wasomi hawa watakuambia kwanini ameteuliwa u RC na kuwekwa mbeya tha is rubish tha is an anilysis ya nawana mmoja ambaye alipata kufanya kazi na hao watu.tatizo lao hawawezi kukaa pamoja na kujadili kuna shetani gani amewapitia.every one is proud of himself. in my opinion hakuna aliyebora.
 
Back
Top Bottom